MZIMU ULIOREJEA
Sehemu -39 & 40
Ilipoishia................................
............
Baada ya Martin kuweka simu ile sikioni,akapiga namba zile alizoachiwa na kamishna!,
akapewa maelezo mahali muhusika anapopatikana...
Jb akaingia katika gari lake,kuelekea sehemu ile...
ni kwa mganga bi nwalau nwalau...
#Endelea......
Kilikuwa ni kijumba kidogo!,ambacho ndani ndo aliishi bibi nwalau nwalau....
Bibi huyo akiwa katika kilinge chake alikuwa akicheza,upepo ulivuma kidogo katika kijumba chake kile...
Tayari alishahisi juu ya ujio wa wageni,au mgeni aliyekuwa akija...
Mganga Nwalau nwalau akazidi kucheza!
,hata Martin alipofika,katika kijumba kile kilichozungushi
wa vitambaa vyekundu alinyooshewa ishara tu aketi uku mbibi yule akiendelea kupiga manyanga sambamba na kucheza!.
"hahahaha!,karibu baba hapa ndo kwa bi nwalau nwalau sema tawile! kama niongeacho ni sahii na kama si sahihi kataa"
martin akatingisha kichwa ishara ya kukubali! bibi mganga nwalau nwalau ambaye pia alishiriki katika story ya nakupenda nasra aliyemuumba nasra jini mvaa gauni jekundu(soma riwaya hiyo) nadhani wengi mtakuwa mnamfahamu!.
ghafla akanyamaza kimya na kuketi akakunja miguu! akachukua mbegu flan nyekundu na kuzitingisha akazibwaga chini! mbegu zile zikatawanyika! akaachia kicheko
"umefika!, maisha yako yapo hatarini!,na tangu ulipotoka kwenu kuja huku mizimu ya babu yang iitwayo kilembwembwe imekulinda usingefika salama
unasumbuliwa na mzimu!, pepo chafu lililotoka makaburini na linakutesa sana!
wakati ulipopata wazo la kuja tu alitaka kukuteketeza ila alitokewa na kilembwembwe wangu akamzuia
Martin akashtuka kuskia vile,akauamini uwezo wa bibi yule...japo maelezo Yale akuyaelewa elewa
"tawile bibi!" Ikabidi aitikie...
Bibi akaendelea...
"mzimu ule ni wa jb aliyekuwa rafiki yako!,kipenz kwa nini ulimuua?"
"nitamaha tu babu nsaidie nimekoma!"
bibi nwalau nwalau akaachia kicheko na kuimba kidogo!,
"wewe ndo umeutenda vibaya u mzimu unajua kwa nini umekuacha mpaka saivi ukiwa hai?! hali ya kuwa wewe ndo muhusika mkuu?"
Martin akatingisha kichwa ishara ya kukataa!
",kuna siri kubwa na lazima tuijue."
"mimi nnachotaka tu unsaidie tusisumbuliwe na ikiwezekana ukiangamize."
bibi yule akacheka tena! na kupiga manyanga,
"mizimu kilembwembwe inataka sadaka! ,tena sadaka ya damu,
damu ya mama yako!
uinywe na nyingine ndo itolewe kama kafara! mzimu ule sasa umejificha na ukifanya hivyo utashikwa na hasira utatoka ukitoka tu mizimu yangu inammaliza."
martin akuamin amuue mama yake?! kwa mara ya kwanza akapakumbuka nyumbani tangu ameondoka hakuwah kurudi...
kumbukumb zake zikarudi nyuma miaka mingi ilopita.
MIAKA 35 NYUMA!
"mdogo wangu usilie! haya yote ni maisha yatapita tu!,kijana mmoja alo onekana mkubwa,mwenye miaka 12 alimbembeleza mdogo wake! ambaye alikuwa na miaka 7 walikuwa katikati ya pori wakikata kuni!"
"yani kama tukitoka hapa tukafue sisi tupike sisi!, shambani sisi mama anaridhika au siyo mama yetu yule?
"hapana mdogo wangu Martin yule ni mama yetu anatupenda sana ila tatizo ni kwa baba yetu ndo anatupa kazi hizi mama awezi ingilia kwa sababu atapigwa! au wewe upo tayari mama apigwe?!"
kijana yule akamuuliza mdogo wake,ambaye alitingisha kichwa kukataa mama yake kupigwa!
"bas kama haupo tazar tuvumilie tu mdogo wangu!"
akamalizia kijana yule aitwaye BRAYSON akamtwisha mdogo wake mzigo mdogo wa kuni wakaondoka!,kue
lekea nyumbani
hayo ndo yalikuwa maisha yao,waliyolazimika kuyazoea
Bryson na Martin walikuwa ni watoto wa bi veriana, bi veriana alikuwa na watoto wa tano wawili baba yao alishakufa, na hao wa tatu mmoja alikuwa mtoto wake alomzaa na huyo mwanaume wawili wakiwa wa huyo baba alozaa na wanawake wa nje!
akawaleta nyumbani
wote walikuwa wa kiume
mzee yule aliwapenda wanae hao wa tatu ila hao wawil wa mkewe aliwachukia
kazi zote wenyewe ndo walifanya ,ila walivumilia mwisho uvumilivu ukawashinda!
siku hiyo ilikuwa hivi!....
Bryson alikuwa shambani akilima ,mdogo wake martin alimwacha nyumbani akicheza na watoto wenzake,
watoto wale wakawa wanacheza mchezo wa mawe, kwa kudhamiria mtoto mmoja akaokota jiwe na kumtandika nalo martin jiwe la mgongoni,
akampasua na damu zikaanza kuchurizika kama bomba la maji!,
bryson kuja akukubali akamvamia yule mtoto alompiga mdogo wake na kuanza kumshambulia, mpaka akamzimisha
bray akajua lazima ameua!
akaamua akimbie kijiji kile!, akiazimia kutokurudi tena huku akimwacha mdogo wake katika mateso makali.
ila hakuwa na budi kupasahau nyumbani! na kweli akapasahau,
akavuka mito,mabonde milima,toka SINGIDA akaja kuishia ARUSHA! mgodin..
Akiwa na miaka ile ile 14,akaanza kufanya kazi za nguvu, Kusaga mawe,
kupeta mchanga, mpaka kuchimba madini na kupasua miamba alipofika kule ili kuogopa kujulikana akabadilisha jina kutoka BRYSON mpaka JACOB au jb!...
na upande wa pili! Martin baada ya kaka yake bray kukimbia, baba yake wa kambo alipokuja! na kuambiwa mwanaye kapigwa mpaka kufikia kuzimia kisa martin hasira zikampanda akampiga martin,na akazidi kumtesa!,
martin akaona sotusheni atoroke akamsake kaka ake bry!, maskin laiti angejua?!!
sijui nini kiliendelea je martin atafanikiwa kumpata kaka yake bry(jb) kumbuka hii ni kumbukumbu anayekumbuka martin akiwa kwa mganga.na kumbuka martin ajui kama jb ni kaka yake
#No_40
Ilipoishia........................
..........
Martin baada ya kaka yake Bray kukimbia, baba yake wa kambo alipokuja! Na kuambiwa mwanaye kapigwa mpaka kufikia kuzimia kisa Martin hasira zikampanda akampiga Martin sambamba na kumzidishia mateso makali...
Martin akaona solution atoroke akamsake kaka yake BRY (JB)!,maskin laiti angejua?!!!......
Songa nayo.....
Njia nzima Nurdin alijawa na wasiwasi,hasa kwa kuwa akujua sehemu anapoelekea,ila aliona afadhali ateseke mtahani,kuliko mateso ya kule nyumbani!,japo akuwa hata na senti tano lakin aliadhimia kusafiri!
Siku ya siku iliwadia,akafanikiwa kutoroka nyumbani,akiwa amependeza,akakaa kwenye siti na safari ikaanza!,pembeni yake aliketi mmama wa makamo ambaye alikuwa amembeba mtoto,baada ya mwendo kidogo wakiwa katikati ya pori kondakta akaanza kupitia tiketi!,kwa kuwa nurdin akuwa nayo alikiegemeza kichwa chake katika magoti yake,ni wazi alikuwa mbali kimawazo!...
kondakta yule alimfikia na kumshtua akiitaji tiketi! martin akamwambia wazi kuwa ana!,kondakta yule akasimamisha gari kwa lengo la kumshusha palepale!
"wew kaka kuwa na huruma sasa ukimshushia hapa porini ataendea wapi? au unataka aliwe na wanyama wa kali?"
dada yule alokuwa kambeba mtoto aliongea,akimwa
ngalia kondakta yule!
"hapana sistar hawa ndo wanaenda jijini kuwa majambazi!,jua hii ni kazi mbaya zaidi kakalia siti!...oya dogo shuka bhana kabla sijakupa kelbu!"
"ngoja! kwanza!..." yule dada akamzuia Nurdin kushuka akafungua pochi yake na kutoa hela akamkabidhi kondakta
"mambo sindo hayo bhana!" konda akajibu tabasamu likiupendezesha uso wake,akaruka siti ile na kuelekea siti za nyuma!
"asante sana dada yangu!,MUNGU atakulipa kwa wema wako sina cha kukulipa mimi!" aliongea Martin huku akilia! dada yule alimuonea huruma akaanza kumbembeleza...
"usilie mdogo wangu!,yameisha we dar unaenda kwa nani?!"
"Naenda kumtafuta kaka yangu!..."
"unajua mahali alipo!"
Nurdin akatingisha kichwa ishara ya kukataa dada yule alimsikitikia sana
"Basi utaenda kukaa kwangu kipindi ambacho unamtafuta kaka yako! kwani tofauti na ivyo utakuwa mtoto wa mtahani!"
Martin alifurahi kuskia vile!,uzuni yote ikatoweka,furaha ikatawala!,aliuona mwangaza wa maisha yake mapya
************************************
Hatimaye mida ya mchana wakaingia katika jiji lile!,jiji lenye shamrashamra,na pilika pilika za hapa na pale!
kama kawaida ya mgeni pindi afikapo eneo ambalo ni geni kwake kushangaa shangaa,hata kwa Nurdin ilikuwa ivyo hivyo!
alilishangaa jiji lile,wakaingia katika basi la tmk na safari nyingine ikaanza!
mara kadhaa wakikutana na "jam" barabarani zilizowachelewesha!
Hatimaye safari yao ikafika mwisho,katika maeneo ya uswazi!...
"we malaya! naona umeamua kwenda kunletea mtoto wako huko shambani kwenu!"
ndivyo walivyopokelewa na baba mwenye nyumba ile!
"siyo hivyo mume wangu,baada ya kunkaribisha na kuniuliza habari za safari unaanza manen...."
"kimya wew mwanamke! sina haja ya kujua hayo naondoka nkirudi nisikikute icho kimdoli chako."
Baada ya jamaa yule kumaliza maneno yale,akafungua mlango na kutoka!
"usijali mwanangu! utayazoea maisha haya,we kaoge ntakuonesha mahali upumzike!"
"ahsante mama!" wote wawili wakanyanyuka na dada yule akaenda kumuonesha Nurdin bafuni,Akaoga na alipotoka akaoneshwa chumba chake akajilaza,kutokana na uchovu kijana yule akukawia kupitiwa na usingizi!
alikuja kuzinduka,njaa ilikuwa ikilishambulia tumbo lake!
akajinyanyua na kukaa! ghafla akaskia kicheko,mara vicheko na sauti ya mama yake yule alomsaidia akiongea!,
akapiga mwayo mrefu na kujinyanyua!,akaelekea sebuleni alipomkuta mama yule na wasichana wengine wawili walofanana kila kitu rika lake wakiwa wanaangalia tv!
Akupata tabu kung'amua kuwa wale ni mapacha
"umeamka mwanangu?!"
dada yule akamshtua kwa sauti
"ndiyo mama!"
"ok njoo nkutambulishe dada zako!,unakumbuka nlikwambia mimi nawatoto wawili mapacha? basi ndo hawa hapa huyu mkubwa kurwa anaitwa Janeth na huyu mdogo ake anaitwa Jenipha wapo kidato cha tatu"
"nashkuru kuwafahamu mama!"
akaitika martin akicheka!
Alistaajabishwa na jinsi walivyofanana
"janeth na jenipha huyu ni kaka yenu anaitwa Nurdin atakuwa hapa nyumbani mkisaidiana kazi mpeni ushirikiano"
"Sawa mama ndo house boy?" janeth akauliza akimwangalia kwa dharau!
"si house boy ni kaka yenu!"
"mbona ukutuambia kama una mtoto mama?" Jenipha naye akadakia!
"muulizeni mama yenu labda nyie atawaskia! nilimwambia si mtaki huyo mtoto! hapa"
Wote wakashtuka na kuangalia sauti ilipotokea
Ndiyo alikuwa Yule yule mume wake,kijana aliye jaa jazba,hasira na wivu teke
"Huyu mtoto hawezi kwenda popote!"
Mama Janeth akaongea kwa hasira
"Kama Mimi ni mume wako lazima aondoke"
"Utanipiga utaniua lakini huyu mtoto aondoki hapaa"
mama janeth akazidi kuweka Ngumu akikimbilia chumbani,mume wake akamfata kwa hasira baada ya dakika chache kilio cha mama janeth kikasikika akiomba msaada,mume wake alikuwa akimpiga...
"Watu wengine bwana mpaka mnasababisha matatizo katika nyumba za watu utakiwi bado unang'ang'ania si uondoke?!"
Janeth akazidi kumsakama,Nurdin
Kijana yule akupenda kusakamwa,alipenda familia ile iishi kwa amani ghafla wazo la kuondoka likamjia akajinyanyua na kukimbilia ndani akaanza kukusanya kila kilicho chake
Ila ghafla,....
Nini tena?! Nini kiliendelea
Itaendelea...