Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Kitaeleweka tu
 
SEHEMU INAYOFUATA..............

Nilifikiria sana kauli ya mke wangu, kwanini ahisi ESTA ana mapungufu fulani, lakini nilikuwa na majibu kuwa sababu inayomfanya aonekane hivi ni kwasababu kapigika

Ukiwa na maisha fulani ya mazuri yaani hela ya kubadilisha mboga haikosekani, unaweza kuapa kutofanya kazi zozote za kijinga, yaani unakuwa mithili ya mhitimu wa chuo ambaye kulingana na alichosomea huwa wanajipangia hata mishahara,

Yaani anachagua kazi na kutaka kulipwa anachotaka anasahau kuwa mitaa haihitaji Elimu ya kwenye makaratasi Bali watu, wanapeana connection na marefa ambao bila kuwa na takrima fulani basi utatembea na bahasha miaka yote huku ukijenga urafiki na kazi ambazo ulikuwa ukizikataa mwanzo.

Hivyo kwa upande wa ESTA ni msongo wa mawazo tu unamsumbua huyu akipewa mtaji afanye biashara mbona atatulia huyu?

Lakini Kuna jambo inabidi asaidiwe huyu, ngoja nitamshirikisha mke wangu, nikainuka kuelekea alipo bimkubwa kwakuwa alikuwa akiniita .

Daniel mwanangu kama nilivyokuambia, mkeo kajifungua bila matatizo yoyote, hivyo ni wakati mzuri wa sisi kurejea nyumbani, alisisitiza Mama.

Haaaaa mamaaaa mbona bado?
Mimi nakutegemeeni nyinyi kwa Kila kitu huyu bado hajawa sawa pili huyu dada wa kazi naamini hawezi kummudu mzazi akiwa peke yake,

Naomba ukae kidogo mama, niliongea kwa kumaanisha maana niliona sitakuwa free kabisa nikiwa kazini,

Hapana mwanangu, tumekaa sana pili Mimi najua mkeo Hana tatizo lolote Kuna mambo ambayo sisi huwa tunaangalia yanayotupa tumaini kwa mgonjwa, Mimi niliwahi fanya kazi ya unesi japo Mimi ni darasa la Saba umesahau miaka ile ?

Hivyo nazifahamu hizi kazi sana tu,
Lakini mwanangu huu ni msimu wa kuandaa Mashamba hata baba yako ameshaanza kulaumu, hivyo niache niende nitamwacha dada yako kwa muda mpaka atapotengamaa mkeo japo hapaswi kuchelewa, aliweka kituo.

Sawa mama Mimi nimekuelewa vizuri sana mama.

Nilimaliza mambo yangu huku nikiwa na furaha fulani siku hiyo hasa nikimwangalia ESTA,nikikumbuka ule mchongo wa madam nikaona safi kabisa lazima nipige hela

Kesho asubuhi nilitoa maagizo fulani kwa mke wangu kuwa kwakuwa mama anahitaji kuondoka ningeomba basi baade mida ya saa tisa tuonane mjini .

Nikakubaliana na mke wangu kuwa ESTA kwakuwa ni mzoefu wa mjini atampeleka mama yangu duka lenye nguo za kike hasa watu wazima halafu Mimi nitawafuata baada ya kutoka kazini,

Nilipiga kazi ofisini mida ya saa nane mchana nikapokea simu ya mama kuwa wapo na ESTA kwenye duka fulani maarufu mjini,

Nikafunga vitu vyangu licha ya kuwa ule muda halisi wa kufunga ilikuwa bado nikamuaga meneja kuwa Nina dharula jambo ambalo hakukuwa na tabu,

Nilifika dukani pale , nikatulia zangu nje ya lile duka huku nikimwambia mama Kila kitu kizuri akikiona achague, kweli ikawa hivyo nikaletewa hesabu nikalipa,
Ni mama yangu mzazi ni lazima nimfanyie Kila chema na chenye kumpa faraja.

Wakati nikiwa pale nje hata sijaondoka lilikuja gari fulani la bei ghali sana , nalikumbuka si geni machoni mwangu , akashuka Madam ambaye alikuwa ni Boss wangu wa mwanzo lakini bado alikuwa ni Boss wangu kwakuwa nafanya kazi kwenye ofisi zao.

Tulisalimiana Kisha akazama dukani , kule ambako ESTA na mama mzazi bado wapo wakiwa wanachagua nguo fulani ya ESTA maana mama alinishauri kuwa hatupaswi kumtenga ni mtu kafanya kazi kubwa sana hivyo lazima naye apate zawadi na si yeye tu watu wote wapate yaani familia nzima hasa ukizingatia nyumbani kwangu karibu wote ni wanawake

Nilihisi bajeti itaongezeka lakini acha akina mama waitwe mama, Kila mtu alipata nguo kwa ushauri wa mama huku bajeti ikiwa hata haikufika niliyokuwa nimejiwekea.

Muda kama dakika kumi alitoka Madam akiwa amefurahi sana,

Jamani tolu kumbe huyu ndiye MAMA yetu jamani, nimefurahi sana kumuona MUNGU amlinde jamani,
Aliongea kwa hisia sana ,

Huku kimoyomoyo nikisema siulisema wasikanyage ofisini kwako kipindi nipo mahabusu licha ya kufika hukutaka kuonana nao,

Waliongea wakicheka na kufurahi sana huku nikiwa pembeni natabasamu nikiwaza unafiki wa wanawake hususani kule kukumbatiana Kati ya madam na ESTA.

Eeenhee naona mmekuja kufanya shopping ya nguvu tolu? Aliuliza madam

Ndiyo, ni bimkubwa anasafiri kuelekea mkoani nikaamua nimlete angalau aangalie vitambaa hapa, nilijibu

Sawa Sasa mwambie mama achague nguo anazotaka, wakaingia dukani kwa Mara ya pili huku ESTA akibaki ,akiwa kama hajapendezwa na ujio wa madam pale, just imagine mtu ambaye alikukosea,halafu ana maisha ambayo pengine yangekuwa ni yako, but kila binadamu ana riziki yake pengine isingekuwa hivyo.

Huku mama alitoka na begi jipya kabisa ambalo kanunuliwa na madam mule ndani huku zile pockets za pale dukani zikiwa kama hazina kazi.

Baada ya sisi tumshukuru yeye madam

Akawa anatushukuru sisi akidai ni kama MUNGU tu kamleta pale, tuliagana nikatafuta usafiri binafsi tukaondoka huku nikitambua mama hajafurahishwa na mambo aliyofanyiwa na madam.

Hivi Dani huyu ndiyo boss wako ambaye alikusumbua mwanangu, yaani nimeshindwa hata kukataa hivi vitu lakini ningefanyaje, pia kanipa hii hela mule ndani dukani ni hii shilling laki moja, nimepokea tu maana huyu Binti namuona kama ana wadhifa mkubwa sana, alimalizia Mama.

Mama yanguuu, Mimi natambua Kila kitu ni jinsi gani mmeumia kitendo walichonifanyia Hawa lakini tambueni kuwa nipo kwenye kampuni zao bado, hivi kama Kila kampuni ambayo itatokea migogoro nikaapa kutokufanya kazi nitazisusia kampuni ngapi?

Kikubwa mama mniombee tu , kazi hazipatikani kirahisi lakini pia, matatizo hutokea na lazima nikabiliane nayo,

Wewe hizo zawadi ulizopewa kuwa nazo na amani yaliyotokea tusahau,

Hebu fikiria mke wangu kajifungua na familia ni kubwa ningekuwa Sina kazi ingekuwaje?

Mama alikubaliana na Mimi kwa shingo upande.

Tena Mimi kanipa namba zake za simu eti nimtafute muda wowote, sitaki mazoea naye na hii namba naifuta, alizungumza ESTA tukiwa tunakaribia kushuka.

Kitendo Cha kuonekana wamepeana na namba kilinishtua sana,

Je, ESTA anafuta namba za madam ni kweli, kama ni hivyo sawa, na je kama madam naye anazo za huyu wakaongea wakabembelezana itakuwa sawa lakini mbona kama mpango wangu utavurugika?

Wakisameheana Hawa nitapata hela kweli si watapeana wenyewe, kwanza najuta hata sana kuwakutanisha,

Itakuwaje sehemu ijayo Ina majibu usikose.

Itaendelea.................
 
tupo tunaenda pamoja ivo ivo mdgo mdgo
 
INAYOFUATA..........

Tulifika nyumbani, mke wangu akitoka chumbani kuja kutupokea pale sebuleni,

Vipi kamanda wangu anasemaje, niliulizia maendeleo ya mtoto wetu mchanga.

Kalala muda mwingi sana mbona, huku furaha zikizidi pale ukumbini baada ya watu kuwa wanapeana surprise mbalimbali, nikaacha nikaingia chumbani kwangu, na kuelekea bafuni.

Siku iliyofuata saa kumi na mbili asubuhi Mimi na mama ilitukuta ubungo stendi kuu ya mkoa kipindi hicho tukiwa tumeshikilia tiketi huku nikisomasoma zile siti kuhakikisha mama anakaa siti husika asije kusumbuliwa baadaye na watu wengine nilizugazuga pale Hadi pale nilipohakikisha gari imeingia Morogoro road huku tukipungiana mkono na bimkubwa nikimtakia safari njema.

Niliishika barabara ya Mandela road kurudi nyumbani kwakuwa ile siku haikuwa ya kazini basi nilitulia nyumbani huku nikifanya kazi ndogo ndogo ikiwemo kutatua mgogoro fulani wa majirani ambao walikuwa wakinisubiri kwa hamu Mimi nikiwa kama shahidi wa kile kiwanja ,

Huku ikiwa kila baada ya lisaa nampigia mama kujua alipo.

Oyaa Mr Daniel Kuna mwanamke yupo pale kwako ni mrefu hivi mweupe, unamwitaje yule, aliuliza yule jamaa ambaye ametoka kushinda ule mgogoro baada ya Mimi kumsaidia beacon zilipo,

Yule anaitwa ESTA, vivi kaka umemwelewa Nini?
Niliuliza,.

Bado tu hujanijibu Dani, nataka kujua uhusiano wenu, ni dada yako, ni shemeji yako au ni nani tako?
Aliongea jamaa,

Hapana yule Hana undugu kabisa na Mimi Wala mke wangu Bali ni rafiki tu wa mke wangu kaja kumsaidia wife baada ya kuwa kajifungua, nilimjibu

Basi sawa , anavutia sana yule mwanamke kifupi natamani hata ningepata namba zake za simu niwe nawasiliana naye, aliongea jamaa ambaye hakuwa akitania,namjua ana hela sana hivyo inawezekana ESTA akapata bahati kuwa na jamaa.

Lakini kaka we si una mke lakini , nilimtania,

Kwanza Mimi Dini yangu inaruhusu Dani, jua Hilo halafu lingine kama labda ni mbadala wa mkeo kwenye hiki kipindi anacholea niambie Mr,
Aliongea jamaa huku akiingia kwenye gari lake,

Hapana kaka yule Mimi naheshimiana naye sana tu siwezi hata kumtongoza ujue, au nikuitie kabisa maana yule ni mtu mzima mnaweza kuyajenga we vipi bwanaaaa, niliongea tukacheka.

Sawa Mr Daniel, Mimi nawahi Leo Nina wageni ofisini kwangu, aliongea huyu jamaa ambaye aliwahi kumiliki duka la pembejeo za kilimo na mifugo miaka ile na Sasa ana miliki kampuni ya ulinzi mjini. Aliwasha gari akaondoka, kitu pekee nilichofurahi ni kusahau kuchukua namba ya ESTA,

Sikutaka apate namba ya ESTA, kwasababu,

Kama ESTA akipata bwana wanguvu kwasasa ni ngumu Mimi kumshawishi aelewane na madam, atakuwa kapata pa kuegemea ni ngumu sana kumshawishi

Na huyu jamaa ni ana pesa ni rahisi kumbadilisha ESTA kwa muda mfupi sana, ngoja nitaongea na mke wangu jambo

Nikarudi nyumbani nikamkuta mke wangu anazungumza na dada yangu nikamuomba tuongee jambo akaja chumbani,

Yaani mume wangu hata hupumziki yaani hata weekend kama hii wewe ni wa kwenda mitaani tu? Mimi unanikera sana ujue, aliongea kwa kumaanisha

Lakini haikunisumbua ni kawaida yeye kuwa na wivu na Mimi hasa kipindi hiki akiwa mbichi nilimpoza maisha yakaendelea,

Sasa mke wangu nilitaka kuongea na wewe jambo kuhusu ESTA , naamini alikusimulia Kila kitu kuhusu matukio yake ya nyuma Kati ya yeye na aliye kuwa boss wangu,

Ndiyo najua si anadai hataki hata mawasiliano naye si eti? Aliuliza

Eeeh Sasa unafikiri atakaa hapa Hadi muda gani , mke wangu?

Kwahiyo ulitakaje mume wangu maana ndiyo tushapata mgeni mume wangu.

Sasa yule mbaya wake yeye hana neno kabisa Tena kapanga kama ESTA atakubali atampa hata mtaji Tena kima Cha kuanzia ni milioni tano Sasa yeye hataki,

Haaaaa kumbe huyu dada ni mjinga eh unaikataaje milioni tano ikiwa maisha yako ni mabaya namna hii, alidakia mke wangu bila hata kujua mambo yanapangwaje.

Nisikilize mke wangu , ni hivi kwanza ESTA hajajua kuwa atapewa hicho kiasi, pili Mimi Nina mpango fulani wa kuweza kupata hela kwa madam kupitia huyu ESTA, maana ubaya ubaya tu walinitesa sana hawa lazima nijifanye namsaidia ESTA ili tu niweze kujipatia hela ambazo naziona zitakuwa ni za Kila Mara yaani, wewe unaemaje mke wangu.

Mume wangu mi naona Kama si vizuri kujipatia hela kwa njia ya utapeli huyo boss wako akijua , na ESTA akijua kuwa umemgeuza chumio atakuonaje,
Utajishushia heshima mume wangu, kwanza Mimi najivunia kabisa kuwa na mwanaume kama wewe , hivyo kwa ulivyo sijategemea kuwa na mawazo kama haya wewe kama unamsaidia ESTA msaidie tu, muunganishe na huyo madam ili wakipatana utabarikiwa sana maana

Kwenye biblia kumeandikwa,

Heri wale wapatanishi
Sasa ikiwa wewe utapatanisha watu kwa masilahi yako binafsi sioni kama inapendeza kwa kweli mume wangu, alisisitiza mke wangu.

Nilijiona nimetoa pasi mbovu kuwa kwanini nimemshirikisha , huyu yeye ni mtu wa kuletewa tu, Kila kitu kinanihusu Mimi hivi anadhani bila mipango ya pesa kwenye vyanzo vingi hii itakuwaje,
Ukiambiwa mjini akili ndiyo haya nayomweleza, Sasa kwanini anapinga?
Niliwaza huku nikijilaumu kumshirikisha, Sasa ataniona Mimi nani nitahakikisha napiga hela bila yeye kujua Wala ESTA mwenyewe kujua,

Sawa mke wangu Mimi wewe ndiyo katibu wangu kwenye hii nyumba kwahiyo naheshimu mtazamo wako MAMA, niliongea ili nimridhishe tu lakini mpango wangu ulikuwa pale pale , hawezi kunipangia huyu hajui tunavyohenyeka.

Saa kumi na moja nikapokea simu kutoka kwa mama akiwa ananitaarifu kuwa amefika salama salimini, nikafurahi sana, nikaona huu ni muda wa kuongea na ESTA jambo.

Nikamuita nikiwa na dada yangu, sikutaka tuwe wawili tu hapana isije mke wangu akahisi vibaya tena

Tukakaa nje, huku nikivunja ukimya lengo nimuulize maswali fulani nijue ana mipango gani?

