The Professor
JF-Expert Member
- Apr 30, 2013
- 2,223
- 4,587
- Thread starter
- #21
vipi mkuu? tatizo nn?
ABCDEFGHIJKLMNOPQRSTUVWXYZ
ABCDEFGHIJKLMNOPQRSTUVWXYZ
Daaahhh.... Tang nizaliwe hii ndo Riwaya ya pil kunitoa machoz.... Ya kwanza n mfadhili enz hzo nkiwa 4m six...!NISAMEHE GRACE - 16
Ilipoishia…
Mimi ndiye niliyemuongezea binti yenu damu yenye maambukizi….
Songa nayo…
Ilikua ni siku ya jumatatu tarehe 23 mwezi wa 10 mwaka 2006 siku nilipokua daktari wa zamu katika hospitali ya Wadi Muqshin ambapo majira ya saa 2 na nusu usiku binti mmoja mwenye umri wa kati ya miaka 19-20 aliletwa akiwa amezirai huku akionekana kupoteza damu nyingi sana kwa sababu ya yale majeraha aliyokua nayo ambayo yalitokana na ajali mbaya ya gari baada ya kumpokea mimi pamoja na timu yangu tulimpeleka mpaka katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya kumsafisha yale majeraha pamoja na kuyashona.’ yule dereva tax alisema.
Na baada ya kumfikisha katika chumba cha upasuaji kitu cha kwanza ilikua ni lazima tumuongezee damu na hapo ndipo matatizo yalipoanzia maana damu zote za group 0 zilikua zimeisha katika bank ya hospitali hiyo kitu kilichofanya mimi pamoja na wale madaktari wenzangu tupime damu zetu na ndipo damu yangu ikaendana na damu ya binti yenu lakini nilisita kabisa kumuongezea damu yangu maana nilijua wazi kua nilikua nimeathirika.
‘hebu muongeze damu tusipofanya hivyo ni lazima atakufa’ madaktari wenzangu waliniambia.
‘najua kua atakufa lakini mimi ni muathirika’ niliwajibu.
‘wewe ni daktari lazima ujue thamani ya uhai wa mgonjwa wako hebu muongezee tu maana inaweza kuusogeza uhai wake hata miaka 5 mbele huoni ni afadhali kuliko akifa hapa’ waliniambia.
Yale maneno ya madaktari wenzangu yalifanya nimtazame kwa huruma yule binti aliyekua ameletwa pale hospitalini na wasamaria wema akiwa amezirai kitu kilichopelekea kufanya yale maamuzi magumu ya kutoa damu yangu yenye maambukizi na kumuongezea ili kuyaokoa maisha yake yaliyoonekana kuelekea ukiongoni na hapo ndipo nilipoamua kutoa damu yangu yenye maambukizi na kumuongezea’ yule dereva tax aliyasema yote hayo huku akilia kama mtoto mdogo mbele ya wazazi wake na Nairath angali akiwa bado amepiga magoti.
‘si bora ungeacha binti yetu afe kuliko anavyoteseka hivi sasa’ mama Nairath alimwambia huku na yeye akilia kwa sababu ya ule upendo na uchungu wa kimama.
‘hakustahili kufa sababu alikua bado binti mdogo sana’ yule dereva tax alisema.
‘tutauamini vipi kama kweli haukukusudia?.’ Mzee Fa-thiya alimuuliza
‘sikukusudia kabisa ndio maana baada ya tukio hilo nilijiwajibisha mimi mwenyewe kwa kuacha kazi na kua dereva tax huku nikiamini siku moja katika mizunguko yangu nitaweza kuonana na binti huyo ili niweze kumuomba msamaha juu ya kile niliyomfanyia lakini nilizunguka karibu miji yote ya hapa Oman pasipo kumuona ma mdio maana nimeshindwa kujizuia kujisema hapa ili miweze kusamehewa na kuitubu dhambi hii iliyonitesa na kunitafuna kwa muda mrefu sana’ alisema.
Sote hatukumjibu chochote bali tuliishia kumuangalia kwa macho yenye hasira na huzuni nyingi hakuna hata mmoja kati yetu aliyetambua thamani ya ule wema wake alioutenda wala uzito wa yale machozi yake yaliyokua yakimdondoka na kukisindikiza kile kilio chake kikubwa cha uchungu kwani wote tuliishia kumhukumu ingawa kiukweli alikua ametenda wema mkubwa ulioyasogeza maisha ya Nairath kufikia mpaka muda huo aliokua amelazwa pale hospitalini Good health.
‘haijalishi umetenda wema kiasi gani kamwe hatutokusamehe mpaka pale binti yetu atakapo kusamehe yeye mwenyewe ndipo nasi tutakusamehe’ mzee Fa-thiya alisema.
Na baada ya maongezi hayo mazito yenye kuumiza sana safari ya kuelekea hospitalini Good health kumuona Nairath ilianza huku ile kesi yangu pamoja na makosa yangu yote niliyotenda yakionekana kuamia juu ya yule dereva tax.
haikua safari ndefu sana kwani baada ya mwendo wa karibu dakika 10 tulifanikiwa kufika salama mpaka pale hospitalini Good health na kisha tukaanza kupiga hatua huku nikiwa nimewabeba watoto wangu kuelekea sehemu ilipokuwepo wodi aliyokua amelazwa Nairath ambapo baada ya mwendo wa kama dakika 2 na nusu hivi tuliifikia wodi hiyo.
‘Nairaaaaaaaaaath!!!! nimekuja hapa kwa ajili yako’ nilisema mara tu baada ya kuingia wodini na kumuona Nairath akiwa amelala kisha nikamkimbilia na kumkumbatia nusura ya kuwaangusha wale watoto wetu.
lakini cha ajabu Nairath hakunijibu kitu sababu ya kushindwa kuongea bali aliishia tu kuniangalia mimi pamoja na wale watoto wetu niliokua nimewabeba.
sikuweza kabisa kuyazuia machozi yasinitoke baada tu ya kumuona Nairath kiukweli nililia sana sikuataka kuamini kama niliyemuona hapo ndiye yule Nairath niliyeonana nae kule St.Anna university muda mrefu uliopita maana Nairath huyu niliyemuona hospitalini hapo alikua amekonda sana bila huruma vipele viliushambulia mwili wake na kuuharibu sana uzuri wa ile sura yake kwani yale macho yake makubwa meupe ya duara yalionekana kuingia ndani ya sura yake huku zile pua zake nyembamba zikionekana kukonda sana na kubaki mifupa mitupu wakati ile midomo yake iliyokua imezawadiwa lips laini ilionekana kujaa vidonda na kukauka kabisa huku zile nywele zake nzuri nyeusi alizokua akipenda kuzilaza kwa nyumba zikionekana kunyonyoka sana na kua kama kuku aliyenyonyolewa kwenye maji ya moto.
Sote tulilia sana hasa yule dereva tax alionekana kulia sana huku akimuomba Nairath msamaha kwa sababu ya kumsababishia mateso yote hayo kwa kumuongezea ile damu yake yenye maambukizi.
‘nisamehe sana binti sikukusudia kabisa kukufanyia hivi’ yule dereva tax alimwambia Nairath huku akilia na kumsimulia kisa kizima jinsi kilivyokua siku ile ambayo Nairath alipata ajali.
Maneno yalionekana kumuumiza sana Nairath ambaye naye alianza kulia huku akionekana kuilazimisha ile midomo yake iliyokua imekauka na kujaa vidonda iseme chochote.
‘u.s.i.ja.l.i ni.me.ku.s.amehe.. i.li.k.u.a ni .kwa..a.j.i.li .yangu’ Nairath alimwambia kwa shida kwa sababu ya maumivu ya vile vidonda vilivyokua vimeushambulia mdomo wake bila huruma na kisha baada ya kumwambia yule dereva tax Nairath aliinita kwa shida tena.
‘Javier na.ku.pe.nda s.an.a, na.o.mba .u.nisa.me.he kabla s.ijafa’ Nairath alinambia.
‘nikusamehe kwa lipi wakati mimi ndiye niliyekukosea tafadhali naomba usiseme hivyo wewe haufi Nairath’ nilimwambia.
‘Javier ni.liku.ku.bali a.ngali ,nili.jua .kua nimea.th.i.ri.ka ni.kwa.sababu n.ili.ku.a na.kup.enda .sana..ndi.o. maana nilishind.w.a ku.ku.ambia. ukweli.’ aliniambia.
‘youre not a crime but love is a crime’
(wewe sio muhalifu mapenzi ndio mahalifu) nilimwambia.
Hivyo ndivyo ilivyokua kwani hali ya Nairath ilizidi kua mbaya siku hadi siku yani kila siku ikawa ni afadhali ya jana kitu kilichofanya nikae pale nchini Oman kwa muda wa miezi mitatu huku nikisaidiana na wazazi wake pamoja na yule dereva tax kumuuguza Nairath mpaka siku alipokuja kufariki dunia tarehe 26 mwezi wa 9 siku ya jumatano ambayo kamwe sitakuja kuisahau katika maisha yangu.
na baada ya kifo chake niliendelea kukaa pale Oman mpaka arobaini yake ilipopita ambapo kwa shingo upande wazazi wake walikubali kunikabidhi wale watoto wangu ili nirudi nao nchini Tanzania huku wakiomba niwalee na kuwatunza katika maadili mema yampendezayo Mungu.
‘asanteni sana kwa wema wenu nitawalea watoto hawa katika maadili mema’ niliwashukuru huku nikiwaaidi kusaidiana na yule mamdogo wake na Nairath aliyeko masaki katika kuwalea hao watoto wangu.
Wao pia walinishukuru sana, wakanitakia kila la heri halafu wakanizawadia na albamu kubwa mbili zilizojaa picha za marehemu Nairath kwa ajili ya kumbukumbu na mwisho tukaagana kwa huzuni kubwa huku wakiniomba isiwe mwisho kwenda tena Oman kuwasalimu na kuwapeleka wajukuu zao kuwasalimia.
Na baada ya kuagana nao niliondoka na wale watoto wangu pamoja na yule dereva tax ambaye mpaka wakati huo alikua amekua kama ndugu mpaka Fahud sehemu yalipokuwepo makaburi ambapo baada ya kufika sote tulikwenda moja kwa moja mpaka mahali lilipokuwepo kaburi la Nairath ambalo kwa mara ya mwisho nililiwekea maua pamoja na kumsalia Nairath dua langu la mwisho.
‘kwa heri Nairath kamwe sitakusahau nahaidi nitawalea watoto wetu kama tulivyokua tumejipangia hapo awali katika zile nyakati zetu za furaha pale St.Anna’ nilisema huku nikipiga hatua zangu kuelekea garini na kuianza ile safari yetu ya kurudi hotelini pale Gulf of Oman.
Tulifika salama mpaka pale hotelini Gulf of Oman sehemu nilipoagana na yule rafiki yangu dereva tax ambaye alihaidi kunitafuta pindi atakapo rejea nyumbani nchini Tanzania.
‘kila la heri sitokusahau’
‘mimi pia sitokusahau kila la heri’ tuliagana.
Ilikua ni huzuni kubwa sana katika kuagana kwetu ambapo baada ya kumaliza niliingia mpaka hotelini nikiwa pamoja na wale watoto wangu na nikaanza kupanga mizigo yangu pamoja na kile chumba nilichokikabidhi siku hiyo muda mchache kabla ya kwenda airport kuianza ile safari ya kurejea nyumbani nchini Tanzania.
Nilienda mpaka airport pale Musqat mjini nikiwa pamoja na watoto wangu sote tukaingia ndani ya ndege ya Oman airways mali ya serikali hiyo na baada ya kuingia safari yetu ya kuelekea nyumbani nchini Tanzania ikaanza.
licha ya ule urefu wa safari pamoja na usumbufu nilioupata kutoka kwa wale malaika wangu wadogo tulifanikiwa kufika na kutua salama juu ya kiwanja cha ndege cha mwl Julias Nyerere na bila kuchelewa nilichukua tax nikapakia mizigo yangu pamoja na wale watoto wangu na safari ya kuelekea nyumbani kwa wazazi wangu ikaanza huku hofu kubwa ikionekana kuuvaa mwili wangu kwa sababu ya kuogopa kupokea taarifa zozote mbaya za Grace pamoja na lawama zilizokua zikisubiri kunishambulia.
Tulifika salama mpaka nyumbani kwa wazazi wangu na baada ya kufika kwa wasiwasi mwingi na hofu kubwa niliusogelea ule mlango wa kuingilia sebleni huku nikiwa nimewabeba watoto wangu pamoja na ile mizigo yangu.
sikuamini kabisa nilichokiona mara tu baada ya mimi kuingia ndani.
Nilimuona mama yangu mzazi akiwa anacheza na mtoto mdogo wa kike ambaye alionekana kufanana sana na Grace.
‘mama mwanao nimerudi naomba unisamehe sana mama’ nilisema huku nikilia na kuwashusha wale watoto wangu kisha nikapiga magoti na kumsogelea.
‘karibu sana mwanangu’ mama alinijibu huku akinikumbatia kwa furaha.
‘asante mama naomba unisamehe sana’ nilimwambia.
‘nisha kusamehe mwanangu’ alinijibu.
‘asante mama vipi Grace yuko wapi’ nilimuuliza kwa hofu kubwa kwa sababu ya kuogopa kunyeshewa mvua ya lawama.
‘Grace alifariki mwanangu pole sana babaa’ aliniambia
‘whaaaaat! ilikuajeee’ nilimuuliza kwa mshangao sababu ya kutoamini alichokisema.
‘mwanangu Grace alifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike ambaye ndiye huyu hapa lakini baada ya kutoka hospitali na kurudi nyumbani kwenu kule mbezi beach alikutana na barua yako juu ya meza uliyomuandikia kuhusu kwenda kwako huko Oman kumtafuta Nairath kiukweli barua hiyo ndiyo ilikua chanzo kikubwa cha kifo chake kwani baada ya kuisoma tu presha ilimpanda akaanguka chini na kupoteza fahamu kitu kilichofanya arudi tena hospitali ambako alilazwa siku 3 na siku ya 4 saa 5 na nusu usiku akaaga dunia pasipo hata kumpa jina mtoto wake.’ mama aliniambia.
‘ni makosa yangu mama, kwa hiyo huyu ni mwanangu’ nilimuuliza.
‘ndiyo ni mwanao kabisa’ mama alinijibu.
‘mmempa jina gani?’ nilimuuliza tena.
‘tuliamua kumpa jina la Nairath kama ishara ya kuwakumbuka nyote’ alisema.
‘Nairaaaath!!?’ nilimuuliza kwa mshangao.
‘ndio anaitwa Nairath mbona umeshtuka’ aliniuliza huku nae akianza kulia.
‘mama Nairath nae amefariki na hawa hapa ni watoto wetu huyu wa kiume anaitwa Javier,na huyu wa kike anaitwa Grace’
Nilimwambia mama yangu huku nikizidi kulia na kumuelezea kila kitu na baada ya kumueleza aliwasogelea na kuwakumbatia huku na mimi kwa mara ya kwanza nikimnyanyua yule mtoto wangu na Grace na kumkumbatia kwa furaha na huzuni nyingi kwa sababu ya jina lake la Nairath kunikumbusha yale yote yaliyotokea kule Oman .
baada ya hayo yote mama alitutarishia chakula nika kila na kukimaliza kisha nae kwa mara ya kwanza akaenda kuwaogesha wale wajukuu wake wawili nilioenda nao na kuwanywesha maziwa ya kopo aliyokua akiyatumia yule Nairath mdogo na ghafla akiwa katika kuwanywesha baba yangu mzee Hernandez aliingia ndani akiwa ametoka national stadium kuangalia mpira na baada ya kuingia tulisalimiana akawaona wajukuu wake wapya tukaongea mengi na kisha tukaenda kulala.
Nilikuja kuamka majira ya saa 3 asubuhi kwa sababu ya uchovu, nikamsaidia mama yangu kuwaogesha wale watoto wangu nikanywa chai halafu nikampigia simu yule rafiki yangu kipenzi bwana Khamis Rajabu aliyekua akiishi kule masaki nikamuomba ampitie yule mamdogo wake na Nairath ambaye naye alikua akiishi masaki na wote waje nyumbani.
kwa wema mkubwa yule rafiki yangu alitii kwani walikuja wote nyumbani majira ya saa 5 asubuhi na tukaongea mengi wakawaona watoto wangu na kisha nikawaomba tuende sote mpaka nyumbani kwa mzee Sebastian tena kwa mara nyingine walikubali tukanda sote mpaka nyumbani kwa mzee Sebastiana na mkewe sehemu tulipoongea na kusameheana kabisa kila kitu huku tukionyana na kupeana tahadhari ili haya yote yasije kujirudia tena.
Tulisameheana kabisa na kusahau kila kitu kisha wakanipeleka mpaka sehemu lilipokuwepo kaburi ka Grace ambapo nilitoa heshima zangu za mwisho nikamuombea dua na kisha nikamuomba msamaha kwa sababu ya kukisababisha kifo chake.
‘Nisamehe Grace’ nilisema huku nikilia na kulitazama kaburi lake.
‘Javier usilie sana maana ulimpoteza Grace na sasa hivi unae Grace ulimpoteza Nairath na sasa hivi unae Nairath bila kusahau nyongeza ya Javier Hernandez’ yule rafiki yangu aliniambia.
‘ni kweli ninao wote lakini hii hainizuii kumuomba msamhama’ nilimwambia huku nikizidi kusema
‘kamwe sijatujia sababu ya kushindwa kutimiza ndoto zangu za kuwa daktari wa upasuaji wa neva na saikolojia bali nitajutia kwa sababu ya kusabisha kifo chako na kutoutambua upendo wako kwangu hakika kamwe sitokuasau.
Mmhhh Nisamehe Grace.
Na maisha yakaendelea kama kawaida.
….mwisho…
ABCDEFGHIJKLMNOPQRSTUVWXYZ
Daaahhh.... Tang nizaliwe hii ndo Riwaya ya pil kunitoa machoz.... Ya kwanza n mfadhili enz hzo nkiwa 4m six...!
#Kaz nzur.... Hongera sana mkuu[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
°•°Faith •Hope •Charity•°•
NISAMEHE GRACE - 16

i like it
MKUU upo vizuri kwa uandishi mzuri kwa kweli. ila umemaliza simulizi pasipo kueleza hadhira ukweli, Je! waliobakia walibaki salama or naowalikuwa wameathirika na vvu kati ya baba na watoto.
Ntarudi