FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,229
- 4,345
- Thread starter
- #61
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 29.
ENDELEA.......
“Zote zinaweza kuwa ni sababu za msingi, kijana umefanya jambo hilo liwe nje ya mkono wangu lakini kabla ya kukufanyia maamuzi ya mwisho nataka kujua ni kwa namna gani umeweza kuniingiza kwenye kesi na waziri mpaka ayahitaji maisha yangu yaende? Anajua kama sababu ni wewe kulala na binti yangu?”
“Hapana hajui hilo ndiyo maana natakiwa kukuua kabla hajaweza kulijua hilo”
“Wewe hapo ndo unataka kuniua mimi?”
“Unahisi haiwezekani?”
“Nimekufunza mwenyewe, naijua kila sehemu ambayo ni dhaifu kwenye mwili wako, hauna hata nafasi ya kuusogelea mwili wangu. Umefanya jambo gani mpumbavu wewe?” aliongeza sauti na kuifanya kuwa kali.
“Nilitambua kwamba umejua natoka na binti yako hivyo ungekuja kunisababishia matatizo makubwa kwa hapo baadae hivyo nikaamua kukuwahi kwanza. Mimi nilikutana na baadhi ya wanasiasa wa upinzani kupitia watu wa mtaani ambao niliwalipa, watu hawa walienda pale kwa jina lako na utambulisho wako ambapo niliiba baadhi ya barua zako ambazo zina sahihi yako na kuzitumia kama ushahidi. Wana siasa hao baada ya kupata habari hiyo waliona ni fursa ya kumuangusha waziri lakini kabla ya yote kufanyika nikavujisha habari na kwake pia hivyo akajua na kuwafuata hao watu na kwa sababu yeye ni mkubwa na wanamuogopa, ikawalazimu kusema ukweli kwamba ni wewe ndiye uliwafuata.
Jambo hilo limempa hasira, hasira ambayo imetosha kufanya maamuzi ya mimi kukuua wewe bila kuacha ushahidi wowote ule. Hiyo ndiyo sababu ambayo ilinifanya leo niigize kama naondoka hapa kwa sababu nilijua kabisa kwamba kila mtu ataamini leo sitakuwepo hivyo kama wewe ukifa hakuna mtu hata mmoja ambaye atanihisi kwamba ni mimi nimehusika hivyo nitakuwa salama hata kwa mwanao ambaye naenda kumzalisha na nikijisikia nitamuoa maana hatajua na wewe hautakuwepo kuweza kumfumbua macho”
“Mtoto wa malaya wewe kijana”
“Malaya ni binti yako ambaye nilimtoa bikra mzee wa……” wakati anamalizia sentensi hiyo aliinama baada ya kuona vitu vinakuja kwa kasi, zilikuwa ni sindano zenye sumu. Aliinuka na kukutanishwa na mkuu wa kifua ambapo aliburuzika kidogo nyuma akanata kwa kukunja vidole vya mbele vya mguuni ambavyo vilikifanya kiatu kutulia kwenye smenti akasimama vyema kabisa.
“Nilijua utapaniki kwa sababu inauma kupigiwa mwanao na kijana ambaye humpendi au unaona hafai kuwa na mwanao. Umesema kwamba siwezi kukusogelea hata nguo zako ila sio kweli mzee, mimi sio mjinga mpaka kukubali kazi ya kukuua tena nikiwa mwenyewe. Kama kweli ningekuwa sikuwezi basi ningeikataa kazi na hata kama ningeifanya basi ningekuwa na watu zaidi ya mmoja”
“Umefanya nini mjinga wewe!?’’ mzee huyo aliongea huku akihisi kama mwili wake ulianza kuwa wa tofauti, alijigusa kwenye mdomo wake na kugundua kwamba alikuwa anavuja damu.
“Unaikumbuka ile dawa yako ya asili ambayo huwa unaitumia! Sasa ile dawa kabla ya kuondoka mimi nimetia sumu ndani yake, ni masaa mengi yamepita maana yake ile sumu ishaanza kufanya kazi hivyo itakulegeza. Mbali na hilo kuna jambo lingine ambalo haukuwahi kulijua kutoka kwangu mzee, nadhani nimekuambia kwamba mimi ni mtu ambaye huwa napenda kujiongeza kwenye kila jambo ambalo ninalifanya, vivyo hivyo na kwako niliamua kujiongeza pia. Wakati nakwambia kwamba nilikuwa nafanyia mazoezi chumbani nilikuwa namaanisha, binafsi baada ya kugundua kwamba hili ndilo eneo ambalo hata wewe huwa unafanyia mazoezi na ni watu kadhaa huwa wanaruhiwa kufika hapa, nilijiongeza kwa kutega kamera kwa sababu niliamini kwamba mwisho wetu unaweza usiwe mzuri.
Kupitia kamera hiyo, nilianza kujifunza mambo mengi kuhusu wewe kuanzia udhaifu wako, uimara wako uko wapi lakini pia niliweza kuona staili zako za siri za mapigano ambazo hata mimi mwanafunzi wako pendwa haukuwahi kunionyesha wala kuhitaji niweze kuzifahamu. Staili hizo niliweza kujifunza mimi mwenyewe, nilikuwa nautumia muda wa kuweza kupumzika kufanya mazoezi nikiwa ndani kwangu kwani niliamini hii siku ingekuja kuja kwa namna yoyote ile. Mimi leo kuja hapa sijaja kwa bahati mbaya, najua kila sehemu ambayo ungeweza kupitia. Kuna siri moja ambayo watu wengi walikuwa hawaijui kutoka kwako, siri ya kwamba kwenye mwili wako ulikuwa na nguvu za ajabu ambayo umeamua kuishi nazo miaka na miaka na jambo hilo pia niliweza kulitambua kupitia kamera yangu.
Baada ya kutambua hilo nilelewa kwamba licha ya kuweza kujifunza kila aina ya mazoezi bado nisingeweza kusimama na wewe na ndiyo sababu ambayo ilinifanya nikaamua kutumia sumu. Nilijua kwamba mwili wako ukiwa na sumu hautakuwa unaweza kuzitumia hizo nguvu zako kwa sababu kama ukijaribu kuzitumia basi utakuwa inaipasua mishipa ndani ya mwili wako jambo ambalo litafanya ujiue mwenyewe. Na ni simu ambayo imekufanya hata ule uwezo wa hisia zako kali kuweza kupotea ndiyo maana nimeweza kufika mpaka hapa ukiwa hauna taarifa kama nimeingia kwa zaidi ya dakika tano nikitazama ambacho unakifanya hapa. Kwahiyo kwa siku ya leo utahitajika kutumia zile nguvu zako za mazoezi tu na sio hizo za asili lakini pia utambue kwamba sumu imeanza kukuathiri tayari mpaka damu inakutoka mdomoni na kila muda utakavyo zidi kwenda ndivyo hali yako itakuwa hatari zaidi labda kama utawahi kupatiwa matibabu” maelezo marefu ya Jaden ndiyo ambayo yalihitimisha mzee huyo kujua kwamba kijana alikuwa amedhamiria kweli kuweza kuondoka na maisha yake. Alitabasamu kwa sababu kwenye maisha yake aliwahi kujiona kwamba yeye ni mtu mmoja makini, kuzidiwa na kijana tena ambaye alikuwa anazidi kumtengeneza mwenyewe kwake kilikuwa kama kichekesho.
“Sikuwahi kufikiria hata siku moja kwamba anaweza kutokea kijana wa kawaida kama wewe akaja kunifanyia mimi haya. Siku zote nimekuwa nikijiona kama mtu ambaye nipo makini kwa kila hatua ambayo nina ifanya ila sikuwa sahihi, kuna mahali nilifanya mahesabu yangu vibaya ambayo yanaenda kuniingiza matatizoni. Lakini hili jambo ilitakiwa Aimi aweze kujua na wafanyakazi wangu wote hivyo hakuna mahali bado unaenda”
“Aaaaaaah! Mzee wangu unataka ufe kwa aibu namna hiyo? Unahisi dunia itakuonaje hata kama utapona ikigundulika kwamba ulimkimbia mwanafunzi wako? Nani ataamani kwamba wewe ni yale masalia ya Samurai huku unaukimbia upanga na kwenda kulia lia mbele ya binti yako akusaidie? Naelewa vizuri historia ya Samurai, naelewa historia ya Japan lakini historia yako wewe pia. Kwenu heshima ni kitu kikubwa kuliko hata uhai hivyo unatakiwa ushike upanga wako na kujaribu kupambana na mimi hapa na sio kunikimbia. Ni muda wa wewe kuweza kujaribu bahati yako ya mwisho ili ukishindwa ufe kwa heshima kwamba ulikuwa unaipambania heshima yako kwa sababu siri zako zitazikwa na wewe hakuna mtu atakuja kujua kwamba wewe ulikuwa muuaji kama mimi ambavyo nipo kwa sasa. je utakimbia?”
“Moja kati ya makosa makubwa ambayo niliyafanya ni kukuona kama kijana wa kawaida na kama ningejua hili mapema basi nilitakiwa kuishi na wewe kwa namna nyingine”
“Kwa bahati mbaya ni kwamba muda haupo upande wako kwa sasa, muda sio rafiki kwani una dakika kadhaa za kuweza kuendelea kuishi”
“Nakuapia kijana, nitakuua na nitaishi halafu baada ya hapo nitarudi kwenye zile zama zangu hivyo naenda kumuua huyo mshenzi waziri na familia yake yote”
“Kama utakuwa na hiyo bahati ya kutoka hapa salama basi binafsi nakuruhusu ukafanye lolote ambalo unalitaka mwenyewe ila kumbuka tu huu sio usiku wangu wa mimi kuweza kufa, mpaka hapo nadhani unajua kabisa kwamba mtu ambaye anatakiwa kufa ni wewe na sio mimi” Shimamoto alichukizwa zaidi, kijana yule alikuwa anaongea bila heshima mbele yake na kumchukulia kama mtoto mwenzake, hali hiyo ndiyo ambao ilimtaka yeye kumfanyia mbaya Jaden.
Aliikunja mikono yake ambayo iliitikia kwa sauti ya mifupa ambayo ilikomaa, mikono hiyo aliikunjua lakini wakati huo alikuwa tayari anasogea kwa kujivuta mbele kuelekea mahali ambapo alikuwepo Jaden. Ujio wa mzee Shimamoto ulikuwa ni mkali ambao ulimtaka yeye kuwa makini zaidi kwa sababu vinginevyo alikuwa anakufa. Ule mkono mmoja wa kulia uliikosa shingo yake na kugusa kwenye ukuta ambapo ukuta ulibabuka kwa nguvu ambayo ilitumika. Mzee Shimamoto aligeuka kwa mguu mmoja mmoja ukiwa unaelea, Jaden alitumia mikono yake kuupangua ule mguu lakini ule mwingine ulikuwa unakuja kwa kasi ambapo ulitua kwenye mbavu yake akarudi nyuma kidogo.
Aliinua uso wake wakati ambao aliona vazi la mzee huyo linakuja kwa kuzunguka, hakuelewa mikono ipo sehemu gani hivyo kwenye kulikabili lile vazi alijikuta anapigwa kwenye shingo, alikohoa na kujinyoosha haraka kwani alitaka kumeza ulimi wake, mkono mwingine ulitua kwenye paji lake la uso hapo ndipo alitambua kwamba anafanya uzembe mwingi ambao ulikuwa unaweza kwenda na maisha yake. Aliipanga mikono yake na yeye huku akiwa anainyoosha shingo yake, mzee Shimamoto alidunda kwenye kasafu akajigeuza kama mshale, alimkosa Jaden miguu ikatua kwenye ukuta wakati huo aligeuka na mikono yake miguu ikiwa bado ukutani.
29 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.