Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,926
- Thread starter
- #61
Sehemu ya 38
“Sijambo.” Mtoto wa kike nilijibu nikiwa sijiwezi kabisa mbele ya mwanaume yule. Sauti yangu niliitolea puani ili kumvutia mwanaume yule.
Kwa kweli Mr macho makubwa alikuwa ni kiboko yangu. Siku hiyo likuwa amevaa vizuri tofauti na alivyokuwa jana yake.
Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya kisasa, T’shart nyeupe ya Von dutch iliyomkaa vizuri. Chini alikuwa na raba kali ya bei mbaya.
“Hivi jina lako huwa unaitwa nani?” Mr macho makubwa akaniuliza.
“Naitwa Sofia. Wewe je?”
“Mimi naitwa...” kabla hajajibu mara akatokeza mwanamke mmoja nyuma yake, akamshika bega.
“MAMBO Victor,”mwanamke yule alimsalimu huku akimwangalia usoni kwa macho malegevu mkono wake ukiwa begani kwa mvulana huyo.
Sasa kupitia yule mwanamke, nilitambua kumbe Mr Macho makubwa anaitwa Victor. Walisalimiana na mwanamke yule kwa uchangamfu mkubwa.
Kwa kumwangalia mara moja tu mwanamke yule, nikabaini ni moja ya wanawake waliokubuhu kwa ushangingi mjini.
Asije tu kunipora mwanaume wangu huyu. Niliwaza.
Nilikuwa na wivu na Victor japokuwa hatukuwa tumeingia kwenye uhusiano wa kimapenzi. Siku hiyo ilikuwa ni siku ya kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu na handsome boy huyo.
Upendo wangu kwakwe nisingeweza tena kuuficha. Nilikuwa tayari kuonekana wa hovyo mbele yake, lakini tu atambue kwamba nampenda.
Mapenzi kikohozi. Kuficha huwezi.
Baada ya kumaliza kusalimiana na jana jike lile, Victor alirudisha macho kwangu.
“Nani yule?” nilihoji, nilishindwa kabisa kuficha wivu usoni mwangu. “Mshikaji tu.”alijibu.
Ukimya mfupi ulipita kati yetu. Nilinyanya glasi ya kinywaji na kupiga fundo moja refu, lile donge kavu lililotokana na wivu nikahisi linayeyuka na kupotelea tumboni.
“Kumbe wewe unaitwa Victor!” nilianzisha mazungumzo upya.
“Aagh! Yes naitwa Victor.”
“Mbona leo hujakwenda kazini Victor?”
“Leo ni siku yangu ya off.”
“Kumbe leo upo Off. Ndio maana sikukuona,” “Kwani ulikwenda Maktaba?”
“Ndio Victor. Nilikwenda kwa ajili ya kukuona wewe tu.” Nilimwambia.
Akatabasamu, tabasamu lake ndio huwa linanimaliza kabisa mtoto wa kike.
Nikamuuliza tena.
“Unaishi wapi Victor?”