Simulizi: Pole kwa Mama Omary

AmbaB

Member
Sep 1, 2016
51
27
Mama Omary, mama aliyeishi maisha ya kifahari akiwa na mumewe miaka ya 1990s. Mume wake alikuwa anafanya kazi wizara ya Fedha miaka hiyo na bahati mbaya alipata ajali wakiwa kwenye shughuli za kikazi mkoani Sumbawanga.

Mama Omary akiwa muuguzi(Nurse) katika hospitali ya Amana, aliachiwa mali kadhaa, ikiwemo nyumba kubwa ya kifahari maeneo ya Keko Mwanga Dar es salaam, nyumba ambayo aliamua awe anaishi yeye na wanae watatu, wa kiume, yaani Omary(35), Shaban (29) na Zuber (26).

Omary akiwa na kazi yake nzuri benki moja mjini maeneo ya posta, aliamua kuoa na kuondoka nyumbani kwani tangu kifo cha baba yao walikuwa wakiishi wote wanne ndani ya nyumba hiyo walioachiwa na baba yao mzee Yusuph Kimbani Mhende. Waliishii na mama yao ili asiwe mpweke huku wakiwa wanasaidiwa kazi za usafi na wadada kadhaa wa kazi.

Shaban alimaliza chuo, asiwe na kazi, akawa ni mtu wa kutafuta ajira akitokea nyumban kwa mama yake , kila mmoja alipewa chumba chake cha kuishi, wakawa wanakutana wakati wa chakula cha pamoja.

Zuberi, kitinda mimba, yeye akiwa bado anasoma chuo cha usimamizi wa fedha, IFM, mjini maeneo ya posta, bado nae hakuona haja ya kuhama nyumbani.

Mnamo mwezi wa nne 2007, Mama Omary (52) , akapata binti mpya wa kazi, Lisa (26) alikuwa kapigika sana na maisha mjini, akaomba kazi ndani ya nyumba hiyo na kupewa kazi ya usafi lakini akiwa anatokea nyumbani kwao, akawa anakuja asubuhi na kuondoka majira ya saa kumi jioni akiwa kafanya kazi zote na pamoja na kuwapikia chakula.

Lissa alikuwa ni mdada ambaye alimueleza kila kitu mama Omary, hasa kuhusu maisha yake ya nyuma ,na namna alinyanyaswa na mumewe mpaka wakaachana akiwa kijijin Chato ndipo akaamua kuja mjin Dar kwa ajiri ya kutafuta kazi. Bahati mbaya mwenyeji wake akampeleka kujiuza maeneo ya Ambiansi Sinza, kikawa ndiyo kijiwe chake kikubwa, akafanya kila aina ya starehe huko na kutokana na mnato wa mvuto wa rangi yake na umbo lake maridhawa hakuwahi kukosa wateja akiwa kazin kwake.

Alifanya kazi hiyo akaweza kulipa kodi ya chumba chake na kununua baadhi ya mali. Bahati mbaya alianza kuugua sana na kusababisha kuuza mali zake zote , mwisho wa siku akiwa kamaliza kila kitu akajikuta hana uwezo wa kulipa kodi wala kula, akawa anadhoofika sana, siyo Lisa yule maarufu kwenye viti virefu. Ndipo akaamia keko karibu na kwa mama Omary, baada ya kuumwa sana na kupatwa na VVU.

Lissa aendesheje maisha, akaenda kuomba kazi kwa mama Omary, bahati nzuri akapata.
Akiwa anakuja kufanya kazi hapo, kila kijana wa mama Omary akawa amenzisha uhusiano wa kimapenzi na Lissa kwa muda wake, Omary pamoja na kuoa, akija kumsalimia mama akakutana na jicho zuri la Lissa na asiweze kujizuia kumgongoza mrembo wa zamani yule. Kwa shida za Lisa haikuwa rahisi kumkatalia Omary kijana mtanashati akiwa anakuja na gari yake aina ya Alteza, pesa si ndiyo hii ! Lissa alijisemea, akaingia kwenye uhusiano na Omary ihali tayari alikuwa na mahusiano na wadogo wake wote. Kila mmoja akiwa anapata huduma kwa wakati wake.

Ikawa ni jumamosi, Mama Omary, bi.Halima, hajaenda kazini, akamuona (kupitia dirisha) Lissa anatapika sana nje ya nyumba yake, alijawa na huruma sana na kumsihi amkinbize hospitali, kufika hospitali wakapima akawa kapatwa na Mimba ya mwezi mmoja, bi Halima akakumbuka Lissa hakuolewa, kumhoji sana nani mhusika wa mimba ? Lissa akwa mtu wa kulia sana, na kuomba msamaha kwa mama.

Mama akamuomba daktari amsaidie kumpima Vvu, akawa kweli amepatikana na virusi vya Ukimwi.
Kesho yake Lissa akiwa kwake, akaamua kumwambia mama ukweli, ukweli juu ya kuwa mhusika wa Mimba ni Omary, na ya kwamba vijana wake wengine wote walikuwa wapenzi tu ila mhusika wa mimba ni Omary.

Huzuni na simanzi ndani ya nyumba ya Bi Halima maarufu kama mama Omary, aliwaita vijana wake wote watatu, wakakaa kikao na kuamua kwenda kupima afya zao wakiwa pamoja na majibu akayapokea yeye. Masikini, Mama Omary, akapoteza maisha mara baada ya kuona majibu chanya ya wanae wote watatu, akapata mshituko ambao haukuweza kumrudisha kwenye uhai wake mpaka leo.

Saikolojia ikawa imewaathiri saana vijana wa bi Halima kwa kuwa kila anayekuja msibani alijua kisa hiki, mara baada tu ya mazishi vijana wote watatu wakapotea na wala wasijulikane walipo.

Mpaka mwandishi anaingia kushika kalamu hii, hakuwa anajua vijana wa Mama Omary wameelekea wapi, wamejinyonga? Hakuna anayejua, wamehama nchi? Ndoto za vijana zikawa zimeingiliwa .....

.....itaendelea

Na;
Ambangile, B

Inst.( ambangile_b)
 
Dah inasikitisha sana. Mungu atunusurie vijana wetu. Na mm nina vijana watatu nataka wakikua sileti dada wa kazi wapambane wenyewe na kazi maana nahisi watamsarandia au nilete mmama mkubwa. Nawaza tuu maana jamani kulea kazii bila msaada wa Mungu
 
Dah inasikitisha sana. Mungu atunusurie vijana wetu. Na mm nina vijana watatu nataka wakikua sileti dada wa kazi wapambane wenyewe na kazi maana nahisi watamsarandia au nilete mmama mkubwa. Nawaza tuu maana jamani kulea kazii bila msaada wa Mungu

Aaaah😁😁 kaz ipo.
 
Dah inasikitisha sana. Mungu atunusurie vijana wetu. Na mm nina vijana watatu nataka wakikua sileti dada wa kazi wapambane wenyewe na kazi maana nahisi watamsarandia au nilete mmama mkubwa. Nawaza tuu maana jamani kulea kazii bila msaada wa Mungu
Bora umpime kuliko kudhania eti watamuacha kwa Kuwa ni aged, maisha hayapo hivyo.
 
NI ya ukweli au ni ya Kutunga? Plz tell me ni ya Kutunga ..
 
Dah inasikitisha sana. Mungu atunusurie vijana wetu. Na mm nina vijana watatu nataka wakikua sileti dada wa kazi wapambane wenyewe na kazi maana nahisi watamsarandia au nilete mmama mkubwa. Nawaza tuu maana jamani kulea kazii bila msaada wa Mungu
Huko mtaani pia utawafunga dada? Wewe leta dada wa kazi, mpime afya acha wanao wachukue kozi hapo, wengine ndio tulipoanzia
 
Yaani huyo maza naye...
Baaada ya kupata story ya huyo binti alitakiwa kumuondoa mapema.
Huruma imemgharimu
 
Back
Top Bottom