XAVERY EMMANUEL LUOGA
“PENDO HURU’
0672493994
EPISODE 15
Naaaam! Askari wakaitika wito na kupanga mstari mmoja. Ibo akachukua nafasi yake na kuamlisha na kusubiri amri kutoka kwa mfalme, lakini cha kushangaza Mfalme hakuongea chochote kile zaidi ya kuondoka zake.
Alishamkabidhi ila kitu Ibo ambaye ndiye kiongozi wa Msafara. Alishajua Ibo iwe mvua au juwa, kifo au Mateso lazima Saleh na Zawadi wapatikane.
Wakatawanyika eneo la tukio. Wakaondoka mashujaa wale kutafuta kitu walichoagizwa. Walibaki askari wachache sana kwa ajili ya ulizi wa mfalme. Hawakuondoka wote.
**********
Dakika mbili mbele kukawa na ugeni katika kasri ya mfalme, walikuwa wageni rasmi kwa mfalme alfajiri hii. Sadiki akiwaongoza Mama na Baba Saleh, Mama na Baba yake, pamoja na Sala mke wake.
Aliwaongoza kuonana na mtukufu mfalme ambaye amewashikilia ndugu yao. Walikuja kwaajili ya kuomba msamaha na kuomba kupunguziwa kwa adhabu mtoto wao.
Sawa ni jambo jema lakini walimkuta Mfalme akiwa na hali mbaya sana. Mfalme alikuwa katika hali ya hasira. Hakuelewa na wala hakuwa na mswalia mtume. Akashika mbuzi zote zilizosogelea eneo lake la mazao. Akafungia ndani.
“Lakini Baba siye hatujui kabisa kuhusu watoto!, mguu hu ndio ulikuwa kuwaombea Baba” alikuwa mama na Sadiki ambaye alionesha huruma ya uzee wake mchanga kwa Mfalme.
“Eh Baba, tunakuomba utuondoe hapa. Na sisi tukawatafute baba, wakipatikana tutawaleta” Mama Saleh naye aliitikia wito wa Mama Sadiki, vidume vilifungwa mbali kidogo. Havikuwa na neno kwa muda hule vilitafakari tu laana ambayo watoto wao wamejizolea kwa kukosa heshika hata kwa Mfalme wao. walishapata habari kuwa Saleh ametoroka na binti ya mfalme.
“Hakika hamtakuwa sawa katika maisha yenu hapa Malindi mpaka mtoto wangu apatikane” Mfalme alihitimisha ibada ya sadaka hiyo kwa umati huo wa familia.
Aliwapasha kuwa wanayemtolea msamaha ametoloka. Amejiongezea mashitaka, hivyo wakashikiliwa wazazi wake kwa dhumuni kuwa hana pa kukimbilia. Na kama Saleh akisikia wazazi wake wameshikwa kwa mfalme basi atarudi tu. Akawaweka na wazazi hao katika mateso. Mfalme alikuwa zaidi ya Shetani. hakuwa hata na kumbukumbu kuwa mmoja kati yao ni Mke wa mtoto wake wa kiume. hakujua kabisa.
************************
Mashujaa waliotumwa sasa waligawanywa kila kona ya Malindi. Kuna baadhi walienda moja kwa moja nyumbani kwa kina Saleh. Hawakukuta mtu muda huo. wakafika bustanini; hakukuwa hata na alama ya jembe kwa siku hiyo. Wakarudi walikoahidiana kukutana.
Wengine safari yao iliwapeleka hadi nyumabani kwa kina Sadiki, walikuta kuku tu ndio kiumbe pekee chenye uhai. Hawakukuta mtu yeyote. Wakati huo wakina Sadiki Mama na Baba Sadiki na Saleh walishatoka na kuelekea kwa mfalme. Walipishana na Mashujaa hawa ambao kila mmoja alikuwa na usongo wa kuwashika watuhumiwa ili kuongezewa cheo.
Kila mmoja alikuwa shuta kuliko mwenzake. Nao wakarudi sehemu ambayo waliahidiana watakutana. Wakaungana na waliowakuta.
Kundi lingine Lilikuwa linawasaka nyumba hadi nyumba. Walipita karibu kijiji kizima kwa sekunde tu.
Haraka zao ziliwakaribia hadi Mama na mwanae Zena. Nao wakapata taarifa. Walikuwa wamejiziuka, hawana kazi ya kufanya Mama na Mwana, walijadili mambo ya ngono tu kama msingi wa familia yao. Mama alikuwa fundi, mtoto mrejesha vifaa. walijenga na kubomoa. Waligawana Malindi nzima.
Baada ya Mashujaa hao kuhakikisha kuwa hakuna wanachokitafuta nyumbani humo wakatoweka.
Zena akasongamana nao kwa kuwavizia apate upenyo wa kuwafuatilia wanaelekea wapi Mashujaa hao.
Zena aliumia juu ya taarifa za kushikiliwa wazazi wa kina Saleh. Hakujali nafasi yake kwa Saleh, alitoka mbio kuelekea kwa mfalme. Afanye njama zozote zile kuhokoa jaazi hili. wanasema ukubwa Dawa. Zena akacheza na akili zake. akajua tu kaka Saleh alishikwa na Zawadi na wametoloka. basi wazazi wake wameenda kwa mfalme bila kujua Saleh ametoloka.
Kwanza aliwafuatilia mashujaa hawa hadi walipokutana. Aliwasikia tu wakijadili kuwa wanaenda katika msitu wa Malindi kuhakikisha kama wamepotelea huko, baada ya kuwakosa kijiji kizima.
Walitaka kuivalia njuga suala la Mfalme kwa kuwapata popote pale wakiwa hai au wamekufa.
Zena akawaacha watu hao waende huko msituni na yeye kuelekea kwa mfalme ambapo aliamini kuwa kama wazazi hao watathubutu kwenda kwa Mfalme basi watakuwa wameshikiliwa huko.
Akashika njia Zena kwenda kwa Mfalme. Kichwani kwake kulikuwa na akili mbili tu. Moja ni wapi alipo Saleh ambaye Inasemekana amekimbia na Zawadi. Pili ni wapi walipo wazazi wa Saleh na Sadiki ambao wanatafutwa kila kona Malindi na hawapatikani. Akili ya Zena ilimtuma kabisa kuna kitu katika nyumba ya mfalme. Akatumia fursa ya kuwa karibu na Mfalme na kwenda kufanya utafiti huko.
Kwa kuwa alikuwa mwenyeji katika kasri ya Mfalme ikampa nafasi ya kujongea hadi lango kuu la mfalme. Kwa uzoefu wake wa kulala na wanaume wengi ulifanya wanaume wengine wawe dhaifu kila wakimwona Zena. Akatumia vema umbo lake kuwashawishi askari waliopo kando ili wamdokeze kwa undani nini kinaendelea Malindi.
“Ahya!, niambie” Zena alimuuliza kijana mmoja ambaye alimbanza nyuma ya ukuta wa Kasri la Mfalme karibu na mlango wa ndani.
Alimshawishi kwa kumuahidi iwapo atasema basi usiku huo watakuwa wakilinda wote. Watalala pamoja na hato sita kumpa penzi lake. Mkate ule wenye viungo vigumu ulishawishika na kuwa mlaini kabisa mbele ya supu Zena. Akaeleza kila kitu.
“Mfalme anamtafuta Binti yake ambaye ametoweka kusiko julikana na Saleh!, pia wazazi wake na Sadiki na Saleh wamefungwa katika upande ule wa lango la kulia. Funguo za lango hili anazo mfalme. Hajamuamini kijana wowote” kijana huyo akajieleza. Alijieleza alipoona Zena ameshajitoa tayari kuwa karibu naye.
Zena aliumia sana baada ya kupata uhakika wa kweli Saleh na Zawadi wamekimbia pamoja.
“Yhani! Da Zawadi amekubali kumkimbia baba yake sababu ya mapenzi?, Hmmm! Hapa sina changu. …. Uhhh!, sijui hata nifanyaje!, lakini ngoja” Zena aliona kabisa kiwango cha mapenzi ambacho anamuonyesha Saleh hakitoshi kabisa kama kiwango ambacho ameshamuonesha Zawadi. Alikata tamaa Zena, akainua mguu wake pale.
“Vipi ahadi yangu!” yule kijana alimsimamisha Zena, alikuwa anaulizia ujira wake amabo ameahidiwa. Zena akarudi hadi pale alipo yule kijana. Alimpa busu tu la mdomoni na kumnong’oneza sikioni.
“Baadaye!” akaondoka zake Zena. Ulikuwa Mguu wa Mfalme.
Aliupigisha kwata kumtafuta mfalme. Moja kwa moja kukalibia ndani kabisa. Akafungua mlango lakini ulikuwa mgumu. Akasukuma tena, bado ulikuwa mgumu.
“Umefungwa!, wapi upo baba!” Zena aliongea peke yake. Alikuwa na mawazo ya mapinduzi sasa. Alitaka kufanya jambo la hatari muda hule. Kilikuwa ni kisasi cha mapenzi yake kwa utawala huu.
Akazunguka nyuma ya nyumba hii ya mfalme iliyopo ndani ya eneo la utawala. Akamwona mfalme akikoroma kando yake.
Alikuwa amesinzia kabisa Mfalme. Alikuwa peke yake bila mlinzi. Mlinzi aliyemuamini tayari alishika njia kuelekea msituni kusaka Binti ya Mfalme na Saleh. Mfalme alilala uzingizi wa mawazo. Mboga ilichacha. mke wake alimfungia ndani kwa kosa la kumtoa binti nje ya kasri, mtoto wake wa pekee ametokomea kusikojulikana. aliwaza adi kupitiwa na usingizi.
“Baba!” Zena aliita huku akimpapasa Mfalme kama anaweza kupata funguo. Alimpapasa hadi Mfalme kuzinduka katika usingizi.
“Zena unafanya nini hapa?” Lilikuwa swali kwa Zena. Mfalme alishitushwa na ujio wa Zena kwa wakati ule. ilikua sio mida yake. Alitaka kujua.
“Jamani Baba, na siku nyingi mno sijakuona!” alilegeza sauti Zena. Mfalme akabaki kudawaa kama kijana mdogo aliyelishwa parachichi.
“Sio wakati wake huu mama!, nitamuwagiza mtu!” aliongea Mfalme akiwa bado macho yake yasiganduke kiononi mwa Zena.
“Baba bhana!, mi hadi nimekufuta!, ba-abaa” alizidisha manjonjo Zena. Alishamteka Mfalme.
Maisha ya Zena yalikuwa katika uzinzi mzito, mara kadhaa alishashiliki ngono na Mfalme. Tokea kwa mara ya kwanza Zena anatangazwa ndio kiongozi wa utamaduni kwa upande wa kike basi alikuwa na wakati mzuri sana wa kulala na Mtukufu Mfalme kwa siri. Alilala naye sana bila mtu yeyote kushitukia siri hii.
Ilikuwa siri nzito ambayo hata Mama Zena na yeye hakuifahamu. Ulikuwa wakati wa Zena kwa Mfalme......

.....
Naaam. Zena mikononi kwa Mfalme kutaka kuwafungua Wazazi ws kina Saleh na Sadiki. Je ipi hatma kwa penzi lake na Saleh. Oya wanangu Saleh njoo huku Mama kashikwa na Baba yako et, mwambie na Zawadi Mama mkwe wake yupo kifungoni.... Swali ni Je wapi wanapatikana kina Saleh na Zawadi?.
ITAENDELEA .....!
Starxav