Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

Simulizi: Nilipanga nyumba moja na majini

Mwisho sehemu ya 10
Endelea...
"Kaka unajua ukija kwangu njoo kwa heshima
zako zote na hoja zenye msingi, usije kama
mwendawazimu mpya, wewe unachokisema mimi
sijakisema kwako? Ulichukua hatua gani wakati
naumia mimi?"
"Lini umeniambia?"
"Wewe sijawahi kukupigia simu kukwambia? Tena
ukasema kama vipi nihame lakini sitarudishiwa
kodi ya nyumba na mimi nikakujibu niko tayari
kwa hilo"
"Sasa wewe ulikuwa ukiteswa kwa lipi, weka
ushahidi hapa kwamba ulikuwa ukiteseka sana."
"Sina haja, mimi ndiyo najua."
Wakati tukijibizana hivyo, wale waombaji walikuja
juu kwa kuomba. Walipaza sauti sana wakisema
moto uteketeze kila hila na jambo lolote ambalo
linakwenda kinyume na mimi ndani ya nyumba
ile.
Ghafla, nilimwona yule dalali akianza kuyumba
kama mlenvi, alikwenda kulia, kushoto,
akasimama, akawa
kama ananijia mimi, nikamkwepa, akaenda
kushoto na kuanguka puu!
Kwangu ilikuwa ni furaha kwani nilipata picha
kwamba, yule dalali alikuwa anahusika moja kwa
moja na matukio yote ya ajabu mle ndani.
Niliwaita wale watu wanaofanya maombi na
kuwataka washuhudie ambapo walipomwangalia
dalali waliongeza mkazo wa maombi yao.
Mwisho, dalali aliamka akiwa kama hana
ufahamu, alikalishwa chini na kuhojiwa ambapo
alisema mambo ya ajabu sana. Alisema
mwanaume aliyekuwa akiishi ndani ya vyumba
vile ni yeye na mkewe, akasema mkewe ni jini
kwa asilimia mia moja ila yeye si jini bali mkewe
alimfanya awe na uwezo wa kutoonekana wala
kujulikana na mtu.
Alipoulizwa kama alikuwa anapata faida yoyote
kwa kitendo cha kugeuka kuwa jini alijibu hakuna
ila alikuwa anasikia raha.
"Mfano, huyu bwana tangu ameishi humu
hajawahi kutuona kwa macho lakini sisi tulikuwa
tunamuona siku zote, tulikuwa tunaingia
chumbani mwake na kumfanyia mambo yetu
yeye hajui."
Jambo lingine ambalo lilinishangaza sana ni pale
dalali huyo aliposema yeye alikuwa na uwezo wa
kujua anachokusudia kukifanya mtu hata akiwa
Dodoma na akakizuia mapema. Ila, anashindwa
kujua endapo mtu huyo atakuwa anakusudia
kufanya jambo kwa kuliwaza moyoni mwake bila
kulisema kwa mtu.
Nilimuuliza mfano, akajibu mfano ni mimi na
mfanyakazi mwenzangu tulipokuwa tumepanga
kutumia bangi kuwaangamizi yeye na mkewe,
walijua kwa sababu tulijadili kwa sauti ndiyo
maana wao walijua. Akaongeza hata nilipoingia
ndani na yule mzee aliyeshindwa akatimua,
walijua tumepanga ndiyo maana wakawahi kwa
kuchukua simu na kufanya mahoka mengine.
Yule mzee mkubwa wa wale waombaji
akamuuliza: "Ina maana mkeo jini kwa sasa yuko
wapi?"
Yule bwana akajibu atakuwa amerudi ujinini kwa
sababu wakati wanaanza kuomba mkewe ndiye
aliyekuwa wa kwanza kuhisi anaungua moto na
kuanza kulia kwa sauti mpaka ndugu zake
wakajitokeza kumtwaa kwenda naye ujinini.
Yule mzee mkubwa wao akauliza swali jingine
ambalo na mimi nilitaka kuuliza. Alimuuliza hivi:
"Sasa watu wanasema majini wana uwezo
mkubwa, wanaweza kupata fedha na mali yoyote
ile, sasa kama wewe ulikuwa mume wa jini kweli
ni kwa nini aliamua uwe dalali?"
Dalali akajibu: "Mimi sikuwa dalali, bali nilijifanya
dalali ili nipate mtu wa kumpangisha ndani kwa
sababu mimi na mke wangu tulipenda
kuwachezea watu wanaoishi ndani.
"Mimi nina eneo Ilala la kuuza magari, pia nina
duka kubwa sana Mnazi Mmoja, sina shida ya
maisha wala ya fedha."
Kwa maneno yake hayo nilikubaliana na yeye
kwani ni kweli hali yake haikuwa ya kuchoka.
Hata siku ya kwanza nilipokutana naye
nilishangaa dalali gani ana mwonekano wa
kibosibosi ingawa hakuwa na gari. Hapo na mimi
nikapata nguvu ya kumuuliza swali:
"Sasa bwana dalali wa bandia, uliwezaje
kusababisha mimi nipate namba yako ya simu
kwa rafiki yangu anaitwa Mohamed Kombe na
akasema wewe ni dalali unaitwa Yusuf
Mwamba?"
"Sikia bwana Humuli. Nimeshasema sisi tuna
uwezo wa kujua kile kinachojadiliwa mahali na
kukifanyia kazi.
Dalali anayeitwa Yusuf Mwamba yupo, huyo rafiki
yako tulimchezesha ulimi wakati wa kutaja
namba, akazitaja zangu badala ya za Yusuf."
Nilichoka kabisa, yule mzee mkuu akasema
tumwingize ndani maana watu waliokuwa
wakipita walianza kukodolea macho pale nje.
Kule ndani, dalali aliendelea kuzungumza mambo
mengi sana lakini kuna wakati alijipinda na
kujishika mgongo akidai anahisi maumivu makali
ya moto. Alisema sehemu hiyo ipo kama kuna
mtu amebandika jiko la mkaa.
"Mungu amekuponya sana labda kama hutajutia
matendo yako ya nyuma," alisema yule mzee
aliyenisaidia.
"Mimi sitaki tena, kwanza najuta kwa nini
niligeuka adui na kufanya vile kwa watu wengine.
Naomba mniombee sana kwa huyo Mungu wetu."
Yule mzee alimwelekeza kanisa lake ambalo
halikuwa mbali na pale nyumbani, yule dalali
akasema atakwenda kesho yake mapema.
Mimi pia nilialikwa, nikakubali kwenda kesho
yake. Walipoondoka, nilibaki na dalali. Wasiwasi
ulinishika lakini
nikawa nasikilizia. Kila baada ya dakika tano
dalali aliingia chumbani kwangu na kuniomba
nimsamehe kwa yote yaliyopita.
Usiku nililala usingizi mzuri hadi kunakucha kiasi
kwamba sikuamini kama ni kweli ile nyumba
ilikuwa vile. Kesho yake nilikwenda kazini, jioni
nilikwenda kwenye lile kanisa ambapo nilimkuta
dalali ameshafika.
Tulianza kuwa waumini wa kanisa hilo. Baada ya
wiki mbili, dalali alimleta mke wake na mtoto
mmoja ndani, kumbe alioa na familia yake ilikuwa
Dodoma. Baada ya mwezi mmoja na mimi
nilihamia Buguruni ambapo nilioa lakini bado
nasali kulekule Magomeni na yule dalali.
Namshukuru sana Mungu kwa kunipigania. Ile
mikono ilikuwa si salama bila neema ya Mungu.
Nadhani shetani alipanga nife lakini ameshindwa
katika jina la Mungu. Amina.
MWISHO.
***Neno La Muandishi***
-EWE MWANADAMU MUOGOPE MUNGU, WALA
USIZITEGEMEE AKILI ZAKO MWENYEWE KATIKA
KUTATUA MAGUMU UNAYOPITIA, MTEGEMEE
MUNGU, KAMA HUMULI NA HATIMAYE
ALIFANIKIWA.
Mengineyo
-WIKI IJAYO KUTAKUWEPO NA HADITHI MPYA
YA MKUFU WA MALKIA WA KIJINI
PIA USISAHAU KUSHARE STORY HII, KESHO
SHAIJA ITAKUEPO
 
S
Hii hadithi ilikua inatoka kwenye gazeti la ijumaa au kiu sikumbuki vizuri...

Ila ipo mtandaoni tangu 2012 ikiwa inapatikana kwenye website ya gazeti husika.

Leo imeletwa humu mwandishi kabadilika na watu wote wanaonesha hawaijui.
Jamaa umefanya plagiarism.
Sio kweli wala hazifanan
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom