Mnachihanguuu
JF-Expert Member
- Feb 10, 2023
- 4,973
- 7,333
Mkuu safi sana
Duuu, niliona imepotezewa mpaka Mimi mwenyewe nikaisahauLete mwendelezo
Tunafuatilia kwa ukaribu, tuletee vitu mtaalamDuuu, niliona imepotezewa mpaka Mimi mwenyewe nikaisahau
Kaka kupoteza simulizi kali kama hii?Duuu, niliona imepotezewa mpaka Mimi mwenyewe nikaisahau
Mimi masubiri ya jumba jeupeSTORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
Storyteller: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
UTANGULIZI.....
EPISODE 1.
BANZOKA
Pembezoni mwa barabara ndogo ya vumbi ambayo ilikuwa inaingia kwenye kichaka kilichokuwa kimemezwa na miti ya kutosha, mwanaume mmoja alikuwa akijikokota huku akiwa anavuja damu kwa wingi. Alikuwa anauburuza mguu wake ambao haukuwa kwenye hali nzuri kabisa, mguu wake ulikuwa una alama za kukatwa na makovu kadhaa ambayo hayakumfanya bwana huyo kuwa kwenye hali nzuri kiafya.
Hatua zake hazikuwa za kuridhisha kabisa kwa sababu alionekana kuwa mtu ambaye alitembea kwa muda mrefu bila kuwa na msaada. Alionyesha hofu usoni ambayo iliufanya hata moyo wake kwenda mbio kiasi cha kupiga mpaka kwenye kifua chake hata mtu ambaye angekuwa umbali kadhaa kutoka mahali ambapo alikuwepo basi angetambua kwamba bwana huyo alikuwa amemezwa na taharuki ambayo ilimnyima raha na amani kiasi cha kumpatia mawazo ya namna hiyo.
Sura yake haikuwa ikionekana vizuri huenda kwa sababu ya kiza ambacho kilikuwa kimelimeza lile eneo ukijumlisha na miti ambayo ilizungukia eneo hilo ndiyo kabisa ilizalisha kiza na kulifanya kuwa tulivu isipokuwa hatua za bwana huyo ambazo hazikuwa na umakini kwa sababu ya kukosa utaratibu maalumu kwani alikuwa akiumia. Kwa mwonekano wake wa mbali hakuwa mtu mwepesi, alionekana kuwa shupavu na shababi ambaye mwili wake ulikuwa umeshiba vilivyo kama sio kwa mazoezi makali basi bwana huyo alikuwa amezoea maisha magumu ama yale maisha ambayo hayana utulivu kabisa ndani yake.
Tafsiri ya maisha yake ilikuwa inakuja kwa namna alivyokuwa na hali ambayo alikuwa nayo kwa wakati huo, alikokuwa ametoka kwa nyakati hizo hakukuonekana kuwa na usalama wa kutosha ndiyo maana hali haikuwa inavutia kwa upande wake. Alisikika akiwa anahema kwa nguvu, ile sauti yenye kitetemeshi ndani yake mithili ya mtu ambaye alikuwa anautua mzigo mzito ambao aliubeba kwa muda mrefu kwenye mwili wake na moyo wake kwa ujumla. Mbalamwezi ilichanua nyakati hizo na kusababisha mwanga kwa mbali ambao ulifanya hata lile jasho lake kuchuruzika na kumpa nafasi ya kuona umbali mdogo ambao hata yeye mwenyewe hakuonyesha kama umbali huo ulikuwa unaenda kuwa na msaada kwa upande wake yeye.
Aligeuka nyuma mithili ya mtu ambaye alikuwa anahakiki jambo ama kuna kitu alikisahau huko ambako alitoka, aligundua kwamba hakukuwa na usalama wa kutosha kwani mwili wake haukuwa na utulivu, alikuwa anapata misisimko ambayo ilizidi kumpatia tahadhari juu ya eneo ambalo alikuwepo, mpaka wakati huo alitambua kabisa kwamba lilikuwa ni suala la muda tu kuweza kufikiwa mahali ambapo yeye alikuwepo. Mwili wake ulikuwa kama unashindana na nguvu zake za kutembea kwani alijihisi kama ana kizunguzungu kikali kwa nyakati hizo, kilikuja katikati ya hiyo safari yake na kwenye kumbukumbu za maisha yake hakuwahi kufikiria kama aliwahi kuwa na tatizo la namna hiyo kabla.
Alitikisa kichwa ili aweze kuwa sawa ila alihisi kama anaona nyota mbilimbili mbele yake, alishika kichwa huku akiwa anaguna kwa maumivu ambayo yalitosha kumfanya jicho lake kutoa chozi bila kupenda. Bwana huyo alijigeuza akiwa anazunguka hiyo sehemu na maumivu yake, hapo ndipo mwili wake ulionekana vyema. Upande wa ubavu mmoja ulikuwa na kisu ambacho kiligota hapo, kwenye mgongo wake kulikuwa na nondo fupi ambayo ilisalia kwenye huo mwili wake lakini pia upande wa nyuma wa shingo yake ulikuwa umetobolewa kidogo eneo ambalo lilikuwa linatoa damu taratibu. Mwili wake ulionekana kuchakaa vya kutosha kwa kipigo ukiacha upande wa mbele ambao alionekana aliulinda ipasavyo ndiyo maana ulionekana kuwa ngangali bado.
Bwana huyo ile hali ilionekana kabisa kumuelemea pale alipokuwepo, hakuweza kusimama tena kama mwanzo, aliyumba yumba na kujisogeza mpaka pembezoni eneo ambalo lilikuwa na mti mfupi na mnene. Alidondokea upande wa pili na kuegamia mti huo huku akiwa bado anahangaika na maumivu ya mwili, kichwa ambayo kwa pamoja yalikuwa yanashindana na mawazo yake.
“Zyra” alitamka jina ambalo lilionekana kuwa la kike kwa sauti yenye kitete lakini ambayo ilishiba vya kutosha, alilitamka neno hilo kwa sauti ndogo na nyepesi ila ule uzito wake ndio ambao uliifanya isikike kwa mbali. Haikueleweka sababu ya mtu huyo kuweza kulitaja jina hilo tena akiwa sehemu kama hiyo ambayo ilionekana kutokuwa salama kabisa kwa upande wake. Huenda lilikuwa ni jina ambalo ndiyo ilikuwa sababu ya yeye kuishia sehemu ama eneo hilo ama lilikuwa ni jina ambalo lilikuwa na maana kubwa kwenye maisha yake, kwa nyakati hizo ni yeye pekee ambaye alikuwa ana majibu ya sababu za kulitaja jina hilo eneo kama hiyo na wakati kama huo.
Aliketi kwa kuuegamia huo mti lakini akiwa anahangaika na maumivu makali ambayo yalimvaa huku akijua kabisa maisha yake yalikuwa kwenye hatari kubwa, akili yake ilimrudisha nyuma dakika kadhaa ambazo zilikuwa zimepita. Bwana huyo alikuwa anakimbia kwa spidi ambazo kama mtu ambaye alikuwa anamfukuza asingekuwa na kasi ya kutosha basi abadani asingempata kwenye maisha yake yote. Alionekana kukimbia ili kuiponya nafsi yake ambayo haikuwa na usalama wa kutosha kwa nyakati hizo, alitamani kama angekuwa anafukuzwa na mtu mmoja ama wawili lakini haikuwa hivyo, walikuwa ni wanaume wapatao sita ambao walikuwa wapo nyuma yake kula naye sahani moja.
Ile miondoko yake ambayo ilikuwa inakatisha tamaa kwa wakimbizaji, haikufua dafu kuweza kuwafanya wanaume hao kughairi safari ya kumpata bwana huyo. Akiwa anaendelea kukimbia ni kama mwili wake ulianza kuchoka mpaka akahisi ile hali haikuwa ya kawaida kwake, hakuwa mbovu namna ile kiasi kwamba kwa muda mfupi tu aweze kuwa na ule uchovu. Akiwa anaendelea kujiwazia huku akiwa anaendelea kuikata nyika ndipo alihisi hali isiyo ya kawaida, ni ile hali ya mvumo wa upepo, ni kama ilizidi kwa upande wake, alihisi kuja jambo zito nyuma yake hivyo alijivutia pembeni ambapo kulikuwa na mti. Kujivuta kwake kulimsaidia kuikwepa nondo moja ndefu kiasi na yenye makali ya kutosha ikaenda kukita kwenye mti mdogo ambao ulikuwa mbele yake kiasi kwamba nondo hiyo ilizama na kutokezea upande wa pili.
Kama ingefanikiwa kuingia kwenye mwili wake basi mpaka muda huo asingekuwa hai kwa namna yoyote ile. Alihema na kuendelea na safari yake kwani alikuwa ameshaanza kuvisikia vishindo vizito vikiwa vinakuja karibu na alipo tena wahusika wakionekana kuwa na usongo mkali na huyo bwana kama wangempata. Kila ambavyo alikuwa anajaribu kukimbia ndivyo ambavyo mwili wake ulizidi kuwa wa utofauti mpaka yeye mwenyewe akaanza kujitilia shaka na hizo harakati zake za kujiokoa. Kujiuliza uliza mara mbili mbili wakati ambao alitakiwa kuyapambania maisha yake kwanza likawa kosa lake la maisha ambalo kila dakika ilivyozidi kwenda mbele alianza kulijutia kwa maumivu makali.
Ule wakati ambao aliutumia kuwaza ni wakati ambao alikuwa amefikiwa, alichotwa kwa nguvu kubwa na kwa sababu hakuwa na balansi ya kutosha, bwana yule alibaki anaelea hewani huku akitoa sauti ile ya mshtuko wa kutoamini bado kama jambo hilo lilikuwa linamfika hizo nyakati eneo ambalo yeye mwenyewe alitambua kwamba hakuwa na msaada kutoka kwa mtu yeyote yule zaidi ya mikono yake na mbio zake tu pekee. Alitua kwa sarakasi nne ambazo zilimfanya kuyumba kwani hakutarajia, muda ambao alikuwa anaendelea kujipanga alihisi kama kuna kitu kimezama kwenye mwili wake hapo akaundua kwamba ni nondo fupi ilipita nyuma ya tumbo. Alipiga hesabu za kujivuta mbele zaidi ila huko ndiko kulioonekana kuwa na hatari kubwa zaidi ya nyuma.
Alikutana na mguu ambao ulitua kwenye shingo yake, ule mguu ulikuwa mithili ya mtu ambaye alikuwa anapiga mpira aina ya volley. Damu ilimtoka mdomoni bila kupenda huku akiwa anatokwa na jasho jingi na nondo ikiwa kwenye mwili wake. Alisogea pembeni akiwa anahema kama kuku ambaye aliwekwa kati kwa ajili ya kuliwa na wali, hapo ndipo akawaona hao mabwana ambao walikuwa wanayahitaji maisha yake kwa nyakati hizo. Walikuwa watatu, wawili mbele na mmoja nyuma, moyo wake ulipiga kite baada ya kugundua kwamba aliingizwa kwenye mtego mwingine uliohitaji muda wa kutosha kuweza kuutegua lakini kwa habati mbaya hata huo muda hakuwa nao. Aligundua kwamba wanaume hao walikuwa sita tangu mwanzo, sasa hao watatu walikuwa wapi? Haukuwa muda sahihi kwa yeye kuweza kulijibu hilo swali lake zaidi ya kuweza kuyapigania maisha yake.
“Ulitakiwa kulihama hili taifa wakati ambao ulikuwa na nafasi, unajua kabisa ambacho kimewatokea watangulizi wako ambao wamewahi kuwa kwenye hiyo nafasi yako lakini bado ukaleta jeuri. Maisha hayaendi hivyo ndugu yangu, ona sasa muda huu unaenda kufa tena kama mbwa bila msaada ndani ya kichaka kidogo kama hiki kisicho na sifa hata ya kuitwa msitu” alitamka bwana mmoja ambaye alikuwa amevaa nguo zilizokuwa nzito lakini kwa upande wake hata huo uzito haukuwepo kabisa, alikuwa anaongea na mtu aliyekuwa katikati yao akiwa hana mahali pakwenda. Walionekana kutambuana kwenye maisha mengine ambayo yalipita ila kwa wakati huo ni huyo mwanaume mmoja ambaye alitakiwa kuyapigania maisha yake kutoka kwa hao mabwana.
Hakuwapa nafasi ya kuwajibu maneno yake ya thamani kwani alijua kabisa kwamba hayakuwa na msaada wowote kwa upande wake. Alizikunja ngumi zake kwa ustadi na kuwanyooshea wanaume hao ambao walimfuata kwa pamoja pale kati. Alikimbilia mbele na kuinama akipiga goti ambapo alijilaza kabisa na kughala ghala huku akiwa makini ile nondo isizidi kuingia ndani kiasi kwamba wale mabwana wakapishana naye akaibukia upande wa pili, hakusimama, bali zilikuwa ni mbio ambazo zilitakiwa kumponya. Kwenye kukimbia kwake ndiko ambako kulimponza kwa sababu baada ya sekunde thalathini tu alirudi nyuma kwa hatua kama kumi baada ya kukutanishwa na kitu ambacho yeye alihisi ni kama nyundo nzito imetua kwenye kifua chake.
Ndiyo kwanza kabisa naifunua episode ya kwanza ya simulizi hii bora mno ya JUMBA JEUSI. Ni simulizi ambayo ina mengi ya kutupatia ndani yake, utaisoma siasa kwa undani zaidi na namna inavyofanya kazi hususani kwenye mataifa ya Afrika hivyo nakusihi ungana nami kuanzia mwanzo mpaka siku ambayo nitatua nukta ya mwisho na kusema nimeimaliza rasmi.
Nyuma ya kalamu ni mwandishi wako pendwa wa siku zote, FEBIANI BABUYA wao wanapenda kuniita Bux the storyteller.
Wasalaam.
YesKaka kupoteza simulizi kali kama hii?
OkayMimi masubiri ya jumba jeupe
😂😂😂😂Imetosha..
Wakachangie sasa buku buku huko insta......
Shukrani mtaalam FEBIANI BABUYASTORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
EPISODE 17.
ENDELEA.......
“Nashukuru kwa kuniokolea muda kwa sababu unaonekana kuwa mwanamke muelewa tofauti na nilivyokuwa nakufikiria”
“Ni kazi gani unataka kunipatia?”
“Kuna binti unatakiwa umtafute kisha umlinde hata ikikulazimu kuyatoa maisha yako yote”
“Unamaanisha kitu gani?”
“Ni kwamba kuna binti anasoma ndani ya chuo cha mwalimu Nyerere, ni binti ambaye hata mimi simfahamu ila unatakiwa kumpata”
“Unanipa kazi ya kumtafuta mtu ambaye hata wewe mwenyewe haumjui?”
“Ndiyo”
“Siwezi kuifanya kazi kama hiyo kwa sababu haiwezekani”
“Wewe ndiye ambaye unatakiwa kutafuta njia ya kuhakikisha jambo hilo linawezekana”
“Kwanini unahisi naweza kuifanya kazi kama hiyo?”
“Kwa sababu ndiyo maisha yako Jessica”
“Sasa nitamjuaje?”
“Utamjua kwa sababu ni tofauti na mabinti wengine, huo utofauti wake ndio ambao unafanya awe wa mhimu kuliko hata maisha yako hivyo nakuomba sana hakikisha unampata huyu binti”
“Jina lake anaitwa nani?”
“Luana ndilo jina lake la kuzaliwa japo kwa sasa anaweza kuwa na jina tofauti kutokana na historia ya maisha yake ambayo sipo tayari kukupatia hapa”
“Baada ya kumpata natakiwa nimpeleke wapi?”
“Unatakiwa umlinde mpaka siku ambayo utakuwa na uhakika na usalama wake”
“Kuna jambo ambalo hautaki kuniambia si ndiyo?”
“Yapo mengi binti ila kwa bahati mbaya haupo kwenye nafasi ya kuweza kuyajua haya mambo kwa sasa”
“Kama ni hivyo unanipa kazi ngumu kuweza kukusaidia ombi lako”
“Kuna jambo baya linaenda kulikumba hili taifa ndiyo maana nimehitaji msaada wako”
“Jambo gani hilo?”
“Kama nikikwambia hali itakuwa mbaya zaidi”
“Mpaka unakuja kwangu maana yake kwenye hesabu yako uliona kwamba mimi unaweza ukaniamini kiasi kwamba ukanipa nafasi ya kumlinda mtu ambaye bila shaka kwako ni mhimu sana hivyo sioni kama kuna jambo kubwa zaidi ya huyo binti”
“Raisi anaenda kuuawa”
“Samahani umesema?”
“Muda sio mrefu taifa hili linaingia gizani, raisi anatakiwa kufa”
“Ni nani huyo mwenye hiyo jeuri ya kupanga njama za kuweza kumuua raisi?”
“Sio kila mtu ni mwema na sio kila mtu ni dhaifu kuliko raisi bibie”
“Mimi na wewe tunajua kabisa kwamba jambo hili haliwezekani kabisa kutokea”
“Mimi ninajua kwamba linawezekana na hakuna wa kuweza kulizuia ndiyo maana nimekuja hapa kwako”
“Bado sijakuelewa, ni nani ambaye anaweza kumuua raisi? Na jambo hata kama halipo, imekuwaje usalama wa taifa hawajui? Inakuwaje shirika letu halina taarifa hizi?”
“Nisikilize bibie, taifa hili linawatambua usalama wa taifa tu, hilo shirika lenu halitambuliki kama lipo kwa sababu ni kama wazo la kufikirika tu ndiyo maana hata wewe hakuna mtu anaye ijua kazi yako zaidi ya watu kadhaa tu hususani wakubwa zako. Hata kama wangejua hao usalama, una uhakika gani kwamba wao hawawezi kuwa sehemu ya huo mpango?”
“Kama unaweza naomba unipe nafasi ya kumsaidia raisi wangu”
“Nasikitika kusema kwamba hauwezi kufanya hivyo na hakuna namna unaweza kuzuia hili jambo zaidi utafanya mambo kuwa mabaya zaidi”
“Raisi anajua kuhusu hili?”
“Hapana”
“Unaonekana unajali kuhusu yeye sasa kwanini usimsaidie?”
“Mambo hayaendi hivyo bibie ndiyo maana nimekwambia kwamba siwezi kukupa taarifa zote ambazo unazitaka wewe. Ipo siku muda ukifika tunaweza kukutana ama kuna watu watakuja kukupa taarifa kamili na sababu za msingi za huyo binti kutakuwa kulindwa na wewe”
“Kwanini wanahitaji kumuua raisi?”
“Ni sababu nyingi ila kikubwa ni kwamba uzalendo wake ndio umekuwa shida kubwa”
“Uzelendo? Hilo ndilo jambo la msingi zaidi kwa taifa sasa kivipi raisi kuwa mzalendo iwe sababu ya yeye kufa?”
“Unahisi hao watu wenye pesa wanajali lolote kuhusu uzalendo? Unahisi wanajali lolote kuhusu raia wa taifa hili? Kama ulikuwa unawaza hivyo basi bado una mengi ya kujifunza. Siasa haipo hivyo bibie, siasa ni mlima mkubwa zaidi hata ya ule mlima pendwa wa Kilimanjaro, siasa ina mambo mengi ndani yake lakini pia ina watu wengi ambao wana malengo na maono tofauti lakini ono moja kubwa kuliko yote ni pesa. Hao watu wote ambao nimekutajia hapo lengo lao kuu ni pesa hivyo kama ukija na mlengo wa kutaka kuzuia jambo hilo kwao unakuwa hauna umuhimu wowote ukiwa hai hivyo ni bora ufe”
“Unamaanisha wanamuua kwa kazi nzuri ambayo anaifanya?”
“Kuanzia wakati huu hatutakiwi kulizungumzia jambo hili kwa mara nyingine tena na wala nisije kusikia unalitaja mahali popote kwa sababu itachukua dakika kumi tu mimi kupata habari hizi pindi ukiufungua mdomo wako. Kuanzia sasa unatakiwa kwenda kumlinda binti huyo na kama ukimpata basi hakikisha unaondoka naye hata ikiwezekana mbali na taifa hili mimi nitakutafuta” maelezo ya mzee huyo yalibaki yanamshangaza kwani hakuwa anamuelewa kwa sababu alikuwa anaongea mambo magumu na ya kutisha kwa lugha rahisi na ya kawaida kana kwamba alikuwa anaenda kuwinda ndege wa mwituni.
“Na chuo?”
“Chuo na maisha ya mtu kipi kina thamani kubwa? Huyo binti anaweza kusoma sehemu yoyote hapa duniani hivyo mtafute kwanza”
“Kwanini mimi?”
“Kwa sababu unafaa kwa hii kazi. Kumbuka tu huyo binti kuwa hai ni jukumu lako wewe na kama atapata tatizo lolote lile basi sitakusamehe maisha yako yote” mzee huyo alishuka akiwa amejifunika na kofia na wakati anashuka kuna gari ilifika hapo akaingia ikatoweka ikiwa na namba za Ikulu jambo ambalo lilimshangaza Jessica kwani bado alikuwa yupo njiapanda akihisi kama ni mtu ambaye alikuwa ndotoni na muda wowote ule angeshtuka lakini haikuwa hivyo.
Kazi ambayo alisisitizwa kuifanya mpaka wakati huo ilionekana kwamba ilikuwa imemshinda ndiyo maana alihitaji kujua ukweli kuhusu maisha ya Bazoka kama alikuwa hai aweze kumsaidia kwani ni yeye pekee ambaye aliamini kwamba angekuwa na uwezo wa kumsaidia. Sasa ngempatia wapi mwanaume huyo ambaye mpaka muda huo ilikuwa ni hamsini hamsini kwamba yupo hai au emekufa. Sehemu ilikuwa ni moja tu ya kuweza kupata dodoso za mwamba huyo, kwa mpenzi wake.
Baada ya kupewa taarifa ya kufa kwa raisi akiwa bado hai kabisa alianza kufuatilia taarifa za watu wa karibu zaidi na raisi ili aweze kumtambua ambaye alimpa kazi lakini alihitaji kuwa na uhakika kama yule mtu alikuwa sahihi au alitaka kumtumia kwa kazi zake binafsi kupitia Ikulu jambo ambalo alijua ni wengi huwa wanautumia huyo mwanya kuweza kukamilisha kazi zao binafsi. Hivyo moja ya watu ambao alianza kuyafuatilia maisha yao kwa ukaribu alikuwa ni mlinzi mkuu wa raisi. Mwanaume huyo aliipata historia yake ambayo haikuwa ndefu japo kwenye hiyo taarifa kulikuwa na habari moja ambayo ilimvutia kuweza kuifuatilia kwani ingemfunulia mengi kwenye hiyo safari.
Habari ambayo ilikuwa nzuri kwake ni baada ya kugundua kwamba bwana huyo alikuwa kwenye penzi la siri na mrembo mmoja ambaye alikuwa akifanya biashara ya vipodozi. Mwanamke huyo alikuwa maarufu mno nchini kwa sababu alikuwa ni Miss Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo lakini pia mwaka huo alitoka kushinda tuzo ya Miss East Africa. Kutokana na mvuto tukuka wa huyo mwanamke, ni wanaume wengi walikuwa wanatamani kuweza kumpata lakini waliishia kugonga mwamba kwa sababu hakuwa tayari kuwa na mwanaume yeyote yule akidai kwamba alikuwa na mwanaume wake ambaye alimpenda mno na muda mfupi baadae wangeenda kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mume na mke.
17 inafika mwisho.
FEBIANI BABUYA.