SIMULIZI: Nisamehe Grace

SIMULIZI: Nisamehe Grace

The Professor

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Posts
2,223
Reaction score
4,587
NISAMEHE GRACE-01



Anza nayo..

“Grace Sebastian ni msichana aliyetokea kunipenda sana tokea siku ya kwanza nilipoonana nae chuoni kila mara nilipokua nikikutana nae hakuchoka kunitamkia wazi kua ananipenda kiukweli siwezi kueleza ni jinsi gani binti huyu alivyokua akinipenda kwani alijaribu kufanya kila njia ilimradi aweze kuushawishi moyo wangu ili uweze kuzikubali hisia zake lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kwani moyo wangu haukuonekana kushawishika hata kidogo sio kwa sababu alikua mbaya bali kwa sababu ya moyo wangu kuzidiwa na nguvu ya macho yangu ambayo yalitokea kuvutiwa sana na uzuri wa msichana mmoja aitwae Nairath ambaye alionekana kuwa chotara wa kiarabu, kusema ukweli nilitokea kumpenda sana Nairath ambaye ndiye aliyekua ameuteka na kuuvutia moyo wangu kiasi cha kuufanya ushindwe kuzikubali hisia za Grace ambaye kiukweli alionekana kunipenda sana tena kwa dhati kwani licha ya kumueleza wazi na kumuambia ukweli kua sikua nikimpenda bado hakuchoka kuacha kunipenda.
yote haya yalikua ni ndani ya chuo kikuu cha kimataifa cha Mt.Anna kilichopo katikati ya jiji la Dar es salaam sehemu na mahali ambapo nilikutana na wasichana hao wawili ambao kiukweli walitokea kuyabadilisha na kuyayumbisha sana maisha yangu kiasi cha kufanya nishindwe kuyafikia malengo yangu na kushindwa kuwasahau na kuwatoa kabisa katika kumbukumbu za maisha yangu.

Ilikua ni tarehe 9 mwezi wa 4 mwaka 2011 wakati ambapo kwa mara ya kwanza nilikua nikipiga hatua zangu kuingia ndani ya majengo makubwa ya kisasa ya chuo hicho cha Mt.Anna kilichokua kikimilikiwa na familia moja ya kitajiri sana kutoka nchini Ujerumani.
Nilikua ninaenda kuchukua degree yangu ya kwanza ya udaktari katika magonjwa ya upasuaji wa neva pamoja na baadhi ya masomo ya saikolojia ambayo toka ningali mtoto mdogo nilikua na nikitamani sana kuja kuwa daktari hasa katika mambo hayo ya upasuaji wa neva pamoja na saikolojia.
basi mara baada ya kuingia ndani ya chuo hicho nilianza kuyatembelea maeneo yake ya ndani huku nikiyaangalia majengo yake marefu ya ghorofa yaliyokua yamejengwa kwa ustadi mkubwa sana huku nikizifurahia kuta zake zilizokua zimepambwa kwa rangi nyeupe pamoja na madirisha makubwa ya vioo yaliyoonekana kuyapendezesha sana majengo hayo ya ghorofa hakika nilihisi ni lazima ningepata mafanikio makubwa sana ndani ya chuo hicho cha kisasa kilichoonekana kuwa na karibu kila kitu kilichokua kikihitajika katika masomo ya kidaktari kuanzia mahabara mpaka maktaba na sehemu mbali mbali za kufanyia majaribio.

Basi baada ya kumaliza juma moja pale chuoni siku moja majira ya saa 5 asubuhi muda wa mapumziko nikiwa ninarandaranda ndani ya bustani za chuo hicho huku mawazo pamoja na akili zangu zote zikiwa zimeelekea ndani ya kitabu cha hadithi kiitwacho ‘I will be back’ nilichokua nikikisoma kwa makini sana huku miguu yangu ikijivuta vuta kwenye majani yenye rangi ya dhahabu yaliyokua yamepandikizwa katika kila kiunga wakati ambapo mwanga wa jua na kivuli ulikua ukionekana kuchezacheza juu ya matawi ya miti mikubwa iliyokua ndani ya bustanini hiyo.
Ghafla!! Nikiwa katika kusoma kitabu hicho cha hadithi kikichokua kimeandikwa na mwandishi mashuhuri sana aitwae Fredrick Libena nilishtuka kuona msichana mmoja wa umri wa kati ya miaka 23 – 25 akiwa mita chache mbele yangu huku akiwa anapiga hatua zake kuja sehemu nilipokua nimekaa kiasi cha kufanya nizifunike kurasa za kile kitabu nilichokua nikikisoma ambapo mara tu baada ya yule msichana kunifikia alinisalimia kisha akaketi mahali nilipokua nimekaa na kuanza kuniambia maneno ambayo kiukweli sikutegemea kabisa kuyasikia kutoka katika midomo ya binti huyo aliyeonekana kuwa na uzuri wa aina yake.
Kiukweli sikutaka kuyaamini kabisa maneno aliyokua ameniambia msichana huyo ambaye alikua amejitambulisha kwangu kwa jina la Grace Sebastian kitendo cha msichana huyo kuniambia kuwa ananipenda kilifanya nijione ni kama nilikua ndotoni kiasi cha kufanya akili yangu iwe ngumu kuamini kama kweli masikio yangu yalikua yameisikia vyema sauti laini ya binti huyo iliyoonekana kujaa utulivu wa hali ya juu kabisa.
Grace alikua ni mwanamke mzuri sana nakumbuka alikua na uchangamfu fulani ambao nilikua nikiupenda sana kifupi alikua mchangamfu sana kila mahali alionekana kuongea na kila mtu alikua ni mwepesi wa kucheka kiukweli kwa muda mchache nilioongea naye alifanya nijisikie vizuri sana hakika Grace alinivutia kwa kila kitu kuanzia nywele zake zilizouzunguka uso wake katika mtindo maarufu wa afro huku zaidi ya yote haiba na uchangamfu wake ukionekana kunivutia zaidi toka mwanzo kwa sababu ya mimi kua mkimya mwenye kuwaza mambo yangu na yeye kuonekana kuwa mwema na mchangamfu sana.
Sikumjibu kitu chochote mara baaada ya yeye kuwa ameniambia maneno hayo sio kwa sababu sikua nikimpenda bali ni kwa sababu ndio ilikua mara yangu ya kwanza katika maisha yangu kutamkiwa na mwanamke kua alikua akinipenda tena mwanamke ambaye ndio kwanza nilikua nimeonana nae siku chache huku yale yote tuliyayaongea ndio yakiwa maongezi yetu ya kwanza kabisa toka nionane nae.

Lilikua ni jambo gumu sana kumkataa msichana mzuri kama Grace ambaye alionekana kunivutia sana lakini pia ilikua ngumu sana kumkubalia Grace hasa kwa sababu ndio kwanza tulikua tumefahamiana nilijikuta nikimuomba Grace anipe muda wa kufahamiana kiundani zaidi huku nikimuomba kwanza tuwe marafiki mpaka pale muda ambao ningeona unafaa kwa sisi kuwa wapenzi utakapofika nashukuru Mungu kwani Grace alinielewa huku akisisitiza niweze kumfikiria kiundani zaidi kwa sababu alikua ametokea kunipenda sana kiasi cha kufanya ashindwe kujizuia kunitamkia hisia zake.
hapo ndipo urafiki na ukaribu wangu Grace ulipoanzia mara kwa mara Grace alionekana kuufurahia sana ule ukaribu wetu huku akinisaidia kwa kila kitu kutokana na uwezo na utajiri wa wazazi wake kiasi cha mpaka kufikia hatua ambapo watu wengi pale chuoni walianza kudhani kuwa nilikua nikitembea na Grace kiasi cha kuwafanya baadhi ya wanafunzi wenzangu ikiwemo na baadhi ya marafiki zangu waje kunipongeza huku wengine wakionekana kunitania sana kwa kusema walikua wakinionea wivu kwa sababu nilikua nikiufaidi uzuri wa sura na umbo aliokua nao Grace kitu ambacho kiukweli hakikua hivyo.

Ukaribu wangu mimi na Grace ulionekana kuwa wa furaha sana kiasi cha kufanya mpaka Grace aamini kua nilikua nimemkubali ombi lake ambalo kiukweli kwa ukaribu tuliokua nao sikua sikihitaji tena kumwambia kuwa nilikua nikimpenda kwa sababu mimi mwenyewe nilijikuta nikiwa ndani ya mapenzi mazito na Grace ambaye mpaka wakati huo sikua nimemtamkia wazi kama nilikua nikimpenda ingawa kiukweli mimi mwenye nilikua nikijihisi kuwa nilikua nikimpenda ten asana.
nakumbuka ukaribu wetu huo wa furaha ulidumu kwa muda wa miezi miwili na nusu mpaka ilipofika siku moja ambayo nilikwenda chuoni kwa kuchelewa na kwa sababu ya mvua kubwa iliyoonekana kunyesha ndani ya jiji zima la Dar es salaam kiasi cha kufanya nifike chuoni nikiwa nimelowana na kumkuta msichana mzuri sana aliyeonekana kuwa chotara wa kiarabu ambaye alionekana kuwa mgeni darasani humo akiwa ameketi juu ya kiti pamoja na meza yangu ya kukalia.
“ hii ni nafasi yangu lakini kwa sababu ya uzuri wako nitakuachia”
Nilijikuta nikimwambia yule mwanamke niliyemkuta amekaa juu ya kiti changu kwa sauti tena bila kujizuia huku nikiziinua hatua zangu kuelekea sehemu ilipokuwepo stoo ya chuo hicho kwa ajili ya kuchukua kiti kingine kiasi cha kufanya darasa zima pamoja na uyo msichana mwenyewe waonekane kuvunjika mbavu kwa kucheka sana huku kile kitendo cha mvua ile kunyesha kikionekana kutowapa ma lecture nafasi ya kuingia darasani kabisa.

Basi mara baada ya kuchukua kiti kingine nilikwenda kukiweka sehemu ileile ilipokuwepo nafasi nyangu mahali ambapo yule msichana mrembo alikua amekaa na mara baada ya kukiweka kile kiti na kukaa kabla hata sijamsemesha neno lolote yule msichana alinishukuru sana na kuniomba samahani kwa usumbufu huku akinitolea tabasamu zuri sana ambalo kiukweli liliufanya moyo wangu uanze kuzisahau habari za Grace ambaye mpaka wakati huo hakua bado amefika darasani.
“Usijali karibu sana ninaitwa Javier jisikie hupo nyumbani sawa kabisa na huko utokako”
Nilijikuta nikimwambia msichana yule huku nikijitambulisha jina langu ambapo mara baada ya kujitambulisha na yeye pia alijitambulisha kua alikua anaitwa Nairath na alikua amehamia chuoni hapo mara baada ya kuwa amemaliza masomo yake ya awali ya udaktari katika visiwa vya Oman.

Hapo ndipo ukaribu wetu mimi na Grace ulipooanza kuharibika kwani moyo wangu uligundua mara moja kua ulikua umeshaanza kumpenda sana Nairath kiasi cha kuanza kuuvunja ule ukaribu niliokua nao kati yangu mimi na Grace.
Nairath alikua mwanamke mrembo na mzuri sana pengine kuliko hata Grace hivyo ndivyo moyo ulivyokua umegundua hasa mara baada ya macho kuwa yakiuangalia uzuri wa Nairath kila siku huku yeye mwenyewe akiishia kutabasamu tu kila mara alipokua akigundua kuwa nilikua nikimuangalia sana.
uso wake mwembamba uliokua umepambwa kwa ngozi laini nyeupe huku macho makubwa meupe mazuri makubwa ya duara, pua yake ndefu nyembamba pamoja na midomo yake mizuri iliyokua imezawadiwa lips nzuri nyembamba laini sana zenye rangi nyekundu vikionekana kuupamba sana uso wa Nairath huku nywele zake ndefu nyeusi alizozilaza kwa nyuma zikionekana kunivutia zaidi kuliko ata ule uchangamfu wa Grace kiasi cha kufanya nishindwe kujizuia kumsahau Grace ambaye maskini ya Mungu alionekana kunipenda sana na kuumia kwa ajili yangu lakini sikua na jinsi zaidi ya kuzifuata hisia za moyo wangu.

Ilifika hatua nikashindwa kujizuia kabisa kumwambia ukweli Grace kuwa sikua nikimpenda kwa sababu kiukweli nilimuona amegeuka kua kero kutokana na kunisumbua mara kwa mara hasa kila alipokua akiniona nikiwa nimesimama au nikiwa ninaongea na Nairath ambaye mpaka wakati huo tulikua tumekua marafiki wa karibu kabisa kiasi cha kufanya nisiwe na wasiwasi wa kusubiria majibu atakayonipa mara tu baada ya mimi kumwambia kua nilikua nikimpenda sana.
“nisamehe sana Javier kwa kukusumbua kiukweli nakupenda sana siwezi kuishi bila wewe”
Grace aliniambia maneno hayo huku akiwa amepiga magoti na kulia kwa uchungu sana kiasi cha kuyafanya machozi yaliyokua yakitoka machoni kwake yazilowanishe nguo zake alizokua amezivaa.
Kiukweli sikua nikifurahi kumuona Grace akilia kwa sababu yangu nilikua nikiumia sana kumuona msichana yule mdogo tena wa familia ya kitajiri akiumia na kuteseka kwa sababu yangu na wala sikua nikimfanyia kusudi bali ni kwa sababu ya mapenzi mazito niliyokua nayo juu ya Nairath.
“Grace usilie! Kwa sababu yangu najua kuwa unanipenda sana na ninakushukuru sana kwa
Kunipenda lakini fahamu wazi sitoweza kuwa na wewe naomba unielewes Grace”
Nilijikuta nikimwambia Grace huku na mimi bila kujizuia nikashangaa mvua kubwa ya machozi ikianza kunyesha machoni kwagu huku ikisindikizwa na kilio kikubwa cha kwikwi.

Hivyo ndivyo ilivyokua lakini pamoja na hayo yote bado Grace hakuacha kunipenda mara kadhaa alikua akiniomba anirudishe nyumbani kwetu kwa gari lake aina ya Rv4 sikua nikimkatalia kwa sababu nilijua kama nikifanya hivyo lazima atazidi kuumia sana.
kitendo cha Nairath kuyakubali maombi yangu yangu ya kimapenzi ndicho kilichoonekana kumuumiza sana Grace kitu ambacho hata mimi mwenyewe nilikiona wazi kabisa kwani afya yake ilionekana kuanza kudhoofika sana kiasi hata cha Grace kuanza kulazwa hospitalini na kuongezewa maji mara kwa mara kwa sababu ya msongo wa mawazo aliokua nao.
ilifika hatua Grace akaumwa sana kiasi cha kuwafanya wazazi wake waje nyumbani kwetu kuongea na mimi pamoja na wazazi wangu huku wakiahidi kunipa kila kitu ninachokitaka kama endapo ningekubali kuwa na mtoto wao ambaye alionekana kuumwa ugonjwa wa kichaa cha mapenzi kwa sababu yangu.
kiukweli kitendo cha wazazi wake na Grace bwana na bibi Sebastian kuja nyumbani kwetu na kuongea kila kitu mbele ya wazazi wangu kilimuumiza kila mtu kwani kwa mara ya kwanza toka nizaliwe nilimuona mama yangu akilia machozi tena sio machozi ya furaha kusema labda mwanae nilikua naoa bali yalikua ni machozi ya huzuni ambayo kiukweli kila yalipokua yanadondoka sakafuni ndivyo nilivyojikuta na mimi nikianza kulia kiasi cha kufanya nijaribu kuulazimisha moyo wangu umsahau Nairath kitu ambacho kilionekana kuwa zaidi ya mchezo wa kuigiza ambao haukua na director kwani nilishindwa kabisa kiasi cha kuwafanya wazazi wa pande zote mbili wakubaliane na matokeo kitu ambacho kilionekana kuuweka uhai wa Grace matatani.
hivyo ndivyo hali halisi ilivyokua upande wa Grace ambaye aliukataa mpango wa wazazi wake kumtafutia chuo kingine nchini Marekani kwa sababu ya kuogopa kukaa mbali na mimi kwani licha ya wazazi wake kuamini kua huenda mpango huo ungemsaidia lakini Grace hakua tayari hata kidogo kwani aliamini kuwa ni lazima angekufa kama angekaa bila kuniona kwa muda wa wiki moja mfululizo.

Kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo mapenzi yangu mimi na Nairath yalivyozidi kuongezeka kiasi cha kuzidi kuihatarisha afya ya Grace ambaye ilifikia hatua mpaka akawa anapumulia mashine kwa sababu ya mawazo mazito aliyokua nayo kuonekana kuipandisha sana presha yake.
kiukweli hakuna aliyedhani kama Grace atapona hasa kwa sababu ya afya yake kuonekana kudhoofika zaidi ya ilivyokua safari za mwanzo hasa kile kitendo cha Grace kufungiwa mipira ya oksijeni kilisababisha darasa letu ligubikwe na huzuni kubwa huku baadhi ya wanafunzi wenzetu wakianza kunihukumu mimi kua nilikua muuaji kwa sababu ya kuwa chanzo cha matatizo ya Grace kiasi cha kutoridhika na hukumu yao hio isiyo ya haki na kuanza kumzonga na kumuandama sana Nairath ambaye mpaka wakati huo nilikua nikimuona ni kama ndiye pumziko la maisha yangu.

Itaendelea…..

nb: hii ni simulizi yangu ya kwanza kuiandika mwaka 2014 ko mapungufu yoyote tuvumilie, asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE-02



Hali ya Grace Sebastian ilizidi kua mbaya sana huku habari za kuumwa na kuugua kwake zikionekana kuenea na kusambaa ndani ya chuo kizima cha Mt.Anna kiasi cha kufanya jina la msichana huyu mdogo aliyekua akisumbuliwa na ugonjwa wa mapenzi ligeuke na kua gumzo midomoni mwa wanafunzi wengi ndani na nje ya chuo kikuu hichocha Mt.Anna.
kitendo cha Grace kufahamika sana machoni pa wanafunzi wengi kwa sababu ya ule mvuto aliokua nao na ile haiba ya uchangamfu wake kilionekana kuwafanya wanafunzi wajenge na kuonyesha chuki zao za wazi juu yangu huku wengi wao wakinihukumu na kuniona kama nilikua muuaji kwa sababu ya kuyaweka maisha ya Grace mashakani kwani kitendo cha Grace kupumua kwa kutumia mashine za oksijeni kilionekana kumkatisha tamaa kila mtu sio wazazi wake tu bali ata ndugu zake pamoja na wanafunzi wenzetu wote walionekana kukata tamaa kiasi cha kuwafanya waje kuniomba na kunisihi sana niweze kuitumia ile nafasi muhimu na finyu sana iliyokua imebaki ili kwa pamoja tujaribu kuyaokoa maisha ya msichana huyu mdogo aliyekua karibu kufa kwa sababu ya mateso na maumivu makubwa ya mapenzi.
kiukweli sikua na jinsi zaidi ya kukubali yale yote niliyokua nimeombwa kuyafanya ili tuweze kuyanusuru maisha ya Grace , nilikubali kumsaidia Grace ingawa nilijua wazi kua ni lazima Nairath angeumia sana kwa sababu alikua akinipenda na mimi nilikua nikimpenda sana lakini mwisho wa siku hakukua na jinsi zaidi ya wote wawili kukubali matokeo na kuamua kuvumiliana na kuangalia jinsi ya kuuokoa uhai wa yule msichana mdogo aliyeonekana kuwa kipenzi na kivutio kikubwa machoni pa watu wengi.

“Javier wangu najua kua hauna jinsi lakini jua nakupenda sana tafadhali usije ukapitiliza ukanisahau”
yalikua nia maneno ya Nairath aliyeniambia mara tu baada ya mimi kuamua kumwambia wazi kua nilikua nimekubali kwenda kusaidiana na wazazi pamoja na ndugu wa Grace katika harakati za mwisho za kuyanusuru maisha ya msichana huyu mdogo.
“Nairath wewe ndio mwanamke wa maisha yangu, tena mwanamke wa ndoto zangu hakika sitoweza
kukuacha wala kukusahau naomba uamini kua ninakupenda sana kuliko kitu chochote”
nilimwambia Nairath ambaye muda wote huo alikua akilia kwa huzuni na uchungu mkubwa sana kiasi cha kufanya yale macho yake makubwa meupe ya duara yaonekane kufumbwa kwa uwingi wa machozi yaliyokua yakimtoka kiasi cha kuyalowanisha mashavu yake yaliokua yamepambwa na mibonyeo mikubwa ya mashimo mawili maarufu kama dimpoz katika kila shavu.
“Nakupenda pia Javier na kabla hujaondoka ningeomba leo unipatie haki yangu ya kimapenzi”
Nairath aliniambia huku akinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu kisha akaanza kuinyonya midomo yangu kitu kilichopelekea tuondoke yale maeneo ya chuo na kuingia katika gari aina ya Noah alilokua akilitumia Nairath mwenyewe mpaka maeneo ya masaki nyumbani kwa Ma mdogo wake mahali alipokua akiishi Nairath ambapo mara tu baada ya kufika tulifanya mapenzi tena bila kutumia mpira kitu kilichoonekana kumfurahisha sana Nairath.
basi mara baada ya kufanya mapenzi, Nairath alinirudisha mpaka nyumbani kwetu nilipokua nikiishi kwa kutumia lile gari lake aina ya Noah ambapo mara tu baada ya kunifikisha nyumbani tuliagana kisha nikaenda moja kwa moja mpaka sebuleni na kuwakuta wazazi wake na Grace wakiwa wananisubiri ambapo mara baada ya kuwasalimia niliingia chumbani kwangu na kuchukua begi langu la nguo kisha mimi pamoja na wazazi wake na Grace tukawaaga wazazi wangu ambao walikabidhiwa pesa taslimu sh.milion 5 na baba yake na Grace ikiwa kama shukrani kwa wao kuridhia mimi niende kusaidiana nao katika jitihada za mwisho za kuuokoa uhai wa binti yao wa pekee Grace Sebastian.

Ilikua ni majira ya saa moja na nusu asubuhi wakati ambapo kwa mara ya kwanza nilikua nimesimama mbele ya kitanda kikubwa cha chuma ndani ya chumba kikubwa cha moja ya wodi maalumu ndani ya hospitali kubwa ya taifa ya muhimbili huku macho yangu yakizitazama kwa hofu kubwa zile mashine kubwa na ile mipira mikubwa ya plastiki iliyokua imefungwa mdomoni na puani mwa Grace kwa ajili kusaidia kupitisha hewa ya oksijeni kiasi cha kufanya uso wake uonekane kuvimba na kubadilika rangi.
kiukweli nilijikuta nikianza kulia kwa uchungu huku nikimtazama Grace aliyeonekana kulala kimya kama shina la mgomba lililokua limeangushwa na upepo huku kile kitendo cha macho yake kufumba bila hata ya kope kutingishika kikifanya nianze kuamini zile hukumu za wale wanafunzi kua kweli nilikua muuaji kwani kama isingekua kitendo cha ile screen ya ile mashine ya oksijeni kuonyesha ile chat ya jinsi oksijeni inavyoingia na kutoka hakika usingeweza kubisha kua Grace alikua amekufa.
“Nisamehe Grace!! nilijikuta nikiongea huku nikimwambia Grace ambaye muda wote huo hakuonekana kujua kitu chochote kilichokua kinaendelea, nisamehe sana Grace nisamehe bure nilijikuta nikizidi kusema huku nikilia kwa uchungu kiasi cha kufanya macho yangu yaanze kuuona ukungu mzito ukitanda mbele yangu kwa sababu ya kuanza kufumbwa na uwingi wa machozi yaliyokua yakinitoka.

Kitendo changu cha kulia bila kujizuia kilionekana kuwakatisha sana tamaa wazazi pamoja na ndugu zake na Grace ambao ndo kwanza walikua wamenigeuza mimi na kuniona kama tumaini lao katika kuunusuru uhai wa mwisho wa Grace.
ambapo mara baada ya kumaliza wiki moja kwa shida na kwa machozi makubwa hospitalini hapo bila ya Grace kuamka wala kutingishika baba yake mzee Sebastian alikata shauri na kuamua kumsafirisha Grace mpaka nchini China huku akisema kuwa ni lazima niongozane nao kitendo ambacho kiukweli kilionekana kuwa pigo kubwa sana kwangu kwa sababu nilijua kabisa licha ya kuyakosa masomo chuoni ni lazima ningemkosa Nairath mwanamke niliyetokea kumpenda na kumuamini sana kiasi cha kufanya nione uamuzi huo wa mzee Sebastian ulikua pigo kubwa sana kwangu.
sikua na jinsi zaidi ya kukabiliana na hali halisi naukumbuka siku moja kabla ya safari hiyo nilikwenda kumuaga Nairath ambaye kiukweli hakuonekana kukubaliana kabisa na huo uamuzi niliouchukua kiukweli niliumia sana hasa kila mara nilipokua nikimuona Nairath akilia nilijikuta nikianza kujiona mjinga na mpuuzi kwa kuyaruhusu machozi ya mwanamke niliyekua nikimpenda kupita kiasi yamwagike kirahisi rahisi tu kama kopo la maji lililokua limetoboka.
“usinisahau Javier ninakupenda sana” sauti ya kilio kikavu kilichokua kikisindikizwa na sauti ya kwikwi kutoka katika kinywa cha Nairath ilisikika ikiniambia kwa msisitizo na uchungu mkubwa sana kiasi cha kuufanya mwili wake uonekane kudhoofika sana kwa sababu ya kilio hicho.
“Nairath upo ndani ya mzunguko wangu wa damu kamwe sitoweza kukusahau hata kwa muda wa sekunde moja”
nilimwambia Nairath ambaye tulitumia muda wa zaidi ya masaa 5 kuagana ikiwa ni pamoja na kufanya tendo la ndoa kwa mara nyingine tena ambapo mara baada ya kuagana na kumaliza yale yote tuliyoyafanya nilikwenda moja kwa moja mpaka nyumbani ambapo mara baada ya kufika niliwaeleza wazazi wangu yote yaliyotokea kisha nikawaaga na wao wakanipa baraka zao na kunitakia kila la heri.

Ilikua ni jumanne ya tarehe 7 mwezi wa 6 mwaka 2011 majira saa nane usiku wakati tulipokua tukiianza ile safari ya kwenda kujaribu bahati ya mwisho ya kuyaokoa maisha ya Grace Sebastian ambaye alionekana kulala juu kitanda kwa muda wa zaidi ya wiki moja bila ya kuwa na fahamu ambapo mara baada kumaliza zaidi ya masaa 18 hewani tulifanikiwa kufika na kutua salama juu ya uwanja wa ndege wa Canning ndani ya jiji la Beijing nchini China.
tulitua juu ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Canning ndani ya jiji la Beijing majira ya saa 10 za jioni kwa saa za nchini China siku ya jumatano ambapo mara baada ya kutua tulisaidiwa na uongozi wa uwanja wa ndege huo kumpeleka na kumfikisha Grace mpaka ndani ya hospitali kubwa ya kisasa ambayo toka nianze masomo yangu ya udaktari sikua nimewahi kuiona wala kuisikia.
sikutegemea kabisa kama siku moja nitakuja kuingia ndani ya hospitali ya kisasa namna hiyo ilikua ni hospitali ya Guangzhou maarufu kwa jina Canton jina lililozoeleka na wakazi wa nchini humo kutokana na huduma zao za uhakika zilizokua zikitolewa.

Tulikaa hospitalini hapo Guangzhou kwa zaidi ya muda wa mwezi mmoja na nusu mpaka siku ya jumatatu tarehe 18 mwezi wa 7 majira ya saa sita na nusu usiku wakati ambapo baba yake na Grace mzee Sebastian alipoonekana kusinzia kwa sababu ya uchovu huku mimi nikiwa bado nimeutua uso wangu yangu juu ya kitanda alicholalia Grace huku macho yangu yaliyokua yakibubujikwa machozi yakiutazama uso wake ambao bado ulikua umefungwa mipira yakupitishia oksijeni kwa shida sana kwa sababu ya usingizi niliokua nao.

Ghafla!! nikiwa katika kuuangalia uso wake nilishtuka kuona Grace anakohoa.
“Kho! kho! kho! kho! ilikua ni sauti ya kikohozi iliyosikika kutoka kwa Grace ambae sikua nimeisikia sauti yake kwa zaidi ya mwezi na wiki kadhaa zilizopita kwa sababu ya kuumwa kwake.
kitendo cha Grace kukohoa kilinifanya nipige kelele za furaha huku nikiyafuta machozi ambayo bado yalikua yakiendelea kububujika machoni kwangu .
“Ameamka! ameamka!, amekohoa! amekohoa! nilijikuta nikiongea kwa sauti kubwa sana huku nikimsogelea Grace pale kitandani kiasi cha kumuamsha baba yake mzee Sebastian aliyekua amesinzia ambapo mara baada ya baba yake kuamka bila hata kusema neno aliufungua mlango wa wodi hio na kukimbia kuelekea katika chumba cha daktari huku akipiga kelele
“Doctor she wake!!, she wake!! She still alive”
(dokta ameamka!!, ameamka!! bado ni mzima”
Mzee Sebastian alisema kwa sauti kubwa ya furaha huku akikimbilia katika chumba cha daktari huku furaha yake ikimfanya asahau kuwa hakua amevaa nguo yoyote zaidi ya chupi tu.
haukupita muda daktari pamoja na mzee Sebastian walikuja tena mle wodini ambapo daktari alimtolea Grace ile mipira ya oksijeni ya kupumulia kisha baada ya nusu saa alimlisha kwa kutumia mipira na kisha akatuagiza tumuache Grace apumzike .

Baada ya Grace kupata fahamu tulikaa tena pale hospitalini Guangzhou kwa muda wa wiki moja zaidi mpaka ambapo Grace alionekana kupona kisawasawa ndipo tulipopewa ruhusa ya kuondoka pale hospitali huku ule ushauri aliotupa yule daktari bwana Lee Tianjin ukionekana kuwa mgumu sana kwangu kuutekeleza kwani kitendo cha kutuambia kwamba ili Grace asipatwe tena na matatizo kama yale ya mshtuko ambayo kitaalamu yalikua yakiitwa heart attack ni lazima awe karibu kabisa na mtu ampendaye tena sio kuwa karibu tu bali atimiziwe kila kitu alichokua akikitaka.
nilijua wazi kabisa kuwa ushauri huo kwangu utakua ni mgumu kuutekeleza kwa sababu kiukweli niliona kufanya hivyo itakua ni sawa na kumsaliti Nairath msichana wangu kipenzi ambaye kiukweli sikutaka kumuumiza hata kidogo.
ule ushauri wa yule daktari ulimfanya mzee Sebastian aniite pembeni kabla ya kuanza kuondoka ndani ya hospitali hiyo ya Guangzhou ambapo mara baada ya kuniita alinisihi sana na kuniomba nijaribu kuwa na Grace hata kama simpendi walau nimpumbaze tu ili matatizo yake yasije kujirudia tena na kufanya safari yetu hiyi iwe bure kabisa kitu ambacho kwangu kilikua kigumu sana lakini kutokana na huruma iliyonishika niliamua kukubali kwa shingo upande huku moyo pamoja na ufahamu wangu ukiniambia wazi kabisa kuwa nilikua nikiyahatarisha mapenzi yangu mimi na Nairath.

`Basi mara baada ya kutoka pale hospitali Guangzhou tulikwenda moja kwa moja mpaka katika hotel ya Shijiazhuang ambapo tulikaa huko kwa muda wa mwiki mbili huku nikiifanya ile kazi ngumu ya kuishi kama mume na mtu ambaye sikua na hisia nae hata kidogo kitu kilichoonekana kuumiza sana moyo sana kiasi cha kujikuta nikimfurahisha sana Grace pamoja na baba yake ambaye kila siku alikua akitutembeza mitaa na vitongoji mbalimbali ya nchi hio ya China vikiwemo vile vya Wuhan,Shenyang, Harbin,Shanghai,Xi’an pamoja na Talyuan mahali paliposadikika kuwepo na kaburi la stering kichaa ambaye nilikua nimeziona sinema na filamu zake miaka mingi iliyopita.
Mzee Sebastian aliyafanya yote haya ili kumfurahisa mwanawe huku akijua wazi kabisa kua nilikua nikiumia sana kwani kiukweli nilikosa sana raha kwani kitendo cha kuwa mtumwa wa mapenzi kwa ajili ya kuwafurahisha ya watu wengine kilionekana kuuchosha sana moyo wangu kiasi cha kufanya nianze kumwambia ukweli mzee Sebastian kuwa nilikua nimewakumbuka sana wazazi wangu pamoja na mpenzi wangu Nairath ambapo licha ya kumwambia ukweli huo bado mzee Sebastian hakua akinielewa kwani alionekana kupuuzia sana mpaka siku ambapo nilimtishia kuwa ningemuambiwa wazi tena binti Grace kwa mara nyingine kuwa sikua nikimpenda kitendo ambacho kingesababisha tena matatizo ya Grace.
Kitendo cha kumwambia yale maneno mzee Sebastian kilionekana kumshtua sana kiasi cha kuahidi kwamba kesho angekwenda kukata tiketi za ndege kwa ajili ya kuianza safari yetu ndefu ya kurudi nyumbani nchini Tanzania kitu ambacho kilionekana kunipa furaha kubwa sana kwani niliamini muda si mrefu ningeenda kuonana na wazazi wangu pamoja na mpenzi wangu Nairath.

Ilikua ni saa 12 afrajili wakati nilipoamka na kukuta funguo zikiwa ziketupwa chini ya kitanda nilichokua nimelala na Grace, funguo zile zilionekana kunishtua sana kwani zilikua ni za mlango wa chumba cha mzee Sebastian kiasi cha kufanya nishindwe kuelewa kama yule mzee alikua amelala mlango wazi ama vipi ilibidi niufungue mlango wa chumba chetu na kisha nikatoka nje na kupandisha ngazi moja kwa moja mpaka katika mlango wa chumba cha mzee Sebastian ambapo mara baada ya kuufikia niliukuta umefungwa nilipopiga hodi kwa zaidi ya mara tatu haukufunguliwa kitu kilichofanya niufungue kwa kutumia zile funguo nilizoziokota pale chini ya kitanda chetu.
Sikutaka kuamini kitu nilichokiona mara baada ya kuufungua ule mlango na kuingia ndani kwani sikumkuta mzee Sebastian wala sikuliona hata begi lake la nguo ghafla nikiwa katika kushangaa niliona kipande cha karatasi kikiwa juu ya mto wa kitanda ambapo nilikichukua na kuanza kukisoma

“Samahani sana mwanangu Javier Hernandez kwa kuchukua uamuzi huu ambao najua wazi kuwa utakuumiza sana, nimeamua, nimeamua kufanya hivi kwa sababu nampenda sana mwanangu hivi usomapo ujumbe huu nipo ndani ya ndege ya ethiopia airline nikirudi nyumbani nchini Tanzania pesa zote za matumizi utazikuta ndani ya briefcase chini ya uvungu wa kitanda ila unisamehe kwa kuondoka na hati zenu za kusafiria”

Maskini ya Mungu maneno yale ya ile barua yalifanya nisiweze kustahimili kwa zaidi ya dakika 2 kwani nilijikuta nikanguka chini na kupoteza fahamu mara baada ya akili yangu kugundua kua mzee yule alikua amenitelekeza pale nchini China kwa sababu ya kuyalazimisha mapenzi yangu yaamie juu ya mwanae.

….. itaendelea …

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE-03



Nilikuja kushtuka na kujikuta nikiwa juu ya kitanda kikubwa cha ndani ya ile hospitali ya Guangzhou mahali alipokua amelazwa Grace siku moja iliyopita, huku kile kitendo cha kuamka kikifanya niangaze macho yangu pande zote za ndani ya kile chumba nilichojikuta nimelazwa ndani yake ambapo katika kuangaza nilimuona yule daktari aliemuhudumia Grace siku moja iliyopita bwana Lee Tianjin akiwa ananihudumia huku Grace mwenyewe akiwa amekaa pembeni ya kile kitanda mahali nilipokua nikikaa mimi wakati yeye alipokua akiumwa siku chache zilizopita huku akiwa analia.
kitendo cha kuzinduka na kurudiwa na fahamu kilionekana kuirejesha furaha yote ya Grace ambaye muda wote huo alikua akilia kwani mara tu baada ya mimi kuzinduka bila hata kuchelewa aliinuka kutoka mahali alipokua amekaa na kunisogelea kisha akanikuambatia na kunipiga busu katika midomo yangu kitendo ambacho kiukweli kilinichafua sana kiasi cha kuzirudisha kumbukumbu zangu juu ya unyama wote alionitendea baba yake mzee Sebastian ambayo ulifanya nianze kumchukia sana Grace na kumuona kama mtu aliyekua akiziharibu ndoto za maisha yangu za mimi kuishi na mwanamke niliyekua nikimpenda sana katika maisha yangu Nairath.
mara baada ya kuzinduka na kurudiwa na fahamu yule daktari bwana Lee Tianjin alinisogelea kisha baada ya kunifikia aliichomoa sindano kubwa ya dripu iliyokua ikining’ia mkono wangu wa kulia halafu akaniambia nipumzike kwa muda wa nusu saa ambapo mara baada ya muda huo kupita alikuja akanipa ruhusa ya kuondoka huku akinipa pole juu ya matatizo yote yaliyonikuta tokea siku ya kwanza niliyoenda hospitalini pale nikiwa na mzee Sebastian pamoja na Grace ambaye muda huo alikua hajitambui mpaka siku hiyo niliyokua nikiondoka na Grace .

Ilikua ni majira ya saa 7 mchana kwa saa za nchini China wakati ambao mimi pamoja na Grace tulikua njiani kuelekea katika ile hoteli ya Shijiazhuang mara tu baada ya kuruhusiwa kutoka pale hospitalini Guangzhou na yule daktari bwana Lee Tianjin ambaye alionekana kua mwema na mkarimu sana tokea siku ya kwanza alipoanza kutuhudumia katika yale matatizo ya mwanzo kabisa ya Grace.
tulitumia muda wa zaidi ya nusu saa mpaka kufika pale hotelini Shijiazhuang ambapo mara tu baada ya kufika ilitugharimu dollar 40(zaidi ya sh.elfu 64 za tz) kumlipa yule dereva tax aliyetutoa pale hospitalini Guangzhou mpaka kutufikisha pale hotelini ambapo mara baada ya kumlipa pesa yule dereva tulienda moja kwa moja mpaka ndani ya kile chumba chetu tulichokua tukikaa mimi na Grace.

Tulifanikiwa kufika salama mpaka ndani ya kile chumba tulichokua tukiishi pale hotelini ambapo mara baada ya kuingia ndani bila kupoteza muda nilienda kuoga ndani ya bafu kubwa la kisasa lililokuwepo ndani ya chumba hicho ambalo kiukweli sikutegemea kama siku moja katika maisha yangu nitakuja kutumia au kuoga ndani ya bafu zuri kama lile.
lilikua ni bafu zuri sana tena la kisasa ambalo sikuwa nimewahi kuliona kwa macho yangu zaidi ya kuishia kuliona tu katika sinema na filamu za kigeni hasa za kutoka katika nchi za kimagharibi nina hakika kama ungeingia ndani yake basi ni lazima usingetamani kutoka.
lakini Ghaflaa!! nikiwa katika kuoga nilishtuka na kushangaa sana mara baada ya kumuona Grace akiwa amesimama mbele yangu kama alivyozaliwa huku macho yake yakiwa yametua juu ya nyeti zangu ambazo hazikua zimesitiriwa na kitu chochote.

“Javier lazima niuridhishe moyo wangu , lazima unipe mapenzi yako yote leo”
Grace aliniambia huku akinisogelea mara baada ya kuniona nimesimaa huku nikiwa nimepigwa na butwaa kwa sababu ya kutoamini kile kilichokua kinaendelea muda huo.
“No!! no,no,no tafadhali Grace naomba usifanye hivyo please”
nilijikuta nikimjibu Grace huku nikizisitiri nyeti zangu kwa kuzifunika na viganja vya mkono wangu kiukweli nilijaribu kumzuia sio kwa sababu nilikua siwezi kumridhisha bali kwa sababu nilijua kufanya vile ni sawa na kumsaliti Nairath msichana niliyekua nikimpenda sana kuliko kitu chochote
“oowh,Javier nakupenda sana kiukweli siwezi kujizuia kabisa”.
Grace aliniambia huku akivitoa vile viganja vilivyokua vimezisitiri nyeti zangu mara tu baada ya kuwa amenifika pale nilipokua nimesimama.

Kile kitendo cha Grace kuvitoa vile viganja vyangu na kufanya nyeti zangu zibaki wazi kilifanya nishindwe kujizuia kuzitimiza haja zake kwani kitendo cha nyeti zangu kubaki wazi kilimpa nafasi ya yeye kufanya anachokitaka kwani alinifanyia mambo ambayo kiukweli kwa mwanaume yoyote rijali ni lazima angeshawishika kufanya kama alivyokua akitaka Grace.
Ooooooowh aaassssssssh aaaahhhhhhhh,” ilikua ni milio ya sauti laini ya kudeka kutoka kwa Grace ambayo ndiyo iliyonichanganya sana kiasi cha kufanya moyo wangu pamoja na akili zangu zote zimsahau Nairath na kujikuta nikitoa na kumpa ushirikianao wote Grace ambaye alikifurahia sana kitendo kile huku kutotumia kinga kukionekana kumfurahisha zaidi kiasi cha kufanya ashindwe kulizuia kabisa tabasamu zito liliokua limeutawala uso wake.

“Asante sana Javier,umenifrahisha,umeniridhisha kiukweli nime enjoy hakika nitazidi kukupenda sana”
Grace aliniambia huku akizichezea nyeti zangu na kuniogesha ndani ya ile swimming pool kubwa iliyokuwepo ndani ya lile bafu la kisasa lilokua na kila kitu kwa ajili ya usafi wa mwili mara tu baada ya kuwa tumemaliza kufanya kile kitendo.
nilijikuta nikiishia kumuangalia tu bila kumwambia neno lolote Grace huku yale maneno yake yaliyo ambatana na tabasamu kubwa pamoja na sauti ya kudeka vikionekana kuniudhi sana kwani mara tu baada ya kumaliza kile kitendo moyo wangu ulianza kunisuta sana huku ile akili iliyokua imemsahau kabisa Nairath wakati wa kitendo kile ikionekena kuipitisha sura na taswira ya Nairath mbele ya macho yangu kiasi cha kuifanya dhamira yangu inisute kwa sababu ya kuivunja ile ahadi niliyokua nikimuhaidia Nairath kila siku iendayo kwa Mungu kuwa kamwe sitoweza kumsaliti hata siku moja.

Maskini ya Mungu nilijikuta nikilia sana huku nikiziangalia picha za Nairath nilizokua nazo ndani ya begi langu na kuanza kuziomba sana masamaha kana kwamba zilikua zikinielewa.
kile kitendo changu cha kulia mbele ya picha za Nairath kilionekana kumuumiza sana Grace kwa sababu alikua akinipenda sana kwani licha ya juhudi zake alizozifanya za kunipagawisha katika mahaba tuliyopeana bado hakua amefanikiwa kuushawishi moyo wangu.
“Javier jaribu kusahau kuhusu Nairath, kwani haya ndiyo maisha yetu mapya kwani tutaendelea kuishi hapa nchini China hebu angalia pesa kama pesa tunazo za kutosha kwanini hutaki kunielewa”
Grace aliniambia huku akinionyesha lile briefcase lililokua limejaa pesa zilizoachwa na baba yake mzee Sebastian kwa ajili ya matumizi ya kuufanikisha ule mpango wao.
“Grace pesa sio kila kitu kama unavyodhani lakini kwanini wewe pamoja na baba yako mmeamua kuniadhibu kiasi hichi kosa gani nililowakosea”
ilijikuta nikimwambia Grace kwa ukali huku yale maneno yake yakionekana kunichefua zaidi kiasi cha kuipanua mishipa mishipa yangu ya damu na kuifanya hasira kubwa nilikokua nayo ipenye na kuingia ndani ya mzunguko huo wa damu nabkuenea mwili mzima.
“Javier naomba unisamehe najua unaumia sana lakini mimi pia naumia please chukua hizi pesa na kuanzia sasa utakua mume wangu na mimi nitakua mkeo”
Grace aliniambia huku akinikabidhi lile briefcase lililokua limejaa pesa tena noti za dollar mia moja mia moja (dollar100=sh.160,000 za tz)
kitendo cha Grace kunikabidhi lile briefcase lililokua limejaa pesa kilifanya nishindwe kujizuia kwani niliinuka pale kitandani na kuzitupa chini zile picha za Nairath na kumumbatia Grace huku nikilichukua lile briefcase na kwa mara ya kwanza kwa hiali yangu nikainyonya midomo yake kitendo kilichomfanya Grace aamini kuwa yeye pamoja na wazazi wake walikua wameufaulu ule mchezo waliokua wameupanga.

Nilikaa na Grace pale nchini China kwa muda wa zaidi ya minne huku kile kitendo cha Grace kunikabidhi zile pesa kikionekana kunituliza kabisa kwani nilianza kumpa Grace kila alichokua akikitaka ikiwemo hata kufanya mapenzi nilifanya yote hayo sio kwa sababu pesa aliyonipa ilikua ni kila kitu bali nilifanya hivi kwa sababu nyuma ya pazia akili yangu ilikua ikinituma kufanya kile kitendo alichonifanyia baba yake kiukweli japo Grace hakua na makosa yoyote niliamua kufanya hivo kwa ajili ya kurudi nyumbani nchini Tanzania kwa lengo kubwa la kuja kuwaona wazazi wangu,Nairath pamoja na ndugu zangu ambao sikua nimewasiliana nao kwa jumla ya miezi sita na ziku kadhaa zilizopita muda ambao nilikua nimeumaliza nchini China kuanzia miezi minne niliyokaa na Grace nchini humo pamoja na ile miezi miwili na kidogo niliyokaa pamoja na mzee Sebastian wakati wa kuumwa kwa Grace.

Ule muda wa miezi minne niliokaa na Grace pale nchini China niliutumia kwa kuomba hati ya kusafiria kimya kimya bila ya Grace kujua jambo lolote linaloendelea tena kwa kutumia ileile pesa ya baba yake aliyonipatia yeye mwenyewe huku msaada wa yule daktari bwana Lee Tianjin niliyekutana nae pale hospitalini Guangzhou wa kunionyesha mahali zilipokua balozi za Tanzania nchini China ukinisaidia sana kwani mara tu baada ya kufika balozini hapo nilisaidiwa na watanzia wenzangu tena kwa upendo mkubwa kiasi cha kudhihirisha kweli watanzia tulikua wakarimu.
nilifanikiwa kupata hati ya kusafiria tena kwa huruma nilimtafutia na Grace pia sio kwa sababu nilikua ninataka arudi nchini Tanzania kwa sababu ya kuteseka pindi atakaponiona nikiwa na Nairath hapana bali niliamua umtafutia nae hati kwa sababu nilijua kama angejua nimemtoroka ni lazima angenifuata na bila ya kuwa na hati ni lazima angelazimika kusubiri tena muda wa zaidi ya mwezi mmoja ama miwili ndipo aweze kupata hati nyingine kutokana na sheria ya nchi yoyote isemavyo na nilifanya hivi pia kwa sababu nilijua wazi kabisa kua huenda Grace angeamua kuchukua uamuzi mbaya pengine hata kujiua kama katika muda huo ambao angetakiwa kusubiria hati hiyo ya kusafiria.

Ilikua ni tarehe 5 mwezi wa 1 mwaka 2012 wakati ambapo ilikua imebaki siku moja kabla ya kuianza ile safari yangu ya siri ambayio nilijua wazi kua ni lazima ingemuumiza sana Grace lakini sikua na jinsi zaidi ya kufanya hivyo licha ya kwamba Grace alionekana kua mjamzito kwani kitendo tulichokifanya siku ile tena bila kutumia kinga kilionekana kumpa ujauzito Grace ambaye tokea mwanzo alionekana kujua jambo hilo hasa kutokana na kufurahi na kunishukuru kwake mara kwa mara.
nakumbuka mchana mzima wa siku hio niliutumia sana kuiangalia tiketi yangu ya ndege ya shirika Fly Emirates huku nikimuomba Mungu aepushe hatari zozote ambazo zingeweza kutokea kwa Grace ambaye mpaka muda huo alionekana kuilea na kuitunza ile mimba niliyompa kwa umakini mkubwa tena wa hali ya juu sana.
nilijikuta nikianza kulia sana tena kwa uchungu mkubwa kwa sababu licha ya kwamba sikua nikimpenda Grace lakini kile kiumbe kilichokua ndani ya tumbo lake kilikua ni damu yangu kabisa na nilijua wazi kua ninaiacha damu yangu pengine hata kuisababishia matatizo lakini kila nilipomkubuka Nairath wangu nilie muacha nyumbani nchini Tanzania moyo wangu ulichukua maamuzi magumua sana ya kuamua kuiacha damu yangu iliyokua ndani ya tumbo la Grace sio kwa sababu sikuipenda bali kwa sababu kile kitendo change cha kufanya mapenzi pia na Nairath tena mara mbili bila kutumia kinga kilionekana kinipa moyo na kuamua kurudi nyumbani kwa sababu kama kweli alikua na ujauzito kama nilivyokua nikidhani basi ni lazima angekua katika harakati na siku zake za mwisho za kujifungua.
Niliamua kuchukua maamuzi magumu ambayo bila shaka yangemuumiza kila mtu si mimi tub alia Grace angeumia kwa sababu ya kumtelekeza wakati akiwa na ujauzito wangu, pia mimi ningeumia kwa kukosa kukihudumia kiumbe changu kilichopo ndani ya tumbo la msichana aliyetokea kunipenda sana pia Nairath wangu angeumia sana kama angefahamu kua nilimsaliti na kumpa Grace ujauzito huku mwisho kile kiumbe kilichopo ndani ya tumbo la Grace kingeumia kwa kukosa mapezi ya baba yake aliyekua hampendi mama yake hata kidogo.

“Kwaheri Grace,,najua kua ni lazima utaumia sana pindi utakaporudi kutoka hospitalini kwenye mazoezi ya kumlea mtoto wetu, lakini ninaomba unisamehe sana tena pengine kuliko hata mimi nilivyomsamehe baba yako kwa kitendo chake cha kututelekeza hapa,
nimejikuta nimeanza sana kukupenda sio kimapenzi kama utakavyo bali kwa sababu ya kuhifadhi damu yangu ndani ya tumbo lako tafadhali sana ninaomba ukitunze kiumbe chetu kwa sababu ni mwanetu sote hata kama bado ajazaliwa, mimi ninatangulia nyumbani nchini Tanzania kwa sababu ya kuwaona wazazi wangu wapendwa pamoja na kipenzi chaangu Nairath ambaye bila shaka nae atakua mjamzito kwa sababu ya kitendo nilichokifanya nae hakitofautiani sana na mazingira tuliyofanya mimi na wewe.
Mimi ninakutangulia tu wala sikukimbii kama alivyotukimbia baba yako mzee Sebastian na ndio maana katika kuutambua na kuthamini mapendo yaki kwangu nimeamua kukutafutia hati ya kusafiria mara baada ya kuchukua vielelezo vyako voye ndani ya website ya chuo chetu cha St.Anna mahali tulipokuana mimi na wewe mpaka kufikia katika hali hii, pia ninakuachia nusu ya pesa zote alizotachia baba yako mzee Sebastian kama alivyofanya nawe pia utazikuta chini ya uvungu.
Nakutakia kila la heri mama wa kiumbe change mpaka pale tutakapo kutana nyumbani nchini Tanzania na kuusubiria kwa hamu wakati mzuri wa kukipokea kiumbe chetu na kukikaribisha katika ardhi za wazazi wetu in our motherland kwa lugha ya kigeni.
Ni mimi wako umpendae Javier Hernandez.

Nilijikuta nikimuandikia Grace baruaa hiyo kwa uchungu huku machozi yakinitoka na kuilowanisha nusu ya karatasi la hiyo barua nzima niliyoiandika.
Kisha mara baada ya kumaliza kuandika nikachukua nusu ya zile pesa kutoka kwenye briefcase nikaziweka kwenye begi langu la nguo kisha nikachukua ile hati ya kusafiria ya Grace nayo nikaiweka ndani ya lile briefcase pamoja na zile pesa zilizobaki kisha nikalifunga na kuliweka chini ya uvungu wa kile kitanda cha kisasa tulichokua tukilalia halafu ile barua niliyoiandika nikaiweka juu ya mto wangu wa kulalia na nikaanza kuhesaba masaa machache yaliyobaki ili niweze kuianza safari yangu hiyo ya kumtangulia Grace ambaye muda wote huo alikua ameenda katika jimbo la Wuhan katika hospitali maalumu ya akina mama wajawazito ambapo ingemlazimu kukaa huko kwa muda wa siku 2 kwa ajili ya kufanya mazoezi maalumu yaa akina mama wajawazito yaliyokua yakitolewa na serikali hiyo ya nchini China katika majimbo yake kadhaa likiwemo lile la Wuhan na mwengineyo kama ya Changqing,Kunming,Nanning,Changchun na Harbin.

…….itaendelea……..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE - 04



Ilikua ni majira ya saa saba na nusu usiku wakati mawingu mazito yalipoonekana kuufunika mwezi na kufanya nyota zionekane kukosa ushirikiano kiasi cha kufanya giza kubwa liutawale mtaa wa Nanning mahali ilipokuwepo airport maarufu ya jiji la Beijing.
lakini wakati mawingu mazito yanapoonekana kuufunika mwezi na giza kubwa kuutawala mtaa wa Nanning hali ilionekana kuwa tofauti kidogo katika maeneo ulipokuwepo uwanja wa ndege katika mtaa huo.
kwani taa nyingi kubwa zilionekana kutoa mwanga mkubwa bila uchoyo wowote na kuusaidia umati mkubwa wa watu karibu watu 300 waliokua wakisubiria kukaguliwa mizigo yao kwa ajili ya kuianza safari yao ndefu ya kutoka katika bara lililokua likiaminika kuwa bara kubwa kuliko bara lolote duniani.
wakati taa hizo kubwa zikionekana kuutendea mema ule umati wa watu zaidi ya 300 mimi pia nilionekana kuwepo miongoni mwa ule umati wa watu ulioonekana kutendewa wema na zile taa kubwa zilizokua zimelizunguka karibu eneo zima la uwanaja wa ndege wa pale jijini Beijing.
nilikua nimeenda kuianza ile safari yangu ndefu kabisa ambayo nilijua ni lazima ingemuumiza Grace ambaye muda huo alikua katika jimbo la Wuhan kwa ajili ya kufanya mazoezi maalumu pamoja na kujua maendeleo ya afya ya kiumbe kilichokua ndani ya tumbo lake.

Ilikua imefika saa 8 kamili wakati ambapo abiria wote tuliokua tukisafiri kwa ndege ya shirika la Fly emirates tulipoonekana kuingia ndani ya ndege hiyo mara tu baada ya kuwa tumekaguliwa mizigo yetu na kila kitu tulichokua nacho.
na mara baada ya abiria wote kumalizika kuingia ndani ya ndege hiyo injini za ndege hiyo zilianza kuunguruma kisha magurudumu ya ndege hiyo yakaanza kuutimiza wajibu wake wa kuhakikisha yanaikimbiza ndege hiyo ipasavyo ambapo mara baada ya ndege hiyo kwa karibu dakika 2 ilianza kuyainua magurudumu yake ya mbele kuashiria kuwa tulikua tumeanza kupaa.

Ndege hiyo ya shirika la Fly emirates ilifanikiwa kupaa salama ambapo ndani ya dakika chache toka ipae ilionekana kuchepuka ndani ya anga la nchi ya China lililokua limezungukwa na mawingu mazito yaliyokua yakisindikizwa na giza zito sana ambalo lilionekana kusababisha ukimya mkubwa ndani ya ile ndege kutokana na asilimia kubwa ya abiria wote kuonekana kusinzia huku ule ukimya wa ndani ya ndege ile uliotokana na kusinzia kwa abiria wengi ukionekana kuipa nafsi na dhamira yangu nafasi ya kunisuta na kunihukumu kwa sababu ya ule uamuzi mzito niliokua nimeuchukua wa kumuacha Grace mwanamke aliyekua akinipenda sana ambaye maskini ya Mungu mpaka wakati huo alikua amebeba kiumbe changu ndani ya tumbo lake ambalo alionekana kulitunza sana na kulithamini sana hasa mara baada ya kugundua kua alikua ameihifadhi kiumbe changu kitendo ambacho kilionekana kumfurahisha sana.

Kadri ndege hiyo ya Fly emirates ilivyozidi kuchepuka na kuzidi kulifaidi anga la nchi hiyo ya China ndivyo navyo ukimya ule wa ndani ya ndege hiyo ulivyozidi kuongezeka kwa sababu kadri muda ulivyozidi kusonga mbele ndivyo idadi ya watu waliokua wakisinzia ilivyozidi kuongezeka kiasi cha kuuongeza ukimya ambao hakika ulihirusu nafsi yangu inisute kiasi cha kufanya nikose hata lepe la usingizi kabisa.

Nilijikuta nikikosa usingizi kabisa huku moyo wangu ukionekana kugombana na fikra zangu kwa sababu ya mapendo yangu yote kuonekana kua juu ya Nairath huku fikra zangu zote pamoja na mawazo yangu yakionekana kuwa juu ya Grace ambaye nilijikuta nikianza kumuwaza sana hasa mara tu baada ya kugundua kuwa alikua amebeba ujauzito wangu ambao ulifanya mpaka wakati huo niwe ninaitwa baba kijacho.
“.. Eeh Mungu ninaomba unisamehe sana kwa haya yote niliyoyafanya najua kuwa nimekukosea Mungu wangu lakini ninaomba unisamehe na uniongoze katika mitihani hii migumu niliyokua nayo..”

Nilijikuta nikianza kumuomba Mungu kimyakimya hasa mara baada ya kuyakumbuka yale mafundisho ya mama yangu aliyokua akinihusia sana toka ningali mtoto mdogo kutosahau kumuomba Mungu sana katika nyakati zote za furaha,shida,huzuni na uchungu pia.
“..Mumgu wangu ninaomba umsaidie pia Grace ninaomba umuepushie matatizo yoyote pia umsaidie katika maamuzi atakayotaka kuyachukua pindi atakaporudi hotelini Shijiazhuang na kuikuta ile barua niliyomuachia itakayomfanya agundue kua nimeondoka bila ruhusa yake”
Nilijikuta nikizidi kumuomba Mungu ambaye alionekana kuzisikiliza sala zangu na kufanya ule usemi wa Mungu hamtupi mja wake uonekane kutimia kwani wakati namaliza tu kumuomba moyo wangu ulionekana kupata amani ambayo ilionekana kuifukuza ile hofu kubwa iliyokua imeuvaa mwili wangu kiasi cha kufanya na mimi nionekane kuunga mkono ukimya ule mkubwa uliokua umetawala ndani ya ndege hio kubwa kwani nilijikuta nikipata usingizi tena usingizi mzito ulionifanya nisinzie kana kwamba nilikua nimelala masaa mengi yaliyopita a kuwa overtake wote waliokua wamenitangulia kusinzia.

Nilikuja kushtuka majira ya saa 4 asubuhi wakati ambapo ndege hiyo tuliyokua tumeipanda ilionekana kuchepuka juu ya anga la usawa wa bahari ya hindi ambapo baaada ya masaa machache tulifanikiwa kutua salama ndani ya mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo baadhi ya abiria walishuka na kisha tukaendelea na safari ya kuelekea moja kwa moja mpaka nchini Tanzania.

Ilikua ni karibu saa 2 na nusu usiku wakati ambapo ile ndege ya shirika la Fly emirates ilipoonekana kutua juu ya ardhi ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julius kambarage Nyerere kitendo kilichoonekana kunifurahisha sana na kiasi cha kufanya nishindwe kuizuia furaha yangu ya kukanyaga tena juu ya ardhi ya nchi za mama zetu au in our motherland kama ilivyokua imezoewa kutamkwa kwa lugha ya kigeni ambayo ilikua ikiongelewa kwa ufasaha na watanzania wachache sana .
Basi mara baad ya ndege ile kutua ndai ya uwanja ule wa mwalimu Nyerere sikutaka kuchelewa wala kupoteza muda nilienda moja kwa moja mpaka katika mlango wa kutokea nje ya uwanja huo ambapo mara baaada ya kutoka nilichukua usafiri wa tax na kuelekea moja kwa moja mpaka nyumbani kwa wazazi wangu.

Ilituchukua muda wa nusu saa mpaka kufika nyumbani kwa wazazi wangu ambapo ilikua ni majira ya saa tatu usiku wakati ambapo sikuamini kabisa kama kweli nilikua nikipiga hatua zangu kuingia nyumbani kwa wazazi wangu ambao sikua nimeonana nao kariobu nusu mwaka ama miezi sita na kidogo iliyopita.
Ngo! Ngo!ngo!
Nilipiga hodi juu ya mlango wa mbele wa nyumba yetu mara tu baada ya kuufikia ambapo toka nipige hodi hazikupita hata dakika 3 mlango ukafunguliwa .
Mungu wangu !! sikutaka kuamini mtu niliyemuona akiwa amesimama mbele yangu mara tu baada ya ule mlango kufunguliwa.
alikua ni mama yangu mzazi ambaye mara tu baada ya kuufungua mlango na kuniona mtoto wake nikiwa nimesimama mbele ya macho yake alinikumbatia kwa nguvu na kwa upendo mwingi sana wa kimama huku akilia kwa na kupiga kelele za furaha zilizoonekana kumshtua sana baba yangu mzee Hernandez ambaye alikua ndani ya nyumba hiyo.
“..jamani! jamani! Mwanangu amerudiiiiiiiiiiiiiiii amerudiiiiiiiiiiiii Javier wewe kweli umerudiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii”
Zilikua ni kelele za sauti ya mama yangu zilizoambatana na uchungu wa mwana huku zikionekana kuchanganyikana na huzuni pamoja na furaha ndani yake kiasi cha kumfanya baba yangu mzee Hernandez akurupuke na kutoka nje mpaka pale mlangoni tulipokua tumesimama ambapo mara baada ya kutufikia alinikumbatia kwa furaha sana huku akinipa pole na kunikaribisha tena nyumbani.

Basi baada tu baada ya kupokelewa na wazazi wangu na kunikaribisha ndani mama yangu kwa upendo na furaha kubwa ya kimama aliniandalia maji ya kuoga ambapo mara baada ya kuoga niliandaliwa chakula na mara baad ya kumaliza kukila kwa mara ya kwanza toka miezi 6 iliyopita nikasali na wazazi wangu na kumshukuru Mungu kwa furaha kubwa kwa sababu ya wema wake wa kunifikisha nyumbani salama na mara baada ya kumaliza kusali nwazazi wangu wakaniruhusu niende kupumzika huku wakiniambia kua tutaingea kwa kina zaidi kesho .

Nilikwenda kulala ambapo nilikuja kuaamka kesho yake majira ya saa mbili asubuhi ambapo mara baada ya kujiandaa na kunywa chai niliwaaga wazazi wangu kua nilikua ninakwenda chuoni pale St.Anna kwa ajili ya kuonana na Nairath kipenzi cha roho na moyo wangu.
Kitendo cha kuwaaga wazazi wangu na kuwaambia kua nilikua nikienda chuoni kwa ajili ya kumuona Nairath mwanamke niliyekua nikimpenda sana kuliko kitu chochote kilionekana kuwahuzunisha sana wazazi wangu kiasi cha kuwafanya waanze kuniambia kwa huzuni kubwa mambo ambayo kiukweli yalionekana kuumiza sana moyo wangu kiasi cha kufanya niujutuie ule wema wangu wote nilioutenda kwa Grace pamoja na wazaze wake wa kwenda nchini China na kumuacha Nairath wangu.

“Javier mwanangu, mpenzi wako Nairath alikuja hapa kukutafuta na kukuulizia sana karibu miezi 2 au mi 3 mfululizo iliyopita huku kitendo cha kukukosa kila wakati alipokua akija kilimuhuzunisha sana kiasi cha kumfanya atuachie barua pamoja na picha zake zilizomuonyesha kuwa mjamzito huku akitusisitiza sana kuwa tuje tukukabidhi barua hii pamoja na hizi picha kisha akatuaga na kutuambia kua alikua anarudi nyumbani kwao huko visiwani Oman kwa sababu alijua kua umeshakolea katika mapenzi ya Grace kitu ambacho kingemuumiza sana pindi ambapo mngerudi na huku Tanzania mkiwa kama wapenzi na ndio maana akaamua kufanya hivyo.”
Yalikua ni maneno mazito sana kutika katika kinywa cha mama yangu ambaye alikua akiniambia huku akilia kwa sababu ya uchungu ambao alijua ni lazima nitaupata na kunikabidhi ile barua walioachiwa na Nairath pamoja na zile picha zilzomuonesha akiwa mjamzito tena aliyeonekana kuukaribia chungu wa kujifungua kwa sababu ya tumbo lake kuonekana kua kubwa kuliko lile la Grace niliyemuacha nchini China.

Yale maneno ya mama yangu yalinifanya nikose kabisa hata neno la kumjibu kwani nilijikuta nikiichukua ile barua na zile picha tena bila hata kuzitazama wala kuisoma ile barua kisha nikatoka nje na kuanza kukimbia kuelekea sehemu kilipokuwepo kile chuo chetu cha Mt.Anna ili kuhakikisha kama kweli Nairath hukuwepo kwani kuchanganyikiwa kwangu kulifanya nishindwe kabisa kuyaamini maneno ya mama yangu mzazi licha ya kuwepo kwa ule ushahidi wa ile barua.
Nilifika mpaka chuoni ambapo nilipokelewa kwa mshangao mkubwa wa wanafunzi wengi pamoja na waalimu ambao hawakuonekana kuyasahau matukio yetu hata kidogo kwani wengi sana walionekana kuniulizia habari za Grace msichana aliyeonekana kua maarufu sana machoni kwa wanafunzi hao kwa sababu ya ule uchangamfu wake aliokua nao pia wanafunzi wengine pamoja na walimu walionekana kunipa pole pia za kuondoka kwa Nairath kiasi cha kufanya niyaamini maneno ya mama yangu kutokana na msaada mkubwa niliyopewa na mkuu wa department ya academic lecture Julius Elimias ambaye aliniambia na kunionyesha vielelezo vyote vya Nairath kuhama chuo na kurudi nyumbani kwao visiwani Oman.
Kiukweli nilijikuta nikichanganyikiwa sana kwani bila hata kuaga wala kuwasalimia wanafunzi wenzangu nilitoka nduki tena mpaka sehemua ambapo Nairath alikua akipenda sana kulipaku gari lake aina ya Noah ambapo palikua patupu bila hata ya kuwa na dalili za gari kupark hao sio siri nilijikuta nikilia sana huku nikijutia wema wangu ulioniponza na kufanya Nairath wangu kipenzi aondoke.

Lazima nikutafute Nairath, ni lazima nikufuate ulipo, lazima,lazima,lazima nije kuiona damu yangu ambayo bila shaka itakua imeuchukua uzuri wa sura yako . nilijikuta nikijisemea kimya kimya huku nikiondoka pale sehemu ambapo kipenzi changu Nairath alikua akipenda kupark gari lake na kuelekea moja kwa moja mpaka maeneo ya masaki kwa mama yake mdogo mahali alipokua akikaa Nairath ambapo mara baada ya kufika nilipokelewa na kufuri kubwa lilokua liking’inia juu ya geti kubw jeusi ambalo lilionekana kuchafuka sana kitendo kilichoashiria kuwa nyumba hiyo haikua na dalili za kuwa na watu kabisa kwa muda mrefu uliopita kitendo ambacho kiukweli kiliniumiza sana kiasi cha kufanya niitoe barua hiyo ya Nairath na kuanza kuisoma huku nikiwa nimekaa chini na kuliegemea geti hilo lililoonekana kujaa uchafu wa aina yake.

“Mpenzi wangu Javier najua utaumia sana kwa…….
Yalikua ni maneno ya juu kabisa ambayo nilikutana nayo mara tu baada ya kuanza kuisoma ile barua ya Nairath.

…..itaendelea……


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE -05



Ilipoishia…

“Mpenzi wangu Javier najua utaumia sana kwa. . . . .
yalikua ni maneno ya juu kabisa ambayo nilikutana nayo mara tu baada ya
kuanza kuisoma ile barua ya Nairath.

Songa nayo….

Sababu ya uamuzi wangu mzito niliouchukua, ninafahamu kua unanipenda sana Javier, ninajua wazi ni jinsi gani utakavyoumia pindi utakapokua ukiisoma barua hii kwa huzuni kubwa huku ukizitazama picha zangu nilizokuachia kwa macho ya uchungu ambayo pengine bila shaka yatakua yamefumbwa kwa uwingi wa machozi mazito yatakayokua yakikububujika pindi uisomapo barua hii.
Mimi ni mzima kiasi sababu mara kwa mara nimekua nikisumbuliwa na magonjwa madogo madogo ya hapa na pale ambayo kiukweli yamegeuka kua kero kwangu kwa sababu ya kufanya muda wangu mwingi uwe unamalizika karibu na mazingira ya hospitali mara kwa mara lakini ninaomba nikutoe hofu mpenzi wangu licha ya kero hii lakini sitachoka kushinda hospitali kwa sababu ya afya ya kiumbe chetu nilichokihifadhi ndani ya tumbo langu ambapo muda wowote kuanzia sasa ninaweza nikajifungua.
Nimeamua kurudi nyumbani kwetu Oman kwa ajili ya kupumzika, kwa sababu kiukweli nilikata tamaa mara baada ya kukusubiri kwa karibu miezi minne mfululizo bila ya kuona dalili yoyote ya wewe kurudi, Javier mpenzi wangu kitendo cha mimi kuja kwenu kukuulizia miezi minne mfululizo na kupokelewa na majibu mabaya ya kuwa bado hujarudi kiliniumiza sana hakika kama ingekua sio ujauzito ulionipa basi ni lazima ningejiua kwa sababu mpaka sasa hivi niiandikapo barua hii na hadi muda utakapo kua ukuiisoma bado moyo wangu unaumia sana kwa sababu ninajua wazi kabisa kua umeyahamisha mapenzi yako yote kwa Grace kiasi cha kufanya ukae nae nchini China kwa muda wote huo bila hata ya kunikumbuka mpenzi wako either kwa kunipigia simu ama hata kunitumia email.
Javier mpenzi wangu sijui Grace amekupa kitu gani kiasi cha kufanya uwasahau hata wazazi wako kwa muda wote huo kwani kitendo cha wazazi wako kukosa hata namba zako za simu za huko nchini China kinahashiria wazi kabisa kua ni jinsi gani ulivyokolea kwa Grace msichana ambaye anaonekana kukupenda sana lakini ninapenda nikuhakikishie kua Javier wewe bado ni mwanaume wa maisha yangu na ninakupenda sana ndio maana niliamua kukukabidhi moyo wangu tena kama haitoshi niliamua kukukabidhi na mwili wangu pia uufanye vyovyote utakavyo hakika Javier sijutii kukupenda na kamwe sitasikitika kwa mambo yote haya yaliyotokea kwa sababu ninajua kuwa ulilazimika kufanya haya yote ili kuuokoa uhai wa Grace uliokua ukingoni kama mshumaa uwakao ndani ya upepo mkubwa sana ambao bila shaka muda wowote unaweza kukazimika lakini kitu ninachosikitika ni kwa jinsi gani mtoto wetu atakaezaliwa ataweza kuishi bila baba,ninasikitika sana kwa sababu ninajua wazi kua nitashindwa kumjibu maswali atakayokuja kuniuuliza baadae kuhusu uwepo wako wewe baba yake ambaye muda wote huu hata siku moja hukuyasogeza masikio yako juu ya tumbo langu na kuisikia sauti ya mtoto wetu huyu akicheza tumboni mwangu kwa sababu ya kuufurahia upendo na mapenzi yetu sisi wazazi wake ambayo mpaka sasa yanaonekana kuvunjika kwa sababu ya wewe baba yake kuonekana kukosa mapenzi ya dhati kati yetu sisi mimi pamoja na huyu mtoto wetu mtarajiwa.
Nimeamua kurudi nyumbani kwetu kwa sababu ya kuepusha matatizo kwa kua ninafahamu wazi nisingeweza kuvumilia pindi ambapo ungerejea na Grace nchini Tanzania mkiwa kama wapenzi ni wazi kua ningeumia sana na ndio maana nimefanya maamuzi haya ili pengine kuyaokoa maisha yangu pamoja na ya Grace ambaye kiukweli inaonekana kua umetokea kumpenda sana kiasi cha kukufanya uwe mwepesi sana wa kuzisahau ahadi zako ulizokua ukiniambia mara kwa mara pamoja na mambo yetu mengi tuliyokua tumejipangia.
Kama kweli uta bahatika kuisoma barua hii basi ninaomba niambatanishe na shukrani zangu za dhati kwa sababu ya ujauzito ulionipa ambao kiukweli umekua faraja kubwa sana kwangu dhidi ya haya matatizo yote yaliyotokea labda nikuhaidie tu mpenzi wangu kama nitajifungua salama tena nikibahatika kupata mtoto wa kiume basi bila shaka nitampatia jina lako kamili la Javier Hernandez na pia kama nikibahatika kupata mtoto wa kike basi bila shaka nitamuita Grace ili iwe kumbukumbu nzuri sana juu ya haya mambo yote yaliyotokea ambayo kiukweli yamenifundisha mambo mengi sana kuhusu mapenzi na athari zake katika maisha yangu ya kila siku.
Ni mimi nikupendae kwa dhati.
Nairath Al-Jabri.

Ilikua ni barua ndefu sana yenye kuhuzunisha na kukatisha tamaa kabisa kutoka kwa Nairath msichana ambaye kiukweli nilitokea kumpenda na kumthamini sana pengine kuliko kitu chochote.
Kiukweli barua ile ya Nairath ilinihuzunisha sana nilijikuta nikikosa hata nguvu za kusimama kiasi cha kufanya nibaki nimekaa pale chini mbele ya lile geti kubwa la nyumbani kwa mamdogo yake na Nairath ambalo lilikualimeshindiliwa na kufuli kubwa huku nikiwa ninalia kwa uchungu mwingi mithili ya mtoto mdogo aliyekua akilia mara baada ya kua amenyimwa ziwa na mama yake.
Nililia sana tena kwa uchungu mwingi kwa sababu nisingeweza kupinga zaidi kua ilikua wazi kwamba nisingeweza kuonana tena na Nairath ambaye licha ya kunipenda sana aliamua kuondoka na kwenda kuishi mbali na mimi kwa sababu ya kuogopa kuumizwa moyo wake ambao ndio ulikua kiungo muhimu sana katika mwili wa mwanamke huyu mrembo aliyeumbika na kuzawadiwa uzuri wa aina yake.

Nilijikuta nikianza kujuta kwanini niliamua kumsaidia Grace kiasi cha kufanya niende nae nchini China na kukaa nae huko kwa muda wa zaidi ya miezi sita na kidogo na angali mpenzi wangu Nairath alikua mjamzito kiukweli nilizidi kulia sana tena kwa uchungu zaidi huku nikianza kumchukia sana mzee Sebastian baba yake na Grace ambaye ndiye alikua chanzo cha matatizo yote hayo kwani kitendo chake cha kuamua kututelekeza mimi pamoja na mwanae Grace nchini China tena kwa makusudi kabisa na kuamua kubeba mpaka hati zetu za kusafiria ili iwe ngumu kwa mimi kusafiri kurudi nyumbani kuonana na wazazi pamoja na mpenzi wangu Nairath ambaye maskini ya Mungu licha ya kuumizwa na kitendo kile bado hakuchoka kuilea ile mimba yangu niliyompa kabla sijaondoka kuelekea nchini China kwenda kutoa msaada kwa Grace ambao mpaka wakati huo nilikua nikiujutia sana.

‘Nisamehe Nairath, nisamehe sana mpenzi wangu’, nilisema huku nikiikunja ile barua ya Nairath iliyokua imelowana kwa mvua kubwa ya machozi iliyokua ikinyesha machoni kwamgu kiasi cha kufanya macho yangu yaonekane kuvimba na kujaa ukungu mzito uliotokana na uwingi wa machozi hayo.
Nilitamani sana niipaze sauti yangu kwa nguvu zote ili iweze kumfikia Nairath popote alipo na kumueleza ukweli wote wa jinsi mambo yalivyokua.
‘ee Mungu nisaidie niote mbawa mie mja wako walau nipeperuke mpaka kwa Nairath nikameleze ukweli wote ,ee Mungu wangu nisaidie’ nilijikuta nikizidi kusali na kumuomba Mungu huku kuchanganyikiwa kwangu kukifanya nimuombe Mungu anipe mbawa ambazo kwa jinsi akili yangu ilivyokua ikinituma wakati huo ningezitumia kupeperuka mpaka katika visiwa vya Oman na kumtafuta Nairath popote alipo na kisha kumueleza ukweli wa mambo yote jinsi ulivyokua hakika nilitamani Mungu amfunulie Nairath walau hata kwa ndoto uovu wote ambao mzee Sebastian alinitendea wa kutoroka na hati yangu ya kusafiria tena katika nchi ya watu ambayo sikua nimewahi kwenda hata mara moja kiasi cha kufanya iwe ngumu kwangu kurudi nyumbani na kuonekana kama nilikua nimemsahau kabisa Nairath pamoja na wazazi wangu.

Ghafla!!! nikiwa katika kulia kwangu kama mtoto mdogo aliyenyimwa pipi ama ice cream huku miguu yangu ikijivutavuta kwenye mchanga uliokuwepo pembezoni mwa lile geti nilisikia honi kubwa ya gari ikisikika kutoka mita chache mbele yangu kiasi cha kufanya niache kulia na kumtazama mpigaji wa ile honi ambayo kiukweli ilinighutusha sana.
ilikua ni karibu saa 6 na nusu mchana wakati ile honi iliposikika kutoka kwenye gari la rafiki yangu kipenzi bwana Khamis Rajabu ambaye kwa mara ya kwanza nilifahamiana miaka miwili iliyopita wakati tulipokutana katika pub moja ya hoteli maarufu ya Maryland iliyopo maeneo ya coco beach sehemu nilipokua nikienda kutazama mpira mara kwa mara kitendo kilichopelekea mimi na bwana Khamis tufahamiane na kuwa marafiki wakubwa sana kwa sababu ya sisi sote kuwa mashabiki wakubwa wa timu kubwa ya Manchester united inayocheza katika ligi kubwa ambayo kiukweli ina ushindani mkubwa kiasi cha kufanya timu yako ionekane kuwa kubwa pindi inapochukua kombe kubwa la ligi hiyo kubwa yenye ushindani mkubwa hakika ni furaha kubwa timu yako kua kubwa ndani ya ligi hiyo kubwa yenye ushindani mkubwa kwani inakufanya wewe na timu yako wote muonekane kuwa wakubwa.

“Owh!, my God, Javier ni wewe kweli?” rafiki yangu bwana Khamis aliniuliza mara tu baada ya kunipigia ile honi huku akifungua mlango wa gari lake na kuanza kunisogelea kule nilipokua nimekaa huku nikilia kama mtoto mdago.

“Ndio ni mimi” nilimjibu yule rafiki yangu mara tu baada ya yeye kuniuliza lile swali.

“sasa mbona unalia tena katika mazingira haya machafu vipi kuna tatizo kwani? Halafu mbona siku hizi sikuoni kule Maryland rafiki yangu kila siku ninakiangalia kiti chako ulichokua ukipenda kukiklia mara kwa mara” bwana Khamis alizidi kuniambia ambapo mara tu baada ya kufika pale mahali nilipokua nimekaa alinisaidia kuinuka kwa kunivuta mkono wangu wa kulia.

“Ni stori ndefu rafiki yangu tena iliyoambatana na matatizo makubwa ndani yake” nilimjibu yule rafiki yangu bwana Khamis ambaye alionekana kua muumini mzuri sana wa dini ya kiislamu kwani kitendo chake cha kua ndani ya kanzu nzuri jeupe pamoja na uwingi wa ndevu zilizokua zikining’inia chini ya kidevu chake vilionekana kumtambulisha wazi.

“Ooh! pole sana ndugu yangu naomba twende basi nikusogeze mpaka nyumbani ukaweke mwili safi halafu tutafute sehemu nzuri iliyotulia ikiwezekana tuende tena mpaka pale Maryland hotel ukanieleze matatizo yako nione pengine huenda nikaweza kukusaidia katika kuyatafutia ufumbuzi wake” rafiki yangu kipenzi bwana Khamis liniambia ambapo mara baada ya kuniambia yale maneno sikutaka kupingana nae kwani sote tulianza kupiga hatua zetu kulisogelea lile gari lake ambapo mara baada ya kulifikia sote tuliingia ndani na rafiki yangu akaanza kuliendesha huku akifuata maelekezo yangu kwa sababu hakua amewahi kufika nyumbani kwetu hapo awali.

Ilituchukua muda wa kama saa moja na nusu mpaka kufika nyumbani kwetu kwa sababu ya uwingi wa foleni tuliokutana nao barabarani ambapo uwingi ule ulionekana kuichosha sana barabara ile kiasi cha kufanya baadhi ya sehemu zionekane kupasuka na kuchimbika chimbika na kufanya mashimo ya ukubwa tofauti tofauti ambayo yalionekana kua kero kubwa sana kwa madereva wengi.
Basi mara baada kufika nyumbani kwetu tuliwakuta wazazi wangu wakiwa wamekaa nje huku wakionekana kukosa raha kwa sababu ya matatizo makubwa yaliyokua yamenikuta kiasi cha kuanya niyakose hata masomo yangu ya mwanzo ya udaktari juu ya maswala ya upasuaji wa neva na saikolojia ambayo ndo kwanza nilikua nimeanza kuyasoma pale katika kile chuo cha St.Anna mahali ambapo palionekana kuwa chanzo cha matatizo yangu kwa sababu y kunikutanisha na wale wasichana wawili Grace pamoja na Nairath.

Licha ya sura za wazazi wangu kuonekana kukosa furaha kabisa kwa sababu ya kugubikwa na huzuni kubwa iliyotokana na matatizo yangu lakini walijitahidi kuonyesha tabasamu bandia kwa rafiki yangu bwana Khamis Rajabu ambaye nilikua nimeenda nae kitendo kilichonekana kuipunguza ile huzuni iliyokua imetawala katika nyuso zao kwani walionekana kumchangamkia sana yule mgeni wangu.

“Habari za tokea asubuhi?”, baba na mama huyu ni rafiki yangu kipenzi anaitwa bwana Khamis” niliwaambia wazazi mara tu baada ya kuwafikia pale mahali walipokua wamekaa ambapo mara baada ya kumtambulisha yule rafiki yangu walisalimiana tena kwa furaha na uchangamfu wa bandia wazazi wangu walimkaribisha yule rafiki yangu huku wakimtaka ajisikie yupo nyumbani.

Baada ya kusalimiana na kukaribishana niliingia ndani pamoja na yule rafiki yangu ambaye nilimuacha amekaa sebuleni akinywa juisi niliyompelekea kwenye grasi ya udongo huku akinisubiri kitendo kilichofanya nisipoteze muda kabisa kwani baada ya kumpa ile juisi niliingia moja kwa moja mpaka bafuni ambapo nilioga na kuweka mwili safi kisha nikaenda chumbani kwangu nikavalia jinsi dark blue pamoja na t-shirt nyeupe kisha chini nikatupia all sconvesa nyeupe hlafu nikachukua ela kiasi kutoka kwenye lile rundo la pesa nilizopewa na Grace kule nchini China ambazo nilikua nimezificha chini ya kitanda change tokea siku ya kwanza nilipofika nyumbani kutokea kule China.

“Aghrrh!! Eeh bhana daanh umenoga mwanangu umetokelezea ile mbaya” Khamis aliniambia mara tu baada ya mimi kutoka chumbani kwangu na kwenda pale sebuleni alipokua amekaa akinisubiri.

“Mmhh! Mbona kawaida chalii yangu afu vipi mbona unazingua muda wote huu bado hujamaliza hiki ki juisi grass moja tu” nilimuambia Khamis mara tu baada ya yeye kuniambia yale maneno huku nikimshangaa kwa sababu ya kutoimaliza ile juisi niliyompa.

“Usiwaze hapa nyumbani bwana kwani ipo siku nyingine nitakuja nitamaliza jagi zima hadi ushangae hebu kama tayari fanya basi twende” yule rafiki yangu bwana Khamis aliniambia huku akicheka kimatani na kusimama kutoka pale kitini alipokua amekaa na mara baada ya yeye kusimama niliichukua ile juisi aliyokua ameiacha kwenye ile grasi nikaikata fasta kisha nikaipeleka ile grasi mpaka jikoni kwenye sink la vyombo vichafu halafu nikamrudia Khamis kule sebuleni tukatoka na kuwaaga wazazi ambao walinisihi nisichelewe kurudi kwa sababu ya hali yangu kutokua nzuri.

Baada ya kuwaaga wazazi wangu tuliingia ndani ya lile gari la rafiki yangu na kwenda moja kwa moja mpaka maeneo ya coco beach sehemu ilipokuwepo ile hoteli ya Maryland iliyokua na uzuri na umaarufu wa aina yake ambapo mara baada ya kufika na kupark lile gari tulienda mpaka ndani ya ile pub tuliyokua tukiangalizia mpira mara kwa mara sehemu ambapo ndipo urafiki wangu mimi na bwana Khamis ulipoanzia .
ukimya mkubwa tuliokutana nao mle ndani ya ile pub uliotokana na kukosa watu kwa sababu ya kutokuwepo na mechi yoyote siku hiyo ulionekana kutupa fursa nzuri ya mimi pamoja na yule rafiki yangu bwana Khamis rajab kuzungumza na kusikilizana kwa utulivu mkubwa.
ambapo baada ya kukaa katika zile siti zetu za kila siku tuliagiza vinywaji na kisha tukaanza maongezi yetu ambapo nilianza kumwambia yule rafiki yangu kila kitu tokea siku ya kwanza nilipoenda chuoni kwetu na kukutana na yule msichana aitwae Grace mbaye alinitamkia kua ananipenda name nikashindwa kumkubalia mapema kisha nikazidi kumueleza bwana Khamis kila kitu bila kumficha jambo lolote jinsi ukaribu wangu na yule binti ulivyokua mkubwa kana kwamba tulikua wapenzi halafu nikaendelea kumuelezea mpaka siku ambapo msichana mwingine aitwae Nairath alipohamia pale chuoni kwetu na kuuharibu ule ukaribu wangu na Grace kwa sababu ya mimi kutokea kumpenda sana yule msichana Nairath tokea siku ya kwanza alipohamia pale chuoni kwetu St.Anna.
nilimueleza rafiki yangu bwana Khamis jinsi ambavyo yule Grace alianza kuumwa kwa sababu ya mawazo makubwa aliyokua akiyapata kwa sababu ya mimi kuwa karibu na kuonyesha mapenzi yangu wazi juu ya Nairath ambaye naye alionekana kunipenda sana.


….itaendelea…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE - 06



Ilipoishia….

Nilizidi kumwambia yule rafiki yangu bwana Khamis rajabu mambo yote yaliyonitokea
Kiasi cha kumfanya abaki akishangaa sana

Songa nayo…

Rafiki yangu bwana Khamis Rajabu alionekana kushangazwa sana na yale mambo yote niliyomwambia kiasi cha kufanya iwe ngumu sana kwake kuniamini pale nilipoanza kumwambia juu ya habari za ule ugonjwa wa ajabu alioupata Grace mara tu baada ya mimi na Nairath kuwa wapenzi kitu kilichosababisha Grace augue ugonjwa wa ajabu uliomfanya apoteze fahamu karibu wiki moja bila ya kutingishika wala hata kuzichezesha kope za macho yake kitu kilichosababisha baba yake mzee Sebastian aamue kumpeleka nchini China ili kujaribu nafasi ya mwisho ya kuuokoa uhai wa binti yake ambaye kiukweli aliotokea kumpenda sana kwa sababu alikua ndiye mtoto wake wa pekee.

“Pole sana ndugu yangu mmh kwa hiyo ikawaje” rafiki yangu bwana Khamis alinipa pole na kuniuliza huku akionekana kuyasubiri majibu yangu kwa shauku kubwa sana.

“Asante sana ndugu yangu,, Mmhhmmhh” nilimjibu rafiki yangu bwana Khamis huku nikilisafisha koromeo langu na ndipo nikaanza kumsimulia tena juu ya zile habari za ugonjwa wa ajabu alioupata Grace ambao kiukweli ndio ulionekana kuwa chanzo kikubwa cha matatizo yangu yote yaliyonipata.

“Rafiki yangu bwana Khamis mapenzi ni mabaya sana pengine kuliko unavyofikiria, unajua mwanzo mimi pia sikua nikiamini kama kweli mapenzi yanaweza kuua mtu ama kusababisha kifo mpaka pale nilipokuja kusimama mbele ya kitanda cha chuma hospitalini muhimbili kwa zaidi ya wiki moja na wiki mbili nyingine kule hospitalini Guangzhou nchini China huku nikimtaza Grace aliyekua akipumua kwa kutumia mashine za oksijeni hapo ndipo nilipoanza kuamini kua ni kweli mapenzi yanaua tena yanaweza kuua watu wengi sana ndani ya muda mfupi, najua ni vigumu sana kuamini lakini jaribu kusikia hata vyombo vya habari mara utasikia mume kamuua mkewe kwa sababu ya kuchepuka ama utasikia mwanafunzi kajiua kwa sababu yakusalitiwa yote haya ni madhara ya mapenzi” nilimwambia rafiki yangu bwana Khamis ambaye muda wote huu alikua akinisikiliza kwa makini zaidi kuliko ilivyokua hapo mwanzoni na kisha nikaendelea kumwambia.

“Bwana Khamis , matatizo yangu yote yalianza pindi tu mimi na Nairath tulipokua wapenzi kwani hapo ndipo afya ya Grace ilipoonekana kuanza kudhoofika na kupata matatizo ambayo mimi mwenyewe nilikua nikiyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe.
Kwa sababu ule ukaribu wangu wa kimapenzi na Nairath ulionekana kumtesa sana Grace ambaye maskini ya Mungu alitokea kunipenda sana kiasi cha kumfanya aanze kudhoofika kwani hata ule uzuri wa shape na umbo lake aliokua nao ulionekana kuanza kupotea kwa sababu Grace alionekana kuanza kukonda na kupungua sana nadhani ni kwasababu ya maumivu mazito ya mapenzi pamoja na uwingi wa mawazo aliyokua akiyapata ambao kitaalamu ulionekana kumletea matatizo mengi ikiwemo kuzipandisha presha zake na kumfanya aanze kuumwa sana mpaka kufikia hatua ya yeye kuongezewa maji mara mbili mpaka tatu kwa wiki.
Nilizidi kumwambia habari za Grace yule rafiki yangu bwana Khamis ambaye muda wote huu alikua akinisikiliza kwa makini sana huku kile kitendo cha kumueleza jinsi ambavyo ule ugonjwa wa Grace ulivyonifanya niende mpaka nchini China ambapo baba yake alinitoroka na kuchukua hati yangu ya kusafiria na kunifanya nikae huko kwa zaidi ya miezi sita kiasi cha kumfanya Nairath kipenzi cha moyo wangu niliyekua nikimpenda sana achoke kunisubiri kwa kudhani kua nilikua nimemsaliti na kuamua kurudi nyumbani kwao huko visiwani Oman kilionekana kumhuzunisha sana yule rafiki yangu kiasi cha kumfanya yeye mwenyewe aanze kuamini kuwa kweli mapenzi yanaweza kuua..

“Pole sana ndugu yangu Javier sas nimeamini kweli mapenzi yanaweza kuua, lakini vipi umemua kuchukua uamuzi gani mpaka sasa?” yule rafiki yangu bwana Khamis aliniuliza huku akichukua leso kutoka kwenye mfuko wa ile kanzu yake nyeupe aliyokua ameivaa na kuanza kuyafuta machozi ambayo yalikua yamemlenga machoni kwake kwa sababu ya kunisikitikia mimi.

“Bwana Khamis, siwezi kupinga hata kidogo kuwa siwezi kuishi bila ya Nairath ni lazima niende hukohuko nyumbani kwao Oman, ni lazima nikamtafute Nairath wangu kwa sababu kiukweli bado nampenda sana” nilimjibu bwana Khamis ambaye mpaka wakati huo alikua bado ameishika ile leso yake huku akiendelea kuyafuta macho yake yaliyoonekana kulengwa na machozi.

“Ni wazo zuri sana Javier, lakini vipi sasa kuhusu Grace ambaye mpaka sasa umemtelekeza huko nchini China angali yu na ujauzito wako” rafiki yangu aliniuliza huku lile swali lake likionekana kumuhurumia sana Grace ambaye mpaka wakati huo alikua bado nchini China.

“Khamis mimi sijamtelekeza Grace hata kidogo baba yake ndiye aliyenitelekeza mimi kiasi cha kuyaharibu mapenzi yangu na Nairath, Grace na baba yake wameniumiza sana kwa sababu ya pesa zao,hijalishi ujauzito wake aliokua nao najua kua ni wa kwangu lakini hauwezi kunizuia mimi kumtafuta mpenzi wangu Nairath ambaye kiukweli najua nimemkosea sana kupita maelezo” nilimwambia Khamis ambaye mara tu baada ya kumwambia maneno haya alionekana kuguswa sana kiasi cha kumfanya ahaidi kunisaidia.

“Ni kweli Javier mimi nitakusaidia, lakini unatakiwa uwe makini sana kwani usipoangalia unaweza ukampoteza Grace pamoja na kiumbe chenu kilichopo ndani ya tumbo lake. Khamis aliniambia huku kile kitendo cha kusema ataniasidia kikifanya nichanganyikiwe kiasi cha kutozitilia tena mkazo zile habari za Grace pamoja na ile mimba yangu aliyokua nayo.

“Bwana Khamis, kama unaweza kunisaidia nisaidie hata sasa hivi, habari za Grace wewe achana nazo wao si wana pesa acha wazitumie kuyatatua matatizo yake na familia yao”. nilimjibu rafiki yangu bwana Khamis huku nikisubiri kwa hamu kubwa sana ule msaada aliosema atanisaidia.

“Javier kule Oman ni sawa na nyumbani kwetu kwanza kwa sababu ya dini yangu pili kwa sababu ya biashara zangu zilizopelekea niishi muda mwingi huko na kufahamiana na watu wengi sana visiwani humo kiasi cha kufanya nipate ndugu pamoja na marafiki wa kufikia ambao ninataka niwaombe kama wataweza kukusaidia halafu tuone unakwendaje huko.” rafiki yangu kipenzi aliniambia kitendo kilichonifanya nisimame kutoka kwenye kiti na kuruka ruka kwa furaha huku nikimshukuru sana.

Kiukweli yale maneno ya yule rafiki yangu kipenzi bwana Khamis Rajabu ambaye licha ya utofauti wetu wa dini aliamua kunisaidia kwa moyo wote kitu kilichofanya nihisi kuwa ni lazima ningefanikiwa kumpata kipenzi changu Nairath ambaye muda wowote kuanzia wakati ule alikua anaweza kujifungua ule ujauzito wangu niliompa siku za nyuma kabisa wakati nikiondoka kwenda nchini China.

Basi mara baada ya kuongea mengi tuliagana na yule rafiki yangu bwana Khamis ambaye aliniambia nimtafute mara baada ya siku mbili ili anipe majibu atakayokua amepewa na wale rafiki zake wa huko visiwani Oman ambao aliniambia kuwa atafanya nao mawasiliano ilituone jinsi itakavyokua kabla ya mimi kuondoka kwenda visiwani humo kumtafuta Nairath mwanamke wa ndoto zangu.
Mara baada ya kuagana na bwana Khamis niliondoka na kwenda mpaka mlimani city huku nikimkatalia yule rafiki yangu kunipa lifti kama alivyokua akitaka na mara baada ya kumkatalia aliamua kukubali kwa shingo upande akaondoka zake huku akizidi kunisisitiza kua nimtafute mara baada ya siku mbili.

Niliondoka pale Maryland hotel , na kwenda moja kwa moja mpaka mlimani city ambapo nilikwenda kuwanunua wazazi wangu vitu vya matumizi madogo madogo ya nyumbani na baada ya kuwanunulia nikaenda mpaka sehemu zilipokua zikiuzwa nguo za watoto wachanga pamoja na vitoi vya kuchezea ambapo nilinunua nguo za mtoto mdogo wa kiume pamoja na vitoi vya kuchezea kwa kutumia ile ela aliyonipa Grace kule nchini China, nilinunua sio kwa sababu nilijua kua Nairath atajifungua mtoto wa kiume bali nilifanya hivi kwa sababu ile barua ya Nairath ilifanya nimchukie sana Grace pamoja na baba yake mzee Sebastian ambapo niliamua kununua zile nguo za mtoto wa kiume ili kuonyesha msisitizo kwa Mungu kua nilikua ninaomba anisaidie sana Nairath ajifungue mtoto wa kiume ili niepukane na ile adha ya Nairath kumuita mtoto wetu jina la Grace kama alivyoniambia katika ile barua yake aliyoniachia kwa sababu nilijua wazi kuwa hasira zangu nilizokua nazo juu ya Grace na baba yake zingefanya nilichukie lile jina la Grace ambalo bila shaka Nairath alikua ameliandaa kwa sababu ya mtoto wetu kama tu angebahatika kujifungua mtoto wetu wa kiume.

Basi mara baada ya kumaliza manunuzi yangu nilichukua tax lililonipeleka mpaka nyumbani kwetu ambapo mara tu baada ya kufika nilimlipa yule dereva ela yake kisha nikaichukua mizigo yangu na nikaenda moja kwa moja mpaka sebuleni kwetu ambapo kile kitendo changu cha kuingia ndani tu kilifanya nipokelewe na habari mbaya ambazo maskini ya Mungu zilionekana kuwaliza wazazi wangu kwani alama za machozi kukaukia mashavuni mwao zilionekana kueleza wazi kua walikua wametoka kulia muda si mrefu.

“Mama na baba, vipi mbona mnalia kunatatizo gani?,” niliwauliza wazazi wangu ambao nyuso zao zilionekana kujaa huzuni kubwa sana kitu ambacho kilinisikitisha sana kwani haikua kawaida wazazi wangu kuwa katika hali ile mara kwa mara.

“Mwanangu Javier ,,mzee Sebastian kaja hapa muda si mrefu” mama yangu aliniambia mara tu baada ya mimi kuwauliza lile swali ambalo lilikua limechanganyikana na hofu kubwa ndani yake.

“Mzee Sebastian!!!?? Nilimuuliza mama yangu kwa hofu na mshangao mkubwa sana kiasi cha kuiangusha ile mizigo niliyokua nimeishika mkononi kwangu kitu kilichofanya ile Rambo iliyokua na zile nguo pamoja na vitoi ipasuke na nguo zote pamoja na vitoi vimwagike chini.

“Mwanangu mzee Sebastian kaja hapa kukuulizia, tumemwambia ukweli kua umerudi ila umetoka na amesema atarudi kesho kukutafuta sana pia amesisitiza sana kuwa endapo atakukosa atakufungulia mashtaka ya kumpa mtoto wake ujauzito na kumtoroka kule nchini China. Ilikua ni kauli ya mama yangu ambayo kiukweli ilionekana kunishtua sana kiasi cha kufanya ile furaha yote ya rafiki yangu bwana Khamis kunisaidia ipotee kwani nilijikuta nikianza kulia kitendo kilichoonekana kuirudisha ile huzuni ya wazazi wangu.
Nilijikuta nikimchukia sana mzee Sebastian tena safari hii nilimchukia mara mbili zaidi ya awali kwa sababu licha ya uovu wake wa kunitoroka kule nchini China na hati yangu ya kusafiria bado hakuridhika ten licha ya kuyalazimisha mapenzi yangu yahamie kwa mwanae pamoja na wema wote niliomtendea bado hakutosheka mpaka kuamua kuja kwa wazazi wangu na kuwaeleza yale maneno ambayo kiukweli yalionekana kuniumiza sana.
“Mama kwa nini hawa watu wenye pesa wana viburi sana kwanini ni wajeuri kiasi hiki kwani sisi kua maskini imekua kosa , hivi huyu mzee Sebastian ananitaka nini mimi mbona nilishamueleza wazi kua mimi simpendi binti yake tena simpendi hata kidogo mbona ananilazimisha na kunifuatilia kiasi hiki kwani mimi nimemkosea kitu gani? Mbona yeye ndiye aliyenikosea” nilijikuta nikizidi kulia tena kwa uchungu sana kitu kilichoonekana kuwaumiza sana wazazi wangu.

…..itaendelea…..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE - 07



Ilipoishia…..

Baada ya kutoka mlimani city kufanya manunuzi madogo madogo nilirudi nyumbani ambapo mara tu baada ya kufika na kuingia ndani nilipokelewa na habari mbaya kutoka kwa wazazi wangu kuwa mzee Sebastian alikua amekuja kunitafuta huku akiahidi kunifungulia mashtaka kwa sababu ya kumtelekeza binti yake Grace kule nchini China angali alikua ni mjamzito.

Songa nayo….

“Mama haiwezekani!!, haiwezekani hata kidogo hivi huyu mzee Sebastian anataka nini kutoka kwangu yani pamoja na wema wote niliomtendea bado hajaridhika yale makosa yake yote aliyonifanyia anajidai ameyasahau, anadhani mimi sikuumia pindi alivyonitoroka kule nchini China pamoja na hati yangu ya kusafiria kiasi cha kufanya niishi na binti yake kama mume na mke wakati sikua nikimpenda mpaka kuyaharibu mahusiano yangu na Nairath, hakika mama kamwe sitakubali”.
nilimwambia mama yangu huku nikilia kwa huzuni mara tu baada ya yeye kuniambia zile habari za mzee Sebastian.

“Mwanangu kama kweli Grace ni mjamzito basi hauna budi kuishi nae” mama yangu aliniambia mara baada ya mimi kumwambia yale maneno huku akionyesha msisitizo mkubwa kwa sababu ya ile hofu kubwa ya vitisho vya mzee Sebastian.

“Whaaat!! Mama, ninakupenda na ninakuheshimu sana, lakini suala la kuishi na Grace litakua ngumu sana haijalishi hata kama ni mjamzito ,wazazi wangu kumbukeni nyie wenyewe kwa mikono yenu ndio mlionikabidhi ile barua ya Nairath pamoja na zile picha zake ambazo zilikua zikiuonyesha wazi ujauzito wake leo hii mtaniambiaje niishi na Grace nisie mpenda na kumuacha Nairath”. Niliwambia wazazi wangu mama pamoja na baba yangu ambao kiukweli walionekana kutishika sana na vile vitisho vya mzee Sebastian.

“Javier mwanangu, jaribu kumsikiliza mama yako anachokisema, jaribu kumsahau Nairath na uanze maisha mapya na Grace kwani huwezi kujua huyo Nairath wako huko kwao alikokwenda pengine na yeye kapata mwanaume mwingine wa kumuoa” baba yangu aliniambia huku sauti yake kavu iliyojaa kwikwi kwa sababu ya huzuni nyingi ikionekana kumuunga mama yangu mkono.

“Baba na mama, samahani sana kama ninawakosea lakini hio haijalishi kwani barua aliyoniachia Nairath bado inaonyesha wazi kabisa upendo wake mwingi aliokua nao juu yangu hata kama ataamua kuolewa lakini mimi bado ninampenda tena sana japo nilimkosea lakini ninaamini Nairath wangu ni lazima atanisamehe tu kwa mambo yote niliyomfanyia ambayo kiukweli sikukusudia wala sikudhamiria kumfanyia haya yote”
niliwaambia wazazi wangu ambao walionekana kushangazwa na msimamo wangu niliowambia ambao kiukweli ulionekana kuwashangaza sana na kuwatia wasiwasi na hofu kubwa sana.

“Mwanangu hebu kwanza achana na habari za Nairath, sasa hivi inatakiwa tupange jinsi tutakavyofanya kesho kwa sababu mzee Sebastian amesema ni lazima atakuja tena kukutafuta” mama yangu aliniambia huku akilia kwa sababu ya uchungu wa mwana kitu kilichofanya niumie sana kwani katika maisha yangu sikutaka hata siku moja kuona wazazi wangu wanaumia ama kulia kwa ajili yangu.

“mama,najua kuwa mnanipenda sana mimi pia ninawapenda sana tena kuliko mnavyofikiria lakini sitaki huruma yenu iyaharibu maisha yangu nimeshawaambia wazi kua mimi simpendi Grace na hata huyo baba yake mzee Sebastian mimi simuogopi kwa sababu kiukweli mimi sijamkosea hata kidogo tena kama anadhani pesa zake ndio kila kitu basi” asizitumie kwangu akazitumie kwa huyo binti yake Grace ambaye ameyaharibu sana maisha yangu .

Niliwaambia wazazi wangu ambao walionekana kujaa hofu kwa sababu ya vile vitisho vya mzee Sebastian tena hata kabla hawajanijibu neno lolote niliiokota ile mizigo yangu niliyoinunua pale mlimani city kisha nikawakabidhi vile vitu vya ndani nilivyowanunulia halafu nikachukua vile vitoi pamoja na zile nguo za kitoto nikaenda nazo mpaka chumbani kwangu na kuwaacha wazazi wangu wakiwa bado wamekaa pale sebuleni huku wakionekana kushangazwa sana na ule msimamo wangu niliokua nao ambao kiukweli ulionekana kuwakatisha sana tamaa ya wao kunishauri tena.
basi baada ya kuingia chumbani kwangu nilifunga mlango kwa komeo la ndani kisha nikaenda mpaka kitandani kwangu ambapo nilifiunua godoro na kuchukua zile pesa alizonipa Grace kule nchini China na nikaanza kuzihesabu kwa makini huku akili yangu ikionekana kuzipangia bajeti kwa sababu ndizo nilizokua nimepanga kuzitumia katika safari yangu ya siri ya kuelekea visiwani Oman ambayo kiukweli sikutaka wazazi wangu wahifahamu kwasababu nilijua wazi kabisa kua ni lazima wangenizuia kama ningewaambia kua ninaenda Oman kumtafuta Nairath.

Nilizihesabu zile pesa kwa makini sana tena kwa utulivu mkubwa ambazo zilikua ni zaidi ya dollar elfu 20(ml32 za tz) baada ya kuzihesabu zile pesa na kuamini kua zingetosha kunifikisha mpaka Oman nilianza kupanga nguo zangu ambapo nilichukua nguo mpya nilizozinunua kule nchini China nikazichanganya pamoja na zile nguo za kitoto pamoja na vile vitoi kisha nikaziweka ndani ya begi moja ambalo nilikua nimepanga kulitumia katika safari hiyo hata kabla sijakutana na yule rafiki yangu bwana Khamis ambaye alikua ameahidi kunisaidia.
baada ya kumaliza kupanga nguo zangu na kuhakikisha kila kitu kipo sawa nilizirudisha zile pesa chini ya godoro langu kisha nikajitupa kitandani nikaanza kuziangalia zile picha za Nairath huku nikiwaza ni jinsi gani safari yangu hiyo iliyoonekana kujaa ugumu ndani yake itakavyokua .

“Najua safari hii itakua ngumu sana pengine kuliko hata ile safari yangu ya China lakini mimi ni mwanaume kwanini niogope kusafiri, hapana, hapana ni lazima nisafiri ni lazima niende Oman kumtafuta Nairath wangu hata kama nitapata matatizo basi nitakua nimepambana kiume kuliko kukaa hapa na kuishia kumuona huyu mzee Sebastian akifanya upumbavu wake”
Nilijikuta nikijisemea kimoyo moyo huku nikizidi kuziangalia zile picha za Nairath zilizokua zikiuonyesha wazi ukubwa wa tumbo lake kwa sababu ya ule ujauzito aliokua nao.
“naamini Nairath utanisamehe kwa mabaya yote niliyoyatenda kiukweli sikukusudia kufanya hivi nilizidi kusema huku machozi yakinitoka na kuziangalia zile picha kana kwamba zilikua zikinisikia.
kadri nilivyozidi kuziangalia zile picha za Nairath ndivyo machozi ya uchungu yalivyozidi kunitoka kwa sababu kwa sababu uzuri wa Nairath niliokua nikiuona juu ya picha hizo ulifanya akili yangu iirudishe kumbukumbu zangu nyuma na kuanza kuyakumbuka yale matukio yote ya jinsi nilivyokutana na Nairath pale chuoni tokea siku ya kwanza alipohamia na kumkuta akiwa amekaa juu ya kiti changu nikazidi kukumbuka jinsi nilivyokwenda kuchukua kiti kingine na kukiweka palepale alipokua amekaa ambapo ndipo ukaribu wetu ulianzia mpaka ukafikia hatua ya kua wapenzi kisha nikakumbuka muda nilio isikia sauti yake kwa mara ya kwanza kama haitoshi nikakumbuka mpaka ile siku aliponipa lile jibu langu la ndio mara baada ya kua nimemuambia hisia zangu juu yake jambo lilonofanya nijione kua miongoni mwa wanaume wachache wenye bahati kubwa huku ile taswira ya kile kitendo cha kufanya nae mapenzi iliyokua ikijirudia kichwani kwangu ikifanya nishindwe kabisa kuisahau ile sauti yake laini na tamu ya kudeka iliyokua ikisikika pindi tulipokua tukifanya mapenzi, taswira ya juu ya matukio yote haya yaliyokua yakijirudia kichwani kwangu pamoja na zile kumbukumbu za ahadi nilizomuahidi Nairath za kumwambia hata siku moja sitomfanya alie na kujutia kunipenda zililifanya niamue kusafiri mpaka Oman kwenda kumtafuta Nairath ambaye muda huo nilikua nikilia huku nikiishia kumtazama na kumuona kwenye zile picha alizoniachia.

“Siwezi kuupinga huu ukweli uliopo mbele yangu,kama nisipoamua kumtafuta Nairath basi sitamuona tena hata mtoto wangu mtarajiwa nae sitamuona hapana haiwezekani ni lazima niende Oman”
Niliendelea kujisemea kimoyo moyo ambapo hata kabla sijamaliza kujisemea nilikatishwa na hodi kubwa iliyosikika kugonga kwenye ule mlango wa chumba changu ambao nilikua nimeufunga na komeo kwa ndani.

“Nani?, niliuliza mara tu baada ya hodi kusikika huku nikiyafuta yale machozi yaliyokua yameyalemea macho yangu kiasi cha kufanya macho yangu yauone ule mwanga wa ile bulb kubwa ya wat100 liyokua ikining’inia juu ya singbodi kana kwamba ulikua ukififia.

“Javier mwanangu chakula kipo tayari” ilikua ni sauti ya mama yangu iliyoonekana kujaa huzuni kubwa ndani yake ndiyo iliyosikika kutoka upande wa pili wa ule mlango.

“Oh mama ninakuja,” nilimjibu mama yangu huku nikienda kuufungua ule mlango ambapo mara baada ya kuufungua nilimkuta akiwa amesimama kwa huzuni huku mapendo yake ya kimama yakimfanya anisubiri na kwenda nae mpaka sebule ndogo sehemu ilipokuwepo meza ya chakula.

Tulifika mpaka sebuleni sehemu ilipokuwepo meza ya chakula ambapo tulianza kukila kile chakula huku ukimya mkubwa ukionekana kutawala pale sebuleni kwa sababu ya huzuni na hali ya kukata tamaa kwa wazazi wangu walioonekana kumuunga mkono mzee Sebastian kwa ajili ya kuogopa vile vitisho vyake.
Niliendelea kula kile chakula huku nikiwatazama wazazi wangu ambao kiukweli walionekana kunyong’onyea sana yote hii ni kwa sababu ya mapendo yao ya dhati waliyokua nayo juu yangu niliwahurumia sana na nilitamani sana niwafurahishe kwa kukubali mawazo yao ya kumuuo Grace lakini ilikua ngumu sana kwa sababu nilijua kuwa nitakua ninawafurahisha wengine angali mimi mwenyewe nitakua nikiumia moyoni mwangu.
baada ya kumaliza kula niliwashukuru wazazi wangu kwa chakula na upendo mkubwa waliouonyesha kwangu huku nikiwadanganya ili kuwatoa hofu na wasiwasi kwa kuwaambia kua nitayafanyia kazi mawazo pamoja na ushauri wao kitu kilichoonekana kuwapa haueni juu ya maradhi ya hofu waliyokua nayo.

Niliwadanganya wazazi kwangu sio kwa sababu niliwadharau bali kwa sababu sikupenda kuwaona wakiwa katika hali ya huzuni ambayo ilionekana kusababisha ukimya mkubwa sana mule ndani kitu ambacho kilikua hakipendezi.
baada ya maongezi madogo pamoja na ahadi niliyowahaidia wazazi wangu ambayo nilijua wazi kua nisingeweza kuitimiza nilienda moja kwa moja mpaka chumbani kwangu ambapo baada ya kuingia nilifanya kama hapo awali kwani niliufunga tena mlango wangu kwa komeo kisha nikazipanga vizuri zile picha za Nairath nilizokua nimeziacha pale kitandani wakati ambao mama alikua amekuja kunigongea mlango halafu baaada ya kuzipanga nikaisogelea swichi ya taa nikaizima na kwenda kujitupa kitandani tena bila hata ya kushusha neti na nikaanza kuutafuta usingizi ambao ulionekana kutonitendea wema kabisa kwa sababu ya kutonibana haraka kitu kilichofanya nibaki nimetoa macho tu mpaka ule muda ambao usingizi ulikuja kunibana bila ya mimi kujua ilikua ni saa ngapi na kuja kushtuka asubuhi kukiwa kumeshakucha.

Sikuelewa ni muda gani ambao usingizi ulinibana lakini nilikuja kushtuka kukiwa kumeshakucha ilikua ni saa 2 kasorobo za asubuhi ambapo bila hata kuchelewa toka niamke niliichukua simu yangu na kumpigia yule rafiki yangu bwana Khamis ambaye japo muda wa zile siku mbili alizonipa ulikua bado hujafika lakini sikua na jinsi niliamua kumpigia ili kumueleza hali halisi niliyoikuta.
haikupiata dakika moja toka nipige namba zake ambapo sauti yake ilionekana kusikika kutoka kwenye spika za simu yangu.

“Hellow Javier mbona unaonekana una haraka sana zile siku mbili nado hazijaisha bwana vipi wewe inaonekana huyo Nairath wako amekukamata kweli” rafiki yangu bwana Khamis aliniambia mara tu baada ya kupokea simu yangu huku akicheka kwa utani kwa sababu ya kudhani kua nilikua nimempigia ili kuuliza ule msaada aliokua ameniahidi.

“Sio hivyo ndugu yangu nina matatizo bwana, yule mzee Sebastian niliyekueleza habari zake jana, alikuja nyumbani kunitafuta ambapo mara baada ya kunikosa aliamua kuwatisha wazazi wangu kwa sababu ya jeuri ya pesa zake huku akiwaambia kuwa anipashe habari kua ni lazima atanifungulia mashtaka kama nikikataa kusihi na binti yake” nilimwambia rafiki yangu kipenzi.

“Akufungulie mashtaka gani tena? wakati yeye ndiye aliyekukosea” sauti ya rafiki yangu Khamis ilionekana kusikika kutoka kwenye spika za simu yangu huku ikionekana kuwa na mshangao mkubwa.

“Kasema atanifungulia mashtaka kwa sababu ya kumtoroka na kumtelekeza mtoto wake kule nchini China angali nilijua kua ni mjamzito huku amewambia wazazi wangu kua ni lazima anifunge kama nikataa kumuoa binti yake anadai kama simpendi mtoto wake kwanini nimempa ujauzito halafu nimemuacha wakati yeye mwenyewe ndiye chanzo cha haya yote”

Nilimwambia rafiki yangu bwana Khamis ambaye mara baada ya kumwambia aliniambia nimtafute baadae ili tuone tunafanyaje kuhusu vile vitisho vya yule mzee Sebastian.

……itaendelea…..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE - 08



Ilipoishia….

Baada ya kumpigia simu Khamis na kumueleza matatizo niliyoyakuta nyumbani aliniambia nionane nae ili aweze kuona na jinsi gani ataweza kunisaidia.

Songa nayo…

Baada ya kuongea na Khamis na kuniambia tuonane sikutaka kuchelewa kwani nilienda moja kwa moja mpaka bafuni kuoga na kuweka mwili safi halafu nikavaa nguo zangu kisha nikanywa chai na kuwaaga wazazi wangu kua nilikua ninakwenda chuoni kufuatilia masuala yangu jinsi ya kuanza upya yale masomo yangu ya udaktari ambao sikua nimeyasoma kwa zaidi ya semister moja na nusu ama na zaidi kwa sababu ya yale matatizo yaliyokua yamejitokeza hapo katikati kwa muda wa kipindi kirefu.
kiukweli sikua nikienda chuoni kama nilivyowambia wazazi wangu bali niliwadanganya ili kuwatoa hofu kwa sababu sikua na njia nyingine zaidi ya kuwaongopea ingawa nilijua wazi kua nilikua ninawakosea lakini sikua na jinsi kwani uongo huo ulionekana kunisaidia sana.

Baada ya kufaulu kuwaongopea wazazi wangu niliondoka nyumbani na kwenda mpaka ile sehemu tuliyokua tumezoea kukutana mara kwa mara na Khamis pale Maryland hotel.
ilikua ni karibu saa 4 na robo za asubuhi muda niliofika pale Maryland hotel na kumpigia simu yule rafiki yangu bwana Khamis ambaye baada ya kumpigia aliahidi ndani ya muda wa robo saa atakua amefika pale Maryland hotel sehemu nilipokua nikimsubiria.
mara baada ya kuongea na Khamis niliagiza soda ya baridi pamoja na chupa kubwa ya maji safi ambapo nilianza kwanza kuinywa ile soda ya baridi polepole huku nikimsubiri yule rafiki yangu ambaye hata kabla sijaimaliza ile soda alikua ameshafika pale hotelini Maryland na alikua akipiga hatua zake kuja sehemu nilipokua nimekaa kitendo kilichofanya nimuone Khamis kua rafiki yangu wa kweli kwa sababu ya kuonekana kuyajali sana matatizo yangu kiasi hata cha kuziacha shughuli zake na kuja mpaka pale hotelini kuzisikiliza shida zangu.

Baada ya rafiki yangu Khamis kufika pale nilipokua nimekaa tulisalimiana kisha tukayaanza mazungumzo yetu ambapo nilimueleza hali halisi niliyoikuta jana pale nyumbani mara baada ya mimi nay eye kua tumeachana katika ileile hoteli ya Maryland.
sikutaka kumficha kabisa bwana Khamis kwani nilimueleza kila kitu wazi kuhusu vitisho vya mzee Sebastian pia nilimueleza juu ya ile hofu kubwa waliyokua nayo wazazi wangu pamoja na yale mashtaka yake ya kipuuzi aliyoahidi kunifungulia kwa sababu ya ule ujauzito niliompa binti yake ambao yeye aliuona kua kama chambo cha kunipelekesha mimi kama anavyotaka.

“Pole sana Javier, lakini kwanini usianze wewe kumfungulia mashtaka ili ajue kua haumuogopi”
rafiki Khamis aliniambia huku akinishauri mara tu baada ya kumaliza kunisikiliza yale yote niliyomwambia.

“Mimi simuogopi hata kidogo kwasababu najua wazi kua sikumkosea , halafu nikisema nimshtaki nitachelewa ile safari yangu ya kwenda Oman kumtafuta Nairath, bwana Khamis wewe mwenyewe unajua ni jinsi gani natakiwa niifanye hii safari kwa haraka tena hata kabla huyo mwanae Grace hajarudi ili kuepusha mabalaa na matatizo mengine yasijitokeze”
nilimwambia yule rafiki yangu kipenzi bwana Khamis ambaye mara baada ya kumwambia hayo maneno alishauri niende nikalale nyumbani kwake ili kumkwepa mzee Sebastian aliyeahidi kuja nyumbani kwetu siku hiyo kunitafuta kwa mara nyingine tena.

Niliukubali ule ushauri wa rafiki yangu tena bila kipingamizi nilindoka nae mpaka nyumbani kwake maeneo ya masaki huku tukipita ileile barabara ya nyumbani kwa mamdogo yake na Nairath ambapo hali tuliyoikuta haikutofautiana na hapo awali kwani baada ya kufika usawa wa ile nyumba sehemu lilipokuwepo lile geti kubwa mahali nilipokua nikilia siku ile bado kulikua na kufuli kubwa lilioonekana kuning’inia kwenye komeo za chuma za geti hilo kitendo kilichofanya niamini kuwa bila shaka mamdogo huyo alikua ameondoka na Nairath kwenda Oman kitu kilichozidi kuaminisha kua bila shaka Nairath anaweza asirudi tena kuzikanyaga ardhi za nchi hii ya Tanzania.

