Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

SEHEMU INAYOFUATA...........

Nilizubaa zubaa pale stand ya ubungo,huku simu ikiwa inaita kwa fujo, lakini bado akili yangu ilitaka nionane ESTA kwanza,nikamalize haja zangu maana ,kutokana na ratiba zangu kubana.

Sioni muda mwingine nitakaopata,

Jamani Dani,umeniambia umeshafika,mbona muda unazidi kwenda ,fanya haraka bwana nataka niwahi kurudi,alisema ESTA upande wapili

Uwahi kurudi? kurudi wapi, Mimi nilitegemea nachukua logde tunalala,mpaka asubuhi,hayo mambo ya short time hayo bwana mi siwezi,sisi ni watu wazima mamaa,
Niliongea kwa sauti ya kukata tamaa,

Hapana Dani,natambua hilo lakini jua kuwa hata Mimi ni ratiba zangu ambazo sitakiwi kuzivunja,hata hivyo kumbuka nilikukatalia muda mrefu sana kuwa kwa Leo ratiba zimebana ukaniambia unahitaji masaa mawili tu ya kuwa na Mimi, iweje unanibadilikia unataka tulale,aliongeza ESTA

Nikaona dah,ni kweli nikiwa nambembeleza alikataa hata hivyo nikamuomba masaa mawili, yaani ni Kama maneno ya kutongozea , kumbe kashikilia hapo hapo, siyo mbaya hata Kama nusu saa lazima nikamvue nguo yule,

Simu ya mke wa boss iliingia,

Naam boss,nilisema hivyo baada ya kupokea

,niambie Dani umefikia wapi,hujaingia Dar es salaam bado?

Ah samahani boss gari nililopanda nilitegemea niingie saa kumi,hata hivyo liliharibika njiani lakini pia Kuna jamu tuliipata njiani foleni imechukua muda kifupi ndiyo naingia muda huu,

Jamani Dani my friend,tumetumia muda mwingi sana kusubiri hicho kifaa,na imani yetu wote,ipo kwako lakini mbona ni kama unatoka nje ya mstari,kiufupi fanya mpango hiyo spare ifike,kesho ipelekwe site

,alisema mke wa boss safari hii akiwa anaamrisha,

Nikaona dah mbona ishu ishakuwa ngumu nirudi kule store nifate spare Mara kuipelekaaaaaa,

Ah sinitafika nyumbani saa usiku wa manane Mimi,wakati nikiwaza hayo nikapokea simu yenye code number ya South Africa, nilitetemeka kidogo kwakuwa nilishajua,

Halooo,sauti ya bosi wa kiume ilisikika Mara tu baada ya kupokea simu,

Daniel, Daniel, Daniel nimekuita Mara tatu,sihitaji maelezo mengi,kifupi mbona unatupa wasi wasi? Alisema yule boss wa kiume.

Nilijitetea sana ,Tena sana kwamba spare ninayo na kesho asubuhi amtume dereva aifuate,hakujibu kitu lakini baada ya dakika tano nikapokea sms toka kwa boss boss mwanamke ikiwa inasomeka

"HATUKUELEWI"

Nikaona ni wasiwasi wao tu mbona Kila kitu kipo ok.

Nikampigia ESTA nimfahamishe kuwa tayari nakuja,

Naomba uwahi yaani sitalala maana nahitaji nirudi kikajiandae maana kesho Nina safari Tena ni ya lazima kwahiyo nakwambia kabisa ili usije kunibadilikia maana wanaume ndivyo mlivyo nyinyi.

Nikaishika barabara ya Sam nujoma kuelekea alipo yule ESTA.

Lakini wakati huo nikaona nimpigie wife maana tangu nipo kwenye gari ya mkoa niliongea naye saa nne asubuhi,nimeshuka kwenye gari naongea na watu wengine tu,

Ngoja niongee naye nimwambie gari imeharibika njiani kwahiyo sitafika Leo,

Mke wangu akapokea simu tuliongea mengi ya hapa na pale huku akinitaka niwe makini,

Lakini mume wangu,naomba ruhusa kesho nataka nimsindikize rafiki yangu mahali fulani,

Ni wapi unaenda,niliuliza

Akataja ni maeneo ya njia ya kilwa road kuelekea Mkuranga huko,

Nikauliza ni nani unampeleka,huko

Akajibu,

Ni yule rafiki yangu aliyekuja siku ile akajitambulisha kwa jina la ESTA,
Unajua Nini mume wangu yule ile siku anakuja pale nyumbani alikuwa na mambo mengi ya kuongea hata hivyo,we ulikuwa una haraka tu,ni kwamba yule ni muathirika anaishi na virusi vya ukimwi mwaka wa tatu Sasa hata hivyo yeye dozi yake huwa anachukulia hospitali ya..........(akaitaja hiyo hospital)

Kwahiyo Kuna ulazima gani wa wewe kwenda huko,niliuliza huku nilitetemeka baada ya kusikia habari inayomuhusu ESTA,kumbe nimwathirika huyu,nikaanza kumchukua ghafla kana kwamba yeye ndiye aliyenitongoza.

Mke wangu akaendelea,,

Hapana mume wangu,siyo kwamba lengo ni yeye tu hapana nahitaji kwenda kuangalia/kukagua Mashamba yetu ambayo Kila siku unanilaumu kuwa umenunua rasilimali za wote lakini nashindwa kuzifuatilia,nilimpongeza sana,huku nikishuka kituo Cha karibu kabisa nikighairi safari ya kwenda kwa ESTA baada tu ya kusikia habari hiyo mpya kwangu, kwahiyo alitaka kuniua huyu malaya nilitukana kimoyo moyo,

Nikampigia simu kuwa nimepata dharula kwahiyo hakuna uwezekano wa kuja Tena,akalaumu kiasi japo alinielewa.

Nikatafuta logde nyingine nikalala,

Asubuhi nilishitushwa na simu ya dereva wa kampuni akiwa anataka tukutane ubungo tuchukue kifaa chetu,

Muda wa saa mbili nikafika pale ubungo terminal nikimkuta dereva fulani mwenye lafudhi ya kimakonde akiwa kachangamka huku nikicheka chinichini alivyojipigilia suti yake iliyopauka na tai paana,haoooooo

Tupo store na wahudumu wa pale waliangalia vyumba vyote hatukuiona store pekua pekua na wewe hakuna kipindi hicho shati langu lote limeloa kwa jasho,ikabidi niwashirikishe maaskari waliokuwa kituo kidogo Cha mule ndani ,licha ya wale vijana kuhojiwa bado walidai ilikuwa ndani mulemule,

Nikaona mtihani huu, lakini yule dereva aliwaambia maaskari kuwa niwekwe chini ya ulinzi ikiwa ni maelekezo toka kwa boss wake,

Maaskari wakataka simu ipigwe kwa boss wajiridhishe,wakidai wananiwekaje chini ya ulinzi,wakati Mimi niliwakabidhi watu hiyo spare na waliokabidhiwa wanakiri waliipokea,lakini

Upande wa pili bosi alisema kuwa Hana uhakika kama kweli hao niliwakabidhi maana usumbufu niliuonesha tangu jana,huenda hao vijana wa matoroli wanajichanganya tu lakini spare hawakuipokea,

Watu wakapata pointi kuanzia maaskari Hadi wale vijana wasukuma matoroli wakanigeuka nikawa chini ya ulinzi rasmi.

Inaendeleaa usichoke..............
.,,,,
jitahid iwe leo leo mkuu. maana yoga nae kule kasema tumsubili next week
 
SEHEMU INAYOFUATA.......

Dunia hadaa, ulimwengu shujaa,

Ni maneno yaliyokuwa Yanamtoka Askari mmoja baada ya kufikishwa kwenye central moja maarufu hapa mjini.

Malizia huo mkanda basi,we fala ,yaani mnatumwa ma mabosi wenu halafu mnaleta tamaa,ila tambueni kuwa Sheria ni msumeno .

Kila siku tunawatafuta watu kama nyinyi wasio waaminifu,na jeshi letu lipo makini tutahakikisha mnafikishwa kunakostahili,hebu njoo huku,

alimalizia yule Askari huku wale vijana wake wakinisukumiza niingie selo kwa nguvu,

Niliomba sana nipewe simu angalau niwasiliane na watu wangu wa karibu ili wajue nilipo nilikatazwa huku nikitishiwa kupigwa.

Niliyaanza maisha mapya ya selo,huku kukiwa na amri kadha wa kadha,ikiwemo kusachiwa kinguvu kwa mahabusu wapya,kupigana kusikoisha huku,wale wanaoletewa vyakula na ndugu zao wengi wao wakiporwa kinguvu na wababe wa mule kwa kuzidiwa nguvu

Niliwaza sana nikiwa mule, niliwaza kuhusu familia yangu,niliwaza kuhusu hatima yangu tangu nilipokuwa Sina kazi Hadi kuipata hii kazi yangu mpya.

Nimekatazwa kuongea na ndugu zangu,je,watajuaje nilipo.halafu hapa Kuna marafiki zangu maaskari Tena wakubwa sana tu,wangeweza kunisaidia hata kupiga simu tu,

Machozi yakaanza kunitoka bila kujua,

Oyaaaa wewe Carlos,muone huyu mnyasa machozi Yanamtoka,

Alisema dogo mmoja akimwambia mahabusu ambaye tangu naingia niligundua ni mbabe namba moja na amepinda kweli kweli, yaani kavaa Pete kidoleni nikajiuliza maswali mengi sana.ina maana maaskari hawamuoni

Oyaaa we mluga luga acha kujiliza hapa siyo hospital sawa,hapa hakuna atakaye kuonea huruma,mnayakanyaga huko huku mkiwa mdebwedo namna hiyo.na ole wako utoe sauti nakuwamba makofi,aliongea huyo Carlos huku nikimwangalia ni mtu wa kawaida tu yaani watu mabonge na wanyanyua vyuma wote ambao niliona wanammudu kutokana na miili yao Hawakuthubutu hata kumsogelea.

Nilitamani nimjibu,lakini nikakonyezwa na baadhi ya wafungwa/mahabusu wakinitaadharisha Nini kitatokea.

Siku ya kwanza tu ndiyo hivi,hapa si tutauana,Mimi akinichokoza mtu sikubali,lakini wakati nainuka niende chooni niligundua sitaweza kupigana,

Wakati nashuka ubungo sikula Chochote ile Jana, nilitegemea tutakula nikiwa na ESTA.

Lakini mawazo ya hapa na pale kwa taarifa niliyopewa na mke wangu kuwa ana ukimwi,nilighairi hata kula nikalala tu wakati hata huko njiani sikula vitu vya maana,

Lakini pia,asubuhi nilikurupushwa mapema mno nikaona nikachukue mzigo wa watu kama kula nitakula tu haikuwa hivyo,mpaka nawekwa chini ya ulinzi kule Ubungo sikuhisi njaa tena,time hii nikajikuta mwepesi tumbo halina kitu,licha ya kuwa sikuhisi njaa.

SIWEZI KUPIGANA.nilijisemea

Huku wakiongezeka mahabusu wangine, ambao wasio jua taratibu za mule walitaka kupigana lakini walichangiwa Hadi walinyoosha mikono,

Muda wa kulala ulifika hapa nilishuhudia ukatili wa hali ya juu mno yaani mnalala mchongoma, yaani yule Carlos kakaa katulia tu huku akitoa maelezo kwa vijana wake wanapiga watu,nikaona hapa si mchezo we tolu nyoosha miguu mwenzio alale,halafu usiangalie juu ukajifanya una mawazo sana lala ubavu,umeacha kitanda nyumbani kwako ukaona huku ndiyo kuzuri,Sasa nikwambie tu kuwa huku utafuata taratibu, nilishikwa na hasira baada ya kukumbuka nyumbani kwangu aiseeh
Nilirusha teke huku nimelala chini maana mi ni mrefu,

Aisee kipigo nilichopata kama si ujio wa maaskari pengine ningekufa yaani nilipigwa kama mwizi watu zaidi ya kumi walinichangia huku kukiwa hakuna anayeamua watu wanaogopa

Maaskari wakaja wakatupiga virungu vya uongo na ukweli huku nikiwaeleza kuwa nimeonewa lakini waliishia kunitolea lugha chafu.

Nikalala na maumivu makubwa mno,asubuhi ikafika,huku nikiangaza macho huku na huku nikiona mahabusu wameongezeka na alikuwepo jamaa ambaye sura yake sikuiona kwakuwa alikuwa bado kalala.

Wakaja maaskari watatu akiwemo mwenye OCS,we muamusheni huyo anadhani yupo nyumbani kwake hapa,akaamka huku nilijiuliza mbona huyu anaonekana kama anaogopwa?

Tukahesabiwa mahabusu wa Jana,na wale walioingia usiku mnene wakachukuliwa idadi yao Kisha maaskari wakiondoka,nilijaribu kuwaita maaskari niwaambie jambo lakini nilizuiwa kwa kuangalia jicho baya na wale watukutu,maaskari wakaondoka.

Vipi Simon,uko poa umeingia saa ngapi tena,aliuliza dogo fulani anamuuliza mahabusu yule,

Ni mida ya saa kumi alfajiri,Hawa wakuda wameniotea bwana Leo ningekuwa tajiri homeboy,

Aliongea yule Simon huku, akionekana ni mwenyeji mle ndani ni kama kwao,

Pale kwenye Kona analala nani,

Yule mbabe Carlos akajibu,ni Mimi mkuu,nikaona ama kweli Kila mbabe na mbabe wake,

Kuanzia Leo tafuta sehemu nyingine ya kufumba(kulala)hapo nitakuwa nafumba Mimi sawa,, aliongeza yule Simon huku wengi wakimwita Sai mule ndani,

Yule Carlos akahamisha maji yake,akaenda kumfanyia ubabe mwingine ili amnyanganye ile sehemu,

Oyaaa vipi home boy,mbona unawatoa watu kinguvu,acha watu wafikirie kesi zao,ni namna gani wanatokaje, siyo kuwafanyia ubabe usiokuwa na maana,au mnasemaje wanangu wote tukajibu NDIYOO!!!!!?

Aliongea yule Simon,

Kama we unaitwa Nani ,yule dogo akajibu naitwa Roja (Rajabu)

Jamaa likacheka,una kosa gani ,

Dogo akajibu, niliangusha gari ya bosi nikaiharibu pamoja na mizigo iliyokuwa ndani,

Hii siyo kesi dogo,jitahidi tu ukifika mahakamani hakuna kesi hapa,

Maana ulivyo,ukienda jela utakuwa Chakula Cha wahuni maana umezubaa sana.aliongea yule Simon.
Watu walicheeeeka,huku yule dogo akijawa na uso wa hofu.

Tofauti yake na Jana ambapo watu walikuwa wanazuiliwa hata kupiga stori Leo watu wakawa na amani kiasi,nikaona nisiwe nyuma lazima huyu Carlos anayeonekana ana hekima niongee naye nikamsogelea na kumuita bro huku nikijua namzidi miaka mingi lakini nikijinyenyekeza kidogo,

Eeh vipi kaka mbona umevimba uliiba Nini nikamwambia nilipigwa mule ndani,akanijibu mule mkorofi lazima apigwe tu.

Sikutaka mambo mengi,nikamweleza tu kuwa nahitaji kuongea na maaskari ili nitoe maagizo fulani lakini pia masuala ya dhamana,nikimsisitiza kuwa muda wote sikupata nafasi kuwaogopa wale vijana,

Akajibu ni sawa,ila Kuna utaratibu wanatambua janjajanja ya mahabusu wapya kutwa kukaa mlangoni Kila mtu akihitaji kuongea na Askari hali inayosababisha kuwa kero na hayo na ubabe wa mule ndani ni maagizo ya maaskari kwa mahabusu anayejifanya kichwa maji.

Hata hivyo afande akija utaongea naye bro hakuna taabu, kwani una kosa gani, nikamweleza kwa kirefu makosa yangu,

Pole sana ndugu hata hivyo,mbona kesi ndogo hii,sema we komaa na maafande upate mawasiliano na ndugu zako,

Wakati hayo yakiendelea alikuja afande ninayemjua,na ananijua akiwa anawaletea vitu fulani wahuni wa mule... .

Itaendelea.
 
SEHEMU INAYOFUATA.....

Ooooy oy oyii Mmarekani,Mmarekani,waliimba vijana wa mule wakiwa Wanafurahia ile mikate waliyoiletewa,

Aliponiona alishangaa sana,oyaa bro vipi Tena uko huyu,hebu sogea mlangoni,nikamfuata alipo
ni bwana mdogo fulani namjua mvuta bange na sijui hata alipataje kazi ya upolisi tangu sekondari alikuwa mtu wa mjani,

kifupi ni kwamba tunaheshimiana kulingana na wadhifa niliokuwa nao,

Afande Amina yupo hapa,niliuliza

Madam hayupo hapa mbona ni kitambo kahamia Tabora kwani huna taarifa,halafu si demu wako yule alishindwaje kukupa taarifa,

(Kwa sauti ya chini)we samahani mke wa mtu yule Niko humu ñdani unataka kuniongezea misala?

Hapana bro nakutania tu najua hujatembea naye ila tuligundua anakukubali sana yaani wewe tu ndiyo ulichelewa bro.

Oyaa American cop,mbona chete tu,(kidogo)wakimaanisha kile walichokikuta kwenye ile mikate,unayumba afande wetu,halafu we mwanetu ujue, Sema ndiyo hivyo tu ulichagua kazi ya kisnitch lakini we ndiyo Jesus na mwokozi wetu,walizungumza wale wahuni.

Hebu keleleni nyie,halafu habari za kunizoeazoea sipendi sawa,nikiingia humo sitakuwa na msalia mtume.aliwasisitiza yule afande ambaye nilimuona kabisa Kuna miiko ya kiaskari anaikiuka.

Sawa bwana,Afande Juma naye,

Huyo yupo hapahapa ila kwa Sasa kachukua likizo fupi,kwani bro una tatizo gani,aliuliza yule afande

Nikamjibu na kumweleza mwanzo mwisho,

Sawa,nimekumbuka OCS alikuwa anaongea na boss mwanamke mmoja kuwa wahakikishe hapewi dhamana,na licha ya OCS wetu kumwambia kuwa dhamana ni haki ya mtuhumiwa na kosa alilotenda halimnyimi dhamana,yule mwanamke alikaza kwamba lazima amtese kama alivyomtesa yeye kwa kumnyima usingizi, hasa hapa nikilinganisha na maelezo yako naona ni wewe kabisa.alimalizia yule afande,. Moyo Ukiwa unadunda kwa Kasi nilihoji Sasa utanisaidiaje ili tu ndugu zangu wapate taarifa.
Nilihoji kwa pupa,

Usijali nitakusaidia,umesema simu yako ni aina gani?

Nikamtajia ilivyo,akafikiria kidogo Kisha akasema

ndugu yangu pole sana,nitajitahidi hata hivyo hili suala si jepesi kama ni wewe ambaye ulikuwa unazungumziwa.akaondoka

Nilihuzunika sana,nikarudi nikakaa nikajiinamia huku machozi yakinilenga baada ya kuona bado kama masaa mawili tu nilale nianze kuitafuta siku nyingine,

Kesho asubuhi,walikuja maafande wakatuhesabu kama kawaida huku dhamana zikitolewa watu mbalimbali wanatoka lakini kwangu bado ilikuwa ni zile hesabu ngumu za Isaac Newton mbele ya mwanafunzi wa darasa la kwanza.

Saa saba ulikuja ugali ambao nguvu yako ndiyo mtaji wako,lakini sikugombania kwakuwa sikuweza,nilichoka nilihisi maumivu nilifikiria kesi yangu, nilifikiria hatima yangu nikajikatia tamaa,

Wakati zaidi ya watu sabini na hekaheka za kugombania ugali kwenye visado huku wazee wakipigwa vikumbo lakini hawakubali mimi nilibana kwenye Kona yangu.

Oy bro samahani usichague chakula humu ñdani,utakufa njaa hata Kama ni kibaya wewe Kali kuweka kitu tumboni,nenda kachukue alisema yule dogo huku akilamba vimchuzi kana kwamba ni vitamu sana.

Nilikaa,nikakaa Kila afande nikidai basi nipelekwe mahakamani hawataki nikawa Sina namna.nikaanza kuzoea mazingira ya mule ndani,uoga ukanitoka,huruma ikanitoka Kuna mzee mmoja aliingia siku hiyo ikawa ana ndugu wengi akaletewa Chakula kwenye poti,tulinyang'anya tukala ikawa mwendo wa ubabe,

Ningefanyaje sasa.

Bahati nzuri alipewa dhamana siku hiyo hiyo,wale mahabusu wapya unaangalia nani anaonekana lazy lazy basi mwendo wa kupora kinguvu

Kumbuka tangu niingie sikuwahi kuletewa hata punje ya mchele,

Lakini Kuna siku alikuja OCS ni mwanamke mule akaingia akiwa na maaskari wengine watatu,

Ikawa unaulizwa jina,na unataja kesi yako kwaajili ya kujua kesi ambazo zinatakiwa kwenda mahakamani ilipofika zamu yangu,alishangaa we Daniel upo humu,

Na Mimi nikashangaa kwani kanijuaje?ila nilifurahi kama najulikana

Akaamuru Mimi nikae pembeni akaendelea na zoezi lake mpaka alipomaliza akaniambia nimfuate,

Nikaingia kwenye ile ofisi nikawakuta maafisa wengi tu, akaniambia nikae nje,huku wapo maaskari wawili kuhakikisha sifanyi chochote

Baada ya muda akatoka akiwa na hasira sana akiwaamrisha wanirudishe selo,baada ya dakika kumi nikaitwa Tena huku yule Simon ambaye tulikuja kujuana zaidi baada ya kuwa alikuwa ni muumini mzuri kanisani ila akageuka jambazi, akasema

Wahi mwanangu,ukiona unaitwaitwa Kila muda ujue karibu utatoka.

Nikaenda nikamkuta yule OCS,akiwa kwenye ofisi ndogo ya peke yake akiwa anazungumza na simu,akiniashiria niketi

Alipomaliza mazungumzo,akaniuliza

Daniel kwani ulimkosea Nini huyu mwanamke yaani ni hakupendi,unajua hakupendi

Maana anatamani hata ungefungwa Leo hii,

Nilimtazama kwa kujihurumia sana.
Akaendelea, akajitambulisha nikamkumbuka.

Akaendelea,

Daniel hunijui vizuri,ila wewe nakujua ulikuwa unafanya kazi kampuni fulani (akaitaja) nashangaa huyu mama anasema ulikuwa kwenye kampuni yao ilikuwaje ukaacha kule ukaja huku,nikamweleza Kila kitu,

Ahaaa Sasa Dani,hii kampuni si nzuri yaani watu wote waliikosea hii kampuni huwa wanasumbuliwa sana na Hawa maboss wako,sijui waliipata hii Mali kwa taabu maana yaani siwaelew

Aliongea yule afande ambaye mpaka muda huo sikumjua vizuri licha ya kuwa namkumbuka.

Naomba ufikishe ujumbe kwenye familia yangu wajue nilipo, tafadhali naomba unipatie simu nipate kuwasiliana na ndugu zangu.

Ila Dani umekonda,pole shemeji yangu,akazidi kunichanganya,

Akaendelea

Wewe Ukiwa kwenye kazi yako ya mwanzo ulikuwa unapenda sana kunywa bia kwenye baa ya Shedy rafiki yako ila Kuna siku ulilewa ukamtongoza Amina afande mwenzangu ambaye hayupo hapa,akakukubalia Ila awamu nyingine tulionana pale pale akasema ombi lako kakukubalia ulimshangaa sana na pia ulikataa katakata kuwa hukumtongoza hata hivyo,

Mimi nilifurahi ulivyo na msimamo jambo ambalo wanaume wengi hawaliwezi,ila mwenzangu Afande alikuelewa Hadi ilifikia hapa haipiti siku lazima akuzungumzie,akawa anakera sana ,

Kuna siku tulipanga tuonane pale kwa Shedy lengo nikubembeleze umwelewe Lakini Cha ajabu ulikuja na mkeo,nikashindwa hata Cha kufanya,

Pole afande
,niliongea huku nikijilazimisha kutabasam

Mwenzangu ila nakukubali,na afande Amina nimemwambia uko hapa kashauri upewe dhamana,yaani bado anakupenda sana

Niliitikia kinyonge huku nikichoshwa na zile habari sema ndiyo sikuwa na la kufanya,

Akaagizwa aje mpelelezi wangu ambaye muda wa siku kumi na tatu sikuwa nimemjua na hakuwahi hata kuniita niongee naye.akaja jamaa mmoja ambaye nilimkumbuka vizuri sana,nilimshitakia juu ya upotevu wa mzigo wangu yule ndiye alikuwa wa kwanza kuchukua maelezo pale ubungo.

Habari kiongozi,alisalimia huku akiandika andika vitu fulani, akajitambulisha Kisha akaniambia

Pole ndugu,Mimi ni Askari mpelelezi ambaye kule tulipokutana huwa naenda Mara mojamoja ila kwa kipindi upo ndani nilikuwa sikosi kufika kule maana kule huwa Kuna mchezo wa kubadilishana mizigo iwe bahati mbaya au makusudi.

Ila nilishindwa kuwasiliana na wewe kisa ubize lakini kubwa zaidi huna maboss tumepewa vitisho japo havisumbui lakini ukiona mtu anakuwa vile tayari anakutoa kwenye reli anyway nisimalize maneno mnaweza kusameheana hapa mkaanza kutuita wachonganishi.

Kumbe sisi tunafuata Sheria,

Wakati tukiendelea yule OCS akaingia tukawa watatu,

Yule mpelelezi akaendelea

Mr Daniel pole sana mzigo hukuiba Bali ulijichanganya ila pengine ni namna ya MUNGU kufundisha kitu.

Nikatetemeka kwa shauku ya kutaka kujua nani kaiba,

Akaendelea....

Mzigo umepatikana Leo hii....

Enheeeeeeeee unasemaje afande?

Itaendelea.........
 
SEHEMU INAYOFUATA.....

Nilimaliza mazungumzo na wale maafande huku wakiwa na kigugumizi Cha kuniacha huru, Mara huyu anataka nirudishwe selo ikawa fujo tupu,yule afande mwanamke yaani OCS akaniambia nimpe PPR yangu,akaangalia , akatoka nje huku pale mlangoni akiwaacha maaskari kadhaa wenye sare za FFU.

Akarudi akiwa na vitu vyangu vingi,yaani viatu,mkanda na simu.

Akanitazama akaniambia simu yako ni hii nikamjibu ndiyo,ila mbona imefubaa hivyo afande,niliuliza

akajibu,naye hajui

Wakati hayo yakiendelea kumbe walikuwa na mawasiliano na mabosi wangu, nikiwa kwenye ile ofisi ndogo yenye AC ambapo hata inlet yenyewe haikuwa ikifanya kazi,nikawa nimejiinamia nikashangaa nikakuta kundi dogo la watu wanaingia.

Akiwa boss wangu wa kike na watu wake wakiwa na nyuso zinazolazimisha kununa,

Tulisalimiana huku, bosi akitamka maneno haya,

Siyo Mimi niliyekufunga Daniel imekufunga Sheria,
Ni Sheria imefuata mkondo wake hujafikisha hata mwaka kwenye kampuni yangu unadhani ningekuamini vipi,

Hata Kama angefikisha, miaka ishirini boss kosa alilofanya ulikuwa na haki ya kumfikisha hapa kwakuwa mzigo ulipotelea mikononi mwake,haijalishi bahati mbaya au makusudi Bali uzembe ambao unaweza gharimu maisha yake.

Alidakia kijana mmoja ambaye sikuwahi kumuona huku akionesha kujuana na maaskari na ni much know sana,ni wale mawakili uchwara hapa mjini,hirizi nyingi kuliko Elimu yake.

Boss akafunguka zaidi kuwa ,alipanga nikae ndani hadi pale ambapo angerudi mumewe,nikawaza sana kwahiyo hata angekaa mwaka huko Mimi ningeozea humu bila kupelekwa mahakamani,yaani Central kubwa kama hii ambapo Ina wetu wengi wanasheria na wapembuzi wa mambo wangeshindwa kusema niende mahakamani,

Ananitisha tu huyu, mbona hata hivyo yule OCS alisema mahabusu wa zaidi ya wiki mbili wote jumatano (keshokutwa)

Wangepelekwa mahakamani.

Boss aliendelea kuongea huku,akiniambia kuwa amemaliza Kila kitu hata hivyo nipo huru.akanipa kiasi Cha laki tano,akidai hiyo ni nauli lakini pia baada ya wiki moja niende ofisini kwake.

Nilitamani kujua,spare imepatikanaje lakini haikuwa mahali pake kuuliza kuuliza haya maswali.baada ya yule boss wangu kuondoka nikaletewa vifaa vyangu vyote,bila hela .

Ikabidi niulize kuhusu hela zangu laki mbili na themanini ambazo niliziandikisha kule kituo kidogo ubungo kukawa hakuna hela.

Nikagundua kitu, kuwa hata hivyo nikiwa ndani ya selo baada ya kuona Chakula Cha mule hakifai niliomba ninunuliwe Chakula kwakuwa hela yangu ipo afande aliondoka kwa madai anaenda kuchukua lakini baada ya kurudi alisema mbona Sina hela,kule kwao

Watu wote Hawa mbona hela zao zipo japo si ruhusa kula humu lakini kama hela yako ipo ungeletewa hata mkate,bwana wewe hakuna hela kule Tena hatutaki hayo maswali yako.

Ndiyo,nakumbuka niliishiwa kutishiwa.

Nikamwambia yule OCS kuwa, hela zangu nazipataje,

Unajua Dani labda umechanganyikiwa,kwasababu kwa mtu uliyemaliza wiki mbili Ukiwa ndani huwazii mambo yako,huwazi kuhusu familia yako,unaiwaza laki mbili na themanini,ungeacha gari je.

Ni haki yangu lakini afande,

Sawa ngoja nimuite mpelelezi wako,
Akaitwa yule afande, akasema hela niliziandikisha anazo yeye ila kwa siku hiyo ana elfu sitini tu nyingine tupeane namba atanimalizia,

Nilicheka kwa sauti kwa Mara ya kwanza tangu nitoke mule kwenye selo,maana dah si kwa njaa zile Kuna watu Wana njaa,nikauliza simu yangu alikuwa anatumia nani mbona hata peni ya kutouch simu imevunjika wakanitolea tu ukali kuwa sipaswi kuuliza maswali hayo

Huyo nikashika njia ya uraiani huku nikifaidi vizuri upepo wa huku nje,jamani acha kizuizi kiitwe kizuizi upepo huu kumbe una Raha yake,watu watasema Dar Kuna joto Mimi nasema hakuna.

Nikashika njia fulani ya posta ili nikachukue daladala za moja kwa moja Hadi nyumbani,nilikuwa na hamu ya kuwajulisha ndugu, jamaa na marafiki kuwatoa hofu ila simu yangu haikuwa na chaji.

Hatimaye nikafika nyumbani,nikiwa nimechoka sana labda ni baada ya kubadili mazingira,

Nikakuta familia imeongezeka nilishangaa kuwakuta mama yangu mzazi na dada yangu, masikini

Walitoka mkoani,kuja kujua hatimaye ya mtoto wao lakini ni kama swala anaye jaribu kumnasua mwanae kutoka kwenye mikono ya Simba.

Watu walilia,wakalia mke wangu alikonda,hali kadhalika mama pia mpaka yule dada wa kazi machozi yakinilenga alivyoniona ,alikuwa sahihi ni ndugu yetu,Mimi ni kama kaka yake tumezoeana alikuwa na haki,mama yangu alisisitiza,kuwa mji haufai uza nyumba rudi kijijini

Yaani nikawa na kazi ya kuwatuliza Mimi hata kuoga sijaoga nikawa nawatuliza watu ambao wote walikuwa hawajiwezi,walikuwa na uchungu kuliko ile kawaida.

Vilio vilitawala mule ndani kiasi Cha majirani kusogea,huku nikijua kulia huwa kunaambukiza majirani baadhi ya wanawake wakaungana wakaanza kulia kwa sauti,huyu akitaja, Daniel,Mara huyu mume wangu,huyu akitaja shemu basi fujo tupu

kubwa zaidi mama yangu aliniita jina la utoto kabisa akiniita FURAHA jina ambalo hata mke wangu halijui,ila ndugu zangu.

Mwanangu,nilikupa jina la FURAHA ikiwa ni sehemu ya kushindwa kuficha hisia zangu nzuri baada ya kuzaliwa mtoto wa kiume pekee kwenye familia,ila nimehuzunika mwanangu.

Hapa hapakufai, baba.

Nilimtuliza mama kuwa Mimi ni mwanaume,ambaye sipaswi kushindwa Wala kufeli,kama ningekaa tu nyumbani pengine yasingenikuta haya

Kwahiyo mitihani mingi ni mapambano ya utafutaji hivyo nilimtuliza mama yangu,

Huku mke wangu akiwa hawezi kuzungumza kuliko wote kwa wakati huo,

Niliingia bafuni nikiwa nimezimisi hata kuta eti, kabla sijaanza hata kuoga nilijiuliza maswali yafuatayo

Mke wangu,anapafahamu fika sehemu napofanyia kazi, alishindwaje kufika,kumuulizia mume wake?

Haya tufanye walimwelekeza nilipo, alishindwaje kutafuta wadhamini,nikakaa kipindi chote hicho?

Tufanye dhamana ilikataliwa,alishindwa hata kuniona?

Nina marafiki na waandamizi kibao,mtaani Tena wenye majina makubwa neno dhamana lilikuwa ni jambo dogo, niliwaorodhesha kichwani nikagundua hii Dunia Kila mtu alikuja peke yake,nikajifunza kuwa peke yangu kwanza.

Kuhusu wazazi wangu walifikaje,mjini tukatane sehemu inayofuata,kisa bado kibichi hiki

Itaendelea......
 
Kama hautakuja kuwa na mahusiano ya kimapenz na boss wako mwanamke basi badilisha heading
 
SEHEMU INAYOFUATA.....

Baada ya vilio vya hapa na pale,

Baadhi ya watu waliondoka huku familia yangu ikiwa haiamini kuwa nimerudi huku mke wangu akizichoma moto eti ni nguo zenye mkosi, nilimuhurumia sana, lakini acha aamini anacho kiamini.

Baada ya muda niliungana na familia yangu pale sebuleni, nikiwa HURU Kuna tofauti kubwa Kati yaana Uhuru, yaani unajipangia mambo yako bila kubughudhiwa,

Tulipata Chakula Cha usiku,tukagawana vyumba tayari muda wa kulala ,

Mume wangu,nikaitika,

Pole Sana,tena pole sana mume wangu,aliongea kwa hisia mke wangu.

Hapana kama pole mshanipa muda mrefu yaishe hayo tugange yajayo nilimjibu huku nikiwa nasearch Vitu kwenye PC yangu,

Mume wangu, nakupa pole kwakuwa huna marafiki, Tena huna hata chembe Bali umezungukwa na kundi la mbwa mwitu wenye vazi la kondoo,

Baada ya wewe kutokufika nyumbani, kwa muda wa kutwa nzima tangu uliponipigia Jana yake kwamba hutafika mapema na utalala Mimi niliamua kukufuatilia kazini kwako, lakini baada ya kufika mapokezi niliambiwa mumeo kasafiri kaenda nje ya nchi,.

Jambo ambalo niliona si kweli navyokujua mume wangu lazima ningekuwa na taarifa,

Baada ya kuambiwa hivyo Kila jambo nililouliza nilijibiwa kwa kifupi, wale watu wa mapokezi walikuwa bize sana hawakuonesha ushirikiano wowote ule japo hapohapo nilikuwa naona watu wengi wakiingia wakipokelewa vizuri na kujibiwa vizuri, lakini kwangu ikawa tofauti.

Baada ya masaa matatu niliambiwa, Kuna Boss ananiita, kweli nilipandisha ngazi kuelekea kule juu aliko nilikutana na mwanamke mwenzangu ambaye ni kama mama yangu, nilimsalimia lakini hakujibu salamu yangu, alichukua faili moja likiwa na makaratasi yaliyobanwa kwa pamoja mengi sana,

We ni mke wa Daniel, nikajibu ni Mimi,

Aaaaah wapi, we ni hawara yake tu yule hawezi kuwa ma mke tokea lini tapeli akaoa, mnajipeleka tu kwa wanaume kisa njaa, nikwambie tu mwanangu kuwa yule si mtu wa kuishi naye mtu ambaye muda wowote atakuacha mkiwa,

Yule mumeo ni tapeli ni mwizi na nikwambie tu kuwa kwenye hii kampuni safari hii kanasa kama alizoea kuiba ni huko huko hapa kwetu Cha kwanza ni uaminifu.

Lakini huyo boss wako licha ya kumbembeleza wanielekeze upo kituo gani ,alinitukana matusi ya nguoni kwamba kwanza ni marufuku
kukanyaga pale,nilitoka nikiwa nimenyongea lakini nikiwa mawazo tofauti kwamba hapa lazima mume wangu nijue alipo.

Najua yupo mahabusu lakini hawaniambii yupo wapi,nikatoka nikaenda kituo kidogo Cha polisi cha (akakitaja) kilicho karibu na ile kampuni,nikatoa maelezo kuwa ni nani mume wangu ambaye alikuwa/anafanya kazi kampuni fulani hata hivyo Kuna tatizo limempata akiwa mikononi mwa kampuni hiyo kwahiyo nahisi wamemuweka lock up.

Sasa tukusaidie Nini mama maana mumeo ni mwizi ndiyo maana kashikiliwa kampuni ya fulani (akitajwa bosi wa kiume)

Ni kampuni inayozingatia haki za binadamu halafu ni watu wapo vizuri kwenye mambo yao , kwahiyo ukilalamika ooh sijui mume wanguuu,kampuni hiyo haijamuonea

Alimalizia mke wangu Huku akionekana kujua mambo mengi kuliko mimi,

Mume wangu nilichanganyikiwa nilianza kukulaumu ni tamaa gani zimekuponza baba watoto?

Lakini niliwaambia wale maaskari kuwa sikuja kwa dhumuni la kupinga kwamba mume wangu siyo mhalifu bali nahitaji kujua kawekwa kituo kipi .

Ahaaa unataka kujua sawa, tunajua lengo lako ni kumpelekea ugali huko mahabusu maana kuhusu suala la kumtoa we sahau mama, hivi huyu Mwenye kampuni unamjua kweli, na saizi yupo nje ya nchi subiri arudi ana wanasheria Kila angle sijui huyo mumeo Cha uroho kama atatoboa,

walisema wale maaskari kwa dharau,

Lakini Cha kukusaidia ni kwamba tunampigia huyo boss wenu ili akwambie yupo kituo gani,

Wakapiga simu kuulizia akawambia yupo Central maarufu hapa mjini iitwayo(jina kapuni).

Nilichanganyikiwa mume wangu,kama ni central ile nilijua utateseka sana,nilipiga simu kwa shemeji Shedy kumweleza haya matatizo, akanijibu sawa atashughulikia,hata hivyo niliona muda unaenda nikaenda Hadi nyumbani kwake nikamkuta yupo na mkewe,nikawaeleza kwa kifupi matatizo yako, lakini hawakuonesha kushtuka badala yake alidai kuwa hiyo ni mitihani ya kawaida.nisijali

Niliwapigia ndugu zako mkoa kuwaeleza haya mambo,wakaahidi kuwa watakuja, nikaamua kufunga safari kuja ulipo, lakini baada ya kujitambulisha walidai kuwa sipaswi kukuona na hakuna ndugu yako yeyote ambaye atakutoa hapo wewe ni wa kwenda jela tu

Lakini baada ya kuwasumbua sana, walidai kuwa aliyekuweka ndani anadai umepoteza mzigo wa million kumi na tano,kwahiyo tukilipa mume wangu unatoka,na kama hicho kiasi Sina wao hawawezi kukuachia kwa dhamana yeyote ile,

Ila Cha kushangaza mume wangu ni kwamba wakati natoka pale kituoni mida ya saa tatu usiku baada ya mizunguko ya kutwa nzima,nilirudi nyumbani na kumkuta shemeji Shedy akiwa na dada wa kazi,

Nilimsalimia,huku nikiwa na mashaka Sasa hapa anafuata Nini na wewe upo matatizoni,hata ukiwepo sijawahi ona akija hapa mida mida mibaya kwanini aje,

Nilipitiliza Hadi chumbani huku dada wa kazi akiniita kuwa mgeni anataka tuongee, nikatoka nikamsikilza,

Akasema kuwa tatizo lako ni kubwa hivyo Mimi Kama mwanamke sitaweza mimwachie yeye atamaliza akaniahidi kuwa kesho yake ningekuona,

Wakati Mimi najua wazi namna msala ulivyokuwa mzito nikikataliwa hata kukuona ,nilitambua dhamira na nia yake ovu nikamtimua,hasa baada ya kuanza kusema niinuke tukaongelee ndani ya gari lake yaani mtu nipo kwangu lakini.....!?;:'*"'

Aliongea mengi mke wangu Huku akishikwa kigugumizi Cha hasira.

(Nikajiuliza moyoni)

Shedy huyu huyu alitaka kunisaidia mpaka alale na mke wangu.

Mke wangu akaendelea...

Kwahiyo baada ya kumtimua alinitisha kuwa Sasa tutaona kama atatoka huyu unayeringia,

Asubuhi na mapema niliamka nikapokea simu kutoka mkoani kuwa Kuna watu wanakuja kwaajili ya dhamana yaani mama mkwe na wifi yangu, lakini bado nilihisi huo si msaada kwakuwa sisi wote ni wanawake.

Pole mke wangu,ni kweli kabisa bado ilikuwa vigumu kufanikisha,nilidakia

Kumbuka kutwa nzima nilikuwa na Chakula ambacho nilikiweka kwenye poti jipya kabisa lakini kilichacha baada ya maaskari kukataa kupokea wakinambia mahabusu mnakula huko huko,kwanza hujafungwa kwahiyo ni lazima uteseke kwanza,mida ya saa kumi nilienda ubungo kuwapokea wageni wangu,

Nilipofika nilisubiri kidogo mule ndani huku nikiambiwa bado kama lisaa tu Lile bus la kampuni ya happy nation liingie, lakini wakati nikisubiri kulitokea mabishano Kati ya mzee mmoja na wale wabeba mizigo ya stendi kuwa aliagiza mzigo wake akiwa mkoani akidai utangulie watapokea vijana wake Cha ambapo ilikuwa ni gearbox ya gari ndogo na plate clutch yaani vije virekebishwe hapa mjini.

Cha ajabu baada ya kufika akapokea mavyuma asiyoyajua

aliwaka yule mzee huku polisi wakiingilia Kati kuwa kumekuwa na malalamiko makubwa sana ya abiria
Kubadilishiwa mizigo bahati nzuri wengi huwa wanagundua hapo hapo.

Bahati nzuri yule mzee alirudisha vile vitu ambavyo vilikuwa kwenye pikipiki ya matairi matatu, lakini sikujua kilichoendelea baada ya lile gari la mkoani likiwa linaingia niliwapokea wageni wangu tukarudi nyumbani, sikuweza kugundua haraka Wala kuunganisha matukio kwakuwa uliniambia unakwenda kuchukua mzigo, Ila sikujua mzigo Gani.

Kiufupi kesho yake nilikuja na ndugu zako pale kituoni tukaambiwa kuwa haupo pale umepelekwa gerezani kwahiyo Wala tusijisumbue, licha ya kuhoji kaendaje jela bila kwenda mahakamani, tulitishwa kuwa tusubiri baada ya wiki mbili tuache namba tutapigiwa.

Tukaona hakuna namna tukarudi nyumbani huku tukikusanya wachungaji wote kufanya maombi ili wepesi upatikane,

Hapa nilicheka kidogo, jinsi wachungaji wanavyopiga hela kupitia matatizo ya watu maskini.

Mke wangu akaendelea..

Hata hivyo majuzi Kuna tulikuwa tukijaribu kujadiliana hapa kwamba huo mzigo ni upi haswa, ikaonekana wenzangu waliuona kuwa yalikuwa kama machuma fulani,

Nikakumbuka kitu mume wangu,....

Itaendelea............!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom