SIMULIZI: Sura Ya Kivuli

SIMULIZI: Sura Ya Kivuli

fenisher

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
339
Reaction score
733
Sehemu ya kwanza °01°

Asubuhi na mapema foru anapoamka na kufungua macho yake anaangaza huku na kule anagundua sehemu alipokua amelala si mahala pake na anapoinuka anashindwa kusimama na anaanza kuhisi maumivu ya mwili mzima na kichwa kinauma sana, anakaa na kuanza kuangalia chumba chote na anagundua pembeni ake kuna watu wawili wamelala wakiwa karibu karibu,mmoja alionekana mwanamke na mwingine mwanaume, hadi mda huo akili yake ilikua haijakaa sawa na anaamua kutuliza akili na kufikiria kabla ya kulala alikua wapi?!!, alikua na nani? na alikua anafanya nini? Lakini cha ajabu anashindwa kukumbuka kitu chochote kutoka katika ubongo wake na hali hiyo inamfanya mapigo yake ya moyo kwenda kasi ghafla na anagundua hakumbuki kitu chochote kutoka kwenye ubongo wake. Anaamua kujikaza na kuinuka kuelekea mlangoni kwa mwendo wa polepole na anapokaribia mlangoni anagundua ameipita kamera iliyokua bado inaendelea kurekodi vidio ikiwa imesimamishwa katika stendi yake, akili ake inapata kumbukumbu ya kuwa yeye ndiye aliyekua anaiweka kamera hiyo pale ilipo na kumbukumbu kukata, swala hilo linamfanya abadili mawazo ya kutoka ndani ya chumba iko na kuifata kamera ili aone matukio ambayo kamera imechukua toka mwanzo kwani hiyo ingemsaidia katika kurudisha kumbukumbu zake kichwani na anapoikaribia na kuishika kamera GHAFLA..!! Mlango unavunjwa na kuingia watu wakiwa wamevaa suti wote pamoja na miwani meusi na kila mmoja wao akiwa ameshika silaha aina ya bunduki na kutamka maneno kwa sauti ya juu " ukisogeza hata ukucha nakudungua risasi" Kauli hiyo inamfanya foru agande kama roboti na kudondosha kamera chini, hapo inamrudia kumbukumbu ya yeye akiwa anakabidhiwa bunduki na mtu na anaambiwa amtwange risasi mtu ambaye aliyekua mbele ake na nafsi yake inakataa na kudondosha bunduki chini kuashiria hawezi kufanya jambo hilo. Anaporudi kutoka katika kumbukumbu bado alikua amewapa kisogo watu wale walioingia ndani kwa kuvunja mlango na wanamwambia ageuke nyuma huku mikono yake ikiwa juu, anapogeuka na kuwaangalia watu hao ila kitu cha ajabu watu wote wanaanza kumshangaa na mmoja wao akisema kwa sauti ya chini " haiwezekani mtu huyu yupo hai" watu wale walionekana kuogopa kumkaribia moja kwa moja na hali hiyo inamfanya aanze kufikiria ni kwanini watu wenye miili iliyoshiba na wanaonekana wako sawa kiafya wanaogopa kumsogelea yeye ambaye ni mwembamba na dhoofu kwa anavyookana. " K.. mfunge pingu mimi nakulinda" alisikika mmoja wa watu wale akiwa anamwangalia mwenzake aliyekua upande wake wa kushoto na kumuonyesha ishara ya kusogea alipokua amesimama Foru na anamwambia wa upande wa kulia akawaangalie watu waliokua wamelala pale chini. Foru anapowaangalia watu wale anagundua wapo makini kwa kila hatua wanayokanyaga na anapowahesabu anagundua wapo watu saba lakini kila mmoja wao akiwa katika sehemu yake katika hali ya utulivu na ukakamavu,.. " mheshimiwa waziri amefariki na mkewe pia" alisema yule aliyeambiwa akague watu wale waliolala pale....kumbukumbu inarudi kukumbuka nikiwa nakabidhiwa nishani ya maua na mwanaume nikiwa nimevalia joho na mkononi nikiwa nimeshika cheti pamoja na kofia ya joho nililovaa na kumbukumbu inakatika tena. Yule aliyeambiwa aje kunifunga pingu alikua ameshanifikia na alikua ni mtu mwenye tahadhari kubwa na kunigeuza na akaanza kunifunga pingu huku akisema " uaijaribu kufany upumbavu wowote" Wakati ananiinua na kunisamamisha niliweza kuona nje kupitia dirisha la vioo kuwa tuko juu milima yani nje kote kulikua na milima na nikagundua sehemu tuliokuepo ni mlimani juu kabisa ...Jambo la kushangaza niliweza kupiga mahesabu ya kujirusha dirishani lakini kabla ya hapo nilitakiwa kuchukua begi lililo karibu na dirisha na kudondokea chini ya milima hiyo, ndani ya sekunde kadhaa nilipata jibu na haraka kumsukuma yule mtu mmoja aliyeniweka pingu na kuchukua bag na kujitupa kwenye dirisha lenye vioo na milio ya risasi ilinifuata kwa nyuma na kuvaa begi hewani nikiwa nadondoka kwenda chini ya milima hiyo. Hapa kuna kitu Foru alikua anawaza akiwa anadondoka kwanini!!? yule jamaa alimfunga pingu kwenye mkono mmoja na alimfinya mara mbili na yeye ndio akapata akili ya kuchukua begi na kujirusha kupitia dirishani......
 
