SEHEMU INAYOFUATA.........
Kila mtu alishangaa ujio wa mke wa Shedy nyumbani kwetu, tukiwa na shauku ya kutaka kujua anataka nini,
Si mgeni sana kwangu, labda kwa mke wangu,
Tumetoka mkoa mmoja, ni mwanamke ambaye ananiheshimu tu akitaka ila akiamua huwa ananisimanga kama mwanaye nikionesha mtazamo tofauti na yeye, labda kwakuwa tunafahamiana kitambo
Habari shemu, habari za utokako, nilimsalimia.
Kwema kiasi, au si kwema kabisa na naomba kwa kufupisha tu nilikuwa naomba tuzungumze wawili tu mi na wewe. Alizungumza mke wa Shedy.
Weeeeeeeeeh ishia hapohapo msipende kunigeuza mwendawazimu au mtu nisiyejitambua , yaani uongee na mume wangu wapi, mmezoea eeh?
Sasa nikwambie tu kuwa ongea hapahapa mbele yangu, kama hawezi uondoke, aling'aka mke wangu.
Ikabidi mke wa Shedy awe Mpole.
Jamani kwa nakuomba sana mdogo wangu nisamehe sana lakini lengo la kutaka kuzungumza faragha na mumeo si baya ila kwakuwa huna Imani basi nitaongea tu,
Bila kupoteza muda ni kwamba, nimekuja kwa lengo la kuwaomba sana mtusaidie jambo Mimi na mume wangu, ni kuhusu biashara na mambo yetu yaani hayaendi kabisa siku hizi. na Kila tunachokifanya hakiendi kabisa.
Lakini mume wangu Kuna ukweli ambao, kanieleza ni baada ya kuwa kila tukienda kwa wataalamu wanasema Kuna mtu Ana manung'unuko juu yake na ndiyo maana mambo hayaendi, aliweka kituo
Kwahiyo huyo mtaalamu kakuambia mume wangu au sisi ndiyo chanzo? Tena weee dada utukome, mbona mnatusingizia sisi? mke wangu alikuwa moto kiasi Cha kunishangaza ,
Hapana ndugu yangu siyo nyinyi nimembana mume wangu kaniambia Kuna mtu anaitwa ESTA na anaishi hapa, naomba kama yupo niitiwe Nina maongezi marefu sana, alimalizia.
Hapana shemu huyo mtu hapa kashahama muda tu, hatujui alipo labda nikupe namba zake, nilimjibu kwa mtego,
sawa nipe namba zake niwasiliane naye, alijibu.
Sawa,
Unajua shemu huwezi kuleta taarifa ya kwamba maisha yako yanashuka Kila kitu kinayumba halafu eti Kuna mtu anasababisha,
Hivi nakupatiaje hiyo namba mkiumizana je?
Hapo ulipo tu umekuja huku nikikuona ulivyo mshari, halafu nikupe namba ukiua?
Wewe mtafute kwa njia zingine kwangu Hilo halitawezekana
Nilimjibu.
Ujue shemu,tumefikia nyakati mbaya kimahusiano Kati yetu na sisi,siamini kama ni wale ambao tulikuwa tukitembeleana na kufurahi Mara kwa Mara yaani tumetengana, nasikia tu juu juu kuwa hata mkeo kajifungua,lakini jamani hata taarifa Mimi nadhani lazima wote wanne Mimi na mume wangu na nyinyi tukae chini tujue ni shetani gani anatuvuruga,...............
Shetani gani, malaya wakubwa nyie, yaani wewe wa kutafuta shetani?
Wakati mumeo kazi yake ni kutembea na watu kusudi aibe nyota za watu kwaajili ya kukuza biashara yake, hapa unamtafuta ESTA kwasababu gani,
Bila aibu wakati rafiki yake yupo mahabusu alinitaka nilale naye ndipo anisaidie,Sasa ndiyo nimejua,kumbe huwa anawatumia wanawake kama mtaji wake huyo malaya wako?
