three phase
JF-Expert Member
- Mar 31, 2021
- 343
- 507
Tolu uyo madam sijui kama ulimuacha hivihivi
NimechekaKali sana hi story ilinibidi nisitishe kumfatilia mwamposa ili nisome tu sas acha niendelee na ibadaa asnt mkuu kma utaweka kipande kingine naomba unitag
Ndo uone tunavyotofautiana mawazo na vipaumbeleKijana anapiga hesabu za kumsaidia mtu kwa faida mtu anapiga hesabu za kuliwa hii kazi Sana
Mkuu acha kbsa nilikuwa ibadani Kuna mwana anatoa ushuhuda kwa kupona nguvu za kiume kwa mafuta na maji ya upako bas naoana mwana anajieleza sna jins alivyopambna na tatizo la kupotelewa nguvu za kiume bas nikaona acha nichungulie kwa jf haswa hi simulizi ndio nikakuta jamaa ametoka kushusha kipande nikakisoma chote nakumaliza na kuendelea kusikiliza shuhuda mbali mbali za watu bwwanaa asifiwe sanaaaN
Nimecheka
Daaaah hii ktu kla inavoenda mbele ndo inazdi kuwa tamuSEHEMU INAYOFUATA..........
Siku hiyo nilirudi nyumbani nikiwa nimefurahi, nilitamani nimshirikishe mke wangu, kama ujuavyo Kuna vitu vidogo vidogo unamshirikisha mkeo ili mfurahi pamoja, lakini nisingefanya hivyo mke wangu alishanikataza hii mipango yangu.
Nikahifadhi mzigo wangu sehemu salama na isiyojulikana na mtu, Kisha nikataka kutoka,
Mume wangu naona juu juu tu unataka kwenda wapi,umefika nyumbani tulia, aliongea mke wangu
Nilimwangalia kwa macho ya huruma, yaani mtu sipo nyumbani kwa zaidi ya masaa kumi ningetaka kufanya ushenzi yeye angejuaje huyu ,niliwaza ni jinsi gani natakiwa niishi bila kumkera mke wangu .
Hapana mke wangu,we unajua namna ambavyo Nina muda mchache sana ,Mimi na kazini,kazini na Mimi, kwahiyo lazima Kuna nilazimishe vifanyike,Kuna fundi naenda kumuona anipe maelekezo fulani,umesahau ule ujenzi wetu?
Nilimaliza kwa swali.
Ahaaa hapo sawa,ila kuwa makini mume wangu ni usiku huu ujue.
Nilitoka moja kwa moja nikielekea kwa ESTA tukaongee jambo letu
Nilifika nikakaribishwa vizuri sana huku nikiangalia ile nyumba iliyoonesha Ina wapangaji wengi kupindukia yaani muda niliokaa pale dakika chache nilisikia matusi ya Kila aina .
Karibu ndani shemu,usifikie nje bwana njoo ndani,aliongea ESTA kwa sauti ya wizi wa mapenzi.
Hapana shemu hapa nje mbona pazuri tu,lakini pia shemu naomba mstari wa heshima Kati yetu unyooke na ubaki vile vile,niliongea kwa sauti ya kumaanisha.
Heeee dada,si tukajua huyu Ndiye shemeji ,Sasa mbona anafikia nje?aliongea mmoja wa wapangaji ambaye anaonekana mjuaji na muongeaji mzuri sana.
Hapana jamani huyu ni shemeji mume wa mdogo wangu tunaheshimiana sana,aliwajibu wale wanawake ambao ni kama wanafahamiana,nikajiuliza huyu ESTA hapa ni mgeni,Hawa wamezoeana saa ngapi?
Eeeh shemu nambie,karibu sana kwenye makazi mapya,
Ahsante na wewe hongera kwa kupata sehemu yako isiyokuwa na bughudha utajipangia mambo yako kadri utakavyo, nilimjibu
Nikaendelea
Shem lengo la kuja hapa ni kutaka nikwambie tu kuwa ile hela ya kulipia fremu na kununua vifaa imeshapatikana hivyo unaweza kunipa taratibu ni kitatakiwa kufanyika,
Waooh shemu ahsante kwa kunipigania na sijui nitakulipa Nini shemeji yangu,mpaka Sasa nashindwa kuelewa ni upendo gani uliokuwa nao wewe kwani Kila kitu unachofanya hujadai malipo yaani una moyo ambao nimepita kwingi sijawahi kumpata mtu mwenye kujitolea kwa dhati kama wewe,aliongea yote hayo akiwa kanikumbatia kwa nguvu kiasi Cha Mimi kujikuta kama nataka kuingia mkenge.
Nikamsukuma baada ya simu yangu kuita ,ni simu ya madamu nilitoka pale nikaongelee pembeni sikutaka ESTA asikie Wala ajue chochote kumuhusu madam.
Eh habari za muda huu tolu,
Samahani kwa usumbufu kukupigia usiku,
Bila samahani madam, nilimjibu.
Akaendelea,naomba kujua ni akaunti ya benki ipi nitumie ile pesa niliyokuahidi mchana.
Tuma kwenye,******
Nikitaja jina la benki akakata simu.
Nilirudi pale kwa ESTA huku nikisikia kejeli toka kwa wapangaji wasio na adabu hata kidogo.
Heheeeeeee mwanamke kujiongeza bwana,Sasa wewe unapokea mgeni badala ya uchakarike kuandaa Chakula ili mgeni ale ndipo aondoke ,weee unapiga naye stori,
Labda kungwi wa huyo mtu hakumfunda vyema,ndiyo maana tunaachika mwaya, wanaume wenyewe hamna ni wakushikilia kama muwashaji wa kibatari aliyebakiwa na njiti mbili za kiberiti mbele ya upepo mkali.
Waliongea wale wanawake kwa kupokezana Mimi na ESTA tukaangaliana.
Hawa wananisema Mimi shemu, alisema ESTA kwa manung'unuko.
Hapana shemu mi naamini kwenye mtu kuji keep busy na mambo yako usiyajali sana haya,Bali unapaswa uww na misimamo na aina nyingine ya maisha,sisemi udharai mtu Bali uyadharau Yale wanayoyaongea
Sasa hapa tumekaa hawajui Nini kinazungumzwa tayari mtu anakulaumu,dawa yao ni kuwapuuza Wala usioneshe umehuzunika we relax jifanye hujui kama walikuwa wanakuongelea wewe.
Nilimfariji ESTA baada ya kuona ananyongea.
Huku nikiwaza jinsi wanawake walivyokuwa kama watoto halafu ESTA mwenyewe haya maisha ya kiswahili plus udangaji mwingi kapitia sana, haya anajifanya yanamuumiza
Aache unafiki. Nilijiwazia moyoni.
Tulikubaliana kesho yake nimletee pesa kwaajili ya kufuata vifaa vyote vya saloon huku hela aliyonitajia pamoja na malipo ya frem ikiwa inabaki hela nyingi tu.
Lakini Dani umenisaidia mambo mengi, umenipangia chumba kama hivi, basi nakuomba uje ukione chumba ulicholipa kwa hela yako, njoo utie baraka basi.
Hilo halitawezekana na pia lazima tutafute sehemu nyingine ya kukutania kwasababu kwa hii aina ya wapangaji niliowaona wanaweza kumtafuta mkeo popote alipo ili wampe umbea nikajikuta najiharibia.
Niliongea Kisha tukaagana huku akiwa bado ana hamu ya kuongea na mimi, nikiwa njiani nilifikiria jinsi ESTA alivyokuwa akidharau miaka ile,
Ambapo nikiwa bado ile hali ya mkoani haijanitoka, siku moja tukiwa kanisani nilimuagiza , dada mmoja kuwa baada ya ibada kuisha anistulie ESTA, kweli ESTA akiwa bize na mambo yake alipata wito akaja mpaka kwangu nikiwa nyuma ya kanisa, akaja huku akionesha kunishangaa mithili ya mtu ambaye hajawahi kumuona,
Huku akinitaka niongee haraka haraka, nikafunguka mambo yangu ya moyoni , akacheeeeeeeka kidharau Kisha akaniambia , kama nataka hivyo niwasiliane na viongozi wa kanisa ili tufunge ndoa kabisa, niliona kanidharau mno nikakata tamaa hata yule mtu niliyekuwa nimemtuma aniitie nikasikie alitukwanwa sana kwa kumpotezea muda ESTA aliyekuwa hashikiki.
Lakini Leo hii kaishiwa Kawa mpoole eti niingie ndani , lengo nilale naye,
Haiwezekani kabisa, Nina familia inanitegemea alikopitapita ni kwingi hivyo lazima niwe makini.
Kwanza mpango wangu ukitiki tu ataona nitakavyokuwa mbali naye
Nilijiwazia.
Kesho asubuhi nikiwa kazini nilipokea simu toka kwa kijana wa kiume nisiyemfahamu akasema katumwa na madam anitumie hela, nikawa nimemkumbuka anajihusisha sana na mambo ya transactions, ni kijana anayetumiwa na MADAM kutuma hela ambazo si za kiofisi.
Nikapokea kiasi ambacho kilikuwa ni kingi kuliko nilivyotabiri, nilikosa Raha kutwa nzima hata yule mwanamke ambaye kwa Sasa Niko naye ofisi moja kwakuwa kazi zetu zinafanana, alinijua kuwa sipo sawa.
Mr Daniel, nakuona kama hauko sawa, kama unahisi mwili unasumbua usilazimishe kazi ni Bora uongee na uongozi wa kupe permission ukapumzike, aliongea yule dada.
Hapana mbona nipo sawa , nimejikuta nawaza tu kuhusu haya maisha.nilidanganya.
Kiasi Cha milioni ishirini ni nyingi mno, naamini ipo siku madam na ESTA watapatana ni lazima hili halipingiki Sasa nikijitoa ufahamu hapa nakuja kuaibika.
Ile hela aliyonipa Jana ,imetosha hela ya frem na vifaa Lakini pia hela niliyolipa Kodi alikopanga ESTA nilikata na bado chenji imebaki ya kutosha,
Sasa Leo imeingia hela nyingi kiasi hiki mmmmmmmh TAMAA ni mbaya yasije yakanitokea puani, niliwaza nikaendelea na kazi.
Simu ya dogo aliyenitumia hela iliingia,
Samahani kiongozi nilitaka nikuelekeze maagizo niliyopewa na madam,ni kwamba hicho kiasi alichotuma , asilimia ishirini na tano ni zako,na asilimia hamsini ni za nani sijui wewe unajua, nyingine Kaa nazo Hadi pale utakapofanikiwa kumshawishi huyo mtu,ukifanikiwa tu basi ni zako.
Nilishusha pumzi kwa nguvu huku nikitafakari juu ya umasikini ambapo nilikuwa Nina mawazo mabaya ya kumdhulumu ESTA.
Hii hela naenda kumpa ESTA,Lakini namwambiaje ,nitasema ni yaninj ikiwa kila kitu tayari kipo sawa.
Simu ya madam iliingia,
Bila Shaka umepata maagizo yangu,
Ndiyo nimepata madam,nilijibu kwa kuhema.
Sawa,naomba ujitahidi umshawishi bwana maana pengine nitapata nafuu maana Kila nikilala nahisj kudaiwa kitu na ESTA.
Alimalizia Kisha akakata simu.
Nilifikiri kidogo , akili ikaniambia lazima nimwambie ESTA ukweli maisha ya dhuluma , ukizingatia nafanya kazi kwenye kampuni inayomhusu MADAM halafu mwisho wa siku akasikia nilipiga hela zake atanionaje Mimi,
Lakini uoga umasikini,kwanza alishasema hawezi kufuatilia mipango ya ESTA,pengine naogopa bure tu ,kwani Mimi nu mahakama ya kupatanisha watu , kwanza sikumuomba , yeye ndiye aliyeanza Mara ooh nahisi namuonea ESTA.
Kumbe MUNGU anipe Nini , pengine hizi ni fadhila napewa na MUNGU baada ya kusaidia ESTA.
Kakaa nyumbani kipindi kirefu huku Kila kitu nikiwajibika Mimi , Leo hii napata hela naanza kuziogopa.
Naweza hata kukwambia madam kuwa nimeshindwa kumshawishi ESTA apatane na wewe,kwani lazima nionekane naweza ,walikoharibiana maisha na kurogana sijui,Mimi n nilikuwepo ,huyu madam vipi bwana Mimi na ESTA tumeshamalizana ,chumba kapata, pia yupo mbioni kukamilisha biashara yake MUNGU ampe Nini Tena hapa duniani?
Kama ni maisha mazuri aliyapata akachezea,pengine angekuwa mmoja wa malkia wa nguvu hapa mjini,
Leo hii Daniel napata riziki naanza kubanwa banwa .
Tena kesho ni weekend naenda kabisa kwa mganga ili awatengeneze wasije kunikumbuka.nilijiwazia kijinga sana
PESA acha iitwe PESA.
Baada ya kupokea mpunga tamaa ziliniingia nikajikuta nahalalisha uharamu huku nikiharamisha uhalali.
Ushirikina nao ukawa unaninyemelea, roho mbaya na ya kishetani iliniingia sikuwa tayari kubadili msimamo wangu.
Je, nitafanikiwa, sehemu ijayo Ina majibu,
zingatia kuwa inaitwa
MIMI NA BOSS WANGU.
Inaendeleaa very soon...............
Nashukuru sna mkuu acha nikushukuru kbal sijaanza kusoma kipande hiki mnk nimekuwa kilaabadaa ya masaa kadha bas. Nitachungulia humu kuona jipyaSEHEMU INAYOFUATA.......
Nilitoka ofisini siku ile ya ijumaa huku nikiwa najiamini kupita kiasi ili kuhalalisha ile dhuluma nilitafuta baa moja , ni matata sana nikaanza kupiga local beer taratibu huku Dj akiwa anaweka nyimbo za dansi
Nikakitamani sana kibao Cha Elimu Dunia sijui hata nilitaka niweje siku hiyo, muda fulani alikuja mzee fulani wa makamo ambaye anaonekana ana maisha ya kawaida.
Habari mzee,naona unaangaza macho unamtafuta nani?
Niliongea kwa sauti ya kilevi.
Namwangalia jamaa mmoja hapa huwa wanachukua mbuzi kwangu kwa kukopa hivyo waliniambia nije Leo kuchukua mzigo wangu, aliweka kituo.
Unakunywa kinywaji gani we mzee, niliuliza.
Hapana baba ahsante nashukuru ngoja niende kwanza usawa wa jikoni pengine nitamuona.
Siku hiyo nilikuwa najiamini huku nikiilazimisha kudhulumu japo hofu nayo haikuwa nyuma, yaani kama ningejua bangi inauzwa chimbo gani , ningenunua nivute ili ile hali ya uoga initoke.
Yule mzee nikamwona akirudi.
Aisee mwanangu nimemkosa huyu mtu nimeambiwa kafuata mbuzi hii njia ya kuelekea Bagamoyo,
Sasa wee mzee, unafanyaje biashara za kukopesha ona Sasa unavyozungushwa kama kataupepo haya umeyataka mwenyewe baba, kwanza ita kinywaji we mzee vipi bwana, utakaaje na Mimi huna hata maji mezani, niliongea kwa tambo.
Yule mzee alicheka Kisha akaagiza soda, akaendelea.....
Unajua Nini mwanangu, kwenye maisha Kuna kitu kinaitwa UAMINIFU
Hili ni neno lililobeba hatima ya maisha ya tulio wengi,
Tunahitaji tupate vitu kwa UAMINIFU,
Tunahitaji mke muaminifu,
Tunahitaji tuzae watoto waaminifu
Tunahitaji marafiki waaminifu.
Hata jambazi sugu anahitaji washirika wake wawe wa aminifu,kibaka akiambiwa na genge lake kuwa tunahitaji simu aina fulani uilete,ataenda atapora atafanikiwa atakuwa kafanya kazi kwa UAMINIFU
Tayari waliomtuma hiyo kazi watakuwa na Imani naye.
UAMINIFU hutengeneza msingi wa IMANI, je,wewe huhitaji timu ya watu waminifu?
Aliniuliza yule mzee
Nahitaji Tena sana tu. Nilimjibu
Sawa najua hilo,nilimjibu
Lakini bahati mbaya tunahitaji kitu ambacho hatuwezi kukifanya sisi wenyewe. IMANI tuliyokuwa nayo ni kwa manufaa binafsi hatujali maumivu ya wengine.
Kwa mfano Kila mwanaume anapenda kuwa na mwanamke mwaminifu,na angependa mkewe abaki nyumbani tu,huku yeye akienda club ambako anataka awakute wanawake warembo,
Anasahau kuwa huenda ni wake za watu hapaswi kuwatongoza kama ambavyo hapendi mkewe afanyiwe.
Mimi naleta mbuzi hapa,muda mwingine wanafuata wenyewe Tena hata wakiwa hawana hela,nawakopesha kwakuwa tunaaminiana,
Hata Mimi huwa nakuja hapa nikikwama nachukua kiasi Cha hela hata kama mzigo Sina.
Msingi wetu pande zote mbili ni UAMINIFU yaani kila mtu Ana IMANI na mwenzie.
Alizungumza yule mzee huku akijimiminia soda ili aimalize apate kuondoka.
Tukaagana akaondoka.
Muda wa saa tano usiku niliita Taxi ikanipeleka Hadi nyumbani nilimkuta mke wangu akiwa anaangalia tamthilia huku mwanga wa taa Ukiwa unadhuru kwa muda ule.Nikaingia chumbani nikajilaza, kuja kushtuka ni asubuhi tayari, nilitoka nikaangia bafuni huku nikijiona ni mwepesi Nina njaa lakini bado nilikuwa na hangover.nilifikiria kuhusu wazo la kutaka kudhulumu hela nikajikuta Yale maneno yanayohusu UAMINIFU aliyoyazungumza yule mzee jana yananichoma sana tu,nikajikuta nabadili msimamo ni Bora nikamwambie tu ESTA kuwa ni nani anayetoa zile hela
Kwanza Kuna asilimia ishirini na tano hizo ni zangu tu,pili kama nikifanikisha kumshawishi ESTA apatane na madam bado Kuna ganji ya maana jumla nitakuwa na asilimia hamsini kabisa,
Nikatoka nikatulia sebuleni huku dada wa kazi akiwa anatenga breakfast,
kwani huyo anaye ongea huko nje ni nani, niliuliza baada ya kusikia sauti ya kitoto kule nje
Ungejuaje kama mwanao Jack karudi, yaani mtu unarudi umelewa chakari mbaya zaidi unaletwa na Taxi.
Hivi we mume wangu umesahau shida tulizopitia tayari unajiona tajiri, wewe una hela gani kiasi Cha kufuja hela, hata mwanao Jack karudi likizo hii naamini unajua fika ada itakayotakiwa kwenye muhula mpya , nilitaka apelekwe shule za kawaida we uling'ang'ania huko,
Lakini kwa mwendo huu tutatoka kweli, alillalamika mke wangu.
Nilitoka nje nikamkumbatia my first born Jack, nilimisi sana licha ya kuwa huwa naenda Mara kwa Mara shuleni kwao lakini nilifurahi kumuona siku ya Leo.
Sasa mke Mimi natoka kidogo hata breakfast nitapata mbele kwa mbele.
Huyo tena, yeye huyo yaani umerudi usiku wa manane lakini tayari unataka kutoka , Tulia baba Leo weekend cheza na wanao basi,
Alisisitiza mke wangu
Hapana Kuna jambo la muhimu, mke wangu nafatilia, nilisema huku nainuka.
Haya nenda, nenda kazichangie hizo kampuni za vinywaji, Tena kunywa maana wewe si sheli ya kuwekea beer, sikujali nikashika njia huku nikimpigia ESTA nijue alipo,
Akanieleza kuwa yupo kwenye hiyo ofisi yake, nilifika pale nikimkuta na vijana wawili ,
Aaaaah afadhali umekuja, shemu yaani siamini kwa kilichotokea kumbe bajeti ya kwenye makaratasi siyo kabisa yaani nimejikuta nanunua vitu nusu nusu kwakuwa hela haikutosha kabisa.
Unajua Nini huyu dada hii biashara licha ya kuwa anaijua vizuri lakini alifanya zamani sana, hakujua kuwa kwa Sasa bidhaa zipo juu halafu, maana kama unavyoona hapa kunatakiwa kabati fulani la kisasa pamoja na vitu vidogo vidogo vingi lakini pia Kuna enga za kisasa zinatakiwa kwaajili ya kutundika vitu kiustadi kama nywele za bandia na vinginevyo vitakavyomvutia mteja
Alisema kijana mmoja ambaye alikuwa anatengeneza socket ya umeme.
ESTA akanivuta pembeni kidogo ili maongezi yetu yasisikike.
Unajua Nini shemeji hata hivyo sijui nisemeje juu ya msaada wote ulionipa Mimi nashukuru sana. Vitu vingine nitaweka kadri siku zinavyokwenda kulingana na ujio wa wateja, kwanza unalionaje hili eneo hopo mbele mita chache Kuna soko pia huku Kuna zahanati yaani ni sehemu fulani ambayo inawakutanisha wanawake Mara kwa Mara na pia hili eneo hakuna saloon ya nyingine ya kike.
Naiona kabisa biashara itakavyokuwa hapa.
Aliongeza ESTA akiwa kafurahi sana.
Tukatafuta sehemu tukakaa, nikavunja ukimya
Shemu we ni mcha MUNGU sana, umeamua kumrudia MUNGU hali ambayo imeonesha ukomavu fulani kwako.
Amina, aliitikia
Lakini mbona Kuna vitu huachilii ,Kuna mambo bado yanakushinda shemu kwanini?
Niliuliza kwa mtego
Fafanua vizuri shem mbona Mimi Niko poa sana tu, makosa ni sehemu ya maisha ya binadamu kama Kuna mtu nilimkwaza pengine hata wewe naomba uweke wazi, alihoji.
Hapana siyo Mimi Wala nani ,
Ni kuhusiana na yule mwanamke aliyekuwa boss wangu, yule anataka mpatane , lakini shem hutaki , mbaya zaidi alikupa namba zake pale dukani lakini ulifuta hutaki kuwasiliana naye, kwanini? Niliuliza
(Alicheka kidogo)
Shemu bwana, kumbe ni huyo, kwahiyo unadhani kutokuwa na uhusiano na huyo Mimi napungukiwa Nini, Mimi kwanza sijamchukia, nina maisha yangu na yeye ana maisha yake, kama ni huyo shemu asikusumbue, Mimi nashukuru tu kwamba shemu una moyo ambao sijawahi kuona kwa mwanaume yoyote, hata matajiri wanaweza kukupa unachotaka lakini wakakufanyia vitu ambavyo si vya kibinadamu.
Kama ni huyo boss wako shemu usihangaike naye ni mpuuzi tu utajiri wake Mimi haunihusu acha nianze upya haya maisha. Alisisitiza.
Shemu Mimi naamini unaisoma vyema biblia, kukiwa na maandiko yanayosema,
Litakalofungwa Duniani na mbinguni limefungwa,
Lakini pia
Litakalofunguliwa Duniani na mbinguni kitafunguliwa.
Niliweka kituo.
Shemu unaniacha njia panda sana nashindwa nikujibu vipi baba yangu huyo mtu simtaki, unayosema kuhusu maandiko ni kweli naona Kuna kitu nimejifungia lakini acha iwe hivyo shemu simpendi na simtaki, alinionea mno huyo mtu, aliongea huku
akitaka kulia.
Shemu Mimi mwenyewe waliniweka ndani niliumia sana lakini yameisha na maisha yanaendelea hakuna sababu za kuweza kuhifadhi mambo ya zamani moyoni, halafu jambo jema ni kuwa yeye ndiye anakuomba myamalize,
Hebu fikiria shemu,boss mwenye pesa kama yule anakubembeleza wewe mtu maskini huoni kwanza ni kama bahati, nilihoji
Shemu kuhusu wewe kuwekwa mahabusu uliwekwa kisheria si ulipoteza mzigo?halafu pili ni kosa dogo kulinganisha na aliyonifanyia Mimi yule ni shetani nakwambia.sitaki uhusiano naye
Moyo unanisuta kuhusu dhuluma niliyopanga kuifanya,
Madam anaomba Leo kesho apatane na ESTA, lakini ESTA naye hataki Tena hayupo tayari kabisa , nawezaje kumshawishi akakubali,
Je ni kweli nitashindwa, mimi mwanaume ?
Sehemu ijayo Ina majibu
Itaendelea.......