Simulizi: Scaila Michael

Simulizi: Scaila Michael

Msione kimya jamani namsubiri huyu brother man nyemo apost niwaletee
 
Scaila scaila scail... Kazi nzuri japo kuna makosa madogo madogo ya hapa na pale...
 
usiku mwingine huu kweli mvumilivu hula mbivu ,nasubiri shunie
 
usiku mwingine huu kweli mvumilivu hula mbivu ,nasubiri shunie
Aisee ii methali ilishabadilika, mvumilivu hula zilizooza, methali nying zshabadilika iki kizazi, mficha uchi huzaa kwa operation
 
Mtunzi Nyemo Chilongani

Sehemu ya 01.

Nilikuwa chumbani kwangu, kichwa changu kilikuwa na mawazo tele. Akili yangu ilichanganyikiwa, kulikuwa na mambo mengi ambayo yalinichanganya kipindi hicho, ila kubwa zaidi ni kuhusu msichana niliyekuwa nikimpenda kwa moyo wangu wote, Shasta Karina.

Naweza kusema kwamba miongoni mwa wasichana ambao nilikuwa nao katika maisha yangu, huyu nilimpenda mno. Alikuwa msichana mrembo ambaye ninaweza kusema alistahili kuwa mke wangu wa ndoa, nimuoe na hatimaye tujenge familia pamoja.

Nilikutana na Shasta miaka miwili iliyopita maeneo ya Victoria, Mikocheni kaika Mgahawa wa KFC. Siku hiyo nilikuwa nikitoka kumtembelea rafiki yangu aliyekuwa akiishi Msasani.

Nakumbuka nilipofika maeneo hayo, nilipaki gari langu na kwenda kwenye mgahawa huo uliokuwa mahali hapo, nikaingia na kukaa kwenye meza moja.

Nilikuwa kimya mno, sikutaka kuwa na presha yoyote ile, humo ndani macho yangu yalikuwa yakiangalia huku na kule kama nilikuwa namtafuta mtu fulani hivi, macho yangu yakatua kwa mhudumu mmoja, aliyevalia nguo zake safi, harakaharaka akaja pale nilipokuwa.

“Karibu!” aliniambia kwa sauti nyembamba, na kwa jinsi alivyokuwa mzuri, nilihisi kama nikipata hali fulani moyoni.

“Ahsante sana!” niliitikia na kumkazia macho, sikutaka kuyatoa kutoka usoni mwake.

Nilibaki nikimwangalia kwa sekunde kadhaa, alikuwa akiangalia pembeni huku akionekana kusikia aibu kupita kawaida. “Karibu!” alinikaribisha tena, akasindikiza na tabasamu fulani pana.

“Nashukuru sana! Ninahitaji chakula kizuri kama ulivyo,” nilimwambia kiutani huku macho yangu yakiendelea kubaki usoni mwake.

“Oh!”
“Ndiyo! Chipsi combo!” nilimwambia.
Msichana huyo akaondoka, nilibaki nikimwangalia, alionekana kuwa miongoni mwa wasichana warembo mno ambao niliwahi kukutana nao katika maisha yangu.

Kipindi hicho nilikuwa singo, niliachana na msichana aliyeitwa kwa jina la Evelyne kwa sababu tu hakuwa na sifa za kuwa mwanamke wa kuishi naye.

Ninapomfuata msichana kuna vitu vingi ninaviangalia, cha kwanza ni uwezo wa akili yake, je, nikiwa naye anaweza kulea watoto wangu kwa staili ninayoitaka?View attachment 1120636
WALE WOOOOOOOOOOOOOOOTE MNAOIFUATILIA HII HADITHI ANDAENI SHILINGI 10,000 YA KUNUNUA KITABU MAANA HII HADITHI HAITOMALIZIKA HUMU JAMIIFORUMS MUENDELEZO MTAUPATA KWENYE KITABU
 
SEHEMU YA 39

Hiza hakutaka kunificha, alihitaji kuniokoa rafiki yake hivyo akaanza kuniambia kuhusu Scaila. Hakutakiwa kunificha, kama kweli nilikuwa rafiki yake wa dhati basi ilikuwa ni lazima aniambie kuhusu msichana huyo.

Akaanza kuniambia tangu siku ya kwanza alipokutana na msichana huyo huko Maisha Club. Alichoniambia ni kwamba siku hiyo alikwenda huko na rafiki yake aliyeitwa kwa jina la Cosmas.

Baada ya kufika, waliingia na kucheza, humo ndani ndipo alipokutana na Scaila ambaye alikuwa na marafiki zake wawili na kuanza kuzungumza nao.

Rafiki yake mmoja alichoniambia ni kwamba alinyoa kiduku huku nywele zake akiziweka breach. Alijazia kwa nyuma na kwa jinsi alivyonipa maelezo hayo niligundua alikuwa Janeth.

“Ikawaje?”
Akaendelea kuniambia kwamba waliwanunulia pombe na rafiki yake huyo kuondoka na Scaila kwenda nyumbani kwake ambapo alilala naye mpaka asubuhi.

Scaila hakuwa kama ambavyo nilihisi alikuwa, alikuwa msichana mwingine kabisa. Hiyo haikuwa mara ya mwisho kuwachukua, waliwachukua mara nyingi kwani walikuwa wakijiuza na kuwalipa vizuri.

“Hiza....nitakufa,” nilimwambia huku nikirudi kochini na kukaa.
Nilihisi mwili wangu ukipigwa ganzi, sikuweza kuamini kama kile nilichoambiwa kilimuhusu Scaila au mtu mwingine. Wakati mwingine nilitamani kumwambia Hiza kwamba alichanganya na yule aliyekuwa akizungumza naye hakuwa Scaila niliyekuwa na mipango ya kumuoa.

Nilibaki kwenye hali hiyo kwa dakika kadhaa huku nikitumia muda huo kumfikiria Scaila, mwanamke niliyekuwa nikimpenda kutoka moyoni mwangu.

Alikuwa mcheshi, mpole lakini kile nilichoambiwa kuhusu yeye, kilinichoma moyoni mwangu na wakati mwingine nilihisi kabisa kulikuwa na mtu aliyeuchukua msumali wa moto na kunichoma vilivyo.

“Scaila ni malaya anayejiuza klabu?” niliuliza huku nikionekana kuchanganyikiwa, ndani ya nyumba ile kulikuwa na kiyoyozi lakini cha kushangaza kijasho chembamba kilianza kunitoka mwilini.

“Nyemo! Come down rafiki yangu!” aliniambia Hiza huku akinisogelea, alijaribu kunipoza lakini sikupozeka hata kidogo.

“Yaani Scaila huyuhuyu ama mwingine?” niliuliza.
“Ndivyo wanawake walivyo!”
 
SEHEMU YA 40

“Ila Scaila amezidi! Kwangu anatabasamu vizuri kumbe ni malaya! Jana nimefuatilia mawasiliano yake na huyo rafiki yake! Yamenichoma sana, yameniumiza kupita kawaida.

Hiza, hebu fikiria, mwanamke unamuahidi utamuoa, unampa kila kitu, unamjali, unamshirikisha mambo yako, unamfanyia kila kitu na mwisho wa siku anachati na rafiki yake na kumwambia amewakumbuka mabwana zake wa klabu.

“Kuna mtu anaitwa Alfred, huyu ni bwana wake, nilikwenda nyumbani kwao, nikamuona akitoka naye chumbani, yaani jamaa alikula mzigo humohumo, mbaya zaidi mpaka mama yake anafahamu hilo.

Hiza, hili jambo linaniuma sana na wakati mwingine naanza kumfikiria Shasta wangu! Kwa nini Scaila ananifanyia hivi?” nilitoa maelezo marefu na kumalizia kwa swali.

Macho yakaanza kujikusanya machoni mwangu na kuanza kutiririka mashavuni. Kitu kile kiliniumiza sana lakini pamoja na hayo yote nilitakiwa kutabasamu kila nitakapokuwa mbele ya Scaila, yaani hakutakiwa kufahamu kitu chochote kile.
“Kwa hiyo utafanyaje?” aliniuliza Hiza huku akiniangalia.

“Nitajua cha kufanya!”
“Ila usiue!”
“Siwezi kufanya hivyo!”
“Wala usimpige!”
“Siwezi kufanya hivyo pia. Kwa sababu ni masuala ya kidemokrasia, basi nitamalizana naye kidemokrasia,” nilimwambia Hiza, nikaondoka zangu.

Nikaondoka na kuelekea kwenye biashara zangu, kiukweli nilichanganyikiwa kupita kawaida, nilikuwa nikitembea na maumivu makali mno, kichwa changu kilibeba mzigo mzito ambao sikujua ni muda gani ningeweza kuutua.

Ni kweli Scaila alikuwa msichana mrembo mno, tena mno lakini kwa mambo yake hakustahili kuwa na mimi hata kidogo. Kulikuwa na jambo moja ambalo nilitakiwa kulifanya, kumuacha msichana huyo na kufanya mambo yangu tu.

Sikutakiwa kumuacha kwa ugomvi, ilikuwa ni lazima nitumie akili kubwa kumuacha, kwanza niwe na uthibitisho wa mambo yake yote ambayo anayafanya, baada ya hapo ndiyo niamue ni kitu gani hasa nilitakiwa kufanya.
 
SEHEMU YA 41

Hakuna kitu cha raha kama kumuacha mtu huku ukiwa na uthibitisho wa asilimia mia moja kwamba ni mzinguaji. Najua angeweza kujitetea kwa mara ya kwanza lakini baada ya kumpa uthibitisho, nilikuwa na uhakika asilimia mia moja angeufyata ulimi wake na kunyamaza kimya.

Nilikwenda kwenye biashara zangu, siku hiyo sikuwa kawaida kabisa, mapenzi yaliniumiza na muda mwingi nilikuwa nikimfikiria msichana huyu.

Kipindi hicho ndicho nilichogundua maumivu halisi ya mapenzi, zamani nilishawahi kuumia lakini ilikuwa tofauti na siku hiyo. Nilihisi kama moyo wangu ulikuwa karibu na kaa la moto, nilijitahidi kufanya mambo yangu mengine ilimradi tu nisifikirie kuhusu msichana huyo lakini ilishindikana kabisa.

Wakati nikiendelea na shughuli zangu kama kawaida, simu yangu ikaanza kuita, haraka sana nikaichukua kutoka mfukoni, nikakiangalia kioo, alikuwa Scaila.

Mapenzi ni kitu cha kipumbavu sana. Kiukweli nilichukizwa na kile alichokuwa akikifanya msichana huyu, nilichukia mno lakini jambo la ajabu kabisa baada ya kuona simu yake, moyo wangu ukawa kama umemwagiwa maji na kuanza kupoa kabisa.

Yaani yale maumivu ni kama yalianza kutoka moyoni mwangu na upande mwingine kuhisi kile nilichokiona hakikuwa sahihi, inawezekana nilikuwa naota ama kulikuwa na fikira mbovu zilizokuwa zimeniingia.

“Halo mpenzi! Mbona umechelewa kupokea simu?” aliniuliza huku sauti yake ikisikika kama mtu aliyekuwa akideka.
“Samahani mamiii! Nilikuwa bize kidogo! Ila nimekumiss sana mpenzi,” nilimwambia.

“Nimekumiss pia baba watoto! Unarudi muda gani nyumbani?” aliniuliza.
“Muda wowote ule kipenzi!”
“Basi nakusubiri! Nimekumiss sana,” aliniambia na kisha kunipiga busu la kwenye simu.

Huyu mwanamke alikuwa ni shetani, nina uhakika huo kwani busu hilo liliifanya damu yangu kukaa kwenye mzunguko mzuri, nilihisi kama matatizo yote niliyokuwanayo maishani mwangu yakiondoka kabisa.

Yaani akili yangu ilichanganyikiwa na ndiyo maana mpaka leo ninapokaa na kuanza kumfirikiria Scaila, huwa ninashindwa kujua ni kwa kiasi gani msichana yule alinichanganya sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom