Sehemu ya saba •07•
....Anarudi hadi alipokua analala na asubuhi yake ankwenda kwenye stendi ya mabasi kwa ajili ya kurudi nyumban. Baada ya basi kuwasili katika mji ambao sham anaishi anapiga simu kwa dereva aliyemfuata na kumwambia amewasili na yupo nje ya stand ya mabasi na anafuatwa na kuingia ndani ya gari na kuelekea nyumbani kwao.
Nurdin anapofungua sura ya CAPTAIN anabaki na mshangao na tabasamu lilianza kuonekana na kumwambia kumbe ni wewe KAMBI, wanakumbatiana na kusalimiana na huku wale wafuasi wengine walianza kushangaa kilichokua kinatokea pale na CAPTAIN anaanza kwa kusema "huyu ni ndugu yetu na huyu mmoja kati ya waanzilishi wa kikundi hiki huko nyuma", anamkabidhi vitu vyake na kumwambia hakikisha kam vipo salama vimetimia na dereva atakufikisha salama hadi nyumbani. Anafika nyumbani na kupokelewa na wazazi wake na baada kupumzika na kupata chakula anaitwa faragha na baba yake na kuulizwa kuhusu barua ambayo alituma siku chache za nyuma, Nurdin anamjibu baba yake kuwa yote ni kweli na amebakiza wiki mbili kurudi huko kwenye maisha yake mapya na baba yake anamtakia kila la heri kijana wake na kumwambia afuate kile moyo wake unachopenda. Baada ya wiki anawaaga nyumbani kwao na kuwaambia kuwa amepata nafasi ya kuendeleza elimu yake nje ya nchi, anapanda basi kurudi alipokua anaishi na kuwasili jioni na anapofika kwenye chumba chake anashusha begi na kujilaza kitandani na kuanza kufikiria majukumu atayokuja kukutana nayo huko mbeleni, akiwa anaanza kusinzia mara ghafla simu yake inaita na anapopekea inasikika sauti ya kiume ..." hallo nina simu aina ya [emoji768] na nimeambiwa unatafuta na anataja na bei. [emoji768] ni aina ya simu ambayo nilikua naipenda na aliponiambia bei yake ilikua ni ndogo na nilimjibu kesho aniletee na ntainunua. Baada ya siku mbili nilihamisha vitu vyote na kuviuza na vingine niligawa kwa wapangaji wenzangu mule ndani na nilienda kupanga nyumba ya wageni kwa ajili ya siku zilizobakia na baada ya wiki kuisha nilipigiwa simu kufika mahala fulani kwa ajili ya kuanza maisha mapya.
.....Katika mtaa mmoja kulionekana kikundi cha watu kikiwa kinamvuta vuta kijana mmoja huku wengine wakiwa wanampiga makofi na mateke wakidai ni mwizi na adhabu yake yafaa auwawe lakini kikundi kile kilidai wao ni mwizi wao na watamalizana nae wenyewe na wanaenda nae kuingia katika nyumba fulani na kumwambia wanahitaji warudishiwe gari yao aliokua anafanyia kazi ya tax na anawajibu kuwa atawalipa gharama za gari yao na fidia lakini hawakutaka kumsikiliza na kumwambia tutakachokufanyia leo hutosahau, mmoja kati ya watu wale anasema hebu tumpeni nafasi ya kuongea huyu Dulla. Wanamwachia na anaanza kuongea kwa tabu na sauti ya chini na kusema " nimeanza kazi ya udereva tax kabla yenu nyinyi wote hapa na nimeenda kukaa jela mara 3 kwa makosa ambayo sikuwahi kufanya lakini nilijipa moyo na hadi hadi kifungo cha mwisho kupata msamaha wa raisi na niliporudi hapa kijiweni niliapa kuwa mwadilifu na dereva bora kuwahi kutokea lakini mara nyingi nakutana na mitihani ambayo mungu hunipa na pamoja na mara ya mwisho nilikua na gari yenu na nitawalipa gari yenu na mmoja kati yenu atoke nyuma ya nyumba hii atafute sehemu ambayo ilichimbwa na kufukiwa na afukue na atakuta kiasi cha pesa na mchukue na mniache na maisha yangu" ...Mmoja ya watu wale anatoka na baada ya dakika kadhaa aarudi akiwa ameshika mfuko uliokua na hela na anwaambia humu kuna fedha nying zinatosha hata kununua magari mawili kama lililopotea na wote wanabaki na mshangao na kumwambia wewe hizi fedha zote umetoa wapi lakini dulla anawajibu kama mmepata fedha zenu naomba mniache na maisha yangu. Wanaamua kumuacha na kuondoka watu wote wakimwambia una bahati umelipa na fidia za usumbufu. Huyu ni DEREVA na anakjikaza na kwenda nyuma ya jumba lile na kufukua sehemu na kutoa simu na anaiwasha na kupiga namba moja na kusema "nipo tayari mnifuate"........
Inaendelea