Fenisher endelea kumwaga sumu...inaelekea hii safi sana
 
Sehemu ya pili °02°

Hapa kuna kitu Foru alikua anawaza akiwa anadondoka kwanini!!!? Yule jamaa alimfunga pingu kwenye mkono mmoja na alimfinya mara mbili na yeye ndio akapata akili ya kuchukua begi na kujirusha dirishani.....
Katika idara ya ulinzi ya nchi ya SOKOFI kulihitajika mtu ambaye angeweza pia kuichunguza idara hiyo ya usalama yani kulitakiwa mtu ambaye awe hajulikani na idara hiyo lakini awe ndani ya hiyo idara, mkuu wa kitengo cha idara hiyo kwenye maswala ya tehama alitoa wazo hilo kwa kua watu wa usalama walikua wanatoa taarifa za siri na kuzivujisha kwa wanasiasa na matajiri. Wazo hilo lilikubaliwa na atakayekua anasimamia alitakiwa asijulikane na mtu yoyote isipokua Raisi ndo anamteua kutoka ndani idara ya usalama wa nchi. Na hapo wazo hilo likafika kwa Raisi na yeye kukubali na kusema atateua jina moja baada ya miezi mitatu, yule mkuu wa idara ya tehama aliyetoa wazo lile alifurahi baada ya kusikia wazo lake limepitishwa lakini wakuu wa idara zingine walikua wanapinga wazo lile kwa kua lilikua linampa mamlaka makubwa mtu huyo kwani anakua na uwezo wa kuwa na maelezo yoyote anayohitaji na anaweza kuamua chochote kwa kua yupo peke ake na hajulikani ni nani hata hao maafisa wa juu walikua hawana uwezo wa kumgusa isipokua Raisi peke ake. Mtu huyo aliwapa wasiwasi wakuu hao na kuona si vyema kuwepo kwa mtu huyo wa siri.
Kijana nurdin tasada alizaliwa katika kijijini kabisa katika familia ya mzee tasada ambaye ni mkulima na mwenyekiti wa serikali ya mtaa hapo kijijini, mzee huyo alikua mtu asiyependa kuongea sana na mtu mwenye busara nyingi iliyomfanya wanakijijini hapo wampende sana, alikua ni mkulima mkubwa hapo kijijini na aliwahamasisha wanakijiji kujishughurisha na kilimo na ufugaji katika kujikwamua kimaisha. Mzee tasada alikua na familia ndogo ya watoto wawili na mkewe kufanya jumla ya watu wanne katika familia. Mtoto wake wa kwanza aliitwa nurdin na wa pili aliitwa nuru huyu alikua wa kike, kijana baada ya kumaliza elimu ya sekondari na kufaulu vizuri kabisa lakini hakutaka kuendelea na elimu ya kidato cha sita, alitaka akasome maswala ya tehama kwani ndicho alichokua anapenda. Baba yake hakua na shida na alimsomesha hadi kumaliza na kupata shahada ya tehama, alisoma kwa miaka sita na akafanikiwa kuajiriwa katika kampuni ya simu ambayo alidumu na kazi hiyo kwa mda mrefu. Nurdin alikua ni mtu mkimya kama mzee wake na aliyekua anapendwa na wafanyakazi wenzake. Siku moja alikwenda kumtembelea baba yake kijijini kwa kutumia usafiri wa basi na alibeba zawadi nyingi na ilikua kawaida ake kila mwisho wa mwaka lazima akawasalimie wazazi. Ndani ya basi alikua amekaa siti moja na mzee wa makamo kama baba yake na mzee akionekana yupo busy na simu yake mda wote, hadi basi linakaribia kufika anaposhuka nurdin hakuna aliyemuongelesha mwenzake isipokua salamu wakati mzee huyo alipokuja kukaa katika kiti cha basi. Wakati Nurdin anakaribia kushuka alimwomba mzee yule aanze kutoa mizigo yake kwani anakaribia kushuka lakini basi hilo lilikua linaendelea na safari. Basi lilifika stendi anaposhuka nurdin na alianza kutoa mizigo kupitia dirishani ambapo mtu aliyekuja kumpokea alikua akichukua mizigo hiyo. Alipomaliza kutoa mizigo yote alimuaga yule mzee na kumwambia safari njema mi nashukuru nimefika salama. " Asant kijana na hii baki nayo" alisema mzee yule na kumkabidhi karatasi ambayo ilikua imeandikwa barua pepe. Alipokea haraka na kuiweka mfukoni na kushuka ndani ya basi. Alifika kwa wazazi wake na kama kawaida ake alishegherekea mwaka mpya akiwa kwao. Alikaa kwa siku tano na kurudi mjini na kuendelea na majukumu yake kama kawaida. Siku ya kupumzika alikua anafua nguo zake na wakati anatoa vitu katika mifuko alikutana na ile karatasi ilikua na barua pepe. Alichukua simu yake na kutuma meseji kwenye barua pepe hiyo na kuendelea na usafi wa nguo zake....akiwa anakaribia kumaliza kazi ake mara simu yake ilianza kuita, anajifuta maji na kupokea huku akiwa mnyenyekevu kwa kua ilikua ni namba ambayo hakua nayo katika na ilisikika sauti ya kiume ikimwambia umefaulu kujiunga na idara ya usalama wa nchi......
 
Ni nzuri sana lakini tatizo hapa Jf saivi arosto zinaongezeka
 
Sehemu ya tatu ° 03°

Akiwa anakaribia kumaliza kazi ake mara simu simu yake ilianza kuita, anajifuta maji na kupokea huku akiwa mnyenyekevu kwa kua ilikua ni namba ambayo hakua nayo katika simu na ilisikika sauti ya kiume ikimwambia umefaulu kujiunga na idara ya usalama wa nchi...Alibaki ameduwaa na mshangao wa ajabu kwa kua hakuamini kile alichokua anasikia na aliendelea kuongea yule mtu kwenye simu "unatakiwa kufika katika hoteli ya madono kwa ajili ya mahojiano" alafu simu inakatika, hapa nurdin anabaki bado na mshangao kwa kua miaka miwili iliyopita alifeli usahili huo wa idara hiyo na sasa inakuaje aambiwe amefaulu kujiunga nao sasa. Kesho yake asubuhi jumatatu anapiga simu kazini kwake kua amepata dharura kwahiyo atachelewa kufika na mkuu wake anamjibu kwa kumwambia watampa ushirikiano kwa lolote litakaloendelea na simu kukatika, lakini nurdin bado anabaki na maswali kuhusu kauli ya mkuu wake kuhusu kumpa ushirikiano na wakati hajawaambia ni dharura gani yeye alieipata. Akiwa kwenye daladala anakumbuka kitu kimoja na anaamua kushuka kwenye daladala haraka na kisha kutabasamu kujiambia kua mimi ni mjinga na naenda kutapeliwa huku. Anaamua kupanda daladala ingine na kurudi kuelekea kazini kwake. Aliwaza akiwa kwenye daladala " mara ya kwanza tulifanya interview kwenye ofisi za idara ya usalama lakini kwanini leo naitwa niende hotelini alafu mi nilishafeli huo usahili kwanini aniambie nimefaulu tena na kivip na miaka yote hiyo ipite" alifika kituo anachoshuka na kuelekea ndani ofisini kwa kua ofisi ilikua karibu kabisa na kituo cha daladala na anapoingia ndani kama kawaida baada ya kumsalimu walinz waliopo mlangoni anapita ndani kuwasalimia wafanyakazi wenzake na wanaitikia na anakwenda kwenye dawati anapokaa anakuta hakuna hata kitu kimoja ni kompyuta pekee na hakukua na karatasi ya aina yoyote. Anapogeuka na kuwaangalia mfanyakazi wake wa pembeni anakuta anamshangaa na wengine wote wanageukia pembeni baada ya kukuta amegeuka.!!! Anajiuliza kuna tatizo gani na inamaana ameachishwa kazi!!? Alimwuliza aliye jirani ake kwa upole " kuna tatizo gani mbona mnanishangaa!!??" Akajibu yule mfanyakazi mwenzake " haturuhusiwi kuongea na wewe isipokua mkuu wako wa kazi na naomba unisamehe kwa hilo " ...nurdin anainuka na kwenda moja kwa moja kweny ofisi ya mkuu wake na anaingia bila ya kugonga na kumwuliza mkuu wake ni nini tatizo bila hata ya kukaa chini, mkuu anamwambia haturusiwi kuongea na wewe kwa kuwa wewe ni mtuhumiwa wa kesi kubwa. Kushika simu na kupiga na kusema amefika mda huu na yupo ofisini kwangu na kukata simu. Ghafla wanaingia walinzi wa pale mlangoni na mmoja kumwonyoshea bunduki akimwambia atulie kama akivyo na mwingine anakuj na kumfunga pingu na kumtoa nje ya ofisi na baada ya dakika ya kumi na tano inakuja gari ya askari na kumuingiza ndani ya gari ya hao na kuondoka nae, njiani kwenye gari wanamfunga kitambaa cheusi usoni na kuendelea na safari, gari inasimama sehemu na kushushwa na kuingizwa kwenye chumba kilichokua na godoro peke ake baada ya kufunguliwa pingu na kitambaa cha usoni. Nurdin anawaza ni kitu gani haswa kinachofanya yeye awepo pale na ni aina ya kituo cha polisi alichopelekwa chenye godoro ndani ake..!!! Na kwanini wafanyakazi wenzie wakatae kuongea na yeye na hakuna siku aliokorofishana na mtu yoyote hivi karibuni wala siku yoyote katika maisha ake...Kichwa chote cha nurdin kilikua kimevurugika kwa kua hakuna jibu alilopata kwanini yupo sehemu ile. Anastuka alikua akiamshwa na sauti ya kike " kijana..!! kijana..!!" Na anaamka na anamuona mwanamama wa akimwangalia na anagundua ni siku kwakua kilikua ni kiza mule ndani na yule mama anamwambia kula chakula na anmsogezea sahani ya chakula na maji kwenye chupa. Anachukua chupa ya maji anakunywa kwa haraka na anachukua sahani ya chakula anakula na baada ya kumaliza ankunywa tena maji yote na mikono ake anajifuta kwenye suruali ake na wakati wote anakula yule mama alikua akimwangalia usoni na yule mama akasema naweza kuongea na wewe sasa!!?
Nurdin: ndio
Mama: kwanini upo hapa?
Nurdin: sijui na natamani nifahamu
Mama: unaitwa nurdin na una miaka 26
Nurdin: ndio ila naomba uniambie kwanini nipo hapa
Mama: wew ni maji kwenye mwili wa binadamu
Nurdin: una maana gani?
Mama: nakupa dakika kumi nikirudi uniambie kwanini upo hapa!!?

Hapa nurdin anashangaa na yule mama kutoka nje ya chumba huku akiwa anaangalia saa yake ya mkononi na nurdin anavuta pumzi kwa nguvu na anatuliza akili ake akiamini akikumbuka kitu chochote anaweza kutolewa sehemu ile. Anafikiria kuanzia asubuhi ya siku zote za mapumziko hadi anapokamatwa je amemkwaza nani!?? Na anafikiria ni mtu mmoja pekee ambaya atakua amemkwaza ni si mwingine ni yule mtu aliemwambia aende hotelini lakini yeye hakufika na inaonekana kutakua uhusiano kidogo na kukamatwa kwake labda kwa sababu alimdharau mtu yule kwa kua anaweza kua mkuu idara ya usalama. Hilo ndio jibu pekee alilokua nalo kichwani na alifikiria kumwueleza yule mama..baada ya dakika kumi yule mama anarudi ndani na kumwuliza je zimekutosha au nikuongezee zingine huku akitabasamu. Nurdin anamwangalia yule mama na kumwambia hapana zinatosha.

Mama: haya niambie kwanini upo hapa
Nurdin: barua pepe ndani ya basi
Mama: anatabasamu na kumwambia naomba ufafanue
Nurdin: nimekosea kwa kumdharau mtu wa usalama
Mama: una uhakika!?
Nurdini: ndio nina uhakika
Mama: Asante. Na karibu katika kuilinda nchi na wananchi wake
Nurdin: kuilinda nchi kivip!??
Mama: umechaguliwa na kujiunga na jeshi la usalama wa nchi
Nurdin: sawa na je naweza kutoka ndani ya chumba hiki
Mama: ndio
.....itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom