Sehemu ya tano °05°
Alipomaliza akatuaga na kutuambia twende chumba namba 10...Hapa tulipata majina ya kutambuana kwani hakuna aliyethubutu kumwelezea mwenzake jina lake na maisha ake, tulikua tunaitana kwa majina ya utani tu hii ni kutokana na maandishi yaliondikwa juu ya bahasha, nilikua natamani kujua kwanini tumepewa majina yale na yana maana gani. Tulikwenda hadi kufika chumba namba 10 na kukutana na dada ambaye alikua amekaa kwenye kiti na akatukaribisha na kujitambulisha " mimi naitwa 22 - fantasia " na nimepewa maelekezo kwa kila mmoja wenu na naomba kila mmoja wenu ayafuate na yeyote atakaekiuka atapata adhabu kali kutoka kwangu. Akatuonyesha kabati lililokua pembeni yetu na kutuambia tuchukue kila mtu begi lake kutoka katika hilo kabati na tukasogea na kuchukua lakini hapa palikua na tatizo kwani kila begi liliabdikwa namba yani 20,21,22,23,24 na hapakua na namba 25 yani ile namba yangu, wenzangu walichukua mabegi kutokana na namba zao na mimi niliendelea kujiuliza na badae nikaamua kuacha lile begi moja lililobakia yani namba 22 na kurudi waliposimama wenzangu bila ya begi na yule dada akaniuliza kwanini sijachukua begi na kumjibu kuwa hapakua na begi lenye namba yangu na akasema kosa moja utakalolifanya katika kazi hii basi inasababisha madhara kwa wananchi na kusema unatakiwa uwe makini na kichwa chako kifanye kazi kwa haraka na kunirushia begi alilokua ameshika mkononi na kusema mnatakiwa mkaoneni na familia zenu kwa wiki mbili na baada ya hapo mtarudi. Na kisha kuondoka na kwenda kwenye kabati na kuchukua lile begi naye kuanza kutoka na kusema tumfuate yeye kwa ajili ya usafiri.
Tulifika na kukutana na gari ambayo tulitakiwa kuweka mabegi yetu na kabla ya kuingia ndani gari kwa ajili ya usafiri tulitakiwa kwenda kusaini kwenye chumba kilichopo karibu na gari tulioweka mabegi. Tulikwenda na kuanza kuingia mmoja mmoja na ilichukua nusu saa kwa mtu mmoja kutoka na ilipofika zamu yangu niliingia na kupewa shati jeupe na tai nivae haraka na baada ya hapo nilipigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole mkononi na kusaini mara tatu na kupimwa urefu, uzito na kila sehemu ya mwili wangu kuchukuliwa vipimo vya urefu na upana. Niliambiwa tayari na nivue nguo zile na kuvaa za kwangu na kurusiwa kutoka nje, tukasubiria wengine waingie wamalize ndipo safari ianze. Wa mwisho alipokua anatoka katika kile chumba alikua anefuatana na mmoja kati ya watu waliokua mule ndani na alikuja na kutuambia tukae mstari na akatufunga pingu wote na kutufunga vitambaa usoni vilivotufanya tushindwe kuona mbele akatusaidia kuingia kwenye gari na yeye akawasha gari na safari ya kutoka katika jumba hilo ilianza, kitu ambacho kilinishangaza ni kwanini walimfunga na yule dada aliyekua anatupa maelekezo, nilikua nikidhani nae ni kiongozi katika ile idara lakini nilishindwa kujua yupo kama sisi au vip. Baada ya mwendo wa masaa mengi nilihisi nafunguliwa pingu katika mikono yangu na baada ya sekunde kadhaa pingu ilikwisha tolewa mikononi mwangu lakini kile kitambaa kilibaki usoni na baada ya dakika tano tuliambiwa tutoe vile vitambaa usoni mwetu na kuona yule dada akiwa amezishika pingu zote na wakati wote gari ilkua ikiendelea na safari, ina maana yule dada ndiye aliyekua ametufungua pingu hali ya kuwa nae alifungwa, nilimwangalia usoni kwa kumkazia macho na yeye akaanza kuongea na kusema tunakaribia kiwanja cha ndege na kila mtu atapelekwa kwa wazazi wake na kukaa wiki na wiki nyingine utarudi ulikua unaishi kwa ajili ya kuhamisha vitu vyako.
