SEHEMU INAYOFUATA.. .. ... ..
Baada ya kuongea na yule mzee, ambaye alionesha upendo wa dhati kabisa kwangu, walianza kukonyeza Kati ya yeye na mkewe, nikagundua ni masuala ya Chakula, ikabidi niwazuie. Kisha nikaaga ili niondoke.
Kwanza kijana wangu nakupongeza kwa kuwa imara na msimamo wa kweli hivyo nakukaribisha sana, karibu tena kwa Mara nyingine alisisitiza yule mzee huku na yule mama wakionesha furaha zao.
Nilishika njia ya nyumbani huku nikisikia njaa, yaani ile njaa ambayo ilikuwa hainisumbui sababu ya mawazo Sasa ikawa , inauma barabara. Tena haswaa,
Baada ya kufika nyumbani niliamrisha Chakula kiwahi kidogo maana nilikuwa na njaa sana.
Nilitulia sebuleni huku nikiwa napoteza muda kwenye TV hususani matangazo ya mwisho wa mwaka yaani punguzo la bei za bidhaa mbalimbali, Kila channel ukiweka matangazo ya bidhaa kwa msimu wa Christmas na mwaka mpya yalikithiri. Huku nikiwa nayachukia Yale matangazo,. Labda kwakuwa sikuwa na hela. Maana bidhaa zipo chini lakini bado huwezi kuharibu bajeti zako, nilichukia sana.
Mume wangu, Kuna tamthilia yangu imeshaanza hivyo naomba hiyo remote, Mke wangu alisema huku nikiwa Sina namna maana Hawa ndiyo wenye TV. nikainuka na kwenda chumbani huku, hali ya kusimamishwa kazi Kila wakati nikigundua sipo kwenye hali nzuri, huu ni mkosi, nikijikumbusha washkaji zangu kibao ambao, huwa wanazingua sana kwenye mishe zao lakini bado huwezi Kuta wakiwa na stori mbaya kama hii yangu, hii kwangu ni nuksi. nilijisemea
Unajua kuremba nako si kuzuri, yaani Kuna muda nilikuwa karibu na yule Boss wangu, Bora hata ningetembea naye ili haya yanayoongelewa nione labda nimekosea.
Tena alivyomaarufu ingekuwa poa maana huenda angenisaidia kwenye hii kadhia maana si ingekuwa kweli?
lakini ni ujinga tu, mbona Kuna watoto wabichi sana mtaani kumshinda yeye.
Niliendelea kuwaza yale mambo
ya kijinga huku nikiwa nachati na Rose kule chumbani.
Mume wangu Kuna wageni tunakuomba uje. ilikuwa sauti ya mke wangu ikiita.
Nilitoka huku nikikutana na wanawake wawili na mwanaume mmoja, huku mwanamke mmoja akiwa ni mke wa rafiki yangu Shedy, na wengine ni wageni huku mwanamke mwingine alijitambulisha kama rafiki yake na yule mke wa Shedy. na yule mwanaume alijitambulisha kivyake huku akisema yeye ni dereva wa Bajaj.
Karibuni sana jamani, lakini mbona muda huu vipi Kuna nini, halafu mbona shemeji yangu
Kama una majonzi vipi, niliuliza Huku nijiset vizuri kwenye kiti.
Shemu kwanza samahani sana kwa usumbufu, Hawa unaowana wamenisindikiza Mimi kuja hapa, suala ni kwamba mume wangu leo ni siku ya nne haonekani nyumbani, mwanzo niliingiwa na wivu kuwa huenda kafungiwa na mwanamke. Lakini baada ya kutimia siku ya nne
Ndipo, niliposhtuka kuwa huenda kapatwa na matatizo, hivyo nisharipoti kituo Cha polisi, na nimezunguka kwenye vituo vingi tu, bado maaskari wananieleza kuwa wapo kwenye mchakato kuhakikisha anapatikana.
Hivyo kwa Imani yangu, japokuwa mimi na nyie hatuna uhusiano mzuri ninakuomba au niwaombe wote wewe na mdogo wangu (akimaanisha mke wangu) naomba mnisaidie ndugu zangu, shemu wewe ni wa nyumbani kabisa, naomba waache hao naomba nisaidie mwenzio(huku akiongea kwa kilugha)hali iliyopelekea mke wangu atake kumaindi
Sawa nimekuelewa, na wote tunashukuru kwa taarifa hiyo maana jambo hilo ni zito sana,. Kwani gari lake liko wapi. niliuliza.
Gari lipo tu nyumbani maana lilishaharibika kitambo, hivyo shughuli zake za udalali alikuwa akitumia gari la rafiki yake. alijibu
Sawa, wewe Dada Mimi sikuchukii, kupotea, au kutoonekana kwa mumeo najua ni jambo linaumiza, ila naomba uwe unaongea kiswahili ili wote tujue, kuongea kilugha na mume wangu , jua kuwa huyu hawezi toa msaada wowote kama sijamruhusu.
aliongea kwa hasira mke wangu,.
Jamani eeh, Mimi shemu nimekuelewa sana, ila simu si tunazo? Kila kitakachojiri tutafahishana. Nilijibu kifupi kwani mke wangu na familia ya Shedy ni kama mbwa na paka. lengo nilitaka waondoke.
Kaka, kakaeee naomba tuongee kidogo hapa nje, samahani lakini mzee mwenzangu. aliongea yule jamaa aliyejitambulisha kama dereva Bajaj.
Kwanza nimekuita chemba lengo nikwambie ukweli,
Huyo rafiki yako sijui ndugu yakoooo,
Nisikufiche alijiingiza kwenye ujambazi baada ya shughuli za udalali kuwa haziendi kihivyo, lakini pia baa yake Alishafunga, baada ya wa kuwa hakuna wateja, na alikuwa malimbikizo ya madeni kwa wafanyakazi wake, wapo waliosamehe na wapo walioufungua kesi ya madai mahakamani. Upo kaka,
aliongea yule jamaa huku nikimsikiliza kwa umakini.
Akaendelea..........
Mtaani kwake pale Hana dhamana, kwanza ni tabia yake ya kutembea na wake za watu, tabia ambayo imewafanya watu wakose Imani naye.
Pili, Kuna tetesi jamaa, kajiingiza kwenye unyang'anyi wa kutumia silaha hivyo tayari baadhi ya watu hawataki kushirikana naye.
Lakiniiii, mke mtu yeye hajui hata kidogo yeye kwanza aliingiza wivu akijua mumewe labda yupo kwa mchepuko, Sasa basi za ndani kabisa inasemekana Shedy, washirika wake walimgeuka lengo na kumpiga risasi, ila mkewe hajui, hivyo basi wewe kama wewe leo tunaomba kushirikiana na wewe tujifanye kama tunamtafuta. aliweka kituo.
Wakati tunamtafuta tunashirikiana na nani na wewe umesema kwamba, baadhi ya majirani.,hawataki na pia tunamtafutia wapi, niliuliza.
Mbona inajulikana watu wa Bajaj na boda boda wote tayari wameshajipanga huku tukiongozwa na polisi, Kila kitu kinajulikana mbona. aliongea yule jamaa.
Kwanza wewe ni nani na kwanini uwe karibu na huyu shemej yangu?
Hii Bajaj unayoiona ni ya huyu mwanamke alinipa Mimi, na hata huyu marehemu mume wake alikuwa hajui kuwa mke wake ana miliki hii Bajaj. alijibu yule jamaa mwenye asili ya pwani ni muongeaji mzuri utasema tunafahamiana kitambo.
Tulirudi ndani huku nikijiona Sina matatizo kumbe Kuna watu Wana matatizo, niliwaruhusu watangulie wale wageni Kisha nikawaahidi kuwa nawafuata punde.
Mke wangu, naomba niruhusu niende kwa Hawa jamaa nahisi Kuna matatizo. nilishauriana na mke wangu.
Mmmh Hawa nao wamekosa watu woooote wameona waje huku, mtaa wa ishirini,mume wangu nenda ila kuwa makini maana wewe mwenyewe una yako tena yanakushinda.
Nilitoka huku nikijikoki vyema, huku tayari huruma na moyo wa kibinadamu vikinitesa , nikimuwaza Shedy huku nikilaumu shetani, kwanini alijiingiza kwenye ujambazi na kazi za hatari?
Nikikumbuka kuanzia utoto wetu, ujana, na mengine mengi nilijikuta naumia sana, wakati nikiikaribia nyumba ya Shedy niliwakuta maaskari wakimtukana mke wa Shedy.
Sikiliza wewe mwanamke, umekuja kuripoti kupotea kwa jambazi lako kumbe unatuchoresha tu, Sasa mumeo aliua, na yupo kituoni na wewe ingia kwenye gari.
Jeshi lipo imara, tutahakikisha watu kama mumeo na washirika wake wote wanaingia kwenye mkono wa Sheria, walimchukua yule mwanamke huku huruma ikiniingia sana , japo kusogea niliogopa, maana usijekuta unasombwa na maaskari wenye jazba.
Jamani mwacheni MUNGU aitwe MUNGU huyu , inasemekana kaua mwenzake Kisha akawa anatoroka hata hivyo kakatiwa mbali kabisa na maskini mke wake Wala hakuwa anajua, alisikika jirani mmoja.
Taarifa zilikuwa nyingi huku nikishindwa niiamini ipi, nikaona hapa hakuna Nini wala Nini maana niliambiwa amekufa, saizi nasikia kaua, ikabidi nichukue Bajaj hadi central moja kubwa.
Nilifika pale huku mke wa jamaa akiwa analia kama mtoto pale nje ni kweli niliambiwa na maaskari kuwa jamaa aliua, huku nikiambiwa uchunguzi unaendelea ili wajue sababu ya kuua ni Nini. Huku tulionywa kutokusambaza taarifa zisizo za kweli badala yake tuliachie jeshi lifanye kazi yake.
Nilimchukua yule shemeji yangu kwa nguvu maana alikuwa yupo nje analia tu huku maaskari walimkejeli na kumzidishia maumivu.
Nilifika nyumbani kwa Shedy,nikawakuta watoto nao wanalia sana , jamani Yale ndiyo yanaitwa matatizo sisi wengine tunapitia changamoto tu.
Niliwaita majirani na tukaungana huku nikiwashauri majirani kuwa ule si wakati wa vinyongo na visasi tusahau na tumsaidie mwenzetu, wengi walinielewa huku wanawake wawili wakikubali kulala pale pale, nilifurahi huku tukiagana ule muda wa saa Saba za usiku, nikiwaambia ngoja nikapunguze usingizi, na tutajua Cha kufanya kukipambazuka.
Inaendeleaa...........