Simulizi: Pendo Huru

Simulizi: Pendo Huru

XAVERY LUOGA
“PENDO HURU’
0672493994

EPISODE 16
Maisha ya Zena yalikuwa katika uzinzi mzito, mara kadhaa alishashiliki ngono na Mfalme. Tokea kwa mara ya kwanza Zena anatangazwa ndio kiongozi wa utamaduni kwa upande wa kike basi alikuwa na wakati mzuri sana wa kulala na Mtukufu Mfalme kwa siri. Alilala naye sana bila mtu yeyote kushitukia siri hii.

Ilikuwa siri nzito ambayo hata Mama Zena na yeye hakuifahamu. Ulikuwa wakati wa Zena kwa Mfalme...

“AAh! Zenaa!” alianza kuweuka Mfalme. Usingizi ule wa mwanzo ukamtoka. Akabaki na uzee wa matanio kwa kijana mwenye rika ya watoto wake. Akashawishika Mfalme.

“Baba kweli nimekumisi!” Zena aling’ata na kucha zake kwa ulegevu kabisa kummaliza Mfalme.

Mfalme naye akaingia kingi. Alishapata hamu muda ule. Alikuwa hajapata mambo haya kwa kitambo sasa. Mke wake mkubwa ndio huyo amemfungia ndani kwa makosa ya kuruhusu Binti yake kutoka na mwanaume nje ya eneo la utawala. Nani atampa?.

“OOuh! We mtoto!” Zena tayari alikuwa ameshika ikuru ya Mfalme.

Sasa alikuwa mtawala mkuu, alicheza kila kona. Japo kuwa Mfalme hakuwa na nguvu zile za kusimamisha mti wake mkavu sababu ya uzee lakini alijitahidi. Akasimamisha Mtukufu Mfalme. Uchizi ulipomkolea akaangusha hadi funguo. funguo ya sehemu ambapo Wakina Sadiki wamefungiwa.

“Yes!” kiingereza kikamtoka Zena. Alijipigia makofi mwenyewe moyoni kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Alikuwa anahitaji funguo tu. Na akaipata. Mfalme hakuwa na akili tena wapi yupo na nini dhumuni la Zena. Alijuwa tu Zena yupo hapa kumpa burudani ambayo ameikosa kwa kitambo sasa. Akaendelea kuchizika.

Zena akaendelea kumchezea Mfalme pasi kuona kabisa anafikia hatua ya kutojiweza. Akaokota funguo na kuzikamata kisawasawa kiganjani mwake. Alikuwa anatabasamu sasa Zena. Akawa anatafuta sasa gia za kutoka pale. ni jinsi gani atamtoroka Mfalme.

“Ooh!, baba! Samahani. Nomba kwanza nifanye kitu.” Akajichomoa Zena mikononi mwa Mfalme. Mfalme akagundua kitu. maana toka toka ya Zena ilikuwa ya kushangaza.

“Naomba nikakojoe kabisa Baba!” aliomba Zena baada ya kuona Mfalme anajirudi katika hali yake ya kawaida.

“Ukakojoe?!” aliuliza Mfalme huku akikaza macho mkononi mwa Zena. Aliona ameshika kitu.

Akatabasamu Mfalme. Akanyanyuka pale alipokaa na kumsogelea Zena mabaye bado alikuwa anajiamini kupita maelezo. Mfalme akapitisha mdomo wake katika shingo ya Zena bila kusema chochote, alikuwa kama mtu anayenusa hivi, au mtoto atafutae pingili ya nyonyo kwa *****.

“Hunukii kujiandaa kabisa yani!” alisema Mfalme. Alisema hayo baada ya kuona Zena hanukii chochote kile.

Mara kadhaa Zena anapoenda kutoa mapenzi kwa Mfalme basi kuna manukato ambayo Mfalme anayependa sana. Anapaka hayo kumvutia zaidi Mfalme. Lakini kwa pale alikuwa mtupu Zena. Alisahahu kitu hicho kama kipo akilini mwa Mfalme.

