Sehemu ya 40
Kwa masaa machache niliyokutana na Victor, a.k.a Mr Macho makubwa, nilijikuta nikifurahia mno maisha, nilitamani mwanaume huyo awe wangu peke yangu maisha yangu yote.
Baada ya kuchoka kuchezea majini, tulitoka ndani ya bahari na kurudi chumbani kuvaa nguo zetu. Wakati huo ilikuwa yaelekea magharibi.
Jua la jioni lilikuwa linaishilizia na kuacha mwanga wa manjano katika bahari.Upepo na baridi ukawa unavuma kwa kasi kuja pwani, nikawa natetemeka hadi meno yanagongana.
Victor akanisogelea na kunikumbatia, joto la mwili wake likanipa raha ya aina yake, nikatamani anikumbatie muda wote bila kuniacha.
“Pole kwa baridi mrembo, nadhani tuondoke sasa.” Victor alisema.
Nilikosa raha, hadi wakati huo hatukuwa kwenye makabaliano au mazungumzo yoyote ya kuingia katika uhusiano wa kimapenzi.
Kauli ya kuondoka, ilininyima raha, bado kuna kitu nilikuwa nakihitaji kwa mwanaume huyo, kauli yake ya ‘tuondoke’ ilinikosesha amani ya roho.
“Vipi mbona umekosa raha.”
“Sitaki uniache Victor, nakupenda.”
nilijikuta naropoka.
Victor akaningalia usoni bila kusema kitu, angalia yake ikanitia haya, nikashindwa kabisa kumtizama usoni. Sijui alinifikiriaje kwa kujilipua kule.
“Umekuja na gari lako?” aliniuliza.
Nikashindwa kuelewa gari langu linaingiliana vipi na kauli niliyomwambia. Hata hivyo ningefanya nini? Nilikwisha kuwa sijiwezi mbele ya mwanaume huyo. Nilitikisa kichwa kumkubalia.
“Twende.”
Nilitembea nikiwa sijielewi, nilikuwa nimeghafirika vibaya sana, asikwambie mtu hakuna jambo gumu kwa mwanamke wa kiafrika kama kumtongoza mwanaume.
Nilikuwa kama kondoo kwa mwanaume huyo, nilitii kila asemacho, mapenzi yalizidi nguvu ya utashi wangu.
Tuliingia ndani ya gari langu. Bila kujua mwanaume huyo alilenga nini hasa kwa kutaka tuingie garini.
Baada ya kufunga milango tu. Ghafla. Victor alinirukia kama fisi mwenye njaa, akanivutia kwakwe kisha akaninyonya ulimi wangu a.k.a denda.
Kufumba na kufumbua akaanza kunivua nguo zangu.
“Victor kwenye gari!!” nilisema nikiwa sijui kama natakiwa nimkubalie ama nimkatalie.
VICTOR hakujibu, alikazana kuifungua zipu ya sketi yangu kwa pupa. Pumzi zilikuwa zikimtoka kwa kasi kama mwanariadha wa mbio za marathoni.