Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Aiseee,yaani naifuatilia haswa, thanks
 
SEHEMU INAYOFUATA............

Siku hiyo ya jumamosi ilikaribia kuisha, nikarudi nyumbani mapema tu, huku nikifikiria

Dah nilijua ESTA atakuwa mwepesi kwenye hili suala lakini ni kasheshe yaani kumbe ESTA akisikia madam amekufa atafurahi eeh, ndiyo siyo kwa moyo ule mgumu.

Nilifika pale home nikipokelewa na mwanangu mwenye kiswanglish kingi mdomoni kiasi Cha baadhi ya watu mle ndani wakawa hawamwelewi,.

Mume wangu, tatizo hushindi hapa nyumbani na hapa Kuna shida.

Shida gani? niliuliza

Ni huyu Dada wa kazi yaani amebadilika tena Kawa wamoto huwezi amini ananiletea ujeuri hata Mimi, hapa Mimi naona tumpe tu nauli aondoke maana Kila muda vijana wa kiume wanapishana hapa mbaya zaidi Jana usiku nasikia Kuna watu wameumizana hapa wakigombania huyu house maid wetu,hivyo Kila nikiongea naye ananijibu kijeuri sana

Naomba niitie, niongee naye
Nikamwomba mke wangu atupishe kidogo.

Ni msichana alikuja akiwa mdogo sana tumeishi naye vizuri kama mtoto wetu hivyo mabadiliko yanayojitokeza kwenye upande wake
Busara zinapaswa zitumike na si kumkaripia.

Enheee hebu niambie mnashindana Nini na dada yako, maana ninavyojua anakupenda sana, halafu Sasa hivi ni kipindi ambacho yeye ana mtoto mdogo huoni kama utakuwa unanionea Mimi mdogo wangu?

Na ujue kuwa Mimi ndiye nilikufuata mkoani huku ikiwa ni vigumu sana wazazi wako kukuachia wakidai kuwa malezi ya mjini Mara nyingi huharibu wasichana na kujikuta wanazalishwa watoto wasiokuwa na baba, hivyo naona kile walichokiwa hawataki wazazi wako ndicho unachokifanya. Ni kwanini?

Wewe hakukatazi mtu kuwa na mpenzi kwakuwa hapo ulipo tayari ni msichana mkubwa, sisi tunahitaji wewe mchumba atakaye tokea ututambulishe tumjue na tutakushauri kuwa huyu anafaa na huyu hafai.

Na hata kama tutaona anafaa zitatumika taratibu za wewe kuhalalishana awe mtu wako rasmi kama ni mipango ya ndoa ifanyike huku tukuwashifikisha wazazi wako kinyume na hapo utakuwa nje ya maadili.

Mbaya zaidi Kuna magonjwa mengi siku hizi,nilikuchukua ukiwa mzima wewe nitaonekanaje ukirudi una kasoro family yako itanionaje? Niliweka kituo.

Hapana kwanza Mimi Sina mchumba hata mmoja bali ni wao huwa wananifuatafuata nikitoka sokoni, na yule aliyepigwa Jana usiku ni mtu mzima ambaye aliniita akitaka nimuitie yule dada ESTA aliyeondoka ndipo kundi la vijana likajua labda huwa ananifuata Mimi na kuwaharibia wakaamua kumpiga.

Unamfahamu huyo mtu, niliuliza.

Hapana simjui.

Haya nenda kaendelee na kazi zako ,
Lakini nikisikia taarifa hizi kwa Mara nyingine jua kuwa tutakupandisha kwenye gari urudi mkoani. Nilimtishia.

Ni dada ambaye alitokea kutupenda sana sisi yaani ukimwambia nitakufudisha kwenu alikuwa anajisikia vibaya sana sijui kwanini .
Akaendelea na shughuli zake .

Ni Binti mkubwa kwa Sasa, anavutia kiasi Cha kuwagonganisha vijana, hayaepukiki kwa Yale afanyayo atafanya tu, hata hivyo lazima mikwara iwe mingi tusijeonekana tunabariki mambo yale .

Asubuhi siku ya jumapili hakuna aliyeenda sehemu tofauti
Na dada yangu mpenzi kwenda kanisani ambaye naye nilikuwa na mashaka kupenda kwake kanisani .

Nikiwa nafuatilia uchambuzi wa mpira kwe TV nilipokea ujumbe mfupi toka kwa ESTA uliouliza vipi siendi kumtembelea?

Nilimjibu kuwa nitaenda jioni, kwakuwa hata moyo wangu nilipanga kwenda kuendeleza mapambano dhidi yake, lakini ilikuwa lazima nishinde nyumbani kuiridhisha familia yangu, ukisikia mwanaume mateso siyo kuihangaikia familia tu, wakati mwingine Kuna Uhuru fulani unakosa yaani watu wanataka wawe wanakuona tu nyumbani.

Mume wangu gesi imeisha, Tena MUNGU saidia mkaa ulikuwepo kwahiyo nahitaji ukatuchukulie au ita yule kijana alete.

Weeee sikutaka kumuita kijana Wala nini ilikuwa point nzuri Mimi kutoka nilienda sehemu napochukuaga huku nikimsisitiza kuwa mtungi wa mwanzo ulikuwa na regulator mbovu hivyo ajitahidi kunichagulia mzuri Kisha aagize kijana anipelekee nyumbani. Mimi huyooo mpaka kwa ofisini kwa ESTA.

Ooooh shemu huyoo unajua sana kujali Hadi wivu yaani, mdogo wangu anafaidi sana.

Haaaaa da ESTA kwani huyu siyo mumeo !!!!! Aliuliza Binti fulani kwa mshangao.

Hapana ni shemeji yangu,kwani vipi
Waliulizana.

Unajua jana mlivyokaa mkipiga stori kila mtu hapa alijua mke na mume hata Mimi nilijua hivyo kabisaaa, ila mnaendana bwana hata kama .
Aliongea yule Binti mcharuko.

Nikajisemea kweli Hawa ni watu wa saloon yaani lazima umkute mtu anayeongea kupitiliza.

Weee koma , huyu mume wa mtu tunaendana vipi, aliongea ESTA huku wakicheka na kufurahi, nilichojua hata yeye kuambiwa vile alijisikia faraja sana.

Shemu hapa nimekuja kushinda tu ili pawe wazi na Leo natoa ofa mtu yoyote ambaye atakuja kawaida nywele chache itakuwa bure, na kama njia nyingi basi atachangia kiasi kidogo.

Sasa shemu unawezaje kukaa kutwa nzima ukifanya kazi ya bure? Niliuliza.

Hapana ni njia ya kuvutia wateja tu, mbona tangu asubuhi nipo hapa nishatoa huduma kwa watu wengi sana ujue,

Heeey tangu asubuhi kumbe yupo hapa Ina maana hata kanisani hajaenda huyu, ila sikutaka kujua,.

Hana muda huyu hata ulokole wake atauacha japo haitakuwa vizuri lakini ni njaa tu zilikuwa zinamsumbua.

Maneno ya kisaluni saluni yalitawala huku mabinti wakipishana pale michambo, masimango na lugha za mtaani zilitamalaki huku nikiwa namuona ESTA mwenyewe naye mjua ESTA ambaye alirudisha makucha kipindi kapigika Leo hii namuona namna anavyojuamini,

Nilimshukuru MUNGU kwa hatua ile maana angekaa kwangu ningezidi kujenga mpasuko kwenye familia, Bora kapata sehemu ya kushinda. Lakini nikichokisoma pale kwenye saloon nilipanga siku nikipanga biashara za kufanya mke wangu Ile ya saloon hata kwenye miamoja Bora haipo.

Sasa shemu ulisema Nini kimekosekana kwenye ofisi? Niliuliza

Vingi tu, Kuna kabati fulani bado lakini haya madude ya kuchomea nywele tungepata hata mawili Hadi matatu.

Sikia we orodhesha Kila kinachotakiwa niliongea kwa sifa huku mabinti waliosikia wakiniangalia kwa macho ya wivu sana, kama ningekuwa mgeni wa mji au ni mshenzi basi mabinti wangenikoma, bahati nzuri nahitaji heshima kwangu na kwa mke wangu pia.

ESTA mwenyewe safari hii alishangaa,

Shemu wee ni mtu wa ajabu sana nashindwa kujua Nini unatafuta kwangu baba, hii ni fadhila gani, we ni mtume? Maana unazidi kujitolea tu kwangu bila kujua unataka Nini
Alizidi kuhoji

Alikuwa sahihi nikaona ni muda wa kulipua bomu japo siyo kirahisi, tukaa Kaa sehemu fulani huku tukipiga stori za hapa na pale,.

Lakini shemeji ni vyema ukasamehe na kuachilia si ajabu maisha magumu kwako ni sababu ya vifungo vilivyo ndani ya roho yako, msamahe mwanamke mwenzio,
Ni binadamu tu mliyoyafanya kipindi hicho ni mambo ya kuwahiana tu hata wewe pengine uliwahi jaribu kumfanyia vibaya mwenzio, sema hukufanikiwa tu Mimi nawajua wanawake nyinyi,nilikazia

Weeee shemu Kila nilichofanya ilikuwa ni njia ya kujirudisha kwenye ramani nilienda kwa waganga wa Kila namna si kwaajili ya kuharibu nyota ya mtu Bali kutafuta umaarufu wangu lakini Cha ajabu mwenzangu alikuwa anaenda kwa wataalamu kuniharibia Mimi,.......aliongea huku uso Ukiwa unabadilika

Hapana shemu na ndiyo maana,
Tuko hapa kuzungumza hayo madam ni mtu ambaye ameona makosa yake na amejuta kwa dhati kabisa kiasi Cha kutaka kupatana na wewe ,kwani Kuna mtu kamlazimisha hapana,ni yeye tu kaona ana deni moyoni mwake.nilisisitiza

Lakini shemeji mbona umelishikilia sana hili jambo yaani tunashindwa kuongea mengine imekuwa Kila ukija lazima ugusie hili jambo kwanini?

Nafanya kile nachoagizwa nafanya kazi yangu kwa UAMINIFU yule ni boss wangu siwezi kumgomea,lakini kwa upande wako ungekuwa na maisha mazuri ningekuacha tu lakini kama mtu kajitolea kuwa atakusaidia na kwa jinsi maisha yako yalivyo huruma iliniingia naona kama unachezea shilingi chooni , niliweka kituo.

Shemu Kuna kitu nakiona,mbona kama Kuna picha inanijia?

Ahaaaaaaaa ndiyo maana Kuna mtu aliniambia kuwa hakuna mtu Duniani atakupa msaada wa bureeeee,hata mataifa makubwa pindi yakitoa msaada kwenye mataifa madogo huwa Kuna mikataba ya mabadilishano ya vitu hakuna kitu Cha bure Duniani.
Mimi nilijiuliza Daniel alinitongoza kipindi kile Lakini kutokana na matatizo yake ilishindikana kufanya tulicho kubaliana nikiwa najua Leo kesho tutafanya mambo yetu, lakini ikawa holaa Hadi nahamia kwako bado ilikuwa tofauti Leo hii Daniel ananisaidia kwa minajili ipi Sasa nimeshajua . alizungumza ESTA akiwa kanyongea Sana.

Je,Sasa itakuwaje saloon ndiyo hiyo hapo

ESTA dizaini kama kashtukia kuwa huenda msaada anaye toa ni madam siyo Mimi,je alithibitisha itakuwaje?

Itaendelea..........
 
Siyo siri.. Hadi nasisimka
Yaaan ni motooo!!!
 
Naelekea arusha saa kumi jioni nitapitia kama umetupia kipande kingine
 
Aaaah jmni sina la kusema zaid ila huu mzgo ni balaa aseee
 
SEHEMU INAYOFUATA..............

Baada ya kugundua kuwa huenda ESTA Keshajua kuhusu msaada wangu nilimpozapoza kiaina Kisha tukaagana pale freshi kabisa nikarudi nyumbani kwangu.

Nilikuwa na amani ya moyo kiasi fulani.

Kama kajua ni fresh maana Kitengo Cha Mimi kuonekana namsaidia kwa hela yangu ya mfukoni si kweli ipo siku mambo yatakaa hadharani nikajikuta naaibika bure, nilijisemea.

Siku zilizidi kwenda huku mzigo wa watu nikiwa nishatoa kiasi fulani benki ili ESTA akinikubalia nimkanidhi mzigo wake, nakumbuka Kuna madam alinipigia simu akitaka nimpe maendeleo, baada ya kuonana tulizungumza mengi huku lawama zikianza kuninyemelea,

Tolu bwana, unaniangusha sana, sikutegemea jambo hili la kiume likushinde , Kuna watu chungu mzima ambao ningewapa hii kazi majibu yangetoka fasta nakwambia , lakini wewe umekuwa mzito sana,

Mtu mwenyewe yule Hana pesa Wala umaarufu wowote kwamba labda inaweza kumpa kiburi ,unashindwaje?

Sisi wanawake ni wepesi sana tu hasa kama mtu unajua kucheza na maneno,tongoza,tumia mbinu zako zote za kiume yule mbona atalainika?
Alizungumza madam huku akionesha kashaanza kukosa Imani na mimi.

Hapana madam,ujue najitahidi sana tu,ila mtu mwenyewe tunatakiwa twende naye kiupole mi naamini Hana siku nyingi nitawakutanisha akiwa tayari kabisa boss lady,
Niliongea kwa mbwembwe kiasi Cha yeye kulegea na kushusha ile Presha niliyomkuta nayo.tukaagana

Nikiwa peke yangu nilifikiria nikaona kama naonewa huku Kuna wakati nikianza kujilaumu kukubali maswala ya kijinga, kwanza nilishayataa haya, yaani Mimi niache shughuli zangu nianze kubembeleza mtu, kwanza hata sijajua kwanini anataka wapatane ni matajiri Hawa wanaweza hata kumdhuru.

Haiwezekani habari za miaka mingi we ukae ukizifikiria eti sijui mikosi, sijui nini ila basi maji nimeyavulia nguo haya, niliwaza kwa hasira.

Nilifika nyumbani hata sikukaa sana kwakuwa nilishakuwa mtu wa madam ikabidi nimpigie simu ESTA tuonane,

Jamani shemu, Kila siku nakuwaza nikaona mbona umenitupa sana baba, nimekumiss sana jamani.
Yalikuwa maneno ya ESTA baada ya kupokea simu.

Nakuja hukohuko,
nilimjibu kwa mkato.

Nilifika maeneo ya ile saloon huku nikifurahi jinsi palivyokuwa na wateja pale huku wengine wakilaumu kuwa wamefika muda mwingi bila huduma, lakini wengine wakidai yale madude ya kukaushia nywele nimachache, ESTA akawa anawapoza tu kuwa biashara siyo ya siku nyingi hivyo wasijali mambo yatakuwa sawa.

Nilimwita pembeni huku, nikimuuliza wale madada wawili wanaomsaidia kazi ni akina nani maana hata siku fulani mwanzoni niliwaona.

Ha ha haa(akicheka)
Hizi kazi za salooo mtu huwezi kuwa peke yako , utawezaje kumudu wateja wengi namna hii,

Haya wewe mwenyewe umekuja ili tuongee unadhani ningepata wapi nafasi ya kuongea na wewe? alijibu kwa mtindo wa swali.

Je, unawalipaje maana kazi yako bado changa hii, nilihoji.

Hawa ni deiwaka (day workers)

Hivyo kinaangaliwa kilichoingia, kama kazi nzuri tunaenda sawa na kama siku hiyo wateja wachache tunabalansiana hivyo hivyo uzuri ni kazi niliwahi ifanya, pia Mimi nishapiga sana deiwaka miezi michache iliyopita.

Eenhee nambie shemu maana toka nikukatalie kuwa siwezi kupatana na yule mwanamke basi hujanitafuta teeeena mpaka Leo, alihoji huku akiwa na tabasamu usoni.

Mimi ni mpatanishi, nampenda madam, ni boss wangu,
Ni rafiki yangu,
Mwisho kabisa ni binadamu kama binadamu wengine, anakosea pia kilichonifurahisha hata ikanisukuma niongee na wewe, ni vile alivyotambua na kujuta makosa yake hiyo ikawa chachu ya kuja kukwambia habari zake.

Lakini pia wewe,
Ni shemeji yangu,
Ni rafiki yangu,
Umeishi maisha ya manyanyaso kwa kipindi kirefu nimeamua kukusaidia, uzuri zaidi Kila ulipoona umeelemewa ulituweka wazi, hivyo nishatambua udhaifu na uimara wako,

Wewe ni jasiri napongeza misimamo yako lakini pia una kisirani kwa namna fulani, pamoja na kwamba umeokoka upo karibu na MUNGU lakini bado unapaswa kuwa na roho ya kusamehe na kuachilia yaliyopita yapite, kwanza utafungua milango mingi yenye baraka, ujue unapokuwa na kitu fulani moyoni hususani kuhifadhi roho za visasi basi hata mambo yako mengi yanakuwa hayaendi, kwakuwa unakuwa na deni la rohoni,

Sasa iweje ujitese kwenye maisha kwenye vitu vya kupita?
Niliweka kituo.

Sawa shemeji Mimi tangu siku ile nilikuelewa sana dhumuni lako ila sikupenda mazoea na yule mwanamke kiukweli, yaani hata tukipatana Mimi sitaki mazoea naye, alisisitiza.

Si lazima kuzoeana wala kushirikana kwa lolote lile lengo ni kumridhisha tu , lakini usisahau kuwa hupaswi kuwa katikati ila ukiamua kusamehe samehe moja kwa moja shemu,
Niliongeza.

Haina shida shemu wewe mwambie kuwa nipo tayari , alijibu kwa kifupi huku nikifurahi sana maana tayari nilikuwa nateseka kutwa kumbembeleza mtu hujui atakubali lini,basi shemu kesho asubuhi nitakupitishia mzigo wako ambao unatoka kwa madam, niwe muwazi na mkweli hakutaka kukuomba msamaha bure, Kuna takrima fulani aliagiza,.

Sawa untaniletea, alijibu Kisha tukaagana huku nikimwangalia jinsi alivyobadilika ghafla yaani kule kufubaa ilikuwa njaa tu kudadeki, nasikia hata kanisani siku hizi haendi, ataendaje?

Ile ilikuwa ni sehemu ya kwenda kutafuta faraja tu neno IMANI siyo la mchezo. Nilijisemea moyoni.

Kesho saa kumi na mbili nilimwamsha akanikaribisha nikapita hadi ndani, ilikuwa lazima niingie ili nimpe hela zake,

Weeeeeeeeeh shemu, hela zote hizi ni za nini, alihoji kwa mshangao.

Ni zako nikipewa na MADAM kwaajli ya kukuomba msamaha kama nilivyokuelekeza jana.

Hapana, hapana, narudia tena hapana hii si zaidi ya milioni hamsini hizi, aliuliza .

Ni milioni kumi hizi Wala hazijafika huko kote, utahesabu taratibu Mimi nawahi kazini.

Wewe Daniel, nakuita kwa jina lako hizi hela ondoka nazo, ni kweli nilikubali kupokea pesa ulizosema ila akili zangu zilicheza kwenye laki tano kushuka chini, lakini si kwa kiasi hiki, hivyo siwezi kuuza utu wangu kwaajili ya hela, ni kweli hela nazitaka na nahitaji kwelikweli, lakini huu mbona ni mtego?

Hapa naona usalama wangu ni mdogo kukipambazuka vizuri naenda polisi, naenda kuripoti juu ya usalama wangu, haiwezekani lundo kama hili uniambie kuwa eti ni hela ya msamaha, alihoji kiasi Cha kunitisha.

Sikiliza ESTA shemeji yanguuuuu, niliongea kwa upole ili sauti isisikike kwenye ile nyumba ya kiswahili,

Unazijua kampuni mbili za mzee( jina kapuni) jinsi zilivyokubwa?
Natambua unajua fika Tena wewe unamjua Hadi mwanaye mtoto wa taita.

Unamjua vyema madam yupo kwenye nafasi gani, ana vyeo viwili,
Ni mkurugenzi kwenye kampuni ambayo nilifanya kazi zamani,hicho ni cheo Cha kwanza.

Cha pili, ni mke wa boss, yaani pengine hata angekaa tu bila kazi mambo yake yangekuwa super.

Kingine unafahamu kama ana kampuni zake za upambaji ,
Unajua fika maduka yake matatu huku kubwa zaidi likiwa mkoani ambako ndiko alikozaliwa likijumuisha vifaa vyote vya ujenzi Tena vya kisasa, kitu gani uulize kwenye duka lake ukose, Nini ,
rangi, gypsum au Nini? Nilizidi kumlainisha

Ahaa lile duka ambalo, anatumia jina ambalo si lake, kwanza nasikia hataki ajulikane kama ni lake sijui kwanini, alizidi kunisapoti ESTA.

Ewaaaah, Mimi sikuwa nikiyajua haya nayasikia tu pale kazini. Hivyo milioni kumi kwake si kitu kwake hasa kwa makosa aliyokutendea , Tena hii hela mi naiona ndogo kwa makosa aliyokutendea. Nilizidi kumlainisha

Hapana hata kama najua ana miliki Mali nyingi sana lakini siyo kutoa kiasi hiki kwaajili ya kuomba msamaha labda ingekuwa kwa mtu mwenye hadhi kidogo lakini siyo kwangu, lazima niende polisi yaani kwangu usalama ni mdogo, alisisitiza akionesha hatanii hata kidogo.

Au nimekurupuka kumpa mzigo wote, au ningetoa kidogo kidogo kwanza, hii ishj ikibumbuluka ikifika kwa mke wangu mpaka mkoani kwa wazazi wangu ni kasheshe, jasho jembamba Lilianza kunitoka .

Wakati nawaza hayo ESTA alipiga simu ambayo nadhani aliongea na watu wake wa saloon akiwaambia kuwa atachelewa kufika, nikajua moja kwa moja hii ni polisi tu.

Muda nao ulizidi kwenda, bado nipo nikimbembeleza.
Hela za unafuu zilianza kunitokea puani kidume mpatanishi wa ugomvi wa watu hata historia yake sina, walianzia wapi.

Neno limekuwa neno.

Itaendelea..........................
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…