Samahani shemeji, kwa kuwakatisha shughuli zenu ambazo mlikuwa mkifanya, lengo langu nataka kujua kuwa una mipango gani , maana Kuna mchongo huko mjini nimeupata ila nilikuwa naogopa kukweleza maana isije kuwa una mawazo yako mengine,

Akadakia, niwe na mpango gani masikini Mimi, we shemu kama Kuna maisha sehemu yanapatukana we usisite kuniambia, natamani niwe hata kwenye kibarua fulani maana haya nayoishi siyo maisha kabisa,
Aliongea kwa sauti ya kukwaruza huku akijizuia kulia nikajisemea hapa nimeshinda,.

Najua jumatatu nitazunguza vipi na madam, nilijisemea moyoni
Mke wangu hawezi nipangia jinsi ya kutafuta hela yeye atulie tu atakachotaka atapewa.

Jumatatu ilifika kama kawaida yangu muda wa kula nilitoka nje lengo nipate na nafasi ya kuongea na simu kwa kirefu maana mule ndani Kila dakika mtu anagonga lakini pia maboss hawapendi sana mfanyakazi kuongea na simu binafsi.

Nikatoka nje ya fence nikampigia MADAM

Eeh tolu nambie nimeona kimya tangu ile majuzi, lakini pia ESTA nilimpa namba yangu anitafute vipi mbona amekuwa mkimya?

Mimi kwa kweli sijui,ila nikirudi nitamuuliza mbona hajakutafuta,nilijibu kiuongo huku nikijua ESTA hataki mawasiliano na madam.

Sikia tolu huyo achana naye twende taratibu mbembeleze ,huku ukijifanya unamtafutia biashara fulani afanye kama tulivyokubaliana, alimalizia.

Nikaona siyo muda nitakuwa mshindi,tulimaliza kuongea na madam nikampigia simu ESTA nikimsisitiza akae pembeni,

Shemu bwana nimefikiria
Jambo fulani kuhusu tuliyoongea nimeona tutafute frem ili ufungue hata ya kuuza urembo tu, labda wewe unapendekeza Nini, niliuliza

Waooh shemu kwanza nakushuru kwa kuendelea kunipigania , Mimi shemu biashara ya haraka haraka hapa kwangu kama Kuna uwezekano ni saloon ya kike, hiyo kwangu naiweza na naijua vyema nimekuwa nikipita kwenye saloon za wenzangu kuomba kazi ya ususi , kwa malipo ya chini sana lakini kama nitapata ofisi yangu nitafurahi sana,
Labda kwakuwa sijajua bajeti yako aliweka kituo

Kwani Nini kinatakiwa kwenye hiyo biashara?niliuliza

Sawa kwanza inatakiwa tupate sehemu yenye mzunguko wa watu wengi, Ila siyo mjini kule mafremu ni gharama, kwahiyo tukipata frem ambalo liko kwenye V au junction itakuwa poa sana shemu,

Kuhusu frem usijali,vipi kuhusu bajeti ya vitendea kazi, niliuliza.

Hapo shemu panakuwa pagumu kwakuwa sijui mfuko wako
Ila ukiondoa hela ya frem hela ya vifaa kwa kukadiria ni kama milion moja na nusu, hapo kila kitu kitakuwa sawa.aliweka kituo

Shemu milioni na nusu mbona ndogo labda Kama unafungua biashara
hiyo kijijini, niliongeza

Kwani shemu ulikuwa na kiasi gani, aliuliza kwa pupa.

Ipo kama kama milion tatu hivi . nilimjibu

Ahsante sana shemu, sikutegemea kabisa kweli MUNGU anaweza acha MUNGU aitwe MUNGU, aliongea kwa hisia sana ,
Yaani hapo kila kitu nitaweka nitahakikisha hata kama ni sehemu ndogo lakini iwe ya kisasa,
Japo ya kiswahili

Inaonekana hiyo biashara unaijua vizuri sana shemu, niliuliza

Naijua vizuri sana, ni kwakuwa kwanza Nina sura ya mauzo kitu ambacho ni point namba moja kwenye biashara.

Nikajiuliza hao anaowasuka watakuwa ni wanawake wenzie sura yake nzuri itahusika vipi ingekuwa ni saloon anahudumia wanaume sawa, ila namwachia mwenyewe,

Tafadhali shemu hakikisha mke wangu hapati hii taarifa maana isije kuwa matatizo baadaye, nilionya kwa tahadhari.

Shemu, najielewa, nakuelewa wewe, pia namuelewa mke wako hivyo kuwa na amani kabisa, labda wewe ndiyo umwambie.

Nikakata simu huku nikiwa nimepanga kumtafuta MADAM kesho yake ili mipango ya hela/pesa ifanyike

Nilirudi nyumbani, nikaikuta familia ikiwa na amani ya kutosha, lakini ESTA alikuwa na furaha kuliko mtu yoyote mle ñdani.

ESTA anafurahi baada ya kuahidiwa kutengenezewa kijiofisi Cha kuzugia,

Mimi namuahidi hela ambayo sijaitia mikononi mwangu, je jambo hili litafanikiwa ?

Vipi kuhusu mke wangu akigundua.?
Usikose kufuatilia mambo mazuri yanakuja.

Itaendelea.....,?!:"":!
 
Inafundisha San story yako
 
Inafundisha San unaweza mamb yako yaka kwama kutokana na masikitiko ya watu wanaolalamika kuhusu wew
 
Mwanzo nillikuaa naipuuza hi story kumbe Ni nzur na inauahalisia Kia's na mafundisho sana
 
SEHEMU INAYOFUATA..........

Jambo ambalo lilikwamisha mpango wa Mimi na ESTA kuhusu biashara ya saloon,ni baada ya madam kusafiri kwa muda wa wiki nzima huku akiniahidi akirudi mipango itakuwa kama kawaida.

Matukio ya kununiana bila sababu ndani ya nyumba, mashtaka mbalimbali yalijitokeza ila ilikuwa ni kama kawaida tu kwakuwa wanawake ndivyo walivyo,

Kuna siku nikiwa ofisini nilipokea taarifa ya watu kuumizana Kati ya Dada yangu wa tumbo moja na ESTA , wakipigana kwa sababu zisizoelezeka huku mke wangu akiwa upande wa ndugu yangu.

Nilifikiria kuhusu ESTA, nikagundua wamepanga kumuhamisha kwa nguvu, lakini madam si atarudi siku si nyingi? nilijiuliza

Nikarudi nyumbani,nakumbuka dada yangu na mke wangu walichachamaa huku wote wakidai,Bora wote
Wote tuondoke mkoani ili wewe ukae na ESTA

Mtu gani Kila tukimwambia hatumtaki anang'ang'ania tu , mtoe nakwambia muondoe huyo malaya wako, alizungumza mke wangu,
Huku nikimtazama nikikumbuka urafiki wao wa siku ya kwanza namna walivyokuwa wanakaribishana.

Wakati hayo yakiendelea ESTA alikuwa kashika mkoba mdogo wa kike mkononi huku akiwa na begi dogo la mgongoni,

Leta begi hilo, la kwako ? Yaani mchana kweupe unaniibia,
Ni maneno toka kwa dada yangu wa tumbo moja ambaye alishindwa kuwa na hekima ni kwasababu tu yalifanana, ESTA akarudisha like begi ndani akachukua la kwake,

Muda huu anaenda wapi huyu ,lazima nisimame kama mwanaume huku nikihakikisha , Kila mmoja namdhibiti , sikuwa na maneno na dada yangu, jicho nililomwangalia lilitosha kumfanya akimbilie chumbani kwake , huku nikitoa ukali na msimamo wenye kutaka Kila mmoja aingie ndani si ESTA Wala na nani , niliingia chumbani huku mke wangu akiwa Hana hata neno la kuniambia ikabidi atoke aingie kwenye chumba Chake anacholala na mtoto kwa kipindi hicho.

Nakumbuka nililala bila kula, saa kumi alfajiri niliamka nikajiandaa fresh, Kisha nikawaamsha wote,
Nikasema yafuatayo,

Hii nyumba kiongozi ni nani? Niliuliza

Wote wakajibu ni wewe.

Sasa kuanzia Leo naomba ESTA tafuta pa kwenda sitaki migogoro na malumbano yasiyo ya lazima ndani kwangu, lakini pia wewe mke wangu na dada yangu naomba mniandalie majibu mazuri ni kwanini mmekosa heshima na adabu kwa Sasa, au kwakuwa mama kaondoka ?

Nawapa kutwa nzima Kila mmoja awe na majibu, niliongea huku nikionesha sura ambayo hakuna aliyenijibu,

Sasa shemeji namimi nikupe jibu gani maana Mimi sijui chochote, aliongeza dada wa kazi akijitetea

Wewe haupo naongea na Hawa, nikainuka kuwahi kazini kwangu, kama kawaida shughuli ziliendelea huku uzoefu ukiongezeka, kiasi Cha baadhi ya wafanyakazi kuwa wanajiuliza vitu vingi kwangu ilinipa heshima kubwa kwenye kampuni.

Kama kawaida Kuna mdada ana kiherehere sana pale ofisini, aliingia huku akiwa na taarifa mpya, ambayo kwangu ilinistua,

Mr Daniel, Kuna tetesi nazisikia kuwa yule mke mdogo wa boss atakuja kampuni hii, na hapa tunapoongea yupo South Africa kwa mumewe . Ambako yametokea mabadiliko kwamba mtoto wa boss hatahusika Tena hapa Bali atashughulikia habari zake za ufuatiliaji wa mizigo toka nchi za nje na kuiingiza humu,

Ni kazi ambayo alikuwa nayo zamani kabla hajapandishwa cheo, Sasa sijui yule mwanamke akija hapa itakuwaje maana ni ana majungu sijapata kuona Tena ni mchawi sana yule yaani huwa simpendi basi tu.
Japokuwa haijawekwa wazi kuwa hapa atakuwa nani,
Alimalizia yule dada.

Haina shida Mimi naona Mimi na wewe haituhusu kwasababu atakuja kukaa kwenye nafasi yake na sisi tutampa heshima anayostahili,
Nilijibu kwa kujikaza.

Niliwaza sana kama yule atakuja pale ofisini kwetu maana kiukweli ni mtu mzuri mkiwasiliana mkiwa mbalimbali lakini hayuko poa mkiwa sehemu moja.

Anyway hayanihusu haya nitaongeza tu umakini.

Kuja kushtuka kumbe simu kutoka kwa ESTA iliita sana , ikabidi nimpigie ESTA mtu ambaye hajui kususa maana Mimi nilidhanj pengine hatonitafuta Tena huyu mwanamama.

Samahani shemu Mimi nipo sehemu tu kwa mjumbe wa mtaa huu hapa kwako, lengo la kukupigia simu ni kuulizia ule mpango vipi, maana hata eneo na frem nimeshapata siku nyingi sana kwahiyo nakusikiliza.
Alimalizia.

Subiri nitakuja hapohapo ulipo baadae usitoke.
Nikakata simu,

Nikakumbuka ninavyotoka asubuhi nyumbani nilichimba mkwara ambao lengo nikuwatuliza tu wale ili wasinipande kichwani, nikampigia simu mke wangu ambaye alikuwa mpole sana mithili ya kuniogopa, ila nikamtuliza tu.

Nikapanga lazima niende kwa ESTA kwasababu ya ule mpango wangu, isingekuwa huu mpango pengine ningemuacha apambane na hali yake.Japokuwa huu mpango ni kama hauna uhakika sana kwasababu nilizokuwa naziona ila bado nilikuwa na IMANI, nilitoka kazini nikitembea maeneo ya city centre huku nikiangalia maduka mazuri yanayouzwa nguo za kike,

Nikanunua nguo fulani za mke wangu( jina kapuni)
Bangili na urembo urembo nikaweka kwenye pocket huyooo kutafuta daladala zinazoelekea nje ya jiji.

Nikashuka kwenye daladala huku nikielekea kwa mama mmoja mjane ambaye ndiye mjumbe wetu aliyempokea ESTA.
Nilifika tukasalimiana maongezi yakawaanza

Kwanza baba nikushukuru kwa ukarimu wako wa kumpokea huyu ukakaa naye sikuzote hizo, japo ulifanya kosa kutokuziona mamlaka ili wajue kuwa unahifadhi mgeni,
Huyu ni binadamu angekufa ungefanyaje,?

