SIMULIZI: JUMBA JEUSI

SIMULIZI: JUMBA JEUSI

STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 18.
ENDELEA.......

Huyo mwanamke ndiye ulikuwa ubavu wa mlinzi mkuu wa raisi, wanaume wengi kushindwa kumpata mrembo huyo sifa zilizagaa kila kona hivyo ikapelekea kila mtu akawa anahitaji kuweza kumjua mwanaume ambaye alikuwa anampa kiburi mrembo huyo kiasi kwamba akawa anamkataa kila mwanaume ambaye alikuwa anakuja na kuonekana mbele yake lakini wote waligonga mwamba kwa sababu mahusiano yake yalikuwa yana usiri mkubwa mno. Wawili hao walikuwa na mapenzi ya kweli na ya dhati lakini ya siri kutokana na kazi zao kutohusiana moja kwa moja na kama yangekuwa wazi basi ingekuwa hatari kwao wote wawili.

Kwenye kuanza kuzifukua habari hizo ndipo Jessica alipo zipata kwenye mkono wake, alijaribu kufuatilia ili kuweza kuona kama mapenzi hayo yalikuwa na uhusiano wowote na raisi kwenda kuuawa lakini hakuona kasoro wala dosari yoyote ile hivyo akaona ni jambo ambalo halimhusu kwa wakati ule japo kiitifaki haikuwa sawa ila alivutiwa na simulizi ile ya yale mapenzi akajikuta anavutiwa na watu hao wawili hivyo akaamua kuwaacha na maisha yao kama yalivyo. Ila kwenye mazingira ambayo alikuwepo wakati huo akihitaji kuupata ukweli wa maisha ya Bazoka ndipo alimkumbuka mrembo huyo kwa sababu kama ni kujua wapi alipo basi huyo ndiye ambaye alikuwa anapaswa kuwa na taarifa za mwanaume wake ndipo akajikuta analitamka jina hilo
“Zyra” alitoa tabasamu hafifu wakati huo akiwa anavaa haraka haraka na kubeba funguo za gari kisha akatoka ili awahi kwenda kukutana naye ana kwa ana kwani alikuwa na mambo kadhaa ya kuweza kuongea naye.



ZYRA
Lilikuwa ni jina ambalo lilikuwa linatoa tafsiri sahihi ya nini maana ya urembo, jina ambalo lilikuwa linaelezea maana sahihi ya mwanamke ambaye ameumbwa kisha dunia ikamnakshi kwa uzuri wake na kila mtu akabariki jambo hilo. Alikuwa ni miss Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo na mwaka huo wa tatu pia alifanikiwa kuwa Miss East Africa (Afrika ya Mashariki).

Ni miongoni mwa wanawake ambao hawakuwa na umri mkubwa lakini walikuwa na mafanikio makubwa, mafanikio yake yalikuja kutokana na nidhamu yake kwenye kazi ambayo alikuwa anaifanya jambo ambalo lilimsaidia kufika mbali lakini pia aliitumia chapa yake aliyo itengeneza kuweza kutengeneza na kukuza bidhaa zake za vipodozi ambazo zilikuwa zinapendwa kila kona na wadada wengi wa mjini ambao walikuwa wanahitaji kwenda na kasi ya maendeleo ya utandawazi. Zyra hakuwa mwanamke ambaye alipenda kuyaweka maisha yake binafsi kwenye mitandao wala kwenye jamii, alipenda maisha hayo kuwa binafsi baina yake mwenyewe na hao ambao walikuwa wanamhusu kwenye hayo maisha.

Jambo hilo ndilo lilifanya iwe vigumu yeye kutabirika au kujulikana nje ya kazi yake ya umiss ambapo watu walikuwa wakihangaika na kutamani kuweza kulijua hilo lakini haikuwezekana. Hayo maisha yake binafsi ndipo siri kubwa ya mafanikio yake ilipokuwa kwa sababu usiri wake ndio ambao ulifanya maadui zake na wale watu ambao walikuwa wakitamani kushindana naye wasijue ni sehemu gani walitakiwa kumbana ili waweze kumdondosha na kumshinda. Ilikuwa ni zaidi ya miaka mitatu imepita tangu aingie kwenye penzi ambalo lilikuwa limekusudiwa kuwa ndoa, penzi ambalo lilifikia sehemu likaaminiwa kwa ukubwa baina ya hao wawili ambao waliamua kulikubali kwa pamoja.

Oliver Jefferson ndilo lilikuwa jina la mwanaume ambaye yeye alikuwa anapendana naye, mwanaume ambaye alikuwa bado kijana shupavu lakini alipata bahati ya kuwa karibu na mkubwa wa nchi. Alikutana na bwana huyo mwaka mmoja tu baada ya raisi kuchaguliwa wakati ndo ikiwa mwaka wake wa kwanza kuweza kushiriki kwenye mashindano ya umiss. Mrembo huyo na wenzake walikuwa wamealikwa Ikulu na mheshimiwa siku hiyo ambapo sherehe ilichelewa kuisha na mheshimiwa raisi alimtaka mlinzi wake ahakikishe wanawake hao wote wanafika makwao salama kabisa na ndio ulikuwa mwanzo wa wawili hao kufahamiana ambapo matokeo yake ni kwamba walizama kwenye huba zito.

Safari yao ambayo ilianzia pasipo julikana iliishia sehemu ya wawili hao kuaminiana isivyo kawaida na hata yale mafanikio yote ambayo aliyapata Zyra yalifanywa na bwana Oliver ambaye aliamua kujitoa kwa mwanamke huyo kwa kumkutanisha na watu wakubwa ambao ndio waliirahisisha safari yake ambayo huenda asingeweza kuifikia akiwa mwenyewe naye hakufanya ajizi, aliitumia vizuri nafasi hiyo ya kuwa karibu na mlinzi mkuu wa raisi. Safari ilikuwa nzuri na yenye mfano bora mpaka pale ambapo yalitokea matatizo baada ya raisi kufa ndipo tatizo lilipokuwa limeanzia ikiwa ni siku kadhaa tu zimepita na siku hiyo Jessica aliamua kumtembea mrembo huyo kwa sababu alijua ndiyo ilikuwa sehemu pekee ya kuweza kuyapata majibu yake ambayo aliyakosa kwa sababu hiyo ingekuwa safari ya kumpata yule binti ambayo alimpoteza Luana.


Jessica baada ya kufuatilia kwa muda mrefu aligundua kwamba mwanamke huyo siku hiyo alikuwa kwenye moja ya makasino ya bei ghali hivyo ikamlazimu kumsubiri kwani hakutaka kumkurupukia na kumkosa kwa sababu kwake ilikuwa ni mhimu ampate usiku huo. alikuwa amesimama sehemu ya watu kuingilia akipata kinywaji huku akiwa ameegamia nguzo moja akijifanya kuwaangalia watu ambao walikuwa wanatafuta fursa kwenye kamari. Akiwa hapo alikaa kwa muda wa saa zima ndipo akaona mrembo huyo anatoka nje akiwa ana furaha tele lakini kwa nyuma yake kulikuwa na wanaume wanne ambapo mmoja alikuwa amemshikilia kiuno na wale wengine watatu walikuwa nyuma yake wakionekana kabisa kwamba walikuwa ni walinzi. Watu wale walikuwa wanatembea kwa furaha na ni wazi kwamba walikuwa ni watu ambao walijuana kwa muda mrefu jambo ambalo Jessica lilimshangaza kidogo kwani kulikuwa na sintofahamu ya uwepo wa mpenzi wake wa muda mrefu lakini mwenzake alikuwa anafurahia maisha? Kuna roho ilimtaka kuwa mpole kwani alihisi huenda bwana yule alikuwa salama, lakini huyu ambaye alikuwa naye alikuwa nani? Alipotezea kwani hakuona kama inamhusu sana.

Alitoka haraka nyuma yao na kukimbilia upande wa pili kuona tukio ambalo watu hao walikuwa wanaenda kulifanya, walizunguka mpaka sehemu ya nyuma ambako kulikuwa na gari ya kifahari imepaki hapo, walinzi walibaki umbali kadhaa na kugeuka, yule mwanaume alipo ikaribia gari ile alimuinamisha Zyra na kuifunua sketi yake ambapo ndani hakuvaa kitu chochote akaanza kufanya naye mapenzi huku wote wakifurahia hali hiyo na baada ya dakika tano walimaliza. Walinyonyana ndimi zao na mwanaume huyo akamtaka mrembo huyo aingie kwenye gari kisha mlinzi mmoja akaja na kuliwasha gari hilo akaondoka nalo taratibu.

Jessica alibaki ameduwaa kwa muda mpaka alipo ona ile gari inatoka nje kabisa ya eneo lile ndipo akashtuka. Kwa heshima ambayo alikuwa amejitengenezea Zyra kwenye jamii hata siku moja hakutarajia kwamba anaweza akamkuta akiwa anafanya tukio la namna ile ila aliamua kupotezea kwa kuhisi kwamba huenda ndiyo sababu kubwa ambayo ilimfanya mwanamke yule kuamua kutoyaweka maisha yake binafsi bayana na hadharani kwa kila mtu.
Aliingia kwenye gari yake na kuanza kuifuatilia ile gari ili ajue mahali ambako walikuwa wanaelekea majira yale. Jiji lilikuwa limetulia, usiku ulikuwa unazidi kuwa mzito na kila mtu alikuwa anapambana na hali yake kuhakikisha anamalizana na malengo yake ya siku hiyo kabla ya kuianza siku nyingine. Ile gari ilienda kusimama nje ya jumba moja safi ambalo lilikuwa la ghorofa moja, lilikuwa limepambwa vya kutosha na lilipendeza bila shaka bibie alikuwa anaishi maisha ya ndoto za wanawake wengi mjini. Alisimama umbali mrefu akiwa ameizima gari yake kabisa kusubiri kile ambacho kingefuata baada ya pale. Zilipita dakika tano tu ile gari ikatoka mle ndani na kutoka nje na wakati gari inatoka aliona kuna mlinzi mmoja alitoka nayo kisha akarudi ndani.

Ni jambo ambalo lilimfariji zaidi kwa sababu yule mlinzi alikuwa ametokea kwenye kampuni moja ya ulinzi ambayo aliamini haiwezi kuzalisha watu wa hatari hata kidogo, maana yake bibie alikuwa analindwa na watu wa kawaida tu ambao hakutakiwa hata kuwaua. Alivaa gloves kwenye mikono yake na kusogelea kwenye lile geti, aligonga taratibu akatoka yule bwana kwa mara nyingine. Alihitaji kuuliza jina la yule mwanamke ila aligushwa kwenye shingo yake akaenda chini, baada ya kuhakikisha amekamilisha hilo alirukia ndani kwa sarakasi ambapo alikutana na mlinzi mwingine ambaye alikuwa anasogea ili kuweza kuuliza juu ya hali ambayo ilikuwepo hapo ila naye hakuwa na bahati nzuri. Muda ambao aliutumia kutambua kwamba kulikuwa na adui ndani ya hilo eneo ni wakati ambao alikutana na ngumi ya shingo akadondoka na kupoteza fahamu.

Jessica alitambua kwamba eneo hilo lilikuwa na walinzi wawili tu pekee hivyo alikuwa amewamaliza. Aliangalia kwenye jumba hilo kwa umakini na kutambua kwamba usalama ulikuwa ni wa kutosha, sasa taratibu alielekea mlangoni kwani ulikuwa ni wakati wa kuweza kuongea na mwenyeji wake ambaye ndiye alimpeleka hilo eneo. Wakati anafika mlangoni alikigusa kitasa na kugundua kwamba kipo wazi, huenda ni kwa sababu ya uharaka wa mwenyeji au alikuwa anajiamini kwa sababu ana ulinzi ndiyo maana hakuwa makini. Baada ya kufungua alikutana na sebule kubwa ambayo ilikuwa imesheheni vitu vya bei ghali lakini hapakuwa na mtu, aliangaza kila sehemu ndipo akasikia sauti ya maji upande wa juu akagundua kwamba mwenyeji wake alikuwa kuoga.

18 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 19.
ENDELEA.......

Ilikuwa lazima aoge kwa sababu muda mfupi ambao ulipita alitoka kufanya mapenzi ya hovyo hivyo hakuwa na haraka, alisogea kwenye sofa moja na kuiweka bastola yake mezani kisha akaketi na kuendelea kuangalia runinga ambayo ilikuwa imewashwa mbele yake. Ilipita nusu saa akiwa ameketi bila hata wasiwasi ndipo alisikia hatua za mtu akitoa juu kushuka hapo alipokuwepo. Zyra mwenyewe akiwa amevalia nguo za ndani tu alikuwa akishuka huku akiwa anaimba kwa furaha huenda kwa sababu hakujua kama ndani mwake kulikuwa na mgeni mwingine ambaye yeye hakumualika. Alishtuka almanusura adondoke baada ya kumuona mwanamke huyo wakati huo alikuwa amebakisha ngazi kadhaa tu kufika hapo chini.

“Zyra, nimefurahi kuonana na wewe” mgeni wake alimpokea kwa tabasamu zuri kwenye uso wake.
“Wewe ni nani na umeingiaje hapa?”
“Naomba ukae kwa sababu mimi na wewe tuna mazungumzo marefu kidogo usiku huu na hata usifikirie kuhusu walinzi wako kwa sababu mpaka waje waamke sio leo” alimeza mate kwa shida na kuhitaji kukimbia lakini wakati anafikiria kufanya hivyo Jessica alilitambua hilo hivyo aliigusa ile bastola kwa mkono wake na kumtaka binti huyo akae kisha akaiachia tena bastola hiyo.

“Bila shaka mimi na wewe hatufahamiani kabisa kwa sababu hatujawahi kukutana kabla, haujawahi kuniona hata kwa bahati mbaya ila mimi nakujua. Nimekujua kwa miaka mingi ila umakini kwako haujaanza kwa muda mrefu kwa sababu ambazo sitaki kuziweka wazi kwako, unisamehe kwa njia ambayo nimeitumia kuingia kwako kwa sababu ndiyo ilikuwa njia pekee ya mimi na wewe kuweza kukutana na kuongea kwa utulivu kama hivi” alitulia na kumeza mate taratibu wakati ambao Zyra alikuwa akitetemeka vibaya.
“Unahitaji nini kwangu?”
“Upo kwenye mahusiano siriasi Zyra?” ni swali ambalo hakulitegemea kuulizwa tena na mtu ambaye hata hamjui
“Umesema?”
“Umenisikia vizuri ila nahisi unajishauri namna ya kunijibu uongo”
“Ni kwa sababu hayo ni maisha yangu binafsi ambayo huwa sipendi kuyaweka bayana kwa watu au kwenye mitandao”
“Ndiyo maana unajiuza?”

“Umekuja hapa kwangu kunitusi si ndiyo? Mimi ni mwanamke mashuhuri ukanda wote wa Afrika ya Mashariki unahisi naweza kuwa rahisi namna hiyo?”
“Unaweza ukanipa sababu ya wewe kufanya mapenzi hovyo hovyo kila sehemu mpaka nje ya gari?”
“Naomba uondoke nyumbani kwangu kwa sababu maisha yangu hayakuhusu”
“Kwa sasa yananihusu ndiyo maana nipo hapa. Sikiliza binti mimi sijali wewe unafanya mapenzi wapi, unalala na nani, unawavulia nguo zako wanaume wangapi kwa sababu kwa binti kama wewe najua kabisa haujafika hiyo sehemu kwa bahati mbaya, ni wanaume wengi sana mbao umewavulia nguo zako ili wakufikishe hapo ulipo na mimi siwezi kukulaumu kwa sababu kuna wakati inabidi ufanye lolote ili uweze kuyashinda mazingira magumu”

“Kama ni hivyo unataka nini kwangu?”
“Yule kijana ambaye ulikuwa naye kasino mkaishia kufanya mapenzi kwenye ile gari ni nani?”
“Siwezi kukujibu lolote”
“Nina video yenu mkiwa mnafanya mapenzi pale, ukitoa mimi kukuua naweza kuivujisha ukaanza kuwa maarufu na kupoteza sehemu kubwa ya maisha yako na unawajua vizuri watanzania wanavyopenda vitu vya kipuuzi”
“Nina uhakika hauna shida na huyo mtu ambaye mimi nimefanya naye mapenzi, nambie moja kwa moja unahitaji nini?”

“Napenda watu ambao wana upeo mkubwa kama wako. Unajua mara ya kwanza wakati nasoma visa vya mapenzi hapa duniani niliamini kwamba mapenzi ya kweli yapo na huenda kweli yapo ila sina uhakika. Kama haya mapenzi yapo kweli ila yameharibiwa basi sehemu kubwa sisi wanawake ndio ambao tunatakiwa kupokea lawama kubwa. Leo nimeshangazwa na wewe kuendelea kuburudika huku ukionekana kuwa mtu mwenye furaha kubwa wakati upo kwenye matatizo mazito!” aliuliza swali la mshangao akiwa anamwangalia bibie Zyra ambaye alikuwa amejikunyata akiwa anaitazama kwa umakini bastola ambayo ilikuwa mezani, Jessica aliendelea.

“Miaka mitatu na zaidi ambayo imepita wewe kwa mara ya kwanza ulikutana na mwanaume ambaye mlikuwa na mengi ya kuweza kuyafanya pamoja. Mwanaume huyo aliamua kujitoa kwako kwa kila kitu kiasi kwamba ni yeye ambaye amekufanya wewe kuwa hapo ulipo mpaka sasa ila inanishangaza kwamba umemsahau mapema namna hii?”
“Unamaanisha nani? Mimi sijawahi kuwa kwenye mapenzi na mtu yeyote yule”
“Unanifahamu mimi Zyra?”
“Hapana”
“Unahisi hizi taarifa zako nimezipata wapi?”
“Sijui”
“Vizuri, sasa mimi hii ndiyo kazi yangu kupata taarifa ambazo watu wengine hawana uwezo wa kuzipata kirahisi. Unajua sababu ambayo imemfanya raisi kuuawa?”
“Hapana, sijui kama raisi kauawa kwa sababu imetangazwa kwamba amekufa kwa kuumwa”

“Wewe unaamini hilo?”
“Naamini kwa sababu kila siku ni hao ambao wanatupatia hizo taarifa”
“Basi ndiyo maana mimi nipo hapa ili mimi na wewe tuweze kuzungumzia kuhusu kifo cha mheshimiwa raisi” Zyra alishtuka kiasi kwamba alijikuta anaanza kutetemeka wakati ni yeye alitoka kuoga kupunguza jasho la mwili.
“Mimi nahusika vipi na raisi kufa?”
“Ndo nataka kujua wewe unahusika vipi”
“Mimi ni mtu wa kawaida sana kwanini unahisi naweza kuwa nahusika kwenye hilo?”
“Matukio makubwa duniani ambayo yameushangaza ulimwengu wala hayakufanywa na watu wa ajabu bali yalifanywa na watu wa kawaida tu ambao hakuna mtu alikuwa anaweza kuwadhania, wewe unaweza kujiona kwamba ulikuwa mtu wa kawaida lakini ulikuwa na umuhimu wako mkubwa na huenda bila wewe haya yasingewezekana kufanyika”

“Unamaanisha bila mimi raisi asingekufa?”
“Ndiyo maana yake Zayra”
“Nadhani umechanganyikiwa wewe mwanamke”
“Sio muda tutaenda kujua kati yangu mimi na wewe nani amechanganyikiwa. Ila unaweza ukalizuia hili kwa kuniambia ukweli”
“Ukweli gani wakati mimi sijui lolote?”
“Unaweza ukaniambia ni wapi Oliver alipo”
“Whaaaaat?”
“Nilijua utaigiza hilo na kujifanya hujui, umekuwa ukiwahadaa watu kwa miaka zaidi ya mitatu sasa kwa kutotaka mambo yako binafsi kujulikana kwa sababu ulikuwa kwenye mahaba mazito na mlinzi mkuu wa raisi, vipi unataka kugoma?” Zyra alihisi ubaridi unamgusa mpaka kwenye moyo wake, lilikuwa jambo la siri kubwa mno lakini hakujua kama kuna wanadamu walikuwa na hizo taarifa.
“Hata sijui unaongelea nini”

“Ni kweli haujui naongelea nini kwa sababu haukuwahi kuhisi kwamba kuna mtu anaweza kutambua kwamba mpo kwenye mahusiano hivyo sikushangai kwa hili” Jessica wakati huo alitoa picha moja kwenye mfuko wake na kumrushia Zyra, ilikuwa ni yeye na huyo mwanaume ambaye aligoma kabisa kuhusu kwamba hakuelewa ambacho kilikuwa kinaongelewa. Mwanaume alikuwa amevaa pensi fupi akiwa kifua wazi na mrembo huyo alikuwa amevaa bikini wakiwa kwenye bwawa la kuogolea sehemu ambayo ilikuwa tulivu na walionekana kabisa kuzama kwenye mahaba mazito isivyo mfano.
“Umekuwa ukiyafuatilia sana maisha yangu?”
“Mpaka pale ambapo niliona yana umuhimu! Yes”
“Kwanini?”

“Unahisi ni jambo dogo kuwa kwenye mahusiano na mlinzi mkuu wa raisi? Au hilo jambo kwako unaona kama ni maigizo sio? Ukizingatia kwamba raisi amekufa tayari na huyo mlinzi wake hajulikani mahali alipo, unahisi hili linaweza kuwa igizo au jambo la kulipotezea kama sikukuu ya kuzaliwa ya mtu sio?”

19 inatifa tamati

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 20.
ENDELEA.......

“Sijui lolote na wala sitambui ni wapi alipo huyo mtu”
“Lakini mwanzo umekataa kabisa kwa kudai huelewi ninalo lizungumzia hivyo ulikuwa na maana kwamba haumjui Oliver, sasa inakuaje kwa sasa unasema haujui alipo?”
“Ni kweli alikuwa mpenzi wangu ila tuliachana”
“Mhhhhh mliachana kwa muda gani?”
“Zaidi ya miezi miwili ambayo imepita” Jessica alitabasamu kwa sababu mwanamke huyo alikuwa anadanganya kwani miezi miwili iliyopita ndipo kwa mara ya kwanza alipewa kazi ya kumtafuta yule binti ili amlinde na ndio wakati ambao alianza kuyafuatilia kwa ukaribu maisha na mapenzi ya hao watu wawili na hata ile picha ambayo alimuonyesha Zyra ilipigwa ndani ya huo muda ila huenda binti huyo hakuwa mzuri kwenye kudanganya ama alijisahau kwa sababu ya kuwa na presha kwenye nafsi yake.

“Kwa sababu zipi?”
“Basi niliona ni mtu ambaye hana muda na mimi kwa sababu kila mara alikuwa anawaza kazi tu, muda wote ilikuwa ni kazi na yeye, yeye na kazi”
“Ni kweli hiyo ndiyo sababu ambayo inaweza kukufanya wewe ukamkimbia mwanaume ambaye amekupambania kuanzia huna lolote la maana zaidi ya uzuri wako halafu akakufikisha hapo ulipo?”
“Ndiyo, mapenzi ni maamuzi tu. Niliona ni muda wangu wa kufanya mambo mengine kwahiyo sikutaka tena kufuatilia habari zake” Jessica alicheka sana akiwa anaangalia namna binti huyo alivyokuwa mpumbavu kwani alikuwa anashindwa hata kuitengeneza stori yake vizuri.
“Na unaamini kwamba mimi nitaamini hilo?”
“Mimi sijali wewe unaamini nini, najali moyo wangu unataka nini”

“Yeah, jambo ambalo ni zuri kwako. Nisikilize binti, kuna wanawake warembo zaidi yako ambao wewe ukiwekwa nao ni mpuuzi mmoja tu na huenda hata mimi hapa nikisema nijipodoe kama wewe haugusi hata nusu yangu kwa lolote lile lakini unahisi kwanini wewe umefanikiwa kuwa maarufu sana? Unahisi ni kwa sababu ya uzuri? Bahati? Hapana sio kweli kama ni bahati basi sio kupata hiyo nafasi bali ni wewe kukutana na Oliver. Kuna wadada wengi ambao majina yao yalikatwa na walistahili kuwa hapo ulipo ila wewe ukapewa nafasi kwa sababu bwana ako alikuwa anakula na wakubwa na alikuwa akikupitisha muda mwingine bila hata kukwambia, hivyo wewe sio lolote bila yeye maana yake kama ni hivyo haukuwa na huo ubavu wa kuweza kumkimbia kirahisi namna hiyo labda kama kuna stori tofauti ambayo hautaki kuileta kwangu”

“Hakuna jambo mimi nakuficha, kama ningekuwa najua alipo basi ningekwambia mapema”
“Unaonaje kama ukikamatwa kwa sababu ya kuhusika na mauaji ya raisi?”
“Hilo ni jambo ambalo linafanya kila mtu akuone hauna akili. Umkamate mtu kama mimi tena mwanamke na umpe kesi ya mauaji kwa mkuu wa nchi! Unahisi kuna mtu atakuona una akili timamu?”
“Inaweza kuwa hivyo mpaka pale ambapo wau watatambua kwamba ulikuwa kwenye penzi zito na mlinzi wa raisi, vipi kama wote wawili mlihusika kwenye kutengeneza mtego wa kumuua raisi? Bado watu wataniona sina akili?”
“Wewe mwanamke ni shetani, unataka kuniingiza kwenye jambo ambalo hata sijui linafanyikaje”

“Ndiyo maana nipo hapa kuzuia hilo, nataka kujua ni wapi bwana ako alipo mpaka sasa”
“Mimi sijui”
“Sawa” Jessica aliinyanyua ile bastola na kuielekezea kwa yule mwanamke kisha akaikoki ikiwa imenyooka, Zyra ule ujasiri ulimtoka mpaka akajikojolea.
“Niliamua kuongea na wewe kistaarabu ila naona umeanza kuniletea mazoea ukijua mimi ni mwenzako. Usingekuwa na furaha namna ile kama mwanaume ambaye unampenda yupo kwenye matatizo makubwa hivyo nataka kujua Oliver yupo hai au amekufa?” Zyra alimeza mate mpaka akaanza kubabaika.
“Mimi sijui kama atakuwa hai au umekuf….” ilipita risasi moja karibu yake na kwenda kutoboa ukuta na ndipo hapo aligundua kwamba huyo mwanamke hakuwa yule ambaye yeye alikuwa anafanya naye mazungumzo kimasiara hapo.

“Ina maana unajua kwamba alikuwa kwenye hatari?”
“Ndiyo, ndiyo”
“Kwahiyo ulitaka afe?”
“Hapana hapana”
“Sasa inakuaje mwanaume ambaye mlikuwa mkipendana sana yupo kwenye hatari halafu wewe upo kwenye furaha?”
“Kwa sababu nafanya haya ili niishi”
“Ukiwa na maana ipi?”
“Oliver alitakiwa kuuawa”

“Najua hilo, ila nataka kutambua uhusika wako kwenye hili jambo na kwanini ulikuwa unajua na haukufanya jitihada zozote za kumuokoa?”
“Kama ningefanya hivyo ningekufa mimi na yeye mwenyewe bado angekufa tu”
“Una maanisha nini?”
“Mimi nilikuwa najua kwamba raisi anatakiwa kufa muda mrefu sana”
“Whaaaaaat?”
“Umetaka ukweli na huo ndio ukweli, mimi nilijua kwamba raisi lazima afe ila sijamuua mimi”
“Kujua tu njama za raisi kuuawa na hakuna jambo umefanya hilo tayari ni kosa la mauaji kwa sababu unatakiwa kunyongwa hadi kufa tena hadharani”
“lakini hauwezi kufanya hivyo”
“Kwa sababu gani?”
“Mimi sijui unataka nikwambie nini”
“Niambie yote ambayo unayajua”
“Mimi ni mtu wa mbali sana hivyo siwezi kuwa na taarifa za ndani hizo”

“Kujua taarifa za siri kwamba raisi anaenda kufa inakinzana na kauli yako hivyo wewe ni mtu wa ndani kwa sababu hizo taarifa hata vyombo vya usalama havikuwa nazo”
“Kama nikikwambia ukweli wataniua, mimi bado nahitaji kuishi”
“Ina maana wewe ulihusika kwenye hili moja kwa moja si ndiyo?”
“Ndiyo ila nililazimishwa, tafadhali naomba usiniue”
“Hilo nilihisi ingekuwa hivyo, jambo moja ambalo nahitaji kutoka kwako ni uhusika wako kwenye hili na uniambie kwamba ni nani alikutuma kuweza kulifanya hili?”

“Wewe ni mwanamke mwenzangu tafadhali usinifanyie hivi, nimeamua kuishi maisha yangu ya umaarufu na mafanikio yangu tafadhali hili lipo nje ya uwezo wangu”
“Ndiyo maana nahitaji taarifa hizi ili niweze kukuacha hai”
“Niahidi kama hili jambo litaishia hapa hapa baina yetu wawili” msisitizo wa Zayra ulianza kumpatia mwanga Jessica
“Ooh! Hayakuwahi kuwa mapenzi ya kweli si ndiyo bali ni kazi ambayo ulikuwa umepewa?”
“Ndiyo, tangu mwanzo mimi sikuwahi kumpenda Oliver bali ni kwa sababu ya kazi ambayo nilipewa. Nilikuja kumpenda baadae ila nilikuwa nimechelewa kuweza kurudisha nyuma kila jambo ambalo lilitokea”
“Alikuwa anajua juu ya hili?”
“Hapana, hata kama alikuja kujua basi ni wakati ambao alikuwa kwenye matatizo”
“Unamaanisha nini?”
“Mapaka sasa Oliver hawezi kupona, hata kama amefanikikiwa kuwakimbia hawa watu basi ni suala la muda tu kabla hajaweza kufa”
“Una uhakika gani na jambo hilo?”
“Kwa sababu ni mimi ambaye nimpatia sumu mara ya mwisho tulipo kutana”
“Whaaaaaaaaaaaat are you talking about?”

“Mimi nilijua kabisa kwamba raisi angekufa kama nilivyo kwambia, Oliver alikuwa mpenzi wangu ambaye kila wakati ambapo hakuwa sawa alikuwa anakuja kwangu kupata utulivu wa akili hivyo nilikuwa napata mambo mengi ya Ikulu kuliko mtu yeyote yule, kwa maana hiyo nilikuwa najua hatua zake zote”
20 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 21.
ENDELEA.......

“Wakati unapewa hii kazi uliambiwa kwamba unatakiwa kumuua yeye?”
“Mwanzoni haikuwa hivyo, ilikuwa ni raisi tu pekee na yeye kama kungekuwa na mkanganyiko basi alitakiwa kuuziwa kesi”
“Sasa kilibadilika kitu gani mpaka ukahitaji kumuua yeye?”
“Kwa sababu alionekana kuwa mtu hatari zaidi kwa upande wa hawa watu, watu wote ambao wameonekana kuwa tishio mpaka sasa wameuawa isipokuwa yeye pekee mpaka sasa ndiye hajulikani alipo japo najua hawezi kupona”

“Unamaanisha kuanzia vifo vya Tunduma, Askofu, jaji mkuu wote walikuwa kwenye huu mpango kwa sababu ni hatari kwenu?”
“Hao wengine ni kweli lakini jaji mkuu ameuliwa kwa sababu ya kubebeshwa kesi ambayo haikuwa ikimhusu hivyo naweza kusema kwamba yeye hakuwa sehemu ya mpango ila amekuja kuwa sehemu ya mpango baada ya mambo kuharibika”
“Bado sijakuelewa”
“Hauwezi kunielewa kirahisi namna hii ndiyo maana nilikutaka uachane na haya mambo kwa sababu lazima utakufa”

“Ni nani ambaye alikuwa nyuma ya jambo hili lote mpaka linakuja kutokea?”
“Hata mimi simjui”
“Bibie usione kama nipo hapa kwa ajili ya kufurahishana na wewe”
“Nalitambua hilo ndiyo maana nimeamua kukupa taarifa za mambo kadhaa ambayo nayajua, taarifa ambazo hata mimi zinaweza kuondoka na maisha yangu”
“Tuanze na hayo mauaji ya askofu, ni nani ambaye yupo nyuma ya hili jambo?”

“Kama nilivyokwambia kwamba sijui, ila jambo ambalo nalitambua ni kwamba askofu alikuwa sehemu ya watu wa siri wa raisi ambaye amekufa na inadaiwa kwamba kwenye siku zake za mwisho yeye na Oliver walikutana kwa siri na Askofu ambapo kuna mambo mazito yalijadiliwa huko”
“Unajua ni mambo gani yalikuwa yanaendelea baina ya hao watu?”
“Hapana”
“Sasa unajua nini mpuuzi wewe?”
“Kwa sasa najua kwamba watu ambao wapo hai ni wawili, Oliver na mmoja ambaye simjui jina”
“Samahani umesema wawili?”
“Ndiyo kuna binti ambaye naye alikuwa anatafutwa kwa muda mrefu ila sijajua anapatikana wapi”

“Umesema binti?”
“Ndiyo”
“Ni nani huyo binti?”
“Ni mtoto wa nje wa raisi ambaye amefia madarakani”
“No, no, no, nooooooooooooooooo!” Jessica alipiga makelele ambayo kwa wakati huo yasingemsaidia lolote japo alijihisi kama mwili unawaka moto.
“kwani unamjua huyo binti mbona umeshtuka sana?”
“Una taarifa zipi kuhusu huyo binti?”

“Nilisikia kwamba alikuwa anasoma ndani ya chuo cha Mwal. Nyerere hivyo walituma watu kwenda kumtafuta huko na mpaka sasa sijajua watakuwa wameishia wapi na hili zoezi” aliishiwa nguvu Jessica, wakati huo ndipo alipata majibu juu ya binti ambaye alikuwa anapaswa kumlinda. Alikuwa ni mtoto wa damu kabisa wa raisi ndiyo maana mzee yule aliwahi kumwambia kwamba huyo mtoto maisha yake ni mhimu kuliko hata yako wewe, aliduwaa lakini muda ulimsaliti, tayari alikuwa amempoteza binti huyo kwenye mikono ya hao watu. Alitakiwa kufanya nini tena mwali huyo? Aliinua macho yake ambayo yalikuwa mekundu akiwa anamwangalia Zyra kwa macho ya kufuga kisasi.

“Nataka uniambie kila kitu, anzia mwanzo kabisa wa haya mambo mpaka yalipo fikia hivi sasa” bastola ilikuwa imelenga kwenye goti la Zyra wakati anatamkiwa hiyo sentensi, uamuzi ulikuwa ni wake kuweza kutoa siri zote ambazo alikuwa anazijua kwa miaka au aanze kupunguzwa baadhi ya viungo vya mhimu kwenye mwili wake.





MSIBA WA RAISI PHILIP
Yalikuwa ni mazishi ya raisi ambaye alifia madarakani Philip, msiba wake ulikuwa unafanyika nyumbani kwake Mbezi Beach ambako ndiko alizaliwa pia. Msiba huo ulikuwa unaongozwa na raisi ambaye alikuwa ameapishwa kwa wakati huo Darian Julius.
Msiba ulikuwa una watu wengi mno, watu wengi walihudhuria kwa sababu raisi huyo alikuwa ni mtu mwema, alikuwa ni raisi ambaye alikuwa akipendwa na kila mtu kutokana na yale ambayo aliyafanya kipindi yupo marakani na kwenye uhai wake kwa ujumla. Raisi ambaye alidaiwa kuwa ndiye yule aliye ahidiwa kwa ajili ya kuweza kulikomboa taifa lakini ni kama wasemavyo wahenga kwamba chema huwa hakidumu siku zote.

Msiba wake ulifana kwa kuhudhuriwa na viongozi wengi wakubwa duniani na hata wale ambao walishindwa kuweza kufika basi walituma wawakilishi wao kuonyesha heshima kwa kiongozi huyo ambaye kufa kwake ni kama kulizima matarajio makubwa na ndoto za kila mtu kufika kwenye nchi ya ahadi. Msiba ulihudhuriwa na watu wengi kiasi kwamba hata eneo lilionekana kuwa dogo wakati ni eneo ambalo lilikuwa na ukubwa wa kutosha. Msiba huo ulihamishiwa kwenye eneo moja ambalo lililikuwa na eneo kubwa, eneo ambalo lilikuwa limenunuliwa na raisi huyo enzi za uhai wake na mara nyingi alikuwa anapenda kwenda huko pale ambapo angehitaji kufanya maamuzi magumu juu ya taifa.

Eneo hilo liliandaliwa vizuri kabisa, sio kila mtu alikuwa ameruhusiwa kumuaga kutokana na aina ya kifo ambacho alikufa. Serikali ilitoa taarifa kwamba kutokana na aina ya tatizo ambalo lilimpata haikuwa vyema kuanza kuutembeza mwili wake au kuruhusu kila mtu auone huo mwili hivyo ilitumika busara hiyo kwamba angeagwa na watu wachache huku wengi wakionyeshwa kwenye runinga ambapo walikuwa wanapata nafasi ya kuweza kumuaga moja kwa moja na utaratibu ulikuwa hivyo mpaka pale ambapo angerudishwa nyumbani kwake kwenda kuzikwa kwa sababu enzi za uhai wake moja ya sehemu ya usia wake ni kwamba alitakiwa kuzikwa kwenye ile nyumba yake ambayo alikuwa anaishi kwani ndiyo sehemu ambayo alikuwa amemzika baba yake na mama yake hivyo alihitaji kuwa karibu na wazazi wake pindi akipumzika.

Viongozi kadhaa walipewa nafasi ya kuweza kuongea lakini mhimu zaidi ni kwamba raisi ambaye alikuwa madarakani alipewa muda wa kutosha zaidi wa kuweza kuongea kwa sababu alitakiwa pia kulihutubia taifa kwa mara nyingine na kutoa mwelekeo wake kwa wakati huo hususani baada ya mwenzake kuweza kupoteza maisha kwani mzigo wote ulikuwa kwenye mgongo wake na hotuba yake ilikuwa kama ifuatavyo.
“Watanzania wenzangu, nawasalimia kwa jina na bendera ya taifa letu, nawasalimu kwa amani, umoja na mshikamano wa hili taifa pendwa na teule la Mungu. Taifa ambalo tangu lipate uhuru limekuwa na nuru ya amani na umoja ambao kila mtu duniani anatamani kuupata lakini haiwezekani kwa sababu hizi baraka hazipo kwa ajili ya kila mmoja, ni baraka ambazo ni mataifa kadhaa ndiyo yamebahatika kuzipata.

Najua kwamba kwa sasa taifa letu lipo kwenye nyakati za giza, nyakati ambazo hakuna mtu alizitarajia au hata kutamani kuzipitia lakini tangu lini sisi wanadamu tukawa na uwezo wa kupinga alipangalo MUNGU? Yeye ndiye mtoaji wa uhai, yeye ndiye mtoaji wa hii pumzi ambayo hatuilipii zaidi ya kuifaidi bure kabisa hivyo ni yeye mwenye uamuzi wa kuibeba pale anapo ona anamhitaji kondoo wake. Nyakati hizi za giza kwetu kama taifa zinakuja kwa sababu ya kumpoteza shujaa wa taifa hili, shujaa ambaye maisha yake imekuwa kama zawadi kubwa kwetu, zawadi ambayo tunatakiwa kuienzi mpaka pale ambapo pumzi yetu itakapofika mwisho.
Ni mtu ambaye alikuwa na maono ya mbali, mwanadamu ambaye alithubutu na kuhitaji kuibadili nadharia ya taifa hili kutoka kwenye umaskini uliokithiri na kulipeleka mahali ambapo dunia ingeanza kutambua kwamba sisi hatutakiwi kuwa nyuma, sisi tunatakiwa kula nao kwenye meza moja hao ambao wanajiona kuwa wakubwa wa dunia. Tanzania imepaa kwenye anga za kimataifa kwa ajili yake, Tanzania imekuwa mfano mzuri wa mataifa yanayo kimbia kwa kasi kwenye uchumi kwa sababu ya akili yke halafu wakati akiwa anaendekea kuyatimiza haya ndipo umauti ukaja kumtokea na kufanya ndoto hizo kuzima kama mshumaa lakini sitaruhusu hilo liweze kutokea.

Nakumbuka siku mbili kabla ya yeye kupoteza uhai aliniita akiwa kitandani kukamilisha siku zake za hapa duniani. Alipo niona alitabasamu kwa furaha kubwa jambo ambalo lilinishangaza kwani madaktari walikuwa wamenipa habari ambayo ilikuwa mbaya kwenye masikio yangu. Madaktari walidai kwamba mheshimiwa asingeweza kupona kwa namna yoyote ile bali alikuwa amebakiwa na masaa kadhaa ya kuweza kuendelea kuivuta pumzi hii ya dunia kwahiyo tulitakiwa kuyatumia vizuri masaa hayo kumpatia kila ambacho anakipenda. Hali ile ndiyo ilinifanya wakati namwangalia pale kitandani kwake akiwa anatabasamu nitoe machozi, ilinitisha kuona mtu ambaye alijua kabisa kwamba alikuwa na masaa kadhaa ya kuishi ana furaha kubwa kunishinda mimi ambaye sijui kama nitaishi miaka mingapi huko mbele.

21 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 22.
ENDELEA.......
Aliniita na kunitaka nisogee pale alipo baada ya kuniona nina hofu kubwa ndani yangu, alinyanyuka kwa taabu na kuhitaji nimsikilize kwa umakini.
“Darian unahisi kwanini watu huwa wanalia mtu anapokufa?”
“Kwa sababu huwa wanawaza kwamba hawatamuona tena wala kuongea naye tena mheshimiwa”
“Sio kweli Darian, watu huwa wanalia kwa sababu wanaamini ni njia sahihi ya kumuaga mtu ambaye wanampenda ama kuyawazia majukumu yake ambayo alikuwa anayafanya kwamba je wataweza bila yeye? Mtu akiwaza hayo mambo ndipo hujikuta na presha mwisho wa siku anaanza kuumia na kujikuta anamwaga chozi ndiyo maana siku kadhaa tu kama wakipata mtu wa kutimiza hayo mambo ambayo nimekwambia huwa wanamsahau haraka sana marehemu hata kama alikuwa bora sana kwao jambo ambalo linabaki ni kama aliacha kumbukumbu bora duniani ndizo ambazo zitawafanya waendelee kumkumbuka.

Mtu anapokufa inatakiwa ufurahie kwa sababu amemalizana na masaibu ya wanadamu ya kila siku na anakwenda kupumzika mahali ambako hakuna mtu atamsumbua tena, sehemu pekee ambayo ataweza kutuliza akili yake bila kelele. Kwahiyo kifo ni zawadi, kifo ni ahadi ambayo kila mtu ataitimiza ni suala la muda tu hivyo kuumia mtu kupotea haitakiwi kuwa sawa kwa sababu tangu mwanzo wote tunajua kwamba kila mtu lazima atakufa kwa namna yoyote ile. Mimi kama raisi wako nakukumbusha hilo ili usije ukafanya hivyo siku nyingine, mtu yeyote ambaye alizaliwa na mwanamke ana mambo makubwa mawili ya kuyatimiza baada ya kuzaliwa, jambo la kwanza ni kuishi na jambo la pili ni kufa. Unajua kwanini nimekuita hapa muda huu Darian?”
“Hapana mheshimiwa”

“Mimi najua kwamba kuanzia kesho mwili wangu hautakuwa na uhai tena, nitakuwa naanza kusafiri kwenda kwenye dunia ya pili ambayo ipo mbali na wanadamu wa kawaida. Huko nitaishi nikiwa nawaona kwa mbali japo sitakuwa na uwezo wa kuwafikia. Mimi nakufa Darian lakini haimaanishi taifa langu linakufa, haina maana kwamba yale yote ambayo tuliyaanza yanakufa, yale lazima yaendelee na mtu wa kuyaendeleza ni wewe hapo, wewe ndiye mtu ambaye nina amini kwamba utaipeleka Tanzania kule ambapo inatakiwa kuwa. Hili taifa ni urithi wa watanzania, hili taifa ndiyo zawadi pekee ambayo watanzania wapo nayo hivyo hatutakiwi kabisa kuweza kuiharibu hii zawadi.

Huenda unashangaa mimi kukwambia haya yote kwa sababu hukutarajia au huenda haukufikiria haya kutokea lakini wewe ndiye unaenda kuwa raisi wa Tanzania baada ya mimi kufa”
“Mheshim……”
“Nisikilize kwanza, naelewa kwamba katiba yetu inamtaka makamu wangu ndiye awe raisi baada ya mimi kufa lakini ukweli ni kwamba makamu wangu hayupo tayari kuliongoza hili taifa. Siku zote mimi nimekuwa natamani kama taifa tuwe na utaratibu wa kuweza kuandaa watu wa kuja kuwa viongozi wakubwa kwa baadae lakini kabla sijafanikisha hili Mungu amenihitaji zaidi hivyo nakufa nikiwa sijalitimiza hilo lakini kosa ambalo siwezi kulifanya ni kumuweka mtu asiye sahihi kwenye hii nafasi kwani najua ataliharibu taifa hili na kulipeleka ambako siko.

Kwa muda ambao mimi nimeishi Ikulu, wewe kama waziri mkuu wa Tanzania ndiye mtu ambaye nimeona unafaa kukaa kwenye hiki kiti na kulipeleka taifa hili kule ambako linastahili kuwepo. Wewe ndiye mtu pekee ambaye unazijua falsafa zangu kuliko mtu yeyote yule, wewe ndiye mtu ambaye umekuwa zaidi ya hamasa kwangu kwenye kila jambo ambalo nimekuwa nalifanya kwa muda mrefu hivyo sitafanya kosa la kumpatia taifa hili mtu mwingine na najua kama nikifa bila kukamilisha huu utaratibu basi yanaweza kutokea mambo mabaya zaidi ya haya hivyo kabla sijafa hili ndilo jambo la mwisho ambalo naenda kulifanyia taifa hili kwa kukufanya wewe kuwa raisi kwa sababu nina imani kwamba utalifikisha mahali ambapo ni salama.

“Darian najua kuna mengi yanaenda kutokea huko mbele na huenda mengine hutayapenda ila inakulazimu kwa sababu ushakuwa raisi tayari, hakuna jambo lingine ambalo unaweza kulifanya kubadili hayo hivyo uwe tayari kwa jambo lolote ambalo litakuja mbele yako. Kuanzia sasa kila kitu kuihusu Tanzania kipo chini yako hivyo hata siku moja usije ukaniangusha na wala kuliangusha taifa hili kwani ndilo jambo la kwanza na la mwisho mimi kukuomba wewe ulifanye kwa ajili ya usalama wa taifa hili na hakikisha unashirikiana na mwenzako ambaye ni makamu wangu, hakikisha unamfanya kuwa makamu wako pia kwa sababu yule ni kiongozi bora kuliko sisi wote yaani mimi na wewe ila kuna shida moja kwake.
Kwa sasa bado hayupo tayari kuliongoza taifa na wakati wake ukifika atakuwa kiongozi bora mno kuliko mimi na wewe na hakikisha wakati unatoka madarakani uwe umemuandaa vya kutosha kwa sababu ni yeye ambaye anaweza kuibadili jumla historia ya taifa hili. Mfundishe namna ya kuwa kiongozi shupavu mwenye maamuzi magumu panapo hitajika. Mpaka sasa yule ni tunu ya taifa hili ila yeye halijui hilo, amekuwa mwema kupitiliza, amekuwa na roho ya kusamehe maeneo ambayo hatakiwi kusamehe kabisa kwa sababu kuwa raisi kuna muda unatakiwa kufanya maamuzi magumu ambayo yanaweza kuchukiwa na kila mtu ila baadae wakielewa watakuja kuyafurahia hivyo sio kila nyakati usikilize raia wanataka nini, kuna wakati fanya maamuzi kulingana na kwamba ni kipi ni kizuri kwa ajili ya taifa hili.
Hili likumbuke kwenye moyo wako kwamba makamu wangu ni raisi bora na kiongozi bora kuliko mimi na wewe ila hayupo tayari ila hakikisha baada ya wewe ni yeye ambaye anaingia madarakani kwa namna yoyote ile kwa sababu ndiye mtu sahihi zaidi wa kuweza kuyatimiza haya. Baadhi ya mambo mengi makubwa ambayo tumeyafanya, imewezekana kwa sababu ya akili yake yeye hivyo naweza kusema ndiye alikuwa mshauri wangu mkuu japo kuna vitu vidogo tu ndivyo vinatakiwa kufanyiwa kazi kwake, mimi nilikuwa namuonyesha kwa vitendo nadhani alikuwa ananielewa.

Jambo la mwisho kabisa ni kwamba usiniangushe mimi, usiwaangushe watanzania, usiliangushe taifa lao nami nakuombea kwa Mungu aweze kuzibariki harakati zako za mapambano. Kwa sasa naomba usaini kwenye hizi nyaraka kisha baada ya hapo uondoke kwani nataka kutumia muda ulio bakia kuwa karibu na familia yangu watu ambao nawapenda sana”

Hayo ndiyo yalikuwa maneno ya mwisho kutoka kwa raisi wangu mpendwa, mwanaume ambaye kwangu alikuwa zaidi ya mwalimu na bosi wangu. Yeye ndiye alikuwa mtu ambaye alikuwa kioo kwangu kwenye siasa na hata kwenye uongozi, amenifunza mengi na kunipa elimu ya dunia ya siasa, uongozi, maisha, namna ya kuishi na wanadamu. Sikushangazwa na maneno yake ya mwisho juu ya elimu ya kifo ambayo yalinifanya nikalia lakini jambo ambalo lilinishangaza ni yeye kuhitaji mimi kuwa raisi wa Tanzania. Binafsi nilijua haiwezekani kabisa, niliamini lazima makamu wake anatakiwa kuwa raisi lakini sikujua kwamba jambo hilo alikuwa ameongea mpaka na makamu wake mapema kabisa na walikuwa wamekubaliana na makamu wake ndiye ambaye amenitaka mimi nije kuliongea hili jambo hadharani ili watanzania wasiingie kwenye mkanganyiko wowote ule.

Binafsi nilijiona kwamba sipo tayari mpaka wakati ule ila wao waliona kwamba nipo tayari, jambo ambalo lilinishangaza ila nadhani sikuwa na namna naweza kulikwepa hivyo ndivyo mimi nimekuwa raisi wa Tanzania. Watanzania wengi walikuwa na maswali mengi kwamba inawezekanaje waziri mkuu kuwa raisi wa Tanzania, hili jambo limefanyika sio kwa kuvunja katiba yetu bali kwa kuangalia maslahi ya taifa hili zima hivyo nataka tuitumie hii nafasi na wakati kuweza kuyaenzi maisha ya mheshimiwa. Ni matumaini yangu kwamba mimi kwa kushirikiana na mama yangu ambaye alikuwa makamu wa raisi wa Tanzania kuweza kulifanya taifa hili kuwa la mfano tena. Mimi naahidi kwamba nitatimiza kila mradi ambao una maslahi kwa taifa hili, kila mradi ambao ulionekana kuwa wa mhimu kwa watanzania basi nitaupambania kwa nguvu zangu zote, kama ambavyo mheshimiwa aliniamini kwa maisha yake, hii ndiyo itakuwa zawadi yangu bora kwake kama kwaheri kwa maisha yake ambayo alipata kuyaishi na kulitumikia taifa hili. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika”
Ilikuwa ni hotuba ndefu yenye ujumbe mzito ndani yake, hotuba ambayo iliwagusa na kuwaliza wengi lakini ni hotuba ambayo ilitoa mwelekeo mpya wa Tanzania, hotuba ambayo ilitoa mshangao na elimu kwa watanzania wengi ambao walikuwa wapo njiapanda hususani kwa namna mambo yalivyokuwa yanaenda. Mheshimiwa raisi alilitambua hilo ndiyo maana alijumuisha kila kitu kwenye hotuba hiyo. Watanzania walikuwa kwenye majonzi lakini pia waliongezewa mambo mengine ambayo yalizigusa nafsi zao hususani kwa namna ambavyo raisi wao alikuwa analipenda taifa lake hata zile dakika zake za mwisho alikufa huku akiwa analiwazia taifa lake mema. Ilikuwa inaenda kuwa moja ya kumbukumbu bora mno ambazo watanzania walikuwa wanabakiwa nazo kwenye mioyo yao baada ya maisha ya mwamba huyo kufika tamati.



IKULU
Majira ya jioni baada ya msiba mheshimiwa raisi alikuwa ameketi kwenye ofisi yake akiwa anawaza mambo mengi ambayo yalikuwa yametokea na mahali ambako alikuwa anaelekea. Kwenye bilauri kubwa ambalo lilikuwa mezani mvinyo ilijaa ambayo alikuwa anainywa taratibu huku akili yake ikiwa mbali. Alianza kuyawazia maisha yake mahali ambako alitokea na pale ambapo alikuwepo siku hiyo, moyo wake ulijikuta unatabasamu kwa kiwango kikubwa, alijiona kuwa mtu mwenye bahati kuweza kukikalia kiti kikubwa zaidi ndani ya taifa.

22 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 23.
ENDELEA.......

“Siamini kama mimi M-bena kutoka huko Njombe Mtwango leo nimekuwa raisi wa Tanzania. Maisha yanaenda kwa kasi kubwa tofauti na wanadamu tunavyokuwa tunayafikiria tangu huko mwanzo, walikuwa sahihi watu ambao waliwahi kusema usije ukamkatia tamaa mwanaume ambaye bado anatembea aisee, hata mimi sikuwahi kabisa kuwaza kama nitaingia kwenye sehemu kama hii na kuja kuwa raisi wa Tanzania, kumbe kila kitu kinawezekana jambo la mhimu ni kufanya maamuzi tu basi kisha mengine unamuachia Mungu mwenyewe anamalizia panapo bakia” alitamka akiwa anakunywa mvinyo na nafasi yake inazuuzika kwa hayo mafanikio ambao alikuwa amejitengenezea kwenye maisha yake. Hizo fikra za kuyafikiria hayo maisha mapya ambayo alikuwa nayo kwa wakati huo ndizo ambazo zilimrudisha mbali, miaka ya huko nyuma kabla hajaingia kwenye hizo nafasi kubwa za kuanza kula vizuri na watu wazito.

Kumbukumbu zilirudi mpaka ndani ya kijiji cha Mtwango Njombe, ni maeneo ambayo yana yale maisha ya kawaida tu ambayo wanayaishi watu wengi. Wenyeji wa hilo eneo wanaishi kwa shughuli za kawaida za kila siku na ni maisha ambayo kwao wameyazoea tayari na huwa hawaoni kama yana shida yoyote ile, huko ndiko ambako alizaliwa bwana huyo.
Jina lake la kuzaliwa alikuwa akifahamika kama Martin Kibena, kijana ambaye yeye na shule hawakuwa na urafiki mzuri mpaka pale ambapo alifanikiwa kumaliza kidato cha nne ndipo hapo safari yake iliishia kwenye upande wa kuendelea kumwaga wino kwenye karatasi. Maisha ya Njombe hayakumpa nafasi nzuri ya kuishi kwa namna ambavyo alitaka yeye, maisha hayakuwa upande wake kwani hata kufanikiwa kumaliza kidato cha nne ni kwa msaada wa padri mmoja ambaye baada ya kufeli aliamua kumpotezea na kuamua kuwasaidia watoto wengine ambao kwao elimu lilikuwa jambo kubwa.

Martin alikuwa ni kijana yatima ambaye maradhi yalikuwa yamepotea na maisha ya wazazi wake akiwa kwenye umri ambao bado haukumpa nafasi ya kujifanyia maamuzi yake mwenyewe. Kukosa wasimamizi wa maisha yake ndiyo ilikuwa sababu kubwa zaidi ya yeye kupolea kwenye ulimwengu ambao sio salama akalisahau jukumu lake la msingi kuweza kujitoa kwenye umaskini. Baada ya kufeli elimu kijana huyo alijiunga na makundi ya vijana wengi ambao kazi zao kubwa mtaani hapo zilikuwa ni kujishughulisha na ufanyaji kazi wa kupasua na kubeba mbao kuweza kujikimu kimaisha.

Nguvu alikuwa nazo hivyo aliona kwamba ndizo ambazo ulikuwa mtaji wake mkubwa, alikuwa na ndoto kubwa ila hakuelewa angeweza vipi kuzitimiza kwa namna ambayo aliitaka yeye. Alitaka kuonekana maridadi mbele ya wenzake, alihitaji kuonekana wa tofauti jambo ambalo lilimfanya kufanya kazi kwa bidii kubwa mno, ufanyaji kazi wa bidii ulimsaidia yeye kupata pesa za kula, pesa za kuvaa hatimaye akawa kijana mtanashati ambaye alianza kuwa na mvuto mkubwa pale mtaani kwao.

Kwa umri wake alianza kuteseka na mabinti kwani ndio muda wake wa ujana ulikuwa umeanza. Pesa za kula kula kidogo alikuwa anapata kwenye vibarua hivyo anaanza kuruka na mabinti kadhaa ambao aliona kwamba wangemfaa kwa mahitaji yake hatimae akawa kijogoo wa Mtwango. Aliendelea na maisha yake ambayo kwake alijivunia kuwa nayo mpaka pale ambapo alikuja kukutana na mwanamke mmoja mrembo, binti ambaye aliiba akili yake yote, Natasha ndilo lilikuwa jina lake. Binti huyo hakuwa mnyonge, alitoka kwenye familia ambayo haikuwa haba sana kwani baba yake alikuwa ni mfanya biashara ambaye alikuwa anauza mbao na maparachichi na kwenye hizo kazi za baba yake ndiko ambako alikutana na Martin.

Wawili hao penzi lilinoga, penzi lilizivuta upya ndoto za kijana Martin ambaye alikuwa anajituma kuhakikisha anampatia kila kitu mpenzi wake. Binti huyo hata yeye hakutaka kuendelea na masomo kwani aliamini anapoteza muda wake hivyo walikuwa na muda wa kutosha kuweza kula ujana wakiwa pamoja kama ndege waruakao pamoja kwa nyakati zote. Michezo yao ilisababisha Natasha kuweza kupata mimba, binti huyo alishika ujauzito wa Martin jambo ambalo lilimpa tumaini jipya la maisha la kuanza kutengeneza familia yake lakini alisahau msemo usemao “kisicho ridhiki huwa hakiliki” upendo ulimdumaza hakuwahi kuwaza huko mpaka siku ambapo alianza kupokea mabadiliko mbalimbali kutoka kwa binti mrembo ambaye alikuwa amempenda kwa moyo wake mpaka nafsi yake yote ilikuwa kwake.

Kwa mara ya kwanza alihisi huenda ni tatizo la mimba ndilo lilikuwa likimsumbua yule kisura lakini aligundua kwamba sio kweli kwa sababu alikuja kugundua kwamba hata ile mimba alikuwa ameitoa. Kwanini amfanyie vile? Ndipo akaja kuyajua ambayo hakupaswa kuyajua na hata kama angeyajua basi kwa wakati ule hakuwa tayari kabisa kukabiliana nayo. Ule ndio ulikuwa mwanzo kabisa wa maisha yake mengine ambayo huenda tangu mwanzo hakuwahi kuyawazia kabisa. Alimtafuta mrembo wake kuweza kujua tatizo nini ndipo alimkataa waziwazi kwamba wao walitakiwa kuishia pale, ile safari yao haikutakiwa kuendelea kwa sababu mwenzake alikuwa amepata kituo kipya cha kushukia kwani hakuwa tayari kwenda ambako hakuwa na uhitaji wa kwenda.
Kilikuwa zaidi ya kisu mfupani, kisu ambacho kilienda kukata kata moyo wa kijana Martin. Alikuwa tayari amempatia moyo wake mrembo huyo, sasa kwa sababu zipi aamue kuukatili bila huruma namna hiyo? Alihisi kudhulumiwa na hakuona kama jambo hilo lilikuwa na afya kwa upande wake, alighafilika Martin. Alijitahidi kumbembeleza binti huyo lakini haikuwezekana kwa sababu mwenzake hakuwa tayari, nafsi ilimuuma akapata sononeko hivyo alihitaji angalau mwanamke huyo aweze kumpatia sababu za msingi za yeye kuweza kumtenda namna hiyo, jibu alipewa lakini liliongeza maumivu makali kwake.
“Martin haina haja ya mimi kukupa sababu ya kukuacha kwa sababu haina umuhimu wowote ule”
“Ni mhimu kwangu ndiyo maana nimeuliza”
“Kwa sababu mimi na wewe hatukupaswa kuwa pamoja tangu mwanzo”
“Kwanini Natasha?”

“Unajua wewe ni mwanaume ambaye haujasoma, hauna maisha yoyote yaani upo upo tu bila mpango wa maana. Mimi ni mtoto wa kike ambaye nahitaji matunzo, nahitaji mtu ambaye nikitembea naye mtaani jamii iniheshimu, sasa kijana kama wewe una kipi hasa? Hauna lolote Martin ndiyo maana nakwambia hatukutakiwa kuwa wote tangu mwanzo kwahiyo kwa sasa nataka usije kunisumbua tena kwenye maisha yako”
“Kwamba mwanzo haukujua haya yote?”

“Nadhani zilikuwa akili za kitoto tu, hata ndugu zangu wote walipo litambua hili walianza kunicheka na kuniona mimi kama mpuuzi tu kuwa na kijana wa hovyo kama wewe. Baba yangu baada ya kuniuliza jambo ambalo nalitaka hususani alipo tambua kwamba nimetoa mimba alipatwa na hasira alipo gundua kwamba nimepata mimba ya mtu kama wewe. Jibu langu kwake lilikuwa ni kwamba natamani kuwa mke wa mtu hivyo akaniunganisha na mtoto wa rafiki yake ambaye ana uwezo mkubwa kifedha na anaweza kunifanyia kila ambalo nalitaka mimi tofauti na maskini kama wewe ambaye maisha yako yataishia kwenye ubebaji mbao tu” maumivu yalikuwa makali kuambiwa ukweli ambao huenda hakuwa tayari kuweza kuupokea kwa nyakati kama zile.
Penzi ni doa bwana na ili kulitoa kwenye nguo unastahili kuwa na sabuni stahili ya kuweza kuitumia na ndivyo ambavyo hali ilikuwa kwa Martin ila kwa bahati mbaya lile doa ambalo lilikuwa moyoni mwake wa kuliponya hakuwa Natasha.
“Kwanini unaniambia maneno mazito namna hii huku ukijua kabisa kwamba bila wewe siwezi kuishi?”

“Ebu jiangalie kwanza namna ulivyo, una uwezo wa kunitoa out sehemu ambazo nataka mimi? Unaweza kuninunulia japo simu nzuri na yenye uwezo mkubwa nikatamba nayo kwa wenzangu? Unaweza ukanunua hata gari ambayo inaweza kunifanya nisiteseke na jua pamoja na hili vumbi la kijijini? Haina hata haja ya wewe kujibu kwa sababu wote tunajua kwamba hauna uwezo wa kufanya haya. Nimejiona kwamba nilikuwa mjinga kukupenda mwanaume kama wewe usiye na mbele wala nyuma, mwanaume ambaye unanuka umaskini kila sehemu, mwanaume ambaye ushamba wangu ulinifanya nihisi nimefika kwa sababu nimechelewa kuijua dunia na nilipo fanikiwa kuitambua dunia ya kweli ndipo nimegundua kwamba nilifanya kosa kubwa kukuvulia nguo zangu na kushika ujauzito wako. Kiuhalisia ni kwamba hata kitumbua hiki haukupaswa kukigusa kabisa, haukustahili hata kunilaza kwenye kile kitanda kibovu cha miti hivyo katafute fukara mwenzako ambaye unaendana naye na hii iwe mwanzo na mwisho wa wewe kunifuata fuata kama unanidai.
Nataka ujue namna mashababi wanavyo jua kuwatunza wanawake, mwanaume wangu mpya wa sasa nitampa penzi kila sehemu hata akitaka juu ya paa la nyumba, hata kama nipo ni msibani nitamvulia nguo mahali anapotaka yeye. Ni mwanaume na nusu yule, ana uwezo, kwao wana pesa, ananinunulia gari na anaenda kunifanya kuwa mwanamke ambaye wanawake wengi hapa duniani wanatamani kuwa. Hii inakuonyesha kiasi gani nilikurupuka kuwa na mpuuzi mmoja kama wewe hapo hivyo kuanzia sasa unikome na nisije nikalisikia hata jina lako mahali popote pale ambapo mimi naenda ama kuwepo”

23 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 24.
ENDELEA.......


Ni maneno makali zaidi ya tindikali yaliendelea kuurarua moyo wa Martin, kijana ambaye penzi lilimjia kiugeni kwenye akili yake akawekeza akili yake yote kwa mwanadamu ambaye amekutana naye tu hapa duniani na hakuzaliwa naye. Alijihisi kuwa mwenye bahati kuwa sehemu ya maisha ya mrembo huyo lakini wakati ambao alikuwa anaamini kwamba wanasogea kwenye hatua kubwa zaidi ya maisha, ndio wakati ambao alikuwa anampoteza mwanamke wa ndoto zake na sio kumpoteza tu bali alimpoteza kwa aibu na masimango kiasi kwamba alijihisi hakuwa mkamilifu, alijiona sio mwanadamu ambaye anastahili kuishi kama wengine, maisha yake aliyakatia tamaa kwani kwa wakati huo hakuona kama yana umuhimu wowote tena hivyo akajaribu kuingia kwenye njia ambayo imewamaliza vijana wengi na kukatisha ndoto zao.

Alijitupa kwenye ulevi akiamini kwamba pombe ingemsaidia kupunguza mawazo ambayo aliyahifadhi kwenye ubongo wake ila haikuwa kweli. Ilibakia kidogo apate ugonjwa wa akili baada ya kushuhudia kwa macho yake mwanamke huyo akifanya mapenzi na bwana wake mpya, ni wazi kwamba walimfanyia makusudi, Martin akajikuta anazidi kupotea kabisa kwenye maisha. Alinogewa na pombe akasahau kazi na ule utanashati wake, dunia ilianza kumtenga kwani kila mtu alimkataa, alibadilika na kuwa kituko kila sehemu, watoto walimtania, jina la chapombe lilimvaa na kumpendeza, kitaa kikalibariki ndilo likawa jina lake maarufu. Nyakati kadhaa ambazo akili zilikuwa zinamrudia hakujutia kuwa hivyo kwani aliamini kwamba dunia ilimtaka yeye kuishi hivyo, hakuona kama ulimwengu ulikuwa na nafasi nzuri zaidi kwa ajili yake kwahiyo naye aliamua kuishi kwa namna hiyo mpaka siku moja ambapo alitembelewa na mtu mmoja ambaye alikuwa anamuona mara kadhaa hapo mtaani tena akionekana kuja kibiashara na kisha angepotea baada ya muda mrefu.

Hiyo siku ndiyo iliufungua ukurasa mpya wa maisha yake, ukurasa ambao ulimfanya yeye kuja kuwa mtu tofauti kabisa lakini kwa wakati huo hakuwa na ile roho ya huruma, hakuwa na ile roho ya kuwaamini wanadamu wala kuwa mwema kupitiliza. Mtu huyo ambaye alienda kumfuata yeye huko kijijini kwao alikuwa ni mfanya biashara na mwanasiasa ambaye ndoto zake za kuitawala siasa kupitia watu zilikuwa hai, alikuwa ana mipango ya mbali na moja ya mpango wake aliingia kijana Martin ambaye karibia kila mtu alikuwa amemkatia tamaa na hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na mpango naye tena ila kwake ilikuwa ni tofauti kwa kijana huyo.

Alimtaka kijana huyo kurudi kwenye hali yake ya kawaida, kuna watu ambao walikuwa na maisha magumu kuliko yeye na bado walikuwa wanaendelea kupambana halafu yeye anakata tamaa kwa sababu tu ya mwanamke ambaye wamekutana ukubwani? Angeonekana mpumbavu mbele ya sheria kali na misingi ya kiume. Martin alitakiwa kuionyesha jamii kwamba ilifanya kosa kubwa kushindwa kumuamini tangu mwanzo, alitakiwa kuuaminisha ulimwengu kwamba yeye alikuwa bora zaidi ya vile ambavyo watu walikuwa wanamuona lakini pia, Martin alitakiwa kumfanya Natasha aweze kuamini kwamba aliwahi kuipata dhahabu kwenye mikono yake na akaja kuipoteza kizembe kabisa wakati ilikuwa ni yake.

Hakutakiwa kuyapa mapenzi kipaumbele, mapenzi hayana faida kwenye mzunguko wa maisha wa muda mrefu bali mafanikio ndiyo ambayo huwa yana faida kubwa kwani unapokuwa umefanikiwa basi kila kitu kinakuwa upande wako, kila mtu anakuwa mtu wako na kila jambo linakuwa linafanyika kwa namna ambayo wewe unaitaka hata kama kuna baadhi ya watu hawaitaki. Alimtaka kijana huyo kubadilika, kulikuwa kuna maisha ya tofauti ambayo alihitaji kumtengenezea, jambo la kwanza alimfanya kuwa mfanyakazi wake na maisha mapya yakaanza, alimjengea nyumba kule kule mtwango ili atengeneze heshima kwanza kwa wapuuzi kadhaa ambao walikuwa wamempotezea. Jumba la kifahari kuzidi kijiji kizima lilijengwa, gari la kifahari alilipata muda mfupi tu baada ya kuanza kufanya kazi ambayo ilionekana kumlipa sana.

Nani amewahi kukwambia kwamba biashara ya siasa hailipi? Hiyo ni miongoni mwa biashara chache duniani ambazo hazijawahi kuwa na hasara. Watu walianza kumheshimu na kumuogopa kwa wakati mmoja, hakuna mtu anaweza kusimama na kushindana na pesa, wale ambao walikuwa wanamtusi walianza kuwa wapole kwake na hata Natasha baada ya kusikia habari za Martin alitamani dunia immeze lakini zaidi zaidi alitaka kumrudia kijana huyo ambaye alimkana kwa dharau. Yule bwana wa mwanzo ambaye alimpa kiburi alimtumia na kumbwaga kwani aliona kuwa hakuwa mwanamke ambaye alistahili kuwekwa ndani kama mke ila hata Martin hakuwa tayari kumrudia malaya yule ambaye alikuwa anaweza kununulika kirahisi tu.
“Mimi sio mbeba mbaoooo!!!!!!!!!!!!” alitamka kwa sauti nzito na kushtuka kwa sababu mlango wake ulikuwa unagongwa kwa nguvu. Raisi Darian alikuwa anahema kwa nguvu kwa sababu alikuwa kwenye kumbukumbu ambayo ilimrudisha kwenye yale maisha yake ya nyuma na mahali ambako alitoka. Alikuwa anatokwa na jasho jingi mpaka katibu wake alishtuka hususani baada ya kusikia ile kauli ya bosi wake kudai kwamba yeye sio mbeba mbao. Alipewa taarifa kwamba kulikuwa na ugeni wake na mtu huyo alihitaji kuonana naye kwa wakati huo kwani ilikuwa ni mhimu kufanya hivyo kama ambavyo maagizo yake yeye mwenyewe yalikuwa.

Mtu ambaye alikuwa ameingia ofisini kwake alikuwa ni yule mwanaume ambaye alionekana Tunduma akifanya kazi yake. Kwa umri naye alikuwa mtu mzima ambaye walikuwa wakipishana kidogo kwani alionekana kuwa mkubwa hata kwa raisi wake. Alikuwa ni moja ya watu ambao alikuwa akiwatumia kwenye majukumu yake ya siri nje ya ofisi.
“Bila shaka umekuja na taarifa nzuri kwani siku ya leo imekuwa ndefu na mbaya kwa upande wangu”
“Taarifa sio njema kwa sababu ametafutwa kila sehemu na hakuna eneo hata moja ambalo linaonyesha kwamba kuna dalili ya uwepo wake zaidi ya kupatikana damu yake ikiwa imegandiana kwenye mti mmoja”
“Uliaahidi kwamba utampata huyu mtu, inakuaje unaniletea taarifa kama hizo nyakati kama hizi ambazo unajua kabisa kwamba sihitaji taarifa za namna hii?”

“Kuna wakati haitakiwi kuuogopa ukweli, inatakiwa kuufuata ukweli hata kama unakuumiza kwa sababu ndiyo njia pekee ya kuweza kutatua tatizo ambalo lipo mbele yako kama ambavyo leo umewadanganya watanzania na stori ya kutunga kuhusu wewe kukutana na raisi akakukabidhi taifa hili kwenye mikono yako jambo ambalo ni uongo”
“Umetamka nini kwenye mdomo wako?”

“Najua utanitisha, utaitisha familia yangu kama ambavyo siku zote unafanya lakini mimi nipo hapa kukwambia ukweli. Ulinipa hii kazi ya kufanya mambo yako ambapo nimehusika kwenye vifo vya watu wengi ambao hawakuwa na hatia yoyote na usifikiri kwamba nitaogopa kukwambia ukweli. Niamini mimi kama ingetokea hata siku moja hawa raia wakajua aina ya mtu ambaye ameingia Ikulu basi huenda asubuhi kabisa ungekuta haya majumba yamevamiwa na kuvunjwa vunjwa”
“Mhhhhhh umepata wapi ujasiri wa kuniambia maneno ya namna hiyo?”
“Kwa sababu ndiyo kazi yangu kukwambia ukweli na kufanya kazi zako chafu”
“Ambazo bila shaka hauzipendi!”
“Hakuna mtu anapenda kufanya mauaji kwa niaba ya mtu mwingine”
“Umekuja hapa kuniambia hayo maneno tu?”
“Hapana”
“Niambie ambacho kimekuleta”

“Binti yupo kwenye mkono wangu mpaka sasa”
“Una uhakika na hilo ambalo unalisema?”
“Ndiyo”
“Umewezaje kumpata?”
“Kama ambavyo uliwahi kusema kwamba mimi ni mbwa wako na siku zote mbwa anafanya yale ambayo bosi wake anakuwa anamuagiza”
“Ukiwa na maana kwamba?”
“Mbwa wako nakushauri kwamba huu ni muda wa wewe kuweza kuongea na yule binti”
“Unahisi ni jambo zuri kwa sasa?”
“Muda hautusubiri, tunatakiwa kuweza kumtafuta huyu mtu haraka na huyu binti anaweza kuwa njia nzuri ya kufika huko”
“Sawa, unaweza kwenda mimi nitamalizia palipo bakia”
“Haujanipa jibu kuhusu Bazoka bosi”

“Hilo kwa sasa lipo juu ya uwezo wako nitalishughulikia wenyewe” alimjibu bwana huyo mithili ya mtu ambaye alikuwa analazimishwa tu ila hakupenda kuendelea kuongelea hilo.
Baada ya kuhakikisha mtu wake ametoka humo ndani alibaki ametulia akiwazua jambo la kufanya kwa wakati huo. alisogea mpaka kwenye droo ya meza yake akaitoa simu moja kubwa ya kisasa. Aliiwasha na ndani yake kulikuwa na namba moja tu pekee, namba hiyo aliipiga kwa video moja kwa moja ambapo ilisafiri mpaka ndani ya taifa la Japan. Upande wa pili alipokea bwana mmoja ambaye alikuwa ana upara unao ng’aa mno.

“Mwambie Jaden huu ni muda wa kurudi nyumbani”
“Unataka arudi lini bosi?”
“Kesho usiku namhitaji awepo Tanzania”
“Kuna haja ya kumwambia sababu ambayo inamfanya arudi nyumbani ghafla hivi?”

24 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 25.
ENDELEA.......

“Sihitaji kumpa sababu ya kurudi hapa, andaa safari yake haraka kuna jambo la mhimu sana ambalo unahitajika uwepo wake kuweza kutatuliwa”
“Sawa bosi” simu ilikatwa, alihema kwa nguvu na kuamua kuondoka ambapo aliishia ile sehemu ambayo alikuwepo katibu wake, mwanamke mmoja ambaye alikuwa mrembo mno akiwa na asili ya taifa la Ethiopia. Hakuuliza jambo lolote zaidi ya kumshika mrembo huyo ambaye alionyesha tabasamu kwenye uso wake, alimgeuza na kumuinamisha hapo hapo kisha akampandisha sketi yake safi na nguo ya ndani akaishusha, aliufungua mkanda na kuanza kumsulubu na mjeledi wake wa asili mwanamke huyo ambaye alionekana kufurahia penzi la raisi bila kujali kama walikuwa ni kwenye ofisi ya mhimu kwa taifa zima.


AKITA, JAPAN
Moja kati ya majiji ambayo yanapatikana ndani ya taifa la Japan, Akita ni mji wa kale ambao umebeba idadi ya watu wapatao laki tatu ikiwa ni pungufu kidogo kuweza kufikia idadi hiyo ya watu. Ni jiji ambalo limepakana na milima mingi pamoja na bahari hivyo kufanya kuwa eneo zuri kwa ajili ya matamasha ya asili na makumbusho makubwa ya sanaa duniani ambapo watu hutembelea kutoka pande mbalimbali za ulimwengu kwa ajili ya utalii.
Pia ni jiji ambalo linatunza kumbukumbu za masamurai wengi ambao wamepata kuishi ndani ya taifa hilo hivyo wapo pia kadhaa ambao huwa wanaishi ndani ya eneo hilo. Ni moja ya maeneo ambayo baadhi ya misimu hushuhudia baridi kali maeneo hayo ila kwa wenyeji wamesha zoea kwani ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Ndani ya maeneo hayo ya Akita ndiko ambako simu ya mheshimiwa raisi Darian Julius ilifika kwa kijana wake ambaye alimhitaji aweze kurudi nyumbani kwani kulikuwa na kazi kubwa ambayo alikuwa anahitajika kuweza kuifanya. Kwenye moja ya sehemu ambayo ilitengenezwa kwa asili, yalikuwa ni makazi ya samurai mmoja wa zamani ndani ya eneo hilo lakini mtu huyo alikuwa amekufa. Jaden ndiye mwanaume alikuwa anahitajika kurudi ndani ya ardhi ya Tanzania kuja kuifanya kazi ambayo ilianza kumnyima amani mheshimiwa raisi wa Tanzania.

Alikuwa mwanaume ambaye kuishi kwake huko Japan zilikuwa ni moja ya sababu za kuupata uwezo wake ambao baadae kama nyakati za giza ambazo alikuwa anazipitia kiongozi wake zingekuja kumsaidia kwa ukubwa. Ndani ya eneo hilo ambalo lilikuwa linamilikiwa na Samurai huyo wa zamani ambaye alifahamika kama Shimamoto ndipo mahali ambapo alikuwa anaishi bwana huyo yeye kama eneo lilikuwa ni lake vile. Haikuwa bahati mbaya yeye kufanikisha hilo ndani ya hayo maeneo bali ilikuwa ni kwa msaada mkubwa wa waziri wa mambo ya nje wa Japan, Shinto Hiru.

Kiongozi huyo kuwa waziri wa mambo ya nje kulimfanya kujuana na watu wengi ambao walikuwa wapo nje ya utawala wa Japan. Yeye ndiye ambaye alikuwa anashughulikia mambo ya nje yote ya taifa hilo hususani kwenye kukuza uhusiano wa kidiplomasia na moja kati ya mataifa ambayo yalikuwa kwenye hesabu za taifa hilo kwa sababu yana rasilimali za kutosha, ilikuwa ni Tanzania. Tanzania iliwekwa kipaumbele kwa sababu walijua watafaidika vingi kwa kujizolea rasilimali za taifa hilo kwa njia rahisi kabisa kutokana na tamaa ambayo waliiona kwa viongozi wake. Huo ndio ulikuwa mwanzo kabisa wa bwana huyo kupata marafiki ndani ya taifa la Tanzania na miongoni mwa watu ambao waliingia kwenye orodha yake ni raisi wa Tanzania ambaye kwa sasa alikuwa ameingia Ikulu lakini kabla ya hapo alikuwa ndiye mtendaji mkuu wa serikali.

Kiongozi huyo kama walivyo viongozi wengine duniani, naye hakuwa nyuma kwenye kujali maslahi yake. Alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kuja kuwa raisi wa taifa la Japan hivyo alikuwa anajiandaa mapema tangu mwanzo. Kwenye kuiwania nafasi hiyo alijua wazi kwamba angekutana na upinzani mkali wa hapa na pale kutoka kwa viongozi wengine ambao walikuwa wasafi na walikuwa na nguvu kuliko yeye hivyo alitakiwa kutumia mpango wa pili kuweza kukamilisha adhma yake ya kufanikisha jambo hilo. Kwenye hesabu zake zote ambazo alizipiga mezani kuhusu uhakika wa yeye kuingia madarakani ni kwamba kuna baadhi ya viongozi walitakiwa kupunguzwa yaani kuuawa hivyo akawa anahitaji muuaji ambaye angeweza kuitekeleza kazi hiyo.

Alijua kabisa kwamba kama angewatumia watu wao ingekuwa ni hatari kwake, uhatari huo ndio ambao ulimfanya amuombe ushauri rafiki yake wa Tanzania ambaye alikuwa amempata, Darian Julius. Ushauri ambao alimpatia ni kwamba yeye alikuwa tayari kuweza kumpatia kijana wake ambaye anamtegemea kwa makubaliano kadhaa ambayo yaliwekwa mezani. Moja kati ya sehemu ya makubaliano yao ilikuwa ni kwamba kijana huyo alitakiwa kufundishwa baadhi ya vitu hususani uwezo wa ziada na watu wa huko yaani masamurai na kisha kijana huyo angetumika kuweza kufanya shughuli zote ambazo yeye angehitaji kuzitimiza huko kwao Japan.

Makubaliano mengine yalikuwa ni raisi wa Tanzania kuja kunufaika na mipango ya baadae ya taifa la Japan na kama kijana wake angekamatwa kwenye kazi basi wote wangemkataa maana yake ingekuwa inakula kwake mwenyewe bila msaada kutoka sehemu yoyote ile. Kwahiyo Jaden aliingia Japan kwa malengo makubwa mawili, kwanza ilikuwa ni kutengenezwa upya, kupata uwezo wa kutisha zaidi ya ule aliokuwa nao mwanzo lakini kazi ya pili ilikuwa ni kwenda kufanya mauaji. Mwanaume huyo aliifanya kazi ya kuua wanasiasa wengi wa Japan ambao walio onekana kuwa hatari kwa Shinto Hiru na kuhusu kukamatwa kwake ilikuwa ni ngumu kwa sababu watu hao waliamini muuaji ni mmoja wa watu wao kwahiyo walipoteza muda mwingi kuweza kumtafuta mhusika miongoni mwao ila uhalisia ni kwamba walikuwa wanaangalia sehemu ambayo sio sahihi kwani muuaji halisi hakuwa mmoja wao.

Baada ya kuifanya hiyo kazi kwa muda mwanaume huyo alikabidhiwa kwa siri kubwa kwa Samurai mmoja ambaye alikuwa ni wa kale na aliwahi kuwa moja ya viumbe hatari zaidi kuwahi kuishi ndani ya taifa la Japan. Historia yake ilikuwa inatisha mzee huyo, alikuwa na mengi ambayo aliwahi kuyafanya nyuma lakini kwenye kila wema basi huwa kuna makosa kadhaa ambayo yanaweza kumpatia ubaya mtu na kufanya yale mema yake yote kuonekana sio lolote mbele za waungwana. Samurai huyo licha ya kuwa kipenzi kwa wengi lakini bado sio kila mtu alikuwa anamuona hivyo, kuna watu walimuona kama alikuwa na makosa yake kadhaa kwa jamii yao.

Enzi za ujana wake Shimamoto aliwahi kuwa muuaji wa kulipwa kama ambavyo alikuwa Jaden kwa nyakati hizo, naye aliwahi kutumika na wanasiasa wengi zamani hizo kwa ajili ya kutekeleza matakwa ya kisiasa. Yeye alikuwa amekulia kwenye hayo mazingira ya Kisamurai hivyo familia yake ilikuwa ni moja ya familia ambazo zilikuwa zikiheshimiwa kwenye kila kona ya taifa hilo. Kuheshimika kwa familia yake ndiko ambako kuliwafanya wachukuliwe kama ni moja ya sehemu ya utamaduni wa taifa hilo mpaka pale ambapo kazi halisi ya bwana huyo ilipokuja kutambulika kwa watu. Taifa lilikuja kujua kwamba bwana huyo anautumia uwezo wake kuweza kuua viongozi tena akiwa analipwa na baadhi ya wanasiasa kuweza kutekeleza kazi hiyo jambo ambalo liliwapa hasira raia pamoja na Samurai wengine wa taifa hilo hivyo wakajua kama kijana anafanya hayo maana yake kuna mawili nyuma yake. Moja ni kwamba alikuwa anatumwa na familia yake au familia yake ilikuwa inajua ambacho anakifanya ikashindwa kumuweka kwenye mstari mnyoofu, kiufupi ni kwamba walibariki yeye kufanya jambo hilo.

Kwao ulikuwa ni udhalilishaji hivyo wakaamua kumuweka kwenye mstari wenyewe ili yasije kutokea makosa kama hayo kwa baadae kwani yalikuwa yakiwachafua. Samurai ni neno lenye maana ya Shujaa kwa Japan, ni watu ambao wamepata kuwepo kwa miaka mingi sana ambayo imekwisha kupita na alama yao kubwa ni upanga, ulikuwa ukimuona mtu kwenye taifa hilo anatembea akiwa ameushika upanga wake basi ndiyo ilikuwa ishara yao kubwa ama utambulisho wao mkubwa. Kiuhalisia ni kwamba miaka ya leo Samurai wanadaiwa kwamba hawapo na ni kweli hawapo kwa sababu hakuna mtu ambaye anaruhusiwa kuweza kutembea na upanga ndani ya taifa la Japan lakini urithi wao upo.

Kuna baadhi wa familia ama koo ambazo ni masalia ya hao watu, koo ambazo zinaenzi tamaduni za watu hao ambao wamepata kuwepo kwa miaka mingi na kuyaishi maisha ambayo waliyaishi Samurai hivyo ni kama zinaulinda ule utamaduni usije kupotea kwenye ramani ya ulimwengu. Uwepo wa hizo familia pamoja na watu ambao wanaenzi tamaduni hizo ndio ambao huwa unafanya ionekane kwamba hao watu bado wapo kupitia urithi ambao waliuacha. Hivyo kwa familia ambazo huwa zinaenzi tamaduni za mashujaa ambao wamepata kuishi ndani ya taifa hilo huwa zinaheshimika kwa sababu zina historia kubwa na pana ndani ya Japan. Sasa kwa familia kama hizo kuhusika kwenye mambo ya ajabu kama hayo tena ambayo hayana manufaa kwa taifa lao bali kwa watu kadhaa tu ilizikera hata familia zingine ambazo nazo huwa zinauenzi utamaduni wa watu hao.

Jambo hilo ndilo ambalo lilipelekea wao wenyewe kuhitaji kuipa adhabu familia hiyo ambayo alikuwa anatokea Shimamoto ambaye kwa wakati huo alikuwa anajulikana kama Akari Sasaki. Kijana huyo alitafutwa lakini hakuwahi kupatikana hivyo adhabu ikatua kwa familia yake ambapo Samurai wengine ambao walikuwa wanajitanabaisha hivyo waliua familia nzima ya kijana huyo ambaye naye baadae alianza kumtafuta Samurai mmoja mmoja kwa ajili ya kulipa kisasi mpaka pale ambapo utambulisho wake ulikuwa matatani ndipo alikuja kukimbia na kwenda kuishi ndani ya jiji la Akita ambalo ni kilomita 670 kutoka ndani ya jiji la Tokyo ambako alikuwa akiishi tangu mwanzo na familia yake.

25 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 26.
ENDELEA.......


Kwenda kuishi Akita kwa siri ndiyo ilikuwa sababu yake ya msingi ya kubadilisha utambulisho wake kwani huko hakuwa maarufu na kujiita Shimamoto. Aliishi kwa siri kwa miaka mingi na baada ya umri kwenda na sura yake kubadilika kabisa ndipo alijitambulisha kwamba yeye ni masalia ya wale Samurai wa zamani ambao walipata kuishi. Watu hawakuwa wakimkumbuka tena kwa sababu ni muda mrefu ulikuwa umepita, baada ya kujitanabaisha kwamba alikuwa ni Samurai watu walianza kumheshimu mno ndani ya hayo maeneo. Hakuwa akijinadi tu bali hata ule uwezo wake ambao alikuwa nao ulikuwa unaongea wenyewe, alikuwa ni moja ya binadamu hatari kuwahi kuishi ndani ya taifa hilo na ndiyo maana alipata kiburi cha kulipa kisasi kwa wenzake japo baadae aliamua kukimbia baada ya utambulisho wake kuwa mashakani kwani hapo angeenda kupambana na serikali nzima ya Japan.

Maisha siku zote yana pande mbili, unapo jiona kuwa mjanja basi ujue kwamba kuna watu wamewahi kuwa wajanja zaidi yako na wala wewe hautakuwa wa mwisho kuwa mjanja hapa duniani. Shimamoto alikuwa ameizika siri yake kwa miaka mingi na kuanza kuishi kwenye ile misingi ya Kisamurai haswa huku akiongozwa na dini ambayo ilikuwa ni sehemu kubwa ya maisha yake. Alikuwa ni mtu safi ambaye kila mtu alitamani kuwa kama yeye, alikuwa anafanya kazi ya kuwatengeneza samurai wengine wa kuhesabika japo kwa siri kubwa. Kwenye maisha yake bwana huyo alibahatika kuwa na mtoto mmoja tu ambaye alikuwa ni binti Aimi Shimamoto. Binti huyo alimpata kwa mwanamke mrembo Akemi ambaye alikutana naye ndani ya Akita baada ya kuyaanza maisha yake sehemu hiyo lakini kwa bahati mbaya ni kwamba mwanamke huyo alikufa akimuachia binti huyo ambaye alikuwa ni kumbukumbu bora kwake. Binti huyo naye alikuzwa kwenye ile misingi ya Kisamurai hivyo hakuwa mnyonge, alikuwa ameshiba vilivyo na ndiye ambaye alikuwa tumaini la maisha ya bwana huyo Shimamoto.

Sasa ile siri yake haikuwa salama kama ambavyo yeye alikuwa anajiaminisha kwamba ipo, ile siri kuna watu walikuwa wanaifahamu kwamba bwana huyo alikuwa amelikimbia jiji la Tokyo kwa miaka mingi baada ya kufanya uhalifu ambao ulitakiwa kumfanya anyongwe na kwenda kujificha kwenye hilo jiji la Akita. Ni watu kadhaa ambao walikuwa wana siri hiyo ila hakuwa na hizo taarifa mpaka alipo pata mgeni wa ghafla ambaye hakuwahi kuwa na miadi naye wala hawakuwahi kukutana kwenye maisha yao yote yangu mwanzo, jambo hilo lilimshtua bwana Shimamoto kwa sababu haikuwa kawaida kukutana na jambo la namna hiyo.
Ugeni ambao aliupata ulikuwa ni kutoka kwa waziri wa mambo ya nje wa Japan, bwana Shinto Hiru alionekana kabisa kwamba hata yeye alienda eneo hilo kwa siri kubwa, hata yeye hakutaka uwepo wake hapo uweze kutambulika na mtu yeyote yule. Wanaume hao wawili ambapo mmoja alikuwa mzee na mwingine alikuwa bado kijana walikaa sehemu ya siri kwa ajili ya mazungumzo ya watu wawili tu pekee.

“Mzee wangu sisi wanadamu tunaishi tu hapa duniani ila hatuna muda mrefu wa kuwa hai ndiyo maana wakati tunaishi inatakiwa tuishi kwa namna zote ambazo zinatufanya tuwe na furaha au kufanya yale ambayo tunayapenda kwa sababu siku ukiwa kitandani hauna uwezo wa kufanya jambo lolote lile ndipo unaanza kutamani nyakati zirudi nyuma uweze kuutumia vizuri muda wako ila unakuwa umechelewa kwa sababu nyakati hazipo kwa ajili ya kukusubiri” waziri alifungua kinywa chake kwa maneno yenye mkanganyiko.

“Mhhhh mheshimiwa waziri imenishangaza leo wewe kuja nyumbani kwangu, mimi na wewe hatujawahi kufahamiana na kiufupi ni kwamba haunijui mimi hapa. Kwahiyo inanishangaza mtu mkubwa kama wewe kusafiri mpaka huku kwa ajili ya kuja kunipa elimu kuhusu maisha ya mwanadamu! Hapana, naomba niambie sababu ya mtu mzito kama wewe kusafiri kuja pembezoni huku kuongea na mtu ambaye sina thamani kwako tena ukiwa umekuja kwa siri kabisa’’ Shimamoto aligundua kwamba kuna jambo ambalo halikuwa la kawaida kwa kiongozi huyo kwa sababu asingekuja tu kupoteza muda wake ndani ya eneo hilo bila kuwa na sababu ya msingi ya kuwepo hapo.

“Upo sahihi kabisa mzee Shimamoto, ukiacha wewe kujitengenezea heshima kubwa ndani ya eneo hili lakini uhalisia ni kwamba kila mtu huwa ana upande wake wa pili wa shilingi ambao anaujua yeye tu. Upande huo kila mtu huwa hataki kabisa watu wengine wautambue kwa sababu inakuwa ni hatari kama watu wakifanikiwa kuujua na upande huo ndio ambao umenifanya mimi nisafiri kutoka kwangu na kuja hapa kwako siku ya leo tena majira ya usiku wa manane kama huu”
“Ukiwa na maana ipi labda?”

“Mhhhh mzee wangu sisi wote tunajua historia huwa haisemi ukweli siku zote, historia mara nyingi huwa inaelezea kile ambacho mwandishi anataka watu wakipate, wakisome ama kukisikia na sio ule ukweli ambao upo ndani ya nyakati hizo. Hata mimi kipindi nipo mdogo nilikuwa mtu wa kuipenda historia mpaka pale ambapo nilikuja kugundua kwamba sehemu kubwa ya historia ni uongo kwa sababu mengi ambayo jamii ilitakiwa kuyapata hayajaandikwa bali yameandikwa yale ambayo yana maslahi kwa wahusika tu na hata yale ambayo yameandikwa basi kuna namna yamepigwa pigwa kona nyingi’’
“Hayo maelezo yako yana maana gani kwangu?”

“Mimi na wewe wote tunajua kwamba wewe sio Shimamoto” mzee yule alioyesha mshtuko wa wazi kwenye macho yake kwa sababu siri ambayo alikuwa nayo hata mwanae wa damu hakuwa anaijua hivyo alishangaa kuona mtu mkubwa tena waziri wa mambo ya nje ya taifa lake alionekana kumjua bwana huyo.
“Mheshimiwa nadhani uliko toka umekunywa pombe japo simaanishi kukukosea heshima”

“Nilitegemea utaniambia hayo, nisikilize mzee, mimi kuja huku kwako kama ningetaka kukukamata basi ningewasiliana na waziri wa mambo ya ndani ningekuja na msafara wa polisi hata zaidi ya miatano ila mpaka nimekuja mwenyewe ujue kwamba nataka kuwa na mazungumzo binafsi na wewe bwana Akari Sasaki” jina ambalo lilitajwa ndilo ambalo lilimnyanyua kwa kasi pale ambapo alikuwa ameketi mpaka ukutani ambapo aliuchomoa upanga mpaka kwenye shingo ya Shinto Haru.
“Umekosea sehemu ya kuja, unaanza kunitajia majina ya watu wa ajabu ambao siwajui. Sijajua kama kuna mtu gani amekutuma hapa kwangu ila nakuomba uondoke haraka kwa sababu naenda kukuua ndani ya muda mfupi ambao unafuata”

“Mhhhhhh kwamba utamuua waziri wa mambo ya nje wa Japan? Jibu ni hapana kwa sababu una binti wa kumtunza wewe. Naweza kuwa nimekuja kwa siri hili eneo ila haimaanishi kwamba watu wangu hawana taarifa za mimi kuja huku hivyo kama nikipotea kwa masaa kadhaa bila kupatikana hata kwa simu maswali yataanza kuulizwa na unajua kabisa hapa ni serikali ya Japan itakujia hapa na mwisho wa siku siri yako itajulikana. Unajua maisha ambayo atayaishi binti yako ukinyongwa? Unaelewa maisha yanavyokuwa hapa duniani ikijulikana kwamba wewe ni mtoto wa msaliti? Angalau angekuwa mtoto wa kiume ila yule ni binti tena mrembo, nadhani unaniele….”
“Wewe mshenzi usije ukalitaja jina la binti yangu kwenye mdomo wako tena hata kwa bahati mbaya’’

“Safi, sasa kama unataka hilo litokee basi acha kubweka bweka hapa, nitolee huo upanga wako kisha ukae chini unisikilize kwa umakini mkubwa’
“Umefanikiwa vipi kunijua mimi wakati jambo hili nililizika kwa miaka mingi ambayo imepita?”
“Kama nilivyo kwambia bwana Shimamoto, mimi niliwahi kuipenda historia mpaka nilipo gundua kwamba historia inadanganya, historia ina mapungufu mengi ila kwa sababu ya ujinga wa watu na uvivu huwa inawafanya watu kukubali kila ambalo limeandikwa au ambalo linasemwa kutoka kwenye historia ya kitu husika. Ila mimi sio kama hao, mimi sipo kama watu wengine walivyo kwahiyo nikikutana na historia ikanivutia huwa naamua kuifuatilia mwenyewe kwa sababu huwa naamini kwamba kuna baadhi ya taarifa huwa zinaondolewa kwa sababu maalumu na ndilo jambo ambalo lilinivutia kufuatilia kisa chako wewe”
“Unaonekana kuwa mtu makini!”
“Ni kweli, mimi ni mtu makini”

“Sasa ulijua vipi kama kuna taarifa zitakuwa zinakosekana kwenye hii historia yangu ambayo taifa liliamua kujumuisha kwamba mimi nimekufa?”
“Mimi ni mwanasiasa ndugu yangu hivyo naelewa vyema namna siasa inafanya kazi. Kwenye mambo mhimu ya serikali ama kwa taifa sio kila mtu huwa yanamvutia au yana faida kwake. Historia yako ya kuua wanasiasa haikuwa mbaya kwa kila mtu, kuna watu walinufaika na wewe kuwaua baadhi ya wanasiasa ambao walikuwa ni tishio na hatari kwao. Sasa unahisi watu kama hao wangechukizwa na uwepo wako? Sio kweli, kuna watu walikuwa ni mashabiki zako wakubwa japo wewe haukuwahi kulijua hilo. Uwepo wa watu wa namna hii wasingevutiwa na kuandika kila jambo kwenye historia ndiyo maana habari yako ilizimwa ghafla maana yake ni kwamba kuna watu wengi walinufaika na yale ambayo wewe uliyafanya, hiyo ina maana kwamba kama walikuwepo watu wa namna hiyo maana yake ni kwamba lazima kuna baadhi ya taarifa wangezificha kwa ajili ya faida zao za baadae ndiyo sababu kubwa hawakutaka hii historia iandikwe kiundani zaidi kwani walikuwa na imani kwamba hata wao wangeweza kuja kutumia njia yako wewe. Kama ingeandikwa historia nzima maana yake serikali na raia wangekuja kuwa makini na hata kama mtu mwingine angehitaji kuitumia njia kama ile asingefanikiwa kwa sababu ingekuwa inachunguzwa kwa ukubwa” maelezo yake yalionyesha kabisa kwamba hakufika hapo kwa kubahatisha bali alikuwa ni mtu ambaye alijipanga kwa undani zaidi.

26 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 27.
ENDELEA.......

“Kama nimekuelewa ni kwamba moja ya hao wanasiasa ambao walikuwa ni mashabiki zangu wakubwa na wewe upo?”
“Nimetumia lugha ya fasihi ndugu yangu hivyo unaweza ukaelewa kwa namna ambayo unaitaka wewe”
“Mana yake jibu ni ndiyo, sasa unaweza ukaniambia kwanini upo hapa?”
“Nataka kuzirudia zama zako” alitoa jibu lake akiwa anashushia kahawa na moto ukiwa unawaka pembeni yao kuweza kutuliza baridi lilimshangaza Shimamoto.
“Unamaanisha kwamba unataka kuanza kuua wanasiasa wenzako?”
“Ndiyo”
“Hii njia sio salama, haijawahi kuwa nzuri na haijawahi kuwa na mwisho mwema”
“Najua hayo yote ndiyo maana nataka kuitumia”

“Kwa mtu mkubwa kama wewe kutaka kutumia njia kama hii maana yake ni kwamba unataka sehemu kubwa zaidi ya taifa hili. Usiniambie kwamba unataka kuwa raisi!”
“Nani anaweza kujua, maisha hayatabiriki kabisa mzee wangu”
“Sikushauri hilo jambo kwa sababu ni hatari lakini pia sielewi sababu ya wewe kuwepo hapa kwani mimi siwezi kuifanya hiyo kazi tena kwenye maisha yangu”
“Nani kakwambia nataka uifanye hii kazi?”
“Sasa kipi kimekuleta hapa?”
“Kwenye kutembea kwangu duniani, nimekutana na watu wengi, nimepata marafiki wengi lakini pia nimejifunza makosa mengi ambayo yanafanywa na wanadamu hususani kwenye historia yako ndiyo maana nataka niyafanye mambo kwa namna tofauti na yalivyo zoeleka”
“Nakusikiliza”

“Nina kijana wa rafiki yangu mmoja ambaye sitakwambia kwamba ni nani ndiye ambaye nataka aje hapa kwako baada ya muda, utakuwa na kazi kubwa mbili. Kazi ya kwanza kijana huyu atakuwa anaishi hapa kwako kwa siri kubwa kama hifadhi na jambo la pili nahitaji umtengeneze awe kiumbe hatari zaidi kama ambavyo uliwahi kuwa wewe enzi za ujana wako”
“Sijakuelewa, unataka mimi nitengeneze muuaji?”
“Sio kumtengeneza, huyu mtu tayari ni muuaji wa kutisha ila kuna vitu ambavyo nataka uviongezee kwake na wakati huo atakuwa anaendelea kufanya kazi yangu”
“Kwa maana hiyo unataka kumtumia huyu kijana kuua wanasiasa wenzako halafu akimaliza awe anakuja kujificha nyumbani kwangu huku nikiwa nampatia mazoezi?”

“Napenda wazee waelewa kama wewe kwa sababu mnafanya maisha yanakuwa rahisi zaidi”
“Hapana, siwezi kuifanya hiyo kazi, nilisha badilika kwenye maisha yangu hivyo siwezi kuendelea kutengeneza mtu ambaye najua kabisa atakuwa sehemu ya matatizo ya ulimwengu na wala sipo tayari kwa ajili ya kumhifadhi muuaji ndani ya makazi yangu”
“Mzee wangu basi nina imani hii hadithi yangu mimi na wewe haitakuwa na mwisho mwema”
“Ukiwa na maana ya kwamba?”
“Mfikirie binti yako kabla ya kukurupuka kufanya maamuzi ya mwisho. Mimi sijaja hapa kwa ajili ya kukubemebeleza kufanya hili wala sikuombi ila kama ukikataa kufanya hivyo basi nadhani unaelewa kwamba ni jambo gani linafuata”
“Unajua waziri, kwa miaka hii ambayo nimeishi huku, imekuwa miaka yangu bora zaidi mimi kama mwanadamu ambaye nipo hai kwa sababu nimeishi kwa amani na Mungu amenibariki nimepata binti ambaye nampenda sana ila naona kila kitu kimepotea tu baada ya wewe kukanyaga kwenye mlango wangu. Naona kabisa naenda kupoteza kila ambacho nimekipigania kwa hii miaka yangu”

“Ndiyo maana unatakiwa kufanya lililo jema”
“Najua kabisa kwamba hili kwa upande wangu halitaisha vizuri”
“Hayo ulitakiwa kuyawaza kabla ya wewe kukurupuka mara ya kwanza kukubali kuwa muuaji. Kumbuka ni wewe ambaye ulisababisha familia yako ikaingia kwenye hatari na kuuawa huku wewe ukiikimbia hivyo angalau kwa mara moja fanya jambo ambalo ni sahihi ili usije ukamletea matatizo binti yako. Najua kwamba hili kweli linaweza lisiishe vizuri kwako lakini lazima litaisha vizuri kwa binti yako. Wewe maisha yako ulisha yapoteza tangu zamani hivyo ulijua kabisa kuna siku itafika utatakiwa kulipa na muda wenyewe ndio huu kuanzia sasa”
“Anakuja lini huyo kijana na anatokea wapi?”

“Kuhusu anapo tokea inategemea na yeye kama ataamua kukujibu na kama akifanya hivyo basi hata mtoto wako hatakiwi kujua lolote kumhusu huyo mtu na mtu ambaye namtuma hapa hatakiwi kujulikana wala haupaswi kuuliza hilo na siku nikitambua umefanya hivyo nitakufuata mimi mwenyewe hapa na nadhani hatutakuwa na mazungumzo bora”
“Kwa leo naweza kusema umeshinda ila pia hata wewe unatakiwa kutambua athari ya hili jambo ambalo unalianzisha”
“Unahisi sizijui athari zake?”
“Unaweza ukawa unahisi kwamba unajua kwa sababu kwa sasa unaendeshwa na hisia za kuwa kiongozi mkubwa lakini nina uhakika kwamba haupo tayari kuweza kuyapokea matokeo yake”
“Mimi na wewe tutaona bwana Shimamoto, siku nikiingia Ikulu nitakuja hapa kukukumbusha”
“Mhhhhh ni kwanini unamtumia kijana wa nje kufanya hii kazi?”

“Kwa sababu moja kati ya makosa ambayo yalifanyika huko nyuma ni kutumia watu wa ndani ambao wanatambulika kirahisi hivyo nikimtumia mtu wa mbali wakati wanapambana kutafutana miongoni mwetu hawatakuwa na wazo kwamba mhusika ni nani”
“Unaweza kwenda, nitaifanya kazi yako kama ambavyo umehitaji ifanyike” wawili hao walipeana mikono baada ya kumaliza mazungumzo ya kiutu uzima. Mheshimiwa Shinto Hiru alitembea mpaka mlango kisha akasimama na kugeuka nyuma
“Hakikisha hakuna mtu anajua kabisa kwamba huyu kijana anaishi hapa hata kwa bahati mbaya, inatakiwa kuwa siri yako na kwa wafanyakazi wako ambao unawaamini na kama kuna mtu atauliza basi ijulikane kama kijana huyo atakuwa hapa kwa ajili ya kupewa msaada tu na sio jambo lolote lingine” aliitikia kwa kichwa akionyesha kukubaliana na waziri huyo. Hivyo ndivyo kwa mara ya kwanza Jaden alivyo fanikiwa kuingia ndani ya jiji la Akita ambako simu ilikuwa imefika na kumtaka aweze kurudi ndani ya taifa la Tanzania kwa ajili ya kazi ya bosi wake.


Jaden baada ya kufika Japan hakwenda moja kwa moja Akita, aliingia Tokyo kwanza ambako alifanya mauaji ya wanasiasa wawili ndipo akakimbilia huko Akita ambako alianza kuishi kama kijana ambaye alikuwa anahitaji msaada na hata wale watu kadhaa ambao walibahatika kumuona, hawakuweza kumdhania kwa lolote, alionekana kuwa mtu mwema mbele yao ila hawakujua aina ya kiumbe ambacho kiliingia kwenye jamii yao. Bwana huyo alianza kufanya mazoezi ya hatari wakati akiwa huko, alikuwa anafundishwa mapigano ya zama za zamani za mashujaa wa taifa hilo kutoka kwa Shimamoto hali ambayo ilizidi kumfanya kuwa mtu hatari.

Siku zote huwa wanasema sumaku zinapokutaka hasi na chanya ni lazima zivutane kwa namna yoyote ile, ndivyo ambavyo ilikuwa kwa Jaden pamoja na Aimi Shimamoto. Ustaarabu wa kuigiza wa Jaden ulimfanya binti huyo kuvutiwa naye, huenda ni kwa sababu ya upweke na kubaniwa kutowajua wanaume pia ulichangia binti huyo kuweza kumpenda na kuhitaji kuwa na mwanaume wa kazi huyo. Mara ya kwanza alijitahidi kumkwepa binti huyo akihofia kuweza kuharibu kazi lakini siku zote hakuna mwanaume mgumu mbele ya mwanamke mrembo. Lilikuwa ni suala la muda mfupi tu kupita mpaka watu hao wawili walipo amua kujigeuza kuwa mwili mmoja. Aimi alilionja joto la bwana huyo, akachanganyikiwa, ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza hivyo akili ni kama zilimhama, alihitaji kila wakati kuwa karibu naye, alitamani awe mwanaume wake wa maisha na watangaze kabisa kuwa pamoja lakini hilo ni jambo ambalo lisingewezekana kwa wakati huo ama hata milele kwa sababu baba yake asingeruhusu mwanae kuolewa na muuaji ambaye siku zake za kuishi zilikuwa zinahesabika.

27 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 27.
ENDELEA.......

“Kama nimekuelewa ni kwamba moja ya hao wanasiasa ambao walikuwa ni mashabiki zangu wakubwa na wewe upo?”
“Nimetumia lugha ya fasihi ndugu yangu hivyo unaweza ukaelewa kwa namna ambayo unaitaka wewe”
“Mana yake jibu ni ndiyo, sasa unaweza ukaniambia kwanini upo hapa?”
“Nataka kuzirudia zama zako” alitoa jibu lake akiwa anashushia kahawa na moto ukiwa unawaka pembeni yao kuweza kutuliza baridi lilimshangaza Shimamoto.
“Unamaanisha kwamba unataka kuanza kuua wanasiasa wenzako?”
“Ndiyo”
“Hii njia sio salama, haijawahi kuwa nzuri na haijawahi kuwa na mwisho mwema”
“Najua hayo yote ndiyo maana nataka kuitumia”

“Kwa mtu mkubwa kama wewe kutaka kutumia njia kama hii maana yake ni kwamba unataka sehemu kubwa zaidi ya taifa hili. Usiniambie kwamba unataka kuwa raisi!”
“Nani anaweza kujua, maisha hayatabiriki kabisa mzee wangu”
“Sikushauri hilo jambo kwa sababu ni hatari lakini pia sielewi sababu ya wewe kuwepo hapa kwani mimi siwezi kuifanya hiyo kazi tena kwenye maisha yangu”
“Nani kakwambia nataka uifanye hii kazi?”
“Sasa kipi kimekuleta hapa?”
“Kwenye kutembea kwangu duniani, nimekutana na watu wengi, nimepata marafiki wengi lakini pia nimejifunza makosa mengi ambayo yanafanywa na wanadamu hususani kwenye historia yako ndiyo maana nataka niyafanye mambo kwa namna tofauti na yalivyo zoeleka”
“Nakusikiliza”

“Nina kijana wa rafiki yangu mmoja ambaye sitakwambia kwamba ni nani ndiye ambaye nataka aje hapa kwako baada ya muda, utakuwa na kazi kubwa mbili. Kazi ya kwanza kijana huyu atakuwa anaishi hapa kwako kwa siri kubwa kama hifadhi na jambo la pili nahitaji umtengeneze awe kiumbe hatari zaidi kama ambavyo uliwahi kuwa wewe enzi za ujana wako”
“Sijakuelewa, unataka mimi nitengeneze muuaji?”
“Sio kumtengeneza, huyu mtu tayari ni muuaji wa kutisha ila kuna vitu ambavyo nataka uviongezee kwake na wakati huo atakuwa anaendelea kufanya kazi yangu”
“Kwa maana hiyo unataka kumtumia huyu kijana kuua wanasiasa wenzako halafu akimaliza awe anakuja kujificha nyumbani kwangu huku nikiwa nampatia mazoezi?”

“Napenda wazee waelewa kama wewe kwa sababu mnafanya maisha yanakuwa rahisi zaidi”
“Hapana, siwezi kuifanya hiyo kazi, nilisha badilika kwenye maisha yangu hivyo siwezi kuendelea kutengeneza mtu ambaye najua kabisa atakuwa sehemu ya matatizo ya ulimwengu na wala sipo tayari kwa ajili ya kumhifadhi muuaji ndani ya makazi yangu”
“Mzee wangu basi nina imani hii hadithi yangu mimi na wewe haitakuwa na mwisho mwema”
“Ukiwa na maana ya kwamba?”
“Mfikirie binti yako kabla ya kukurupuka kufanya maamuzi ya mwisho. Mimi sijaja hapa kwa ajili ya kukubemebeleza kufanya hili wala sikuombi ila kama ukikataa kufanya hivyo basi nadhani unaelewa kwamba ni jambo gani linafuata”
“Unajua waziri, kwa miaka hii ambayo nimeishi huku, imekuwa miaka yangu bora zaidi mimi kama mwanadamu ambaye nipo hai kwa sababu nimeishi kwa amani na Mungu amenibariki nimepata binti ambaye nampenda sana ila naona kila kitu kimepotea tu baada ya wewe kukanyaga kwenye mlango wangu. Naona kabisa naenda kupoteza kila ambacho nimekipigania kwa hii miaka yangu”

“Ndiyo maana unatakiwa kufanya lililo jema”
“Najua kabisa kwamba hili kwa upande wangu halitaisha vizuri”
“Hayo ulitakiwa kuyawaza kabla ya wewe kukurupuka mara ya kwanza kukubali kuwa muuaji. Kumbuka ni wewe ambaye ulisababisha familia yako ikaingia kwenye hatari na kuuawa huku wewe ukiikimbia hivyo angalau kwa mara moja fanya jambo ambalo ni sahihi ili usije ukamletea matatizo binti yako. Najua kwamba hili kweli linaweza lisiishe vizuri kwako lakini lazima litaisha vizuri kwa binti yako. Wewe maisha yako ulisha yapoteza tangu zamani hivyo ulijua kabisa kuna siku itafika utatakiwa kulipa na muda wenyewe ndio huu kuanzia sasa”
“Anakuja lini huyo kijana na anatokea wapi?”

“Kuhusu anapo tokea inategemea na yeye kama ataamua kukujibu na kama akifanya hivyo basi hata mtoto wako hatakiwi kujua lolote kumhusu huyo mtu na mtu ambaye namtuma hapa hatakiwi kujulikana wala haupaswi kuuliza hilo na siku nikitambua umefanya hivyo nitakufuata mimi mwenyewe hapa na nadhani hatutakuwa na mazungumzo bora”
“Kwa leo naweza kusema umeshinda ila pia hata wewe unatakiwa kutambua athari ya hili jambo ambalo unalianzisha”
“Unahisi sizijui athari zake?”
“Unaweza ukawa unahisi kwamba unajua kwa sababu kwa sasa unaendeshwa na hisia za kuwa kiongozi mkubwa lakini nina uhakika kwamba haupo tayari kuweza kuyapokea matokeo yake”
“Mimi na wewe tutaona bwana Shimamoto, siku nikiingia Ikulu nitakuja hapa kukukumbusha”
“Mhhhhh ni kwanini unamtumia kijana wa nje kufanya hii kazi?”

“Kwa sababu moja kati ya makosa ambayo yalifanyika huko nyuma ni kutumia watu wa ndani ambao wanatambulika kirahisi hivyo nikimtumia mtu wa mbali wakati wanapambana kutafutana miongoni mwetu hawatakuwa na wazo kwamba mhusika ni nani”
“Unaweza kwenda, nitaifanya kazi yako kama ambavyo umehitaji ifanyike” wawili hao walipeana mikono baada ya kumaliza mazungumzo ya kiutu uzima. Mheshimiwa Shinto Hiru alitembea mpaka mlango kisha akasimama na kugeuka nyuma
“Hakikisha hakuna mtu anajua kabisa kwamba huyu kijana anaishi hapa hata kwa bahati mbaya, inatakiwa kuwa siri yako na kwa wafanyakazi wako ambao unawaamini na kama kuna mtu atauliza basi ijulikane kama kijana huyo atakuwa hapa kwa ajili ya kupewa msaada tu na sio jambo lolote lingine” aliitikia kwa kichwa akionyesha kukubaliana na waziri huyo. Hivyo ndivyo kwa mara ya kwanza Jaden alivyo fanikiwa kuingia ndani ya jiji la Akita ambako simu ilikuwa imefika na kumtaka aweze kurudi ndani ya taifa la Tanzania kwa ajili ya kazi ya bosi wake.


Jaden baada ya kufika Japan hakwenda moja kwa moja Akita, aliingia Tokyo kwanza ambako alifanya mauaji ya wanasiasa wawili ndipo akakimbilia huko Akita ambako alianza kuishi kama kijana ambaye alikuwa anahitaji msaada na hata wale watu kadhaa ambao walibahatika kumuona, hawakuweza kumdhania kwa lolote, alionekana kuwa mtu mwema mbele yao ila hawakujua aina ya kiumbe ambacho kiliingia kwenye jamii yao. Bwana huyo alianza kufanya mazoezi ya hatari wakati akiwa huko, alikuwa anafundishwa mapigano ya zama za zamani za mashujaa wa taifa hilo kutoka kwa Shimamoto hali ambayo ilizidi kumfanya kuwa mtu hatari.

Siku zote huwa wanasema sumaku zinapokutaka hasi na chanya ni lazima zivutane kwa namna yoyote ile, ndivyo ambavyo ilikuwa kwa Jaden pamoja na Aimi Shimamoto. Ustaarabu wa kuigiza wa Jaden ulimfanya binti huyo kuvutiwa naye, huenda ni kwa sababu ya upweke na kubaniwa kutowajua wanaume pia ulichangia binti huyo kuweza kumpenda na kuhitaji kuwa na mwanaume wa kazi huyo. Mara ya kwanza alijitahidi kumkwepa binti huyo akihofia kuweza kuharibu kazi lakini siku zote hakuna mwanaume mgumu mbele ya mwanamke mrembo. Lilikuwa ni suala la muda mfupi tu kupita mpaka watu hao wawili walipo amua kujigeuza kuwa mwili mmoja. Aimi alilionja joto la bwana huyo, akachanganyikiwa, ilikuwa ndiyo mara yake ya kwanza hivyo akili ni kama zilimhama, alihitaji kila wakati kuwa karibu naye, alitamani awe mwanaume wake wa maisha na watangaze kabisa kuwa pamoja lakini hilo ni jambo ambalo lisingewezekana kwa wakati huo ama hata milele kwa sababu baba yake asingeruhusu mwanae kuolewa na muuaji ambaye siku zake za kuishi zilikuwa zinahesabika.

27 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
Umetisha mtaalam FEBIANI BABUYA
 
STORY: JUMBA JEUSI
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

EPISODE 28.
ENDELEA.......

Jaden aliendelea kuifanya kazi yake kwa umaridadi huku akiwa karibu zaidi kimapenzi na mtoto wa Shimamoto. Kama ambavyo siku zote wahenga waliwahi kusema kwamba hakuna siri baina ya watu wawili, siri ni ya mtu mmoja tu wakiwa wawili maana yake ni kwamba mmoja anatakiwa kufa nayo. Yalianza kusikika maneno kwamba watu hao wawili walikuwa wamezama hubani jambo ambalo lilimkera mno Shimamoto japo alilikaushia, hakupenda kufanya hivyo ila ilimlazimu kwa sababu kuu mbili; sababu ya kwanza mtu ambaye alimuweka huyo kijana hapo alikuwa ana uwezo wa kumharibia maisha yake yote kwa siku moja tu lakini sababu ya pili ni kwamba hakuwa mtu aliyekuwa anaendeshwa kwa mihemko kwenye ufanyaji wa maamuzi kwahiyo alitaka kujipa muda aweze kuthibitisha hilo kwa waziri wa mambo ya nje.

Kama angeweza kulithibitisha hilo kwa waziri ambaye ndiye alimpatia jukumu la kumpokea kijana huyo ungekuwa mwanzo wa Jaden kuondolewa huko. Lakini siku zote sio kila nyakati mambo yanaenda kama ambavyo wewe unataka yaende, kuna muda asili inakuchagulia vile inataka maisha yako yawe na ndilo jambo ambalo lilikuwa linamtokea mheshimiwa huyo. Akiwa kwenye hesabu za kufanya uchunguzi hata yeye kuna watu walikuwa wanamfanyia uchunguzi bila yeye kujua na jambo hilo lilikuwa linafanywa na Jaden mwenyewe. Mwanaume huyo alitambua kabisa kwamba mzee huyo alikuwa amejua kuhusu yeye na mwanae ila alikuwa anasubiria muda sahihi tu uweze kufika kabla hajaharibu jambo hilo ambalo lingemharibia maisha Jaden na huenda angeuawa kwa sababu angekuwa ameharibu kazi hivyo ilitakiwa yeye ndiye amuwahi mzee huyo.
Kumuwahi kwake ilikuwa ni kumtengenezea kesi ambayo haikuwa ikimhusu kabisa, kesi ya usaliti kwa waziri wa mambo ya nje wa Japan na ndipo mwisho wa Shimamoto ulipo anzia huku akiwa anamfutilia kijana huyo apate ushahidi akasahau kujilinda yeye. Shimamoto alitakiwa kufa na huo mchoro ulichorwa na Jaden mwenyewe kwa mkono wake, mzee huyo alikuwa anaenda kuwa tatizo kwa upande wake lakini alitakiwa kumalizana naye bila kuacha ushahidi wa aina yoyote ile. Ni wakati ambao alikuwa ameiva kwenye upande wa mazoezi na mzee huyo ndiye alikuwa mwalimu wake hivyo wawili hao walikuwa wanatambuana vizuri kabisa.

Namna ya kumuua mzee huyo ilikuwa ni kumtengenezea kesi ya usaliti, alitaka kumfanya mzee huyo aonekane kama anamsaliti waziri wa mambo ya nje. Usaliti wake kwa kiongozi huyo ndio ambao ungefanya jambo hilo kukamilika kwa urahisi zaidi hivyo aliandaa mkutano na viongozi wa kisiasa kadhaa ambapo alitumia jina la mzee huyo kukutana nao kwa kuwapa ahadi ya kwamba mzee huyo kwa sababu anaheshimika Akita angeutumia umaarufu wake kuwasaidia kuupata uraisi mbele ya mpinzani wao ambaye alikuwa ni waziri wa mambo ya nje. Mzee huyo aliahidi kwamba alikuwa anaweza kuzishawishi mpaka familia zenye asili kama yake kuweza kutekeleza kazi hiyo na ikafanyika kwa ubora wa hali ya juu, kuwa na familia ambazo zinaheshimika ulikuwa ni mwanzo bora kabisa wa kuwashika na kuwashawishi wananchi wengi lakini ubaya ni kwamba hayo yote yalikuwa yanafanyika bila mzee mwenyewe kuwa na uelewa wowote juu ya mambo hayo.

Taarifa hiyo ilifika kwenye mkono wa Shinto Hiru, aliipata taarifa hiyo kwenye wakati mbya. Ni wakati ambao yeye hakutegemea kama mtu huyo angeweza kutenda ujinga kama huo kwake hivyo hakutaka hata kulifuatilia kwa undani jambo hilo, alipojua tu kwamba jina la Shimamoto limetajwa upande wa pili kutoka kwa wapinzani wake, alimkabidhi kazi hiyo Jaden mwenyewe aweze kumuua mzee huyo bila kuweza kuacha ushahidi wa aina yoyote ile, jambo ambao yeye ndiye ambaye alikuwa analihitaji zaidi liweze kufanyika kwa namna hiyo kwa sababu ni namna ambayo yeye alikuwa anaitaka.

Usiku mmoja mzee Shimamoto akiwa kwenye sehemu yake ya siri ya kuweza kufanyia meditation na mazeozi ya siri, sehemu ambayo mara nyingi alikuwa akiitumia yeye na Jaden kufanyia mazoezi ili watu wengine wasishtuke, sehemu ambayo ni watu wake wa kuhesabika walikuwa wanaruhusiwa kuweza kuingia huko, alihisi ujio wa mtu. Mzee huyo alikuwa amefumba macho yake akiwa amezama ndani ya tahajudi kwa ajili ya kutengeneza usawa wa mwili na utulivu wa akili. Alikuwa mara nyingi anafanya hivyo akiwa anahitaji kufanya maamuzi magumu ama maamuzi ambayo mwisho wake usingekuwa mzuri ndiyo maana hakuwa anahitaji kukurupuka.
Wakati anayafumbua macho yake aligundua kwamba mtu ambaye alihisi kwamba amefika hapo alikuwa amesimama umbali kadhaa nyuma yake, haikuwa kawaida yeye mtu kumfikia mpaka eneo la karibu kama hilo asiwe na taarifa hivyo alishtuka sana na jambo ambalo lilimshtua zaidi ni kwamba aliyekuwa pale alikuwa ni Jaden. Hakuwa anaruhusiwa kuwepo lile eneo kama sio muda wa mazoezi na kama hajapewa ruhusa maalumu ya kuweza kufika eneo lile hivyo ule ujio wake haukuonekana kuwa mwema kwa mzee Shimamoto.

“Mhhhhhhhhhhhh sio kawaida mtu ufike mpaka hatua za karibu namna hii halafu mimi nisiwe na taarifa juu ya wewe kuweza kuwepo hapa. Imewezekanaje hii?” aliuliza kwa mshangao akiwa anasimama na kulikunja vazi lake vizuri kwenye mikono.
“Haya yote nimejifunza kwako mzee, mara ya kwanza wakati naanza kufanya mazoezi hapa niligundua kwamba mwili wangu ulikuwa bado mzito hivyo nikawa kila siku tukimaliza mazoezi basi najifungia ndani naanza kuyafanyia kazi mwenyewe jambo ambalo limenifanya baadae nikawa mwepesi na nikawa na uwezo wa kuudhibiti mwili wangu ndiyo maana mpaka nafika hapa haukujua kama kuna mtu”
“Kwanini ulifanya haya bila kunipa taarifa?”
“Nadhani kila mwalimu huwa anafurahi zaidi akimuona mwanafunzi wake anafanya vyema zaidi ya yale matarajio yake ya mwanzo ila sidhani kama kwa upande wako umefurahishwa na hili”

“Bado haujanijibu swali langu”
“Kwa sababu nilijua siku kama ya leo itakuja”
“Unataka kusemaje?”
“Nadhani unajua kwanini nipo hapa muda huu” mzee Shimamoto alitabasamu
“Mimi nimetoa taarifa kwa watu wangu kwamba leo usingekuwepo hapa mpaka kesho ili kukupa nafasi ya kwenda kufanya mauaji kama ulivyo zoea, nilitarajia ungerudi ila sio kwa haraka namna hii na hata kama ingekuwa haraka basi haukutakiwa kuja hapa”
“Kwa sababu leo hakukuwa na mtu yeyote wa kwenda kumuua”
“Unaongelea nini?”
“Nilikudanganya”
“Kivipi?”
“Leo sijaenda popote pale”
“Whaaaaaaaaa?”

“Yeah, nilitaka watu waamini mimi sipo na kwa sababu ulikuwa umeanza kuniamini basi hata haukutaka kuhakiki kwamba ni kweli nimeondoka”
“Kwahiyo umefanya hayo ili ujaribu kuniua sio?”
“Sio kujaribu, nipo hapa kwa ajili ya kukuua”
“Hahahah hahahaha hahahah kipi kimekupata bwana mdogo! Bosi wako anajua kama unayafanya haya?”
“Yeye ndiye kanituma mimi nije kukuua wewe”

“Kuniua hiyo ni ndoto kwako ila najua bosi wako hawezi kukutuma na ndiyo sababu itanifanya mimi nisikuue wewe kwakuwa itanilazimu nitoe majibu kwake. Kwahiyo hili nitahesabia kama halikuwahi kutokea, nenda kalale”
“Mambo hayaendi hivyo mzee wangu, kama kweli asingekuwa amenituma yeye basi hata mimi nisingekuwa na sababu ya kukuua kwa sababu lazima nitaulizwa maswali ambayo nitatakiwa kuyajibu na kushindwa kuyajibu basi ataniua”

“Kwanini afikie hatua ya kufanya maamuzi kama haya”
“Sababu nadhani unaijua”
“Unajua kwamba najua kuhusu wewe na Aimi?”
“Ndiyo”
“Kwahiyo ni kweli”
“Nasikitika kusema ni kweli mzee” Shimamoto aliukunja uso wake na kuuma meno.
“Umefanya kosa ambalo siwezi kukusamehe kwenye maisha yangu yote”
“Hata mimi wakati hili linaanza kutokea nilijua kabisa kwamba hautakuja kunisamehe kamwe”
“Na bado ukafanya?”

“Kwa sababu mwanao alikuwa anataka iwe hivyo, alilazimisha mpaka nikawa sina namna nyingine”
“Mwanangu hawezi kumpenda mtu kama wewe, mwanangu anatakiwa kuolewa na moja ya familia kubwa na zenye heshima ndani ya Japan na sio mtu mpuuzi wa namna yako”
“Kwa sababu ni muuji au kwa sababu mimi ni mweusi”
28 inafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom