Kilawo
JF-Expert Member
- Nov 15, 2016
- 1,921
- 3,373
Abaki anasubiri nini?!! Wakati anajua wazi, tunaishi mara moja tu.....
Mwisho sehemu ya 10
Endelea...
"Kaka unajua ukija kwangu njoo kwa heshima
zako zote na hoja zenye msingi, usije kama
mwendawazimu mpya, wewe unachokisema mimi
sijakisema kwako? Ulichukua hatua gani wakati
naumia mimi?"
"Lini umeniambia?"
"Wewe sijawahi kukupigia simu kukwambia? Tena
ukasema kama vipi nihame lakini sitarudishiwa
kodi ya nyumba na mimi nikakujibu niko tayari
kwa hilo"
"Sasa wewe ulikuwa ukiteswa kwa lipi, weka
ushahidi hapa kwamba ulikuwa ukiteseka sana."
"Sina haja, mimi ndiyo najua."
Wakati tukijibizana hivyo, wale waombaji walikuja
juu kwa kuomba. Walipaza sauti sana wakisema
moto uteketeze kila hila na jambo lolote ambalo
linakwenda kinyume na mimi ndani ya nyumba
ile.
Ghafla, nilimwona yule dalali akianza kuyumba
kama mlenvi, alikwenda kulia, kushoto,
akasimama, akawa
kama ananijia mimi, nikamkwepa, akaenda
kushoto na kuanguka puu!
Kwangu ilikuwa ni furaha kwani nilipata picha
kwamba, yule dalali alikuwa anahusika moja kwa
moja na matukio yote ya ajabu mle ndani.
Niliwaita wale watu wanaofanya maombi na
kuwataka washuhudie ambapo walipomwangalia
dalali waliongeza mkazo wa maombi yao.
Mwisho, dalali aliamka akiwa kama hana
ufahamu, alikalishwa chini na kuhojiwa ambapo
alisema mambo ya ajabu sana. Alisema
mwanaume aliyekuwa akiishi ndani ya vyumba
vile ni yeye na mkewe, akasema mkewe ni jini
kwa asilimia mia moja ila yeye si jini bali mkewe
alimfanya awe na uwezo wa kutoonekana wala
kujulikana na mtu.
Alipoulizwa kama alikuwa anapata faida yoyote
kwa kitendo cha kugeuka kuwa jini alijibu hakuna
ila alikuwa anasikia raha.
"Mfano, huyu bwana tangu ameishi humu
hajawahi kutuona kwa macho lakini sisi tulikuwa
tunamuona siku zote, tulikuwa tunaingia
chumbani mwake na kumfanyia mambo yetu
yeye hajui."
Jambo lingine ambalo lilinishangaza sana ni pale
dalali huyo aliposema yeye alikuwa na uwezo wa
kujua anachokusudia kukifanya mtu hata akiwa
Dodoma na akakizuia mapema. Ila, anashindwa
kujua endapo mtu huyo atakuwa anakusudia
kufanya jambo kwa kuliwaza moyoni mwake bila
kulisema kwa mtu.
Nilimuuliza mfano, akajibu mfano ni mimi na
mfanyakazi mwenzangu tulipokuwa tumepanga
kutumia bangi kuwaangamizi yeye na mkewe,
walijua kwa sababu tulijadili kwa sauti ndiyo
maana wao walijua. Akaongeza hata nilipoingia
ndani na yule mzee aliyeshindwa akatimua,
walijua tumepanga ndiyo maana wakawahi kwa
kuchukua simu na kufanya mahoka mengine.
Yule mzee mkubwa wa wale waombaji
akamuuliza: "Ina maana mkeo jini kwa sasa yuko
wapi?"
Yule bwana akajibu atakuwa amerudi ujinini kwa
sababu wakati wanaanza kuomba mkewe ndiye
aliyekuwa wa kwanza kuhisi anaungua moto na
kuanza kulia kwa sauti mpaka ndugu zake
wakajitokeza kumtwaa kwenda naye ujinini.
Yule mzee mkubwa wao akauliza swali jingine
ambalo na mimi nilitaka kuuliza. Alimuuliza hivi:
"Sasa watu wanasema majini wana uwezo
mkubwa, wanaweza kupata fedha na mali yoyote
ile, sasa kama wewe ulikuwa mume wa jini kweli
ni kwa nini aliamua uwe dalali?"
Dalali akajibu: "Mimi sikuwa dalali, bali nilijifanya
dalali ili nipate mtu wa kumpangisha ndani kwa
sababu mimi na mke wangu tulipenda
kuwachezea watu wanaoishi ndani.
"Mimi nina eneo Ilala la kuuza magari, pia nina
duka kubwa sana Mnazi Mmoja, sina shida ya
maisha wala ya fedha."
Kwa maneno yake hayo nilikubaliana na yeye
kwani ni kweli hali yake haikuwa ya kuchoka.
Hata siku ya kwanza nilipokutana naye
nilishangaa dalali gani ana mwonekano wa
kibosibosi ingawa hakuwa na gari. Hapo na mimi
nikapata nguvu ya kumuuliza swali:
"Sasa bwana dalali wa bandia, uliwezaje
kusababisha mimi nipate namba yako ya simu
kwa rafiki yangu anaitwa Mohamed Kombe na
akasema wewe ni dalali unaitwa Yusuf
Mwamba?"
"Sikia bwana Humuli. Nimeshasema sisi tuna
uwezo wa kujua kile kinachojadiliwa mahali na
kukifanyia kazi.
Dalali anayeitwa Yusuf Mwamba yupo, huyo rafiki
yako tulimchezesha ulimi wakati wa kutaja
namba, akazitaja zangu badala ya za Yusuf."
Nilichoka kabisa, yule mzee mkuu akasema
tumwingize ndani maana watu waliokuwa
wakipita walianza kukodolea macho pale nje.
Kule ndani, dalali aliendelea kuzungumza mambo
mengi sana lakini kuna wakati alijipinda na
kujishika mgongo akidai anahisi maumivu makali
ya moto. Alisema sehemu hiyo ipo kama kuna
mtu amebandika jiko la mkaa.
"Mungu amekuponya sana labda kama hutajutia
matendo yako ya nyuma," alisema yule mzee
aliyenisaidia.
"Mimi sitaki tena, kwanza najuta kwa nini
niligeuka adui na kufanya vile kwa watu wengine.
Naomba mniombee sana kwa huyo Mungu wetu."
Yule mzee alimwelekeza kanisa lake ambalo
halikuwa mbali na pale nyumbani, yule dalali
akasema atakwenda kesho yake mapema.
Mimi pia nilialikwa, nikakubali kwenda kesho
yake. Walipoondoka, nilibaki na dalali. Wasiwasi
ulinishika lakini
nikawa nasikilizia. Kila baada ya dakika tano
dalali aliingia chumbani kwangu na kuniomba
nimsamehe kwa yote yaliyopita.
Usiku nililala usingizi mzuri hadi kunakucha kiasi
kwamba sikuamini kama ni kweli ile nyumba
ilikuwa vile. Kesho yake nilikwenda kazini, jioni
nilikwenda kwenye lile kanisa ambapo nilimkuta
dalali ameshafika.
Tulianza kuwa waumini wa kanisa hilo. Baada ya
wiki mbili, dalali alimleta mke wake na mtoto
mmoja ndani, kumbe alioa na familia yake ilikuwa
Dodoma. Baada ya mwezi mmoja na mimi
nilihamia Buguruni ambapo nilioa lakini bado
nasali kulekule Magomeni na yule dalali.
Namshukuru sana Mungu kwa kunipigania. Ile
mikono ilikuwa si salama bila neema ya Mungu.
Nadhani shetani alipanga nife lakini ameshindwa
katika jina la Mungu. Amina.
MWISHO.
***Neno La Muandishi***
-EWE MWANADAMU MUOGOPE MUNGU, WALA
USIZITEGEMEE AKILI ZAKO MWENYEWE KATIKA
KUTATUA MAGUMU UNAYOPITIA, MTEGEMEE
MUNGU, KAMA HUMULI NA HATIMAYE
ALIFANIKIWA.
Mengineyo
-WIKI IJAYO KUTAKUWEPO NA HADITHI MPYA
YA MKUFU WA MALKIA WA KIJINI
PIA USISAHAU KUSHARE STORY HII, KESHO
SHAIJA ITAKUEPO
Hata kama ilishaletwa..haina shida mbona...Mkuu ebu tuma nakara hata moja
Hata kama ilishaletwa..haina shida mbona...
Wengi humu jawakuwahi isoma so asante kwa kutuletea!
Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba unitag kwenye hii mkuu.MKUFU WA MALKIA WA KIJINI
Coming soon
Yesu ndiyo dawa pekee ya hawa ndugu zako majini!Kama vile itaishia kwa wachungaji na walokole!?
Unamoyo baba ingekua Mimi baada tyu ya kusikia maneno kitaani ningeondokaTHE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)
MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI
MWANDISHI: METECK DERTHOD
Sehemu ya 04
Endelea...
Nilitoka sebuleni, nikaenda chumbani, kitandani
nikakuta toilet paper' ikiwa imekatwa sehemu.
Mimi niliicha pembeni ya dirisha, lakini ikaonesha
kuna mtu aliichukua na kunyofoa kidogo kisha
badala ya kuirudishia palepale, yeye aliiacha
kitandani.
Mbali na toilet paper' pia kuna kikopo chenye
vijiti vyenye pamba za masikio kilikuwa kwenye
stuli jirani na kitanda, lakini kwa muda huo
kilikuwa kimeanguka chini halafu vijiti vimebaki
kama vitatu tu kwa maana kwamba, aliyeingia
kuchukua toilet paper' ndiye huyohuyo aliyechota
vijiti vya pamba.
Nilianza kuhisi kuwa sikuwa kwenye nyumba
salama, lakini kwa uthibitisho upi? Moyoni
nikasema nitajua tu, mimi ndiyo mimi.
Nilikaa ndani kwangu hadi usiku ulipoingia,
nikasema nibadili nguo kwa kuvaa bukta na
singilendi halafu nitoke kwenda kula gengeni
kwani siku hiyo sikuwa najisikia kupika chochote.
Ni mara nyingi nilipenda kula gengeni.
Nilitoka, nikasimama mlangoni ili nifunge mlango
wa chumbani, nilipoangalia chini, upande wa
wenzangu nilikuta nje ya mlango wao pana vijiti
vya pamba za masikioni vikiwa vimetumika,
nikiwa katika mshango, mbele nikaona tishu ikiwa
imefutiwa majimaji yenye rangi nyekundu kama
damu.
Nilitembea kwa wasiwasi, nikatoka nje, sikufunga
mlango kwa funguo, lakini niliubamiza tu, funguo
nilikuwa nazo, nikaenda gengeni kula.
Pale kwenye genge ambapo si mbali sana na
nyumbani, alikuja yule mama aliyeniuliza mimi ni
mtu wa wapi, nilimsalimia, lakini kabla hajaitikia
alishtuka kuniona.
"Upo kijana wangu?"Nipo mama, nimetoka kazini nimekuja kupata
kidogo."
"Pole sana, uoe sasa."
"Huo ndiyo mpango wangu mama."
"Ee, uoe halafu mimi nitakupa vyumba viwili pale
kwangu, nakuahidi."
"Nashukuru sana mama. Naanza kujipanga."
"Sawa, vipi wenzako lakini?"
Nilisita kumjibu, nikabaki namwangalia tu, naye
alibaini kwamba nimepata mshtuko na swali lake.
"Vipi wapangaji wenzako, naamini utakuwa
hujaonana nao?"
"Ni kweli mama, tena hebu nakuomba kidogo,"
nilisema nikienda pembeni kidogo ili na yeye
anifuate tukaongee.
"Niambie," alianza kusema.
Nilimuuliza kama kuna anachokijua chochote kile
kuhusu wale wapangaji wenzangu. Alianza kwa
kusema:
"Kusema ule ukweli sina kwa undani, ila napenda
kukwambia kwamba, unaishi na watu ambao
unahitajika moyo wa ziada ili uweze kuendelea
kuishi nao.
"Pale mbali na wewe, pameshakaa wapangaji
wengine saba, tena wote kama wewe, hawajaoa.
Lakini kinachoshangaza ni kwamba, wanaondoka
baada ya wiki mbili, mmoja aliondoka baada ya
siku tatu tu."
"Kwa hiyo hakuna hata mmoja aliyewahi
kukwambia ameona nini kule ndani?
"
"Hakuna."
"Lo! Mimi mama mambo ninayoyaona yanatisha."
"Kama mambo yapi, nisimulie kidogo."
Nilipotaka kuanza kumsimulia huyu mwanamke,
ghafla alitokea msichana mmoja, mweupe, mrefu
kiasi, amejazia sehemu mbalimbali za mwili,
akaguna na kusema:
"Kaka Humuli mambo vipi, za siku?"
Nilipata kigugumizi kikubwa kumjibu mambo poa
kwani sikumjua na sikuwa nakumbuka chochote
kuhusu yeye, sura yake ilikataa kichwani
mwangu.
"Wewe ni nani kwani?" nilimuuliza.
Akaachia tabasamu kwa mbali, uzuri wake
ukaongezeka.
"Ha! Humuli, hunikumbuki mimi, kweli?"
"Sikukumbuki hata kidogo."
"Sasa we binti, kama wewe ndiyo unamkumbuka
si umkumbushe mlionana wapi?" yule mwanamke
alisema kwa sauti ya mshangao.
Lakini yule msichana mrembo alimwangalia yule
mwanamke kwa macho yaliyojaa hasira
"Mama uhusiki."
"Najua, lakini unapoteza muda kwa
kuzungushazungusha wakati kumbe wewe
unamkumbuka, yeye umeshajua hakukumbuki na
amekwambia tayari."
Nilishangaa kumwona yule msichana akibetua
kichwa kama aliyekuwa akiweka vizuri nywele
zake, ghafla yule mwanamke niliyekuwa naye
akajishika kichwa na kulalamika kinamuuma
sana.
"Jamani kichwa! Kichwa jamani, daa!"
"Vipi mama, imekuwaje kwani?" nilimuuliza.
"Kichwa Humuli, kinavuta ghafla! Uwiii."
Nilianza kuogopa, nilihisi naangukiwa na msala
maana akifa pale na watu waliona nikienda naye
pembeni si nitahojiwa mimi?
"Kwani mama una kawaida ya
kuumwa kichwa?"
nilimuuliza nikimsogelea ambapo yeye sasa
alikuwa ameinama.
"Sina, ndiyo nashangaa hapa."
Niliona hakuna dawa nyingine zaidi ya kumpeleka
kwake ili nikaungane na familia yake kumpeleka
hospitali. Lakini kabla ya kufanya hivyo niliinua
macho ili nimwambie yule dada anisaidie na
kama anataka kunikumbusha, hayo yangefanyika
baadaye.
Ile naanaza kusema anti huku nikiwa nimeinua
macho, nilishangaa kutomwona yule msichana
pale.
"Khaa!" nilijikuta nikisema hivyo.
"Mama twende nyumbani ili tukupeleke hospitali
na watoto wako."
"Ha! Mbona kimeachia," alisema akionekana
kushangaa na kuniangalia, alikuwa amepanua
kinywa.
"Kweli?"
"Eee, niko mzima kabisa."
"Au?" nilitaka kusema neno lakini zikulimaliza,
nikahisi ulimi unakuwa mzito si kwa kushikwa bali
kwa matakwa yangu.
"Humuli."
"Naam."
"Ni kweli yule binti humjui?"
"Simjui mama."
"Kuna mawili hapo, humjui au humkumbuki."
"Vyote mama, simkumbuki na pia simjui."
"Lakini wewe si alikutaja kwa jina?"
"Mwenyewe nilishangaa sana."
"Basi Humuli nimeshaelewa, kwaheri, nimeelawa
ni kwa nini nimeugua kichwa na yule ni nani, pole
sana wewe kijana," alisema yule mwanamke
huku akiondoka zake kuelekea kwake.
Nilimtazama, lakini baadaye nilirudi kwenye
kibanda cha chipsi.
"Mzee nakuona na miss jini," muuza chipsi
mmoja alisema.
"Yupi, yule mwanamke?"
"Hapana, yule msichana."
"Mi simjui, kwani anaishi wapi?
Maana kasema
ananijua, ameniita na jina."
"Khaa! Kumbe wewe kama sisi. Huyu dada
anaishi mitaa hiihii, lakini hakuna hata mmoja
anayejua nyumba anayoishi!
"Kuna jamaa mmoja anaitwa Maleke, Maleke
aliwahi kumfuatilia kwa nyuma lakini alishindwa
kujua aliingia nyumba gani!"
"Mh! Au jini?" niliuliza kwa mshtuko mkubwa.
"Ndivyo watu wanavyosema, sasa alipokuja
kusimama na wewe, tukawa tunabishana,
wengine wanasema ni miss jini, wengine siye,
lakini alipokuwa anaondoka tukagundua ni miss
jini."
Basi, tuliishia hapo, nikachukua chipsi zangu na
kwenda nazo nyumbani, niliamua kwenda kulia
kule.
Nilifika, nikasukuma mlango mkubwa nikazama
ndani kwangu. Lakini wakati napita kwenye
usawa wa chumba cha wale wenzangu nikasikia
vicheko, tena vicheko kwelikweli.
Sikuwajali, nikaingia sebuleni kwangu, nikafunga
mlango kwa ndani, nikaweka chipsi juu ya meza,
nikaenda pembeni ya chumba ambako kuna ndoo
ya maji ili nichote ya kunawa. Wakati naanza
kula nilihisi na kugundua kitu. Niligundua
mabakimabaki ya chipsi na kuku juu ya meza
yangu wakati ukweli ni kwamba, tangu nimehamia
pale sikuwahi kula chipsi wala kuku
.
"Humu ndani kuna mtu anaingia kufanya mambo
yake, lini mimi nimekula chipsi na kuku humu
ndani?" nilijiuliza, nikasikia kicheko kutoka kwa
wenzangu.
"Haa! Haaa! Ha! Haaaa haah"
ITAENDELEA...
SIMULIZI: THE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)
MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI
MWANDISHI: METECK DERTHOD
Sehemu ya 03
Endelea...
"Wale wapangaji wenzangu siwaelewi kabisa."
"Kivipi?"
"Ah! Watu gani mimi mgeni nimehamia
washindwe kutoka kunisalimia ili angalau
tufahamiane?"
Dalali alicheka sana kisha akasema:
"Wale ndivyo walivyo bwana, si unajua tena
malezi, mwingine kalelewa vile, mwingine hivi. Ila
ulichokisema ni kweli, haiwezekani nyumba
mnayoishi mpate mgeni halafu msitambuane,
sasa mkikutana njiani je?"
"Si ndiyo hapo sasa," nilisema nikijifanya lawama
zangu ni kwa ajili ya hilo tu, lakini kumbe
nilikuwa na zaidi ya hapo.
Kazini siku hiyo nilishinda sina amani, sina raha,
mwili ulikuwa kama umetoka kufanya kazi nzito
ambayo sijawahi kuifanya kwa siku nyingi,
wenyeji wa Pwani wanaita mavune.
Kwa upande mwingine nilitamani sana jioni ifike
ili nikaone siku hiyo kitatokea kitu gani kipya
kwenye nyumba ile. Jioni ilifika, nikaondoka
kazini, sikutaka kupitia popote, dukuduku langu
lilikuwa kwenda nyumbani tu.
Nilichukua kama saa moja kutoka kazini hadi
kufika nyumbani. Nje nilikuta mfuko wa rambo
mweusi, ndani yake ulionekana kuwa na kitu
kwani ulikuwa umetuna sana. Niliinama
kuipekenyua ili nijue ndani kulikuwa na nini,
nilishangaa kuona ni vipande vya nyama za
kuchoma tena vilikuwa vya moto
.
"Kha! Atakuwa nani ameweka?" nilijiuliza
mwenyewe, nikauacha palepale, mimi nikapanda
ngazi za kuingia ndani. Mlango ulikuwa wazi hali
iliyoashiria kwamba, wenzangu walisharudi.
Nilisukuma mlango, nikaingia. Nilikutana na
harufu ya pafyumu, nikahisi walikuwa wakijiandaa
kutoka.
"Jamani za leo?" nilisalimia kwa sauti ya juu
licha ya kwamba, mlango wao ulikuwa
umefungwa, hakuna aliyeniitikia, hilo sikulijali
sana kwani niliamini kwa kuwa walikuwa ndani,
isingekuwa rahisi wasikie salamu yangu.
Niliingia sebuleni kwangu, kisha nikaenda
chumbani, kuna kitu kilinishangaza, nikasimama
kwa mshtuko. Nilikuta sehemu nilipoweka kiberiti
asubuhi siyo, nilikiacha juu ya meza, nikakikuta
juu ya kitanda.
Niliacha kioo na kitana juu ya
kitanda, lakini nikavikuta kwenye stuli, niliguna!
Nilikishika kioo na kukiangalia kwa umakini kama
kina mabadiliko yoyote, lakini sikuona, nikashika
kitana. Nilipokigaua sana pia sikuona kitu cha
tofauti, nikaamua kuchania, nikahisi kuguswa na
kitu kama nywele ndefu kama za mtu aliyefuga.
Nilikiweka kitana juu usawa wa dirishani, nikaona
nywelenywele nene, nyeusi, mwili wote
ukasisimka.
Ninavyojua mimi, mwanamke mwenye nywele
nyingi akichania kitana, ndiyo huacha nywele,
sasa mimi nilikuwa na nywele fupi sana
zisingeweza kuacha nywele ndefu kwenye kitana.
"Mh! Hapa kuna kinachoendelea," nilisema
moyoni huku nikikaa. Nilishtuka zaidi kuona soksi
zikiwa kwenye msumari nyuma ya mlango wakati
niliacha chini.
"Huyu ni nani?" niliuliza kwa sauti ya ukali.
Ghafla nikasikia kicheko kutoka chumbani kwa
wale wenzangu. Nilikaa kwenye kochi, nikaanza
kuangalia sehemu mbalimbali za mle ndani
ambazo niliamini naweza kuona mabadiliko
mengine mbali na yale ambayo nilishayaona,
lakini sikubahatika.
Nilitoka, nikaenda sebuleni ambako nako nilianza
kuangalia kila kona ya sebule.
Nilishangaa kuona
glasi ya maji ya kunywa ambayo niliitumia
asubuhi kisha nikaacha maji yamejaa, ikiwa haina
hata tone la maji mbaya zaidi, iliwekwa juu ya
kabati ambapo mimi niliiweka kwenye meza ya
katikati ya sebule.
"Mh! Hii kali sasa," nilijikuta nikisema kwa sauti,
mara nikasikia kicheko tena kutokea upande wa
pili kule kwa wenzangu. Sasa nikaanza kama
kuhisi kitu kuhusu watu hao. Ni kwa nini kila
nilipoongea kwa sauti ndipo na wao waliangua
kicheko?
Niliamua kujaribu tena, nikasema kwa sauti:
"Nitakuja kuua mtu, kweli tena." Nikasikia
kicheko tena, safari hii kilidumu kwa muda.
Moyoni nikasema naanza kufanyia kazi uhusiano
wa maneno yangu na vicheko vya wale majirani.
Nilitoka kurudi chumbani, wakati napita kwenye
korido, nilisimama jirani na mlango wao.
Walikuwa wakiongea, lakini niliposimama mimi,
kukawa kimya ghafla kama hakuna watu.
Nilipozama chumbani, nyuma wakaanza kuongea
tena. Sikufunga mlango ili niweze kusikia
wanachokiongea, lakini jamani kwa kusema ule
ukweli wa Mungu, sikujua walikuwa wakitumia
lugha gani katika kuwasiliana hata pale
nilipojitahidi kutega masikio kwa umakini wa hali
ya juu sana.
Kuna wakati utadhani wanatumia sana neno
dotikom, lakini ukisema usikilize zaidi unasikia
wakisema sana kotoko au kiburate, wakati
mwingine sauti ya kike ilisema kaunto, ya kiume
ikarudia hivyohivyo, kaunto.
Nia yangu kubwa ilikuwa kuwaona kwa sura na
kufahamu kama ni ngozi nyeusi au nyeupe. Hilo
peke yake lingenipa mwanga ni watu wa aina
gani naishi nao pale ndani ya nyumba.
Nilisikia mlango wa chumbani kwao ukifunguliwa
na mimi nikatoka haraka sana, cha ajabu sikuona
mtu akitoka lakini mlangoni kulikuwa na
kandambili pea moja tu wakati zilikuwa pea mbili.
Hilo lilimaanisha kwamba, mmoja wao alitoka
kwenda chooni, nilichofanya ni kuamua
kusimama katikati ya mlango wangu ili huyo
aliyekwenda chooni akirudi nimuone. Ni kweli
mmoja wao alikwenda chooni kwani nilisikia mlio
wa maji.
NilijiTahidi kusimama mlangoni kwangu
kumsubiria. Kwa ramani ya nyumba ile ilivyo,
asingeweza kutoka chooni bila mimi kumwona
hata kama angekuwa anataka kutoka kwenda nje
au uani.
Mlio wa maji ulikosa kusikika, nikawa natumbulia
macho kule huku moyoni nikisema:
"Leo ndiyo
leo, asemaye kesho mwongo, hata afanyaje,
hawezi kunichenga hapa hata kidogo," nilisema
moyoni, ingawa wakati huo mapigo ya moyo
yalikuwa yakinienda kwa kasi.
Nilipoanza kuhisi muda unakwenda na hakuna
mtu aliyetoka, nikampa dakika tatu kwamba
lazima atakuwa anavaa ndiyo maana
anachelewa: "Labda alikuwa anajisaidia haja
kubwa, maana wengine huwa wanavua nguo
zote, lakini mimi nipo, siendi kokote," nilisema
moyoni nikiwa bado nimesimama mlangoni
kwangu.
Baada ya muda, nikasikia watu wakiongea
chumbani kwao, nikashtuka, nilijikuta nikisema:
"Haa!"
Haraka sana nilitupa macho mlangoni kuangalia
kandambili, nikazikuta pea mbili, nikashangaa:
"Ina maana amenipita hapahapa au?
Haiwezekani, asingeweza kunipita hata kama
ingekuwaje?" niliwaza. Nilitoka kuelekea chooni,
nikakuta mlango uko wazi, nikachungulia ndani,
hakukuwa na mtu, nikanyoosha mikoni, nikarudi
ndani.
Nilifikia kwenye kochi sebuleni, nikahema kwa
nguvu kwani niliamini nimo ndani ya miujiza
mikubwa ya ndani ya nyumba ile.
"Hivi ni kwa nini dalali alinidanganya hivi?"
nilijiuliza mwenyewe nikiamini kwamba, dalali
aliyenipangisha nyumba ile alijua mchezo mzima
ila alitaka kupata fedha tu ndiyo maana
alinipangisha bila kunipa tahadhari....!
ITAENDELEA...
Nishida kweli me mwenyewe nimeona mauzauza mengi sana hukoDaaa nyumba zakupanga nishida
Dah kazi kweli kweliSIMULIZI: THE HOUSE OF THE DEVIL (Nyumba
ya kishetani)
SEHEMU YA 02
MSIMULIAJI: HUMULI SAMAKI
MWANDISHI: METECK DERTHOD
Endelea...
Lakini sikulala mpaka nikampigia simu dalali
kumuuliza kama wale wapangaji wenzangu ni
weupe au waswahili kama mimi, akasema hata
yeye hajui kwani hakuwahi kuwaona hata siku
moja.
Basi, nililala. Asubuhi niliamka nikiwa nimechoka
sana. Wakati nakwenda bafuni kuoga niligundua
ni mimi peke yangu ndiye niliyekuwa nimetangulia
kuamka, kwani bafuni hakukuwa na maji
yaliyomwagika kwa muda huo.
Baada ya kuoga nilirudi chumbani kwangu
kujiandaa kwenda kazini. Wakati najiandaa,
nilisikia mlango ukifunguliwa, nikajua ni wenzangu
wanakwenda kuoga au chooni kama ilivyo
kawaida kwa wanadamu wakiamka asubuhi.
Niliamua kutumia nafasi hiyo kuwatambua.
Nilivizia pale niliposikia mlio wa maji bafuni na
mimi nikatoka kwenda kupiga mswaki kwa marau
ya pili. Sehemu niliyosimama, mtu akitoka bafuni
kwenda ndani ilikuwa lazima nimuone kwani
ilikuwa kiasi cha kugeuka tu.
Lakini cha kushangaza, nilikuwa sisikii maji
kumwagika, nikageuka na kuona mlango wa
bafuni upo wazi. Mbali na mlango kuwa wazi, pia
chini nikaona alama za kandambili nne zikiwa
zimekanyaga, nikajua wametoka.
"Lakini wamepitaje hapa?" nilijiuliza.
Nilirudi ndani, mlangoni kwao nilikuta kandambili
pea mbili zikiwa bado na majimaji kwa mbali,
jambo hili lilinifanya nijiulize sana.
Nilijipa ujasiri na kuamua kuchungulia ndani ya
chumba hicho kwa kutumia nafasi ya katikati ya
mlango ambapo niliweza kuona hadi kitanda
lakini sikumwona mtu mwingine.
Niliingia kwangu, nikaweka mswaki, nikavaa vizuri
na kuondoka zangu. Nilitegemea wenzangu
nimewaacha ndani, kwani nilipofika mlangoni
nilikuta umefunguliwa na upo wazi. Nilirudi ndani
hadi kwenye mlango wao.
"Wa ndugu," niliita kwa sauti.
"Jamani wa ndugu."
Ukimya ndiyo ulinifanya nibaini walishaondoka.
Kwani kulikuwa kimya sana na kandambili
zilikuwa pembeni ya mlango si pale pa kwanza.
Nilifunga mlango mkubwa nikaondoka, mbele
nilimwona yule mama aliyekuja usiku kuniuliza
maswali. Alikuwa amesimama nje ya nyumba
yake, aliponiona akashutuka na kuita majina
mawili ya watu. Wakatoka watoto wake wawili, ni
mabinti wenye miaka kama kumi na nane na
ishirini na mbili hivi.
"Hujambo kijana?" yule mama alinisalimia kwa
furaha.
"Sijambo mama, shikamoo."
"Marhaba." Kisha akawaambia kitu wale watoto
wake nao wakanikazia macho.
"Mama umewaona majirani zangu hapa?"
"Majirani zako akina nani?"
"Wapangaji wenzangu."
"Kijana, kua uyaone ya dunia. We si umeshakua,
utayaona ya dunia."
Kauli hiyo iliniogopesha sana, nikashtuka na
kumuuliza mama.
"Mama una maana gani?"
"Sisi hatutaki umbeya kijana."
"We si umeambiwa utayaona kwa hiyo subiri tu,"
alidakia binti yake mkubwa.
Miguu ilitetemeka, mwili uliisha nguvu, nikajikuta
nataka kukaa, lakini sikuweza. Nilichoamua ni
kuondoka huku nampigia simu yule dalali.
"Vipi hujambo bwana?"
"Mimi sijambo."
"Za makazi mapya."
"Si nzuri bwana."
"Kwa nini tena?"
"Sielewielewi."
"Kivipi?"
"Kuna mambo kama si ya kawaida."
"Yapi hayo?"
ITAENDELEA...
NATAKA KULIKE KWA SANA PIA
COMMENT YAKO NI MUHIMU