Nikakiri kosa hasa ukizingatia hata mama yangu mzazi alishasema kipindi fulani nikapuuzia.

Akaendelea yule mjumbe..

Sasa naweza kuwaacha mkaongea wenyewe maana kaniambia wewe ndiye anakutegemea kwa vitu vingi kwa sasa.

Akatupisha,

Nilizungumza mengi na ESTA alishauri angepanga chumba, nilifikiria kidogo nikaona ni wazo zuri Bora apange, lengo awe kwenye himaya yangu mpaka nitakapopiga hela kwa madam, nikashauri atafute chumba kesho yake.
Huku nikimuita yule mama mjumbe.

Kwanza mama Mimi nikushukuru kwa kumpokea huyu ndugu yangu ni kwamba si Mimi niliyemfukuza Bali kalazimika kutoka, nilijitetea

Wewe mwananguu (akiongea kwa sauti ya chini ESTA asisikie)
Mwanamke mzuri Kama huyu unampotezaje? Yaani ningekuwa na mtoto wa kiume ningemwambia amuoe kabisa mtoto kaumbika mtoto mashallah, hebu mpangie chumba basi na wewe hutaki kuwa na wanawake wawili?

Maana kutwa nzima nilimuhoji ananiambia hujawahi hata kutembea naye mwanangu,? Acha uzembe bwanaaa, unaniangusha.aliongea bila breki yule mama mjumbe mswahili kupitiliza mwenye kabila fulani maarufu mwambao wa bahari ya hindi

Sikumjibu neno zaidi ya kucheka tu, nikiwaza jinsi watu tulivyokuwa nyuma kwenye mambo mengi,

Kweli Elimu ni muhimu, yaani kusoma si lazima upate kazi kwanza unaongeza ufahamu, hebu fikiria mtu anafahamiana na mwanamke kwa Mara ya kwanza tayari anawaza angekuwa na mtoto wa kiume amuoe. Hawazi kuhusu magonjwa ya zinaa na ukimwi. Yaani waswahili tunarahisisha sana mambo.

Na ndiko magonjwa mengi ya ngono yaliko,niliwaza sana.

Sasa baba yanguuu nisikufiche niwe mkweli Sina kitu humu ñdani, unaniachaje?

Aliongea yule mama ambaye huenda kwenye ujana wake alikuwa shangingi na sijui, ujumbe aliupataje
Ikabidi nimpe Msimbazi mmoja.
Huku nikiwaza kweli wanaume tumeumbwa mateso,

Yaani muda wote lazima uwe na hela japo do lazima kutoa, lakini Kuna ile kujiepusha na lawama ndogo ndogo.
Tukaagana huku nikisisitiza ESTA atafute chumba. Najua ule mpango wa Mimi na madam Sina uhakika ila ESTA simwachi lazima nibeti hebu fikiria unaipata milioni tano kwa pamoja bila kutumia nguvu nyingi.
Weeee ESTA ninaye , nilijisemea

Nikafika nyumbani kila huku Kila akiwa mtu mnyonge mnyonge, nikamuita mke wangu nikambembeleza plus uongo mwingi huyoo kalainika, niwanawake tu Hawa wametoka kwenye mbavu zetu. Kama huwezi kubembeleza mwanamke basi utapata tabu sana kwenye ndoa yako, watu wengi wameshindwa kukaa na wake au wapenzi kwa kujitia misimamo ambayo baadaye iligeuka Majuto.

Lazima muda mwingine umpe ushindi hata asiostahili kwa ustawi wa penzi au NDOA.
Tuliendelea kutaniana na mke wangu Huku nikiwa namsoma vitu Fulani Mara tukaitwa na dada wa kazi, natoka nje nakutana na mke wa Shedy akiwa kama kakasirika hivi,.

MADAM nasikia tetesi kuwa huenda tukawa sehemu moja, Haina shida je mpango wangu kwa ESTA utafanikiwa? Na ESTA simuachi

Mke wa Shedy anatafuta Nini huyu maan anajua wazi Hawa hatuna uhusiano nao mzuri.

Sehemu ijayo Ina majibu.usichoke

Inaendeleaa.......
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…