XAVERY LUOGA
“PENDO HURU’
0672493994
EPISODE 18
Walisogea na miale yao ya moto hadi kando na walipo Saleh na Zawadi. Kizuri hadi wakati huo hawakuonekana.
Mioyo yao ilikuwa inadunda mno utadhani ng’ombe ambaye anachinjwa. Walikuwa ni wasumbufu wa roho. Walihemeana wao kwa wao bila kuruhusu pumzi zao kufikiwa na watu waliopo karibu yao.
Jamani kuna watu wanahisia!! Kha!!. Ibo alipofika karibu na kichaka hicho kilichofunikwa na miti midogo na nyasi ngumu, alisimamisha msafara na kutoa hotuba fupi. Hotuba ambayo iliambatana na kusitishwa kwa msafara huo hadi kesho yake asubuhi.
“Vijana wangu!, sasa tupumzike hapa hadi kesho asubuhi. Hawapo mbali hawa washenzi!, kinachonipa kiburi ni huyu Malaya!. Hawezi kabisa kukimbia, mwanamke ni mwanamke tu. Kwahiyo hata kama wakimbie vipi kuna mawili tu. Niwashike au washikwe na wanyama humu wafe wote!, hawana umuhimu kabisa..” Ibo aliishiwa kauli kabisa, maneno yake japo yalikuwa ya ujasili lakini yaliashilia kukataa tamaa. hakuja akitafutacho kipo karibu kumtazama.
Msafara ikaweka kambi mahari hapo. Vijana wawili kutoka nyuma ambao walishikilia mzoga wa mnyama walikuaja mbele ya kiongozi wao na kuanza kuandaa chakula.
Waliweka kabisa kitoweo kwa jinsi shughuli ya kusaka binadamu ilivyonzito. Wakachinja, wakachuna!, wakala na kisaza!!,.
wakapeana majukumu ya kulinda kwa masaa ili kuwa huru na uhai wao. Kiongozi akatangaza kujipendelea.
“Ndaku na Poye!, Mnatosha kabisa. Mtalinda hadi asubuhi”. Akatoa amri Ibo. Hakuna aliyepinga. Aliabudiwa kama Mfalme ajaye.
“Tunatokaje hapa mpenzi!” ilikuwa ni kauli ya Zawadi kuelekea kwa Saleh ambaye macho yake yalikuwa bize kuangalia kinachotendeka na watu hao.
“Mhhh!, hapa tuwe kimya tu!, tuwe wavumulivu Zawadi”. Aliongea Saleh ambaye hakuwa na hata plani kichwani kwake.
Naaam! Dakika chache tu palinuka moshi sehemu ile, tayari ibo na wenzake walishapata msosi. Walikula na kuacha nyama ikiteketea katika mkungu kwenye moto. Walilala karibia wote lakini sio hawa askari wawili walioambiwa walinde usiku kucha. Walikuwa imara sana kwa kipindi kirefu. Walisimama tu. Walikuwa kama masanamu kwa kipindi kirefu.
“Kwaa! Kwaa! Kwaaah!” hatua za askari mmoja wapo zilisogea hadi mahali mwenzake alipo, akamuuma sikio na mwingine kutikisa kichwa kuashilia kwamba wamekubaliana.
Aliyeenda kwa mwingine akaongoza njia kwenda walipo kina Zawadi na Saleh. Alipofika kando akashusha kaniki yake na kumimina kojo la nguvu. Kojo lililonuka harufu ya nyama iliyoozea tumboni.
Baada hapo akapandisha kaniki yake na kurudi alipokuwa mwanzo. Miguu akanyoosha kusini na kichwa magharibi. Akalala askari yule na kumwacha mmoja ambaye yaonekana walikubaliana kuwa wanalinda kwa zamu. Itakapofika mda wa kulala yeye basi atamwamusha mwenzake. Walikubaliana hivyo.
Ikapita punde kirefu kimya kikatawala. Hakuna dalili za kupumua kutoka kwa askari aliyeachiwa zamu. Alipokaa hakutikisika. Alikuwa kimya tu.
“Subiri hapo usitoke!” Saleh alimwambia Zawadi asitoke pale alipo na kuelekea pale walipo wale wakina Ibo.
Akamkagua yule askari ambaye alilala wakati macho yapo wazi. Aliachama tu mdomo wazi macho wazi, alilala kishujaa sana.
Saleh akanyata hadi pale palipo na zile nyama kwenye ule moto akakongowa moja ya nyama yenye unafuu pale, nyingine zilikuwa zinaelekea kuungaua moja kwa moja. Akajihakikishia usalama wa sehemu anayorudi alipofika karibu akaita kwa sauti ya upole.
“Zai, Zawadi!. Pita huku tukimbie!, Usipige kelele!” alimwita Zawadi huku akiwa amekumbatia nyama hiyo tumboni kwake.
Zawadi akatoka kwa ustadi na hatimaye akawa nje ya hicho kichaka. Wakatokomea sehemu nyingine ambayo walihishi ni salama zaidi. Saleh na Zawadi sasa waliusogeza msitu bila kuangalia wapi wanakanyaga. Lilikuwa ni giza totoro.
Hakuna tumaini la kufikia mbele lakini walienda tu. Walienda bila ramani wala mtu wa kuwaongoza. Waliongozwa na hisia wawili hawa.
Walisogea mbele hadi kuona walipo panatosha kabisa kuweka makazi mapya. Wakajificha tena kwenye kichaka wapete angalau chakula kilicholetwa na adui zao.
Hii inaitwa mwombee kheri adui wako. Au wenye misemo yao wanasema mgeni njoo mwenyeji apone. Walifakamia chakula hicho bila kuulizana ilikuwa ni nyama ya nini walikula tu kwa baa la njaa walilokuwa nalo. Mate yao yakawa kinywaji. Walikula kushiba.
“Saleh!, kwani ni dhambi kukupenda?” Lilikuwa ni swali lenye majibu ya kuchanganya sana, swali ambalo wakina Socrates na plato walishindwa kuleta majibu yaliyostaiki.
“Hapana, kwani kuna dhambi gani mimi kukupenda wewe?” Naye sadiki akamuunga na swali lake pasi kumpa jibu sahihi.
Wakajikuta wanasahau wapo sehemu gani. Walisahau kabisa kukumbuka kama wanatafutwa.
Wakazama dunia hile ambayo kwa nchi tofauti na Tegemeo hairuhusiwi kwa vijana chini umri wa miaka kumi na nane. Walizamia huko miaka kenda rudi.
Bahari ikawa bahari, vumbi likawa vumbi, mwezi ukazima na jua kuchomoza. Hatimaye wakazinduka mapema kabla asubuhi kufika. Walijikuta wameenza kulowa kabisa. Maajabu!! Wamelowa!, wamelowaje?!.
“Mvua!” wote wakahamaki kwa pamoja?, mvua itoke wapi msimu wa kiangazi Malindi nzima. Likawa jambo gumu kulifafanua. Walianza kutapatapa kulowa na mvua hiyo ambayo ilionesha haina utani kabisa. iliamua kunyesha.
“Khaa!” wakainuka pale walipo wakikumbatiana kwa baridi. Waliona haya kwa hali waliyojikutanayo Ahsubui hiyo. Kulianza kupambazuka.
Zawadi alishamtunuku Saleh penzi usiku ule, naye Saleh alishaonesha makucha yake kwenye pendo la Zawadi. wote walikuwa si haba. japo hakuna mzoefu kati yao lakini walifanya tosha kuwaridhisha. Wakazoeana sana. Wakabaki kukumbatiana tu.
“Saleh wanakujaa!” Zawadi alipiga kelele za kumshitua Saleh, lakini kelele hizo ziliwakuta hadi wakina Ibo na kufanya wao kuonekana.
Hawakujali mvua Saleh na Zawadi tayari walishikana mikono kuanza safari ya kumkombia adui huku unaonekana. Walijitahidi sana kukimbia kadili ya uwezo wao.
Hawakuwa karibu karibu kusema kwamba labda wangewashika kwa urahisi. Walionekana kwa mbali sana. Ikawa nafuu kwao kupata na nafasi ya kupumua japo kwa dakika. Japo Zawadi alikuwa anakimbia kwa 'kusokwa', kufa kupona lakini yeye alikuwa anaona raha tu. Yupo karibu na mtu anayempenda. Hakuwa na shaka kabisa Zawadi. alishaanza kupenda hii michezo ya kukimbizana.
Ibo na askari wake waliotambulika kama mashujaa Malindi, waliendelea kuzifuatilia hatua za wawili hawa kila pande. Walikuwa usawa mmoja lakini umbali tofauti. Waliwaona tu waleee!. Wakakaza mwendo na kwenda mbele.
Kwa upande wa Saleh na Zawadi wao walikuwa hawajui wanaenda wapi. Walizunguka tu msitu mzima pasi na sehemu ya makazi ya watu kutokea.
Walizunguka sana. Na hatimaye Zawadi kukataa pumzi. Akakaa chini akisubili mapigo ya moyo yakae sawa. Alichoka Zawadi. Presha ikapanda kwa Saleh. Hakuna na la kufanya. Akaanza kubuni mbinu za kuwachelewesha wanaowatafuta.... Jamani mwanamke vitani? [emoji849] [emoji849].
ITAENDELEA Episode ya 19.
Join Group SAYARI YA SIMULIZI
SAYARI YA SIMULIZI 🗺
Starxav