“Mmmmhhh!!mmmmh!!” nilishusha pumzi za kukata tamaa mara baada ya kufika usawa wa nyumba ile na kuona lile kufuli kubwa lililonipokea jana yake likiwa bado linaning’inia juu ya lile geti jeusi lililoonekana kuchafuka kwa sababu ya kukosa matunzo kwa siku kadhaa.

“Usihofu Javier ni lazima tu utampata huyo Nairath wako ndani ya muda mfupi ujao” alisema yule rafiki yangu mara baada ya kuona nimezishusha zile pumzi zangu zilizoashiria kukata tamaa.

Sikumjibu kitu chochote yule rafiki yangu zaidi ya kuishia kuiangalia ile nyumba iliyokua ikimalizika kuonekana kwa sababu ya ule mwendo kasi wa gari huku nikizikumbuka zile siku alizonileta Nairath ndani ya nyumba hiyo ambayo tulifanyia mapenzi mara mbili ndani yake mpaka kupelekea Nairath apate ujauzito wangu.
ilituchukua muda wa dakika 20 kutoka usawa wa ile nyumba ya mamdogo wake na Nairath mpaka kufika nyumbani kwa yule rafiki yangu bwana Khamis ambapo ilikua ni karibu saa 6 na nusu mchana huku tukiwa tumetumia muda wa zaidi ya masaa mawili barabarani kutoka kule hotelini Maryland mpaka kufika pale nyumbani kwake kwa sababu ya foleni kubwa tuliyokutana nayo barabarani.
baada ya kufika nyumbani kwake bwana Khamis alinikaribisha ndani huku akilipiza ule wema wa wazazi wangu wa kunitaka nijisikie kama nipo nyumbani huku kitendo chake cha kuto kuoa kikionekana kutupa uhuru wa sisi kuongea na kupanga mipango mingi juu ya ile safari yangu ya kwenda Oman kwani mara tu baada ya kuingia ndani alinipa juis halafu akaenda chumbani kwake kuchukua laptop yake kisha akaiwasha na kuanza kunionyesha picha zake alizopiga kule Oman pamoja na wale rafiki zake aliosema atawaomba wanisaidie.

“Na hii ndio ramani ya nchi ya Oman bwana Khamis aliniambia mara baada ya kumaliza kunionyesha zile picha alizopiga pamoja na marafiki zake wa huko Oman.

“Na hapa ni Masqat(muscat) moja kati ya mji maarufu sana nchini Oman ni kama Dar es salaam kwa hapa kwetu Tanzania bwana Khamis alizidi kuniambia huku akinionyesha ule mji wa Masqat kwenye ile ramani iliyokua ndani ya laptop yake.
na hapa ni Barka, hapa Qalhat, hapa ni Quarayyat, hapa Dank , hapa Ar Rustaq , na hapa ni Al Ashkharah, hapa ni Adam yote hii ni miji midogo inayouzunguka mji huu wa Musqat ambapo ninaamini bila shaka huyo Nairth wako ni lazima atakuwepo ndani ya moja ya mijii hii ambapo karibu miji yote hii ina marafiki zangu wa kutosha ambao bila shaka hawatasita kukusaidia kama tu nikiwaomba wafanye hivyo rafiki yangu bwana Khamis alizidi kuniambia huku akinionyesha ile miji yote aliyoitaja kwa kugusa ile screen ya laptop yake ambayo ilikua ikiionyesha ramani ya nchi hiyo ya Oman ambayo kwa aslimia kubwa ilikua imezungukwa na maji pande zote.
Baada ya bwana Khamis kumaliza kunionyesha ile miji maarufu ya nchini Oman alinitajia na baadhi ya miji mingine kama vile miji ya Haima, Fahud, Duqm, Khaluf, Daqwa, Thamarit, Marmul, Sawqirah, Salalah, Raysut pamoja na historia za miji hiyo kwa ufupi ambayo kutokana na maelezo yake aliniambia kua alikwisha wahi kuitembelea yote hiyo kwa sababu ya biashara zake pamoja na dini yake ambayo mara kwa mara vyote kwa pamoja vilikua vikifanya aishi huko kwa muda mrefu kitu kilichomfanya apate marafiki na ndugu wengi wa kufikia katika nchi hio.
kisha baada ya kumaliza kunionyesha miji hiyo yote pamoja na historia zake kwa ufupi alichukua simu yak na kuanza kuwapigia wale rafiki zake waliopo kule Oman ambapo mara baada ya kupiga namba kadhaa na kuona hazipokelewi ali I connect ile laptop yake kwenye mtandao kisha akaanza kutuma email kadhaa kwa wale rafiki zake tofauti tofauti ambapo mara baada ya kumaliza kutuma zile email aliizima laptop yake na kuniambia kua ni lazima nikae pale kwake mpaka pale muda wa safari yangu utakapofika huku akiniambia niifunge simu yangu ili kukwepa kero za kupigiwa na wazazi wangu pindi mzee Sebastian atakapokua amefika nyumbani kunitafuta.

Nilikaa pale nyumbani kwa rafiki yangu bwana Khamis kwa muda wa siku kadhaa huku nikisubiria majibu ya zile email alizozituma Khamis kwa wale rafiki zake wa kule Oman wakati siku ya tatu toka azitume zile email majibu yalikuja huku karibu wale rafiki zake wote aliowatumia zile email wakionekana kukubali maombi yake kitu kilichofanya mimi pamoja na Khamis mwenyewe tuhisi kua hakika safari yangu ingekua ni ya mafanikio.

Ilikua ni siku ya Jumatano siku tuliyopata reply za zile email alizozituma Khamis kitendo kilichofanya nisitake kuichelewesha kabisa ile safari yangu kwani nilipanga kuondoka siku ya jumamosi kitendo kilichofanya usiku wa siku hiyo niende nyumbani kwa wazazi wangu kwa lengo la kuwaaga ikiwa ni pamoja na kuchukua zile pesa alizonipa Grace ambazo mpaka wakati huo nilikua nimezificha chini ya godoro chumbani kwangu.

Ilikua ni saa 3 kasorobo usiku wakati nilipoongozana na rafiki yangu bwana Khamis mpaka nyumbani kwa wazazi wangu kwa kutumia usafiri wa gari lake ambapo mita chache kabla hatujafika nyumbani kwetu alisimamisha gari kisha nikashuka na kuanza kupiga hatua zangu kuelekea nyumbani kwa wazazi wangu huku nikimuacha yeye akiwa ndani ya gari lake akiwa ananisubiri.
nilipiga hatua zangu polepole kuelekea sehemu ilipokuwepo nyumba yetu ambapo mita chache kabla sijaufikia mlango wa nyumbani kwetu nilishtuka kuona unafunguliwa na ghaflaa!! kwa mshtuko na mshangao mkubwa nikamuona Grace pamoja na baba yake mzee Sebastian wakitoka ndani huku macho yetu yakigongana uso kwa uso kitu kilichofanya niishiwe nguvu na kubaki nikiwa nimesimama kwa kuduwaa huku macho yangu yakinitoka kama kuku mjane aliyetagia kwa jirani kwa sababu haikuitaji hata akili ya chekechea kujua kama Grace pamoja na baba yake mzee Sebastian wangethubutu kuniachia.

…..itaendelea….



Sent using Jamii Forums mobile app
 
NISAMEHE GRACE - 09



Ilipoishia…

Nilienda nyumbani kwa lengo la kuwaaga wazazi wangu pamoja na kuchukua zile pesa nilizokua nimezificha chini ya godoro chumbani kwangu ambapo mita chache kabla sijaufikia mlango wa nyumbani kwetu nilikutana uso kwa uso na Grace pamoja na baba yake mzee Sebastian kitu kilichofanya niishiwe nguvu na kubaki nikiwa nimesimama huku nimeduwaa…..

Songa nayo….

Kitendo cha kukutana uso kwa uso na Grace pamoja na baba yake mzee Sebastian kilinishtua sana kwani sikutegemea kama kweli Grace angekua amerudi nchini Tanzania kwa sababu mara ya mwisho nilimtoroka na kumuacha kule nchini China kiukweli niliishiwa nguvu sio kwa sababu nilikua nikimuogopa baba yake aliyeahidi kunifungulia mashtaka ya kipuuzi hapana bali niliishiwa nguvu kwa sababu kitendo cha kukutana na Grace ana kwa ana kiliashiria wazi kua ni lazima safari yangu ya kwenda Oman ingeharibika pengine ingetoweka kabisa ama ingekua kwa kuchelewa kitu ambacho kingefanya nichelewe kwenda kumtafuta Nairath wangu ambaye alikua kwenye siku zake za mwisho za kujifungua ambaye mara kwa mara nilikua nikimuombea kwa Mungu asijifungue mtoto wa kike na kumpatia jina la Grace kama alivyoniahidi kwenye ile barua yake.

Kitendo cha kukutana uso kwa uso na Grace pamoja na baba yake kilifanya ukimya mkubwa utawale katika lile eneo la nje ya nyumba yetu kwa sababu kwa muda wa dakika kadhaa hakuna aliekua amemsemesha mwenzake si Grace, si baba yake wala si mimi wote tuliishia kuangaliana tu huku macho yangu yaliyoonekana kujaa hasira yakitua juu ya uso wa mzee Sebastian aliyeonekana kuimung’unya midomo yake kwa sababu ya chuki nyingi alizokua nazo juu yangu.
ule ukimya uliotawala ghafla ulifanya nimuangalie mzee Sebastian kwa dakika kadhaa ambapo mara baada ya kumuangalia macho yangu yalitua tena juu ya uso wa binti yake Grace ambaye muda wote huo alikua akilia kwa huzuni kubwa sana huku mwili wake ukionekana kupungua kidogo tofauti na nilivyomuacha kule nchini China.

“Oohhh!!, Javier wangu kwanini umenifanyia hivi? kwanini ulinitoroka, hata kama haunipendi mimi umeshindwa hata kukijali na kukithamini kiumbe chako kilichopo ndani ya tumbo langu kweli Javier,lakini kwanini unataka uniue jamani ama kukupenda imekua kosa”
Grace aliniambia huku akinisogelea na kunikumbatia mara baada ya mimi kumuangalia kwa dakika kadhaa bila kumsemesha neno lolote.

Kiukweli yale maneno ya Grace yalinichoma sana kiasi cha kufanya nishindwe kuyazuia macho yasitoe machozi nilijikuta nikimkumbatia Grace kwa huzuni nyingi huku nikipiga magoti na kulishika lile tumbo lake lilionekana kua kubwa sababu ya ule ujauzito aliokua nao ambapo baada ya kulishika niliegemeza kichwa changu kisha nikalibusu na kupaza sauti kwa kelele kubwa sana ambayo iliwafanya wazazi wangu watoke nje pamoja na yule rafiki yangu Khamis aliyekua akinisubiri ndani ya gari lake aje mpaka pale nilipokua nimepiga magoti mbele ya Grace.

“Nisamehe mwanangu, najua nimekukosea, nisamehe sana” nilizidi kuongea kwa sauti huku nikiwa nimekiinamisha kichwa change mbele ya tumbo lake kana kwamba yule mtoto aliyekua tumboni mwake alikua ananisikia.

Kitendo changu cha kulia kama mtoto na kupiga magoti mbele ya Grace kilionekana kumgusa kila mtu kiasi cha kufanya wazazi wangu pamoja na yule rafiki yangu Khamis waanze kulia na kufanya ule ukimya wote uliokua umetawala pale nje uonekane kupotea kabisa.

“Mimi nimekusamehe Javier kwa niaba ya mtoto wetu, please usilie tena utazidi kuniumiza inuka twende ndani basi yamekwisha”
Grace aliniambia huku akiniinua ambapo baada ya kuniinua aliinyonya midomo yangu halafu akanikumbatia na tukaelekea ndani ya nyumba yetu kitendo ambacho kilionekana kumfurahisha sana mzee Sebastian pamoja na wazazi wangu wakati yule rafiki yangu kipenzi bwana Khamis akibaki amesimama huku akionekana kupigwa na bumbuwazi kwa sababu bila shaka alidhania kua nimeshayabadili maamuzi yangu ambayo yalifanya juhudi zake zote za kunisaidia zionekane kua bure.

Baada ya mimi na Grace kuingia mle ndani tuliendelea kubusiana huku ile huzuni niliyokua nayo ikifanya nikose hata nguvu za kumzuia Grace kufanya kile kitendo cha kunipiga mabusu mfululizo pasipo hata kuniachia nafasi ya mimi kumeza mate kitu ambacho kilionekana kumfurahisha sana kwasababu bila shaka aliamini kua mapenzi yetu ya kule nchini China yalikua yamejirudia tena hapa nchini Tanzania basi tuliendelea kubusiana na Grace kwa muda wa dakika kadhaa mpaka pale ambapo mlango wa kuingilia sebuleni uliposikika ukifunguliwa ndipo tulipoacha kubusiana na kuwaona waliokua wameufungua mlango ule ambao si wengine bali walikua ni wazazi wangu, mzee Sebastian pamoja na yule rafiki yangu Khamis ndio waliokua wameufungua mlango ule na kuingia ndani na kutukuta mimi pamoja na Grace tukiwa tumekaa juu ya sofa moja huku Grace akiwa amekilaza kichwa chake kifuani kwangu kitendo kilichoonekana kuzidi kuwafurahisha sana wazazi wangu kiasi cha kufanya ile furaha iliyokua imepotea hapo awali ionekane kurudi tena kwani tabasamu zilizokua zikionekana juu ya nyuso zao zilionekana kueleza kila kitu wazi.

Mara baada ya wao kuingia maongezi mazito yalianza ambapo wazazi wangu walinishauri kua niachane na Nairath ambaye walidai kua habari zake za sasa hazijulikana kwani pengine huenda atakua ameolewa ama amekufa na nianze kuijenga familia yangu pamoja na maisha yangu upya pamoja na Grace kitu ambacho kilionekana kumfurahisha sana Grace pamoja na baba yake huku zile habari za kutokuwepo kwa Nairath zikionekana kuzidi kumfurahisha sana Grace kiasi cha kufanya aanze kuniangalia kwa macho malegevu ya kudeka na kuanza kuzichezea sharubu zangu nilizotoka kuzi shave wiki moja iliyopita.
kiukweli maneno ya wazazi wangu yalionekana kuniingia sana huku zile pongezi za kutoka kwa rafiki yangu Khamis ambaye muda wote ule alionekana kushangaa zikifanya nishindwe kuyakataa maneno ya wazazi wangu kwa kuogopa kuirudisha upya ile huzuni kubwa iliyokua imepotea kwani nilijikuta sina jinsi zaidi ya kukubali kuishi na Grace kama mume na mke ambapo mara baada ya kukubali baba yake kipenzi mzee Sebastian aliahidi kutununulia nyumba mpya pamoja na gari mbili za kutembelea huku ile furaha kubwa aliyokua nayo ikimfanya asahau hata kuuliza juu ya zile pesa alizonipatia Grace kule nchini China ambazo muda wote huo nilikua nimezificha chini ya godoro la kitanda changu chumbani mwangu.
“Wazazi wangu, nimekubali kuishi na Grace kuanzia sasa lakini bila ndoa kwa sababu ningependa mpaka ajifungue kwanza ndipo tuweze kuona tunafanyaje juu ya masuala ya ndoa”
niliwaambia huku nikiukwepa kabisa ule mpango wa wao pamoja na mzee Sebastian kutaka mimi nifunge ndoa na Grace kwa sababu moyo wangu ulijua wazi kua sikua nikimpenda Grace kiasi cha kufanya nikwepe uo ushauri wao wa kutaka mimi nifunge nae ndoa kwa sababu nilijua wazi kama nikifanya hivyo ni lazima nitajifungwa kwa jinsi kanuni na taratibu za dini yangu zilivyokua zinasema.

Nilikubali kuishi na Grace ambaye muda mfupi toka niukubali mpango huo wa kuishi nae wazazi wake mama yake pamoja na baba yake mzee Sebastian walitununulia nyumba ya kifahari maeneo ya mbezi beach pamoja na magari mawili ya kifahari ya kutembelea aina ya BMW kitu kilichoonekana kuongeza furaha kubwa sana katika ule mpango wangu wa kuishi na Grace kiasi cha kufanya nionekane kumsahau kabisa Nairath ambaye bila shaka mpaka muda huo wa miezi mitatu niliyokua nimeanza kuishi na Grace upya kama mke na mume hapa nchini Tanzania alikua amekwisha jifungua.

Niliishi na Grace binti Sebastian kwa muda wa karibu miezi 6 na kidogo huku furaha yetu ikionekana kuwa kubwa kupita kiasi kitu kilichofanya tuyasahau matatizo yote yaliyokua yametokea kwani hata habari za Nairath zilionekana kupotea polepole kichwani kwangu hata yale mawazo ya kwenda kumtafuta tena kule visiwani Oman yalionekana kunitoka kabisa kiasi cha kufanya nizidi kuwa bize kumhudumia Grace na ule ujauzito wake ambao dalili zake za kujifungua zilianza kuonekana wazi.
“Ninakupenda sana mume wangu Javier tena ninapenda nikijifungua wewe ndio uwe wa kwanza kumshika mtoto wetu na umchagulie jina zuri sana”
Yalikua ni maneno ya Grace ambayo alipenda kuniambia mara kwa mara kila tulipokua tumepumzika huku akiichukua mikono yangu na kuiweka juu ya tumbo lake aliloonekana kulijali sana na kuniambia mara kwa mara nisikie jinsi mtoto alivyokua akicheza tumboni mwake kitu kilichomfanya aniambie kua ni lazima mtoto wetu angekua wa kiume kwa sababu ya utundu wa kuruka ruka vijisarakasi vya kichanga ndani ya tumbo lake.

Mahusiano hayo kati yangu na Grace yaliyofanya nimsahau kabisa Nairath yalidumu kwa muda wa miezi 6 na kidogo mpaka siku moja wakati nilipokua nikiendesha moja ya lile gari aina ya BMW alilotununulia mzee Sebastian, nakumbuka nilikua nikiendesha lile gari kuelekea kwa rafiki yangu kipenzi bwana Khamis ambaye majira ya saa 3 siku hiyo tulikua tumepanga kwenda kuangalia mpira pale Maryland hotel kama ilivyokua kawaida yetu kwa sababu ya uwingi wa mashabiki ambao huongeza sana radha ya kuangalia mpira.
Ilikua ni majira ya saa 1 na nusu jioni wakati nilipotoka nyumbani kwangu nmbezi beach na kumuacha Grace ambaye aliniruhusu niondoke kwa shingo upande akiwa amepumzika.
nilikua nikienda nyumbani kwa yule rafiki yangu Khamis ambapo bila kukusudia wala kua kuwaza lolote nilipita ile njia ya nyumbani kwa mamdogo yake na Nairath ambapo mara baada ya kufika usawa wa ile nyumba yake nilishangaa sana kuliona lile geti kubwa likiwa wazi bila ya kufuli lolote kuonekana kuning’inia juu yake huku kitendo cha mwanga wa kuonekana kumulika ndani ya ile nyumba kikifanya nishindwe kujizuia kulisimamisha lile gari langu kwa sababu kitendo cha nyumba hiyo kuonekana kua na watu ndani yake kilinikumbusha matukio yangu yote na Nairath ambaye nilikua nimeshazisahau habari zake.

Nilishuka ndani ya lile gari langu na kulisogelea lile geti lililoonekana kua wazi ambapo baada ya kulifikia nilibisha hodi kisha ndani ya dakika 1 na nusu hivi binti mdogo mwenye asili ya kichotara alikuja pale getini ambapo alinisalimia na kuniuliza shida yangu.

“Nina shida na Nairath kama yupo tafadhali ninaomba uniruhusu nionane naye” nilimwambia yule binti ambaye baada ya kumwambia alinijibu kua Nairath hayupo bali mamdogo wake ndiye yupo ndani.

“Ok naomba nimuone” nilimwambia yule binti ambaye aliniruhusu kuingia ndani ambapo nilikwenda nae mpaka sebuleni kwao na kumkuta yule mamdogo na Nairath ambaye alionekana kustuka sana mara baada ya kuniona.

“ooh Javier ni wewe karibu sana” aliniambia.

“asante mama lakini nimekua nikipita hapa muda mrefu kumtafuta Nairath lakini kwa bahati mbaya sikua nikikuta mtu” nilimwambia.
“Ni kweli, kwanza pole kwa matatizo,Nairath alirudi nyumbani kule Omanmaara baada ya kukusubiri kwa muda mrefu bila mafanikio wala dalili za wewe kurudi na nimetoka huko Oman wik moja iliyopita.”

“hata mimi nilihisi hivyo mara baada ya kuja hapa mara kadhaa na kukukosa, lakini vipi hali yake” nilimuuliza.

“hali yake si shwari Nairath anaumwa sana na muda mwingi amekua akishinda sana hospitali”

“anasumbuliwa na nini? Na vipi ule ujauzito alifanikiwa kujifungua salama”

“Mh ugonjwa wake bado sijaujua lakini ingekua vizuri kama ungeenda kuonana nae kwa sababu sidhani kama atarudi tena huku nchini Tanzania kwa sababu ya afya yake na kuhusu kujifungua alifanikiwa kwani alijifungua salama tena amebahatika kujifungua watoto mapacha wa kiume mmoja na wa kike wawili”

“na vipi kuhusu majina yao? Nilimuuliza mara tu baada ya kuniambia

“Yule wa kiume nadhani anaitwa Javier Hernandez nadhani ni kwa sababu ya mapendo ya Nairath juu yako ndio maana alimuita vile pia yule wa kike ambaye ndiye wa pili kuzaliwa bila shaka kama sikosei anaitwa G….r…a….c…..

“What? anaitwa Grace?” nilimuuliza mamdogo yake na Nairath huku hata kabla hajamaliza kuniambia lile jina lake.

……. Itaendelea……



ABCDEFGHIJKLMNOPQRSTUVWXYZ
 
NISAMEHE GRACE - 10



Ilipoishia….

Niliingia mpaka sebuleni na kukutana na mamdogo wake na Nairath ambaye mara baada ya kusalimiana alianza kuniambia habari za Nairath mwanamke niliyekua nikimpenda sana huku kile kitendo cha huyo mamdogo wake kuniambia kua mmoja kati ya watoto wangu amepewa jina la Grace kikionekana kunistua sana…

Songa nayo….

“What anaitwa Grace!!, sasa mama utaachaje Nairath amuite mtoto wangu Grace na wakati wewe mwenyewe unajua wazi kua Grace ndiye mwanamke aliyetusababishia matatizo yote hayo mpaka kusababisha mimi na Nairath kufikia hatua hii ya kutengana” nilimuambia yule mamdogo yake na Nairath ambaye alionekana kushtushwa sana na kitendo changu cha kulikataa lile jina la Grace.

“Javier mwanangu huu si muda wa kulaumiana kabisa, Nairath ndiye mama wa hao watoto unadhani ningeweza kupinga maamuzi yake” aliniambia.

“Ok sawa, na vipi kuhusu huyo mtoto mwingine wa tatu amempa jina gani?” nilimuuliza huku nikionekana kuyakubali majibu yake kwa shingo upande.

“Mmmh, Javier pole sana mwanangu, Nairath alijifungua watoto mapacha watatu, mmoja wa kiume na wawili wa kike,lakini kwa bahati mbaya kile kichanga cha mwisho kilifariki muda mfupi mara baada ya kuzaliwa”
mamdogo yake na Nairath alinambia huku akizishusha pumzi zake na kuanza kulia.

Kiukweli nilijikuta nikishindwa kuyazuia machozi yasinitoke mara baada ya kuisikia ile kauli yake huku kitendo cha mtoto wangu wa mwisho kufariki bila kuiona sura ya mimi baba yake kikionekana kuniumiza sana kiasi cha kufanya nianze kulia na kushindwa kunjibu neno lolote huyo mamdogo wake na Nairath.

“Pole sana Javier yote hii ni mitihani ya maisha tu, hebu nyamaza maana kulia sasa hivi haisaidii kwani unachotakiwa kufanya ni kwenda huko huko Oman kumuangalia Nairath kwasababu afya yake si nzuri na usipoangalia hata hao watoto wenu wawili waliobaki unaweza ukawapoteza”
alizidi kuniambia huku akininyamazisha mara baada ya kuona nimeanza kulia bila ya kumsemesha neno lolote.

“Mama nimemkosea sana Nairath sidhani kama siku nikionana nae atakubali kunisamehe kweli maana najua kua nimemuumiza sana ingawa sikukusudia kufanya hivyo” nilimwambia huku nikiendelea kwa sababu ya kushindwa kunyamaza.

“Javier,Nairath bado anakupenda sana ni lazima atakusamehe kwa sababu kila siku alikua akiniambia juu yahabari zako pamoja na mipango yenu mingi mliyojiwekea hapo awali kabla ya haya matatizo yote kutokea kitu ambacho kinaeleza wazi ni jinsi gani anavyokupenda bado na kwasasa hivi hautakiwi kufikiria kitu kingine zaidi ya hawa watoto wenu wawili waliobaki” aliniambia.

Ambapo mara baada ya kuniambia mambo yote hayo akili yangu ilikata rufaa na kuamua kua ni lazima niende mpaka Oman kumtafuta Nairath ambaye kutokana na maelezo ya huyo mamdogo wake alionekana kuumwa sana kiasi cha hospitali kugeuka kua makazi yake ya kudumu.

‘Ni lazima niende Oman kama Nairath akikataa na kushindwa kunisamehe basi nitaishia kuwaona watoto wangu hakika hii itakua ni zawadi kubwa na muhimu sana kwangu kuliko kukaa hapa na kuishia kufaidi anasa tena na mwanamke nisiyempenda’
Nilijisemea kimoyomoyo huku nikichukua anuani,namba za simu pamoja na location ya sehemu alipokua akiishi Nairath pamoja na wazazi wake karibu kabisa na ile hospitali ya Good healthy alipokua amelazwa Nairath ambapo mara baada ya kuchukua vile vitu na vielelezo vyote vya muhimu vitakavyofanikisha mimi kumpata Nairath nilimuaga yule mamdogo wake na kuondoka moja kwa moja mpaka nyumbani kwangu huku zile habari mbaya nilizozisikia kkutoka kwake pamoja na ile huzuni kubwa niliyokua nayo vikifanya mood yangu yote ya kwenda kuangalia mpira iishe kiasi cha kufanya nishindwe kwenda tena kwa yule rafiki yangu kipenzi bwana Khamis.

Niliondoka na kwenda moja kwa moja mpaka nyumbani kwangu maeneo ya mbezi beach ambapo mara baada ya kufika nilimkuta Grace akiwa amejilaza kwenye kiti huku akionekana kunisubiria kwa hamu kubwa sana kwani mara tu baada ya kuingia ndani alinisogelea na kunikumbatia kitu kilichofanya hasira yangu niliyokua nayo ionekane kuongezeka mara mbili zaidi.

‘Baby karibu nilikua nakusubiri kwa hamu kubwa sana halafu vipi mbona unaonekana kama umekasirika nini taizo’ Grace aliniambia mara tu baada ya mimi kuingia ndani huku akinikumbatia na kuiona wazi ile hasira kubwa iliyokua imeuvaa mwili wangu.

‘Tumefungwa’ nilimjibu huku nikimdanganya wazi kwa sababu ya kumficha ule ukweli.

‘Sasa baby kufungwa tu ndio una nuna kiasi hicho kama umetoka kung’oa jino’ aliniambia

‘Sasa ulitaka nifurahi wakati tumefungwa’ nilimjibu kwa hasira kwa sababu nilijikuta nimeanza kumchukia ghafla huku kile kitendo cha Nairath kumuita mtoto wangu wa kike jina la Grace kikionekana kuizidisha hasira yangu zaidi kiasi cha kufanya nianze kumchukia Grace upya bila kujali ule ujauzito aliokua nao ambao muda wowote kuanzia wakati ule angeenda kujifungua kutokana na dalili alizokua akizionyesha mara kwa mara.

‘Pole jamani nisamehe kama nimekuudhi naomba usikasirike sababu utanifanya nilie’ Grace aliniambia kwa sauti laini ya kubembeleza.

Ambapo licha ya kuniomba samahani kwa kuniambia maneno hayo yenye sauti ya utulivu sikumjibu neno lolote zaidi ya kuishia kumwangalia na kisha nikainuka na kwenda mpaka chumbani kwetu ambapo mara baada ya kufika nilijitupa kitandani na kumuacha Grace akiwa amekaa sebuleni huku akionekana kukosa raha kabisa kwa sababu ya ile hali yangu ya hasira niliyokua nayo.

Nilienda mpaka chumbani na kujitupa kitandani bila kuelewa muda nilioshikwa na usingizi kwani nilikuja kuamka na kukuta kumekwisha pambazuka.
ilikua ni saa tatu kasorobo asubuhi kwa mujibu wa ile saa kubwa ya ukutani iliyokua imetundikwa pembezoni karibu kabisa na kile kitanda chetu ambapo mara baada ya kuamka niliangaza kitandani pasipo ya kumuona Grace kitendo kilichofanya niamini kua ni alikua ameamua kulala palepale sebuleni kutokana na mimi kumgombeza jana usiku, niliinikuka pale kitandani na kuchukua mswaki pamoja na taulo kisha nikaingia bafuni kuoga na kuweka mwili safi ambapo hata kabla sijamaliza kuoga mlango wa bafuni ulifunguliwa alikua ni Grace ambaye aliingia na kuanza kuniogesha kama mtoto mdogo yote alifanya kwa sababu ya mapendo yake ya dhati aliyokua juu yangu.
‘Baby Jamani timu yako kufungwa jana tu ndo unalala kama punda hebu ngoja nikuogeshe mume wangu halafu tukanywe chai ipo tayari mezani nimekwisha iandaa’
Grace aliniambia kwa sauti nzuri sana ya kudeka iliyoambatana na wema wake mwingi aliokua akiufanya kwangu kiasi cha kufanya nishindwe kabisa kumzuia kufanya kile kitendo cha kuniogesha.
kitendo kile alichokifanya Grace kilinifanya nimuhurumie kiasi cha kuanza kumuonea huruma kwa sababu nilijua wazi ni lazima ataumia sana kwani muda huu nilikua nimeshaamua kwenda Oman.
nilijikuta nikimuangalia sana Grace huku nikilitazama lile tumbo lake lililokua limeuifadhi ule ujauzito wangu kwa huzuni sana kwa sababu nilijua wazi kua ni lazima nitaondoka muda mfupi ujao huku
kile kitendo cha Grace kuniogesha kwa upendo mkubwa tena wa dhati bila kujali hali yake ya ujauzito pamoja na kuniandalia chai licha ya kwamba nilimfokea usiku wa jana kilifanya akili yangu pamoja na moyo wangu vionekane kubishana kwani akili yangu ilionekana kuniambia wazi
‘wewe kwanini unataka kumuacha Grace wakati anakupenda sana usiwe mjinga usimuache usijaribu’ huku moyo wangu nao ukionekana kuipinga ile akili yangu kwakua ulikua mzito sana kuzipokea hisia za Grace kiasi cha kuthibitisha wazi kabisa kua Nairath ndio alikua upendo wake wa kwanza.
niliendelea kukaa na Grace pale nyumbani kwetu mbezi beach ambapo licha ya upendo wake mkubwa aliokua akiuonyesha kwangu bado mawazo yangu hayakuonekana kubadilika kwani licha ya siku zake za kujifungua kukaribia mimi sikuonekana kujali lolote sio kwa sababu sikua nikimpenda bali sikujali kwa sababu mawazo yangu yote yalikua yameamia juu ya ile safari yangu ya kwenda Oman.

Ilikua ni siku ya Jumatano majira ya saa 10 jioni wakati nilipoenda mpaka mahali zilipokuwepo ofisi za shirika la ndege la Fast jet ambapo nilienda kukata tiketi yangu ya ndege kwa siri kubwa sana pasipo kumshirikisha mtu yoyote kwani hata yule rafiki yangu kipenzi bwana Khamis sikumjuza.
Nilikata tiketi ya kuondoka siku ya Jumamosi ambapo kwa mujibu wa tiketi hiyo safari ilikua ikianza majira ya saa 7 kamili usiku kitendo kilichoonekana kuniumiza sana kichwa kwa sababu ya kuwaza ni jinsi gani nitaweza kumtoroka tena Grace kwa mara ya pili mara baada ya kumtoroka mara ya kwanza kule nchini China muda mrefu uliopita.
mara baada ya kukata ile tiketi ya ndege nilienda moja kwa moja mpaka nyumbani kwa wazazi wangu ambapo nilijidai kana kwamba nilikua nimeenda kuwasalimia kumbe maskini ya Mungu ndiyo nilikua nikiwaaga pasipo ya wao kujua kiasi cha kufanya maongezi yetu yawe marefu mpaka kufika majira ya saa tatu karibu na nusu za usiku wakati nilipowapa kwa heri yangu ya mwisho pasipo ya wao kujua na kuanza kurudi nyumbani huku nikiumia sana kwa sababu ya kujua wazi kua sitoonana nao tena.
na baada ya kutoka kwa wazazi wangu nilirudi mpaka nyumbani kwangu na kumkuta Grace akiwa ananisubiri kwa ule upendo wake mwingi kama ilivyokua kawaida yake ya siku zote ambapo baada ya kunipokea tulienda mpaka mezani na kula chakula cha usiku huku yeye akionekana kula kidogo sana kwa sababu ya kujisikia kichefuchefu kitendo kilichomfanya aache kula na kuanza kunilisha kama mtoto kile chakula alichokipia mwenyewe.

Ilikua ni jumamosi majira ya asubuhi wakati ambapo Grace alikua ameenda katika kituo cha afya kwa ajili ya kupima maendeleo ya afya yake pamoja na ule ujauzito wake kitendo kilichoonekana kunipa nafasi ya mimi kuipanga upya ile mizigo yangu niliyoipanga mara ya mwisho kule nyumbani kwa wazazi wangu siku chache zilizopita ambapo mara baada ya kuipanga nilichukua karatasi pamoja na biki kisha nikaanza kuandika barua niliyopanga kumuachia Grace pindi nitakapokua nikimtoroka

“NISAMEHE GRACE, ninajua ni jinsi gani ulivyolia na kutoa machozi mengi kwa ajili yangu nakushukuru sana kwa kunipenda na kuonyesha kunijali na kunihitaji sana kuliko mwanamke yoyote yule najua utaumia sana pindi mwanaume atakiwaye kukupa faraja wakati wa uchungu wako atakapokua ameondoka.
Grace nimeamua kufanya hivi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu kamwe sitokuchukia kwa sababu eti sikupendi hapana bali nitakuchukia kwa sababu upendo wako kwangu uliyaharibu maisha yangu pamoja na malengo yangu mengi niliyokua nimejiwekea pamoja na Nairath.
Grace japo wewe na baba yako mmeniumiza sana lakini nakushukuru kwa sababu umefanya nijifunze mambo mengi sana kuhusu mapenzi pamoja na athari zake katika maisha yangu ya kila siku, Grace umefanya niamini kua kweli mapenzi yanaua pindi ulipokua ukipumua kwa kutumia mpira ya Oksijeni, pia umenifanya nijue kua mapenzi yanaweza kuharibu future ya mtu kwa sababu ya kufanya mimi, wewe pamoja na Nairath tushindwe kumaliza masomo yetu ya udaktari na kutofikia malengo yetu ambapo pengine tungeweza kuwasidia wagonjwa kadha wa kadha.

Grace pindi utakapokua ukiisoma barua hii nadhani bila shaka nitakua ndani ya ndege nikichepuka zangu na kwenda Oman kumtafuta Nairath mwanamke wa ndoto zangu ambaye amekutangulia wewe kunizawadia zawadi nzuri sana ya watoto wawili , Grace sitaki kuandika hivi kwa lengo la kukukozogoa hapana bali ninaandika hivi ili upate kujifunza kua ni vizuri sana kuheshimu hisia za mtu na kua muelewa pindi anapokwambia kua akupendi kwa sababu kama ungenielewa toka mwanzo pale chuoni St.Anna nasi haya matatizo yote yasingetokea kwani pengine ungekua umeshanisahau na ungekua umepata mwanaume mwingine ambaye bila shaka angekupenda sana kuliko mimi niliyekuumiza sana na kuyafanya maisha yako yawe mashakani.
Mwisho Grace nashukuru kwa kuitunza mimba yangu ingawa sikukusudia kukupatia sikuhukumu kwa hilo bali ninakuomba umtunze sana mtoto wetu na siku Mungu akipenda tutakuja kuonana tena.
NISAMEHE GRACE, NISAMEHE GRACE, NISAMEHE SANA GRACE.
Ni mimi baba kijacho
Javier Hernandez.

Ilikua barua ndefu sana yenye kuhuzunisha ambayo hadi nimalize kuiandika ilikua imeshalowana kwa sababu ya uwingi wa jasho na machozi yaliyokua yakinitoka.
baada kumaliza kuiandika ile barua niliiweka ndani ya bahasha na nikaitunza mfukoni kwangu kisha nikajidai ni kama sijui lolote linaloendelea mpaka ule muda ambao Grace alitoka hospitali na kunikuta nikiwa nyumbani ambapo muda mwingi alionekana kulala kwa sababu ya uchovu.

Ilikua imefika saa 4 karibu na nusu usiku wakati mimi na Grace tulipokua tumelala huku mimi nikionekana kukosa usingizi kabisa kwa sababu ya kuwaza jinsi gani nitakavyomtoroka Grace ambapo gaflaa!! Nikiwa katika kuwaza nilishtushwa sana na sauti ya kelele za uchungu kutoka kwa Grace.

‘Javier mtoto anakuja, anakuja mama weweee nipeleke hospitali’ Grace alikua analia kwa kelele za uchungu huku akigalagala pale kitandani wakati matone madogo ya damu yalioonekana kuanza kuchulizika miguuni.
Kitendo cha Grace kulia kwa kuugulia maumivu ya uchungu kilifanya nisahau habari za safari yangu iliyokua inaanza ndani ya masaa matatu yajayo na kuamua kumkimbiza harakaharaka hospitali.



….itaendelea….

ABCDEFGHIJKLMNOPQRSTUVWXYZ
 
NISAMEHE GRACE - 11



Ilipoishia…

Yakiwa yamebaki masaa matatu kabla ya ile safari yangu ya kwenda Oman kuanza Grace alishikwa na uchungu kitendo kilichofanya nimkimbize haraka hospitali na kusahau habari za ile safari yangu kwa muda.

Songa nayo….

Kitendo cha Grace kushikwa na uchungu kilifanya nisahau kuhusu ile safari yangu ya kwenda Oman kwa muda kwa sababu mara tu baada ya yeye kushikwa na uchungu nilimnyanyua haraka kutoka pale kitandani na kumpeleka mpaka ndani ya gari halafu nikachukua pesa kiasi kisha nikafunga milango yote ya nyumbani na kuanza safari ya kumpeleka hospital ambayo ilionekana kuwa ya mateso makubwa sana kwa Grace kwa sababu muda wote wa safari hiyo alionekana kulia sana kwa sababu ya maumivu ya ule uchungu uliokua umemshika kitu kilichofanya nimuonee sana huruma huku kitendo changu cha kuigeuza shingo nyuma mara kwa mara na kuyatua macho yangu katika siti ya nyuma sehemu alipokua amelala kikifanya nizidi kuumia sana kwa sababu ya ule muonekano wake wa kuchoka na kukata tamaa ambao kukweli ulinihuzunisha sana.

‘Javier, fanya haraka mume wangu uwwwhhh!! mama yangu wee nakufa’ yalikua ni maneno ya Grace yaliyoonekana kujaa kilio kingi cha maumivu huku yakitaka niwahi kumuwaisha hospitali.

Maneno yale ya Grace yalifanya nizidi kuumia na kumuhurumia sana kiasi cha kufanya nianze kuilaani ile foleni kubwa niliyokutana nayo pale barabarani ambayo ilisababisha jam kubwa sana na kutufanya tumalize nusu saa nzima pale barabarani pasipo hata ya gari letu kutembea umbali wa mita 10.
kitendo hicho cha kusimama barabarani hapo kwa muda wa nusu saa kilionekana kuyaongeza mateso ya Grace aliyekua karibu kujifungua kwa sababu muda wote huo tuliosimama hapo kilio chake kilionekana kuongezeka sana na kua kikubwa tofauti na hapo awali kitu kilichonitisha sana na kufanya nianze kuyaamini maneno yake kua ni kweli huenda angekufa muda mfupi ujao kama alivyo kua akisema yeye mwenyewe.

Tulikaa barabarani hapo kwa muda wa zaidi ya nusu saa na kidogo ndipo ukubwa wa foleni ile ulipoanza kupungua na kufanya ile jam nayo ionekane kupungua kitu kilichofanya nisitake kuchelewa tena kwani mara tu baada ya ile foleni na ile jam kupungua kulifanya hekaheka na purukushani za pale barabarani zionekane kupungua na kusababisha ukimya ambao ulinishawishi sana kuendesha gari langu kwa mwendo kasi usio wa kawaida ili niwahi kumfikisha Grace hospitali kwani nilijikuta nikibadilisha gia kutoka gia namba 3 nikapandisha mpaka gia namba 5 halafu mguu wangu wa kulia ukakanyaga mafuta mpaka mwisho huku mguu wangu wa kushoto ukisimama stendi bai juu ya breki kwa ajili ya kuukontroo ule mwendo kasi endapo kama kuna mtu au gari lolote lingejitokeza upande wangu kwa mbele na mara baada ya kupandisha gia na kukanyaga mafuta niliongeza mwanga wa taa za mbele kwa ajili ya kuniwezesha kuona vizuri kitu chochote kilichokua kikija kwa mbele yangu kiukweli ulikua ni mwendo mkali sana kiasi cha kuanza kuona kana kwamba zile taa za barabarani zilikua zikikimbia kwa kasi sana kurudi nyuma nakumbuka mshale wa speed miter ulikua ukicheza katikati ya namba 100 mpaka 120 kiasi cha kufanya ndani ya dakika 5 kusiwe na gari lolote lililokua likikatiza mbele yangu kwani nilikua nimempita karibu kila dereva aliyekuwepo pale barabarani.

Japo ule mwendo kasi ulionekana kuwa wa hatari sana kwa sababu ya kuwa nimebeba mwanamke mjamzito lakini ulinisaidia sana kiasi cha kufanya ndani ya dakika 25 niwe nimeshaingia katika maeneo ya hospitali ya taifa ya muhimbili ambapo mara tu baada ya kuingia sikutaka kuchelewa kwani nilimbeba Grace aliyeonekana kulegea na kuchoka sana kwa sababu ya yale maumivu ya ule uchungu na kuanza kumpeleka ndani hospilani huku nikiwa nimembeba juu juu na ghafla nikiwa katika kumpeleka niliwaona wauguzi wawili wakija na kitanda cha magurudumu mpaka katika ule upande niliokuwepo ambapo mara baada ya kunifikia tulimpakia Grace na tukaanza kusaidiana kukisukuma kile kitanda cha magurudumu mpaka sehemu zilipokuwepo wodi maalumu za wamama wajawazito ambazo kitaalamu zilikua zinaitwa ‘Graded wod ama high class wod’ ambazo zilitengenezwa maaulumu kwa ajili ya watu waliokua na kipato cha hali ya juu kwani zilizikua zikitofautiana sana na zile wodi za kawaida tulizozoea kuziona kwa sababu zile wodi zilikua zikilaza mgonjwa mmoja katika kila chumba kimoja na kumpatia matibabu yote tena kwa wakati huku zikionekana kutoa huduma safi kama mashirika ya ki private licha ya kwamba ilikua ni mali ya serikali.

Ilikua ni karibu saa 6 kasorobo usiku waktai tulipokua tukimuingiza Grace mle wodini na hivyo kufanya libaki saa moja tu kabla ya ile safari yangu ya Oman kuanza ambapo mara baada ya kumfikisha na kumuingiza Grace mpaka mule wodini wale wauguzi walinitaka niwapishe na nitoke na kwenda kusubiri nje ili wao wapate nafasi ya kuanza kumuhudumia Grace.
kitendo cha wale wauguzi kunitaka nikakae na kusubiri nje kilifanya nimuone na kumuaga Grace kwa mara ya mwisho kwa sababu nilijua wazi kua sitoonana nae tena kwa sababu licha ya hali yake kuwa mbaya lakini bado haikuweza kunishawishi nihairishe ile safari yangu ya kwenda sio kwa sababu sikua nikimthamini bali ni kwa sababu nilikua nimeshadhamiria kuondoka kweli kwani mpaka muda huo tiketi yangu ya ndege ilikua mfukoni.

Nilijikuta nikianza kumuangalia Grace kwa mara ya mwisho kwa sababu nilijua wazi kua sitoonana nae tena kwa sababu ya ile safari yangu ya kwenda Oman ambayo kiukweli nilijua kua ni lazima itauumiza sana hasa pindi atakapojifungua na kupata fahamu kwa sababu ya kunipenda kwake tena pindi atakapokua akimuona yule mtoto wetu ambaye atakua akihangauika kumlea peke yake ni kana kwamba hana baba.
kabla sijawapisha wale wauguzi kama walivyikua wakinitaka nifanye hivyo niliyasogeza macho yangu na kuyatua juu ya uso wa Grace ambao ulioonekana kuchafuka sana kwa sababu ya zile alama za kukauka kwa jasho pamoja na uwingi wa yale machozi yaliyokua yakimtoka kutokana na maumivu ya ule uchungu kisha niliyatazama yale macho yake aliyokua ameyafumba huku yakionekana kuangalia mbali kikweli nilijikuta nikishindwa kuyazuia machozi yasinitoke kwani kitendo cha yale macho ya Grace kuoneka kufumbwa kwa uwingi wa machozi ya maumivu kilionekana kuniumiza sana licha ya kwamba hakikuweza kuubadilisha ule uamuzi wangu wa kuondoka halafu tena nilijikuta nikiyatua macho yangu mpaka juu ya midomo iliyokua mikavu huku nayo ikioonekana kuchafuka kwa sababu ya kukauka kwa yale mabaki ya mate yaliyokua yakimtoka kiukweli nilizidi kuumia sana kwani ile taswira ya Grace iliyokua ikionekana wakati huo ilifanya nishindwe kumtofautisha Grace na marehemu mtarajiwa.
kisha mara baada ya hayo yote nilichukua kitambaa change nikaufuta ule uso wake pamoja na macho,pua na midomo yake kisha nikauinamisha uso wangu na kuisogeza midomo yangu mpaka juu ya ile midomo yake mikavu na kwa mara ya mwisho nikaionyonya midomo yake huku nikilitazama na kulishika lile tumbo lake lililoonekana kutenda wema mkubwa sana wa kuuifadhi na kuutunza ule ujauzito wangu niliompatia kule nchini China.

‘Kwaheri Grace, ninakushukuru sana kwa kunipenda nina ahidi knitakua nikikuombea kwa Mungu kila siku iendayo kwake ili akupe nguvu ya kunisahau mimi na kumlea mtoto wetu ipasavyo hakika nitajitahidi kukuombea kwake kila siku ili aweze kukupatia mwanaume mwingine utakayampenda tofauti na mimi niliyekuumiza sana kwa heri Mungu akipenda tutaonana tena tafadhali, NAOMBA UNISAMEHE GRACE’ nilijikuta nikijisemea kimoyo moyo ili kwa sababu ya kuogopa kusikiwa na wale wauguzi kambapo mara baada ya kujisemea hayo maneno kimoyomoyo nilimbusu Grace kwa mara ya mwisho tena huku nikiyatazama yale macho yake yaliyoonekana kuniangalia kwa mbali sana tena kwa shida nyingi kwa sababu ya kufumbwa na ule uwingi wa machozi.

Baada ya kumuaga Grace kwa mara ya mwisho kabisa nilitoka mle wodini na kwenda mpaka kwa daktari ambapo nililipa gharama zote za matibabu ya awali kisha nikapiga hatua zangu na kuelekea mpaka sehemu lilipokuwepo gari letu ambalo nililipaki wakati tukiingia hospitalini.
baada ya kulifikia lile gari letu niliingia ndani tena bila kuchelewa niliungurumisha injini na kwa kuanza kuendesha lile gari kwa uleule mwendo kasi niliojia hospitalini hapo ambapo niliendesha kuelekea nyumbani kwangu maeneo ya mbezi beach ambapo mara baada ya kufika niliwapigia simu wazazi wangu pamoja na wazazi wa Grace na kuwafahamisha kuhusu ile hali ya uchungu wa Grace pamoja na hospitali niliyompeleka mara baada ya kuwataarifu nilichukua ile barua niliyomuandikia Grace nikaiweka juu ya meza sebuleni halafu nikachukua kiasi cha pesa taslimu sh.ml 60 kutoka kwenye bagi lake kisha nikabeba mizigo yangu yote nakuipakia ndani ya lilelile gari aliloninunulia baba yale ambapo mara baada ya kuipakia nilifunga milango yote ya pale nyumbani kwetu na kuitupia funguo ndani kupitia uwazi uliokuwepo kwenye mlango mkubwa wa kutokea na kuingilia ndani ya nyumba yetu halafu kwa uchungu mwingi wa kumuacha Grace katika hali ile pamoja na kitendo cha kutokuja kumuona huyo mwanangu mtarajiwa nilianza safari yangu ya kuelekea airport huku zikiwa zimebaki takribani dakika 40 kabla ya ile ndege ya fast jet kuanza ile safari yake ya kwenda omani.


…itaendelea..


ABCDEFGHIJKLMNOPQRSTUVWXYZ
 
NISAMEHE GRACE - 12



Ilipoishia….

Nilianza safari yangu ya kuelekea airport huku zikiwa zimebaki takribani dakika 40 kabla ya ile ndege ya fast jet kuanza ile safari yake ya kuelekea Oman.

Songa nayo….

Ilikua ni saa 6 na dakika 20 usiku wakati nilipokua nikiianza ile safari yangu ya kuelekea airport huku zikiwa zimebaki takribani dakika 40 kabla ya ile ndege ya fast jet niliyotakiwa kusafiri nayo kuanza kupaa kitu kilichofanya niendeshe gari kwa mwendo kasi usiokua wa kawaida ili kuiwahi ndege hiyo ambayo ndani ya muda mfupi ujao ilikua inaanza ile safari yake ya kuruka kuelekea visiwani Oman.

Safari yangu hiyo ya kuelekea airport ilionekana kuwa ya mateso makubwa sana pengine kuliko hata ile safari ya Grace ya kuelekea hospitali kwani ule ukimya mwingi niliokutana nao barabarani ambao ulitokana na uchache wa foleni kwa sababu ya uwingi wa ule usiku ulionekana kuipa nafsi yangu ruhusa ya kunihukumu hasa kwa kile kitendo nilichokua nimekifanya muda mfupi uliopita cha kumtoroka Grace mwanamke aliyekua akinipenda sana tena katika siku yake ya kujifungua.
kadri dakika zilivyozidi kusonga mbele kuisogelea ile saa 7 ndivyo nafsi yangu nayo ilivyozidi kunihukumu kiasi cha kufanya nishindwe kuyazuia machozi yasinitoke kwani nilijikuta nikianza kujiona kana kwamba nilikua muuaji huku ile taswira ya Grace niliyemuacha hospitali ikionekana kujirudia rudia sana kichwani kwangu kiasi cha kufanya niendelee kuyaamini yale maneno yake kua huenda kweli angekufa ndani ya muda mfupi ujao kama alivyokua akisema hapo awali kitu kilichofanya nizidi kuumia sana.

Nilifanikiwa kufika salama mpaka airport ambapo zilikua zimebaki takribani kama dakika 15 kabla ya ile ndege ya fast jet kuanza kupaa na kuianza ile safari yake kitu kilichofanya nisitake kuchelewa kabisa kwani mara tu baada ya kufika pale airport nilishuka kutoka garini pamoja na ile mizigo yangu kisha nikalipiga lock lile gari na kulitelekeza sehemu ya parking halafu bila kuchelewa nikapiga hatua zangu kuelekea mpaka sehemu vilipokuwepo vyumba vya kukagulia mizigo ambapo mara baada ya kukaguliwa mizigo yangu pasipo ya kukutwa na tatizo lolote nilielekea moja kwa moja mpaka sehemu ilipokuwepo ndege ile ya fast jet ambapo mara baada ya kuifikia nilipanda na kuenda kukaa mpaka sehemu ilipokuwepo siti yangu husika.

Nilikua miongoni mwa abiria wa mwisho kabisa kuingia ndani ya ndege hiyo ambapo mara tu baada ya abiria wote kumalizika kuingia ndani ya ndege hiyo mlango ulifungwa kisha ghaflaa sauti laini ya kike yenye lafudhi ya kizungu ilianza kusikika kutoka kwenye spika nzuri za plastiki zilizokua zimefungwa kwenye usawa wa katikati ya kila siti upande wa juu ya paa la ndege hiyo ambayo ilionekana kupendeza sana kuanzia muonekano mpaka mpangilio wake ambao haukuonekana kutofautiana sana na ile ndege ya shirika la fly emerates niliyoipanda kule nchini China wakati nilipokua nikimtoroka Grace kwa mara ya kwanza.

‘Attention!! we are going to fly very soon, every one make sure you wear well the belt’
(angalizo tunakwenda kupaa muda si mrefu kila mtu ahakikishe amefunga vizuri mkanda)
sauti ile ilisikika kusema kisha ikajirudia mpaka mara mbili.

Ilikua ni sauti ya mhudumu wa kike wa ndege hiyo ambayo ilikua ikiwataka abiria wote kufunga mikanda kwa ajili ya kuepusha hekaheka na migongano wakati wa ndege hiyo kupaa.
sauti ile ilionekana kutiliwa sana mkazo kwani mara tu baada ya kuacha kusikika sauti nyingine ya vibanio vya kufungia mikanda ya ndege ilianza kusikika kwa mbali huku kila mtu akionekana kuinama na kufunga mkanda kwa ajili ya usalama wake binafsi kitu kilichofanya ndani ya dakika 5 mikanda yote ya ndani ya ndege hiyo ionekane kupita na kuning’inia juu ya bega la kila abiria.

Baada ya zoezi hilo kukamilika ile sauti laini kutoka kwa yule muhudumu wa kike ambaye hakua akionekana kwa wakati huo ilisikika tena kutoka kwenye zilezile spika za mwanzo.

‘Its our hopes that every one have already wear well the belt’
(ni matumaini yetu kila mtu amekwishafunga mkanda ipasavyo)
sauti ya yule mhudumu wa kike ilisikika tena huku ikizidi kuongea

‘We are going to fly now but for those who have health problems there are plastic pocket behind of each seat just take it,it is special for vomiting’
(tunakwenda kuruka sasa kwa wenye matatizo ya afya kuna mifuko ya plastic nyuma ya kila siti ichukueni ni kwa ajili ya kutapikia)
sauti ile ilizidi kusikika huku ikionekana kusababisha ukimya mkubwa sana ndani ya ndege hiyo.

‘And last we wish you all nice journey and enjoy our service’
(na mwisho tunawatakia wote safari njema na furahieni huduma zetu)
sauti ile ilimalizia kusema kisha ikatulia ambapo mara baada ya kutulia ule ukimya wote ulioonekana kutawala ndani ya ndege hiyo ulianza kupotea polepole kwa sababu ya zile sauti za kukoroma kutoka kwa baadhi ya abiria waliokua wameanza kusinzia.

Ilikua ni saa 7 na robo usiku wakati ambapo injini zote mbili za ndege hiyo zilipoonekana kuwashwa na kuanza kuunguruma huku sauti ya miungurumo hiyo mikubwa ikionekana kupenya na kuanza kusikika mpaka ndani ya ndege hiyo kiasi cha kuonekana kuziunga mkono zile sauti za kukoroma kutoka kwa baadhi ya wale abiria waliokua wamesinzia kiasi cha kufanya ukimya wote uliokua umetawala ndani ya ndege hiyo uonekane kupotea kabisa.

Injini za ndege hiyo zilionekana kuunguruma kwa karibu dakika 5 nzima kisha nayo magurudumu ya ndege hiyo yakaanza kukimbia kwa mwendo mkali sana kiasi cha kufanya sauti nyembamba zionekane kusikika kutoka chini ya ndege hiyo karibu kabisa na yale magurudumu yake kuashiria kua yalikua yameanza kuiacha ardhi ya Tanzania kwa sababu mara baada tu ya sauti hizo kusikika ile ndege iliinuka upande wa mbele na kuanza kupaa.

‘Kwaheri Grace ninaomba unisamehe sana, kwaheri st.Anna,kwaheri Tanzania,kwaheri wazazi wangu hakika kamwe sitowasahau’
nilijikuta nikijisemea kimoyomoyo tena kwa huzuni nyingi kana kwamba wote walikua wakinisikia huku nikitazama nje kupitia yale madirisha ya ndege hiyo na kuona jinsi ambavyo ndege hiyo ilikua ikiiacha ardhi ya Tanzania ambayo kiukweli sikua nimepanga kuja kuikanyaga tena ardhi hiyo pindi nitakapofika Oman na kumpata Nairath mwanamke aliyekua ameuteka sana moyo wangu kupindukia pengine kuliko kitu chochote.
kadri ndege hiyo ilivyozidi kuchepuka na kulifaidi anga la nchi ya Tanzania ndivyo muda nao ulivyoonekana kutokua nyuma katika kuisogelea afrajili ya usiku huo kwani mpaka kufikia muda huo idadi ya abiria waliokua wamesinzia ilionekana kuongezeka na kuwa kubwa zaidi kuliko hapo awali kwa sababu ilikua inaelekea saa 8 za usiku kitu kilichofanya sauti na ngurumo za injini za ndege hiyo zionekane kupungua kwa sababu ya kumezwa na mawingu mazito mara baada ya hiyo ndege kuwa imeruka juu zaidi na kuonekana kuchepuka ndani zaidi ya mawingu la anga la nchi ya Tanzania.

Lakini licha ya abiria wengi kuonekana kusinzia kwangu mambo yalionekana kua tofauti kabisa kwani licha ya kuwa ilikua imefika saa nane za usiku lakini kwangu bado usingizi ulionekana kuwa mgumu sana kunibana kwa sababu ya ule ukimya mkubwa uliokua umetawala tena ndani ya ndege hiyo kuonekana kuiruhusu tena nafsi yangu izidi kunihukumu na kufanya niukose ule usingizi kiasi cha kufanya nigubikwe na mawazo mazito pamoja na majuto mengi juu ya kile kitendo cha kumtoroka Grace nilichokua nimekifanya.

Endelea.


NISAMEHE GRACE - 13

Ilipoishia…

Safari yetu ya kuelekea Oman ilianza huku ukimya mkubwa ukionekana kutawala ndani ya ndege kitu kulichoonekana kuipa nafsi yangu nafasi ya kunihukumu na kusababisha nikose usingizi kabisa kwa sababu ya kuyajutuia yale yote niliyoyatenda kwa Grace.

Songa nayo…

Ilikua ni majira ya saa 8 usiku wakati ambapo ile ndege mali ya shirika la fast jet ilipoonekana kuzidi kuchepuka katikati ya mawingu mazito ya anga la Tanzania huku ule ukimya mkubwa uliokua umetawala ndani ya ndege hiyo ukionekana kuninyima raha kabisa kwa sababu ya kuiruhusu na kuipa nafsi nafasi ya kunihukumu juu ya yale mambo yote niliyokua nimemfanyia Grace kitu kilicho sababisha nikose usingizi kabisa kwani licha ya idadi kubwa ya abiria kuonekana kusinzia kwangu bado mambo yalionekana kua magumu kwa sababu ya kutobanwa na usingizi kabisa.
ule ukimya mkubwa uliokua umetawala ndani ya ndege hiyo ambao ulionekana kuipa nafsi yangu ruhusa ya kunihukumu ulifanya zile sauti za kukoroma za abiria waliosinzia zisikike kwa mbali na kuzipita zile sauti za miungurumo ya injini za ndege hiyo ambazo zilionekana kumezwa na uzito wa mawingu makubwa yaliyokua yamelizunguka anga hilo la Tanzania kiasi cha kufanya mwezi pamoja na nyota za anga hilo vionekane kukosa ushirikiano kabisa na kusababisha giza zito lionekane kula ujana juu ya anga hizo kiasi cha kufanya idadi ya abiria waliosinzia ionekane kuzidi kuongezeka kadri muda ulivyozidi kusonga mbele.
licha ya ule ukimya mkubwa na lile giza zito kuonekana kutenda wema mwingi kwa kufanya idadi ya abiria walio wengi waonekane kusinzia kwangu bado hali ilionekana kua tofauti kabisa kwa sababu ya kutopata hata lepe la usingizi kitu kilichotokana na ule ukimya ulioonekana kutenda wema kwa abiria wengi kuiruhusu na kuipa nafsi yangu nafasi ya kunihukumu.

Kitendo cha nafsi yangu kunihukumu kilifanya nikose usingizi kabisa na kusabisha mawazo mazito yaliyoonekana kujaa majuto ndani yake yauvae mwili wangu na kuingia mpaka katika mzunguko wangu wa damu kitu kilichofanya nipatwe na hofu kubwa sana pamoja na huzuni nyingi kwa sababu ya kile kitendo cha kikubwa kikatili nilichokifanya cha kumkimbia mwanamke aliyekua akinipenda sana tena katika siku yake ya kujifungua ujauzito wangu niliompatia mimi mwenyewe kwa kutumia nyeti zangu.
kiukweli kadri nilivyozidi kujutia juu ya kile kitendo changu kiovu nilichomfanyia Grace ndivyo nilivyozidi kuumia sana kiasi cha kufanya nishindwe kuyazuia machozi ya huzuni na majuto yasinitoke kwani nilijikuta nikianza kulia sana bila kuwajali wale abiria wawili niliokua nimekaa nao siti moja huku kile kitendo cha kujutia kikifanya nianze kuikumbuka ile taswira ya kutisha ya Grace niliyemuacha hospitali akihangaika na kuugulia maumivu makubwa ya uchungu.

‘Ee Mungu naomba unisamehe na unihurumie juu ya yote niliyoyafanya’ nilijisemea kimoyomoyo huku nikizidi kulia kwa uchungu.

Ilikua imefika majira ya saa 10 kumi za usiku wakati ile ndege ya shirika la fast jet ilipoonekana kuingia na kuanza kuchepuka juu ya anga la nchi ya Kenya na hivyo kufanya tubakize nchi tatu ambazo ni Somalia,Ethiopia,na Yemen ndipo tuweze kuingia na kutua juu ya ardhi za nchi ya Oman sehemu nilipokua nikienda kumtafuta kipenzi changu Nairath.
majira hayohayo ya saa 10 ndio muda nilioshikwa na usingizi mzito pasipo ya kujielewa huku ile sala niliyomuomba Mungu muda mfupi uliopita ikionekana kunisaidia kwa kunifanya nipate usingizi mzito ambao ulisababisha nilale fofofo kiasi cha kufanya nionekane kuwa overtake wale wote walionitangulia kulala kwani kitendo changu cha kukoroma kwa sauti kubwa kama chura aliyetoswa kilionyesha wazi ni jinsi gani usingizi ule ulivyokua ukiyafaidi macho yangu.

Usingizi ule mzito ulifanya nisijue kitu kilichokua kinaendelea tena mpaka pale nilipokuja kighutuka usingizini na kukuta kukiwa kumekucha huku karibu kila abiria akionekana kuwa macho kitu kilichofanya ule ukimya mkubwa uliokua umeitawala ndege hiyo usiku mzima uonekane kupotea kabisa kwa sababu ya sauti za maongezi ya baadhi ya abiria kuanza kusikika kutoka karibu katika kila siti.

Ilikua ni saa 2 na nusu za asubuhi wakati ndege hiyo mali ya shirika la fast jet ilipoonekana kuingia na kuendelea kuchepuka katikati ya mawingu mazito ya anga la nchi ya Somalia huku mwanga wa jua liliokua likichomoza ukionekana kulipamba na kuling’arisha sana anga ilo lililokua limezungukwa na mawingu mengi ya rangi ya bluu huku mawingu machache meupe yakionekana kutembea kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kiasi cha kuonekana kana kwamba yalikua yakifukuzana na wale kunguru watukutu walioonekana kufanya mazoezi ya kuruka sarakasi za kikatili kwa ajili ya kukwepua vifaranga.
mwanga wa lile jua changa ulionekana kuyang’arisha sana mawingu ya lile anga la nchi ya Somalia kiasi cha kulifanya lionekane kupendeza sana na pia mwanga huo ulionekana kupenyeza mpaka kwenye baadhi ya vioo vya madirisha ya ndege hiyo kiasi cha kufanya karibu kila abiria aliyekua ameamka achungulie dirishani ku ushuhudia uzuri wa lile anga pamoja yale mashindano ya mbio za mawingu meupe ambayo yalionekana kufukuzana na wale kunguru watukutu waliokua wakifanya mazoezi yao ya sarakasi za kukwepua vifaranga paamoja na kukwepa manati.
kadri ndege hiyo ilivyozidi kulifaidi anga hilo la nchi ya Somalia ndivyo jua nalo lilivyozidi kuyachochea na kuyaongeza makali yake huku muda nao ukionekana kutokua nyuma kuusogelea mchana wa siku hiyo kwani ilikua inaelekea majira ya saa tatu za asubuhi wakati ndege hiyo mali ya shirika la fast jet ilipoonekana kuanza kulisogelea anga la nchi ya Ethiopia na hivyo kufanya tubakize nchi moja ya Yemen ndipo tuweze kutua juu ya ardhi ya nchi ya Oman.
.
Ilikua ni saa 3 za asubuhi wakati tulipokua tunaingia ndani ya nchi ya Ethiopia kitendo kilichofanya tubakize nchi moja ya Yemen ndipo tuweze kuingia na kutua juu ya nchi ya Oman mahali ilipokua nikienda kumtafuta laazizi wangu kipenzi Nairath pamoja na wale watoto wetu wawili ambao mpaka wakati huo sikua nimebahatika kumuona hata mmoja wao kwa macho yangu.

Kitendo cha kuingia ndani ya anga la nchi ya Ethiopia kilionekana kumfurahisha karibu kila abiria kwa sababu kua ya tumekubakiza nchi moja tu ndipo tuweze kuimaliza safari yetu.
lakini licha ya furaha hiyo ule umbali mrefu wa zaidi ya masaa manne na nusu uliokua umebaki kutoka Ethiopia hadi kuingia Yemen ulionekana kuipoozesha tena ile safari yetu kwani mara tu baada ya kumaliza saa moja juu ya anga la nchi hiyo ya Ethiopia ile hali ya ukimya ilianza kujirudia kwa mara nyingine tena kwa sababu ya idadi kubwa ya abiria kuanza kusinzia tena huku abiria wachache sana walionekana kuwa macho kwa sababu ya kujisomea vitabu vyao pamoja na kusikiliza mziki kutoka kwenye simu pamoja na ipad zao.
wakati ukimya ule ulipo onekana kujirudia tena dani ya ndege hiyo mimi pia nilikua miongoni mwa abiria waliosinzia tena huku kile kitendo cha kuchelewa kupata usingizi usiku kikifanya nilale fofofo kuliko nilivyolala usiku wa siku hiyo.

Nililala usingizi mzito sana kiasi cha kufanya nisiujue ule muda tulioingia ndani ya anga la nchi ya Yemen kwani nilikuja kughutuka tena majira ya saa nane na nusu mchana na kuikuta ile ndege ikiwa inechepuka juu ya anga la nchi hiyo ya Yemen na hivyo kufanya yabaki takribani masaa kama matatu ndipo tuweze kuingia ndani ya nchi ya Oman sehemu tulipokua tukiimalizia safari yetu.
nilijitahidi sana nisisinzie tena ndani ya yale masaa matatu yaliyokua yamebaki lakini wapi sikufanikiwa kwani nilijikuta nikiungana tena na idadi kubwa ya abiria walio wengi kusinzia kwa mara nyingine huku kile kitendo changu cha kutofahamiana na mtu kikifanya nisinzie zaidi kwa sababu ya kukosa mtu wa kuongea na kupiga nae stori.

Nilisinzia kwa mara nyingine tena nakumbuka nilikuja kughutuka kutoka usingizini mara baada ya ile sauti ya yule muhudumu wa kike kuanza kusikika tena kutoka kwenye zilezile spika za plastiki za hapo awali.

Ilikua majira ya saa 10 na nusu za nusu za jioni wakati ambapo ile sauti laini ya kizungu ya yule muhudumu wa ndege ilianza kusikika tenda kutoka kwenye zile spika za plastiki za ndege hiyo na kufanya mimi pamoja na abiria wote tuliokua tunasinzia tughutuke kutoka usingizini.

‘Attention please every one make sure you wear the belt we are going to fly down very soon’
(angalizo tafadhali kila mtu ahakikishe amefunga mkanda tunakwenda kutua hivi karibuni)
ilikua ni sauti ya yule mzungu wa kike muhudumu wa ndege hiyo ambapo mara baada ya kuacha kusikika milio ya vibanio vya mikanda ilianza kusikika tena kutoka kwa wale abiria waliokua wameivua mikanda hiyo.

‘We hope that every one have already wear the belt, all the best and welcome all to Oman’
(tunatumaini kila mtu ameshafunga mkanda, kila la heri na karibuni wote Oman)
sauti ile ilisema na kisha ikanyamaza tena.

Ghafla! Mara tu baada ya ile sauti kunyamaza taa kubwa mbili za kijani ziliwaka katikati ya mlango wa kuingilia katika chumba cha marubani na baada ya zile taa kuwaka ndege iliinama na kuanza kuelekea chini kuashiria kuwa tulikua tumeanza kutua juu ya ardhi ya nchi ya Oman.

Ilikua ni saa 11 kamili jioni kwa saa za nchini Oman wakati tulipo fanikiwa kutua salama ndani ya jiji la Musqat mji mkuu wa nchi hiyo ya Oman.
Musqat lilikua ni jiji zuri sana kuliko hata jiji la Dar es salaam kiukweli Musqat ilionekana kupambika sana hasa uzuri,ubora na uimara wa barabara na majengo yake ulionekana kipamba sana Musqat ambayo majengo yake mengi hayakuonekana kutofautiana sana na yale yaliyopo kule visiwani Zanzibari sema tu yenyewe yalionekana kuwa mapya na imara zaidi huku uwingi wa majengo ya misikiti yaliyolizunguka jiji hilo yakifanya karibu kila mtu aliyekua akikatiza mbele ya macho yangu aonekane kuwa ndani ya kanzu ama hijabu huku idadi kubwa ya wakazi wa jiji hilo wakionekana kuwa wa arabu pamoja na machotara wao.

Mara baada ya kutua jijini hapo nilibeba mizigo yangu na kuelekea sehemu vilipokuwepo vituo maalumu vya usafiri wa ndani ambapo mara baada ya kuvifikia nilichukua tax na kwenda mpaka sehemu ilipokuwepo hoteli ya Gulf of Oman ambayo nilielekezwa na mamdogo wake na Nairath pindi nilipoenda kule nyumbani kwake maeneo ya masaki.
basi baada ya kufika pale hotelini nilimlipa yule hela yake yule dereva tax ambaye hakutofautiana sana na Osama kwa sababu ya uwingi wa ndevu zake kisha baada ya kumlipa niliingia ndani hotelini humo na kwenda mpaka mapokezi ambapo nilifanya malipo kwa kutumia dollar na baada ya malipo nikapiga hatua mpaka katika kile chumba nilichokabidhiwa ambapo baada ya kukifikia niliingia na kufunga mlango kwa ndani kisha nikaenda kuoga ndani ya bafu lililokua ndani ya chumba hicho halafu baada ya kuoga nikaagiza chakula ambacho nilikila chote kwa sababu ya njaa iliyokua imeniuma na mara baada ya kula nilijitupa kitandani nikajilaza na kupumzika kwa sababu ya uwingi wa uchovu huku kesho yake asubuhi nikipanga nianze ile kazi yangu nzito iliyonipeleka huko ya kumtafuta Nairath wangu kipenzi pamoja na wale watoto wangu wawili Javier Hernandez pamoja na Grace.

….itaendelea….



ABCDEFGHIJKLMNOPQRSTUVWXYZ
 
Back
Top Bottom