SEHEMU INAYOFUATA.....
Licha ya ESTA kunifumbua macho na masikio juu ya kile ambacho sikuwa nakifahamu kabla,
Nilipanga kutokubadili msimamo wangu.
Yule jamaa kaja mpaka hapa kwangu akiwa na kusudi moja la kufanya kazi na mimi.Na sidhani kama Nina hadhi ya kufuatwa Hadi nyumbani na yule jamaa anayeonekana pesa si tatizo kwake.Nilijisemea moyoni.
Mume wangu,
Naona Kuna mapya hapa Sasa sijui itakuwaje,maana tunaambiwa kumbe hizo ni kampuni za mtu mmoja,
Huoni kama pengine ni mtego mume wangu? alihoji mke wangu .
Hapana,ni lazima niende kwanza wale ni watu wakubwa na maarufu hapa mjini hawawezi kuhangaika na Mimi ambaye Sina hata kipato Cha kueleweka,hivyo ni lazima nifike tu hiyo kesho.nilijibu pasipo kusita.
Sawa mume wangu wote hapa tunakuombea.
Asubuhi ya saa tatu asubuhi tayari nilikuwa maeneo ya mjini huku nikisikia upepo wa fulani kuashiria nipo karibu na bahari nikiwa nimeshika njia kuelekea kwenye ofisi za kampuni mpya
Nilifika huku walinzi wakinihoji maswali mengi ambayo niligundua ni kwa sababu nipo kwa miguu.
Oyaaa we ngosha, hebu mkague kwanza huyo, chunga sana hawa wanaokuja kwa miguu wanakuwa wanetumwa kuja kupeleleza watu
Aliropoka mmoja wa wale walinzi huku mkoba wangu uliobeba CV Ukiwa wa kwanza kufunguliwa.
Kisha nikasachiwa kibabe kuasi Cha wale walinzi kuchafua kaunda suti yangu, sikumaindi sana, labda kwakuwa hawanijui lakini pia ni taratibu za kazi maeneo mengi.
Nikaingia mapokezi nikamkuta jamaa mmoja aliyenichangamkia vizuri sana huku akiniita kwa majina huku nikiwa simjui , lakini haikunipa shida, pengine kapewa maelekezo na wajihi wangu,
Niliruhusiwa kuonana na bosi huku nikipandisha ngazi, kuelekea kule juu ghorofani ilipo ofisi yake, nilikaribishwa kwa heshima zote huku akiwa mchangamfu sana.
Sikutaka kuonesha hofu yoyote nilijilazimisha kujenga tabasamu fake huku nikiwa makini kuliko umakini wenyewe huku nikijiandaa kama yatajitokeza maswali ya kimitego.
Karibu sana bwana, bwanaaaa nani vile,
Nikamtajia full name.
Eeh ok ok,
Bila kukuficha bwana Daniel nilizisikia taarifa zako juu ya upotevu wa chombo sijui, kitu gani vile.
Ni hydraulic separator na pini joint za excavator, nilimjibu huku nikiwa Sina uhakika kama zinaitwa hivyo.
Ahaaaa ulienda kuzichukua mkoani siyo?
Ndiyo bosi . Nilimjibu jamaa huku akiwa anatafuna tafuna vyakula fulani vya asili ya uarabuni huko.
Sawa,hata hivyo kipindi tupo Oman na mzee ,tulizipokea taarifa zile tukakufikiria vibaya kupita maelezo
Lakini licha ya yote mzee wangu alikuwa njia panda,
Yaani alikuwa akikusifia sana kuhusu uchapakazi wako.
Kwani wewe boss unamwitaje?
Swali ambalo lilitakiwa kuishia kufikirika kichwani nilijikuta nimeropoka
Akacheka sana,
Ndiyo Mimi ni mtoto wa kwanza wa mzee (jina kapuni).
Najua umeuliza hivyo kwakuwa nilikudanganya nilipokuja siku ya Kwanza
Nilimwangalia, huku nikimuona kafanana sana na na boss wangu. Tuliongea mengi sana muda ule.
Ujue Daniel yule boss wako ambaye Mimi ni mama yangu mdogo alituaminisha mambo mengi sana kiasi Cha sisi kutaka kukuchukua ili tukuhoji. Pengine ni umetumwa kuja kudhohofisha kampuni zetu.
Lakini baada ya kukuchunguza tuligundua huna unalolijua ndugu yangu pole sana,
Japo nikukumbushe kuwa makini sana ujue kitendo Cha wewe kuibiwa mzigo stendi umeonekana mzembe kuliko maelezo, hii inaleta tafsiri ya kwamba wewe ni mtu wa kuwaamini sana watu haraka haraka.
Sikupaswa kuyasema yote haya ila Mimi nasema kwa upendo tu kwa kuwa wewe ni kama ndugu yangu
Najua nilipokuja kwako siku ile ulishangaa nimefikaje, lakini ni kwamba baada ya wewe kuwekwa ndani Kuna watu walikupeleleza sana kujua unaishi wapi, una familia gani lakini pia nje ya kufanya kazi na sisi unajishughulisha na Nini.
Taarifa zote zililetwa huku tukiwa tunakuchukulia kwa uzito wa juu. Kabla hatujagundua kuwa wewe ni mwepesi tu.
Hata hivyo kazi ya hapa nayokupa ni kubwa zaidi tumeamua kufanya hivi kwakuwa unafiti kukaa hapa lakini pia mzee alikuhurumia wewe kuteseka kule mahabusu, Sasa tukaamua kukupa nafasi nzuri, ila nafasi yako ya Sasa nikwambie ukweli, inahitaki umakini wa hali ya juu,
Ni kwamba utashughulika kuidhinisha vyombo vyote vya site
Yaani Equipments kwahiyo, chombo gani kibovu, kinahitaji kufanyiwa service gani, kinataka kiwekwe spear gani we ndiyo utakaye shughulika ukishirikiana na fundi mkuu wa hii kampuni,
Najua huwa Kuna asili ya majungu sana Kati ya mafundi wadogo na wale ma operator hata hivyo wewe komaa kwenye eneo lako tu , mtu ambaye ataharibikiwa na chombo Chake atamuona fundi mkuu wa site ya kule ambako ulikuwa unatumwa zamani.
Halafu taarifa zitamfikia engineer mkuu ambaye wewe utashirikiana naye kuingiza taarifa kwenye computer na sehemu mbalimbali
Kwasababu huwa Kuna ufanyaji wa maghumashi kwa mafundi kuharibu vyombo kwa makusudi Kisha kutafuta mianya ya kupiga hela.
Hivyo nafasi yako itasaidie kampuni kujua vifaa vilivyoharibika kihalali.
Haya yote nimekwambia kwa upendo tu, sikuwa na haja ya kukuelekeza, kwahiyo nenda kule mapokezi kanisubiri Kuna watu watakuita mida ya mchana baada ya kutoka lunch.
Alimalizia bosi huku Mimi tumbo likiwa linanikoroga kwenye kazi ambayo niliona imekaa kifitini zaidi.
Nilikaa pale nje huku nikifikiria vitu vingi ambavyo hata kupoteza ule mzigo wa kwanza ndugu zangu walihesabu ni ushirikina,kutokana na bifu za mafundi na Mimi Leo hii hata huku wananiweka huku huku Tena mbona ule mtego aliokuwa anasema mke wangu ndiyo huu naouona
Wakati nikiwaza hayo, alikuja mwanamke umri Kati ya miaka 30_35 .
Mr Daniel nifuate ofisini kwangu,
Nikainuka nikamfuata Hadi kule ambapo niliwakuta wanawake wengine wawili , walinikaribisha kwa bashasha mno huku wakiwa na tabasamu na lugha rafiki,
Nikaanza kupigwa spana na wale mademu ambao nadhani nje ya taaluma zao nadhani wapo pale kwa kigezo Cha uzuri wa sura na maumbo yao, niliulizwa maswali kadhaa, nikawajibu vizuri kabisa.
Taratibu zingine zikaendelea huku nikishangaa baada ya kupewa kazi tofauti kabisa na ambayo boss aliniambia pindi tunapiga stori
Cha kuingizwa kwenye computer kiliingizwa Cha kuandikwa kiliandikwa pa kusaini nilisaini, nikimuona ni mkataba rafiki usiotisha .kisha nikaongozana na mwanamke mwingine ambaye ni kama waigizaji wa kimarekani ambao ni ndoto kuwapata,
Tukafika mpaka kwa boss,ambaye aliniangalia kwa kutabasamu baada ya kuona nimepewa kazi tofauti.
Alijaza baadhi ya documents huku kazi yangu ikiwa ni kuanguka signature tu,kisha akamwambia yule dada atoke tukabaki wawili tu.
Safari hii hakuwa na maneno ya kirafiki Bali Kila alichosema alimaanisha,nikajua tayari nishakuwa mfanyakazi wake rasmi,hapa Dani utatakiwa kuripoti kazini kuanzia keshokutwa ,lakini pia nimetoa maelekezo kutoka ile kampuni yako ya mwanzo kwamba wewe utakuwa huku kwangu na mzee anatambua upo huku.tuliagana nikaondoka kwa furaha huku nikipewa laki elfu hamsini ya nauli
Nilifurahi sana hasa baada ya kuambiwa mshahara bwanaaaa.
Asikwambie mtu maisha ni kazi,na utamu wa kazi ni pesa.
Kubwa zaidi kazi niliyokuwa naiota hatimaye ninayo rasmi.
Ni kazi ya ndoto zangu.yenye malipo sahihi na hatimaye Kila kitu kimetimia.
Maisha tunayoishi karne hii ni ya kisasa, na ukisasa umeitawala Dunia haichagua masikini Wala tajiri.
Kila kitu kinaongozwa kisasa,na Kila kitu Cha kisasa ili ukipate ni lazima uwe na PESA.
Maisha ya kumuoa mtoto wa mtu Kisha kumpa Mashamba ni vitu vimepitwa na wakati
Hata wale wanawake wazuri duniani kote Ukiwa na pesa ni rahisi kuwapata, tunaishi Karne ambayo miliki pesa kidogo ugundue tabia za wanadamu hata huyo unayemwita mama mkwe yaani mama wa mkeo Ukiwa na pesa anaweza kukwambia neno la kufuru. Ukaambiwa hicho ulichokiona kwa mwanae yeye anacho Mara mia yake.
Ndiyo, mbona ni mambo nayasikia sana,.
Pata hela halafu ingia klabu matata halafu ukaone wale vidume wanavyojigongesha kwako.
Kama ni mgeni wa mambo ya mjini huwezi kuelewa, lakini ni kwamba hao vijana ni wale ambao wameamua kutusaliti wanaume wenzao kwa sababu wanazozijua wao, ama kweli Dunia inaisha.
Niliwaza sana kabla ya kushtuliwa na konda wa daladala,
Oy jombii vipi unageuka nayo nini,
kuangalia nakuta wale abiria wote wameshuka, gari inajiandaa kugeuza nikagundua nimepitiliza zaidi ya vituo vitano, kuangalia saa no saa kumi na mbili pia simu missed calls ni nyingi sana, nikatulia kwenye siti tayari kwa kurudi, ili nikashuke karibu na kwangu
Yule kinda nilimpa nauli yake akauliza wapi tena kiongozi mbona ulipandia mjini, hujashuka naona unarudi vipi.
Hamna nilipitiliza kituo, nashukia kituo Cha (nikataja)
Kama ni hapo tu shika pesa yako.
Wakati nikiikagua simu nikagundua imepigwa na watu wanne, ila boss wangu wa kike pekee kapiga Mara kumi na tatu, zingatia ni zaidi ya Mara kumi.
Huyu naye anatafuta Nini, nimefanya miezi minne tu kwao Sina ninachowadai na wao hawanidai
Ina maana hawajawasiliana kwamba Mimi nimechukua mkataba mwingine kwenye kampuni kongwe?
Kama nistahiki zangu Mimi nilishasamehe, pale najua nitakanyaga kwa sababu hizi kampuni zina ushirikiano.
Lakini si kwaajili yake huyu, anataka nini kwangu?
Oy kiongozi unawaza Nini tayari ushafika,konda alinishtua pengine ningepitiliza tena
Sehemu ijayo Ina majibu,kisa kinaitwa MIMI NA BOSS WANGU unataka kujua ni boss gani, bado kisa kibichi.
Itaendelea.....