bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
Simulizi:John ze Mwizi
Na: Humph Isack
Whatsapp: 0742817066
Sehemu ya Kwanza
Koooooh!! koooh!! koooh!!" ilikuwa ni sauti ya babuyake john akikohoa kwa nguvu wakati amejilazakitandani,kikohozi kilitoka kikavu kilichopolelekea mpaka mwili wake uruke ruke na kufanya kitandakilichochoka kilalamike kutokana na msoto kinaopitia"Amina naomba uniitie John haraka". Babu yake john alimuagiza Amina ambaye alikuwa ni mke wajohn na walikuwa wakiishi watatu tu katika nyumbayao ya tope,yote hayo ni baada ya wazazi wa johnkufariki kipindi akiwa kijana mdogo na kubakimikononi mwa mzee huyo aliyefahamika kijijini hapo kama Mzee Ndasi Mzee ndasi hakuwa na kipato cha kutosha kumuduMaisha yake na mjukuu wake hivyo hata masomoya john alishindwa kuyamudu kwani hakuwezakununua sare za shule wala madaftari kwaajili yamjukuu wake ispokuwa aliweza kupata chakula chakumtosha yeye na john pekee.
Baada ya kipindi kirefu kupita john alianzakujishughulisha na mazao ya chakula katika shambala babu yake na hivyo kuifanya familia iwezekujiendesha walau katika familia zenye hali yakawaida.Ilifikia kipindi john akabalehe na waswahili hupendakuziita kuwa ni balehe za kwanza kamatunavyoelewa balehe hizi za mwanzo zinavyokuwana msisimko wa hali ya juu kiasi kwamba mhusikaakijichanganya tuu basi anapotelea kwenye hubanzito yenye kina haswaa.
Ndivyo ilivyotokea kwa John bin Ndasi ambaye akiliyake haikutulia nyumbani,ikaanza kutafuta visichanavilivyochipukia kama yeye na kwa bahati akampata Amina kwa kusota mno lengo ikiwa atulizemihemko yake na mshawasha kisha atokomeee bilakujua kuwa amependa kusikopendeka na kadri siku zilivyoyoyoma alizidi kuzama zaidi na zaidi kwabinti yule wa rika lake na kusahau mipango yotealiyokiwekea kabla ya kujihusisha na mahusiano yakimapenzi na binti Amina.
Walianza penzi lao kwa siri na mwisho marafikiwakatambua,siri haikuwa siri tena ikafika kwawazazi wa Amina ambao hawa hawakuwa na dogokijijini pale, waliamini mzee Ndasi ni kigagula yaanimchawi kutokana na itikadi zake zilivyokuwa.Kwakuwa walimfahamu vyema mzee huyo wakaanzamoja kwa moja kumuonya binti yao kuwa ile familiasi nzuri hata kidogo kwahiyo aachane nayo maramoja,lakini binti Amina alisikia kushoto yakatokeakulia usishangae ni kwanini ila sababu ni moja Johnalikuwa ni chaguo la kwanza na mwanaume wakwanza kwa Amina.
Siku zilikatika na penzi likazidi kunoga haswaa nahatimaye likamfikia Mzee wa Wazee yaani kiboko yaWazee wengine ambaye ni Mzee Ndasi,kamakawaida yake alipitia kwanza machozi ya simbaama waswahili wanaita majisafi au pyua na kamahujanielewa naamanisha nini nd'o nakupa jibu kuwani ile pombe iliyopigwa marufuku na serikali nakuwa vita kubwa kati ya wauzaji na Polisi kilakukicha.Hauwezi kuamini kama katika kijiji cha akina john bin Ndasi hakuna aliyelifuatilia suala lile zaidi nazaidi walijumuika wote kupata machozi yasimba.Basi Mzee Ndasi akahakikisha amejaza kwelikatika tumbo lake lisilokuwa na hata dalili yakitambi kisha akaanza taratibu kuifuata njiainayoelekea nyumbani kwake.Kwa mwendo aliokuwa nao mzee Ndasi si rahisikumtilia shaka kuwa amelewa kwani hakuyumbayumba hata kidogo hii ikionesha wazi ni jinsi gani alivyo mzoefu katika matumizi ya pombe kwa mudamrefu.
Hayawi hayawi sasa yalikuwa Mzee Ndasi alifikanyumbani kwake mapema licha ya kuwa ulikuwa niumbali kiasi mpaka kufikia nyumbani kwake lakininyimbo alizokuwa akiimba njiani zilimsindikizaipasavyo."John! john! john! amka weee pumbavu,nasemaamkaaa shenzi weeee!" alianza kutupa maneno Yaleakiwa uwanjaniKwakuwa John alikuwa amelala fofofo hakuwezakusikia chochote kutoka kwa babu yake"Leo utanitambua si unajifanya umekua kidumengoja" Mzee Ndasi alijiongelea huku akiufuatia mtiwa mifolo wengine wanaiita miti ya zabibu japohaitoi zabibuAkakata fimbo ndefu iliyonyooka vyema na kuelekeanayo ndani,alipoingia tu akanyoosha moja kwa mojakatika chumba cha john na kumkuta akiwa amelalahoi hajielewi.
Mzee Ndasi alisimama kwanza akimuangalia johnkupitia mwanga hafifu wa tàa aina ya chemliitumiayo mafuta ya taa,Akatikisa kichwa akisikitikana kujisemea moyoni "Maskini John,unalala fofofokama si mwanaume vile sasa hata wezi wakivamiahumu ndani si wanaweza kukuhamisha kishawakaiba godoro wewe ukalala chin I au ukimuoahuyo binti utamlinda kweli? loooh!! maskini Johnngoja Leo nikufunze wanaume wanavyolala".kwa nguvu zote mzee Ndasi alishusha fimbo usawawa makalio ya john ambaye alikuwa amepoteleausingiziñi huku amejifunika shuka laini mno.Hamadi!! John alikurupuka huku akipiga yowe kali"Babu nakufaaaaaaaaa"