Simulizi: Pendo Huru

Simulizi: Pendo Huru

MTUNZI: XAVERY LUOGA
SIMULIZI: “PENDO HURU’
NAMBA: 0672493994
@Star_xav

EPISODE 08
SEHEMU YA TANO.

Malindi nzima leo ilizizima kwa ngoma za hapa na pale. Ilikuwa siku ya kusaka mshidi wa utamaduni. Vikundi mbalimbali vilijitokeza kusherehesha shughuli hiyo. Kulikuwa na mashindano mengi sana lakini makubwa yalikuwa ni ya aina tatu tu. Kusaka shujaa wa Malindi, kutapa mwimbaji na Mchezaji kwa upande wa kike na wa kiume.

Utamaduni wa Malindi ilikuwa na nafasi kubwa katika ngoma. Ngoma ndio kitovu cha utamaduni wa Malindi. Walitumia ngoma katika kila sehemu, sherehe, mikutano na hata katika kutambikia mizimu ya Malindi. Ngoma ilikuwa na mvuto wa aina yake.

Dirisha la mashindano hayo lilifunguliwa na tamasha la mchezo wa ngumi ambalo liliwakutanisha mashujaa mbalimbali ambao walikuwa wamesajiliwa tayari kugombania kinyang’anyilo cha shujaa wa Malindi. Ibo hakukosa katika nafasi hiyo hakuna alileta wasiwasi kuhusu yeye. Alijulikana kuwa mwanaumwe wa kazi.

Ilianza kwa raundi ya mchujo kwa kuwapata wachache ambao wataonesha uwezo wao kwa Mfalme na kujishindia taji la Malindi. Waliangushana kwelikweli, kila ukianguka basi unasogea nyuma na kuruhusu wengine wachukue nafasi. Unayemwangusha mwenzako basi unasoge mbele na kupangwa raundi inayofuata. Michujo ikawa ya roundi kadhaa na kila kona Ibo aliibuka mshindi.

Hatimaye ikaja fainali, ilikuwa ni saa saba ya mchana. Jua likiwaka kupita maelezo. Uwanjani alisimama Ibo na kijana mwingine aliyekwenda kwa jina la Suma. Suma Alijikongoja kwa kuwaangusha madume kadhaa na hatimaye kufika fainali. Mbele yake alikuwepo shujaa wa Malindi kwa wakati wote. Umati wote ulishangilia kwa mtanange huo, maumbo yao yalithibisha uhodali wao wa kuwepo hatua hiyo. Wote walikuwa mapandikizi ya baba. Watu wakawa wanasubuli kwa kujiuliza maswali kedekede kichwani kwamba je kuna shujaa mpya Malindi au ndio walidhike tu Ibo?.

Filimbi ya amani ikabweka katika uwanja wa Mbio Ndefu, Ibo na suma walikwaruzana kiana. Kila mmoja alishika ubavu wake. Walitikisana kama vidume vya shoka Malindi. Wakaiacha ardhi ya Malindi ibweteke kwa shida. Suma alivumilia kila aina na kipigo kutoka kwa Ibo. japokuwa alirudisha lakini hakufua dafu kwa mwamba Ibo. Ibo, alitikisha umati wote ukimshangilia kwa fujo. Alikuwa na sifa sana Ibo. alikuwa imara katika kudifensi na kuataki kila upande. Haikuwa kazi ngumu kumwangusha Suma. Alifanikiwa na kutangazwa kuwa mbabe mpya na wa miaka yote wa Malindi. Akakaa kando kusubiri washindi wengine wababe makombe yao. Mda ulizidi kuyoyoma..

Likaja kundi la washiriki wa pili wa ngoma na Uimbaji. Ulikuwa ni upande wa kiume ambapo Sadiki alikuwa moja ya washiriki. Sadiki ndio alikuwa anashikilia taji hilo kwa mwaka wa pili sasa. Alilichukua taji kwa mara ya kwanza kutoka mikononi mwa mzoefu wa masuala ya ngoma kwa jina la Mwamba. Kwa mwaka huu Mwamba hakushiliki kabisa mashindano hayo kutokana na afya yake kuwa tete.

Basi mtanange ukaanza. Sadiki alisakata ngoma kama hana akili. Alichanganya staili zote toka enzi za kale hadi sasa. Kelele za fujo ziliongozwa na rafiki yake kipenzi Saleh ambaye alikuwa anamtia moyo siku zote kuwa hakuna wakushinda na wao siku zote. Saleh aliona kushinda kwa Sadiki ni kushinda kwake pia. Akafanya kila aina ya fujo kumpa moyo wa sifa rafiki yake. Hakujali ni kwa jicho gani atatazamwa na Binti ya mfalme. Alimpotezea tu kila jicho likija upande wake. Hatimaye akaibuka kededea Sadiki kwa mashindano ya ngoma ya Malindi kwa upande wa wanaume. Sadiki alikuwa na hatari yake.

Baada ya mapumziko mafupi, ikaja patashika nguo chanika. Ilikuwa ni saa tisa alasiri. Jua la utosi lilishabeba mizigo yake na kuelekea magharibi. Malindi ililipuka kwa shangwe mara baada tu ya mabinti kuingia kati nao kuonesha vipaji vyao mbele ya maelfu. Hakukuwa na kazi siku hiyo. Ilikuwa siku pekee ya burudani ya wote. Kila mtu aliisubiri siku hii kwa hamu sana. Ilikuwa burudani bandika bandua. Kuna watu walisema asiye na mwana aeleke jiwe. Tayari washindi wawili walishapatikana, Ibo Kama shujaa wa Malindi katika ngumi na Sadiki akiwa Shujaa wa kupika na kupakua ngoma ya utamaduni wa Malindi kwa upande wa kiume. Ikaja zamu ya mashindano ya kunengua kwa upande wa kike. Jukwaa lilifana kwa maandalizi ya watoto hao. Wote waliwaka. Ushindani katika hatua hii uliongezeka mara dufu. Lakini kila mmoja macho yake yalianguka kwa Zena.

Filimbi ikalia kuashilia mtanange kufunguliwa. Mchujo wa mashindano haya ulikuwa tofauti na michujo ya mashindano mengine yaliyopita. Hapa ukifanya vizuri unatangazwa mbele ya umati na kupigiwa kura kwenda raundi inayofuata. Washiriki wote walikuwa na ngoma tofauti na wapigaji wao. Zilikuwa ni kelele. Ilikuwa ni cheza unaposikia ala za mziki wako. Watu walijimwaga sana hadi wengine kuzimia. Walikuwa hawana pumzi ya kushindana na Zena. Wakalala mlango wazi. wakaibiwa.

Mikono mitano ikanyanyuliwa juu kuashilia kupita kwenda fainali. Walipigiwa kura na wananchi. Moja kati yao alikuwa ni Zena.

Raundi hii ilikuwa na utaratibu mzuri kidogo. Kila mtu alikuwa anaingia kwa wakati wake na hatimaye kupigiwa kura. Ilikuwa ni fainali ya wanawake watano. Yote ni mapandikizi ya mama.

Wa kwanza akaja akakosea stepu. Alijikanyaga na kuanguka, akaondolewa. Wa pili naye akacheza vizuri tu tena kwa ustadi lakini alikosa shepu ya kuvutia wanaume. Aliundwa undwa tu. Akaondolewa. Wa tatu naye akaja na aina yake ya staili akakonga nyoyo za kina baba hasa wapenda mambo ya kikubwa. Alikuwa anacheza kwa sifa sana. Mara afungue nguo yake na kufunga, mara ainame na mguu mmoja. Akawa kituko hadi kutolewa stejini. Akaja wa nne ambaye yeye alikuwa mshindani kweli. Alikuwa ni Zena. Binti shupavu wa miaka yote katika kunengua kiono.

Alicheza kwa ustadi lakini sio sana kama zama zilizopita. Alizingua zena. Sio kama alicheza vibaya hapana. Alikuwa hana morali kabisa katika raundi hii. Yaonekana ni baada ya kurudiwa na mawazo ya mapenzi ya mwanaume ambaye yupo hapo anamshuhudia. Akatolewa nje ya shindano na yeye na kuruhusiwa wa mwisho aingie.

Huyu wa mwisho alitawala jukwaa kwa kweli, kwa raundi hii huyu alikuwa mshiriki haswaa. Alikua na ramani ya Malindi nzima kichwani. Alikuwa amejiandaa kila idara ya uchezaji, akatumia sifa, mwishoni pumzi ikamjaa akashindwa kumaliza vizuri. Akaanguka chini na kuzima ngoma. naye mwishoni alichemsha. Umati wa watu ukawaka kwa shangwe.

“Irudiweee irudiweee!,”
“Fainali irudiweeee irudiwe!”

Akasimama mtangazaji na kutuliza umati. Akawauliza nini hasa hitaji lao la msingi. Mmoja akajitokeza na sauti yake ya kufoka akisindikizwa na muhemo wa furaha.

“Hapo Zena na huyu Shida warudie Show!” aliongea kwa faida ya wengine na kelele za umati zikifuata.

“Ndiyooooo...! oyooo!” ulikuwa muhemuko usio wa kawaida. Ikawa ponea ya Zena kujiuliza tena katika nungwe hii. Maana kimahesabu tayari alisha garagazwa. Zena akaweka kando utani na kurusha hisia zake kazini. Alifumba macho kuto mwona Saleh, alitaka kumwonesha Zawadi kuwa ana vigezo vyote vya kumnyanganya Saleh. Akawa imara sasa, akapewa nafasi ya kujiuliza.

Kwa baati nzuri safari hii yule dada Shida akaanza kunengua. Akafanya yale yale ya mwanzo hakuwa na maajabu mengine. Zaidi ni sifa tu zilijaa, alishangiliwa kwelikweli. Akawa na tumaini la kumgalagaza Zena. Akajitangaza ki-moyomoyo kuwa yeye ndiye mshindi. Ikaja zamu ya zena. Zena ambaye hakutaka kumwaibisha hata mama yake mzazi sasa alirudi kivngine. mizimu ya marehemu baba yake ikamwongoza haswa... akawa jasiri kwa kubeba roho za binadamu kiganjani mwake.

Kwanza aliruhusu ala za msiki zipasike hadi kwenye moyo wake. Akaanza kutikisha kichwa kilichobeba mabega yake mepesi kwa ustadi.

Haikutosha, kiuno nacho kikaiga kwa kuzunguka kama hakitaki vile, punde ngoma ikachanganya. Akainama zena!. Akaanza kuweweseka hadi mwisho wa ardhi!. Kwanini asiruhusu kushika Miguu yake yote miwili kwenye mguu mmoja?. Aliweza Zena. Akabadili mkono mmoja ushike Miguu yake na mwingine kupandisha shanga yake iliyokuwa hatihani kudondoka. Akainuka zena. hakuwa tena pamoja na umati ule uliomshangilia. Alikuwa dunia yake ya burudani. Akazidisha umaridadi.

Zena sasa alichanganyikiwa. Alichukua ya kulia na kupeleka kushoto, akayabandua ya chini na kuyapeleka juu. Bado alikuwa anapigilia msumali wa kuimalisha fenicha yake. Aliyachukua matiti yake na kuyaweka kiganjani. Mguu mmoja ukiwa hewani na mwingine ardini. Hakusita kukikata kiuno chake bila kupepesuka. Nani asishangilie Malindi Eh!. Alibeba umati mzima na kumfanya hata mfalme kutabasamu, ndio ya mfalme ni ndio ya watu wote. Alikubalika sasa Zena. Kila kona ni nderemo tu na vifijo. walio lala mwanzo wakaamka.

“Zena Zeana.. Zeana Zenaa!” Hawakuchoka kuimba. Hadi tamasha linafikia tamati. Tayari mpinzani wa Zena alishaweka ndio kwa kuruhusu heshima kwa mwana dada huyo. Zena alikuwa Mama Lao.

Naaaaam!, washindi wote watatu walikabiziwa Zawadi zao yakiwemo mataji na kutangazwa hadharani kuwa ni mashujaa wa Malindi. Baada yapo kila mtu alikongosheka roho yake. Kila nafsi ilifurahi siku hiyo. Wakawa wakijadili kila hatua ya mashindano wakiwa njiani.

“Jamani Zena Da da daaaa!”
“Hivi anampenzi kweli yule mtoto!”
“Hahaha, unamtaka?”

“Nani asimtake zena hapa kijijini!, kwa hali hile kila mwanaume atapenda kuwa naye. Mtoto anawaka kila kitu”

“Lakini nasikia sio mchoyo kabisa. Mkikubaliana tu mnafanya tena buree!”

“Ah we!, nani Zena?, huyu Zena wa leo au Zezena?”

“Huyuhuyu Zena. Msifikiri sana kumsifia. hatukatai ni mzuri lakini Uzuri wake haupo kabisa katika tabia. Anagawa sana. Nyie tu ndio hamfahamu hapa Malindi!”

“Ushapata nini mjamaa?!”

“Ah! Nipate niukwae?. Ngoma ya siku hizi kali kweli. Usiombe upigiwe ucheze!”

Zilikuwa nisoga za vijana wanne ambao walitawanyika eneo la tukio huku wakionesha taama kwa zena. Mmoja kati yao alionesha kufahamu vizuri tabia za zena. Zena alikuwa anagawa tamu yake kwa watu tofauti tofauti na kwa nyakati tofauti. Akiwa tu na hamu basi anatongoza yeye na atakaye mtongzoa basi achomoi. uchomoe ili iwaje? yaaani asali mbichi ya asili unaikondoa na kupaka kwenye jeraha!!!

Alikuwa anatumia mbinu zake za kila namna kupata anachokitaka lakini kwa Saleh aligonga mwamba. Hakutaka tu kumpa penzi lake Saleh, bali alitaka Saleh awe baba wa watoto wake. Tabia nzuri za Saleh zilipendezwa na watu karibia kijiji kizima. Alikuwa na hekima ya aina yake, mcheshi na asiyetaka makuu. Heshima ikawa Nguzo yake kila aonapo kitu au mtu amemzidi umri. Aliamkia hadi miti Saleh. Alikuwa na heshima ya juu sana.

Hivyo kuwafanya wanawake wazito kama Binti wa Mfalme kuvutika naye. Alikuwa na swaga Saleh. Akitembea kweli ni kijana. Hiyo tisa kumi ni umaridadi wake katika uwindaji. Alikuwa mwindaji mzuri sana lakini alifanya hivyo kwa siri na walijua wachache sana kama yeye ni mwindaji kwa sababu, Mama yake alishamkanya kujionesha hadharani kwa watu kipawa chake. Aliofia kupotea kama alivyopotea kaka yake. Malindi haina mchezo!, ikipenda kupotea unapotea tu kama kaka yake na Saleh.....!

******
ITAENDELEA…

Starxav
 
Mtunzi; XAVERY EMMANUEL LUOGA
Simulizi; “PENDO HURU’
Namba: 0672493994
@Star_xav

EPISODE 09
Hivyo kuwafanya wanawake wazito kama Binti wa Mfalme kuvutika naye. Alikuwa na swaga Saleh. Akitembea kweli ni kijana. Hiyo tisa kumi ni umaridadi wake katika uwindaji. Alikuwa mwindaji mzuri sana lakini alifanya hivyo kwa siri na walijua wachache sana kama yeye ni mwindaji kwa sababu, Mama yake alishamkanya kujionesha hadharani kwa watu kipawa chake. Aliofia kupotea kama alivyopotea kaka yake. Malindi haina mchezo!, ikipenda kupotea unapotea tu kama kaka yake na Saleh..

******
Upande wa Sadiki yeye alikuwa na ndugu yake wa damu Saleh, waliweka mikono yao mabegani huku wakiimba na kucheza kwa pamoja. Kwa kuwa njia ilikuwa ni moja hawakusita kukutana na Zena pamoja na Mama yake. Hii ni baada ya kukumbana katika mchochoro mmoja.

“We Saleh simama!” ikatoka oda kutoka kwa Mama Zena, baada ya kuona wawili hao wapo kasi kuwapita toka barabara iliyopo mbele yao. Akasimama Saleh.

“Kijana unataka kuniumizia mwanangu eh!” aliongea Mama mikono ikiwa kiunoni na mwanaye zena akisimama mbali kidogo na yeye, sura ikiwa iimeinama chini.

“Kwanini Mama” alijibu Saleh.

“WE ZENA!! NJO!!” aliita kwa sauti Mama Zena na Zena akasogea.

“Aya ili kovu nani kasababisha?” aliongea huku akimgeuza mwanaye ubavu wa kushoto wa shavu lake. Kulikuwa na alama. Alama za kofi kutoka kwa Saleh.

“Lakini Ma…!”

“Wee!, lakini nini. Nakupa dakika kumi tu nenda kwenu kaoge njo kwetu tuyajenge. La sivyo nakuja hukohuko kwenu kukuozesha. Sikuzaa mwanangu mbaya na makovu kama haya. Laah!” shombo la Mama zena liliongozana na msonyo wa maringo. Vyote vikatua usoni mwa Saleh na Sadiki, na kuwaachia alama za mshangao. Wakaondoka Mama na mtoto wake.

“Daah!” Sadiki akachangia neno. Akaona mwenzake anaingia katika matatizo.

“Saleh!, Zena sio mwanamke wa kuoa. Nakushauli!, jana tu alipotoka kwako na kipigo ulichompa, usiku baada ya kutoka kwako nilikutana naye na kunilazimisha tufanye mapenzi. Eti umemwacha katika hali mbaya. Me nikamkazia!, alafu Mpenzi wangu Sala namuweka wapi?”

“Khee!” alitwika mikono kichwani Saleh. Mambo yalianza kumualibia furaha yake ya toka asubuhi.

“Ndio hivyo, hata ilo kofi nadhani Lilikuwa ndogo na ule weupe ilitakiwa mashavu yamtoke kabisa. Hana adabu Msyuuu!” Sadiki akatoa lake la moyo ni kuishia zao. Hawakuwa na mpango na vitisho vya Mama Zena. Wakashika zao njia.

Mwendo wao wa Shuta ilifanya furaha za Sadiki na Saleh zisimame kidedea, walihamasika kama watoto wachanga wapokeapo pipi kama Zawadi. Walifika moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Sadiki. Wakatua taji lao chini na kupiga kidedea. Walikuwa watoto bado. Walikuwa na nia ya kufukua kaburi la furaha lilichimbiwa Malindi. Kaburi ambalo halina mzikaji. Wote waliruka.

“Saleh Sale Saleh.. Sa….ileh! Ahsante sana kwa hamasa yako. Natumai zoezi hili limeenda kama inavyotakiwa kwa jitihada zako. Pasipo wewe hmmmm!! Sidhani! Sidhani kabisa Saleh!. Nashukuru sana.”

“Hahahaha kaka mimi changu kidedea tu, hakuna cha maana nilichofanya. Umepiga kazi kwa kweli. Mungu amesikia kilio chetu cha kila siku. Pongezi kwako kwa kipawa ambacho kinashudiwa na wengi. Wewe ni mtu hapa Malindi.!”

“Mtu?? Ko wewe sokwe!”.

“Inasemekana lakini haina uhakika.”

“Sala!!” aliita Sadiki huku akipotezea utani wa rafiki yake.

“We Sadiki umemleta Sala hadi huku kwa wazazi wako? Duuh!” alinong’oneza Saleh baada ya kuona Sadiki anaita jina mpenzi wake ambaye ni shemeji kwake.

“Sala!!” akaita tena. aliita tena Sadiki.

“Kwani unaita unahakika yupo hapa?”

“Sina hakika. Ndio nataka hakikisha hivyo, hahaha… Salaa!!” kimya kikatanda.

“Hakuna mtu hapa”

“Na sisi kina nani?”

“Ni sokwe!, inasemekena lakini hakuna uhakika” wote wakacheka baada ya kurudia maneno hayo wote kwa pamoja.

***********
Sala, Mama na Baba wa Sadiki wote waliongozana kurudi makwao. Hawakutaka kelele za Sadiki na Saleh waongozane nazo. Walijua kwa sifa za vijana hawa wataleta fujo. Mwendo wao wa kizeezee uliwachanganya wote hadi Sala ambaye yu bado kijana mbichi kabisa.

Njiani waliendelea tu kumsifia mwanao kwa kuwapa heshima Malindi.

“Sasa ulipotaka kuzaa mtoto mpiganaji?, angeweza kweli?” Mama Sadiki alikuwa mbio kujitapa kuwa, alitoa mapema wazo za kuzaa mtoto mwenye kipaji kinachohusu utamaduni wa Malindi.

Na ikawa hivyo. Akabaki kumrushia mipira tu mume wake ambaye miaka yote yeye alitamani sana kuzaa mtoto ambaye atakuwa mpiganaji Malindi nzima. Na hatimaye mkewe akashinda, mtoto hodari wa kucheza na kupiga ngoma akapatikana. Aliwagalagaza vijana wenzake kwa miaka miwili mfurulizo.

“Mke wangu!, mbona wanitia aibu kwa Binti hapa, Eti Sala. Nani wa kujitapa hapa kati ya mimi na mama yako?, sasa huyo mtoto si angetoka wa kike?. Mbona dume sasa!. Hahaha!” Baba Sadiki na yeye hakuwa nyuma. Aliweza haswa michezo ya mke wake. Kwa kuwa walikaa mda mrefu pamoja walijuana tambo zao.

“Eti wakike!!, dume lile!” Mama Sadiki ikaiga sauti ya mume wake kwa kubinya pua. Sala alicheka kufa. Hakuchangia chochote katika sherehe hii ya maneno. Mdogo mdogo wakafika makwao. Waliwashuhudia wanao Sadiki na Saleh waliolowa jasho wakiwa kando na debe la mazungumzo. Waliyatafuna mazungumzo yao kimya kimya. Bila kiny’aa, walikuwa na kunywa, hawakushiba hadi wakakutwa.

“Ndio kilichowaleta Malindi hicho!” Baba alikuwa mkorofi kweli kweli, aliwashitua wanae kwa kauli ya ajabu ambayo iliwaacha hoi Sala na Mama mkwe wake.

“Ah Baba!” Saleh akainuka. Kumsalimu Baba yake na Sadiki, lakini kwa utani, alipitiliza Saleh; akaachana na Mbaba huyo na kuelekea moja kwa moja kwa shemeji yake.

“Shemela!, wajina!.., wewe ndio wa muhimu hapa!, hawa nawaona kila siku!.” Kicheko kikatawala. Kwa kweli siku hii ilijawa na furaha sana walikutanishwa na furaha ya upendo uso kwa uso.

Naam!, Saleh akashinda kwa kina Sadiki siku nzima. Akasahau msala ambao unaenda kutokea nyumbani kwake Mama Zena hana subra kabisa..

************
Karibu sana Mama Zena.., Zena hujambo. Hongera mwanangu!.” Zilikuwa salamu kutoka kwa Mama Saleh kwenda kwa Wageni wake Mama Zena na bintiye Zena. Walishaketishwa tayari kwenye mkeka. Uzuri walimkuta Mama Saleh tu, Saleh alishinda kwa kwa kina Sadiki na Baba Saleh alishaenda kutafuta ulabu ulipo kuburudika na wenzake.

“AAhsantee! Mwayaa”, Baada ya kukaribishwa Mama Zena kwa kuwa alikuwa na mwanamke mwenzake hakuona haja ya kumpanikisha. Akaamua tu kumwingiza chuki ya mapenzi ili mwanaye apate nafasi zaidi.

“Mama Saleh jirani yangu. Watoto wetu ndio haooo, washapevuka!. Vipi wewe umewazaje?” Akamtupia swali Mama Saleh. Swali lenye utata kidogo, lakini fumbo mfumbie Mjinga bhana, mwelevu anang'amua.

“Mhhhh!, nikisema mimi labda naweza kudanganya. Nilitamani angewepo na Baba mwenye nyumba kwa jambo zito kama hilo!” akajibu Mama Saleh jicho likimkagua Zena.

“Ah!, Jamani, we mwanamke bhana Suala lile. alitaka kwa nguvu kisicho riziki kilike

ITAENDELEA Episode 10…


Starxav
 
Amenisikitisha sana kwenda kuomba huduma kwa Sadiki....
Saleh sijui atabaki kwa nani na ameshaambiwa Zawadi ndugu yake.

Labda hiyo miuno yake ndiyo inampeleka resi... na hizo sifa anazosifwa ni mkatikaji mahiri...

Salehe na Zawadi wana undugu wa mbali... ni halali yake... mama yake alimwambia...


Cc: mahondaw
 
Mtunzi: XAVERY LUOGA
Simulizi: “PENDO HURU’
Namba: 0672493994

EPISODE 10
“Ah!, Jamani, we mwanamke bhana, afu hapa Malindi wanawake tumejishusha sana. Mimi ni mwaka wangu wa therethini huu kama sikosei simjui Baba Zena na mambo yanaenda... Ila sawa, maana..” akuongea hadi mwisho. Tayari sumu mdomoni mwake ilikuwa kali. Akakatisha.

“Eh ndio..” Mama Saleh akamruhusu kuendelea.

“Unajua hadi nimefika hapa, Mama Saleh hawa watoto wanapendana sana, sa sijui shida ni sisi wazazi au la!. Mfano mwanangu mimi anaumia Mama saleh. Sidhani kama kuna mzazi anapenda mtoto wake awe katika majonzi.”

“Mhhhh!, kwa Saleh huyu, huyu ninaemjua mimi. Mbona hajawai hata taja neno mpenzi!, mhh labda…” aliweka msimamo Mama Saleh.

“Ebu geuka Zena!” Mama Zena akamwambia zena ageuze upande wake wa shavu la kushoto. Akageuka.

“Si umeona?!”

“Ndio hata mimi nilishangaa sana pale anatumbuiza. Mbona kama Zena amevimba tatizo nini?” akauliza Mama Saleh.

“MAPENZI!.” Mama zena akajibu kwa herufi kubwa huku akibetua mdomo wake kuelekea juu.

“Mapenzi ndio yamemuadhibu hivi jamani au?” alijifanya kutoelewa Mama Saleh

“Mwanao na mwanangu walikutana wapi sijui, na sijui hata walikuwa wanaongea nini!, yaani. Amekuja tu na makovu nyumbani jana. Nilimuuliza kisa nini akasema Saleh amepiga!”

“Saleh!!”
“Eh Saleh mtoto wako”
“Mhh!,”

“Ndio hivyo, sa nikamwambie twende nikahakikishe usije mzingizia mtoto wa watu uko... Akagoma ile jana. Akaniambia tusubili kwanza mpaka mashindano yaishe. Sasa yalivyoisha leo nikakutana na Saleh wakati anarudi. Nikamuuliza akasema oh kweli Mama. Mimi sijui kilikwenda kikarudi!, hakuna anachojibu. Ndio mguu huu!”

“Khaaa!,Salah” Mama Saleh bado alikuwa haamini. Hakuwahi sikia kijana wake amepiga mtoto wa watu toka azaliwe. Leo kampiga mdada Mrembo Zena hadi kumwachia alama?! Alishangaa sana Mama Saleh.

“Ndio hivyo!, hapo nimekuja tu kukuambia kuwa jamani kama mnamtaka Binti yangu basi tukae chini, tuongee. Mana vijana hata ukiwauliza wenyewe wanasema wanapendana, si eti Zena?”

“Ndio!” Zena akaitikia. Tena akaitika bila woga. Mama Saleh akachoka.

“Kwakweli!, aya sawa Mama Zena, mimi nimeelewa, nitakaa na Saleh na Baba yake tuone mambo yanaendaje. Mana wote hawapo hapo.. ila hii ni kubwa sana asee!, huyu Saleh ni chizi eti!”

Naam! Mama zena akaongozana na Mwanaye baada ya kuhakikisha sumu aliyoitoa itaua nyumba nzima. Alipigania penzi la mtoto wake ambalo Lilikuwa halina hata dalili ya kuchipuka. Lilipandwa jangwani..

Aliporudi Saleh akakuta kikao ambacho kilikutanisha familia nzima. Kikao chenye maswali mengi ya ajabu ajabu.

“Utaoa lini?, ni nani utamuoa?, je ni Zena? Na kama sio Zena nani? Na kwa nini?”. Saleh aliwekwa kitimoto siku hiyo. Akaamua kuweka bayana kwa baba yake, japo kuwa Mama yake alifahamu kila kitu. Alijua mwanawe anapenda wapi na vizuizi vipi anakutana navyo.

“Baba ni muda sasa wa kusimamia na kutoniuliza maswali kama hayo mimi ni mwanaume na nina sababu ya kuchagua kule nako kutana. Zena nilimpiga kwa kunikosea heshima. Na sio kama mlivyoelezwa. Simpendi Zena mimi!” aliongea kwa ghasia Saleh.

“Sasa nani?”
“Baba, Mama nampenda sana Binti ya Mfalme, Zawadi!”.
“Heeee! Makubwa!. Zawadi?”
“Ndio baba. Naye pia ananipenda, tatizo..”

“Tatizo Baba yake. Baba yake ndio shida hapa Malindi. Na akijua kama unamahusiano ya kimapenzi na bintiye. Tumekwisha” Mama alimalizia sentensi ya Saleh iliyoishia njiani. Alionesha anafahamu mpango huo.

“Khaa!” Baba alibaki kuhamaki tu, alishaelewa kuwa alibaki pekeyake kufahamu mambo hayo. Wenzake wote wenyeji. Sasa kwa nini asicheke Baba Swaleh. Alicheka sana.

“Ko!, ndio mimi pekee sijui ama?” aliuliza huku akimwangalia Mke wake.

“Kwa sasa Saleh ni mkubwa. Anajua kila kitu. Sasa yeye ndie achague. Afanye kitu. Sisi hatumo. Akiamua kututeketeza sawa, ni yeye. Hakuna namna. Umefika muda wa Malindi kukomboka sasa. Manangu anaweza.” Mama Saleh akamaliza mchezo kwa kufunga bao tano pekeyake. Akawa mfungaji bora wa familia siku hiyo. Wakawekana sawa hadi siku kuisha..

SEHEMU YA SITA.

Siku pili yake, ilikuwa ni siku nyingine ya mapumziko Malindi. Hakuna kufanya kazi. Zilitengwa siku mbili ambazo wakazi wote wa Malindi walizitumia vyema kwa kuto jishughulisha na shughuli yoyote ile. Ilikuwa ni siku ya mapumziko ambapo familia zilipata wasaa wa kukutana na kuongea mawili matatu juu ya mambo yaliyotokea jana yake na kuwapongeza washindi wa tuzo mbalimbali za Malindi.

Kama ilivyo ada kuwa “Mtoto kwa mama hakui”, Zawadi alikutana tena na Mama yake safari hii ilikuwa ni nje ya Kasri la Mfalme. Walikuwa wakitembea tembea tu ili kupisha muda sahihi wa kuzungumzia jambo ambalo linamkela Mama Zawadi.

“Mwanangu!, kwani huwezi kusamehe?” alihoji bila hata kuweka bayana nini anaongelea.

“Kusamehe!! Kipi?” alijibu Zawadi.
“Saleh!”

“Ah Mama!, Saleh nampenda sana lakini si wangu Mamaa, yupo na mtu!”

“Una hakika??, maana mimi ilo suala nimelifuatilia kwa kina sana”
“Lakini Mama tuyaache hayo!, hakuna mengine?”

“Yatoke wapi. We nenda mbele rudi nyuma. Ibo hawezi kukuoa. Kama mimi nipo hai basi Ibo hawezi kukuoa. Simpendi yule kijana mimi. Ni mshenzi sana.”

“Mhhh!, Mshenzi kuliko Zena?”

“Sasa na wewe Zena si ndio walewale tu. Tena walifaa sana waoane hawa!.... tena mwanangu nasikia Zena amelala hadi na Ibo. Sio kulala huku kwa kitoto. Enhe! Hatari!... Ndo mume wako huyo eh! Et nakuuliza?” Mama Zawadi alianza kunena kilugha. Roho mtakatifu alimpanda tayari.

“Mama!”

“Nini!!, habari ndio hiyo, chagua moja, Saleh ambaye umemkuta tu na mdada na hujui nini kinaendelea, na huyo ambaye hadi mimi Mama yako najua kuwa amelala na wanawake karibu kijini kizima!” Sasa aligusa kunako Mama Zawadi.

“Sasaa!, sa mimi nafanyaje masikini!” alilalama Zawadi aking'ata dole lake la kati kati.

“Mrudishe Saleh!, kosa alilofanya kwako linasameheka!”

“Mamaa!, kwanini Saleh!”

“Unaniuliza kwa nini Saleh!, kwani wewe ulitumia kigezo gani kumpenda??” alikuwa mkali Mama Zawadi. Hakutaka mchezo kabisa.

“Mama, sijaangalia chochote kile, moyo wangu tu umependa. Na sijui kwanini!, yaani toka nimuone kwa mara ya kwanza da najikuta kila wakati nataka nimuone tu basi niridhike!”.

“Aya sawa, mana mimi ndio huyooo napeleka kale ka wazo kale ka kukubali kuolewa na huyo mbabe wa kijiji!” alikuwa na vijembe Mama Zawadi.

“Mamaa!”
“Nini?, Shida nini!”
“Nisaidie Mama!”

“Wa kukusaidia ni mimi au baba yako?. Baba yako haziivi kabisa na wanaume wengine hapa kijijini na isitoshe wewe mtoto sana hufahamu vizuri historia ya hii koo pamoja na historia ya koo yetu. Nadhani nipo peke yangu hapa ninayejua siri nzito ya Malindi. Ni mimi tu!” Mama Zawadi alijitapa kuwa yeye pekee ndio shuhuda wa historia ya Malindi. Alisahau kuwa histora hiyo pia ilikuwa inashikiliwa na Mama Saleh na tayari alisha mwaga mchele kwa mwanaye Saleh, kuwa Saleh ni mtoto wa Bana na Zawadi sio mtoto halali wa Bana.

“Mama Baba akimjua Saleh si atamuua?”

“Mwanangu mapenzi hayana kifo. Atakufa lakini kabla ya kufa Saleh nitafanya kitu. Lakini kitu cha kwanza lazima nihakikishe Saleh na wewe mnaoana!. Kwanza nijibu.Unampenda?”

“Nani?”
“Nyoo!.., Ibo”
“Hii Ma…ma hapana!”
“Sa mbona unauliza nani?”

“Saleh Mama, nampenda na nimeshamsamehe, lakini mpaka akili yangu ijue kama yupo mwenyewe na hana mtu. Nataka kuwa huru na penzi langu!.”

“Ama mapenzi, hahahahaha!, sasa nimekutoa nje hapa nikupe nafasi ya kwenda kuonana na Saleh, kimbia nenda. Nakupa dakika hizi!!..” Mama Zawadi alikunja ngumi zake mbili kuashilia kumi.

“Kumi” Zawadi akaitikia.

“Kua mjanja, hakikisha huonekani. Ukuionekana tu tumekwisha mimi na wewe!. We nenda. Mlango wa kuingilia si unaujua?, aya nenda, nenda nenda.. ala!” Mama Zawadi alimsukuma Zawadi mbele na kisha yeye kurudi ndani.

Penzi la Zena limeota mbawa na Kupeperuka, Mama Zawadi afanya juu chini mtoto wake aolewe na Saleh, Je Mfalme Bana ba Ibo wakijua mchezo huu wa Zawadi na Mama yake?...
Usitamani kukosa Mkasa huu.

ITAENDELEA Episode 11…..

Starxav
 
Mtunzi: XAVERY LUOGA
Simulizi: “PENDO HURU’
Namba: 0672493994

EPISODE 11
“Ama mapenzi, hahahahaha!, sasa nimekutoa nje hapa nikupe nafasi ya kwenda kuonana na Saleh, kimbia nenda. Nakupa dakika hizi!!..” Mama Zawadi alikunja ngumi zake mbili kuashilia kumi.

“Kumi” Zawadi akaitikia.

“Kua mjanja, hakikisha huonekani. Ukuionekana tu tumekwisha mimi na wewe!. We nenda. Mlango wa kuingilia si unaujua?, aya nenda, nenda nenda.. ala!” Mama Zawadi alimsukuma Zawadi mbele na kisha yeye kurudi ndani.

Alipita kwa madaha kwa kuwanogesha walinzi wa kasri hiyo ambao walikuwa hawana habari na kile kinachoeendelea. Waliokuwa wanoko kuhusu Mama huyo kumtorosha Binti yake aliwapa rushwa ya thamani kadhaa kila baada ya tukio. Zawadi akatoweka na Mama Zawadi akarudi ndani.

Mama Zawadi alipofika ndani alikuta kuna kikao!. Kikao ambacho kuna nafasi mbili amabazo zipo wazi.

Tayari Mfalme alishakaa katika kiti chake. Kulia kwake alikuwa na Ibo mwenye tabasamu. Kiti cha tatu cha upande wa kulia kilikuwa wazi na ni kiti ambacho kinakaliwa na Malkia wa Malindi ambaye ndio yeye. Ukiachana na hicho pia bado kiti kingine kipo wazi; Zawadi. Zawadi alitakiwa awe pale muda hule. Mama Zawadi likamshuka.

“Ma’ Zawadi, karibu kuketi!” Mfalme alimkaribisha mke wake huku mkono ikimwongoza Mama Zawadi kwenye kiti chake. Akaketi Mama Zawadi.

“Eh Sasa! Hapa kuna kikao cha muda mfupi tu!, lengo kubwa ni kumtambulisha Ibo kwa Za…” Mfalme alianza utambulisho na kukomea kwa jina la mtoto wake. akakumbuka kuwa mtoto huyo naye anahusika katika kikao hicho. akaacha sentensi yake ipotee hewani na kuunda nyingine.

“Niitie Zawadi ndani!” alitoa amri. Amri hiyo ilimyanyua Mama Zawadi kwa haraka hadi ndani. Alijua fika kuwa Zawadi hayupo ndani humo lakini alienda tu kuwazuga kwamba hajui chochote kile kinachoendelea kuhusu Zawadi. aliingia ndani muda mchache na kurudi..

“Hayupo!” akatoa taarifa.

“Hayupo!,” Mfalme alinyanyuka na uzee wake katika kiti chake, akasogeza hatua kwa shida kwenda kuangaza kweli anachosema mke wake!. Akaingia hadi ndani kwa Zawadi. Hora!. Hayupo Zawadi. Akatoka.

“Ibo, mfafute Zawadi kila eneo kuzunguka kasri hili!!, nyanyukaa! Sema kwa watu wamuite aje hapa.” Mfalme aligundua kitu tayari. Alikuwa na jazba mbaya!. Zilishampanda tayari. Akarudi kuketi katika kiti chake huku jicho likimtoke kwa mke wake ambaye alikuwa anapikicha fito tu ya nguo yake kwa kuona aibu. kichwa kilikuwa chini Mama Zawadi. Baada ya mda Ibo akaingia.

“Mtukufu!, hayupo kila eneo la hapa!” Ibo aliyasema hayo huku kichwa chake kikiwa chini. Alikiinamisha toka atoe salamu. Hakukiinua.

“Mama Zawadi!, Zawadi yupo wapi?.” Akauliza kwa upole mfalme.. hakupata jibu la haraka. Akampotezea Mama Zawadi kwa dakika.

“Tafuta Zawadi kila kona ya Malindi. Leta hapa!” alitoa amri nzito mfalme. Ibo akakimbia kutekeleza agizo hilo. Mfalme akapata nafasi nyingine ya kuuliza swali lile lisilo kuwa na jibu sahihi.

“Yupo wapi Zawadi?”

“si jui!, mimi sijui kweli tena!” alijitetea Mama Zawadi. Akiwa mdogo kama pilitoni. alishajua kimenuka. alitamani awe jini apotee mahali pale kumtetea mtoto wake. ikashindikana.

“Njoo hapa!” Mfalme akatoa amri. Amri iliyo ngumu kutekelezeka maana alimfahamu vizuri mume wake. Alikuwa mwepesi sana kunyanyua mkono wake akikosewa.

“Njo!, Mama Zawadi!” akarudia tena. Sasa Mama Zawadi alisikia vizuri. Alijongea taratibu na kushuka hadi chini alipo mume wake. Akapiga magoti. kichwa kikiwa chini na mikono ikiwa haina kazi ya kufanya.

“Sijui mume wangu!” alijitetea.

“Humu ndani kuna mchezo unaendelea si ndio?” aliuliza Mfalme. Alikuwa amekunja uso haswa lakini hakuonekana kutokana na makunyanzi yaliyojaa usoni mwake.

“Nini unachojua wewe?” aliuliza Mfalme.

“Mimi nilikuwa tu nasikia akilalamika usiku wa kuamkia leo, eti oh!, mimi simpenzi Ibo sijui, mimi sijui nampenda Saleh sijui!...”

“Kelele!” Tatari alishashusha kibao Mfalme. Aliona Mke wake anaongea upuuzi. Tena upuuzi wa viwango wa juu. Akamuwasha kofi. Kilio kikashika hatamu. Nyumba ikatikisika. Mama Zawadi alikuwa katika kipindi kigumu kutetea penzi la mtoto wake.
******

Jamani Zawadi unatafutwa huku... ukuje haraka basi Lo!!! ngoja tuone
ITAENDELEA Episode ya 12…
Komenti zikiwa nyingi leo nitashusha Episode ya 12 Mapema sana Leo hii..

Like, comment na Share !.

Starxav
 
Mtunzi: XAVERY LUOGA
Simulizi: “PENDO HURU’
Namba: 0672493994

EPISODE 12

“Mimi nilikuwa tu nasikia akilalamika usiku wa kuamkia leo, eti oh!, mimi simpenzi Ibo sijui, mimi sijui nampenda Saleh sijui!...”

“Kelele!” Tatari alishashusha kibao Mfalme. Aliona Mke wake anaongea upuuzi. Tena upuuzi wa viwango wa juu. Akamuwasha kofi. Kilio kikashika hatamu. Nyumba ikatikisika. Mama Zawadi alikuwa katika kipindi kigumu kutetea penzi la mtoto wake.

*********
Zawadi yeye alishafika kando ya Bustani ya kina saleh. Ni pale pale kwenye lile jiwe ambalo aliwafuma Saleh na Zena wakifanya uzinzi. Kwa kuwa haikuwa siku ya kazi. Saleh na Sadiki walikuwepo hapo kubadilishana mawazo.

“Sa.. Saleh!” Zawadi aliwashitua wawili hao pale walipo. Sadiki ataachaje kutabasamu. Akakohoa tu na kumkalibisha.

“Zawadi, heshima kwako!. Mbona hata wapambe huna!. Vipi kuhusu usalama wako?”

“Jamani Sadikii hongera kaka angu kwa kipaji. Nilifurahi sana jana!, mimi hata sitaki vya ulinzi, wananinyima amani. Na piaa nilitaka niwe huru” akajibu Zawadi akikaribia karibu na walipo Sadiki na Saleh.

“Asante bhana, tunajitahidi hivyo hivyo, hakuna namna hapo Zawadi. Lakini mhhh!, nawe. Unajua ni hatari sana bila hata mlinzi mmoja na kulivyo mbali huku!”

“Usijali!!, vipi Saleh!, mbona kimya sana!” Zawadi alimshitua Saleh ambaye alikua anaonesha sura ya aibu. akikumbuka kwa jinsi alivyofumaniwa siku hiyo. Sadiki akaona awaache wazungumze.

“Konho! Mhu mhu!, sasa Saleh. Ngoja nikusanye haya majani hapa!” Sadiki alitafuta gia ya kutokea.

“Hii jamanii, unatukimbia!”

“Hapana Zawadi!” aliyasema hayo akiwa ameshapiga hatua. Alitoweka Sadiki.

“We mwanume!, mambo!” alianzisha mazungumzo Zawadi.

“Zawadi!, Nashindwa hata niongee nini mbele yako Malkia!” alijitosa Saleh. Moyo wake ulimsuta sana kutamka maneno ambayo kwa upande wake yalikuwa mazito haswa.

“Zawa..” alitaka kuongea tena Saleh.

“Shiii!!!!” Zawadi hakuruhusu hata Saleh ajieleze. Alishajua anatoka kuomba samahani kwa kitendo alichokutwa anafanya na Zena.

“Saleh!, nimeumia sana kwa kipindi kirefu. Naona unachelewa kusema!. Mimi nakupenda Saleh!” Zawadi akajimwaga. Alikuwa mwingi wa tabasamu usoni. akaweka aibu na mambo ya tamaduni kando. akavunja mwiko kusema ukweli.

Saleh aliisi mapicha picha ya marehemu Bruce lee!, yanakaribia kumuumbua. Alihamaki sana kwa mtoto wa kike kama yule kutangaza Alleluya kuu adharani.

“Zawadi!” Saleh akaita kwa mshituko. Alijua Zawadi amevunja amri za mababu. Lakini akanyamazishwa tena.

“Saleh!, huna cha kunidanganya jamani!. Nakupenda sana na haijalishi, haijalishi Saleh nakupenda.” Sasa Zawadi aliona anachoongea aeleweki akapandisha sauti,ili miti, mawe, milima, mito na viumbe vilivyo hai vimsikie.

“Nakupenda Saleh!!” kitendo kilimshangaza sana Saleh. Hata Sadiki ambaye hakuwa mbali sana na eneo hilo, neno nakupenda alilisikia. Ataachaje kughuna sasa. Alighuna Sadiki na kuendelea na mambo yake.

“Zawadi, samahani, nimeshindwa kuwa wa kwanza kukuambia kuhofia Baba yako?”

“Kwani unampenda Baba? au mimi?” akaulizwa swali lililo mbabaisha. Likamyumbisha na kumweka sawa.

“Aaah! Yaani..” alikosa cha kuongea Saleh. Alikuwa anatetemeka kama ile tetemeko ya kipindi kile kule Japani.

“Za..wa..di.. di.” Hakutamka vizuri neno hilo tayari walikuwa sayari nyingine. Kwa mara ya kwanza tangu azaliwe kristo katika karne za mwanzo. Mtoto wa Mfalme anagawa penzi kwa Saleh. Ilikuwa mara ya kwanza kwa Zawadi kuchanganya mate na kiumbe kingine chenye uhai. Lakini mara ya pili kwa Saleh kumimina kimimika chake kwa Mwana feki wa Mfalme. Ilikuwa ni vaisivesa.

Walishikana kisawasawa ili wasiache mapema wanachokifanya. Aibu ikanishika mtazamaji. Nikasogea kando kuwaacha wawe huru. Wafanye wee hadi wachoke. Wakanyonyana hadi kuishiwa. Wakawa kando kando wakichokeana. Walikuwa palepale katika jiwe la Ushindi. Jiwe lililo na upako kwa Saleh. Jiwe lenye bahati ya kumkutanisha na wanawake wawili tofauti.

“Najiskia huru sana leo Mpenzi!” ilikuwa kauli ya Zawadi pembeni mwa Saleh. Walikuwa bado wamekumbatiana na kuruhusu sauti zao zibishane masikioni. Zote zilikuwa na maneno matamu. Ziliwaiingia haswa juu ya penzi lao huru na changa. Mambo yakawa moto na kuacha majivu Malindi. Kamayalivyo matanga. Matanga bhana huja baada ya msiba. Ukatokea msiba mzito kando yao. hakuna aliye amini.

“Heiiiiiyi!!” ulikuwa mshituko wa sauti nzito wa kuogofya. Sauti kali kutoka kwa ndugu Ibo. Mtu katili na jasiri kwa wakati mmoja. Mtu aliyebeba alama ya hatari Malindi. Mtu pekee awezaye kubeba umati wote wa Malindi begani bila kuumia. Alikuwa Ibo kando yao. Wakaachana Saleh na Zawadi, Saleh alikua anatetemeka tu,.

“Kamata wote!!” akatoa amri katika jeshi lake alilokuja nalo kuwatafuta.

Hawakuwa mbali, tayari walikuwa mikononi mwa utawala mpya wa Mfalme. Nafsi ya Saleh iliongea na nafsi ya mama yake huku ikimkumbusha tu, “Si nilikuambia mwanngu!”. Akafumba macho kuacha lolote litokee juu yake. Ashapenda. Yupo tayari kutokwa uhai. Wakashikwa wote wawili.

“Tuachee!” sauti ya Zawadi ilimfanya Sadiki naye asogee sehemu ya tukio. Alichungulia tu kuona kwa jinsi rafiki yake anavyotiwa nguvuni na kuondolewa mahali hapo. Supu ilishaingia nzi tayari. Alileta kirusi cha magonjwa. Hakuna budi kuimwaga. Akaacha waondoke!. Katu hakujitokeza Sadiki.

Walitoka mkukumkuku na Saleh na Zawadi kama watu walioshikwa ugoni. Moja kwa moja wakakatisha vichochoro hadi barabara kuu, mwendo wa haraka kuifuata kasri ya Mfalme. Uharaka wao uliendana na kasi ya muda. Walifika muda muwafaka. Walipitiliza mpaka ‘tiii’ kwa mfalme.

“Mbona wawili!, au ndiye mshauli wa kutoroka kwa mwanangu?” alihoji mfalme kwa ukakasi.

“Tumewakuta huko, wamekumbatiana, kijana rafiki wa yule mshindi.. nani…!, Sadiki. Huyu anaitwa Saleh!” alimaliza Ibo. ulikua utambulisho usio na maneno mengi.

“Saleh!!” alirudia jina lile Mfalme.

“Ndio Mtukufu Mfalme.”

“We mtoto!, ni kweli wewe ndio Swalehe?” aliita Mfalme huku akiita jina jingine kabisa kurahisisha matamshi.

“Ndi.... ndio, ndio Mtukufu!”. alijibu Saleh.

“Shwaaaah!” kofi likasikika.

“Wewe ndio unaniharibia mtoto wangu?!, mwanaharamu wewe!” Mfalme sasa alikuwa na jazba. Alitamani kumkula kabisa Saleh. Huyu ndio mtibua mpango. Kipingamizi kikubwa hiki kwa penzi la Binti yake.

“Baabaaa!, Mwache Saleh jamani. Sio kosa lake, niadhibu mimi” Zawadi akatoa neno la msaada, halikusaidia.
“Kelele!!” Mfalme alikuwa moto kwelikweli, hakuna alichosikia. Mama Zawadi alishafungiwa ndani. Alikuwa anachungulia tuna na kulia chinichini. Hakuwa na la kufanya. alijutia zile dadika kumi alizotoa zimegeuka vita vya Mapezi Malindi.

“Zawadi umekuwa Malaya sana!, umenipaka matope tayari umeni..ni..ni…” Uzee alimfanya mfalme kuwa legevu, alitumia nguvu nyingi sana kuongea na kufanya aliyoyafanya. Mfalme aliitaji msaidizi. Akashusha sauti yake.

“Kwahiyo huyu ndio unampenda eh!” aliuliza kwa mtego.

“Ndio Baba nampenda Saleh. Nampenda. Nipo tayari ku-u-u-faa!” Zawadi aliweka bayana. Mfalme akachoka. Akashindwa nini afanye juu ya aibu hii ambaye mtoto wake ameionesha mbele ya Ibo mwenyewe.

“Mwanangu chagua moja!, kuolewa na ninayemtaka mimi au nimuue huyu Saleh na uolewe kwa lazima”. Akapewa njia ya kupita. Zote zilikuwa zina miba kwake. Akalia sana Zawadi hakuna kilichomtoka mdomoni.

“Toa wote kafungie huko. Baada ya masaa ishilini na nne watabadili maamuzi” mfalme alitoa agizo kwa kijana wake kuwa akawaweke vijana hao sehemu ambaye itawafanya siku ya pili yake kubadili maamuzi yao. Aliwaamuru wapelekwe eneo la mateso.

Naaam!, baada ya muda tu tayari Ibo alishawafunga kila mmoja wao sehemu yake. Aliwatenganisha Saleh na Zawadi, ilikuwa ni oda kutoka kwa mfalme.

“Saleh nilikuonya wewe!, ukawa mbishi. Sasa umeingia katika kumi na nane zangu. Hakika nakuhaidi hata kama mfalme atakuacha hai, mimi sitafanya hilo jambo. Utakufa mikononi mwangu Saleh. Zawadi ni wangu, mimi ndiye mmiliki halali wa hii himaya. Huna kitu Saleh” yalikuwa ni maneno ya Ibo akiwa anamfunga kamba mikono yake juu ya mti Saleh.

Lilikuwa ni eneo kwaajili ya mateso. Eneo ambalo Lilikuwa lipo kama magereza kwa watu wanaovunja sheria na kumkosea Mfalme. Huko ndiko walikoozea Saleh na Zawadi. Wote walifungwa, haikujalisha nani na yupi. Unacheo gani au huna cheo. Wote walifungwa, Saleh akifungwa sehemu ambayo ilikuwa inatope chini la kutosha. Zawadi yeye alifungwa katika chumba chake. Chumba maalumu kabisa kwa ajili ya mateso ya watoto wa kike. Walitelekezwa huko pasi na msaada...

Naaaam, Malindi inateketea kwa Moto. Nini Zena atafanya akisikia Saleh na Zawadi wameshikwa pamoja?, Je baba na Mama Saleh watapokeaje hizo taarifa, wapenzi wawii wapo katika Mateso ya saa ishirini na nne kujiuliza kuhusu penzi lao. hakika "Pendo Huru"...
*******
ITAENDELEA EPISODE 13

Join Group
SAYARI YA SIMULIZI 🗺
like, Comment and Share...!

Starxav
 
Mtunzi: XAVERY LUOGA
Simulizi: “PENDO HURU’
Namba: 0672493994

EPISODE 13
Naaam!, baada ya muda tu tayari Ibo alishawafunga kila mmoja wao sehemu yake. Aliwatenganisha Saleh na Zawadi, ilikuwa ni oda kutoka kwa mfalme.

“Saleh nilikuonya wewe!, ukawa mbishi. Sasa umeingia katika kumi na nane zangu. Hakika nakuhaidi hata kama mfalme atakuacha hai, mimi sitafanya hilo jambo. Utakufa mikononi mwangu Saleh. Zawadi ni wangu, mimi ndiye mmiliki halali wa hii imaya. Huna kitu Saleh” yalikuwa ni maneno ya Ibo akiwa anamfunga kamba mikono yake juu ya mti Saleh.

Lilikuwa ni eneo kwaajili ya mateso. Eneo ambalo Lilikuwa lipo kama magereza kwa watu wanaovunja sheria na kumkosea Mfalme. Huko ndiko walikoozea Saleh na Zawadi. Wote walifungwa, haikujalisha nani na yupi. Unacheo gani au huna cheo. Wote walifungwa, Saleh akifungwa sehemu ambayo ilikuwa inatope chini la kutosha. Zawadi yeye alifungwa katika chumba chake. Chumba maalumu kabisa kwa ajili ya mateso ya watoto wa kike. Walitelekezwa huko.

*******
Kijua cha jioni kileta salamu Malindi, Alikuwa Sadiki ambaye alifika nyumbani kwa Mama na Baba wa Saleh mkuku mkuku. Alihema kama kijana mwenye ndoto ya mauzauza. Breki yake ikazima mikononi mwa Mama Saleh.

“Sa. Sa, Saleh ameshikwa!” alilopoka bila kuangalia mazingira. Yowe la hofu likamtoka Mama Saleh.

“Yoiyooooh!, na nani!”

“Vija-na! wa Mfalme. Amekutwa na Binti ya mfalme..!”

“Maweeee!, uwiiiii!, Saleh Baba nilisema mimi, Yaiweeeh! Uwiii” yowe hili lilimtoa Baba Saleh katika kibanda. Akaja kuhamaki na yeye taarifa mpya masikioni mwake. Hakuacha kulalama kama baba..

Likaja na wazo la kuwashirikisha na Baba na Mama wa Sadiki, wakatoka mkuku hadi Kwa kina Sadiki. Hodi ikabishwa na kukaribishwa bila viti. Walikuwa wageni wengi sana. Viti havikutosha. Kwanza nani akae?, kwa lipi hasa? Na kwa raha gani hadi wakae?.

Wakaamua kusimamia. Hakuna aliye kumbuka kiti. Wanawake walilowa kwa machozi, wakiume walikuwa na dalili tu. Walijikaza kiume. Walijua kabisa Saleh atahukumiwa Adhabu isiyopungua kugahalimu uhai wa mtu kabisa. Historia ya Malindi inajulikana, wengi wamepotea katika mazingira kama hayo. Wakajadili hadi kigiza kinaingia. Kila mtu alikuwa na mawazo yake.

“Baba Saleh!, mimi hapa naunga mkono hoja hii ya Shemeji yangu. Twende tukaombe, chonde chonde!. Japo msamaha tu jamani.”

“Naam Ba Sadiki ni jambo jema, sasa swali ni je!, usiku huu?.”

“Hapana tukienda mda huu litakuwa ni tatizo lingine. Tuache kwanza hadi keso ahsubuhi, ili tujishushe, kwamaana tukienda asubui kidogo italeta mantiki. Kwa adhabu za usikuu huu wale watoto watakuwa wamejifunza kabisa. Naijua vizuri sana Malindi mimi, nimeishi sana hapa kabla.” Mama na Saleh alitoa wazo. Likaungwa mkono na wote. Wakalala pamoja siku hiyo kusubili usiku mrefu ambao ulikuwa unasogea kibishi sana. Usiku uliotia mgomo kuzisukuma saa na kufanya alfajiri ikuche kwa manati. Hakuna aliyopata usingizi. Wote walilala upande mmoja.

********
Usiku uleule, mfalme hakutaka kulala na dukuduku. Alisogea eneo la tukio ambako Saleh amewekwa. Alisikitika mno kumwona kijana mdogo kama huyo anacheza na hisia na mtoto wake anavyotaka yeye. Alimsogelea Saleh.

“Kijana!, kwa hali uliyonayo sasa, hapawi kuwa mbishi. Naenda kulala sasa. Shetani la mauti likinipanda basi kesho ni kifo chako. Tena wewe namaliza polepole bila shida. Na kwa jinsi huna hata jina Malindi!. Ah! Taratibu sana!. Ibo.. hakikisha anajutia huyu!. Umempa adhabu chache sana. Hajatoka hata jasho. Ebu ongeza kijana wangu. Huyu ndio mwizo wako kama sikosei.” Mfalme Bana alikuwa ni katili wa aina yake. Aliyasema hayo akiwa na akili zake timamu ambapo aliona kweli Saleh kapigwa na kuumizwa kiasi cha kutoka damu, lakini hakuona chochote kile kilichofanyika. Akampa tena kichaa rungu.

Baada ya kutoka kwa Saleh alienda kumalizia kwa Binti yake ambaye, kwaza alitaka makubaliano ya polepole lakini ngoma bado ikawa ngumu.

“Baba wewe sio mtu kabisa!, unamuumiza mwaname mwenzako sababu ya Mapenzi” aliwaka Zawadi. Ulikuwa kama ushairi kwa Baba yake.

“Yaani baba sikutegemea kabisa, sidhani kama atakuwa Salama Saleh wangu. Na kama!, Kama! Kama Baba!!, akipotea Saleh na mimi napotea. Eh! Mana sina haki.” Zawadi alikuwa anaongea sana. Kauli zake zilimuuma sana Baba yake akanyanyuka kutaka kuondoka.

“Sitakuja kuelewa na Ibo. Malaya mkubwa huyo!” akatukana mbele ya Mfalme. Mfalme akaona Binti yake amevuka mipaka. Akamchapa kofi la kumnyamazisha. Zawadi akazimia kabisa. Ibo na kijana mwingine wakambembeleza Mfalme awe mpole, kwamaana akizifuata hasira zake basi ataweza kuua.

Wauache usiku upite waje wachukue majibu siku ya pili yake. mfalme alitaka neno ‘ndio’ kutoka kwa mtoto wake. Kuhusu Saleh hakuna wasiwasi kabisa. Ibo atampoteza Saleh kama Maji. Kirahisi sana.

ITAENDELEA .....

Starxav
 
Mtunzi: XAVERY LUOGA
Simulizi; “PENDO HURU’
Namba' 0672493994

EPISODE 14
SEHEMU YA SABA

Alfajiri iliyosubiriwa kwa hamu ikafika. Upepo ukasukuma mawingu kuliziba jua lisiwe kali siku hiyo. Kama ingekuwa ni kipindi cha Masika basi Mvua ingenyea siku hiyo. Kulikuwa na kigiza kidogo amabacho kilishawishi macho ya wengi kutokubali kuwa siku imeshaanza.

Alfajiri ilipofika iliwakuta wakazi wengi wa Malindi bado wapo kitandani ubaridi wa mda huo ulimtoa Saleh katika moja ya kumbukumbu alizokuwa anaziota siku hiyo. Alikuja kuzindika na kuhisi maumivu makali mgongoni na katika mbavu zake za kiume. Alikuwa amechakazwa usiku mzima. Alikuwa hajielewi Saleh. Alikuja tu kushituka yupo bado palepale ambapo kumbukumbu zake zilimrudisha hadi jioni yake aliposhikwa. Alikuwa hatamaniki Saleh.

Alianza kuita lakini sauti haitoki. Walimtesa sana Saleh. Alikata hadi sauti. Sijui nini alifanywa usiku mzima. Alikuwa na mabaka tu ya kipigo Saleh!. Mgongo ulirandwa randwa kama mbao ya msitu Misisipi. Alipigwa na mijeredi Saleh.

Akajikongoja kuona kama anaweza kuinuka. Akashindwa. Hakukuwa na mtu sehemu hiyo walimtelekeza kuashiria kuwa alikuwa sehemu salama na ngumu kutoroka. Saleh alishindwa kutoka kwenye ile kamba. Mapenzi yakaendelea kumtafuna taratibu. hakusita kutoa chozi mwenyewe na kulalamika kwa Mwenyezi Mungu kosa amabalo amefanya katika maisha yake.

“Saleh!, Saleh!” ikasikika sauti ya Zawadi kutoka kwenye ukungu wa alfajiri hiyo. Zawadi akatokea mikononi mwa Saleh. Sijui alijikomboaje, Akamkumbatia kipenzi chake.

Kwa hali ambayo Zawadi amemkuta Saleh ilimtoa chozi, akaanza kulia kwa hali ambayo amemkuta nayo kipenzi chake. Saleh alikuwa hatamaniki. Alichafuka hadi kichwa. utadhani hivi vidudu vinavyosukuma kinyesi.

“Ulikuwa wapi?” aliuza Saleh bila kujali kilio cha Zawadi.

“Saleh!, tutoke hapa. Naogopa!” alijibu Zawadi huku akiangaika kufungua kamba za Saleh lakini zilishikizwa kisawasawa.

“Zawadi, nini kinaendelea?” Saleh hakuwa mchoyo wa maswali aliuliza swali jingine.

“Saleh!, kimya! Shiii.... Tuondoke hapa sasa!” alilalamika Zawadi akifuta machozi na kuangalia kama anaweza pata kitu cha kukataa kamba hiyo. ujasiri ulimvaa Zawadi.

“Yes!” aliwaka Zawadi mara baada ya kupata kipande cha bati kando na alipofungwa Saleh. Akakata kamba hiyo kivivu vivu. Uanauke wake ulikuwa kikwazo katika aina ya eneo kama hilo. Saleh aliisi kujikojolea iwapo wangekutwa hapo anafanya njama za kuokolewa. si Zawadi, si Saleh wote waoga wa kutupwa.

“Haraka Zawadi!” Saleh alikuwa mwoga kwelikweli. Hatimaye akawa huru. Zawadi alikata kamba. Wakakumbatiana na kuruhusu tena hali ya machozi iwajie.

Mkukumkuku wakaandamana kutafuta njia ya siri kutoka katika kasri la mfalme. Wakapita sehemu ambayo kwa mara ya kwanza Zawadi alishikiliwa humo. Lilikuwa ni banda. Banda alilolazwa mtoto wa mfalme usiku nzima bila theruthi ya chakula.

“Chukua hii nguo, jivike!” alisema Zawadi huku akimvua mlinzi mmoja ambaye alionekana amelala ndani ya bando hilo ambalo aliwekwa Zawadi. akampa Saleh nguo ya kuvika kifua chake, maana alivuliwa nguo ya juu wakati anachakazwa na Mhasimu wake Ibo.

“Zawadi!! hayupo macho huyo?” Saleh aliuliza swali la kijinga ambalo Lilikuwa halina majibu kwa wakati hule. Zawadi aliangaika tu na uso wake kutafuta pahali pa kutokea.

“Alikuwa mlinzi huyu. Nikamshawishi akaja ndani, nikampa kisi na kumpiga kitu kizito kichwani. Amekufa!, Nisamehe Saleh!, ni kwaajili yako hii!... Saleh Tupite huku.” Tayari Zawadi alishaona njia ya kupita.

Zawadi aliomesha upendo wa dhati mno. heheheheee... kuomba samahani bila kosa? hakika mapenzi Kazi iliyo na kipato, lakini haina mshahara.

Naaam!!, wakaongozana huko kwa aina mbalimbali za hatua hadi kufanikiwa kuwakwepa askari wazembe ambao hadi muda huo wa kazi bado walikuwa wanasinzia.

Ikawa mpenyo kwao. Wakakimbia. Wakatoweka Saleh na Zawadi. Walitoka nje ya kasri la mfalme, lakini walipita upande ambao sio sahihi. Walipita upande wa Msitu wa Malindi. Msitu usio isha historia katika kijiji hiko. Ulifahamika kama Msitu usijulikana chanzo chake.. wakatokea upande huo.

***********************
Alfajiri hiyohiyi baada ya kutoroka kwa Saleh na Zawadi, Mfalme naye aliona bado hajachelewa. Tayari alishafunga njia kuelekea kwa watuhumuwa wake. Leo ilikuwa kufa au kupona yao.

Mfalme alishatunga katiba yake kichwani iliyo amuru vifungu vya kummaliza kabisa Saleh na kumwozesha Binti yake kwa nguvu. Haikujua mipango yote aliyopanga usiku mzima ni bure kabisa. Hakukuwa na Saleh wala Zawadi aliyepo mbele yao. Walishakula kona.

“Mtukufu Mfalme!, Vijana wamekimbia!” ikaja taarifa miguuni mwake. Ibo alikuwa amepiga goti kuunganisha uzito wa taarifa na heshima yake kwa Mfalme.

“Bado sijakuelewa ki-kijana!, unamaana?” aliuliza apate kuelewa sawasawa Mfalme.

“Sa-Leh, Sale yule kijana na Zawadi wametoroka?” alirudia. Bado taarifa ilimchanganya Mfalme, akuielewa vizuri. Akapelekesha haraka zake hadi sehemu ya Tukio. Hakuna mtu.

“Ayaaa!, Kha kha kha kha! Chee!” alilalama Mfalme. Alitaka kuua mtu. Aliyabinya meno yake machache ya mbele bila kuangalia jua. Uso ukazidi kupauka kwa jazba. Akageuka alipo Ibo ambaye alikuwa anamfuata kwa nyuma.

“Ebu rudia ile taarifa, umesema?” alishapaniki Mfalme alimtega tu Ibo arudie ili apate nafasi ya kumwadhibu. Alishajua Ibo akajihami mapema.

“Ni uzembe wa kijana mmoja Mfalme!” alijibu kwa mashaka. Nguvu za Ibo zikamfanya Mfalme awe na heshima kwake. Akapoa Mfalme.

“Kijana mmoja?? Na wamepita njia gani walinzi kila kona?” aliuliza swali lenye maana sana, kwa maana kasri yote ya mfalme ilijawa na askari hodari. Wamepitaje?

“Ah!, Ah! Unajua Mtuku….!” Alibabaika Ibo asijue cha kusema.

“Nini wewe!, Eh!, Nini Ibo utaniambia. Tayari mshakula rushwa!, Hadi mwanangu?.. Sasa ayaa Tafuta tafuuutaaaa!, usipoteze mda!, Tafuta haraka aaaahg!!, Walinziiiii kuja hapa. Pita kila kona tafuta.” Aliwaka mfalme. Alishindwa kabisa kumuadhibu Ibo sababu ya fikra zake kuwa anaweza kuwa mtawala rasmi wa Malindi. Mfalme alikuwa hana mtoto wa kiume, walijaa wa kike tu na Zawadi ndiye mkubwa sasa kama Zawadi analewa na Ibo si ndio mfalme huyo?.

Naaaam! Askari wakaitika wito na kupanga mstari mmoja. Ibo akachukua nafasi yake kuamlisha na kusubiri amri kutoka kwa mfalme, lakini cha kushangaza Mfalme hakuongea chochote kile zaidi ya kuondoka zake.

Alishamkabidhi kila kitu Ibo ambaye ndiye kiongozi wa Msafara. Alishamjua Ibo iwe mvua au juwa, kifo au Mateso lazima Saleh na Zawadi wapatikane. Wakatawanyika eneo la tukio.

Wakaondoka mashujaa wale kutafuta kitu walichoagizwa. Walibaki askari wachache sana kwa ajili ya ulizi wa mfalme. Hawakuondoka wote.

**********
HAYAHAYA SASA!! Moto umewaka Malindi, Mfalme hashikiki, Mpenzi wa Ibo ametokomea na Saleh Msituni Malindi. Msitu hatari kuliko historia yake. Wazazi wa Saleh si wanaenda kwa Mfalme jamani. Dhambiii..

ITAENDELEA....!
Naitaji Like na Comment yako.. katika Safari hii ya PENDO HURU.

Starxav
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom