XAVERY EMMANUEL LUOGA
“PENDO HURU’
0672493994
EPISODE 21
SEHEMU YA TISA.
Patashika nguo chanika!.
Saleh, Sadiki na Zawadi wakatimba hadi karibu na kasri ya mfalme. Kila mmoja alikuwa na roho ya uchungu ya kufanya mapinduzi Malindi. Saleh, hakutaka tena kushuhudia mauaji yanayoendelea kutoka kila siku pasi wananchi kujua. Sadiki naye hakutaka kabisa kuona uhuru wa Malindi ukiendelea kupeperushwa mbali na upepo wa utawala mbovu. Zawadi naye ni mapenzi tu. Yeye alibeba bendera ya upendo. Mwenye haki na apende. Tena apende bure pasi na sarafu ya rushwa au kikwazo kingine. Watatu hao wakabeba mapinduzi ya miaka zaidi ya miamoja toka kujulikana kwa Malindi. na sasa walikua moto wa kuotea mbali.
Naaaam!, wakaingia hadi ndani ya himaya ya mfalme, hakukuwa na mlinzi hata mmoja mlangoni. Ikashangaza. Lakini ilikuwa hauweni kwao. Wakasogea hadi karibu na mlango wa kuinglia ndani. Nako hakuna hata dalili ya kuwepo na mtu.
Zawadi akasogeza mlango kuangalia kama kuna watu ndani. Mlango ulikuwa ni mwepesi kufunguka. Akafungua lakini ndani hakuna mtu.
“Zawadi, Dada Zawadi!, wapo Mbio ndefu!” Mmoja wa mfakazi wa kasri ya Mfalme ambaye pia alikuwa ni mpambe wa Zawadi alikuja akitokwa na mbio hadi walipo.
“Wanafanya nini!” aliuliza Zawadi kutaka ufafanuzi.
“Wamekusanyika wote. Sasa wanakaribia kujaa uwanja. Kumechafuka!” alitoa taarifa.
“Na wewe kwanini upo hapa!” aliuliza Zawadi maana kama wote wapo uwanjani kwa nini amerudi.
“Ramani. Nimeambiwa nije nichukue ramani.”
“Ya wapi? Na ipo wapi?”
“Ya Malindi nzima. Ipo katika chumba cha Mfalme.”
“Unapajua ilipo?”
“Hapana nimeelekezwa na Mama, nije kuchukua.” Alijieleza kadili alivyoulizwa.
“Subiri!”. Akatoa amri Zawadi na kuingia ndani pekeyake. Dakika sita mbele akatoka na karatasi.
“Ndio hiyo?” akahoji saleh, hakujibiwa.
“Twende!!” likatoka tamko kutoka kwa malkia. Wote wakamfuata, kuelekea uwanja wa Malindi.
Uwamja wa Malindi wa Mbio Ndefu upo mita chache sana karibu na lango la hemaya ya mtukufu Mfalme. Uwanja ambao hushughulisha shughuli nyingi kijijini Malindi. Vikao vyote vya kijiji na matamasha mbalimbali yote yalifanyika huko. Leo kulikuwa na kikao cha kijiji kizima. Siku zote zilikuwa za kushurutishwa kwa kufanyishwa kazi za kuzalisha mazoa bila idhini yao na hatimaye robo ya mazao hao unapeleka kwa Mfalme. ilikua inakera kuliko maelezo, nilime mimi ale mfalme?, Hapanaa!.
Leo uwanja ulipoa mno. sura za huzuni zilitamalaki kila kona. Msiba!, kulikua na msiba.
Wenye mchozi wa karibu tayari ushawatoka hadi kukauka, mwenye sauti kubwa alilia hadi ndege kupeperuka. Mwenye mashetani yalipanda hadi kufika mbinguni. Kila mtu alishiliki huzuni hii kadili awezavyo ilimradi tu iwe imemgusa.
Mbele kabisa ya jukwaa kulikuwa na sanduku ambapo watu walishatangaziwa kuwa aliyekuwepo humo ni mtukufu Mfalme. Mfalme alifaliki mda mchache kabla ya mkusanyiko huo, inaonekana kwa uzee wake alfaliki pindi tu aliposukumwa na Zena. alikufa mazima mfalme.
Pembeni yake alikuwepo Mama Zawadi. Mke pekee wa Mkubwa wa Marehemu Mfalme Bana. Alikuwa mwingi wa chozi pembeni ya sanduku alikolala mume wake. Alikuwa na jambo zito la kusema siku hii.
Mda huo tayari Saleh, Sadiki na Zawadi walishatia timu. Wote walisimama kuendelea kusikiliza na kuona waliyoyashuhudia. Bado hakukuwa na taarifa sahihi walizozipata watatu hao kuusu Mfalme. Walikuwa hawajui taarifa ya kifo.
“Dada, mama anasubiri ramani!” yule Binti alitoa dukuduku lake baada ya kuona Zawadi ameshikilia ramani na hana mpango wa kusogea mbele. Alikuwa anachezesha tu kichwa cheke kumtazama Baba yake ambaye alihisi anakisasi nae lakini katu, hakumuona. Akampa ramani yule Binti. Mbio kuelekea mbele hadi kwenye jukwaa. Akampa ramani mama zawadi na kisha kushuka chini ya jukaa. Mama Zawadi alisubiri ramani ili amwage Mchele hadharani.
Mama Zawadi alichukua mda kabla ajaanza kuzungumzia ukweli wote uliomuhusu. Alikuwa na funda la siri moyoni ambalo lilidumu kwa kindi cha utoto hadi ukubwa wake. Leo lilimshuka kueleza ukweli. Akaanza kuongea baada ya kufuta machozi yaliyoanza kukauka. alilia hadi mara saba, uso ulimkauka kwa kukosa chozi la nane.
“Salamu tena ndugu zangu wa Malindi” alianza kwa salamu lakini hakuna aliyeitikia. Umati uliipisha salamu hiyo na kutoweka angani. Kimya kikatanda.
“Mnisamehe sana kwa kugoma kuongea toka mwanzoni. Nilichokuwa nakisubili ni hiki hapa!” aliinua ramani juu na kuonyesha bila kufungua. Akaendelea.
“Napenda kutoa historia hii kama ifuatavyo. Kitakacho funguliwa humu, ndio kitafunguliwa pia mioyoni mwenu!” baada maneno hayo umati ulishituka. Ukaanza kunong’ona kwa sekunde kisha kuwa kimya. Saleh, Sadiki na Zawadi macho na masikio yao walielekeza juu ya jukwaa.
“AH!, Ndugu zangu wa Malindi. Kijiji chetu kipo ndani ya nchi ya Tegemeo. Ilo kila mtu analijua.!” Aliongea tena akipisha mate yaingie vizuri kooni na kuendelea. Alikuwa na hofu Mama Zawadi.
“Kwaramani, hiki ni kijiji ambacho kimebarikiwa kuwa na maliasili nyingi sana, ikiwemo madini, mafuta na msitu mkubwa wa Malindi. Tuachane na madini pamoja na mafuta kwa maana hakuna mwenye utaalamu wa kufukua vitu hivyo!. Tuje hapa kwenye msitu.
Mwanzo kabisa wa utawala wa nchi ya Tegemeo kulikuwa na vita vikubwa sana. Vita ambavyo viliusisha vijiji takribani nane, vijiji vyote Vilikuwa ndani ya utawala wa nchi ya Tegemeo.
Vita hivyo vilihusishwa katika kugambania kijiji chetu cha Malindi. Lengo kubwa ni umiliki wa mali hizi tatu nilizozitaja hapo juu. Mali mabayo iliwavutia vijiji vingi ni kuwa huu msitu wa Malindi kuwa na ukaribu na kijiji chetu.
Msitu huu ni wa asili!, haujapandwa. Hapo mwanzo Inasemekana ulikuwa mdogo tu, ulitenganisha baina ya vijiji vyote nane. Mapambano yaliyoendelea kutoka katika dhama hizo yalisambalatisha kila kijiji na kubaki na kijiji cha Malindi pekee.
NINA maana kwamba wanamalindi waliungana na kupambana na vijiji vingine saba na hatimaye kushinda. Malindi ilisambaratisha kila kijiji. hatimaye tukabaki wenyewe nchi nzima.
Toka hapo vijiji vyote saba havikuwahi kuonekana tokea hapo na msitu ulizidi kuwa mkubwa na tishio. Jambo lisiloaminika ni kuwa, eti msitu huu wa Malindi pia ni muunganiko wa vijiji vingine saba vilivyopotea kwa utata. baada ya vijiji hivyo kuwa havina watu basi msitu ulisambaa hadi huko. hakuna aliyewahi kutoka nje ya Malindi. pia inasemekana pia, jambo la kukua kwa msitu ni ghadhabu za mizimu ambazo zilikasilika baada hakuona vijiji nane vinataa ya kumwaga damu.
Hivyo dhana ya msitu wa ajabu ilianza kutokea toka kipindi hiko cha mababu.” Aliishia hapo Mama Zawadi na kugawa ramani hiyo kwa mtu aliyepo karibu ili kushuudia anachokiongea. Kisha akaendelea.
“Ah toka hapo Malindi ikabaki kuwa Malindi ya amani tele. Utawala ukarishishwa na kulisishwa. Matambiko kadhaa yakawa yanatolewa mwanzo kabisa wa msitu huu. Ilikuwa jadi yetu. Labda nisiende mabli sana. Ngoja nieleze kipindi hiki ambapo hata mimi nilikuwepo.
Mwanzoni kabisa baada ya kuzaliwa mimi, wazazi wangu wote wawili walifariki kwa ajali ya moto. Nilikuwa nje ya nyumba wakati inaungua. Sikujua sababu wala chanzo cha moto huo. Ila tu ni mapenzi mabaya ya baadhi wa watu.
Baada hapo nikaenda moja kwamoja kushi kwa Mzee mmoja hizi jina lake alikuwaaa… anaitwaaa… ah!, eeeh! Bi Mpembe. Huko nilikuta pia anaishi na kijana mdogo rika yangu naye alikuwa ni wa kike.
Tuliishi kwa kupewa kila kitu kwa usawa lakini kama mjuavyo chuki haimtupi mtu. Nikakumbwa na chuki. Nikamchukia mwenzangu kwa kuwa alikuwa na baati sana kuliko mimi. Alikuwa na umbo nzuri sana la kuvutia kama Zena, ila yeye alikuwa mtoto mtoto.
Basi siku moja tukapata tenda ya kwenda ya kwenda kusafisha nyumba ya Mfalme. Wote tukawa mstari wa mbele kwenda kufanya usafi huko. Kwa bahati nzuri mwenzangu alielewana vizuri na Mfalme na hatimaye akawa naye na mahusiano na kushikishwa mimba. Kwa woga wa mizimu akatoroshwa mbele yangu na kupelekwa kuishi mbali huko ambako taarifa niliyoipata kuwa aliaambiwa atoe hiyo mimba lakini alizaa.
Mimi nikampiga gepu kwa kuwa karibu na Mfalme kama mjakazi wake lakini sikufanikiwa kumuingilia kimahusiano. Siku zikapita chache sana Mfalme Bana ambaye ndiye baba wa Mfalme huyu alipoteza maisha na utawala ukabaki kwa mtoto wake wa pekee wa kiume ambauye ndiye huyu hapa chini.” Zawadi alishituka baada ya kuona Mama yake anaonyesha sanduku lile.
"Baba amefariki?" alijiuliza Zawadi, alianza kukosa nguvu. Saleh akachukua nafasi ya kumliwaza. Akapoa kidogo na Wakaendelea na kusikiliza taarifa ngeni masikioni mwao juu ya ubinafsi wa mke wa Mfalme Mama Zawadi....
JIUNGE na kundi la SAYARI YA SIMULIZI FACEBOOK KWA TAARIFA ZAIDI KUHUSU SIMULIZI MBALIMBALI: VITU VINGI NITAWEKA HUKO.
SAYARI YA SIMULIZI 🗺
..........
Naam historia Mpya inaanza kutengenezwa Malindi.... tukiwa katika sehemu za mwisho mwisho. mchango wako ni muhimu sana....
ITAENDELEA....
Starxav