Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Story tamu sema wanetu punguzeni komenti ndefu kama essay tunajua mwamba kashusha episode kumbe michosho
Ahahahah...mkuu tunashusha koment ku buy buy time mtaalam anapojipanga kushusha uzi😂
 
SEHEMU INAYOFUATA.................... Nilirudi nyumbani usiku wa manane, nikalala kupunguza usingizi, niliamshwa na mke wangu Huku nikigundua ni saa mbili na robo na robo.

Pole mume wangu , naona mkukumkuku wa jana ulikuchosha sana, kaoge ili uje tunywe chai.

Niliingia bafuni nikajiswafi Kisha nikatoka sikutaka hata kusubiri chai badala yake, nilimweleza wife kwa kifupi huku nikiwahi kwa mke wa Shedy.

Sikumkuta mtu yeyote zaidi ya watoto, nikajua Hawa wapo kituoni, nilifika kituoni nikawakuta watu wengi majirani na mke wa Shedy, wakiwa wamenyongea sana.
Niliwasalimia huku nikigundua wanahisi labda nilifanya makusudi kuchelewa, kumbe nilipitiwa tu.

Nawahitaji wahusika wa Shedrack , wanifuate, aliamuru afande Fulani mwenye cheo Cha juu.

Tuliingia kwenye chumba fulani, huku tukiwa watu watano askari wa sita akiwa kazungukwa na maaskari wadogo wenye silaha.

Naitwa afande (jina kapuni)naomba tufahamiane, watu walitaja majina huku wakitaja uhusiano wao wapo vipi na mtuhumiwa, zamu yangu na ya mwisho ilifika, nikataja jina huku afande akiniangalia sana,

Huyu mtu umefahamiana muda gani, aliniuliza,

Kwakweli afande labda waulize wengine swali hilo,huyu Mimi nimecheza naye utotoni, nilijibu huku akionesha kuridhika,

Jamani nimewaita hapa kwasababu, tulikuwa tunasubiri upelelezi ukamilike ilu tujue mtuhumiwa anafunguliwa kesi ya aina gani,

Huyu baada ya kuhojiwa kakiri kuwa ni kweli walikuwa wanajaribu kuvunja duka moja ambapo walikuwa wanne ndipo risasi ilipomkuta mwenzao akafariki pale pale huku wao wakikimbia, hivyo kwa kushirikiana na raia wema waliotutajia hao wahalifu, walipo tukafanikisha kuwanasa mtu pekee aliye tusumbua ni huyu shedy kwani huyu kakamatiwa mkoani kabisa.

Lakini pia, watuhumiwa wote wanakabiliwa na kesi ya jinai na si ya mauaji kama taarifa ya awali ilivyodai,. aliweka kituo

Binafsi nilifurahi kama ni kesi ya jinai maana iliwezekana kumdhamini japo Mimi nilijitoa,

Afande aliendelea.....

Hivyo taratibu za dhamana mtapewa maana Kuna vitu vya kiintelijensia tunakamilisha. mnaweza kwenda, tuliruhusiwa huku wote tukitoka nje na kuwaeleza wenzetu kwa kifupi Kisha tukapanda daladala kuja nyumbani kwa Shedy.

Tulikaa kikao na majirani huku michango ikiendelea na pole nyingi za kinafiki,

Wewe bwana Daniel tunakuomba uwe kiongozi kwenye hili suala la mwenzetu, aliyepatwa na matatizo. aliongea jamaa mmoja.

Hapana haitawezekana kwasababu Mimi mwenyewe nina matatizo hivyo nimekuja tu kwakuwa hili la mwenzangu ni zito. lakini pia sitakuwepo kwenye orodha ya wadhamini badala yake nitatoa kiasi Cha pesa kwa kadri ya uwezo wangu pale pesa itakapohitajika,

simu ya Rose iliita, alipiga ikabidi nitoke chemba, nikaipokea.
Tukasalimiana.

My mbona kimya hivyo, unajua fika siwezi kukutafuta kwasababu ya mipaka tuliyojiwekea, vipi Kuna shida gani.aliongea kwa kulalamika Rose.

Hapana mpenzi wangu, kwanza nisamehe sana, pili Kuna matatizo, Kuna ndugu yangu ana kesi na mpaka muda huu yupo mahabusu na Mimi nipo kwake na wanafamilia wengine tukijadili namna ya kumtoa. nilimfahamisha Rose.

Sawa, ila my Dad kasema kapata dharula kidogo hivyo katoa maelekezo kule kuwa utaenda, hivyo unachotakiwa kufanya ni kujiandaa ili wakakupe maelekezo. aliweka kituo

Sawa, naomba niache kidogo nitakupigia tuongee vizuri maana nahitajika kwenye kikao,

Sawa Wala usijali, alijibu Rose mchepuko wangu, napenda kumwita 3D kwasababu alinionesha UPENDO wa kweli japo Kuna muda alinigeuka, fuatilia stori Hadi mwisho.

Nilirudi kwenye kikao huku watu wote wakinitaka niwe mstari wa mbele kwenye process ya dhamana, ikabidi niwakatae kwa kuwapa maneno haya.......

Huyu mtuhumiwa naweza kusema namfahamu vizuri kuliko wengi wetu hapa bahati nzuri shemeji yangu unalitambua hili. hivyo Mimi ushauri wangu na mtazamo wangu niwe muwazi na mkweli, hili suala lazima litafika mahakamani, hivyo kutakuwa na usumbufu mwingi na dharula za hapa na pale, lakini mtambue hapohapo na Mimi lazima nitakuwa nahitajika kusukuma gurudumu la maisha kwenye vibarua vyetu nikitafuta mkate wa kila siku,

Hivyo basi nashauri wapatikane watu wengine,ili tugawane majukumu huku Mimi nikibeba jukumu la kuisaidia familia ya ndugu yangu itakapokwama kwa lolote , huku nikiwa bega kwa bega na nyinyi. nilijitetea.

Huyu kijana Mimi nimemwelewa vizuri sana, yaani anamaanisha wapatikane watu wengine wawe wadhamini huku yeye mchango wake ni kuilisha familia , jamani hamuoni bado mtu kafanya uungwana.? aliongea mzee mmoja huku wengi wakionesha kumuunga mkono. Wakajitokeza watu watakaokuwa tayari kwa dhamana Mara ripoti kutoka polisi itakapotoka. niliacha kiasi cha pesa, tukaagana nikaondoka mchana ule.

Ndugu wasomaji,
Kama Shedy angekamatwa kwa kosa lingine ningekuwa first line kwenye kumdhamini lakini alikuwa anakabiliwa na kesi ya ujambazi, wizi, unyang'anyi, nisingejitumbukiza kwenye hayo makusudi hasa ukizingatia sikuwa na kazi wakati huo,

Haya ni makusudi, maisha haya ukamwibie mtu kweli?
Hata siamini kwa yule jamaa yangu sikuwahi kumfikiria kuwa ana haya mawazo,

Nilikuwa nampongeza kwa hustlers zake huku nikimuiga baadhi ya vitu .
Kweli moyo wa mtu kichaka
Kinachomsumbua jamaa yangu kwenye maisha ni TAMAA. ana TAMAA mbaya, asione kitu Cha mtu, akihitaji kutimiza malengo yake atalazimisha hata pasipo wezekana.

Hebu tufanye ametoka na yupo uraiani kwa skendo yake ilivyosambaa, si atakufa hata kwa kuviziwa Huyu, ataishije hapa mjini , Nilijiwazia moyoni huku nikikaribia kufika nyumbani .

Eenhee za utokako , maana hata Chakula hukutaka kula ukawa juujuu tu, kama aliyeko ndani ni mwanao wa kumzaa, alihamaki mke wangu.

Mama Jack, ujue jamaa ana kesi nzito na ile Sijui kama atachomoka yaani nyundo zinamuhusu kabisa, nilimwambia

Kwani kakutwa na hatia gani yule, aliuliza mke wangu.

Kesi ya unyang'anyi, tena uchunguzi bado unaendelea, na dhamana wamekataa wanadai Kuna vitu wanaweka sawa, kuna nini hapo, lengo wanataka aende mahakamani, Sasa maisha yenyewe haya na watoto alionaoooooh, ujue inafikirisha mke wangu? na hapo tumetoka kwenye kikao cha kifamilia namba ya kumnusuru jamaa.

Kama kawaida yako , upo mstari wa mbele kusaidia watu , sisemi usisaidie mtu, ila shedy ni mshenzi sana, kipindi upo ndani, nahangaika na tumbo langu, hakujali yeye na mkewe , cha ajabu alikuja kwangu nilidhani anataka kunisaidia kumbe msaada wenyewe hadi alale na mimi yaani mume wangu Sijui una moyo wa aina gani , kwanini usiwaache wapambane wenyewe, hapo tu huna kazi umefukuzwa, lakini bado tu unajiona waweza kuwa msaada wa mtu . aliweka kituo

Wewe nani kakwambia nimefukuzwa kazi. niliuliza nikiwa serious.

Weweeee mjini hapa mtu atakunyima Chakula siyo maneno, ni jana tu nilivyotoka kwenye msaada wa wazungu, ESTA kaniambia Kila kitu. ooh naenda kuonana na boss wangu Mara nini, yaani wewe boss wako kakuponza na ukute hujasingiziwa, na nikawa nashangaa maana Kila nikiuliza sababu ya kusimama kazi ni nini unaniambia vitu havina hata mashiko.haya tuishi baba, tena huna kazi ni fursa nzuri kuhudhuria kesi ya shedy, ambaye alikuwa ananing'iniza miguu kwenye baa yake pindi upo mahabusu huku akinipigia hesabu alale na Mimi.

Leo hii zamu yake kuwa mahabusu, wewe tena hata kula hutaki unawaza rafiki yako yupo ndani, mwache mwache aozee ndani si mwizi?

Ohhh namalizia fence mke wangu, tutanunua gari, nani wa kununua gari , mume wangu huyuhuyu? Hela zenyewe unapata kama homa za vipindi, sisi ni masikini na tutakufa masikini. aliongea mke wangu Huku akishusha freestyle kiasi chakunikasirisha.

Mke wangu Mimi naamini wema haulipwi kwa ubaya, Mimi wala sipo mstari wa mbele kwenye kesi yake badala yake nimebaki kama mshauri tu Wala usinihisi vibaya, nilijishusha maana tayari pengine tungezua mengine mke wangu alikuwa kapaniki Sana.

Weweeee umefukuzwa kazi umenificha, hili utaniambia ukweli?
Ila nikukumbushe tu kuwa kwenda kwenda huko unaweza Kuta mnaswekwa ndani mkitafsirika kama wezi wenzake,. aliongea mke wangu Huku nikigundua heshima yangu ishaanza kushuka, mke wangu hajawahi Wala kuthubutu kunitamkia maneno kwa kujiamini vile. Acha pesa iitwe pesa ukiikosa, mtu anaweza kudai talaka Bila sababu .

Nilikula Chakula Kisha nikampigia Rose, tuongee kuhusu masuala ya kazi, alinielewesha vizuri sana huku akinitahadharisha kuwa nisiwaangushe yeye na baba yake.

Siku za kukumbuka kuzaliwa kwa kristo zilikaribia huku kipande hiki nikiwa Sina wasiwasi kwani akiba nilikuwa nayo, lakini pia matumaini ya kazi iliyoko mbele yangu, yalitosha kushusha Presha japo sikuwa na uhakika wa asilimia mia moja.

Nilikata simu ya Rose nikampigia ESTA lengo nimchane kwanini kuniingilia kwenye familia yangu.?
Akapokea simu.

My huyooo jamani umenikumbuka?
Mbona unakuwa kimya hivyo, huwa unaahidi utanipigia lakini kimya kinakuwa kingi mno baba, aliongea kwa kubana pua akilazimisha sauti ya kitoto.

Sasa wewe , inakuwaje kumwambia mke wangu maneno ya kufukuzwa kazi kwangu, kwanini ufanye hivyo kulikuwa na ulazima gani? niliuliza kwa ukali,.

Eee eeeeeeh baba hasira zako peleka hukoo, kwani kazi si umefukuzwa kweli kwani uongo? alijibu kijeuri huku nikijiona kama Nina mkosi mbona hakuna anayeniheshimu hata ESTA ananipandishia,?

Wewee jiheshimu tena, jua unaongea na nani au hujui kuwa we ndiyo chanzo Cha kufukuzwa kazi au huyo shoga yako hakukwambia chanzo Cha Mimi kutolewa pale.

Wewe Daniel vipi, umesahau kama kazi uliyofanya ulilipwa, Sasa jua kuwa ulichagua kazi ya usuluhishi kuliko kazi yako muhimu, hivyo usitafute mchawi, Wala kutafuta pa kufia sawa baba ........

Niliamua kukata simu huku, nikigundua mwanamke akipaniki siyo wa kubishana naye lakini pia ESTA kwa Sasa wanaiva sana na madam kifupi yupo upande wenye nguvu.
PESA, PESA, PESA.

Alamski.

Itaendelea..........................
 
pesaa shikamoo tumalize kwa moyo mmoja
 
JF tuna watu wanaojua kuandika visa na mikasa ila Jack Daniel umewapita wote tena kwa mbali sana.

Kiswahili fasaha, mipangilio ya kisa imekamilika. Yaani kama unaachia episode fulani somewhere ukaenda na ingine, unarudi kuichukua Ile episode uliyoiacha mahali na kuunganisha kwenye utaratibu mzima.

Pamoja na yote, nakupongeza sana kuchukua muda wako na kuandika kisa hiki ingawa una majukumu mengine ila unatutendea HAKI kwa kweli.


Tuna bahati sana kuwa nawe humu.


My wish ni kuwa ufanye mpango itengenezwe movie kuhusu kisa hiki cha ukweli kwa kuwa kuna mafunzo mengi sana yanayoweza kuisaidia jamii yetu ya kitanzania kwa sasa na wakati ujao endapo itawekwa kwenye movie


Maoni yangu tu.


Narudia kukushukuru sana kwa muda na moyo wako usio na UBINAFSI.
 
Ahsante sana kwa maoni na mtazamo wako, wazo la kutoa movie hata baadhi ya member wengine wameshauri hivyo.

Ila si jambo jepesi, gharama zake ni kubwa hasa kama unataka tamthilia ifike kwa walaji ikiwa na viwango vya 2022, kama stori ilivyo Kunatakiwa Shots na scenes zote ziwe kali, kwa mfano boss awe boss kweli kweli, magari makali, vituo vya polisi kama ni police post iwe hivyo kama ni central, iwe hivyo, lakini pia wahusika nao ni wengi sana,

Yaani movement zote, from 2011 to 2013 ,huku locations zisiwe za kujibana , kumbuka Kuna riwaya na visa vipo humu jamiiforums ni Kali na zenye kuvutia, lakini baada ya wahusika kutoa movie au tamthilia hazikuwa na mvuto kama ilivyo simulizi.

Nikiri wazi hapa Tanzania,kunako bongo movie Kuna vipaji haswa, vya watunzi na waandishi lakini kazi zao Mara nyingi zinakosa .bajeti, bajeti, bajeti,.

Waigizaji mahiri,
Locations nzuri,

Mfano Mimi na madam tulikuwa tunakutana kwenye migahawa tofauti tofauti hivyo inatakiwa hata kwenye tamthilia iwe hivyo hivyo jambo ambalo kivitendo ni ngumu.

Hii inataka mzigo wa kutosha kuiandaa.

Yote kwa yote niwape pongezi wanaoguswa Kila mtu kwa namna yake , tuenjoy simulizi maana ipo hatua za mwisho

Uzuri simulizi inajisimulia yenyewe kwenye vitu vilivyonitokea, nipo tayari kujibu maswali yenu.
 
Kwanin hukurudi kwa mganga wako kuhusu wee kusimamishwa Kaz
 
Hii ya mwisho hata sio nzuri yan...Haina msisimko hata kwa mbali.

Alaf nimegundua hii ni stori ya kutunga sio true stori ndio maana mtunzi anatumia muda sana kubuni na kuunga matukio yahusiane
Watu wa upinde bhn unataka mwandishi akusisimue ili iweje
 
Safi kabisa formula hiyo anaipiga sasa migulu chemba kwa taifa.
 
Duuuuu,Mambo yanaingiliana haswa,huku shed huku
Boss Asante kwa simulizi,haya majina unayotumia ndo ya wahusika au umeyabadilisha,najaribu kufikiria Rosie akipitia huu uzi ,hahhaahha
 
Movie bajet yake si haba mazee sio chini ya 100m
 
Duuuuu,Mambo yanaingiliana haswa,huku shed huku

Boss Asante kwa simulizi,haya majina unayotumia ndo ya wahusika au umeyabadilisha,najaribu kufikiria Rosie akipitia huu uzi ,hahhaahha
Soma kuanzia kwenye utangulizi yaani mwanzo kabisa majibu yapo huko
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…