Kwa taarifa yenu kama ulimtuma alale na Mimi kusudi mkuze biashara yenu ,Mimi sipo hivyo wanaharamu wakubwa nyie,aliongea mke wangu kiasi Cha yule mgeni kuinuka,bila kuaga.
Nakumbuka mke wangu alizungumza mengi sana ambayo anayasikia kuhusu Shedy juu ya kuwatumia wanawake kama njia ya kupandisha nyota yake.
Nilicheka sana,usiku ule nikiwaza jinsi watu wanavyoamini ushirikina kupita kiasi ,hivi kweli mtu huwezi kupush biashara yako bila ndumba?
Mimi mwenyewe Nina mpango wa kuanzisha biashara yoyote kulingana na hali ya uchumi ilivyo lazima niwe na vitega uchumi kwahiyo natakiwa kuwa mshirikina tena,,,,hapaaaana
Siyo kihivyo mi naamini kwenye mipango na mikakati,na ndiyo maana yapo masomo yanayohusu biashara hata Kama Mimi sijui lakini nitatafuta wataalamu wabibezi wa business watanielewesha tu na si ushirikina.
Niliamka asubuhi nikiwa nachati kisiri na ESTA nikiuliza wapi tukutane nimpe hela ya Kodi,
Tukakutana alishukuru sana, japokuwa wanawake Wana udhaifu fulani baada ya kusaidiwa,alionesha mahaba ya wazi sana kwangu, pengine alihisi Yale nayoyafanya namtaka,kumbe siyo,
Sasa shemu Mimi naenda kulipa hii hela japo mwenye nyumba alikuwa anataka miezi sita lakini nilimwambia hali yangu akadai hata miezi mitatu poa tu,Sasa shemu nakuomba sana uje baadaye ukione chumba nitakacholipia lakini pia nitaenda kwa rafiki yangu mmoja kuchukua vitu vyangu ikiwemo kitanda ambavyo niliweka pale baada ya kufukuzwa nilikokuwa nimepanga, alizungumza kana kwamba anamwambia mpenzi wake,
Lakini nilikuwa imara kama ukuta wa Berlin juu ya vishawishi vyake,nikawahi kazini,
Huku nilikuta mapya tofauti na niliyoyaacha jana,ubize wa watu ukiongezeka huku mazingira yakiwa yanasafishwa kwaajili ya ujio wa boss kutoka South Africa, nikajisemea kweli kama boss mwanaume anakuja basi ile taarifa ya madam kuwa hapa huenda ikawa ya kweli.
Nikatulia zangu ofisini nikipangilia vitu kwenye desktop yangu, kujiandaa maana Mimi ni mfanyakazi mpya hapa licha ya kuwa mzee ananifahamu lakini huenda kukawa na maswali juu yangu.
Nakumbuka baada ya zoezi Lile mida ya saa tano aliingia,akitokea kwenye moja ya sehemu za kishua (jina kapuni) yalipo makazi yake
Tukaitwa wote kwenye ukumbi mdogo ambao sikuwa naufahamu, huku nikiwaza Jana tu , niliambiwa wapo na mkewe south Africa, Leo wapo hapa, lakini yalikuwa mawazo ya kimaskini kwangu,
Boss aliingia huku akiwa na vijana fulani wa kisomali pamoja na MADAM,
Madamu akiwa amependeza sana, macho yaligongana akatabasamu , hali iliyopelekea wafanyakazi wenzangu kushangaaa, lakini Mimi nilikuwa najua,
Kikao kidogo kilianza huku utani ukitawala kama mjuavyo wengi huwa tunatetemeka tukiwa na mtu mzito kwahiyo lazima akutanie kukutoa hofu.
Wewe mrefu kama mcheza kikapu huku umekuja lini tena? Aliuliza yule taita
Nikajieleza kana kwamba hajui ujio wangu, watu wakacheka sana.
Inabidi tuanzishe basketball au siyo manager? Tulitaniana Kisha akatueleza juu ya mabadiliko aliyofanya,
Kwanza kwenye ofisi yangu niliongezewa mtu tukawa wawili ni yule dada mwenye kiherehere huwa anapenda sana kuwa karibu na Mimi.
Pili tetesi juu ya kurudi kwa madamu haikuwa kweli ni , hali iliyopelekea nikafurahi sana,
Nilifikiria kamleta huyu hapa (madam)
Lakini mwenyewe kakataa kasema Bora abaki kwenye second company kwahiyo hapa mtakuwa na huyu akitutambulisha kijana fulani wa kisomali ambaye alichangamka sana huku akiwa analazimisha kiswahili ambacho hakuwa anakijua vizuri.
Tulimaliza kikao kile huku Kila mmoja akirudi kuwajibika kwa ofisi yake wakidai wao wanaelekea kwenye kampuni ya pili, kabla hawajaondoka madam aliniita..
Nambie tolu, habari za siku naona unazidi kunawiri mwenyewe,
Hapana madam, kawaida tu za safari, niliuliza.
Nzuri, ila sikwenda mbali nilikuwa hapa hapa ni baada ya kumpokea mume wangu nikawaambia watu kuwa nimesafiri kupunguza kero za simu, aliongea kwa kujiamini.
Sasa Kuna kiasi kidogo Cha pesa nimekuletea kwaajili ya ESTA nyingine nitakutumia kwenye account yako baadae nilimaliza mambo yangu , akamtuma msichana fulani kwenye gari amletee bahasha fulani akanipa ,
Si umesema ushapata fremu?
Aliuliza .Nikamjibu
Eee hiyo kalipe fremu na nyingine nitakutumia baadaye .
Kwahiyo madamu nikishalipa wewe utakuja lini kuliona,
Niliuliza kwa sababu nilizokuwa nazo.
Wewe toluuuu, kwani hiyo biashara ya kwangu Mimi? Wewe kalipe Mimi sihitaji hata kupajua, nimekuamini najua utamsadia yule dada, Tena sikia hakikisha unatumia ufundi wako wote kuhakikisha anakubali tupatane.tulikatisha mazunguzo baada ya mumewe kuja usawa wetu tayari kwa msafara wao.
Kuna baadhi ya wafanyakazi wenzangu walikuwa wakiniangalia sana juu ya ukaribu na yule Madam
Kwao ni mtu mzito wanamuogopa walishangaa akiongea na Mimi huku tukicheka , nilirudi ofisini huku nikiwa Nina shauku ya kuhesabu zile hela,
Niliingia ndani, nikafunga mlango, nikahesab nikapata kiasi Cha milioni nne na nusu, kwanza nilishangaa yaani hii ni hela ya frem tu?
Nikajiongeza labda alijua saloon itafunguliwa mitaa ya uzunguni ila hata kama.
Nikafikiria kuwa ESTA kaniambia fremu moja ni elfu sitini sabini kwa mwezi mahali alipopopata kwahiyo tukilipa miezi sita au mwaka, bado kiasi kikubwa kitabaki, Siyo mbaya
Niliendelea na kazi huku nikiwa natabasamu Kila saa kwa kufurahi, nilimaliza kazi zangu nijafunga ofisi nikaondoka huku nikiwa napanga maneno jinsi gani nitamwambia kuwa haya yote ninayofanya nimemkopesha au nimemsaidia?
ESTA ananiona kama ni wa kipekee kabisa, namna nilivyojitoa kwake, hajui kama Nina malengo yangu.anahisi namtaka
Madam anatoa kiasi Cha pesa kusaidia/au kuomba msamaha kwa ESTA kwa Yale waliyofanyiana kwenye usichana wao.
Mimi nipo katikati yao hakuna anayejua mawazo yangu.
Msichoke inaitwa
MIMI NA BOSS WANGU.
Inaendeleaa...................
Sent using
Jamii Forums mobile app