Tulishuka na kuingia kweny le uwanja wa ndege katika sehemu hiyo ambayo ilikua ni kijijini kidogo na sehemu ya uwanja huo haikua ni kubwa sana na miundombinu yake ilikua ya kawaida. Hatukupitia walipokua wanapita watu wengine yani abiria wa kawaida, tulipita kwenye njia walizokua wanatumia wafanyakazi wa uwanjani hapo na tulipofika kwenye chumba kimoja tulitakiwa kuacha mabegi hapo na tukaelekezwa kwenda ndani ya ndege na kupatiwa sehemu ya kukaa na baada ya nusu saa safari ilianza kwa hilo kuanza kupaa angani. Tukiwa ndani ya ndege tulipewa sehemu tofauti tofauti na ndege ilitua sehemu moja na tiketi niliokabidhiwa ilkua ikionyesha natakiwa kushuka hapo na nikashuka hadi kweny sehemu ya ambayo tulikusanyika wote tulioshuka hapo na cha kushangaza hakuna hata mmoja kati watu niliokua walioshuka hapo. Nilistuka kushikwa mkono na mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa hapo akiniambia natakiwa nimfuate yeye na nilimfuata hadi katika chumba kama cha mwanzo na kukabidhiwa begi langu na kuliweka mgongoni na yule mfanyakazi akaniaga na kuniambia karibu tena. Hapo nilipokua ilikua ni katika mji ambao nimezaliwa na sikua tena ugeni kwani ni sehemu ambayo naifahamu vizuri na wakati natoka nilikutana na madereva tax wakinifuata ba kuniuliza naelekea wapi, hapa nikagundua nilikua sina hata senti moja na ntaendaje hadi kijijini kabisa ambapo ndipo mzee wangu anapoishi na nilitua begi chini kuanza kulifungua kila sehemu na baada ya kufungua zipu ya tatu nikakutana na kiasi kikubwa cha pesa zikiwa zumechanganyika na pesa na kigeni na nilichomoa kiasi fulani cha pesa na kufunga begi na wakati wote wale madereva tax walikua wananiangalia na kuwaambia sitatumia tax na naenda kuchukua pikipiki, waliondoka na huku wakiongea chinichini " jamaa lina pesa lakini bahili" nilifika hadi kwenye kituo cha pikipiki na kuchukua pikipiki na safari kuanza kuelekea nyumbani nilipozaliwa. Njiani ikiwa jua linaanza kuzama dereva wa pikipiki akaanza kusema inabidi tuingie tuongeze mafuta maana haya hatutaweza kufika nayo, nilimwambia ni vizuri tufanye hivyo na tuliingia katika kituo cha mafuta kuongeza mafuta namimi nikashuka na kununua maji na safari ikaanza tena, kutoka miji hadi kijijini kwetu ni muda wa masaa 2 kwa pikipik na niliamua kupanda pikipiki kwani ningefika haraka magari yanachelewa na tax nyingi walikua haawaminiki. Njiani dereva alianza kupunguza mwendo na kuniambia anataka apate haja ndogo nami niliposikia hivyo nilimwambia sawa kwani nami nilikua na wazo hilo. Ilkua tushakaribia na nyumbani ni mwendo wa dakika 15 hadi kufika na giza tayari lilikua lishaingia na wakati tunajisaidia mara GHAFL..!!! Likatokea kundi la watu wengi wakiwa wameshika mapanga na marungu na kusema tulieni na toa kila kitu ulichokua nacho, yani hapa walikua wananiambia mimi na nilipomwangalia yule dereva wa pikipiki alikua hana wasiwasi na yeye akaongezea kwa kusema umewasikia walichosema..!?? Mapigo ya moyo yalikua yanaenda mbio na nilifunga suruali angu na kuvua begi na kuweka chini na kuwaambia kuwa wanafanya makosa kumuibia yeye, walicheka wote kwa dharau na yule dereva wa pikipiki akaokota lile begi na kusema nitoe kila kitu katika mifuko yangu ya nguo zote na nilitoa na zile pesa nilizoweka mfukoni na kutupia chini na baada ya kuokota yule mwenye dereva akasema tumsubiri CAPTAIN tujue tunamfanya nini huyu mjingamjinga....!???
Itaendelea