“We bado ni mtoto mdogo sana!, uanataka kuniteka nipoteze dhima yangu?” aligutuka Mfalme. Sasa alikuwa anampa makavu Zena. alishajua Zena kwanini yupo pale kwa wakati hule.

Zena lilimshuka, hakuna alichojivunia tena. Mwili wake ukashuka thamani ghafla kama sarufu zinazoshinda na dora. Akapoa zena.

“Haya leta!, leta hizo funguo!” alimuomba Zena kwa upole tu. Zena akaendelea kuwa kimya akiwa amezishika funguo hizo bila kuziachia. Alikuwa anatafakari nini afanye ili apate anachokiitaji. Akaona hana thamani tena kwa Mfalme. Akaamua kumpotezea. Hakumpa funguo Mfalme.

“Funguo!” alirudia tena Mfalme huku akikazana kufungua mkono wa Zena uliobana kisawasawa.

Hakutaka kuachia Zena. Alikomaa na shoo. Kwa kuwa Mfalme hakuwa na nguvu za kiushindani kutokana na umri. Akazidiwa. Akataka kutumia nguvu.

“Nisamehe Baba!” Zena alitamka kauli hiyo kuashilia liwalo na liwe. Hakuona tena nafasi yake kwa Mfalme. Akaamua kukisanua.

Akavaa roho ya Mama yake wakati yupo kijana. roho ngumu isiyo na huruma. Akamsukuma Mfalme.

Alimsukuma kwa kutumia mikono yake yote miwili. Mfalme hakuwa na hiyana, alielekea upande uliopo karibu na kiti chake alichokalia. Hakuwa na nguvu za kujizuia. Akaegeza kichwa sehemu kilipo kiti. Akaanguka vibaya mno bila chembe ya damu. Mfalme akawa kimya ghafla palepale chini. hakupata muda wa kupumua.

“Maamaaa!” alijisemea Zena huku nafsi yake ikimsuta. Aliona hali inaanza kubadilika pale. Upepo mbaya umempitia.
akashika njia kuelekea sehemu ambayo alielekezwa ndugu wa kina Saleh wameshikiliwa huko.

Kwa haraka akafungua mlango. Kweli!. Walikuwako wote. Mama na Baba Sadiki, na Saleh, pamoja na Sala. Hakuwambia neno lolote lile hadi akawafungua. Ingawa walikuwa na maswali mengi sana. Lakini yote hawakupata majibu.

Zena alikua na kisasi cha moyo. aliwasaidia tu kuwatoa hapo na si vinginevyo. hakuja kupiga hadithi.

Walimfuata mzoefu Zena hadi kutoka katika eneo hilo. Atimaye wakapita vichochoro hadi nje ya hekaru. Wakapita na vinjia vya mkato hadi huko mabondeni. yule askari aliyepewa ahadi na Zena aliwaacha tu. alikua pekeyake pale na kina Zena walikua zaidi ya sita. akawaacha.

Zena alijitosa kuwatorosha. Alikuwa na maana yake. Alileta uhuru wa watu hao, wakajichimbia huko mashambani kwa muda. Zena hakurudi kwao.

“Mimi naona sasa!, hakuna kitu cha kuficha tena!, nitaweka ukweli hadharani!.” Mama yake Saleh alitoa la moyoni kuelekeza kwa wenzake. walikuwa katika gofu walilofichwa na Zena.

“Mama, Malindi inahitaji mabadiliko sasa.” Zena naye akafuata kuunga mkono. alibadilika Zena, akili za ngono zikawa za kishujaa.

“Mwanangu sijui huko alipo kama bado yupo hai” Mama Saleh aliendelea kuongea. chozi lilianza kumruka.

“HMmmm!, kwa njama za kina Ibo nilizosikia, hapa ni dua tu Mama Sizani.” Alijibu Zena. aliwaona pindi walipo kutana katika mkutano, wakiwa wanaelekezana jinsi ya kufanya.

“Na kama wakimuua mwanangu basi wameua kizazi chote cha kina Bana!” alilopoka Mama saleh.

“Mama, unaongelea nini!” Sadiki hakuelewa kabisa. Akabaki njia panda.

“Utaelewa tu mwanangu. Mda umefika sasa. Kama wanataka kuniua na mimi sawa. Nimeshakula chumvi nyingi sana. Kwa sasa anaenda tena kijijini.

Napita nyumba hadi nyumba kuhakikisha watu wanajua siri hii na wanafanya mabadiliko Malindi. Manyanyaso yamezidi. Watu wanapotea bila hata taarifa. Malindi imekuwa sehemu ya ajabu ajabu sana”.

“Mh!, Mama, Watakuua kweli!” Zena alipinga wazo la Mama Saleh.

“Mwanangu utajua tu pindi mapinduzi yakifanikiwa. Niruhusu mimi nitoke”.

“Mke wangu, nipo pamoja na wewe. Tutetee huu ufalme usije kuhangamia. Maana anayekuja sijui kama tutapona” Baba Saleh naye aliungana na Mke wake. Alihofu utawala kupewa mtu asiye stahiki.

“Lakini mimi….. da!, yani hadi nachanganyikiwa. Sina hakikia kama.. kama… Mfalme atakuwa hai!” alitoa kauli iliyofanya kila mmoja kumuangalia. Alianza kulia Zena. Aliogopa kufa kwa kesi ya kuua.

“Kwanini?” sadiki akawai kuuliza.

“Nakumbuka nilimsukuma mara ya mwisho na wala hakuamka nilipokuja kuwafungua nyinyi, sasa sijiuiii…” aliongea Zena kwa hofu.

“Masikini. Asife kabla ya kumjua mtoto wake!” aliongea nusunusu Mama Saleh. Sadiki akashituka. Lakini akawa kimya tu.

“Saleh ni mtoto wa mwisho wa kiume wa Mtukufu Mfalme Bana!” Mama Saleh sasa aliweka bayana kila kitu. Mama sadiki, Baba Sadiki, Sadiki na Sala wakashituka. Hawakutarajia maneno kama hayo wakawa na rundo la maswali vichwani mwao. Lakin Baba Saleh alishalijua hilo.

Naaaam! Akawaweka sawa kuhusu suala hilo la kwanini Saleh ni mtoto wa Mfalme.

kiwehuwehu kikawapanda na kukubaliana kuondoka hapo na kusambaza habari hiyo ifike Malindi kote. Ili popote alipo Saleh ajue kuwa mapinduzi yameanza.

Pia kama Mfalme yupo hai basi apate taarifa hizi. Wote walikubaliana kufanya hivyo lakini Zena yeye aligoma katakata, aliamua kubaki hapo hadi mwisho wa Malindi.

Alijutia jambo lake la kumwangusha Mfalme hadi chini. Alihisi kabisa ameua Zena. Tena ameua mtu mkubwa sana, Mfalme wake na baba wa kipenzi roho yake. Mengi yakamsuta. Akajikuta anajutia peke yake katika jumba hilo. wakamuacha.

Walipotokea nje wakaanza kugawana kupita kijiji kizima kutangaza habari la maandamano na mapinduzi kwa ataye hitaji.

Kiongozi alikuwa ni Mama Saleh. Alibeba bendera ya mafanikio mkononi. Akiipeperusha Malindi nzima. Sadiki yeye aliamua kutimkia Msituni kumtafuta rafiki yake huko. Mama na Baba Sadiki na Sala wao waliungana na Mama Saleh kutangaza mapinduzi Malindi..

Kwa upande wa Mama Saleh yeye alitembea karibia kijiji kizima akiimba na kuwashawishi watu wajitokeze katika uwanja wa Mbio ndefu. Alimtonya kila mtu, hadi viumbe ambavyo havina haki ya kuwa binadamu. Ulikuwa ujumbe wa ushawishi uliofanya kila mtu apatwe na shauku ya kutaka mabadiliko.

“Karibu uwanjwa wa Malindi ushuhudie historia mpya!”
huo ndio ulikuwa moja ya msemo ambayo ulitembea katika kichwa cha mwana Malindi.

Watu wakaacha kazi zao na kujikusanya uwanjani. Walipinga na kuogopa wakabaki nyumbani. Mama Salah akakusanya umati wake na kuweka begani moja kwa moja katika uwanja wa Mbio ndefu. Aliwatoa hofu kuusu Mfalme, kwa maana watu walikuwa wanogopa sana jambo hilo sababu ni ukali na ukatili wa Mfalme.

Mama Sadiki naye alikuja na watu wake uwanjani Mbio ndefu, alikadhalika Baba Sadiki na Sala, wote walikuja na watu. Ingawa sio kila mtu alifika rakini ilikuwa nirobo tatu ya kijiji. Watu walikuja kuona maajabu ya historia mpya ya Malindi. shauku ziliwajaa mikononi mwao.

Sadiki yeye mbio zake zilifika hadi sehemu ya kuingilia msituni humo. Akili zake zilikuwa zinamtuma kuwa wawili hao bado wanaishi na wapo katika msitu huo.

Akafuta kabisa ile dhana ya kutisha kwa msitu huo na kuingia ndani kabisa. Alipokelewa tu na kwato za wanaume wengi ambao alijuwa kuwa wakina Ibo nao wapo humo kuwatafuta Saleh na Zawadi. Akachoma ndani Sadiki iwe yeye au au wawili hao. Lazima watoke wazima. Yalikuwa mapinduzi kila sehemu.

.... Naaaam, MAPINDUZI KATIKA PENDO HURU. Mfalme anaonekana hana Pumzi tena. Zena kabaki mashambani kujutia alichofanya. Mama Saleh ataka Malindi ufahamu sasa historia Mpya. Sadiki ndio huyooo ameapa kufa kupona lazima Saleh na Zawadi wapatikane... Kweli atawapata kwa muda muafaka?

ITAENDELEA ....


Starxav
 
XAVERY LUOGA
“PENDO HURU’
0672493994

EPISODE 17
SEHEMU YA NANE

Saleh na Zawadi waliamua kutoweka kabisa kijijini, waliamua kabisa kuachana Malindi na kutaka kukimbilia kijiji cha mbali. Kijiji cha Malindi kilikuwa na ukubwa wa aina yake. Huwezi kutoka ndani ya kijiji hicho kirahisi rahisi.

“Mpenzi, ni kweli njia ndio hii?” Zawadi alianza kuwa na mashaka juu ya njia iliyopo mbele yao.

Ni kweli walikuwa mbali na Malindi lakini, njia iliyopo mbele yao ilionesha kutisha. Msitu wa Malindi ulikuwa mbele yao. Kwa historia ya mwanzo Saleh alishawai ambiwa na Mama yake kuwa Msitu huo ndio alama ya Udhaifu wa Kijiji chao. Mambo mengi maovu hutendeka mwanzoni tu mwa mistu huo.

Toka histora ya Malindi ishike hatamu haijawai sikika mtu wa aina yoyoyte kuvuka salama katika mistu huo kutokea upande wa pili, hii ni juu ya kutisha kwa mistu huu wa asili.

Ilisemekana ndani ya msitu huo, kuna wanyama wakali sana na mambo ya ajabu ya kutisha. Kabla ya kutoka sehemu ya mwanzoni mwa mistu huo kuna bango kubwa la kuonesha taadhari juu ya mistu huo wa Malindi.

“Zawadi!, hakuna njia, hatuma imani tena na maisha yetu. Bora wewe Zawadi unaweza samehewa, vipi kuhusu mimi? Sina budi kufa kishujaa ndani ya mistu huu lakini si kupata mateso yale niliyokimbia. Zawadi, Nakupenda. Tuwe na imani tu. Tukaishi mbali hiki sio kijiji. Baba yako ni mtu mbaya sana Zawadi” Saleh alionesha yupo katika fikra za kuikimbia Malindi. Mateso aliyopata kutoka kwa Ibo na Mfalme yalikuwa sababu tosha kwa Salah kuondoka.

“Nipo tayari tufe wote Saleh, sina nguvu kwako!” Zawadi naye akajimwaga kifuani kwa Saleh, wakakumbatiana kwa kuianza safari mpya ya kuvuka misitu na kuishi mbali.

Mapenzi yao yalikolezwa na imani ya kweli ya upendo. Zawadi alikubali kuvua taji ya umalkia na kulitupilia mbali. Saleh naye hakuona umuhimu wa Wazazi, hakuwafikilia hata kidogo. Jamani mapenzi kigeugeu!!.

Naaam Miguu yao sasa ikawa ndani ya mistu wa Malindi, misitu wenye historia ya kutisha kijijini kizima. Kila mtu alijua fika kuvuka katika mistu huo ni hatari mno hata kujaribu tu.

Sasa roho za Saleh na Zawadi walikabidhi kwa Mababu zao wawasimamie na kutokea upande wa pili, angali katika historia hakuna aliyewahi kuvuka msitu huo. Malindi ilikuwa Malindi kweli. Kijiji kizima kilivikwa na Msitu Malindi.

Waliipita miti kadhaa kuchanja mbuga kwenye msitu huo. Ilikuwa miti ya wastani, miti halisi kabisa ya kuwakaribisha wageni wote kwa bashasha ya aina yake. Uzuri wa msitu huo ulionekana tu kwa kelele na shangwe za ndege wake kuruka juu kwa kidedea.

kulikuwa hakuna ule upepo unaosemwa na wakazi wa eneo la Malindi kwamba katika msitu huo kuna upepo mkubwa sana. Kulikuwa kimya na hewa ya oksijeni ambavyo vilipokezana tu kuhema.

Zawadi alikuwa mgeni wa kila kitu, alikuwa mtu wa kushangaa tu kila hatua ambayo wanasonga mbele. Msitu ulikuwa ni wa kuvutia hadi kuwafanya kusahau shida za walikotoka.

Walizidi kusonga mbele bila kujali kigiza ambacho ndio kwanza kinaanza kukimbiza mwanga wa jioni kuelekea usiku. Hatua ya Saleh iligusa kitu cha ajabu chini lakini akapotezea na kusonga mbele. Hakutaka kumtisha mpenzi wake kwa kile ambacho amekiona. Wakasonga mbele.

Punde tu Saleh akaona tena kitu cha kutisha, Alichokiona sasa kilikuwa ni mfano halisi wa kile alichokiona mwanzo. Mwanzo aliona fuvu la kichwa cha binadamu, lakini kwa sasa aliona mwili mzima wa binadamu ambao haukuwa na muda mrefu toka utelekezwe. Kwa kutishwa na kitu hicho bado alikuwa na ujasiri wa kumzuia Zawadi asione anachoona yeye. Malindi ilikuwa na maovu nyuma ya panzia, hakuna anayejuwa.

Hatua kwa hatua, huku Saleh kule Zawadi, wote walijitosa katika msitu huu kutafuta njia ya kutoweka Malindi. Hawakujua ukubwa wa msitu ni udogo wa maisha yao. Wakasonga mbele.

“Mamaaaa ah!” ilikuwa sauti ya Zawadi ambayo ililenga kushitushwa na jambo. Mbele ya macho ya Saleh na Zawadi kulikuwa na mizoga mingi sana ya binadamu. Wengi walikuwa wameoza na kubaki mafuvu tu na wengine ndio kwanza wabichi, hawakufua hata dafu ya kuozeana kwa wiki mbili tu. Walikufa angali bado mvua yanyesha. Hawakukauka. miili yao ilikua bado mibichii.

Kilio cha nguvu kikamtoka Zawadi akiwa kifuani mwa Saleh, alijificha kutoona unyama ule wa aina yake.

“Saleh me siwezi!, naogopa!!” Zawadi aling’ang’ana kwa kuomba Saleh afanye jambo ambalo halita mfanya apoteze roho yake mapema kiasi kile. Tamaa ya kurudi nyuma ikaingia..

“Phoooooooo!, Phoo Phonhoooooo!” sauti ya pembe la ngombe ikasikika nyuma yao.
“Wanatutafuta!” Zawadi akaacha kulia ghafla na roho ya ujasili ikamwingia, katu hakuangalia tena ile mizoga ya watu waliotelekezwa pale, akamshika mkono Saleh na kwenda mbele, alijua kabisa sauti ya pembe hilo la Ng'ombe hutumiwa na Ibo ty. tena sehemu za hatari.

“Saleh!!, wakitushika hawa watatufanya kama hawa watu hawa chini. Tukimbie jamani.” Zawadi alizidi kumshika Saleh na kumkokota kama anamlazimisha kukimbia.

Moyo wa Saleh ulishikwa na machungu mazito mara baada ya kuona kuwa mauti ya mamia waliotelekezwa. Mwili mzima ulikufa ganzi. Alikokotwa tu na Zawadi.

Walikimbia mno kuwapoteza wanaowatafuta. Zawadi alishajua mlio ule wa pembe la ngombe ni kuwa kuna watu wanawatafuta na wapo karibu yao, lengo lao la kipiga pembe hilo ni kuwa waliona ishara za watu wanaowatafuta kando, hivyo walipiga ili wakusanyike kwa lengo la kutembea pamoja kwani wapo karibu kuwakamata. Zawadi alijua hili. Alichukua hatua ya kukimbia na Saleh, kufa au kupona kwake. Lazima watoke Malindi.

Kwa binadamu ambaye damu ndio chanzo chake cha uhai, lazima achoke. Binadamu sio mashine. Hiyo iliwakuta wapendanao hawa Saleh na Zawadi ambao walibweteka katika kichaka kimoja ambacho wote waliona salama kujificha walishafika kukaribia nusu ya safari ya kuvuka msitu wa Malindi.

Usiku tayari ulishakaribia katika mboni za binadamu hawa. Kwa mbali waliona watu wanakuja upande waliojificha wao. Walikuwa wamebeba miale ya moto kuwatafuta kwa udi na uvumba.

Walikuwa wanaume wengi sana na wa kutosha. Wote walishiba kisawasawa, lakini hawakutisha sana kama alivyotisha Ibo. Ibo alikuwa haonekani kabisa kwa weusi wake. Japo alikuwa kiongozi wa msafara lakini hakuonekana. Alikuwa mweusi pyuu! Ibo. Ilo hakujali, alichojali ni kupatikana kwa mwandani wake Zawadi na mbaya wake Saleh. Wote walikuwa wanahitajika kwa nyakati mahususi kabisa.

Walisogea na miale yao ya moto hadi kando na walipo Saleh na Zawadi. Kizuri hadi wakati huo hawakuonekana.

Mioyo yao ilikuwa inadunda mno utadhani ng’ombe wa Shinyanga ambaye anachinjwa kutokana na shida ndogo tu, 'Sherehe ya mtoto', Walikuwa ni wasumbufu wa roho. Walihemeana wao kwa wao bila kuruhusu pumzi zao kufikiwa na watu waliopo karibu yao. Vifua vilibana na kuachia... wote walidhibiti pumzi zao kwa Makini...
.........
FUATANA NAMI KATIKA SEHEMU YA KUMI NA NANE YA MKASA HUU...
SAYARI YA SIMULIZI 🗺

ITAENDELEA

Starxav
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom