Simulizi: Namchukia Mama Yangu

Sehemu ya 26

Namshukuru Mungu nilipata ushirikiano wa hali na mali kwa familia, muda wote mpaka wakati wa ndoa yangu.
Niliolewa na Juma, mfanyabiashara wa maduka ya nguo na vyombo vya umeme Kariakoo aliyekuwa amejenga Kibamba.

Namshukuru Mungu baada ya ndoa nilimuweka wazi mume wangu juu maisha yangu niliyopitia na umuhimu na mama Amina kwangu.

Hakuwa na tatizo alinipa ushirikiano ikiwa pamoja na kumualika mama Amina kwetu japokuwa kwenye harusi yangu alihudhuria na kunipa ushirikiano mkubwa sana.

Kuna kitu kimoja kilinifurahisha mama Amina japo mganga wa jadi alikuwa alikuwa wamo.
Akiamua kujilipua na pamba huwezi kuamini kama ni yeye anayevaa kaniki wakati wa kutibu.

Siku ya harusi nilimsahau nilivyolipuka na migold iliyomchafua kichwani mpaka mikononi. Alikuwa mganga wa kileo anayekwenda na wakati.

Namshukuru Mungu maisha ya ndoa yalikwenda vizuri baada ya muda nilishika ujauzito. Mama Amina aliufunga ili nisiupoteze tena.

Mungu alijalia nilijifungua salama mtoto wa kike mwenye afya njema. Kwa kweli maisha niliyoishi na mume wangu yalinikumbusha mbali huku wasiwasi wangu ukiwa ni kutokea yaliyotokea mwanzo.

Nilikuwa na furaha na malezi mazuri ya mume wangu pamoja na familia yangu kwa ujumla ilikuwa karibu. Lakini nilipokumbuka maisha ya zamani na misukosuko moyo ulikosa raha.
Nakumbuka vizuri siku moja nikiwa Kariakoo karibu na kituo cha Msimbazi Big Bon kituo cha mafuta niliguswa bega na mtu.

Nilipogeuka nilikutana na mtalaka wangu Beka.
“Mwaija,” aliniita akionesha kunishangaa.
“Abee.”

Japokuwa nilimpenda kuliko mwanaume yeyote lakini kitendo alichonifanyia sikumchangamkia nilimuona mtu wa kawaida.
“Za siku?”

“Nzuri.”
“Umeolewa?” aliniuliza baada ya kuona pete ya ndoa kidoleni.

“Uliponiacha ulitegemea siolewi tena?” nilijikuta nikizungumza huku nimebinua midomo japokuwa sikukipenda kitu kile katika maisha yangu.

“Mwaija bila vile ningebakia jina,” Beka alisema kwa sauti ya majonzi.
“Si nilikuuliza nani anataka kukubakiza jina huniambii ikabakia siri yako na familia yako huku ukitaka kunigombanisha na mama yangu.”

“Samahani naomba tutafute sehemu nzuri tuzungumze vizuri.”
“Leo ndiyo unaweza kumsema?” nilimuuliza nimemkazia macho.

“Kama mpaka leo hujui tatizo lazima nikueleze huenda likaiokoa ndoa yako ya sasa.”

Kauli ile ilinifanya niwe na hamu ya kumsikiliza. Tulisogea kwenye mgahawa uliokuwa karibu na kutafuta meza ya pembeni.

Baada ya kukaa tuliagiza vinywaji, nilitulia kumsikiliza Beka mtalaka wangu bwana na mwanaume wa usichana wangu ambaye alionekana maisha si mabaya.

“Mwaija najua unaweza kunichukia na kuniona adui yako kutokana na kushindwa kusema ukweli. Lakini nilifanya hivyo kulinda amani iliyo ndani ya familia yenu.

“Nina imani mama yako unampenda sana na unamuamini kwa kila kitu?”

“Ndiyo.”
“Ni vigumu kuamini mama yako ndiye aliyekuwa adui yako namba moja.”
“Etiii!?” nilishtuka kusikia vile.

“Ndiyo maana sikutaka kuyasema hayo kipindi kile kwa vile tungeweza kupotea wote kabla siri haijatoka nje.”
“Una maana gani?” sikumuelewa alimaanisha nini.

“Mwaija nina imani unanijua vizuri kuliko mtu yeyote?”
“Ndiyo.”
“Na maisha yangu unayajua vizuri?”
“Ndiyo.”

“Baada ya ndoa yetu kupigwa mizengwe na wewe kusimama kidete, mwisho tulifanikiwa kuoana. Namshukuru baada ya ndoa maisha yalikuwa mazuri sana, mpaka tukanunua kiwanja na kuanza ujenzi.”

“Ni kweli.”
“Tatizo lilianza baada ya kubeba ujauzito uongo kweli?”
“Ni kweli.”

“Na ujauzito wako ulitoka katika mazingira ya utatanishi?”
“Ni kweli kabisa.”
“Na baada ya hapo ndipo mikosi na mabalaa yalipoanza mpaka nikakosa hata kazi na wewe ni shahidi ulifuata fedha kwenu.”
“Ndiyo.”

“Kwa kweli sikujua chochote kuhusiana na matatizo yale kwa kuamini ni mipango ya Mungu. Lakini nilishikwa mkono na rafiki yangu aliyeshangazwa na anguko langu la ghafla na kunipelekwa kwa mtaalamu Handeni Tanga.

“Nilipofika huko niliyosikia kwanza sikuamini, niliamini mganga ni muongo. Alinieleza mambo mengi kuhusiana na matatizo yangu mpaka ya ndani ya familia yako.”

“Eeh!” nilishtuka kusikia vile.
“Eeh! Ndiyo, alisema chanzo ni mama yenu ndiye aliyefanya mambo ya kishirikina ikiwa ni kukutega mlangoni uliporuka ujauzito ukatoka kisha akaanza kuniwangia mpaka mambo yangu yakawa hayaeleweki.

“Alikwenda kwenye kiwanja na kuifunga nyumba yetu iliyokuwa kwenye hali nzuri ili tusiendelee huku akifunga riziki kila kona. Baada ya kuona pamoja na hali ya maisha kuwa mbaya lakini hutaki kuachana na mimi. Alianza kuitafuta roho yangu kuhakikisha ananitenganisha na wewe.

“Ilionesha hata kama ningekueleza usingekubali kitu ambacho kingefanya nipoteze maisha kwa vile alikuwa na nafasi ya kuja kwetu angenimaliza kwa urahisi.

“Japokuwa maneno ya mganga yalikuwa yakifanana na kweli, bado sikukubaliana naye kwa kuamini kauli ile ni ya uchonganishi ambayo ndicho chanzo cha vitabu vya dini kuikataa ramli.

“Ukweli kuamini moja kwa moja nilishindwa wala kukueleza jambo zito kama lile ambalo lazima lingeleta mpasuko. Nilimueleza mganga jinsi mama mkwe alivyonisaidia mpaka hata kupata nauli ya kwenda kule.

“Alinieleza kama siwezi kukueleza basi niachane na wewe. Ilikuwa vigumu kukubali kuachana na wewe mke wangu kipenzi ambaye naamini mpaka nakufa sitapata mwingine kama wewe.

“Mwaija hata sijui kwa nini nilichukua uamuzi huo heri ningesema mapema kwa jinsi ulivyokuwa ukinipenda ungeweza kunisikiliza, lakini wasiwasi wangu ndiyo ulionifanya nilie kila siku kukumbuka mke wangu mpenzi.

“Basi mganga alinieleza nichague moja katika matatu. Nikueleze ubaya wa mama yako, kama nikishindwa nikuache huku nikikueleza kila kitu anajua mama yako na kama ungemwambia angeujua ubaya wake au vyote vikishindikana nikubali kufa.”

Maneno ya Beka yalinisisimua mwili na kuanza kuamini yote aliyosema hasa baada ya mama Amina kukataa kunitajia mbaya wangu. Niliendelea kumsikiliza mtalaka wangu huku mapigo ya moyo yakinienda kasi.

“Kwa kweli bado sikuwa tayari lakini
alinichambulia moja baada ya lingine kama ameniumba yeye, hata sababu ya dada zako kuachika na kutokuwa na wazo la kuolewa tena.

Kama mtu akitokea anataka kuoa basi hugeuka ugomvi na kumfukuza kama mbwa.”
Maneno yale yalikuwa na ukweli kwa sababu dada alimfukuza mzee Sambi baada ya kumtaka kumuoa.

“Basi alinipa mtihani mmoja ili kuhakikisha anachosema ni kweli, aliniambia angenipa kitu ambacho ningekuja nacho kwenu. Mama yako angeniona angeanguka.

Alinieleza baada ya tukio lile nilitakiwa nikuache na kuondoka haraka kama ningeendelea kuwepo kwenu mama yako angekufa.”

“Ni kwa nini?” niliuliza mkono shavuni.
“Kwa sababu ya ubaya wake.”
“Unafikiri kwa nini amekuwa na tabia hiyo?” nilimuuliza swali ambalo nilitakiwa nilijibu mimi mwenyewe.

“Ni roho mbaya na kupenda kushiriki mambo ya kishirikina yamempelekea kupenda kucheza michezo ya kichawi.”

“Ehe, nini kuliendelea?”
“Kwanza nilikataa na kuamua kuachana na wazo hilo. Baada ya kubahatika kupata kazi katika mradi ya ujenzi barabara njia ya Tanga.

Nilifanya kazi kule kwa muda huku nikiwa na wazo la kutafuta njia mbadala tofauti na maelezo ya mganga.

“Lakini mganga alinieleza kama sijipendi nifanye kinyume na alivyonieleza. Baada ya kufanya kazi kwa muda nilipata nafasi ya kurudi nyumbani.

“Kabla ya kuja Dar nilirudi kwa mtaalamu ambaye alinieleza nifanye kama alivyonielekeza na kunieleza mambo nitakayoyakuta siku nitakayo kuja kwenu na hali itakayojitokeza.

Niliporudi Dar sikukaa nilikuja kwenu kila nilichoelezwa na mganga kilitokea ikiwa pamoja na mama yako kuanguka alipokuwa amekaa baada ya kushtuka kuniona.

“Kwa kweli tukio lile linifanya nichukue uamuzi mgumu wa kukupa talaka na kukuacha na fumbo kuhusiana na talaka yako.

“Niliamini mama yako angekueleza lakini hakukueleza, nilipo ondoka kwa kweli sikutaka kujua habari za nyuma. Leo unaponiona nina siku mbili na kesho naondoka kurudi nilipo, kwa yaliyonitokea nimejikuta sipendi tena kukaa jiji hili.”

Beka mpaka anamaliza kunielezea chanzo cha talaka yangu, macho yake yalikuwa yamejaa machozi. Si yeye hata mimi muda wote nilikuwa nalia huku nikitumia mtandio kujifuta machozi.

Nilijitahidi kuzungumza japokuwa moyo wangu ulikuwa kama umechubuliwa kovu lililoanza kupona na maumivu yake kuwa mara mbili.

“Beka nakubaliana na wewe kwa asilimia mia kuwa mama yangu anahusika, lakini bado hukutakiwa kuutesa moyo wangu kwa maswali yasiyo na majibu.

“Najua pengine mimi ndiye niliyesababisha kwa kutoa siri ya kipato chetu kwa mama. Lakini kwa vile ni mkeo ulitakiwa kuniweka wazi. Siamini kama kuna mwanadamu anaweza kuua bali kwa idhini ya Mungu.

Hata kwenye riziki anaweza kuichelewesha si kuizuia kabisa.

“Beka ungekuwa wazi ningejua nifanye nini, pengine ukimya wako umenifanya nichungulie kaburi au ningezikwa ningali hai.”
“Kwa nini?” Beka aliuliza macho yamemtoka pima.

Nilimueleza yote yaliyotokea baada ya kunipa talaka, maisha niliyoishi nakufika kuugua ugonjwa wa ajabu.
“Dah! Pole sana Mwaija, nina imani hata huyo bwana kuondoka kwake inawezekana mama yako kachangia.”

“Inawekana,” nilimkubalia.
“Lazima ujiulize kwa nini mtu akukimbie wakati wa matatizo?” aliniuliza.
“Beka nashukuru kwa maelezo yako ambayo naamini yamechelewa kunifikia nina imani leo hii tungekuwa pamoja.”

“Ni kweli lakini sina wa kumlaumu bali wasiwasi wa nafsi yangu.”
“Beka naomba nikapumzike kwa vile sijisikii vizuri, pia mwanangu nimemwacha muda mrefu.”
“Ha! Mwaija una mtoto?” Beka alishtuka
Duhhh tamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sehemu ya 27

“Beka nashukuru kwa maelezo yako ambayo naamini yamechelewa kunifikia nina imani leo hii tungekuwa pamoja.”
“Ni kweli lakini sina wa kumlaumu bali wasiwasi wa nafsi yangu.”
“Beka naomba nikapumzike kwa vile sijisikii vizuri, pia mwanangu nimemwacha muda mrefu.”

“Ha! Mwaija una mtoto?” Beka alishtuka.
“Beka uliambiwa mi mgumba?”
“Mmh! Sawa,” Beka alishusha pumzi nzito na kuinamisha kichwa.

“Beka naomba niondoke, kwani hali yangu siielewi nahisi mapigo ya moyo kunienda kasi,” niliongea kwa shida kidogo.
“Hakuna tabu Mwaija kwa vile nina gari nitakupeleka.”

“Hapana Beka, nitakodi au nitamwita mume wangu anifuate.”
“Kwa nini usumbuke nitakupeleka mara moja, kwa hali hii siwezi kukuacha peke yako.”
“Hakuna tatizo.”

Ilibidi nikubali kwa vile sikuelewa baada ya muda hali yangu ingeendeleaje kama ningebaki peke yangu. Kila nilivyofikiria nilikosa jibu na kujikuta moyo ukiniuma kama unataka kutoka.

Beka alinipeleka mpaka kwangu kwani hata nguvu za kutembea sikuwa nazo. Nashukuru nilifika nyumbani salama na kuagana na Beka huku tukipeana namba za simu kwa kuendelea kusalimiana kama marafiki si wapenzi tena.

Nilipofika ndani hali ilizidi kuwa mbaya, kila nilipoyakumbuka yote na siri iliyokuwa imefichwa. Kumbe mama yangu ndiye adui yangu.

Kichwa kiliniuma mapigo ya moyo yalinienda kwa kasi, nilimwambia msichana wa kazi amjulishe mume wangu kwa vile hata uwezo wa kupiga simu sikuwa nao.

Mume wangu baada ya kupewa taarifa alifika mara moja na kunikimbiza hospitali. Presha ilikutwa ipo juu sana na kuwafanya madaktari kupata kazi ya kuishusha.

Walifanikiwa kuishusha baada ya saa mbili ndipo nilipotapa usingizi mpaka asubuhi. Taarifa zilimfikia mama ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika hospitali na kufuatiwa na dada zangu.

Siri ya matatizo yangu sikumueleza mume wangu, alijua ni matatizo ya kawaida japokuwa hali ile haikuwahi kunitokea toka aliponioa. Mama naye alishangaa na kutaka kujua presha ile imesababishwa na nini.
Nilishindwa kumueleza ukweli, nilisingizia imetokea ghafla japokuwa mama alikataa katakata maelezo yangu.

“Hapana Mwaija maelezo aliyonipa mumeo lazima kuna kitu mnanificha wewe na mumeo. Hebu niambie mama nini kimekusibu? Madaktari wanasema presha ile ingeweza kukupofua macho au kupooza mwili ilikuwa juu sana.”

“Hata sijui nimejisikia tu mwili ukikosa nguvu na kumpigia simu mume wangu ambaye alinieleta hapa,” bado niliificha siri ile sikutaka kuisema.

“Mwaija mi mtu mzima maisha ya ndoa nayajua, kama kuna kitu mumeo amekuudhi niambie ili tujue tufanye nini, sitaki yatokee ya mzee Sambi.”

“Haki ya Mungu, kuhusu mume wangu utamuonea. Ananitunza kama malkia, hajawahi hata kunikemea toka anioe na ananipenda mapenzi ya dhati.”

“Sasa tatizo nini?”
“Mama ni hali umenitokea tu hata sielewi, pengi mawazo ya kutaka kuzikwa ningali hai kila nikikumbuka moyo unipaa,” nilitengeneza uongo uliomfanya mama aamini.

“Lakini mwanangu mambo hayo si yameisha isha sasa hivi una ndoa yako nzuri pia una mtoto mambo ambayo awali yalishindikana. Hebu achana nayo ili kuondoa kuishi kwa wasiwasi.”
“Sawa mama nimekuelewa nitajitahidi kusahau.”

“Itabidi ufanyiwe na kisomo ’dua’.”
“Hakuna tatizo.”
Kila alilokuwa akilifanya mama na maneno aliyokuwa akiniambia yenye faraja kwangu yaliufanya moyo wangu ilizidi kuwa njia panda kutoamini aliyefanya ubaya ni yeye.

Niliamini lile lilikuwa fumbo zito ambalo alilifahamu mama Amina pekee ambaye alikuwa na majibu ya maswali yangu.
Nilipanga nikitoka hospitali na kutulia nitamfungia safari na kumfuata ili anieleze ukweli, nilikuwa radhi kumpa kiasi chochote akitakacho ili tu anieleze ukweli.

Baada ya hali yangu kuwa nzuri niliruhusiwa na kurudi nyumbani. Mume wangu naye alitaka kujua sababu ya tatizo lile kama sababu ni yeye. Naye nilimdanganya sababu ile ilitokana na kukumbuka hali iliyonitokea nyuma.

Alinisihi nisiwaze vitu vilivyopita kwa vile ananitunza kama mboni ya jicho lake. Nilimhakikishia hali ile haitajitokeza tena, maneno yangu yalimfariji sana mume wangu na kurudisha tabasamu lililopotea baada ya kuwa na wasiwasi wa tatizo langu kalisababisha yeye.

Nilijitahidi kuwa katika hali ya kawaida ili niweze kuwatoa wasiwasi wote na kunipa nafasi ya kuweza kwenda kwa mama Amina. Siku zilikatika nikiwa katika hali ya kawaida.
Baada ya wote kuamini nipo sawa nilifunga safari hadi kwa mama Amina kutaka kupata ukweli. Aliponiona alifurahi kuniona nikiwa katika afya njema huku mwili wangu ukiwa umerudi kama zamani.

Kwa vile nilikuta watu wengi wakisubiri huduma nami nilikaa kusubiri. Baada ya muda niliitwa ndani, niliingia na kwenda kukaa kwenye mkeka.

“Mwaija naona leo mdogo wangu umenitembelea, vipi familia yako?”
“Namshukuru Mungu haijambo.”
“Una habari gani?”
“Mama Amina naomba msaada wako ambao ni muhimu kuliko kitu chochote.”
“Msaada gani?”

“Kuna jambo umekuwa ukinificha kwa nini usinieleze ili nimjue mbaya wangu?”
“Mwaija, mbaya wako wa nini, tatizo limekwisha unataka kuchimbua nini?”
“Mama Amina ukweli nimeujua lakini nataka msaada wako ili yasijetokea tena.”

“Ukweli gani?”
Nilimweleza yote niliyoelezwa na Beka kuhusu mama ambayo yalikuwa na ukweli asilimia kubwa. Maelezo yangu yalimshangaza sana mama Amina ambaye aliamini pengine nilichokisema nisingekijua.
Baada ya kumshusha pumzi ndefu mama Amina alisema:

“Unayosema ni kweli lakini hakukuwa na umuhimu wa kukueleza kwa vile mbaya wako alijisalimisha na kuzivunja nguvu zake, hivyo hakuwa na madhara tena.”

“Lakini aliyefanya vile ni mama yangu?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni.
“Ndiyo, lakini sasa hivi hana ubaya wowote baada ya kukubali kuzivunja nguvu zake za kishirikina.”

“Hizo nguvu zake zimevunjwa wapi?”
“Hapahapa kwangu.”
“Ilikuwaje mpaka akakubali zikavunja hizo nguvu zake?”

“Baada ya tatizo lako kupelekwa kwa mtaalamu wake ambaye kama angeweza kulitatua tatizo la mke wa bwana uliyekuwa naye basi siri hii ingeendelea kuitafuna familia yenu.

“Lakini Mungu naye ana mambo yake, baada ya kushindikana na wewe kuzidiwa sana na kuletwa kwangu. Hakuwa na jinsi ilibidi ajivue nguo ili kuokoa maisha yako.

Kabla ya kuanza kukuhudumia ilipoangalia niliyaona madudu yake. Kutokana na matatizo yako kuwa ya muda mrefu nisingeweza kukutibu juujuu bila kuanza kungoa mzizi. Hakukuwa na njia nyingine kuvunja nguvu za mama ili niweze kukupata vizuri.

“Ilikuwa kazi kubwa, lakini kutokana na hali yako ilivyokuwa na kumuhakikishia utapona alikubali. Basi nikavunja nguzo zote alizo kuwa nazo na kumsafisha kisha nilikawaosha na dada zako wote.”

“Mama alisema alifanya vile kwa ajili gani?”
“Basi tu alipenda kushiriki mambo ya kishirikina ambayo sitakueleza kwa vile si sehemu yake zaidi ya kukueleza yanayokuhusu.

“Ukiingia katika mchezo ule uchelewi kujiunga kwenye chama cha waharibifu, si wachawi bali wanaozunguka kwa wanganga kuharibu maisha ya watu kama kuwaharibia watu kwenye kazi au kuharibu ujaumzito wa mtu kwa wivu tu wa kijinga.”

“Ina maana kuna watu wengine wanaendelea na mchezo ule aliokuwa nao mama?”
“Ndiyo, tena baada ya kujitoa watamsumbua sana. Juzi tu nimemtoa kitu kizito waliomtupia washirika wake kwa sababu ya kujitoa kwenye chama chao.”
“Mmh! Kwa hiyo sasa hivi mama hajihusishi na mchezo huo?”

“Umegundua mabadiliko gani kwenye familia yako ambayo siku za nyuma hayakuwepo?”
“Kuna tofauti kubwa sana, sasa hivi mama swala tano.”
“Basi shukuru Mungu mama yako amerudi kwenye mstari sahihi.”

“Nakubaliana na wewe kuna mambo mengi yamebadirika kwa sasa, dada wa kati sasa hivi anafanya kazi tofauti na zamani alikuwa mtu wa starehe na kushinda nyumbani tu. Kingine nimeambiwa na mama kuwa dada mkubwa amepata mchumba.”

“Tatizo lilikuwa kwenye vifungo lakini baada kuvifungua na kuondolewa nuksi kila mmoja mambo yake yamenyokea na dada yako anayetaka kuolewa ni mjamzito kwa sasa.”
“Uniambie!” nilishtuka kusikia vile.

“Kila kitu sasa hivi tambalale mengine yakija itakuwa ni kudra ya Mungu si mkono wa mtu.”
“Nashukuru kwa maelezo yako pia nashukuru kwa kumuokoa mama yetu toka kwenye kundi baya.”

“Ndiyo kazi yetu kuona tunatumia fani yetu kutengeneza si kuharibu. Kuna kitu kimoja kinamuumiza mama yako kuhusiana na aliyoyafanya kwa kweli kinakosesha raha nimejitahidi sana kumtuliza.

“Mama yenu anajua humjui chochote na hataki mjue alifanya nini. Nina imani akijua umefahamu ataumia mara mbili.”
“Nataka kumweleza mama ukweli japokuwa sina ujasiri huo.”

“Nakushauri ungeachana nayo kwa vile umeelewa nawe umekuwa tayari kumsamehe.”
“Sawa, nimemsamehe mama kwa vile nampenda sana.”

Baada ya maelezo ya mama Amina nilirudi nyumbani kwangu nikiwa kidogo na afadhali baada kuutua mzigo mzito ulionisumbua. Lakini nilijiuliza kwa nini nisimueleze ili ajua nini alichotufanyia wanaye.

Kutokana na maelezo ya mama Amina jinsi mama yangu anavyoumizwa na matendo yake nilishindwa kumweleza nakuamua kumsamehe kwa vile tayari alikuwa amerudi kwa mola wake.

Sio siri mama yangu nilikuwa nampenda sana kwa malezi yake. Nilishtuka sana kusikia ndiye aliyekuwa adui yangu mkubwa. Lakini nilifarijika baada ya kujirudi na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaye tunaishi katika mstari mzuri baada ya kupotea.
***
Siku zilikatika nikiwa na siri yangu moyoni huku nilijitahidi kuyasahau yote yaliyotokea. Nilijikuta nikimpenda zaidi mama yangu pamoja na yote aliyonitendea.

Kila nilipokumbuka aliyonitokea, nilijifungia ndani na kulia huku nikizidi kumuombea kwa Mungu amsamehe mama yangu.

Niliwaza sana kuhusu siri ile kuwambia dada zangu, bado nafsi ilinisuta kwani niliamini kuwaeleza wasiyo yajua ni sawa na kumvua nguo mama yangu.

Mama alibadilika sana baada ya kuanza kuswali na kuachana na pombe alikuwa mpole mtu mwenye mawazo sana kila alipokuwa peke yake.

Dada zangu walinishangaa hali ya mama kurudi katika ibada kuacha pombe na tabia zote mbaya. Alikuwa mkali kwa mambo machafu na kuwaeleza waige mfano wangu wa kuolewa na si kuzini ovyo.

CD za taarabu alipiga marufuku nyumba yetu kwa kweli ilipoa na kuwashangaza majirani kwani sauti za muziki siku za nyuma zilikuwa juu na kuwakera.

Lakini mabadiliko ya mama yaliwashangaza na kufanya nyumba yetu irudishe heshima ya wakati wa uhai wa marehemu baba.

Taarifa zilizotoka kwa dada zangu zilisema mama amebadilika sana hakai tena sebuleni kama zamani muda mwingi baada ya kusali aliingia chumbani na kukaa peke yake muda mwingi na alipotoka alionesha kuvimba macho akionesha alikuwa akilia.

Japokuwa mabadiliko yale yalikuwa mazuri, lakini hali ya mama ya kokosa raha kushinda chumbani peke yake hata sisi wanae tulikosa raha
 
Ndugu mwandishi riwaya yako ipo vizuri Sana Ila sidhani km ni busara kuweka bandiko hapa mpk usujudiwe au ulambwe miguu...

Unaweka kiepisode kimoja mpk pale ujisikie ndo uweke nyingine....km ulidhamiria kushare na Sisi basi usitupe manyanyaso hvyo...weka mzigo wa kutosha angalau tukate kiu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hana kazi nyingine za kufanya,?

Aiseeee acha ninyamaze tu mkuu hii story mimi nailipia ninapoitoa halafu mimi sio mtunzi ninapoitoa mwenyewe anapost hivihivi

Haulaizimishwi kusoma unaweza acha tu
 
Kunamajitu Humu Yanakera Sana! Kwahio Unataka Mleta Stori Ashinde Nakukesha Jf Akikuridhisa Wewe? Unadhan Hana Kaz Zakufanya?
Hata Kama Akileta Epsode 1/wiki
Ninafac Yake! Hana Hasara Hata Akiacha! Sasa Unapo Mlaumu Unashangaza Sana. Kama Vepe Anzisha Nawewe Uwe Unashinda Jf! Tumbaf Sana
 
Imekukera Sana eee! Kuliko muhusika mwenyewe....kunya boga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamevurugwa...sijui wakukurupuka?

Hivi huwa hasomi au haelewi siku zote unasema kuwa na wewe unanunua na kuweka kwa ikhsani tu?
Any way...
Shukran sana ..
Aiseeee acha ninyamaze tu mkuu hii story mimi nailipia ninapoitoa halafu mimi sio mtunzi ninapoitoa mwenyewe anapost hivihivi

Haulaizimishwi kusoma unaweza acha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom