JC umeyatimba ndugu yangu jiandae kupakiwa mkongo mzee babaMIMI NA MIMI 2
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI NA TANO
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Baada ya Miryam kwenda tu ofisini kwake na kujifungia, nikageuka zangu na kuanza kuondoka hapo ili nirudi tu Mzinga. Ingawa nilikuwa nimetoka kumfunulia mwanamke niliyempenda hisia zangu, bado nilikuwa na mtihani kwake wa kuhakikisha nafaulu kumshawishi azikubali, kwa sababu sikutaka 'hapana' yake moja tu imaanishe ndiyo nimempoteza. Yaani sikuwa tayari kwa ajili ya hilo. Ningefanya kila kitu kuhakikisha Miryam anakubali kwamba ana hisia kwangu pia.
Ingeweza kuonekana kwamba najipa moyo bure tu, lakini hapana, hisia zake kwangu ni kitu ambacho nilihisi pia. Kuna nyakati tulikuwa tunakaa, tunaongea kidogo, tunataniana kidogo, na mara nyingi angeniangalia kwa njia iliyoonyesha hisia nyingi kwangu. Hata maisha yake yalipotishiwa ile juzi, alionekana kujali hali yangu zaidi ya yakwake, kitu ambacho hakingewezekana endapo kama tu angekuwa ananiona kuwa "mdogo" wake wa kawaida. Hayo yalikuwa maneno ya kujihami tu.
Kuna sababu iliyomfanya asitake kukubali kuwa mimi ningeweza kumpenda yeye, huenda akidhani nilitaka tu kumchezea, ama labda aliniona kuwa mdogo mno kwake, bado hakujiona kuwa tayari kuwa na mtu kimahusiano. Kwa vyovyote vile, nilitakiwa kumfungua macho, aachane na mitazamo ya namna hiyo, na aone kwamba upendo wangu kwake ulikuwa wa kweli. Kwa hiyo nisingemwacha, hata kama angesema ama kufanya nini.
Bwana, nikawa nimeamua kupanda bajaji na kuelekea mpaka Zakhem, na baada ya kushuka, nikaendelea kutembea taratibu kuelekea kule kwenye daladala ili nipande tena, na ndiyo nikawa nimepigiwa simu na mama yangu. Nilipenda kuzungumza na mama katika hali tulivu, kwa hiyo sikupokea kwanza shauri ya kuwa barabarani nikipishana na makelele kama yote. Nikaamua kugeuza tena, nikarudi mpaka kwenye mgahawa maridadi wa Zakhem, nami nikatafuta sehemu ya mbele huko na kukaa.
Mhudumu aliponifata, nikamwambia tu aniletee 'milkshake' moja nipoze koo, naye akasepa. Ndiyo nikampigia mama sasa, yaani yeye alikuwa wa kunipigia mara moja, akinikosa, anaacha; labda kama kungekuwa na tatizo kubwa. Kwa hiyo nikampigia zamu hii, na alipopokea tukasalimiana vizuri na yeye kunijulia hali.
"Niko poa tu ma. Jasmine anaendelea vizuri?" nikamuuliza.
"Eeeh. Yupo tu. Ukuje bwana, tumeku-miss," akasema hivyo.
"Nitakuja. Hii hii wiki au ijayo," nikamwambia hivyo.
"Sawa. Nilikupigia kukuuliza kitu. Nasikia eti umetoa... yaani umelipa milioni kumi leo kwenye kampuni, kufidishia hela za mtu fulani aliyekuwa anadaiwa. Ni kweli?" akauliza.
"Mhm... ni mzee amekwambia?"
"Hapana, nina watu wa kunipa taarifa. Na hilo siyo la muhimu..."
"Well... yeah. Ndiyo mama, ni kweli. Nimetoa hiyo fidia," nikamwambia.
"Umetoa milioni hizo zote kwa ajili ya nani J?"
"Ni msichana fulani wa huku. Ni mgonjwa wangu. Nilipokwambiaga kuna mtu namsaidia huku, ndiyo huyo msichana sasa," nikamwambia.
"Mpaka milioni kumi? Ni... anaumwa sana, au? Yaani... Frank alikuwa anamdai hizo hela ndiyo ukaona umtolee?"
"Ni mambo mengi mama. Sijui hata nianzie wapi kuelezea," nikasema hivyo.
"Nieleweshe tu hata kwa ufupi. Napenda tu kujua kwa nini umefanya hivyo, siyo kawaida sana," akaniambia hivyo kwa upole.
Milkshake yangu ikawa imeletwa hatimaye, na mhudumu akasepa.
Nikashusha pumzi kiasi na kusema, "Mama... yaani nimefanya hivyo kiukweli kwa sababu... huyu msichana amenikumbusha mengi ambayo wewe ulipitia. Toka nimeanza kumsaidia, nimemwona kama wewe kabisa... jinsi ulivyoteseka kipindi kile... yaani... ni kama vile yeye tu alivyoteseka sasa...."
"Okay..."
"Sijui ni-delve zaidi ndani kwenye detail..."
"Hapana, Jayden, inatosha. Usijali. Nimekuelewa," akaniambia hivyo kwa upole.
"Yeah, ndiyo hivyo. Ila siyo kwamba namlinganisha na wewe, lakini... yeye na familia yake kwa ujumla... ni watu ambao nimetokea kuwapenda, na kuwajali sana," nikamwambia hivyo.
"Anaitwa nani?" akauliza.
"Mariam," nikamjibu.
"Na, ni mkubwa? Ukisema msichana, ni kwamba ni mwanamke tayari au...."
"Ni mdada, mdogo. Alikuwa na tatizo, matatizo... kwenye ubongo. Matatizo hayo ubongo ndiyo yalimfanya awe kama mtoto, so... nimejitahidi kumsaidia mpaka sasa angalau anaendelea vizuri," nikamwelezea.
"Amepitia hali ngumu?"
"Mno. Kiumri Nuru hajamwacha sana, ila alikuwa na behavior za mtoto mdogo shauri ya hili tatizo tunaita ASD. Ana kaka yake, alikuwa anataka kumwibia yeye na ndugu zake mali zao... hapo juzi akamteka na kupanga kumuua ili afanikiwe kufanya hayo yote. Tulimkuta akiwa karibu sana kubakwa na kuchinjwa mama, na hana kosa lolote kabisa, she's so innocent..." nikamwambia hayo.
Akasema, "Masikini! Ah... pole kwake. Imenigusa sana kujua umetoa msaada kwa mtu namna hiyo yaani, sijui kama Jasmine anaweza kufanya hivyo..."
"Ahah, piga, ua, galagaza..."
"Ahahahah... una moyo mzuri Jayden. Umenifurahisha sana. Basi, mwanzoni nikafikiri labda umetoa na mahali huko bila sisi kujua..." akasema hivyo.
"Ahahah... hapana. Ya mahali lazima mjue, na muda bado," nikamwambia hivyo.
"Sawa. Nimeelewa. Haya, me acha nikuage sasa. Halafu... umepanga kuja lini kabisa?" akauliza.
"Mmm... nimefikiria nije labda Jumapili, au Jumatatu kama Jumapili haitawezekana," nikamwambia hivyo.
"Sawa, ila ndiyo utaniambia kwa uhakika. Vipi ukija naye?" mama akasema hivyo.
"Nini? Nani?" nikamuuliza.
"Huyo Mariam. Ukija, kama utaweza njoo naye nimwone," akaniambia hivyo.
Nikatabasamu kwa hisia na kusema, "Sawa. Nitajitahidi kuja naye."
"Haya. Uwe care huko eh? Tutawasiliana," akaniaga.
"Poa, usisahau kunifinyia shavu la huyo kibonge," nikamwambia hivyo kiutani.
"Hahah... haya sawa."
Hapo ndiyo nikakata simu na kuanza kushusha kinywaji changu taratibu.
Nilifurahia sana hayo maongezi na mama yangu, si unajua jinsi uvutano uliopo kati ya mama na mwana unavyokuwaga wa hali ya juu? Ndivyo ilivyokuwa na huyu mzazi wangu. Sehemu kubwa ya utu wangu mzuri nilikuwa naitoa kwake, na nilipenda sana aliposema kuwa alitaka kumwona Mariam, hivyo ningehitaji kufanikisha hilo kwa kumpeleka binti nyumbani ili ajuane na watu wa familia yangu. Kidogo kidogo tu, ingeanza na Mariam, na hatimaye ingekuja kumfikia bibie Miryam mwenyewe.
★★
Nilipomaliza kinywaji changu, tayari usiku ulikuwa umeshaingia, na baada ya kulipa ndiyo nikaondoka kuelekea Mzinga. Katika hali yangu ya kuwa na mawazo mengi, nikawa nimeamua kufanya zoezi la kutembea mpaka Mzinga badala ya kupanda usafiri, maana sikuhisi uhitaji wa kuingia gym leo. Nigepumzika kidogo. Kwa hiyo taratibu tu nikajongea kutoka hayo maeneo ya Rangi Tatu mpaka nikafika Mzinga ikiwa imeshaingia saa mbili usiku, nami nikaelekea makwetu moja kwa moja.
Nilipofika upande wa nje wa nyumba yake Ankia, nikaweza kuona familia ya Miryam ikiwa imekaa pale varandani, yaani wote walikuwa nje, nami nikaamua kwenda kuwasalimia tena kabla sijarudi huku kuoga. Nilipoingia hapo getini kwao, gari la bibie lilikuwemo, na Miryam mwenyewe alikuwa pamoja na familia yake hapo nje. Alikuwa amesharudi. Ni yeye pekee na Tesha ndiyo waliokuwa wamekaa kwenye viti, huku wakina Bi Zawadi, Bi Jamila, Mariam, pamoja na Shadya, wakiwa wamekaa mkekani kwenye uvaranda.
Mariam kama kawaida yake akanyanyuka na kuja kukutana nami ili kunikumbatia, nami sikumnyima hilo. Nilipomwangalia Miryam, alikuwa ameketi kitini huku akiwa makini kweli na simu yake, kama mtu asiyejali ujio wa mgeni yaani, na nilielewa kwangu mimi ingekuwa namna hiyo kutokea hapa na kuelekea mbele. Alikuwa amevaa dera zuri sana la njano mwenyewe, Mariam akiwa amevaa dera pia, nami nikasogea mpaka hapo varandani pamoja na binti na kusalimiana na wengine pia.
Tesha akataka anipishe ili niketi kitini, lakini nikamwambia hakukuwa na uhitaji kwa sababu nilitaka kwenda kujisafisha mwili kwanza, kwa hiyo yeye akae tu. Nilisemeshana na wengine kwa njia ya uchangamfu sana, lakini Miryam alionekana kutotaka kujihusisha na hayo maongezi kabisa. Hakutaka kabisa mazoea na mimi tena. Nilikuwa namwangalia mara kwa mara, yeye asiniangalie hata mara moja, kisha akanyanyuka na kuelekea ndani.
Nikawekwa wazi kwamba Miryam alikuwa anawarekebishia wengine msosi huko ndani, wakisema aliwahi kurudi hiyo jioni, na mimi nikaona niwaage sasa ili niende tu pale kwa Ankia kuuweka mwili sawa. Lakini kabla sijaondoka, bibie Miryam akawa ametokezea hapo mlangoni na kusimama, naye akanitazama usoni moja kwa moja.
Alionekana kuwa makini tu, naye akasema, "Njoo mara moja."
Alikuwa ananiambia mimi hivyo. Kabla hata sijaongea lolote, akarudi ndani, na kiukweli alifanya mapigo yangu ya moyo yakimbie kwa kasi kiasi kwa sababu ya kutojua la kutarajia litokee huko. Alikuwa ananiitia nini huyo? Siyo 'kumchum kumchum' kweli? Nikajitahidi tu kuonyesha niko kawaida, nami nikawaacha wengine hapo na kuingia sebuleni.
Hakuwepo hapo sebuleni, lakini nikaweza kumwona upande wa kule jikoni akiwa kama amesimama usawa wa jiko lao la umeme/gesi anakoroga mambo. Kisha, akafanya kama kuja huku, lakini akaishia hapo kwenye ukuta uliotenganisha sebule na upande huo, na alisimama huku akiniangalia kwa macho makini. Ikawa wazi kuwa alitaka nimfate, labda tuongee bila wengine kuweza kusikia, nami nikajituliza tu kihisia na kumsogelea.
Akarudi nyuma kidogo ili ukuta huo utufiche kiasi, yaani kama vile alikuwa anataka tunong'onezane sijui? Na kiukweli nilikuwa na misisimko ya hali ya juu. Nikasimama mbele yake huku nikimwangalia kwa utulivu, naye akanyanyua mkono wake mmoja juu kiasi. Nikaona ulikuwa umeshika bahasha ndogo iliyokunjwa, nami nikamtazama machoni tena.
Akiwa bado ameinyanyua bahasha hiyo, akasema kwa sauti ya chini, "Hii hapa... milioni tano na laki nane. Natanguliza, nyingine inayobaki nitamalizia. Shika."
Nikabaki nikimtazama machoni kama vile sikuwa nimemwelewa.
Akakichukua kiganja changu na kujaribu kulazimisha kunishikisha hiyo bahasha, lakini nikagoma na kuutoa mkono wangu kwake kwa nguvu. Akanitazama usoni kimaswali, na kwa njia ya kuudhika.
"Unaanza tena kurudi kule kule ulikotoka Miryam," nikamwambia hivyo kwa sauti ya chini.
"Nini?" akauliza.
"Kale kakiburi kako kale... umeanza kukarudisha tena, kisa tu hutaki kukubaliana na nilichosema leo..." nikamwambia hivyo kwa utulivu.
"Sitaki kukubaliana na lolote wala kusikiliza mahubiri yako kwa...."
"Si kwa sababu unajua ni kweli?" nikamkatisha.
Akatulia na kuendelea kunitazama, eti kwa hasira.
"Ni part ipi ya maneno 'sihitaji unilipe' ambayo huelewi, hm?" nikamuuliza hivyo.
"Sijali maneno yako. Nairudisha pesa yote uliyotoa, kwa sababu...."
"Kwa sababu hutaki kuwa na deni kwangu? Ahah... Miryam, hata ufanye nini, huwezi kulipia deni ulilonalo kwangu kwa pesa," nikamwambia hivyo.
Akakunja uso wake kimaswali kiasi.
"Unajifanya hujui?" nikamuuliza.
Akaendelea kunikazia macho.
"Hizo pesa zimeshaenda, Miryam. Deni ulilonalo wewe kwangu, halihusiani kwa vyovyote na hizo hela. Ninachokudai wewe... ni kukiri kwamba unanipenda pia," nikamwambia hivyo kwa ujasiri.
Akaniangalia kama vile mimi ni mtu niliyechanganyikiwa, na kwa sauti ya chini akasema, "Una wazimu wewe!"
"Yeah. Nina wazimu juu yako," nikasema hivyo.
Akasonya kidogo na kutazama pembeni.
Nikatabasamu kiasi na kumwambia, "Najua kuna sehemu ya moyo wako inayoelewa kwamba huo ni ukweli. Najua unanipenda Miryam."
Akaniangalia kiukali na kusema, "Mimi? Mimi nakupenda wewe?!"
"Ndiyo. Ila bado tu hujatambua hilo," nikasema hivyo.
Akaonekana kutaka kusema kitu fulani kwa hasira, lakini akajizuia. Sijui alikuwa anataka kunitukana?
Kwa sauti tulivu, nikamwambia, "Nimegundua kwamba kukufanya utambue hilo ndiyo itakuwa challenge. Ila kwangu mimi. Nilikuwa nimeshaona upendo wako kwangu Miryam, lakini kwa sababu ya haya matatizo na nini... najua ulikuwa umefunikwa mbali sana kutoka kwenye macho yako, ndiyo sababu mpaka sasa hivi wewe hujauona bado. Lakini upo. Mie nimeshauona kwa upande wangu, na we' nitakusaidia uuone pia."
Alikuwa akiniangalia kwa hisia kali yaani, huku mimi nikimtazama kwa yale macho yangu mazuri, naye akasema, "Unajua... nilikuwa nimeanza kufikiri uko sensible, lakini... yaani... bado sana. Unanifanya natamani hata nikuwashe kofi!"
"Oh, please do!" nikamwambia hivyo na kumsogelea zaidi.
Akarudi nyuma kidogo huku akinitazama kimshangao kiasi.
"Sikukwambiaga kipindi kile uliponizibua, ila kofi lako liliacha mark nzuri sana kwangu. Siyo kwenye shavu... moyoni. Ama hujui? Kofi la mpenzi haliumi, ni tamu," nikamwambia hivyo kiuchokozi.
Midomo yake ikatetemeka kiasi huku akiibana kwa njia iliyoonyesha hasira, kisha kwa kunong'oneza akasema kwa ukali, "Mjinga wewe!"
Akanipita upesi na kuanza kuelekea upande wa chumba chake haraka-haraka, akionekana kukasirika mno, nami nikajikuta natabasamu tu na kushusha pumzi kujipa utulivu.
Huu mchezo haungekwenda kiulaini sana mwanzoni, najua, lakini nilijua pia kwamba ungefika tu muda ambao mwanamke huyo angelainika. Alama zote zilizoonyesha kwamba alikuwa ana hisia kwangu nilikuwa nimeshaziona huko nyuma, hata sasa zilikuwepo, kwa hiyo kazi ambayo ingebaki ingetakiwa kuwa kumfanya akiri kwamba alinipenda pia. Na ungekuwa mtihani.
Nikaamua tu kujiondokea hapo mapema kabla hajatoka na panga huko chumbani, nami nikawaaga wengine na kusema kama ningeweza basi hata baadaye ningekuja tena. Ndiyo nikaelekea kwa Ankia na kuoga, mwenye nyumba wangu huyo akiwa ndani tayari, kisha nikakaa pamoja naye sebuleni ili tupatane kwa mambo ya hapa na pale kabla ya mengine kufuata.
Inaonekana Ankia tayari alikuwa ameshatongozwa na Bobo, maana simu haikumshuka kiganjani kwa muda mrefu sana, akitabasamu-tabasamu na kuniangalia kwa sura yenye madaha. Nikamtania kwamba inawezekana siku si nyingi angenitambulisha kwa 'sugar daddy' wake mpya, naye akakataa kwa kusema eti alikuwa akichat na rafiki na kuangalia utani fulani huko Facebook.
Haya bwana, mimi nikatulia tu, lakini hakujua kwamba nilikuwa nafurahi sana kwa ajili yake, kuona jinsi ambavyo aliburudishwa na Bobo. Kidogo kidogo tu hivyo hivyo ningekuja kushtukia jamaa analetwa hapa kama faza hausi! Nikiwa nimeketi sofani bado pamoja naye, nikawa nimetumiwa ujumbe ulionifanya niwe makini zaidi. Ulitoka kwa askari Ramadhan, akiwa amenitumia maneno rahisi yaliyokuwa yamebeba maana nzito sana.
'Shukran kwa jitihada JC, Sodoma na Gomora zinaanguka. Kufikia asubuhi, kazi kwisha.'
Hiyo ilimaanisha kwamba sasa wakati ambao nilikuwa nimetazamia ufike ulikuwa umewadia, lakini ujumbe wake haukunipa hisia yoyote ya uchangamfu, bali nikahisi wasiwasi tena. Wasiwasi tu. Ikanibidi niende chumbani, nami nikampigia Ramadhan kwa namba yake ile ya siri, na uzuri akapokea.
Nikamwomba anipe ruhusa ya kufanya jambo fulani mapema sana ya kesho, na mwanzoni aliona ombi langu kuwa la kipuuzi na lisilofaa, lakini nikamshawishi aniruhusu tu, na mambo yangekwenda sawa. Akawa amenikubalia hatimaye kwa kusema ningefanya nilichotaka lakini kwa kufuata mwongozo wake, nami nikakubali hilo, kisha ndiyo akakata simu. Nikaamua kuahirisha kwenda kwake Miryam tena ili niweze kupumzika mapema, nami nikawahi kupanda kitandani huku nikiwaza mengi mazito mno ambayo yangetokea kwa siku ya kesho.
★★★
Asubuhi na mapema sana nikawa nimeamka, moja kwa moja nikaanza kujiandaa upesi ili niweze kuondoka. Yaani niliamka saa kumi na mbili leo, nikaoga, nikavaa, huyoo nikaondoka upesi. Safari ilikuwa ni moja tu; kwa madam Bertha. Kutokana na jambo aliloniambia askari Ramadhan jana, nilitaka tu kumwona huyo mwanamke, yaani... nimwone tu. Kisha mengine ambayo yangefuata, yangefuata.
Labda tuseme ni moyo ndiyo uliokuwa ukiniongoza kufanya hivi, maana akili yangu ilielewa vizuri kabisa kwamba sikutakiwa kufanya hivi. Kwa yale ambayo askari Ramadhan na watu wao wote wangehusika kufanya leo, najua nilipaswa kukaa mbali, lakini bado ni moyo tu ndiyo ukawa unanisukuma kutaka kuwa huko kwa huyo mwanamke kabla ya yaliyokuwa yakimjia kumfikia. Mtu hata angeweza kuniambia nina akili sita, na kwa wakati huu ningekubaliana na hilo na kumwambia sijali. Huu ndiyo ulikuwa uamuzi wangu.
Nikachukua usafiri kwenda Makumbusho moja kwa moja, nami nikafika huko Mkwajuni Vunja Bei ikiwa imeshaingia mida ya saa tatu asubuhi. Nilikuwa nimevaa kwa njia makini tu, na nilipoekekea huko hotelini nilitambua kwamba kulikuwa na mazingira fulani ya "utayari" yaliyokuwa yameshawekwa kuizunguka hoteli hiyo, kwa hiyo ni mimi tu ndiye niliyetakiwa kwenda huko juu, kumwona madam, kisha baada ya kumaliza biashara yangu nitoke ili kuyaacha hayo mazingira yafanye kazi yake. Ndiyo mwongozo wa kufata niliokuwa nimepewa na Ramadhan. Najua inaeleweka.
Nikapanda mpaka ghorofani huko, moja mbili tatu mpaka mlangoni kwa madam, nami nikagonga hodi na kungoja. Dakika kama mbili hivi zikapita, ndiyo mlango ukawa umefunguliwa, na hapo mbele yangu akawa amesimama madam Bertha mwenyewe. Alionekana makini kweli usoni kwa jinsi alivyokuwa akinitazama.
"JC?"
Akauliza hivyo kwa kuonekana kutotarajia iwe mimi niliyefika hapo kwa asubuhi hii. Alikuwa ndani ya ki-T-shirt chepesi cheupe, ambacho kilikuwa kifupi mno kuonyesha kitovu chake, na alivalia suruali ya michezo, pana kama zile za wahindi. Yaani alionekana kama dancer. Sijui kwa nini, lakini mkono wake mmoja ulikuwa nyuma ya kiuno chake kama vile ameficha kitu. Nikaendelea kumwangalia usoni.
Akauliza, "Unafanya nini hapa asubuhi yote hii?"
Nikiwa namtazama kwa utulivu tu, nikasema, "Nilitaka kukuona."
"Haujawahi kuniona?" akauliza hivyo.
"Kuwa pamoja nawe kabisa," nikamwambia hivyo kistaarabu.
Akaangalia pembeni na kutabasamu kiasi, kisha akasema, "We' umeamka nazo leo, eti? Na kazi je?"
Nikaendelea tu kumwangalia usoni kwa utulivu.
Akasonya kidogo kimasihara na kusema, "Hebu ingia huko."
Yaani hakuwa na habari!
Akarudi ndani, nami nikaingia pia na kufunga mlango. Sasa ndiyo nikaweza kuona kwamba kwenye mkono aliokuwa ameukunjia mgongoni alishikilia bastola, na nikaitambua kuwa ile bastola ambayo Festo alikuwa amenipa, ikionekana Dotto alimletea huku baada ya mauaji ya wakina Sudi, nami nikasimama kwanza na kumtazama tu mpaka alipogeuka na kuniangalia tena.
Akainyanyua hewani bastola hiyo na kusema, "Sipendi wageni wasio rasmi. Muhimu kuwa careful."
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
Akaishusha bastola na kusema, "Haka ka Taurus kazuri. Festus alikuuzia, au alikupa kishkaji tu?"
"Ali... alinigei tu," nikasema hivyo kwa sauti ya chini.
Akanitazama kwa udadisi kiasi, naye akauliza, "Mbona uko hivyo? Kuna tatizo?"
Nikatikisa kichwa kukanusha na kusema, "Niko poa. Kwa hiyo kama isingekuwa mimi na ni mtu usiyemjua, ungem-shoot tu?"
"Eeh, anakula chuma! Unafikiri naogopa visheria-sheria vya kipuuzi vya hoteli? Naweza tu kusema nilivamiwa, na nina haki ya kujilinda," akaniambia hivyo.
"Na haki ya kumiliki gun?"
"Ninayo. We' unanionaje?"
Nikanyoosha viganja juu kiasi kama kumwambia nimeshindwa.
Akasema, "Kaa hapo basi, tena ni vizuri Kantala wangu umejileta ili tuongee."
Nikajipeleka tu mpaka sofani na kukaa, naye akaiweka bastola yake juu ya droo la kitanda na kuja upande wangu.
"Nilikuwa na mpango wa kwenda Mbezi. Kuna spa fulani kule nzuri kichizi, nilikuwa nataka kung'arisha hii ngozi. Ishaanza kufanana na ya Zuchu," akasema hivyo.
Nikatabasamu kiasi na kumwangalia hadi alipofikia sofani na kukaa karibu yangu pia.
"Kama vipi twende wote," akaniambia hivyo.
"Unataka kwenda saa ngapi?"
"Sa'hivi."
"Asubuhi yote hii?"
"Yeah, asubuhi ndo' raha. Na tena... nimechelewa. Yaani hapa nitafika huko saa sita kabisa."
"Si bora tu uahirishe sasa?"
"A-ah, nimekwambia sina undugu na Zuchu..."
"Ahah... lakini si unapenda asubuhi? Ahirisha leo... utaenda siku nyingine..."
"Lini?" akauliza hivyo.
Nikatazama pembeni tu kwa utulivu. Swali lake likanifanya nijihisi vibaya moyoni.
Akaonekana kunitathmini kidogo, kisha akasema, "Hivi wewe... ni nini kwanza kimekuleta hapa... hm? Maana hadi umeanza kunizuia nisiende kupata some quality time kabisa. Nini kinakusumbua? Unataka mnyanduo, au.. unahofia kwa sababu naenda kufinywa-finywa kidogo na wanaume wenye mamisuli na nini eh... wanipakate-pakate kidogo, na madude yao makubwa-makubwa wayatelezeshe hapa weee... siyo kama hicho kiandunje chako?"
Nikajikuta natabasamu kwa furaha, utani wake ukiwa unamfanya apendeze kwa kiwango fulani machoni mwangu, nami nikamwangalia usoni kwa hisia.
"Ahahah... au uwongo?" akaniuliza hivyo.
"Ni kweli. Nahofia hicho," nikamwambia hivyo.
"Sa' si ndiyo maana nimekwambia twende wote? Au unafikiri me niko easy sana nitawaruhusu wanichezee tu?" akauliza.
"Hapana. Najua uko na msimamo," nikamwambia.
"Sasa je! Acha kufeli," akasema hivyo.
Nikatabasamu kiasi.
"Halafu kweli. Nilikuwa nataka nikwambie, ile hoteli ya kule Buza imepata mteja, kuna mtu ameinunua," akaniambia hivyo.
"Mh? Juzi tu mpaka leo tayari umeshaiuza?"
"Eeh. Hata hivyo, nilikuwa nimeshaiweka sokoni muda... na nimeiuza cheap tu. Nilikuwa nataka nikwambie mapema ili usijisikie vibaya, nimeiuza zawadi yako... lakini Masai ipo..."
"Ahah... hamna shida, me... hata hiyo siihitaji. Lakini... hizo pesa unafanyia nini sasa?"
Akatabasamu na kusema, "Unazitaka eti? Niambie kama unataka nikupe."
"Hamna, hiyo siyo maana yangu. Naona unakusanya pesa nyingi, umeshanunua na gari, nime... nimehisi kuna mabadiliko unataka... unataka kufanya," nikamwambia hivyo.
"Yeah. Haujakosea. Nafikiri sasa hivi natakiwa kuanza... au niseme, niendelee kusonga, lakini upya. Nataka niache kukaa hapa, nirudi kwenye nyumba yangu... hasa sasa hivi kwa sababu Chaz amekufa, na nataka niifanyie renovation kubwa sana. Iwe kama nimeijenga upya. Nataka... nifungue hoteli na club nyingine ya maana... hoteli kubwa three, au four, au five stars ikiwezekana. Ahah... five stars nimefikiria mbali sana, ila... nataka iwe kama fresh start..." akaongea hivyo kwa uhakika.
Nikabaki nikimtazama machoni kwa utulivu tu.
Akanishika mkono na kuniambia, "Tena... nataka iwe ni fresh start nikiwa pamoja na wewe, JC."
Dah!
Nikaangalia pembeni tu, yaani nikiwa nazidi kujihisi vibaya mno moyoni.
"Hey, usifikiri nina-bug hapa. I mean it. Sawa sitakuwa malaika na nini, lakini JC... nataka sasa hivi... moving forward, iwe ni mimi na...."
"Basi, Bertha... usiseme hivyo," nikamkatisha.
Akaniangalia kimaswali kiasi, nami nikamtazama usoni kwa umakini.
"Bertha... hhh... najua, najua unajitahidi lakini, na naona kuna sehemu kubwa ndani ya moyo wako imeridhia kuwa na mimi, ila... siyo mimi ninaye...." nikajikuta nashindwa kuendelea.
"Nini? Unataka kusema nini?" akauliza.
Nikashusha pumzi tu kwa kufadhaika.
"Kwamba hautaki kuwa sehemu ya mpango wangu moving forward?" akauliza hivyo.
Nikamwangalia usoni kwa utulivu.
"Oh, shida ni nini JC? Kwa sababu nimeiuza hiyo hoteli? Ahah... please, ilikuwa imeshazeeka hata hivyo...."
"Sijamaanisha hivyo Bertha..."
"Sasa tatizo ni nini? Bado tu unasumbuliwa na kilichowapata wakina Sudi? Ndiyo hivyo?" akauliza.
Nikainamisha tu uso wangu.
"Oh JC... ulinifata wewe mwenyewe, ukaniambia unanipenda huku ukijua nature yangu, na bado ukataka tuwe sote through all of this, mpaka sasa... shida ni nini sasa hivi? Kinachokupa was...."
Maneno yake Bertha yakakatishwa baada ya simu yake iliyokuwa mezani kuanza kuita, naye akatikisa kichwa kidogo na kuichukua upesi.
Akaangalia mpigaji na kuniambia, "Kinachokupa wasiwasi ni nini wewe... eh? Nilikwambia be a man, be a man bwana. Ah..."
Alikuwa akimalizia maneno yake kwangu, kisha ndiyo akapokea simu yake. Nikawa namtazama tu kwa utulivu mpaka alipoiweka sikioni kumsikiliza mpigaji, na uso wake ukaonyesha jambo nililokuwa nimetarajia upesi sana. Alishtuka.
"Nini?!"
Neno hilo pekee likamtoka midomoni mwake baada ya kuonekana kuwa amesikia jambo fulani baya na lenye kushangaza mno, naye akanitazama usoni kwa macho yaliyoonyesha hofu kubwa. Nikashindwa hata kuigiza yaani na kuendelea kumwangalia tu kwa hisia za huzuni, naye ghafla akasimama na kuirusha simu yake kwa nguvu hadi ilipopiga ukuta na kuvunjika-vunjika!
"Aaaaah!" akapiga kelele kwa hasira na kujishika kichwani kwa viganja vyake vyote.
Nikasimama pia na kumuuliza, "Nini madam? Nini... nini kimetokea?"
Akawa anatembea mbele na nyuma huku akipumua kwa uzito, naye akasema, "Wameharibu, JC! Wameharibu kila kitu!"
Nikaangalia pembeni kwanza, hapo tayari nikiwa naelewa vizuri kilichokuwa kimetokea, nami nikamuuliza, "Huyo alikuwa nani?"
"Msambazaji wangu mmoja! Hapo amenipigia... anakimbia... anasema maaskari wame-seize majengo yetu YOTE ya biashara! How the hell did this happen?!" akaongea hivyo kwa presha.
Nikaendelea kutulia huku nikikunja ngumi kuzuia hisia zangu.
"No... no, no, no... huyu mpumbavu atakuwa amekosea. F(...)! Naomba simu yako JC. Give me your f(......) phone!" akanifokea kama amechizi vile.
Hili itikio nilikuwa nimelitarajia. Nikaitoa simu mfukoni na kumpatia baada ya kutoa lock, naye akaonekana kutafuta namba ya mtu na kupiga.
"Dotto pokea... pokea Dotto... uko wapi?"
Akaongea hivyo na kisha kutulia, halafu akakaza macho yake kwa nguvu na kushusha mkono wake. Nikamnyang'anya simu yangu kabla na yenyewe hajaitupa!
"Vipi madam? Dotto hapatikani?" nikamuuliza hivyo.
"Hapokei. JC, kama kweli maaskari wamefanya round up kote kukamata biashara zangu, inamaanisha wana... damn! Wame.... kila jengo!" akasema hivyo kwa hisia kali.
Nikaangalia tu chini kwa utulivu.
"Ahh... hhahh... how the hell did this.... Dotto atakuwa wapi? Ama na yeye utaniambia.... na yeye... wanamkimbiza, kila... wanaweza ku.... mpigie Festus JC, now! Mpigie haraka..." akaongea kwa kubabaika na uharakishi.
Akatoka hapo alipokuwa amesimama na kuelekea kwenye kabati la nguo, naye akafunua mlango mdogo humo humo ndani na hapo nikaona sanduku la kielektroni la kutunza, ama kufichia vitu. Nikaendelea kumtazama kwa umakini hadi alipobonyeza namba za kulifungulia (nywila), kisha akafungua kimlango chake na kuanza kutoa mabunda ya pesa nyingi sana, akiyarushia kitandani kwa kasi mpaka alipomaliza yote.
Akachukua mkoba mkubwa na mtupu kutoka kwenye stendi pembeni na kukielekea kitanda, naye akaanza kuziweka pesa hizo mkobani huku akisema, "Kama wameweza kufikia sehemu zangu, sehemu zetu zote kwa mkupuo, na kuwakimbiza wajeshi wangu wote, basi watakuwa wamezinusa na kuzifata biashara za wengine pia. Ni lazima kuwe na leak. Ni lazima! Kuna mtu ametu-snitch... this is impossible, haiwezekani... everything was done so carefully, I can't...."
Alikuwa anaongea haraka-haraka kama vile amepagawishwa na madawa ya kulevya, naye akanigeukia kukuta bado nimesimama tu huku nikimtazama.
"Acha kuzubaa JC! Pick something up, mpigie Festus haraka! We have to get out of here! Hao washenzi wanaweza wakawa wanakuja na hapa, tunapaswa tuondoke ASAP...."
Alikuwa ameshamaliza kuzirundika pesa zote kwenye mkoba, naye akavua ki-T-shirt chake na kukirusha huko, kisha akachukua T-shirt jeusi la mikono mirefu na kulivaa upesi, halafu akaivua na hiyo suruali yake na kuanza kuvaa nyingine tena; ile ile ngumu ya leather yenye kung'aa aliyokuwa amevaa juzi alipomuua mume wake.
"Haiwezekani! Haiwezekani kabisa! Haiwezi kuwa mistake, haiwezi kuwa wameotea tu, eti sehemu zote kwa mpigo mmoja, wamewezaje... wamewezaje kufanya hivyo? Ah, ku(.......)! Just when everything was going so perfectly... JC, tuondoke haraka. Chukua funguo zangu za gari hapo. Harakisha!" akaongea kwa msisitizo.
Nikabaki nikimtazama kwa hisia sana.
"What are you doing?! Unafikiri nakutania? Kila kitu kimeharibika! Hatupaswi kuendelea kuwa hapa, kuna mtu ameni-snitch, JC! Harakisha, mpigie na Festus, tuku...."
Akaishia hapo ghafla.
Alikuwa ameinama tena kuelekea shelfu lililokuwa limebebea viatu, bila shaka akitaka kuchukua viatu avae, naye akatulia kidogo kama vile kuonyesha utambuzi wa jambo fulani ulikuwa umemwingia kichwani. Akasimama wima na kuniangalia usoni kwa umakini sana, mimi bado nikiwa namtazama kwa hisia, naye akashusha pumzi kwa njia fulani kama mtu aliyechoka sana.
"Kwa nini haumpigii Festus?" akaniuliza hivyo kwa sauti ya chini.
Nikaangalia pembeni na kubaki kimya tu.
"JC? Hey... mbona hunijibu?" akauliza tena.
Machozi yakaanza kunilenga kabisa, nami nikainamisha uso wangu tu.
"Ahh... JC! JC umefanya nini?" akauliza hivyo kwa sauti yenye kunong'oneza.
Nikajikaza tu kihisia na kumtazama usoni kwa umakini.
Akaninyooshea kidole chake na kusema, "Wewe... wewe ndiyo umefanya hivi? Kwa nini? Huh? Ume... umeni-umenisnichia kwa mapolisi, JC?"
"Bertha..."
"Yaani... una... oh f(...)!" akasema hivyo na kujishika kichwani.
Nikashusha pumzi tu na kuiweka simu mfukoni, nikiwa nataka nimsemeshe tena.
"Yaani kumbe umekuja hapa, to keep me occupied... unizubaishe... ili... na penyewe waje kunisomba? Eh?" akauliza hivyo.
"Sikia Bertha. Kila kitu kimeenda, siyo kwa jinsi nilivyofikiria kingeenda, ni... mambo mengi, lakini... yaani, sijui hata nikwambieje ila...."
Nikiwa naisaka namna ya kumwelezea, nikaona anatazama pale kwenye droo ya kitanda upesi, nami nikaangalia hapo na kuona kwamba aliiangalia bastola yake. Tukaangaliana tena kwa umakini, naye Bertha akakaza macho yake kwa njia iliyoonyesha hasira zaidi, na ule mjongeo wa mbali wa mwili wake wa kutaka kuelekea upande huo ukanifanya nitambue kwamba alidhamiria kuifata bastola yake ili anifundishe adabu.
Na kweli akageukia huko tena na kuonyesha nia ya kuifata bastola hiyo kwa kuanza kukimbia, nami hapo hapo nikaliruka sofa kwa kasi na kukutana naye wakati ambao tayari alikuwa ameshaikamata bastola yake na kujaribu kuigeuzia kwangu ili anitandike risasi. Nikaiwahi mikono yake na kuupamia mwili wake kwa nguvu kiasi, nasi tukadondokea kitandani huku nikiwa juu yake, na nikiikaza mikono yake ili bastola isigeukie kwangu.
"Bertha, subiri... acha..." nikawa najaribu kumzuia.
"Una(......) wewe! Niachie, mpumbavu, msenge wewe! Unanisaliti mimi?!" akaongea kwa uchungu sana.
"Bertha, nisikilize... please..."
"Niachie, nikuonyeshe, mpumbavu... aahh..."
Alikuwa anajaribu kufurukuta kwa nguvu zake zote, na mimi nikaendelea kumkandamiza ili nipate nafasi moja tu ya kuuachia mkono wake mmoja na kuikamata bastola upesi, na nilipofanya hivyo, ikampa mwanya kiasi wa kukaza zaidi viganja vya mikono yake, hivyo akawa amesababisha risasi moja ifyatuke. We! Hiyo kelele!
Risasi ilikuwa imetandika ukuta na kuacha tobo, na najua sauti iliyokuwa imetoa ingeshtua wengi hotelini hapo. Niliumia kiasi masikioni kutokana na hiyo sauti na kushindwa kuendelea kumkaza zaidi, na hiyo ikampa nafasi ya kujigeuza kidogo na kurusha mguu wake chini yangu. Hapo akawa amenipiga sehemu ya siri na kunifanya niishiwe nguvu zaidi, nami nikalegea na kudondokea chini huku nikihisi maumivu kwenye viungo vya uzazi.
Bertha akajitoa kitandani upesi na kushuka chini, naye akasogea mpaka usawa wa lile sofa huku akiielekeza bastola yake upande wangu. Nilikuwa chini bado huku nikimtazama usoni kwa huzuni, yeye akiwa ananiangalia kwa hasira sana na kupumua kwake kukiwa kwa presha yaani utafikiri alikuwa anataka kupasuka. Dah!
Najua alikuwa na hasira, siyo kwamba kwa sababu angekuwa amepoteza huu mchezo, ila kwa kuwa aliyesababisha aupoteze ilikuwa ni mimi. Najua Bertha alikuwa ananipenda, na ni jambo hilo ndiyo lililofanya akasirike zaidi kwa sababu nilimuumiza moyoni kabisa. Yaani kabisa, toka mwanzo, hakufikiria kwamba mimi ndiyo ningekuwa msaliti wake, hata alikuwa tayari kuondoka na kukimbia pamoja nami, lakini sasa akaona wazi kuwa alishindwa kotekote kabisa. Na ni hilo ndiyo lilinifanya nijione kuwa mbaya yaani.
Nikajitahidi kusimama taratibu, huku bado nikijishika usawa wa kiuno kutokana na kuhisi maumivu, nami nikaendelea kumwangalia usoni kwa huzuni sana kutokana jinsi ambavyo aliniangalia kwa zile hasira zilizomfanya alengwe na machozi na pumzi zake kutetemeka sana. Katika wakati kama huu, ikiwa ingekuwa chini ya hali nyingine, labda kama ingekuwa ni mtu mwingine ndiyo kanishikia bastola namna hiyo, huenda ningetetemeka, lakini hapa, sikuwa na wazo la kuhofia kabisa juu ya maisha yangu.
Yaani, kwa lolote ambalo lingetokea, nilikuwa tayari kuacha litokee, na sikujua tu kwa nini ilikuwa namna hiyo. Nilimwangalia Bertha machoni na kuona namna alivyokuwa akihisi uchungu, na kwa njia fulani ikawa kama vile anaushiriki pamoja nami. Mpaka nikawa nahisi kama vile mimi ndiyo mtenda dhambi kwenye hiki kisa. Nilihisi kama vile nimemwonea yaani.
Nikaangalia chini kwa huzuni sana, kisha nikamwangalia usoni tena na kumwambia, "I'm sorry..."
Sikuwa na lingine la kumwambia.
Uso wake ukakunjamana zaidi, akionekana kupandisha hasira zaidi na zaidi huku akikaza bastola viganjani kunielekea kwa nia kuu ya kutaka kufyatua risasi, nami nikaendelea tu kumwangalia usoni kwa hisia sana mpaka machozi yakajaa machoni kwa huzuni kuu niliyohisi kutokana na kuuona uchungu wake.
Akakaza na meno yake akiwa anataka, na anataka kunipasua kichwa kwa usaliti niliokuwa nimemfanyia, nami nikafumba macho yangu taratibu nikiwa naelewa kuwa huu ndiyo ungekuwa mwisho! Nini kingeniokoa kutoka kwenye hasira ya huyu mwanamke?
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
Full Story WhatsApp or inbox
Whatsapp +255 678 017 280
Jc kautaka😂JC umeyatimba ndugu yangu jiandae kupakiwa mkongo mzee baba
Fita Ni Fita Muraaa JC mie timu yako hadi FESTO akuue tuko pamojaMIMI NA MIMI 2
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI NA SABA
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Nikamfata tu askari Ramadhan baada ya hapo na kujiunga pamoja na huyo Festo kutia saini karatasi za kuthibitisha hiki na kile, na kiukweli sikukazia fikira mambo hayo kwa sababu akili yangu bado ilikuwa imetatizwa na suala zima la Festo kuwa hapa, huru, na akionwa kama malaika pia na hawa jamaa. Tena kwa jinsi tu alivyokuwa amenisemesha sekunde chache nyuma yaani ndiyo alizidisha kuthibitisha kwamba hakuwa upande mzuri kikamili, kwa hiyo ningesubiri kusikia aliyotaka kuniambia ili niamue ningemchukulia vipi zaidi.
Baada ya kumaliza kusaini, askari Ramadhan akatuaga kwa kusema kuna mambo mengine tena angeanza kushughulika nayo, nasi tukaondoka hapo ofisini kwao. Kufikia sasa sikuwa nikihisi maumivu tena kutokea kwenye nyonga mpaka sehemu za siri. Nilikuwa nyuma ya Festo, yaani yeye alitangulia mbele yangu na kuelekea mpaka kwenye lifti ili ashuke chini, na najua alitarajia nipande lifti hiyo pamoja naye lakini mimi nikaamua kutumia ngazi kushuka. Sikujali angechukuliaje hilo, yaani angejua mwenyewe.
Nikatoka mpaka kufikia nje ya jengo hilo nikiwa ninafikiria kwenda kuchukua usafiri, ndipo kutokea upande mwingine wa eneo hilo honi ya gari ikawa imepiga mara mbili. Nikaangalia huko na kumwona Festo akiwa amesimama kwa kunitazama karibu na gari zuri jeupe, aina ya Lexus 600
View attachment 3068067
kama lile jipya la Bertha ila la gharama zaidi, nami nikasimama tu na kuendelea kumwangalia. Akaniita kwa kiganja chake tena na kisha kuingia garini bila kusubiri jibu.
Nikatulia kwanza nikitazama huko kwa ufikirio, kisha nikaamua kwenda. Nilipokuwa natembea kulielekea gari hilo, nikatoa simu yangu na kuweka ule mfumo wa kurekodi sauti, kisha nikairudisha mfukoni ili mfumo huo utembee tu katikati ya maongezi yote ambayo ningefanya na huyo jamaa.
Kama alikuwa anapanga tuongee tu, basi mengi ambayo angesema ningeyanasa na hata kuja kuyatumia baadaye ikiwezekana, na kama alkuwa anataka kunidhuru, nilikuwa tayari kupambana pamoja naye. Yaani sasa hivi sikujua na sikujali alikuwa nani huyu mtu. Kama ni chini, basi tungeenda pamoja.
Nikafika kwenye gari lake na kuingia siti ya pembeni na usukani alipokaa yeye, nami nikatulia tu, nikitazama mbele kwa utulivu.
"Utapenda tukiongelea hapa, au tutafute sehemu nyingine?" akauliza hivyo.
"Hapa hapa," nikamjibu.
"Uko sawa? Nimeambiwa umekoswa na risasi leo...."
"Unataka nini, Festo?" nikamkatisha.
"Nataka kujua uliyosema kwa mkubwa kabla sijafika. Ulikuwa umeshaanza kutembeza mdomo wako huko ndani, ulitaka kuwaambia nini kuhusu mimi?" akaniuliza hivyo.
"Kwani itajalisha mimi nasema nini kuhusu wewe?"
"Ndiyo, haijalishi."
"Sasa? Si wamesema toka mwanzo u... si umekuwa unaigiza tu? Unataka nini sasa?"
"Mbona una hasira sana? Hm? Ulikuwa unatarajia na mimi ningekamatwa, si ndiyo?" akaniuliza hivyo.
Nikatazama pembeni tu.
"Kwa hiyo matarajio yako kwenda ndivyo sivyo imekunyima furaha... mhm... umejiona fala," akasema hivyo.
"So, ni uwongo then. Ni uwongo kwamba uko upande wa maaskari, kila kitu ulichofanya kuwasaidia ni nothing but a sham. Si ndiyo?"
"We' unaonaje?"
"Oh, naona jinsi navyoona. Najua haiwezekani kabisa eti kwamba ulikuwa unaigiza tu, Festo. Najua ulikuwa pamoja na Bertha. Tena kwa mengi tu, siyo madawa pekee. Najua we' ndiyo mbaya kuliko hata yeye, ni kwamba tu umeweza kugeuza hilo wimbi lote limzamishe yeye peke yake na wewe usilowane hata kidogo, because...."
"Kwa nini umeumia sana Bertha kukamatwa wakati ni wewe ndiyo umem-snitch tokea mwanzo?" akaniuliza hivyo.
Nikabaki kimya, nikimtazama kwa umakini tu.
"Acha unafiki. Unajua... siku ile umekuja kwangu ukaongea bullshit yote kuhusu wewe kumpenda Bertha, nilikuwa nawaza 'huyu dogo anaongea pumba tu hapa kuni-convince na nini,' lakini sa'hivi nimeanza kuona haikuwa pumba. Umempenda Bertha kiukweli kabisa," akaniambia hivyo.
"Simpendi," nikasema hivyo kwa uhakika.
"Really? Well, kwa nini ulihatarisha maisha yako kumsaidia ulipojua Sudi alitaka kumuua?" akaniuliza hivyo.
"Sikutaka tu auliwe. Hiyo haimaanishi kwamba nampenda. Na... ilikuwa njia nzuri ya kumfanya aendelee kuniamini."
"Mmm?"
"Eeeh. Wewe je? Huo muda wote ulikuwa unajua kila kitu eti, kwa hiyo ukawa unanichora tu, si ndiyo? Umefanyaje Festo mpaka ikawa hivi? Hm? Umewalipa hawa jamaa?"
"How dare you!" akaongea hivyo kwa mkazo.
Nikatulia na kuendelea kumwangalia.
"Unafikiri kwa kuwa nimeficha mambo mengi mabaya basi sina honour hata kidogo?" akaniuliza hivyo.
"We' ndo' uniambie," nikamsemesha kwa ujasiri.
"Nikuelezee nini mtoto mdogo kama wewe? Unafikiri kwa sababu umekuwa ukifanya kazi na maaskari basi hiyo inakufanya uwe msafi? Kwa kila kitu? Hata wewe ni mchafu JC, umecheza tu haka kamchezo kujiaminisha kwamba una nia nzuri, lakini sote tunajua kwamba mimi na wewe ni wabinafsi wa hali ya juu, na tunafanya lolote ili kupata tunayotaka. Kabla ya kujifanya unajua sana kujaji, jiangalie kwenye kioo kwanza," akaniambia hivyo kwa hisia kali.
Nikaangalia pembeni kwanza, nikiwa natafakari maneno yake.
Akasema, "Njia zetu zinatofautiana, lakini we are the same. Ni kwamba me nimekuzidi tu katika mengi mabaya, lakini haimaanishi nimepoteza kabisa nia ya kufanya mazuri. JC..."
Nikamwangalia.
"Ninataka kuacha. Haya maisha ya gizani haya? Ninataka kuyaacha kabisa... ndiyo maana nikafanya hivi," akaniambia.
Nikaendelea kumwangalia kwa umakini.
"Unajua nini mdogo wangu? Toka siku ya kwanza Bertha kakuleta kule Red Room, nilihisi tu kulikuwa na kitu hakiko sawa. Nilikufatilia na kujua ulikuwa pamoja na hawa watu, lakini unajua kwa nini nilikuacha tu?" akaniuliza.
Nikatulia kusubiri ajijibu mwenyewe.
"Nilikuacha kwa sababu ulinisaidia kuona kwamba hayo maisha hayakuwa sahihi kwangu kuendeleza. Oh, na siyo kwamba wewe ndiyo ulifanya nikaona hayo maisha hayafai tena, ni kwamba tu ulikuja kwenye wakati mwafaka ambao nilitaka kuyaacha. Ukafanya boost up tu. Ramadhan anajua kwamba nilikuwa nafanya hizo biashara kweli," akaniambia hivyo.
Nikamwangalia kiumakini zaidi.
"Anajua. Kwa sababu nilimfata mimi mwenyewe kumwambia. Na nilimwambia najua kuhusu wewe kushirikiana naye, na sikuwa na nia ya kukuumiza hata baada ya kujua hilo kwa sababu nilitaka kutoka kwenye hizi ishu. Kwa hiyo tukafanya makubaliano, nijitoe kusaidia kukomesha haya yote mwanzo mwisho. Ningekuwa nataka kuendelea na madawa JC... ungekuwa umeshakufa nilipojua tu unatu-snitch," akaniambia hivyo.
Nikatulia kidogo na kisha kumuuliza, "Kwa nini? Kwa nini ulitaka kuacha?"
Akaangalia mbele na kusema, "Miryam."
Nikafumba macho na kisha kuangalia pembeni. Mada ikarudi kwa bibie. Yaani yeye ndiyo alikuwa katikati ya kila jambo!
"Siku ile ulikuwa unasema 'ooh, kama utajifanya malaika kwa Miryam, hata me nitajifanya Shetani kwa Bertha.' Ahah... nilikuangaliaaa... unajua kweli kuigiza mdogo wangu. Lakini hata me sikuwa nyuma. Niliendelea kuigiza, kukufanya ufikiri kwamba naweza hata kuwaumiza watu wa familia ya huyo mwanamke ili unijaji kama unavyonijaji sasa, lakini mimi siyo mbaya kiasi hicho, na sijali unachofikiri kunihusu JC. Nilikuwa na-play part yangu vizuri ili hii siku ifike, na imefika kama nilivyotaka, lakini sikuwa mtu uliyenidhania nilikuwa. Sikutaka... kujifanya malaika ili nimpate Miryam, nimetaka KUWA huyo malaika ili niweze kumpata Miryam..." akasema hivyo.
Nikiwa nimetazama mbele tu, nikamuuliza, "Kwa hiyo ni kwa sababu ya Miryam ndiyo ukataka kubadilika?"
"Yeah. Tayari nina kila kitu, chochote kile naweza kupata, lakini furaha, bado haikuwepo ile niliyoitaka. Ni kwa sababu nilitaka kuwa na furaha zaidi... hizi mali na nini, siyo furaha. Ndiyo nikaliona hilo jambo kwa Miryam, na... ukweli ni kwamba imekuwa too late kwa sababu hata kama ningefanya nini... huyo mwanamke hajaweza kunipenda," akasema hivyo.
Nikamtazama na kuona uso wake umeshikwa na simanzi kiasi.
"Kuna siku hadi nili-snap kidogo... ahah nikamwambia nitampa, na nitafanya yote kwa ajili yake, lolote lile ili tu akubali nimwoe, na hapo ndiyo nikawa nimeharibu zaidi, maana nilimfanya afikiri kuwa labda namwona kama kitu cha kununua. Lakini yeye bila kujua kuhusu haya maisha yangu na nini... akasema napaswa kujitahidi kufanya vitu vingi kwa wema wa moyo, siyo kwa matarajio ya kupata faida tu, maana... wakati mwingine zinaweza zisije faida, ila hasara. Na mimi hasara yangu ikawa kumpoteza," akasema hivyo na kuniangalia.
Dah! Nikaangalia tu pembeni, maana nilielewa vizuri sana kwamba huo ulikuwa ni ukweli. Huyo alikuwa ndiyo Miryam.
"JC nachukia kuwa dramatic kama hivi, lakini... nimeongea hayo yote kwa sababu umeniona... umeniona nikiwa huko, kwenye familia yake nikijaribu kum-win huyo dada. Sikuwa na ulterior motive, nilimkubali kweli. Lakini hata baada ya kumkosa, haikumaanisha ningetaka kurudi tena kwa hizi mishe, no. Nimetaka kuacha siyo kwa ajili ya Miryam tu tena... but for me. Nataka tu ni..toke. Nime... nimeumiza watu, nimelaghai watu, nimevunja sheria, nimeua... na nikiangalia... sioni faida yoyote ile kubwa niliyopata kufikia sasa hivi zaidi ya majuto, na hilo limenibomoa sana," akasema hivyo.
Nikashusha pumzi kiasi na kuangalia pembeni zaidi.
"Lakini kila mtu si anastahili msamaha? Nikitambua kwamba nimekosea, na kuna uwezekano wa kubadilika, nafanya hivyo. Ndiyo ninachokifanya. Nataka kusafisha maisha yangu kabisa, sitaki kuwa mbinafsi tena, yaani... nataka nianze upya..." akasema hivyo.
"Kwa kuharibu zaidi maisha ya wengine ili kupata hilo unalotaka, huoni kwamba bado unaendelea kuwa mbinafsi?" nikamuuliza hivyo bila kumwangalia.
"Unamwongelea Bertha?" akaniuliza hivyo.
Nikamwangalia na kusema, "Hapana. Namwongelea mtu kama Saidi."
Akabaki kimya.
"Kwa nini ulimuua shefu Saidi?" nikamuuliza.
Akatikisa kichwa kidogo na kusema, "He was collateral damage."
"Ooh kumbe? So maisha yake, familia yake, haikujalisha kabisa... ukaamua tu kumu...."
"Nimeua wengi, JC. Hata wewe ningekuua!" akaniambia hivyo kwa sauti kali.
Nikatulia na kuendelea kumwangalia kwa umakini.
"That's my point! Nimefanya mabaya, I want to stop. Bertha na wengine walikuwa contended kuhusu maisha waliyochagua, hakuna hata mmoja aliyeonyesha kutaka kuyaacha maana huwa yanazidisha kiu tu ya kutaka zaidi, na zaidi, na zaidi... ndiyo maana ilikuwa lazima kuwaacha watumbukie kwenye shimo la simba..."
"Halafu wewe ujiokoe mwenyewe..."
"Tell me, ulitaka nifanye nini? Nijishikishe kwa maaskari kwa yote niliyofanya baada ya kina Bertha kukamatwa, si ndiyo?"
"Yes! Hapo ndiyo ungekuwa umeondoa ubinafsi. Siyo kwamba ukijiona wewe una haki ya kubadili maisha, wengine hawana... na wewe ungejitoa ufungwe," nikamwambia hivyo kwa uhakika.
"Ingesaidia nini? Yote niliyofanya yangekuwa reversed? Huyo Saidi wako angerudi kuwa hai?" akaniuliza hivyo kimkazo.
Nikameza mate kwa hasira huku nikimtazama kwa umakini.
Akashusha pumzi kujipa utulivu, naye akasema, "It doesn't matter. Tunafanya lolote lile ili ku-survive. Okay? Nimetoa... pesa nyingi sana, nimejiachia kutoka kwenye hizo biashara haramu, nimekata tie zote na watu wote wabaya niliokuwa nafanya nao hayo mambo ili niweze kuwa mtu mwingine kuanzia wakati huu, haitoshi? Ni lazima mpaka niende jela, au na me niuwawe ili JC ndo' aridhike sasa eti Festo hakuwa mbinafsi? Hiyo siyo akili, na mimi siishi kwa misingi unayotaka wewe. Unanielewa? Kuanzia sasa nitaishi maisha yangu navyoona fit baada ya kuachana na haya yote... haijalishi ulikuwa unajua nini, maaskari wanajua na hawajui nini, au Bertha ama nani amefanya nini... imekuwa ilivyokuwa. Na itapaswa kuishia kuwa hivyo."
Nikatazama pembeni tu na kutikisa kichwa kwa kutoamini kiasi. Hata kama alikuwa anataka kubadilika lakini bado niliona alikuwa mbinafsi sana, yale mambo ya mtu unaweza kubadili tabia lakini siyo utu wote, ndiyo alilokuwa nalo hilo jambo.
"Sijakuita hapa ili uwe kama judge wangu mkuu, ama labda nikuombe msamaha. Sijakukosea kwa lolote. Nimekuita hapa kwa sababu we' ni mwanaume. Unanielewa vizuri. Sijui sana kama ulikuwa umeshampenda Bertha, lakini najua ulikuwa unamjali. Hata ukatae. Kuna sehemu ndani yako ilikuwa inataka na yeye abadilike... aache haya maisha. Uwongo?" akaniambia hivyo kistaarabu.
Nikainamisha uso wangu tu na kutikisa kichwa kukubali.
"Najua. Lakini kama wengine, ilikuwa imesham-consume sana, hangeacha. Na mimi... namjali pia. Namwonaga kama mdogo wangu, ni bora kumshikisha kwa mapolisi aka-serve miaka mingapi jela, atoke, akiwa salama... labda. Kuliko aje kufa kwenye hili game ambalo.... haina faida yoyote, JC. Na nimekwambia, imeshakuwa jinsi ilivyo, kilichopo kutokea hapa, ni kusonga mbele kwa mengine. Basi," akaniambia hivyo.
Nikiwa bado nimeshusha macho yangu, nikamuuliza, "Kwa hiyo utafanya nini kutokea hapa sasa?"
"Bado kuna vitu natakiwa kuweka sawa. Nataka nimalize kuuondoa uchafu wote kwenye maisha yangu, mengine yatafata tu," akaniambia hivyo.
"Na Miryam?" nikamuuliza hivyo huku nikimtazama kwa jicho la chini.
"Sijui. Huwa najipa matumaini kwamba labda sijampoteza kabisa, lakini kama imeshafika hiyo hatua... nataka kuhakikisha. Na nitajua la kufanya baada ya hapo," akasema hivyo.
Mh! Mwana nikajikausha tu kama vile sikuwa na langu jambo kumwelekea mwanamke yule pia. Hapa nilikuwa na fahali mwenza, lakini nilitulia zaidi tu maana hakujua kwenye zizi alilotaka kulalia mimi pia nilikuwa namendea kuingia.
Akasema, "No hard feelings, JC. Really, yaani kati yangu me na wewe, hakuna ubaya wowote. Sawa? Nataka tu ifike mahali iwe kama hatujawahi kujiingiza kwenye hizi biashara pamoja, yaani... iwe kama hatukuwahi kujuana hivi. Hiyo peace angalau kwa upande wako naihitaji. Sitaki kabisa tuvurugiane maisha mdogo wangu. Naomba ukitoka hapa, usinijue, nisikujue tena. Siyo kwa ubaya, bali kwa usalama, na ndivyo inavyotakiwa. Unanielewa?"
Nikiwa nimetazama mbele sasa, nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
Akashusha pumzi na kusema, "Naweza kukusogeza hapo mbele ukitaka, uchukue usafiri. Unaenda Mbagala?"
"Hamna, kuna sehemu nyingine naenda kwanza. Nitashuka tu na kutembea mpaka hapo," nikamwambia hivyo kwa utulivu.
"Sawa. Good talk. Tutaonana tukionana basi. Safari njema," akasema hivyo.
Sikumjibu lolote na kuamua tu kuufungua mlango, na kabla sijatoka, akaita jina langu. Nikamtazama.
"Be careful," akaniambia hivyo.
Kwa mara nyingine tena, akawa ameniambia maneno hayo yenye kutahadharisha sana, na kabla hata ya kusubiri kuelewa yalimaanishia nini kabisa nikaona nishuke tu na kusimama pembeni, kisha ndiyo yeye akaliwasha gari lake. Nikaanza tu kujiondokea hapo na kuelekea upande wa pili wa barabara, nikiliona gari la jamaa lilipoingia barabarani na kutokomea upande mwingine kutokea eneo hilo.
Nikiwa nasubiria tu usafiri, nikaitoa simu yangu na kukuta bado ikiwa inarekodi sauti, na yote ambayo nilikuwa nimeongea na jamaa iliyaingiza vyema kabisa. Kutokana na yote tuliyozungumzia, sikuona uhitaji wa kutunza rekodi hiyo, lakini katikati ya ile fikira ya "huwezi jua baadaye itakuwaje," nikaamua kuitunza tu kwa ajili ya lolote ambalo lingeihitaji mbeleni. Nilikuwa na mambo mengi sana ya kufikiria baada ya hizi ishu zote kutokea leo, nami nikapanda tu daladala ili niondoke maeneo hayo upesi.
★★
Niliamua kupanda daladala moja baada ya nyingine na kufika Mbagala ikiwa imekwishaingia saa kumi jioni, na mpaka wakati huu sikuwa nimeweka chochote kile tumboni. Hivyo nikaamua kwenda pale Zakhem mgahawani, na nilipapenda, nikaagiza msosi mzuri tu na kula taratibu, kisha shibe ilipokaa vizuri ndiyo nikaelekea kuchukua usafiri tena kwenda Mzinga.
Hali ya hewa kwa leo ilitulia zaidi, mvua haikunyesha japo kuna nyakati wingu lilikuwa linavizia hapa na kule, na nilipofika Mzinga kama kawaida nikatembea mdogo mdogo kuelekea kwa Ankia. Halafu niliona nipite upande usio wa duka lake ili nisihitajike kupita hapo na kumsalimia, maana nilitaka nikatulize tu mwili na akili kwanza. Kwa hiyo nimekuja kufika ndani kabisa ikiwa imeshaingia saa kumi na moja.
Nikafanya kupiga push-up kidogo na kwenda kuoga kwanza, kisha nikajiweka sawa kimwili tena na kuvaa nguo nyepesi, halafu nikaona nicheki jambo fulani. Zile pesa alizonipatia askari Ramadhan bado nilikuwa nazo, zikiwa kibunda, nami nikazotoa mfukoni na kuamua kuzihesabu. Yaani kwa jinsi zilivyokuwa zimebanwa na rubber band ungefikiri siyo nyingi sana, lakini nilipozifungua mpaka zikamwagika chini. Jumla ikawa ni milioni moja, nami nikahisi kuchoka tu na kuzishindilia kwenye kimfuko kidogo, kisha nikaziweka kwenye begi.
Nikatoka humo chumbani na kwenda kukaa sebuleni, nikiangalia kama kungekuwa na jambo fulani kwenye simu la kuweza kunisaidia kuhamisha akili, lakini nayo ikaboa tu. Nikaamua kuwasha TV, niangalie filamu yoyote ya kichina iliyorushwa Azam Kix, nami nikapata moja na kujilazimisha kuiangalia huku nikimsubiri mwenye nyumba wangu arejee.
Nikaendelea kukaa tu hapo hapo sofani nikiangalia TV ikiwa imeshapita saa kumi na mbili jioni kuelekea saa moja, na hata yaliyokuwa yanaonyeshwa filamuni hayakuingia akilini kabisa. Nilikuwa kama nimeganda yaani, akili yangu ikirudi kule kule ilikotoka kwa asubuhi hiyo mpaka kufikia wakati huu, na ndipo Ankia akawa amerejea hapa kwake hatimaye.
Alikuwa amejipendezea mwenyewe kwa kuvaa T-shirt mikono mifupi ya zambarau na suruali ya jeans iliyombana vyema, na sasa hivi alikuwa ameanza kunukia harufu fulani hivi mpya, nzuri, kitu ambacho kilionyesha mtoto alikuwa amebadilisha manukato ili awe mpya zaidi. Akiwa katika hali ya uchangamfu akanisalimia vizuri na kukaa nami sofani, naye alikuwa amekuja na mfuko wenye vyakula na mbogamboga kwa ajili ya usiku.
"Ffff... nina kazi ya upishi hapa, ila nimechoka! Naona uvivu kweli, lakini kula lazima, au siyo?" akawa ameniambia hivyo.
Nikatikisa kichwa kukubali huku nikitazama runinga tu.
"Vipi, umekula mchana?" akaniuliza hivyo.
Nikatikisa nyusi kukubali.
"Umekula nini?"
"Ugali, nyama."
"Nani amekupikia?"
"Ray C," nikamjibu kiutani.
"Umekutana naye wapi?" na yeye akaniuliza kiutani.
"Kwenye kamgahawa kake. Hujui ni mama'ntilie?"
"Ooh, ahahah... sawa. Alikuwa anakujazia-jazia na nyama eh..."
"Tena akanikomesha na pilipili..."
"Ahahahah... JC bwana..."
Nikaangalia tu TV na kutoa tabasamu la kujilazimisha.
"Ulikuwa umeenda Makumbusho tena? Leo umeondoka mapema, hatukuagana," akasema hivyo.
"Eeh... nilikuwa huko..."
"Hivi huwa unaenda kufanya nini huko JC?" akauliza.
Nikamwangalia usoni tu na kubaki kimya.
"Maana huu mwezi wote ulioisha, hutulii. Upo likizo ya kazi gani sasa kama unaondoka tu tena kwenda kujichosha? Ama umeoa huko yakhe? Tuambiane..." akasema hivyo.
"Kwo' kuwa likizoni ndo' imaanishe nikae tu ndani muda wote kama kobe?"
"Aa, tatizo unarudi mara nyingi na sura ya kinyoonge... ndo' maana nakuwa nashangaa. Mambo yako poa?"
Nikamwonyesha kidole gumba kama kukubali.
"Mhm... haya. Me ngoja nianda... eh, halafu subiri kwanza. Vipi suala lako na Miryam? Umeshaongea naye?" akaniuliza hivyo.
"Ah, we' nenda huko kapike bana..."
"Siendi mpaka uniambie..."
"Sikwambii sasa. Toka hapa," nikamfukuza kimasihara.
"Sitoki. Niambie JC," akasisitiza na kunishika shingoni.
"Ih, we' em' niachie bwana. Usianze bangi sa'hivi..."
Nikamwambia hivyo na kusimama kabisa, nikiashiria kutaka kwenda chumbani, naye akasimama pia na kunishika mkononi kwa nguvu.
"JC, acha kuogopa, niambie tu kama umeshamsemesha. Me rafiki yako, naweza nikakusaidia kwa hili au lile, kama bado hujamwambia, ukipenda naweza kukutengenezea mitambo. Maana yule ni mwanamke mwenzangu, namwelewa..." akaniambia hivyo kistaarabu.
Nikawa namtazama tu kwa utulivu, nami nikamwambia, "Huu moto wa kutaka sana kunisaidia, unautoa wapi?"
"Ahah... umekuja tu wenyewe. Nataka kukuona unafurahi... na ukimpata Miryam, najua na yeye atafurahi sana. Nitapenda kuwaona mnafurahi pamoja maana nawapenda nyote," akaniambia hivyo.
Nikatabasamu kiasi na kusema, "Yeah. Nimeshamwambia."
"Kweli?" akauliza hivyo kwa shauku.
Nikatikisa nyusi kukubali.
Alipotambua sikuwa na shauku kama yeye, akaweka uso makini na kuuliza, "Amekujibuje?"
"We' unafikiriaje?" nikamuuliza pia.
"Dah! Kakataa. Pole JC. Ila... usikate tamaa. Labda uendelee kumjaribu," akaniambia hivyo.
"Nani kasema nakata tamaa?" nikamuuliza hivyo.
Akatabasamu kiasi.
"Na siyo labda, ninataka kuendelea kum-please mpaka kieleweke Ankia. Sitaki kushindwa kabisa," nikamwambia.
"Hapo ndo' umeongea. Usiache. Atayeyuka tu," akanitia moyo.
"Unajua nini?"
"Nambie."
"Ninahisi kwamba Miryam ana hisia kwangu pia, lakini bado hajataka kukubali hilo kwa sababu ya mambo mengi yanayomchanganya," nikamwambia.
"Eti eh? Nini kinakufanya uhisi hivyo?" akaniuliza huku akitabasamu kiasi.
Nikageuka pembeni na kuanza kutembea taratibu kama naelekea chumbani, kisha nikasimama na kusema, "Moyo tu, Ankia. Kwa hizi wiki chache zilizopita nimejiachia sana kuamini na kufata kile moyo wangu unahisi... na siyo kwamba matokeo muda wote yanakuwa mazuri lakini nimeona kuwa siyo jambo baya kufuata moyo... kama nilivyokuwaga naogopa kufanya zamani. Moyo unaniambia kwamba Miryam ni wangu, na unanisukuma kufanya yote ambayo nitaweza ili kumleta karibu yangu. Ankia... nampenda sana Miryam. Yaani... mno..."
Ankia akawa amekuja mbele yangu na kuniangalia huku akitabasamu kwa furaha, naye akasema, "Unaongea kama vile unasoma script ya movie yaani. 'Nitafanya lolote kwa ajili yake, moyo wangu unaniambia ye' ni waaangu,' ahahah... hadi raha kukusikia unaongea namna hii. Kumbe mapenzi unayajua vizuri."
Nikatabasamu kiasi na kuangalia chini, nami nikamwambia, "Natamani tu angetambua haraka umuhimu wake kwangu... aniruhusu niingie moyoni mwake upesi ili nimpe upendo anaostahili. Changamoto zote anazopitia, naziona... natamani tu yaani aniruhusu...."
Kabla sijamaliza kuzungumza, nikaona Ankia anashtuka kiasi machoni huku akitazama kuelekea upande wa mlangoni nyuma yangu, nami nikaingiwa na msisimko kwa kuhisi kulikuwa na mtu mwingine ameingia hapo. Nikageuka upesi na kukuta ndiyo, kulikuwa na mtu ameingia hapo, na haikuwa mwingine ila kijana Tesha mwenyewe!
Alikuwa amesimama mlangoni, akituangalia mimi na Ankia kwa umakini sana, nami nikageuka vizuri zaidi na kumtazama usoni kwa utulivu makini. Alisimama kwenye uwazi mdogo uliokuwa umeachwa baada ya Ankia kufika na kuingia bila kufunga mlango, kwa hiyo nikaelewa wazi kwamba kijana angekuwa amesikia niliyokuwa namwambia Ankia.
"Eh, Tesha! Jamani, si ungepiga hata hodi, umenishtua," Ankia akamwambia hivyo kwa sauti ya chini.
Lakini Tesha akaendelea tu kuniangalia kimkazo kiasi, naye Ankia akanitazama usoni kwa wasiwasi. Jamaa akaanza kuja mpaka kufikia sehemu tuliyosimama na kutulia mbele yangu, akiniangalia kwa utafakari mwingi, nami nikaendelea kujipa utulivu pia nikisubiri kusikia ambacho angesema. Sijui angechukuliaje hilo suala yaani!
Tesha akasema, "JC uko sawa kweli? Kuna... hakuna tatizo lolote linalokusumbua?"
Nikabaki kimya tu huku nikimtazama kwa umakini.
"Tesha, ona... labda tukae ili tuongee vizuri eh..." Ankia akamwambia hivyo.
"Kwamba tukikaa ndiyo nitasikia vizuri zaidi ya tukisimama, au? Ni swali simple tu, anaweza kujibu hata akiwa amesimama..." Tesha akasema hivyo.
Nikaendelea tu kumwangalia usoni kwa utulivu. Alionekana kukerwa.
"Kaka, nimesikia yote uliyosema. Siyo yote, yaani... ndiyo nimefika hapo mlangoni nikasikia uliyosema kuhusu Miryam. Ni kweli?" Tesha akaniuliza hivyo.
Ankia akanitazama usoni kwa subira, nami nikamtikisia kichwa Tesha kumpa 'ndiyo' ya swali lake.
"Ahah... JC bana! Uko serious kabisa?" Tesha akaniuliza hivyo kwa kutoamini.
Nikaangalia pembeni tu.
"Tesha, hili ni jambo serious ndiyo. JC anampenda Miryam. Siyo masihara," Ankia akasema hivyo.
"Na wewe ndiyo mwenye uhakika? Wewe Ankia?" Tesha akamsemesha hivyo.
Ankia akamwambia, "Nani sasa mwingine awe na uhakika kama siyo mimi? We' si ndiyo umejua leo? Me naishi naye hapa, ni rafiki yake, najua..."
"Eti rafiki yake! JC, umemlisha nini huyu mpaka akaamini hii kitu bro? Ndo' anakupa support ili uje kumzuzua na dada yangu, halafu ukishamla, na yeye umgeuze rafiki yako," Tesha akasema hivyo.
Nikamwangalia kimkazo na kumsogelea karibu zaidi kwa hasira, naye akarudi nyuma kidogo kwa kushtushwa na hilo.
"JC..." Ankia akaniita kwa sauti ya chini huku akiziba mdomo kwa viganja vyake.
Nikajizuia zaidi kupandisha hasira na kujituliza kihisia, nami nikatazama pembeni na kushusha pumzi.
Tesha, akiwa ananiangalia kwa njia ya kutatizika, akaniambia, "Uko serious."
Nikamwangalia usoni kwa hisia.
"Da' Mimi anajua?" Tesha akaniuliza hivyo.
Nikatikisa kichwa kukubali.
"Ameshamwambia," Ankia akasema hivyo pia.
"Amesemaje?" Tesha akaniuliza.
"Amekataa," nikamwambia hivyo.
"Ahah... ulitegemea Miryam akukubali? JC... huko ni mbali sana umeenda mwanangu. Yaani... bado siamini yaani kama unaweza kumfikiria Miryam hivyo," Tesha akaniambia.
"Ninampenda dada yako Tesha kwa sababu ni kitu ninachohisi, siyo kufikiria," nikamwambia.
"Kumbe ndiyo maana ulikuwa na hasira sana siku ile alipopigwa na yule fala..." Tesha akasema hivyo.
Nikaangalia pembeni tu.
Tesha akanisogelea na kuuliza, "JC unajua Miryam ana miaka mingapi?"
"Kwani miaka ndiyo inazuia mtu kumpenda mtu, Tesha?" Ankia akamuuliza.
"Ankia subiri kwanza. JC nijibu. Unajua miaka yake?" Tesha akasema hivyo.
"Ndiyo," nikamjibu.
"Ana miaka mingapi?" akaniuliza.
"Thelathini na tano," nikamjibu.
"Okay, thelathini na tano. Thelathini na tano JC, ananizidi me miaka kumi, wewe sijui... nane? Na unasema unampenda ile... kwamba imetoka moyoni, unataka awe wako wa moyo, si ndiyo? Hapo tu, yaani hapo tu kwenye umri hata wewe unajua Miryam atakuona kama mtoto unayemfanyia mchezo, ukienda kumfata sijui kumwambia mambo gani... kweli una uhakika una... unaelewa unacho...."
"Ndiyo, Tesha!" nikamkatisha kwa uhakika.
Akatulia na kuendelea kunitazama kwa umakini.
"Nampenda Miryam. Yote niliyokwambia ufanye kwa Happy ile juzi, ndiyo mimi nayotaka kufanya kwa dada yako... na hata zaidi ya hapo. Nafikiri umenielewa," nikamwambia hivyo kistaarabu.
Tesha akaonekana kutathmini maneno yangu na hata kumwangalia Ankia, ambaye naye akamwonyesha ishara kwa macho kuwa sikutania kwelikweli, ndiyo akasema, "Mh! Aisee bro, sikuwa nimetegemea. Hii kali zaidi ya kali niliyokuwa nimeileta."
Nikaangalia pembeni tu.
"Kali gani nyingine?" Ankia akamuuliza.
"Nimeambiwa Chalii Gonga amekufa bwana," Tesha akasema hivyo.
Nikamwangalia usoni.
"Wewee! Lini?" Ankia akamuuliza hivyo.
"Sijajua. Yaani moja juu ya lingine, Chalii amekufa, na sasa hivi nimesikia yule mke wake amekamatwa. Sijui amehusika na hayo mauaji?" Tesha akasema hivyo.
"Mauaji? Kumbe Chalii ameuliwa? Yaani... huyo Bertha ndiyo amemuua mume wake?!" Ankia akashangaa.
"Ndiyo navyosikia, sina uhakika. Kulikuwa na bonge la msako leo huko mbele Kariakoo, Sinza, Mbezi, Kinondo, wapi, yaani... mapolisi walikuwa wanazunguka mno leo. Wamewakamata wengi! Ishu inaonekana ni za mambo kama madawa ya kulevya, hawa madada poa sijui na mashoga, wameunganisha yote mpaka kwenye madangulo yao huko, na huyo mke wake Chalii... amekamatwa..." Tesha akasema.
"Umeyasikia wapi?" Ankia akamuuliza.
"Bobo kaniambia. Habari ya jiji zima sa'hivi. Usiangalie tamthilia leo, angalia habari," Tesha akasema hivyo.
"Mh! Haki ya Mungu. Kama Chalii amekufa na Bertha kakamatwa, nani atasimamia Masai sasa? Hesabu si ni zao?" Ankia akauliza hivyo.
"Watajua tu. Nitamuuliza tena Bobo," Tesha akasema.
"Eeh, kweli ngoja na me nimuulize," Ankia akasema.
Nilikuwa nimetulia tu utafikiri sikujua kuhusu hayo mambo, maana ni mada ya muda mfupi nyuma ndiyo hasa iliyokuwa ikizunguka kichwani kwangu.
"Si ulikuwa huko leo kaka?" Umeona vurugu-vurugu?" Tesha akaniuliza.
"Eeh, nimeona," nikamjibu hivyo kifupi tu.
"Oy, kaka... hii ishu ya da' Mimi, we' jua tu kwamba me niko peace. Sawa? Nilikuona chizi mwanzoni, na... bado nakuona kama chizi, ila... fanya unavyoona kuwa sawa. We' ni mtu mzima. Ukitaka kuendelea kumtongoza, mjaribu. Akiendelea kugoma... usifosi. Unamwacha tu. Maana akiwaga hataki kitu, ndo' hataki. Kama tu kwa yule jamaa mwingine. Hivyo yaani," Tesha akanipa ushauri.
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
Akanisogelea na kunishika begani, naye akasema, "Sikia JC. We ni blood. Nakukubali kinoma. Tumesaidiana kwa vingi na kufanya ujinga mwingi, ila kwa hili najua uko serious. Lifanye serious kweli. Nampenda dada yangu. Kama kweli na we' unatafuta kutulia halafu umempenda Miryam, basi fight. Huwezi jua. Akikukubali mwishowe, mambo yanaweza yakawa mazuri zaidi. Unaweza ukaoa kwetu kabisa."
Akanifanya nitabasamu kwa kufarijika, naye akatabasamu pia.
"Ahahah... itakuwa poa sana. Tesha, ila usije kumwambia mtu mwingine kabisa kuhusu hii, eti? Hata dada yako usimwambie kama unajua," Ankia akasema hivyo.
"Dah, Ankia anaku-support! Ahah... usijali mama, naelewa. Sitamwambia mtu yeyote," Tesha akasema hivyo.
Nikamwangalia usoni na kusema, "Asante Tesha. Kwa kuwa mwelewa. Samahani pia, nilikasirika mpaka..."
"Nini, ukataka kunipiga ngumi? Tungeziruka hapa hapa, we! Najua taekwando," akasema hivyo kimasihara.
"Unaniacha wapi? Ni meza na TV za Ankia ndo' zingeumia," nikamwambia hivyo kiutani.
"Ahahah... tungevuruga sebule nzima, halafu tungemwacha aisafishe, sisi haooo... Masai," Tesha akasema hivyo.
"Nyooo... thubutu!" Ankia akamwambia hivyo.
Sote kwa pamoja tukacheka kidogo kwa furaha, nami pamoja na Tesha tukaunganisha viganja vyetu hewani na kuvutana, tukikumbatiana kwa bega kishkaji na kisha kuachiana tena.
Tesha akanipiga kiasi begani na kusema, "Komaa kaka. Nenda kwa akili tu, Mimi anaweza akakupa chance. Ila, itakuwa kwa msoto."
Nikatikisa kichwa kuonyesha uelewa.
"Yupo nyumbani tayari?" Ankia akamuuliza.
"Yupo eeh. Si utakuja baadaye JC?" Tesha akauliza.
"Yeah, nitakuja kusalimia," nikamwambia.
"Fresh, uje. Nilikuwa naenda kuchukua na Magnesium kwanza hapo dukani, tumbo linajaa migesi tu, kujamba sijambi. Ndo' nikaona nipite..." Tesha akasema hivyo.
"He! Wewe, em' toka hapa usije kunichafulia hali ya hewa ndani kwangu. Nenda huko!" Ankia akamwambia hivyo kiukali wa kimasihara.
"Aaa, tulia basi niachie hapa hata kimoja tu," Tesha akasema hivyo kiutani.
Ankia akasonya na kusema, "Shenzi, em' nenda kajambie huko!"
Akaanza na kumsukuma kabisa ili aondoke, naye Tesha akacheka na kunionyesha ishara ya kwa heri.
Nikabaki tu hapo nikiwa natabasamu baada ya kujisikia faraja kutokana na kuungwa mkono na Tesha pia katika ishu yangu ya kumpenda Miryam, na baada ya jamaa kuondoka, Ankia akanigeukia na kuachia tabasamu la ushindi eti, nami nikatabasamu pia na kuamua kuelekea tu chumbani kwangu. Angalau nikawa nimepunguza stress kidogo baada ya Tesha kuniunga mkono pia.
★★
Saa moja haikukawia kuingia, na mimi nilikuwa chumbani tu nikiwa nimetumia muda mfupi kuiweka akili yangu sawa juu ya mambo ambayo yangefuata baada ya visa vyangu pamoja na madam Bertha kuwa vimefikia ukomo wake. Kwa sasa umakini wangu wote ungetakiwa kuwa kwa Miryam, nifanye kila niwezalo kuhakikisha anakiri kuwa na hisia za kimapenzi kwangu, hata kama ingenihitaji kumroga ningefanya hivyo. Siyo kuroga kwa waganga, kuroga kwa mapenzi. Angeelewa tu!
Ikiwa inakimbilia kuingia saa mbili, nikaamua kutoka kwa Ankia ili nikaisalimu familia ya bibie Miryam hapo kwake, na kwa wakati huu Ankia alikuwa ameshaanza kupika zake wali na nyama. Nikamwacha tu na kwenda hapo kwa marafiki zetu, na kama ilivyokuwa jana, nikawakuta wanafamilia hao wakiwa wamekaa nje kwenye uvaranda wao ili kula upepo kidogo, wote wakiwepo isipokuwa Miryam na Shadya tu, na Shadya hakuwepo kabisa hapa kwa siku hii.
Nikasalimiana na mama wakubwa vizuri, Mariam akiwa amenisalimia pia na kuendelea kuwa bize na simu yake Tesha, na jamaa pia alikuwa hapo akipiga story na mama zao. Mariam alionekana kuwa makini sana kwenye kile alichofanya kwenye simu ya kaka yake, nami nikatambua kuwa alicheza game. Kwa sababu lilikuwa game la kuchangamsha ubongo kwa kupangilia maneno, lilifaa sana hali yake ya kutakiwa kuendelea kuimarisha uwezo wake wa kufikiri, na kwa hilo nikawa nimempa kongole Tesha kulifanya kwa niaba yangu.
Bi Zawadi akamwambia Tesha, "Mfatie mwenzako kiti."
"Ah, hamna shida, ngoja nikafate mwenyewe. Nataka kumsalimia na Miryam. Si yupo ndani?" nikasema hivyo.
"Eee, yupo jikoni anapika. Mhm... tunategea kama kawaida ili atushushie msosi wa maana," Bi Jamila akasema hivyo kama vile ananinong'oneza.
Nikatabasamu kiasi kumwambia, "Sawa. Nakuja."
"Haya," mama wakubwa wakaitikia hivyo kwa pamoja.
Nikaangaliana na Tesha kwa ufupi, ambaye akanitikisia nyusi kama kunipa ishara ya 'nenda,' akinipa kichwa kwenda kumwona dada yake ili nikajaribu kuweka mitambo sawa. Nikamtikisia kichwa pia na kuingia tu huko ndani, nami taratibu nikaelekea mpaka upande wa jikoni na kusimama pale pale ambapo nilisimama pamoja na mwanamke huyo jana alipotaka kunilazimisha nichukue pesa zake, na hapo nikawa nimemwona humo jikoni.
Miryam alisimama usawa wa kaunta la jikoni mwanzoni, pembeni yake likiwepo jiko lao lililowekewa sufuria lililofunikwa na kuonyesha kuchemsha chakula fulani. Kwa mtazamo wa haraka alikuwa akipika ndizi na samaki, na hapo aliposimama ndiyo alikuwa akikatakata viungo kwa ajili ya kuchanganyia pamoja na ndizi zikishachemka vya kutosha. Alikuwa amevaa T-shirt la mikono mifupi lenye rangi mbalimbali pamoja na khanga iliyomsitiri vyema kutokea kiunoni, na nywele zake alizifunika kwa kinguo-kofia cha satini.
Nikaendelea kusimama hapo hapo tu na kumwangalia. Nilifurahi sana moyoni kumwona. Na najua tayari alikuwa ameshatambua uwepo wangu sehemu hiyo, lakini hakugeuka kuniangalia hata mara moja. Nikatabasamu kiasi baada ya kukumbuka nilivyomtania kidogo jana kwa kusema kofi la mpenzi haliumi, na mpaka sasa bado alionekana kuwa tayari kunilabua kofi kabisa kisawasawa kama ningemfanyia mchezo.
Nikajisogeza tu mpaka karibu kabisa na mwingilio wa humo jikoni, pakiwa na mwonekano safi na vyombo vilivyopangiliwa vyema kwenye makabati ya ukutani, nami nikaegamia ukuta usawa wa sehemu aliyokuwa amesimama, na hakuniangalia hata mara moja kwa kukazana kukatakata karoti.
"Za leo Miryam?" nikamsalimia.
Akabaki kimya tu kama vile hajanisikia.
"Umepata habari kuhusu yaliyotokea leo?" nikamuuliza.
Kimya.
"Utakuwa umesikia. Maaskari waliyoyafanya jijini leo kuwakamata watu wengi kwenye biashara haramu na nini... hiyo ndiyo ilikuwa mishe yangu. Wale niliokuwa nakwambia... wamekamatwa leo. Si unaona? Nimefanikiwa kama nilivyosema," nikamwambia hivyo.
Akaendelea tu na kazi yake kwa kuonyesha hajali.
"Oh, usiwe grumpy namna hii Miryam, nimekuja tu kukusalimia," nikamwambia hivyo kwa upole.
Akaendelea kubunda tu, na akikatakata viungo kama vile ana kisirani.
Nikatabasamu kiasi na kuangalia chini, nami nikasema, "Najua una sababu nzuri ya kunichunia, lakini haifai bwana. Me bado rafiki yako, na ni daktari wa Mamu. Unajua tutapaswa kuongea tu."
Nikiwa nimemwangalia sasa, akaacha kukatakata karoti na kufunua sufuria la ndizi kwa kasi, halafu mfuniko akauelekeza kwangu kwa makusudi huku akijifanya kuchungulia ndizi zake kwa umakini, na mvuke ukawa umenifikia usoni. Nikatabasamu kiasi na kusogea nyuma kidogo, naye ndiyo akalifunika na kurudi kukatakata vitu vyake.
Nikaegamia ukuta tena na kumwambia, "Usiwe hivyo. Kuna kitu nahitaji kukuomba... uniruhusu nifanye."
Kakabaki kimya tu na kuanza kupalanganisha vyombo huku na huko.
"Kesho baada ya birthday, namaanisha, kesho-kutwa... nilikuwa nataka kwenda kumwona mama mara moja kule nyumbani. Ikiwa itakuwa sawa kwako, naomba niende na Mamu," nikamwambia hivyo kistaarabu.
Akawa akiendelea kukatakata, nyanya wakati huu, ikiwa kama vile hakujali nilichotoka kusema.
"Ni... mama ndiyo ameomba niende naye. Angependa kumwona Mariam," nikamwambia hivyo kwa upole.
Miryam akasitisha kukatakata nyanya na kuleta macho yake taratibu upande wangu, lakini hakuniangalia usoni. Hapo nikawa nimevuta umakini wake, najua alijiuliza mama yangu alitaka kumwona mdogo wake kwa nini.
Nikasema, "Niliwahi kumzungumzia Mariam kwa mama yangu, na alipenda... alitamani aje kumwona maana, mama yangu ana-relate na shida kama zilizompata Mamu. Anataka tu kuona progress yake maana amempenda hata kabla hajakutana naye..."
Miryam akarudisha umakini wake kwenye ukataji mboga bila kunipa itikio lolote.
"Nikwambie kitu? Hizi siku chache zilizopita, tokea yule jamaa alipotukuta kule Jogoo na kutishia kukuumiza mbele yangu... yaani mambo yameenda faster like crazy. Kila kitu juu ya hiki na hiki, imekuwa overwhelming. Nimeponyoka kifo karibia mara tatu Miryam, hata leo... ilikuwa karibu nife..." nikamwambia hivyo.
Akaendelea tu kufanya kazi yake kama hajali.
"Kuna... hisia fulani ndani yangu ilikuwa inanifanya nisihofie kufa kwa kufikiri labda mwisho wangu tu ndo' umefika... lakini baada ya kuipata hii nafasi ya kuendelea kupumua, mpaka sasa niko hapa tena... nimegundua huo mwisho bado sana. Bado ninatakiwa kuwa na wapendwa wangu, kufanya mengi kwa ajili ya wote naowapenda, nyie wote... hasa wewe Miryam..." nikamwambia hivyo kwa hisia.
Akasitisha tena kukatakata nyanya ambazo tayari zilikuwa zimeshakatwa mpaka zikachoka, naye akaonekana kuweka umakini kwangu zaidi.
"Kwa nini? Unawaza kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu ndiyo kwanza safari yangu pamoja nawe imeanza, Miryam... na hii nafasi ya kuendelea kuishi niliyoipata ndiyo itakuwa msingi mzuri sana kwangu kuhakikisha naufikia mwisho wa hiyo safari pamoja nawe... no matter what. Baada ya kila kitu kilichotokea leo... sitaki kingine tena zaidi ya jambo hilo. Yaani... haitapita siku yoyote kutokea hapa ambayo sitakukumbusha namna navyokupenda, uwe tayari kupokea hilo ama usiwe tayari, ndiyo purpose yangu kutokea hapa Miryam. Na sitaacha... sitaacha mpaka nihakikishe uko tayari kuufungua moyo wako kwangu..." nikamwambia hivyo kwa hisia sana.
Miryam akapandisha macho yake mazuri hatimaye na kunitazama usoni kwa umakini sana, akionekana kuitikia maneno hayo kwa mtazamo wa aina fulani tofauti kutokana na jinsi ambavyo niliyasema bila utani, nami pia nikaendelea kumwangalia kwa hisia.
Macho yake bado yalikuwa yamejaa mashaka makubwa kunielekea, labda akidhani kwamba bado nilikuwa najitafutia tu faida za kizembe au kucheza na hisia zake, lakini muda siyo mrefu nilitaka kumthibitishia kwamba alikuwa amekosea. Nilimaanisha kila neno nililomwambia, na ningehakikisha kweli anakuja kuliona hilo na kutokuwa na jinsi tena ila kuniruhusu nimfanye awe wangu. Yaani hilo ndiyo lilikuwa limebaki. Kama nilivyosema, angeelewa tu!
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★
Full Story WhatsApp or inbox
Whatsapp +255 678 017 280
Chawa kama chawa wa JC 😂😂😂Fita Ni Fita Muraaa JC mie timu yako hadi FESTO akuue tuko pamoja
JC ushayavulia nguo maji kwahiyo utayaoga tu hata kama ni ya baridi kiasi ganiMIMI NA MIMI 2
A Story by Elton Tonny
Familia, Urafiki, Mapenzi, Kazi, Siri, Tamaa, Hila, Usaliti, Ukatili, Mauaji, Mambo Yasiyotazamiwa
R-rated 18+
Enjoy!
★★★★★★★★★★★★★★★★★
SEHEMU YA KUMI NA NANE
★★★★★★★★★★★★★★★★★
Tukaendelea kuangaliana kwa sekunde chache mpaka ilipokuwa wazi kwamba wengine walikuwa wameanza kurudi ndani, naye Miryam akaacha kuniangalia na kugeuzia shingo yake huko jikoni ili asinitazame tena kabisa. Nilikuwa sijapata jibu kuhusiana na ombi langu la kwenda na Mariam kumwona mama hiyo kesho-kutwa, lakini labda hilo lingepaswa kungoja kidogo, maana hapo nilikuwa nimetoka kumshushia bomu zito kwa maneno yenye hisia sana.
Nikaamua tu kumwacha hapo na kwenda sebuleni kujiunga na wengine, Tesha akiwa anataka sote tutazame taarifa ya habari ili tuone matukio yaliyofanyika siku hii tokea asubuhi. Sasa hivi Mariam ndiyo akawa amerudisha umakini wake kwangu baada ya game kumboa, akitaka nikae pamoja naye ili tuambiane hiki na kile, hivyo nikaketi hapo sebuleni karibu yake na kushiriki maongezi ya hapa na pale pamoja nao wote.
Taarifa ya habari ilipoanza, Miryam pia akawa amekuja hapo sebuleni kutazama, na kweli mengi ya matukio ya leo yalionyeshwa kwa vipengele kama vitatu vya taarifa zilizofatana. Moja ikawa imeonyesha picha za Chalii Gonga na hata kutaja majina kama ya Sudi na Ismail, ambao walikuwa na sehemu fulani maalumu katika mfumo wa kisiasa wa wilaya ya huko Kinondoni. Tesha ndiye aliyevutiwa zaidi na mambo haya kwa sababu yalihusiana moja kwa moja na Masai, sehemu ya karibu na kwao iliyokuwa ya mmiliki aliyehusiana na hayo mambo, kwa hiyo story zikaendelea kuongezeka na kuongezeka.
Miryam alikuwa akienda jikoni na kurudi tena sebuleni, kisha ndiyo akaja kwa mara nyingine na kukaa kabisa. Ilionekana chakula ndiyo kilikuwa kwenye hatua nzuri ya kuiva, na bibie alikuwa kimya karibia muda wote kwa kujipa ubize kwenye simu yake. Tesha akawa amenipa ishara kwa uso kama kuuliza 'vipi?' nami nikamwonyeshea ile ya 'bado bado,' dada yake alikuwa mgumu. Ndiyo jamaa akahamishia mada kutoka kwenye masuala ya wakina Chalii na kuanza kuzungumzia kuhusu sherehe ya kuzaliwa Bi Zawadi kesho.
Wote kwa pamoja tulikuwa na hamu kubwa kwa hiyo siku ya kesho, Mariam sanasana kwa sababu kulikuwa na kitu alichokuwa na hamu ya kufanya kesho ambacho nilijua mimi pekee, na nikamshawishi aendelee kukiweka moyoni tu ili kesho aje kukifanya vizuri sana. Bi Zawadi alikuwa anataka kwenda kutengeneza nywele zake kesho saluni nakwambia, yaani alitaka kupendeza haswa, na Miryam akamuunga mkono kwa hilo akisema angekwenda na Shadya baada ya mwanamke huyo kufika hapa. Na Mariam naye akataka kutengenezwa nywele eti!
Tukiwa katikati ya hayo maongezi ndiyo nikaona nitumie fursa hiyo kuzungumzia kuhusu ishu ya mimi kwenda kumsalimu mama yangu, na kutaka niende pamoja na Mariam. We! Iliwapa wengine furaha sana kujua kwamba nilikuwa hadi namwongelea binti huyo kwa mzazi wangu mpaka akampenda, na walionyesha kupendezwa sana na wazo hilo, lakini Miryam hakuwa ameridhia bado. Hakukataa, lakini hakuonekana kutaka.
Uzuri Mariam alikuwa na hamu ya kwenda kuzurura tena kama tulivyofanya ile Jumanne kule kwenye kisinia, hivyo utayari wote wa kwenda aliuonyesha, na sidhani kama kwa hapo dada yake angeweza kuleta upinzani. Lakini Miryam akawa amesema ingefaa tukienda pamoja na Tesha, nami sikuwa na tatizo kwa wazo hilo. Alikuwa anajifanya eti yuko makini kumlinda mdogo wake kana kwamba hakuniamini, ila najua hizo zote zilikuwa swaga za kisirani chake tu.
Tesha alikuwa tayari kama kawaida, akiwa pia na hamu ya kwenda kupaona "kwetu," kwa hiyo jambo hilo likawa limehalalika hatimaye. Mariam alitaka nimwelezee nyumbani kwa mama yangu palivyokuwa, nami nikamwambia asiwaze, angepaona tu, na angefurahia sana. Hii saa mbili ilikuwa inaenda taratibu tu, na katika harakati za Miryam kukaribia kuivisha huko jikoni, nikawa nimepigiwa simu, Adelina akiwa ndiyo amenitafuta.
Nikapokea hapo hapo, na mwanamke huyo alitaka tuzungumze kwa urefu zaidi, hivyo nikamwambia anipe dakika chache: ningempigia tena. Inaonekana alikuwa na jambo au mambo ya muhimu aliyotaka kuniambia, kwa hiyo nikawaomba marafiki zangu samahani ya kuhitaji kuaga, nikisema kulikuwa na mtu aliyetaka kuzungumza nami ana kwa ana kwa hiyo ningehitaji kuondoka. Malalamiko kutoka kwa Bi Zawadi na hata Mariam kuhusu mimi kukimbia mapema hivyo yakaanza, lakini mwishowe wakanikubalia na kunitakia usiku mwema.
Nikaondoka upesi hapo bila ya kuwa nimemuaga Miryam maana kwa muda huo alikuwa jikoni bado, nikaelekea mpaka chumbani kwangu pale kwa Ankia, mwanamke huyo akiwa sebuleni anaangalia tu tamthilia na kuchat, nami ndiyo nikampigia Adelina na kuanza kuongea naye tena. Alikuwa anataka kunifahamisha kwamba askari Ramadhan alimjulisha yeye na familia yake kuhusu Bertha kukamatwa, akiwa ndiyo mhusika wa mauuaji wa Joy miezi miwili iliyopita, na kwamba jamaa alisema nilihusika sana katika kusaidia hilo kutokea.
Adelina ndiyo akawa anataka nimweleze ilikuwaje, na kwa nini sikuwa nimemwambia mpaka sasa hivi. Kwa hiyo nikamwelezea, nikigusia namna ambavyo watu hao wote kwa ujumla walikuwa hatari sana na ndiyo maana sikuwa nimemwambia mapema kuhusu yale niliyokuwa nimejiingiza kufanya. Niliwasaidia maaskari kuwakamata wale watu kwa maovu yao mengi, lakini kuna mambo mengine mabaya pia yalikuwa yametokea katikati ya hiyo jitihada ambayo sikutaka yamwathiri yeye na familia yake kivyovtote, ndiyo maana sikumwambia.
Nilikaa kuzungumza na huyu dada, yaani tuliongea kwenye simu mpaka akawa analia! Alilia kwa sababu ya kutambua kwamba huo muda wote nilikuwa nahangaikia haki ya kifo cha mdogo wake, na sasa ikawa imepatikana baada ya magumu mengi. Nikamtia tu moyo zaidi na kumwambia bado niko pamoja naye, na yeye akasema alithamini mno kujitoa kwangu.
Nikampa wazo la kujiunga nasi siku ya kesho jioni kwa ajili ya sherehe ya mama mkubwa wake na Miryam, ikiwa ni njia nzuri ya kukutana tena na kujitahidi kufurahia wakati mzuri pamoja, naye akasema angenijulisha ikiwa angeweza kufika. Tukaagana ikiwa imeshaingia saa nne kabisa, ndiyo nikaweka simu pembeni na kutafakari mambo kidogo.
Nilihisi kufarijika sana. Jinsi ambavyo watu waliniona kuwa kama mkombozi fulani hivi; Miryam kwa ishu za Joshua japo alipenda kununa-nuna, familia yake nzima kwa msaada niliompatia Mariam, Adelina kwa Joy, yule Kevin aliyetegemea nimsaidie kumuunganisha kwa dada yangu Jasmine, na wengine wengi tu niliokuwa nimejitahidi kuwasaidia, yaani ilinifanya nijihisi vizuri.
Lakini zaidi kwa kipindi hiki ni toka siku ambayo niliamua kuja huku Mzinga kwa ajili ya likizo na kukutana na Miryam, yaani ni kama vile ilipangwa, ili tu safari ya maisha yangu ichukue mkondo mpya na mzuri licha ya changamoto kuwa nyingi. Na sasa nilichokuwa nataka zaidi ni kufanikisha kumweka Miryam karibu yangu ili mkondo huo mzuri wa maisha ujae furaha tele, kwa kuwa ni yeye ndiye aliyekuwa amesalia katika kuiongeza, kama siyo kuikamilisha furaha hiyo.
Nikaamua tu kuelekea huko sebuleni kujiunga na Ankia na kupata msosi, nikiwa na hamu kwa yale ambayo siku ya kesho ingeyaleta katika kuendeleza safari yangu ya maisha kwenye mkondo huo mpya. Nahisi mambo mengi yangekwenda sawa kutokea hapa, iwe kwa raha ama tabu, najua kila kitu kingekuwa sawa tu.
★★★
Jumamosi asubuhi ikawadia, yaani ikafika. Mzee wa 'kila kitu kingekuwa sawa tu' nikaamka mapema, maana usiku uliotangulia nilijitahidi kusinzia mapema pia na kufanikiwa. Saa mbili tu usingizi wote ukawa umepaa, nami nikaona isingekuwa mbaya kuianza siku hii kwa kufanya kazi ya usafi wa ufuaji kwa nguo zangu chache.
Mambo yangekuwa mazuri sana baadaye najua, bila shaka hapo kwa Miryam maandalizi ya mapambo na mahanjumati yangeanza mapema maana watu ambao wangefika wangekuwa idadi ya maana, si unajua mtaani kwa waswahili? Hata kidogo ni kingi! Kwa hiyo nikabeba zangu tu jeans mbili na T-shirt chache, pamoja na viatu, kisha nikaelekea nje ili kuanza kazi. Ankia pia alikuwa ameshaamka, na yeye akawa anafanya usafi ndani ya nyumba na kisha kushughulikia chai.
Nikafua-fua hapo, huku nikichungulia kwa majirani zetu, na gari la bibie halikuwepo. Inawezekana alienda kazini mapema na angewahi kurudi, kwa hiyo tungekuja kuonana baadaye. Nikafua gwanda na viatu na kusafisha choo na bafu pia, kisha ndiyo ukafata usafi wa mwili wangu, halafu nikaingia ndani na kunywa chai kwa mkate pamoja na Ankia. Alinisifia kweli kwa namna nilivyopenda usafi! Yeye pia alikuwa anataka kwenda kufungua duka lake halafu baadaye aje kusaidiana na wanawake wengine kwenye upishi na nini hapo kwa Miryam, hivyo akawahi kuondoka akiwa amejipendezesha kiasi.
Mzee nikaendelea kukaa tu sebuleni, Dina akiwa ameanza kuchat na mimi, ile hamu ya kuniona leo akija huku ikiwa imeshaanza kumtekenya. Na yeye angepaswa tu kuja kuvunjwa moyo. Ikiwa imeshaingia mida ya saa tano, Tesha akanipigia na kuuliza kama nilikuwa hapa, na nilipokubali akaniambia anakuja. Hakukawia kweli, yaani dakika chache tu akawa ameingia ndani hapo na kukaa karibu nami sofani, akiwa na mwonekano wa kawaida tu kinyumbani.
Tukaanza kupiga story, akisema hapo kwao mambo yalikuwa yanaenda taratibu tu, na alikuwa amekwenda kuonana na Bobo kumwomba awaazime yale maspika makubwa kwa ajili ya muziki mnene, na Bobo alikuwa amemkubalia kwa kusema moja ingeletwa baadaye, maana na yeye alikuwa anakuja kwenye sherehe japo Masai ilikuwa na msiba wa Chalii Gonga. Yaani mzuka ungekuwepo kama wote maana hadi masela wangekuja, ila ndiyo tungepaswa kuweka pigo za kistaarabu kwa kuwa bibie Miryam asingependa uhuni mwingi hapo kwake.
Story zikageukia mambo ya maisha zaidi, akimwongelea Happy wake na kusema angekuja leo pia, na kuniuliza kuhusu mipango yangu na dada yake. Sikumwambia mengi maana bado ndiyo nilikuwa kwenye hatua za utongozi, zaidi tu kwamba ningeendelea kuwa na subira kwa ajili yake na kuona tungefika wapi. Akaanza ule mchezo wa kuulizia kuhusu mademu wa zamani, akitaka kujua ladha zangu zilikuwaje, nami nikaona nimwonyeshe tu baadhi ya wanawake ambao niliwahi kutoka nao kwa picha zilizokuwa kwenye simu.
"Dah! Kwa hiyo mpaka leo bado umewatunza tu wapenzi wa zamani?" akaniuliza hivyo.
"Naonaga uvivu kufuta, sometimes nafuta lakini nyingine huwa zinagoma kufutika," nikamwambia hivyo.
"Zinagoma? Yaani nini, picha hazitaki kuiacha simu? Unazingua..."
"Nazingua nini sasa? Kuna ubaya gani zikibaki kwanza?"
"Uba... we' fala kweli, yaani tuseme unampata da' Mimi halafu anazikuta, unajielezeaje?"
"Ahahahah... unanipa matumaini mazuri, asante. Ila we' unanionaje kwani? Naweza kuwa kolo kiasi hicho?"
"Aaa... utakuwa mjanja, au siyo?"
Nikamwambia, "Hakuna haja ya ujanja. Tuseme nikawa na dada yako kweli, akiona hayo makumbukumbu akataka niyafute, nayafuta. Haya mambo ya simu huwa yanazingua kweli, I know, kwo' ni vizuri kuijua nature ya mtu wako ili... unakuwa umeshachukua hatua fulani mapema. Nikijua Miryam hapendi yakae humo, nayafuta kabla hajayaona. Nitajitoa tu uvivu..."
"Si kunakuwa na app za kuficha?"
"Ndiyo, ila me huwa sifichi. Naonaga za kawaida tu, na hata unapita muda siziangalii. Lakini... siyo kwamba naziacha makusudi kweli. Huwa nina tabia ya kutunza video na picha zangu nyingi za gallery, Facebook, wapi... tokea zamani yaani, kwenye akaunti ya Google... kwa hiyo unakuta hata nilipokuwa nabadilisha simu...."
"Zinajirudisha tu," akamalizia maneno yangu.
"Eeeh, so sometimes naacha tu," nikapigia mstari.
Akaanza kupitia picha zangu nyingi na kukutana na watu wengi humo, nyakati mbalimbali, maeneo tofauti, naye alipokuwa akivutiwa na vingi akawa anauliza huyu ni nani, hapo wapi, na kile ni nini, nami nikawa namwelezea kuhusu pindi hizo na watu hao waliokuwa kwenye visa vya hapa na pale vilivyozunguka maisha yangu ya kipindi cha nyuma mpaka kufikia wakati huu.
Alikuwa akipendezwa zaidi na picha za wadada na wanawake fulani waliokuwa na mionekano mizuri, nikimwelezea sasa kuwa baadhi yao ndiyo nilikuwa nimepita nao kimahusiano na wengine wakiwa marafiki na madada, naye akawa ameifikia picha moja ya mwanamke mweupe na mrembo sana; nikiwa kwenye hiyo picha pia nimesimama pamoja naye.
Akauliza, "Na huyu ni nani?"
Nikaiangalia na kusema, "Dada'angu."
"Mzuri! Wa wapi?"
Nikamkata jicho la ukali, kimasihara tu lakini.
"Acha hizo, we' si useme tu? Unaweza ukawa unaniangalia shem na me hapa kwa hawa mabinamu zako, maana inaonekana kwenu damu nzuri kishenzi kuliko hata kwetu," Tesha akasema hivyo.
"Hivi Happy si anakuja leo, mjinga wewe?"
"Ah, Happy mweke pembeni bwana. Niambie huyu ni nani..."
"Tuliza mapepe, huyo siyo kikuku, ooh! Jasmine huyo," nikamwambia.
"Aaaa... dada'ako wa damu kabisa?"
"Eeh."
"Dah! Ndo' maana. Mzuri kama wewe tu. Si ndo' huyu ulisema anakaribia kujifungua?" akauliza.
"Eeh, anakaribia sana."
"Anaishi wapi yeye?"
"Kwake ni huko Sinza pia. Ila sa'hivi yupo Goba kwa wazazi," nikamwambia.
"Ahaa... kwa hiyo kesho tukienda na Mamu kwenu, atakuwepo?"
Nikatikisa kichwa kukubali.
Akaendelea kuangalia picha kadhaa za Jasmine, kisha akasema, "Fresh mwanangu. Umeishi maisha ya maana sana."
Alisema hivyo huku akinirudishia simu, nami nikaipokea na kusema, "Acha zako. Kawaida tu."
"Aa wapi. Hao mademu wote, sijaona mwenye sura ya baba yaani na shepu vipande. Ulikuwaga unajichagulia pisi kali kali tu..."
"Wengi wao walikuwa wananifata. Ila nilipita nao kwa busara, napenda sana usafi kwo' niliangalia usalama nisije nikaambukizwa madude ya ajabu."
"Ahahah, basi inaonekana hupendi kutumia pira kama mimi."
"Yeah, sipendelei..." nikamwambia.
"Halafu unajua nini kaka, nina shida kidogo, inabidi nikuombe kaushauri ka kitiba."
"Nambie."
Akasema, "Yaani mwana, huku hivi sa'hivi yaani, kwenye ngozi ya kafuko kalikobebea wanangu huku..."
"Ahahahah..."
"Usicheke sasa, nisikie..."
"Ahahah... haya niambie..."
"Mwana, yaani inakuwa kama... inamomonyoka sijui? Yaani ile ngozi ya kawaida kama inapukutika, halafu inayobaki inawasha kishenzi. Sometimes hadi panauma..." akasema hivyo.
"Itakuwa ni fungus," nikamwambia.
"Dah! Sidhani ila, ilianza kidogo, sa'hivi inatapakaa mpaka inapanda. Yaani muda mwingine nikikuna, panauma kama panawaka moto vyeee..."
"Okay sawa, kwanza, jitahidi usiwe unakuna, hata pakiwasha vipi. Unaweza ukachubua ngozi. Halafu ukioga, hakikisha unajikausha vizuri huko chini pabaki pakavu. Hiyo huwa inatokana na unyevu unaobaki, ama friction pakiwa pakavu na joto kali sana, na uwe msafi. Badilisha boksa, usiwe unavaa moja wiki nzima, boya wewe," nikamwambia hivyo.
"Ahahahah, me siyo mchafu kama hivyo. Kwa hiyo hapo ndo' tatizo litaisha?"
"Ee, hayo ndo' matunzo mazuri. Ila hiyo kitu yako, tafuta nanilii... nenda duka la dawa tafuta Skyderm, uwe unapaka kila ukitoka kuoga. Ni vizuri ukipaka mara mbili kwa siku. Ikiwa Tesha ataogaga mara mbili kwa siku sasa," nikamwambia hivyo.
"Ah, hivi unanionaje?" Tesha akasema hivyo, nasi tukacheka kidogo.
"Jitahidi sa'. Ukipuuza ikakomaa, ndo' kote kataisha ffff! Kama pangusa," nikamwambia hivyo.
"Ahahahah... we' daktari mmoja fala sana," akaniambia hivyo.
Nikacheka kidogo.
"Sawa, nitaitafuta. Ska-nini umesema?" akauilza.
"Skyderm."
"Ahaa, poa. Ila itabidi niiweke kichwani kama 'sikai na demu' ili nisisahau," akasema hivyo.
Nikamkata jicho.
Akacheka na kusema, "Wengine viingereza havipo fresh kichwani."
Nikatikisa kichwa na kucheka kidogo kwa pumzi. Uhuni tu ndiyo ulikuwa umemjaa!
Tesha akafungua simu yake kusoma ujumbe mpya ulioingia nadhani, kisha akasema, "Sister amerusha hela ya keki, ya hao kusukia, na madikodiko mengine ya jioni. Inabidi nikatoe... halafu niende mapema kufata keki nzuri huko Mbagala."
"Ahaa, sawa. Kumbe sometimes huwa anakutumia hela ndo' mnanunua chakula?"
"Mara moja moja kama anakuwa hajaacha hela, au kama vitu vimeisha ndani. Ila hii si sikukuu? Hao wakishaanza kujazana hapo kupika na nini, kila kitu kinatakiwa kuwepo... na alitakiwa kuacha hela asubuhi, ila naona akawa amesahau. Halafu sa'hivi naona anasahau-sahau kweli, sijui kwa nini," akasema hivyo.
"Kusahau kuacha matumizi?" nikauliza.
"Siyo matumizi tu, hata mambo mengine. Sometimes yaani... anakuwa kama anawaza sanaaa, wakati lile janga la Joshua sa'hivi limeisha. Nilidhani angechill, lakini naona kama amezubaa zaidi... mpaka anakuwa ka' kapotea yaani," akaniambia.
"Kwa nini unasema hivyo?"
"Ndiyo hali halisi. Jana kwa mfano, ulipoondoka, tulikuwa tunakula wote mezani. Yaani dada akawa anakula taratibu, halafu ameangalia upande mmoja kama anawazaa. Mh? Me nikawa namcheki tu. Ma' mkubwa akimsemesha, anatikisa tu kichwa. Mpaka ahahah... kuna muda ma' mkubwa akamwomba amsogezee bakuli lenye ndizi, Mimi akampa bakuli la samaki!" Tesha akaniambia hayo.
Sote tukacheka kidogo.
"Ikabidi ma' mkubwa amuulize 'Miryam nini?' 'Kuna tatizo lolote kazini labda?' Akasema hamna. Yaani hata kula anakula kama hataki, utafikiri hana amani. Me nahisi kuna jamaa atakuwa ameanza kumchanganya akili," akaniambia hivyo.
Nikatazamana naye kwa yale macho yenye kujuana, maana naelewa alisema hivyo kwa makusudi, nasi kwa pamoja tukacheka kidogo. Mwenzangu alikuwa akitania, lakini ikiwa kama alichokisema kilikuwa sahihi, basi huyo jamaa alikuwa mzee mwenyewe hapa, na hiyo ingemaanisha kweli nilikuwa nimeanza kuichanganya akili ya bibie baada ya yale niliyokuwa nimemwambia hiyo jana.
"Tuje tumfatilie tujue huyo jamaa ni nani," Tesha akasema hivyo kimasihara.
Nikamwangalia na kuuliza, "Halafu tukishamjua?"
"Ishi? Tunampiga! Kwa nini anasababisha Mimi ampe samaki ma' mkubwa wakati amemwomba ndizi?" Tesha akaongea kama hana akili.
"Ahahahah... we' ni mjinga sana. Nenda katoe hiyo hela uwapelekee. Ukitaka kwenda kutafuta keki nishtue nikusindikize," nikamwambia hivyo.
"Au siyo? Fresh kaka, ngoja niingie kwa mangi hapo. Afu' tutanunua na maputo," akasema hivyo na kunyanyuka.
Nikamtikisia kichwa kukubaliana na hilo.
Akaondoka kuelekea huko dukani ili aitoe pesa, akiniacha nimekaa tu hapo nikimuwaza dada yake. Aliyoyasema hapo mwishoni kuhusu Miryam yalinifanya nihisi kuringa sana ijapokuwa ilikuwa ni uwezekano tu. Ni kitu ambacho kilifanya motisha yangu ipande juu zaidi ili nisikate tamaa kamwe kumwonyesha mwanamke huyo namna ambavyo nilimpenda, na kwa kuendelea kutokea hapa ingekuwa ni kuongeza visa juu ya visa mpaka aingie ndani ya penzi langu alilokuwa akijitahidi kuliepuka.
★★
Basi, Tesha akawa amefanikiwa kufata vitu hivi na vile na kuvipeleka kwao, kisha ndiyo akaja kunipitia, nasi tukaenda Rangi Tatu huko kutafuta keki moja nzuri. Aliona vyema tukiingia eneo la Dar Live na kutafutia keki kwenye duka mojawapo huko, nasi tukapata moja nzuri sana na kufanikisha kupata usafiri wa bajaji kuibeba na kuipeleka mpaka kwao tena. Tukaiweka kwenye friji bila kuifungua, na kufikia muda huu, bibie Miryam alikuwa amekwisharudi hapo kwake, na akijifungia tu huko chumbani sijui kufanya nini.
Ilikuwa imeshaingia mida ya saa nane tayari, na Bi Zawadi, Mariam, pamoja na Shadya walikuwa wamekwenda saluni huko baada ya mama Chande na wanawake wengine kuwa wamefika hapo kuanza shughuli za mapishi. Kilichokuwepo hapo kwa wakati huu ikawa kufunga maputo mengi kwa ajili ya kupendezesha sebule, maana ndani palikuwa pamepangwa vizuri kweli, na muziki ungetakiwa kuanza kupigwa, kwa hiyo Tesha akampigia Bobo kumuuliza kuhusu ile ishu ya spika.
Inaonekana kuna mambo mengi ambayo Bobo alikuwa anashughulikia, kwa hiyo akawa amemwambia Tesha aende hapo Masai ili wapangane vizuri, na kwa hilo jamaa akakubali. Tesha alipenda kuniita usawa wa dirisha kuwachungulia wanawake waliokuwa hapo nje, lakini nikawa namwambia aache upuuzi na anisaidie kumaliza kuyafunga maputo maana muda ulikuwa unaenda. Ndiyo dada yake akawa amekuja sebuleni kutokea chumbani kwake na kutaka kuiona keki, naye Tesha akamwonyesha.
Miryam alikuwa amebadilisha mwonekano wa nywele zake, na tena siyo kubadilisha yaani, kufumua tu. Alikuwa ameuondoa ule msuko wake wakati huu, akibakiza nywele zake ndefu na laini alizokuwa amezichana vizuri mpaka kugusa mgongo wake, na sijui alikuwa anazipaka nini kuzifanya ziwe ndefu na laini namna hiyo, yaani ungefikiri amevaa wigi la nywele za wazungu kumbe zilikuwa za kwake kabisa. Na hivi alikuwa mweupe! Alivaa gauni refu jeupe la kitambaa kizito wakati huu, lililofanya unawiri wake mwilini uonekane vyema.
Nikatuliza tu mapepe ya hisia zangu na kujitahidi nisimtazame mno. Nikaona nitulie sofani na kuendelea kujaza maputo na kuyafunga mengi kwa pamoja, hapo bibie akiwa anazungumza na mdogo wake juu ya hili na lile, nami nikawa nimepigiwa simu na Adelina. Mwanamke huyo akaniambia kwamba asingeweza kufika leo kutokana na kubanwa na ishu fulani, na akaomba radhi kwa hilo. Nikamwambia tu haina shida, tungekuja kuonana siku nyingine, na baada ya hapo tukaagana vizuri tu.
Miryam akaenda hapo nje kwa wanawake wengine kuwaunga mkono kidogo, na walikuwa wakiongezeka tu, wengine wakija mpaka ndani na kujipitisha-pitisha hapo huku wakiburuza miguu na makalio yao ndani ya madera, na hii ilikuwa sehemu ya burudani nzuri kwa Tesha aliyependa kuwachokoza kwa utani wale aliozoeana nao, lakini mimi sikuwa na shobo hata na mmoja isipokuwa mama Chande kidogo; ambaye alinichangamkia na mimi kumsemesha kwa utani pia.
Bibie Miryam akawa ameenda zake chumbani tena, naye Tesha akasema anaenda sasa hapo Masai ili ahakikishe spika kubwa inakuja, kwamba nimalizie tu kuyafunga maputo yaliyobaki ili yeye awahi, nami nikamkubalia. Akaniacha hapo na kwenda huko Masai upesi. Nilikuwa nayafunganisha maputo yaliyojaa kwa mtindo fulani uliounganika wa kamba moja, ambayo mwishoni ikabaki ndefu vya kutosha ili niyafunge vizuri kwenye kiyoyozi hapo juu. Nilikuwa na lengo fulani la kiburudani pamoja na Tesha kwa kufanya hivyo.
Kwa hiyo nikachukua kiti kutoka dining na kupanda, kisha nikayafunga hapo juu kwa uangalifu mpaka kukifunika kiyoyozi kabisa. Nikajaribu kukiwasha, kwa mwendo wa taratibu tu, na kiyoyozi kikaanza kuzunguka bila kuyafanya yapasuke wala nini. Ilipendeza sana kuona jinsi yalivyozunguka kwa kunesanesa huku na huko, nami ndiyo nikazima kiyoyozi na kurudisha kiti mahali pake, halafu nikaanza kufagia na kukusanya mabaki ya karatasi hizi na zile za mapambo hayo kwa ajili ya kutupa.
Nikiwa ndiyo nimemaliza kuyakusanya, nikamwona bibie Miryam akitokea chumbani kwake, nami nikamtazama kwa umakini. Alikuwa ameshikilia yale mapambo ya vitambaa virefu yenye rangi nyeupe na nyekundu kuendana na rangi ya maputo, na alielekea upande wa chumba chake Tesha huku akimwita kwa sauti yake tamu kupindukia.
"Tesha... Tesha..."
Yaani ilikuwa kama analiimba hilo jina!
Hakuangalia upande wangu kabisa, na kabla hajapitiliza nikasema, "Ameenda hapo Masai mara moja, anakuja."
Ndiyo akasimama na kunitazama kwanza, kisha akaangalia juu na kuyaona maputo yale mengi niliyokuwa nimeweka na kunitazama tena usoni.
Nikamwambia, "Pamependeza, eti? Cheupe atafaidi kuyapasua."
Akaacha kuniangalia na kuelekeza uso wake kwenye mapambo aliyoshika.
Nikawa nimeelewa kwamba alitaka kuyafungia sehemu fulani na alihitaji Tesha amsaidie, nami nikamuuliza, "Unataka kufunga hizo? Leta nikusaidie..."
Nikaweka mabaki yale pembeni na kumfata moja kwa moja ili nichukue mapambo hayo, lakini akakwepesha mikono na mwili wake kwa nguvu na kunipita, akielekea upande wa dining. Nikaendelea kumtazama tu, akiwa kama amenuna yaani, naye akabeba kiti kimoja na kuelekea upande wa dirisha la sebuleni, kisha akapanda na kuanza kufunga mapambo hayo kwenye mabomba yaliyobeba mapazia.
Nikatabasamu tu kiasi, kwa kufurahishwa na kakisirani kake alikokuwa ananionyesha bado, nami nikaamua tu kuchukua yale mabaki na kuyaweka kwenye mfuko uliokuwa umebeba maputo, kisha nikayapeleka nje kwa kupitia mlango wa nyuma wa nyumba hii ili niwaepuke wanawake kule mbele. Walikuwa wamejazana yaani, eti wote wanapika, na baada tu ya mimi kuyaweka mauchafu hayo kwenye fuko nikarudi ndani tena ili nichukue simu na kuondoka kwa sasa; yaani niende kwa Ankia.
Nikafika ndani na kukuta Miryam akiwa ameshafunga mapambo pale dirishani, na sasa alikuwa amekileta kiti huku dining pia usawa wa dirisha, akiwa amepanda hapo kumalizia kufunga mapambo yaliyokuwa yamebaki. Mama Chande akaingia sebuleni na mwanamke mwingine na kusifia mwonekano wa maputo hapo juu, wakaitana na wengine ili wayaone, kisha akaniuliza vipi kuhusu suala la muziki, mbona bado palikuwa hapadundi, ndiyo nikamwambia kuwa Tesha alienda kushughulikia hilo na muda si mrefu spika kubwa ingeletwa. Akawa ameelewa.
Wanawake hao walipotoka tena, nikaifata simu yangu hapo kwenye meza ya dining na kumwangalia bibie alipokuwa akijitahidi kumalizia kufunga pambo moja, na hapo nikaona kwamba lilimpa shida kidogo kutokana na urefu kupungua na hivyo kugoma kuweka fundo imara. Nikawa nataka hata nimsemeshe, ila nikaishia tu kumwangalia, kutokea nyuma, jinsi ambavyo alikuwa amejiinua kwa kusimamia vidole vyake vya miguu na kamwili kake kalivyokuwa kanono balaa.
Katika kulazimisha kufunga na kufunga si kiti chake kikanyanyuka kwa upande kama vile kinataka kupinduka? Nikashtuka kiasi maana na yeye aliweweseka kidogo, nami nikamwahi upesi na kumkamata kiuno ili asidondoke. Lakini hakuwa hata karibu kuanguka, basi tu mimi nilikuwa na presha kwelikweli nikihisi anakaribia kuumia, na kumshika hivyo kiunoni kukawa kumemfanya anitazame kwa ukali na kuisukuma mikono yangu kwa nguvu ili nimwachie.
"Samahani... nilidhani ungeanguka..." nikamwambia hivyo baada ya kumwachia.
Akashuka kutoka kitini na kusimama mbele yangu huku akiniangalia kiukali, naye akasema kwa sauti ya chini, "Halafu Jayden sitaki ujinga! Unanielewa?"
"Asa' me nimefanya nini? Si nilifikiri tu...."
Akaninyooshea kidole chake na kusema, "Mimi siyo mtoto! Jayden, nakuonya. Kaa mbali na mimi. Sipendi michezo ya kipuuzi!"
"Miryam, nilifikiri unakaribia kuanguka. Nilikuwa nataka kukusaidia..." nikamwambia hivyo kiupole.
"Nimekuomba unisaidie?"
"Kwani me kukusaidia huwa ni mpaka uniombe?"
"Nini?"
"Nakusaidia kwa sababu napenda, nimeshakwambia. Uniombe, usiniombe, sikuzote nitakuwa karibu yako, na nitafanya lolote ili kuhakikisha uko sawa," nikamwambia.
"Usiniongeleshe hivyo! Sitaki mazoea ya kipuuzi Jayden, na me nimeshakwambia. Uko hapa kwa ajili ya Mariam na wengine, naheshimu hilo, lakini naomba uondoe huo upuuzi wako kwangu. Ukiendelea hivi tutafikishana pabaya..." akaniambia hivyo.
"Na huko ni wapi?" nikamuuliza hivyo kwa utulivu.
"Nitakuja ku...." akaishia hapo na kuendelea kuniangalia kwa umakini.
Nikampandishia nyusi kama kumwambia namsikiliza, aendelee.
Akashusha pumzi na kutikisa kichwa chake, naye akasema, "Em' nipishe..."
"Subiri. Sema ulichokuwa unataka kusema. Utanifanyaje?" nikamuuliza hivyo kwa sauti ya kizembe.
"Nimesema nipishe..." akaongea kwa msisitizo.
"Uende wapi?" nikamuuliza.
Akataka kunipita lakini nikamzibia njia. Akanitazama usoni kwa macho makini sana.
"Hivi Miryam hujui kwamba unavyoendelea kujifanya kama umenikasirikia, ni wewe tu ndiyo unajiumiza?" nikamuuliza hivyo.
Akaangalia pembeni dirishani na kusema, "Jayden nakuomba utoke mbele yangu!"
Nikajaribu kumsogelea zaidi na kumshika kiganjani, naye akajirudisha nyuma na kuninyooshea kidole chake kwa ukali.
"Wewe! Unaniona me mtoto mwenzio, si ndiyo?" akaniuliza hivyo.
"Hamna. Nakuona kama mtu muhimu zaidi kwangu..." nikamwambia hivyo.
Akatumia upande wa pili kuzungukia meza na kuelekea sehemu ya jikoni ili bila shaka apitie huko kuelekea chumbani, lakini nikamwahi kwa huu upande mwingine na kukutana naye, usawa ule ule wa sehemu ya jikoni nilipokuwa nimesimama jana.
Akaniangalia kwa ukali mno na kurudi nyuma kidogo, naye akasema, "Unafanya nini lakini, Jayden? Umekuwaje wewe?"
"Nakupenda," nikamwambia hivyo kwa uhakika.
"Ahh..." akafanya hivyo kwa hasira na kuangalia pembeni.
"Miryam unajua hilo ni kweli. Na nimekwambia haitapita siku hata moja kutokea hapa ambayo sitakwambia jinsi ninavyoku...."
"Koma! Nasema koma, Jayden!" akaniambia hivyo na kuninyooshea kidole tena.
Nikatulia tu nikitazama kidole chake.
"Usifikiri kwa sababu nakuacha tu hiyo inamaanisha me ni mpumbavu. Kacheze na wanawake wengine Jayden, usinizoee. Mimi siyo Soraya," akasema hivyo.
Eh!
Nikakunja uso kimaswali kiasi, nami nikamuuliza, "Soraya?"
Akashusha kidole chake na kusema, "Unafikiri sijui kuhusu we' na Soraya?"
Nikiwa namwangalia tu kwa ufikirio, nikamuuliza, "Unajua nini?"
"Utajua mwenyewe, usiniulize mimi hivyo," akanijibu namna hiyo.
Nikatabasamu kiasi na kusema, "Kumbe..."
Akabaki akinitazama kwa mkazo.
"Kumbe ni hicho? Unahisi wivu kwa sababu nimeshakuwa na Soraya, eti?" nikamuuliza hivyo kimchezo.
"Wivu? Mimi? Nimwonee Soraya wivu?" akauliza hivyo kwa sauti ya chini kimkazo.
"Kwa nini ushindwe? Inawezekana bado unafikiri natoka naye, na hapana. Sitoki naye, Miryam. Mimi ni mali yako kabisa, yaani mmiliki wangu ni we...."
"Unafikiri kila kitu huwa kinapishwa tu kwa kufanya masihara, eh?" akanikatisha kwa kusema hivyo.
Nikatulia tu na kushusha pumzi kwa kuona tulikuwa tunaelekea sehemu serious. Hapa kujishaua kusingenisaidia, alikuwa amenikamata.
"Ninajua vizuri tabia za vijana kama wewe. Unajifanya unampenda mtu, halafu ukimaliza kumchezea unamtupa. Na wewe najua tatizo lako liko wapi. Unapenda wanawake wenye umri mkubwa. Na ukishapata unachotaka kwa mmoja, unahamia kwa mwingine. Ninaomba ukome kufikiria kwamba mimi nitakuwa kifaa chako cha starehe kama ulivyomfanya Soraya. Hata hauna aibu? Ukatoka na dada wa watu, unajua kabisa ameolewa, ana familia, halafu sasa hivi unaniletea mimi hii bullshit? Unafikiri na me unaweza ukanifanya hivyo, si ndiyo?" akaongea kwa sauti ya chini.
Nikajihisi vibaya kiasi, nami nikaondoa masihara na kusema, "Hapana, Miryam... ni... yaani ni kweli, sikatai, nilikuwa mtu wa namna hiyo mwanzoni. Ni... mambo mengi tu yalichangia, lakini sitaki kuwa hivyo tena, kwa sababu nimeshaku...."
"Siwezi kuwa na mtu wa namna hiyo hata siku moja," akanikatisha.
Nikaendelea kumtazama tu kwa hisia.
"Yaani, hata kama kungekuwa na ile chance ya kusema... niwe na wewe, haingewezekana kuwa na wewe. Ni kitu ambacho hakipo akilini mwangu kuwa na mtu kama wewe unayependa kuwachezea tu wanawake ukidhani wameumbwa wawe kama midoli ya kuchezea na kutupa..."
"Miryam usiseme hivyo," nikamwambia hivyo kwa hisia na kumsogelea zaidi.
Wakati huu, hakujaribu kunikwepa, bali akawa ananiangalia machoni kwa hisia makini.
"Ona... sijakataa... nakiri kwamba nimekuwa na tabia za namna hiyo, lakini... hazija-shape kwa asilimia zote aina ya..."
"Agh, sihitaji maelezo yako Jayden. Sijali. Nataka uache kunisumbua. Basi. Vinginevyo, tutarudi kule kule tulipotoka kipindi kile, I swear," akaniambia hivyo kwa uhakika.
"Lakini siko tayari kufanya hivyo Miryam. Yaani ni bora... ni bora kama tu ukiendelea kunikasirikia kwa sababu ya mimi kukuonyesha wazi kwamba nakupenda, angalau nitajua unahisi kitu fulani kunielekea. Kuliko nikae pembeni na kuigiza kwamba sihisi chochote kile kwako. Nakwambia ukweli Miryam. Sitaweza," nikamsemesha kwa hisia.
Akabaki kimya tu huku akiniangalia usoni kwa utulivu.
"Nina wakati uliopita ambao haukuwa mzuri sana, na... ulifanya nikawa namna hiyo. Ni mambo mengi... ila naomba uniamini, ninachohisi kwako wakati huu ni halisi. Siyo mchezo wa umri wala nini, ni upendo halisi. Nauhisi. Na... najutia kufanya mengi ambayo hayakuwa sahihi mpaka sasa... ila najua kama ni jambo moja ambalo siwezi kujutia tena maishani mwangu... ni kukupenda wewe Miryam," nikamwambia hivyo kwa hisia.
Akafumba macho yake taratibu na kutikisa kichwa chake kwa kutoamini.
Nikajaribu kumshika mikono ili nimwombe anielewe hata zaidi, lakini akaitoa yake upesi na kusogea nyuma akionekana kuudhika.
Nikashusha pumzi kiasi na kusema, "Siwezi kubadili mapito yangu yote, ila yale yatakayofata najua naweza kuyabumba vizuri zaidi. Najua chance ya kuwa na wewe kimahusiano haitakuwa jambo la mchezo... ndiyo maana nilikuahidi nitafanya yote niwezayo kukuonyesha kwamba ninakupenda kweli...."
Kabla sijamaliza kuongea ikawa wazi kwamba kuna mtu aliingia kule sebuleni, labda mmoja wa wale wanawake hapo nje, nami nikasogea nyuma ili kumpa bibie nafasi, na yeye akaingia jikoni zaidi ili kuondoa usomi wowote ule wa ukaribu baina yetu kwa mtu mwingine ambaye angefika hapo. Na kweli akawa ameingia mdada mmoja wa hapo kitaa na kuja upande wetu, mweupe, mnene kiasi, na akiwa ndani ya dera nakwambia na pini puani, naye akasimama usawa wangu na kunitazama kwa makini kutokana na kutotarajia kunikuta hapo nadhani.
Nikampa tabasamu hafifu na kichokozi ili kuondoa wazo lingine kichwani kwake zaidi ya upuuzi ambao ningemfanya afikirie, naye akatabasamu pia kwa shau kidogo na kuushika ukuta. "Dada..." akamwita Miryam hivyo kwa madoido.
Miryam, akiwa ametoa glasi ya maji ya kunywa kabatini, akamwangalia na kusema, "Bee..."
"Kuna mgeni hapa mlangoni, anakuita," huyo dada akamwambia hivyo.
Nikamtazama Miryam, naye akaweka glasi kwenye kaunta na kuanza kuja upande wangu. Akanipita tu na kuelekea upande wa sebule, na huyu mdada mwingine akawa anajivuta-vuta kuondoka hapo huku akiniangalia, nami nikampa tu tabasamu kwa kujilazimisha maana najua alikuwa ameshaanza kuwaza kuombwa namba. Mimi hapo akili yangu yote bado ilikuwa imetekwa na kile tulichoongea na Miryam muda mfupi nyuma, kwa hiyo huyu mwanamke mwingine alikuwa akijisumbua tu kujisogeza kwangu.
Nikatoka hapo nikiamua kuondoka tu ndiyo lingekuwa jambo sahihi kufanya kwa sasa, na huyu chibonge pia akawa ametangulia. Ilikuwa yaani ndiyo nimefika mwanzo wa sebule, pale Miryam alipoingia ndani tena ikionekana anafuatwa na mgeni, kwa hiyo nikaona nisubiri kwanza mgeni aingie ndiyo nioshe sasa. Mgeni akaingia, na hisia zangu zote zikageuka kuwa makini baada ya kumwona kwa sababu sikutarajia kabisa kwamba ingekuwa ni Festo!
Mzee, kama kuchoka ndiyo nikahisi kuchoka tena. Mwamba akawa ameingia sebuleni hapo huku akiwa anatabasamu kiasi, ile kukaribishwa na Miryam yaani, na ndiyo akawa ametazama upande wangu na kuniona, kisha naye akasimama. Yule mdada mwingine akampita Festo na kuelekea nje, kwa hiyo tukabaki watatu sehemu hiyo kukamilisha kitu ambacho tunaita "pembetatu ya mapenzi."
Festo alinitazama kwa umakini, mimi nikimtazama yeye pia kwa umakini, na Miryam akawa amesimama pia huku akituangalia mimi na jamaa kwa njia iliyoonyesha kutatizika kiasi. Yaani najua ile hali nzito hapo sote tuliweza kuihisi kwa sababu kila mmoja wetu alikuwa na lake la kuwaza kuhusu nini ambacho kilifanya sote tuwe hapa, na mimi nilikuwa nikijiuliza tu ni kitu gani kilichokuwa kimemfanya Festo aje sehemu hii. Alitaka nini?
★★★★★★★★★
ITAENDELEA
★★★★★★★★★