stable woman
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 3,887
- 4,467
Yaani wengine hapa tumekosa hadi usingizi tunachungulia kama tumeinjika maharage jikoni
Yaani wengine hapa tumekosa hadi usingizi tunachungulia kama tumeinjika maharage jikoni
Sent using Jamii Forums mobile app
Utaweza?Mimi ngoja nikaushe kama week hivi ili nikirudi nikute zishakua nyingi,nisome nimetulia......
Sent using Jamii Forums mobile app
Sehemu ya 25
Niliingia ndani, nilipotupa macho kwa mbele nilishtuka kumuona mzee Sambi na mkewe wa mwanaume mwingine akiwa na mkewe wakizungumza.
Sikujua walikuwa wakizungumza nini na wale watu. Nilirudi nje haraka ili wasinione, wakati huo nao walionekana wanatoka, niliwachungulia kupitia kwenye tundu la mlangoni na kuona wote wakiingia kwenye gari zao ili waondoke.
Nilimuona mlinzi akisogea mlangoni kufungua geti, nilijificha nyuma ya mti uliokuwepo pale. Baada ya muda gari zilitoka na kuelekea mjini. Pamoja na kuyaona yale yote bado sikujua nini kinaendelea.
Magari yalipotoka na geti kufungwa nilisogea getini ili kutaka kujua zaidi ya ile nyumba yangu. Niligonga geti na mlinzi alitoka na kuniuliza:
“Nikusaidie nini dada, kama kazi sasa hivi hakuna nyumba imemalizika. “
“Sina shida hiyo.”
“Una shida gani?”
“Samahani kaka una muda gani hapa?”
“Una maanisha kuwepo hapa kivipi?”
“Kikazi.”
“Huu mwezi wa pili, kwani vipi?” mlinzi alionesha kunishangaa.
“Ndiyo maana unifahamu.”
“Kwani wewe nani?”
“Mimi...”
Nilianza kujitambulisha kwa kifupi.
“Sasa mbona sijawahi kukuona pia nyumba hii ni ya mkewe mzee Sambi.”
“Ndiyo wanavyosema?” niliuliza macho yamenitoka pima.
“Ndiyo, muda wote ulikuwa wapi?”
“Nilikuwa naumwa.”
“Mmh! Pole sana, kwa kweli siwezi kuchangia chochote labda muonane na mzee.”
“Sawa, na wale watu wamekuja kufanya nini?”
“Ni wapangaji ambao nielezwa wanaingia wiki ijayo.”
“Mmh! Asante.”
“Pole sana dada yangu kama unayosema ni kweli, siamini kama mzee yule anaweza kukufanyia ubaya huo. Basi hata ugonjwa wako naamini mkewe anahusika.”
“Kaka yangu wacha niende.”
“Lakini kama una hati za kiwanja utapata haki yako.”
“Aliichukua.”
“Basi nenda mahakamani nina imani utetezi wako utakusaidia kupata haki yako.”
Japokuwa maneno ya yule kaka yalikuwa yana ushauri mzuri, lakini muda ule yalikuwa yakinivuruga. Niliondoka bila kumuaga na kuelekea zangu barabara ambako nilichukua daladala hadi Mwenge kisha nilipanda za Tandika mpaka nyumbani.
Njia nzima sikupata jibu kuhusu mzee Sambi kwenda na mkewe kwenye nyumba yangu. Kilichonishtua zaidi kusikia ile nyumba ni ya mke wa mzee Sambi. Moyo uliniuma na kutokwa machozi njia nzima mtandio haukucheza mbali na uso wangu kwa ajili ya kufuta machozi.
Nilipofika nyumba nilikwenda chumbani kwangu na kuendelea kulia mpaka kichwa kikaniuma na kumuona mzee Sambi ni muuaji asiye na huruma.
Nilijiuliza kama matatizo ya ugonjwa yaliyotaka kuchukua uhai wangu sababu ni mkewe. Baada ya kuamini siponi alinikimbia bila kujua hatma yangu. Nilishindwa nifanye nini kwani kichwa kiliniuma sana kama kinataka kupasuka.
Mama baada ya kugundua hali yangu alinifuata ndani na kutaka kujua nina tatizo gani.
Sikuwa na jinsi nilimueleza yote niliyokutana nayo siku ile, japokuwa alinikataza kufuatilia chochote kwa mzee Sambi.
“Mwaija mbona mwanangu umekuwa na masikio magumu, nimekueleza achana na kila kitu chake, Una shida gani toka alipokukimbia?”
“Sina mama lakini roho inaniuma ile ilikuwa tayari nyumba yangu.”
“Kama haki yako utaipata kwa njia nyingine mwache kama anajifanya mjanja.”
“Kwa hiyo nifanye nini?”
“Achana naye, jipange kwa maisha mapya.”
Nilikubaliana na mama japokuwa moyo ulikuwa ukiniuma sana kwa unyama alionifanyia mzee Sambi na kuamua kumuachia Mungu.
Siku iliyofuata niliamua kwenda kwa mama Amina ili kumuomba anieleze matatizo yangu kinagaubaga na kumuomba asinifiche hata kitu moja.
Kama kawaida nilipofika nilikuta wagonjwa wengi, baada ya kunisalimia aliendelea na kazi zake. Baada ya saa moja aliniita ndani, nilipoingia na kukaa kwenye mkeka kwanza aliniuliza hali yangu.
“Namshukuru Mungu naweza kusema sasa nimepona.”
“Kazi imebakia moja kuhakikisha nasafisha ndoa yako, kwa vile nyota yako bado ipo juu nina hakika kwa uwezo wa Mungu mambo yako yatakuwa vizuri muda si mrefu.”
“Nashukuru sana mama Amina, ila nilikuwa na ombi moja.”
“Lipi hilo?”
“Kuhusu kufanana kwa matukio yangu.”
“Matukio gani?”
“Ya kuondokewa na wapenzi wangu bila kuelezwa tatizo, naomba leo unieleze kinagaubaga hata kama mama yangu anahusika naomba uniweke wazi nifahamu kisha tujue tufanye nini.”
“Mwaija mambo mengine hayatakiwi kuchambuliwa, kwa vile tatizo lako limekwisha angalia maisha yako yaliyopita achana nayo.”
“Hapana mama Amina huu utakuwa mchezo wa kuigiza, Naweza kupata mwanaume mwingine mambo yakawa yaleyale.”
“Nakuhakikishia matatizo yaliyo tokea hayatatokea tena.”
“Kivipi?”
“Tatizo lililokuwepo nimeishalimaliza japokuwa ilikuwa kazi nzito.”
“Unaweza kuniambia nani aliyefanya mchezo huu?”
“Wapo wawili, mmoja mke wa huyu mzee, na mwingine nina imani naye ameachana na mchezo huu,” mama Amina alinificha.
“Nani mama?”
“Hapana.”
“Sasa nani?”
“Shida yako kupona au kumjua huyo mtu?”
“Vyote.”
“Naomba basi nisikilize, acha kuchimbua vilivyopita. Mshukuru Mungu kukuponya.”
Sikutaka kumchimbua sana na kujikuta mawazo yangu nikihamishia kwa mama. Lakini wazo hilo nilipingana nalo kutokana jinsi mama alivyopigania maisha yangu.
Nilijiuliza atakuwa nani au dada mkubwa niliyemchukulia mpenzi wake. Lakini kama dada angekuwa amefanya vile alikuwa ananionea kwa vile tulikubaliana.
Hata wazo hilo bado sikukubaliana nalo kutokana na matatizo ya awali kunitokea nikiwa ndani ya ndoa yangu. Swali likabakia ni nani aliyenifanyia vile, kwa nini mama Amina hakuniambia kama alivyonieleza ya mke wa mzee Sambi?
Swali lile liliniumiza kichwa, sikutaka kumuuliza sana kwani ningemuuzdhi na kuonesha sina adabu kama makosa niliyofanya mwanzo. Wasiwasi wangu kutokea tatizo lingine na mama Amina kugoma kunisaidia kwa vile si msikivu.
Mama Amina alinipatia dawa za kuoga na makombe ya kunywa. Baada ya zoezi la mwisho alinieleza nifanye chochote bila tatizo. Nilirudi zangu nyumbani kichwa kikiwa kizito cha kujiuliza kwa nini mtu huyo hatakiwi kutajwa, ni nani?
Nilipanda gari la Mbande Tandika na kuteremkia Tandika. Kwa vile kulikuwa na njia ya mkato sikutaka kupanda usafiri wowote nilikatiza kwenda nyumbani.
Nilikuwa navuka barabara ya Devis Kona, nilisikia jina langu linaitwa.
“Mwaija.”
Sikuitika mpaka nilipogeuka na kumuona aliyekuwa akiniita. Alikuwa kaka mmoja tuliyekuwa tukikaa mtaa mmoja siku za nyuma, alikuwa kwenye gari.
“Abee,” niliitika na kugeuka kumsikiliza.
“Unatoka wapi?”
“Mbagala.”
“Kwema?”
“Kwema.”
“Kwa vile naelekea maeneo ya kwenu naomba nikusogeze.”
“Acha tu nitafika.”
“Hapana Mwaija nafika karibia na kwenu ingia twende.”
Sikutaka kuwa mbishi nilifungua mlango wa gari na kuingia. Baada ya kuondoka na tuliporibia Transfoma alinisemesha.
“Leo nina bahati ya kuonana na wewe.”
“Bahati ipi Juma?” nilimuuliza huku nikimtazama.
“Kwanza pole.”
“Asante,” nilimjibu kwa mkato.
“Nimekufuatilia muda mrefu.”
“Kuhusu nini?” nilimkata kauli.
“Subiri basi.”
“Haya endelea.”
“Mwaija kama usingeolewa na Beka ningekuoa mimi.”
“Kivipi?”
“Nilikupenda muda mrefu, huwezi kuamini kila hatua yako niliifuatilia mpaka mlipoachana na Beka. Wakati najiandaa kuja kwenu nilipata safari ya ghafla.
“Niliporudi nilikuta unaumwa sana, bado nikakufuatilia. Leo hii ninaweza kusema hii ni nafasi yangu.”
“Nafasi gani?”
“Ya kutuma maombi ya kukuoa.”
“Juma naomba sasa hivi suala ya mapenzi tuachane nalo.”
“Kwa sababu gani?”
“Nahitaji kupumzika, mapenzi yamesababisha nichungulie kaburi.”
“Bila matatizo hayo ungekuwa tayari?”
“Ndiyo kwa vile heshima ya mwanamke ni ndoa.”
“Kwa nini usinipe nafasi hiyo?”
“Labda baadaye, lakini sasa hivi nahitaji mapumziko ya muda mrefu, kwa sasa nayachukia mapenzi kuliko kitu chochote.”
“Kwa hiyo utakuwa tayari lini?”
“Niache kwanza.”
Juma alinifikisha nyumbani na kuniacha huku akiniomba awe sehemu ya mawazo yangu ya kila siku. Nilimkubalia ili aniache nipumzike kwa vile bado mbaya wangu aliendelea kuwa siri iliyonitesa sana.
Baada ya kufika nyumbani niliendelea kutumia dawa nilizopewa na mama Amina huku ombi la Juma likiwa halipo akilini mwangu.
Lakini kumbe mwenzangu ilikuwa tofauti, kumbe aliendelea kunifuatilia kwa karibu. Baada ya wiki mbili kukatika, mama aliniita na kunipa taarifa ya kujitokeza mtu wa kutaka kunioa ambaye ni Juma.
“Mama naomba suala hilo tuachane nalo kwa sasa.”
“Hapana mwanangu nakuomba ukubaliane nalo.”
“Mama nimechoka kila siku miye tu.”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Mapenzi yamekuwa mateso na kutishia uhai wangu kila siku.”
“Sasa hivi hayatatokea tena.”
“Kwa nini unasema hivyo?”
“Mimi najua, naomba unisikilize mimi mama yako.”
“Mmh! Sawa mama kwa vile nakupenda sana pia umenipigania maisha yangu kwa nguvu zako zote.”
“Nimefurahi mwanangu kunisikiliza mama yako.”
Nilikubaliana na mama kukubali kuolewa, huku nikishangaa mama yangu kuwa mbele katika kukubali kuolewa kwangu tofauti na siku za nyuma.
Majibu yalirudi kuwa nimekubali, mipango ya ndoa ilianza mara moja. Taarifa ile nilimweleza mama Amina na da’ Suzy wote waliniunga mkono uamuzi wa kukubali kuolewa tena.
Namshukuru Mungu nilipata ushirikiano wa hali na mali kwa familia, muda wote mpaka wakati wa ndoa yangu.
Niliolewa na Juma