Simulizi: Jini Katikati ya Shule

Chilojnr

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
302
1,306
Simulizi hii imeandikwa na Nyemo Chilongani

0718069269

SEHEMU YA 01.

“Mume wangu kila siku unarudi usiku tu, mwisho vibaka wakuvamie wakupore hiyo simu yako,” alisema mwanamke mmoja aliyekuwa amevalia dela jekundu lililokuwa na mistari ya njano kwa mbali, alikuwa akizungumza na mume wake aliyekuwa akifanya kazi ya gereji maeneo ya Kagera jijini Dar.

Mwanaume aliyekuwa akiambiwa aliitwa Masalu Mfinanga, alimwangalia mkewe huku akitabasamu kwani kwa kile kitu alichomwambia kwake hakikumuingia akilini hata kidogo.

Alijulikana na wakazi wengi wa Tandale, aliwazoea na mara kwa mara alikuwa akipiga nao stori, alikuwa rafiki wa wahuni wengi, yaani kwa kifupi hakukuwa na mtu yeyote ambaye angembabaisha kwa lolote lile.

Tabasamu lake tu likaonekana kama kuyapuuzia maneno aliyozungumza mkewe, kwamba hicho kitu kamwe kisingewezekana, kwenye maisha yake yote, alirudi nyumbani usiku kwa kuwa kama mwanaume, wakati mwingine ilikuwa ni lazima kuchelewa tu.

Kazi zake zilikuwa zikimalizika majira ya saa kumi na mbili jioni, kurudi muda huo nyumbani kwake lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo, ilikuwa ni lazima apitie kijiweni kwake hapo Kagera kucheza bao ama drafti halafu inapofika majira ya saa tatu ama nne usiku alikuwa akirudi nyumbani kwake.

Kutoka Kagera kwenda Tandale alipokuwa akiishi ilikuwa ni lazima kupita njia ya bondeni kulipoitwa Vinyasi, unapopandisha juu unakutana na shule mbili za kata zilizojengwa eneo moja, Tandale Shule ya Msingi na Hekima, sasa ili uvuke na kutokea barabarani ilikuwa ni lazima upite hapo shuleni.

Shuleni hapo kulikuwa na miti mingi mikubwa, iliyokuwa ikionekana mizuri sana nyakati za mchana lakini ilitisha mno nyakati za usiku. Wengi waliogopa kupita shuleni hapo linapoingia giza lakini hiyo haikuwa kwa mtu kama Masalu ambaye alikuwa akipita muda wowote ule aliotaka.

Mke wake aliongea sana, Masalu hakusikia, kila siku ratiba yake likuwa ni kurudi nyumbani kwake usiku hata kama alimaliza kazi mapema kabisa, ratiba ya kurudi nyumbani wala haikubadilika.

Siku zikakatika na kukatika, hatimaye siku moja baada ya kumaliza kazi zake, akaondoka na kuelekea kijiweni kwake. Kufika huko, akacheza drafti mpaka majira ya saa nne usiku, akavaa viatu vyake na kuondoka mahali hapo.

Njia yake ilikuwa ileile ya Vinyasi, akapandisha na kutokea shuleni. Sasa akaanza kupiga hatua kuelekea barabarani, hapo alikuwa akikatiza shuleni kama kawaida yake.

Alipofika karibu na mwembe mkubwa, akaanza kusikia harufu ya manukato mazuri sana ambayo hakuwahi kuyasikia tangu kuzaliwa kwake. Akafikicha pua yake, akatamani kubaki hapo kwa dakika kadhaa kwani harufu ile ilimvutia kupita kawaida.

Akaanza kuangalia huku na kule kwa kuamini labda angemuona mtu aliyejipulizia manukato hayo, hakuona mtu yeyote yule, sasa harufu hiyo ilitokea wapi? Alijiuliza bila kupata jibu.

Ghafla mbele yake akamuona mwanamke mrembo akiwa amesimama, mkono mwake alishika simu na aliiweka sikioni kama mtu aliyekuwa akiongea na mtu kutoka upande wa pili.

Hapo kukawa na mambo kadhaa yaliyokuwa yakimtatiza. La kwanza, huyo mwanamke alitokea wapi? Wakati pua zake zikiwa zimenusa harufu nzuri ya manukato, aliangalia kila upande, hakukuwa na mtu yeyote yule, akapuuzia lakini kitendo cha kupepesa macho, ghafla tu mbele yake alisimama mwanamke. Hilo lilikuwa la kwanza.

La pili alilojiuliza ni kuhusu huyo mwanamke alichokuwa akikifanya mahali hapo. Ilikuwa ni usiku, ni vigumu sana kumuona mwanamke mahali hapo, cha ajabu, huyo alikuwa hapo, alimsubiri nani? Alionekana kuongea kwa simu, alikuwa akiongea na nani?

La tatu ni baada ya kusogea karibu naye, akapigwa na mshtuko baada ya kugundua alikuwa mwanamke mrembo sana, alikuwa na urembo ambao hakudhani kama jijini Dar es Salaam angekutana na mwanamke mrembo kama huyo.

Hilo halikumshangaza sana, duniani kulikuwa na warembo wengi tu, ila kilichomchanganya ni kwa namna gani aliuona urembo wa msichana huyo?

Kumbuka ilikuwa ni usiku. Kulikuwa na giza kubwa mahali hapo. Ilikuwa ni vigumu hata kumuona mtu sura yake, ila cha ajabu kabisa, aliiona sura yake, aliionaje na wakati kulikuwa na giza.

Hapo akachanganyikiwa!
“Samahani!” alisema yule msichana.
Sasa hapo kikaibuka kitu kingine. Sauti.

Msichana huyo alikuwa na sauti ya kumtoa nyoka pangoni, nyororo fulani hivi hata kama haukuwa na pesa, ulipoisikia ikikwambia alihitaji laki moja, haraka sana ilikuwa ni lazima utafuta pesa hiyo na kumpa.
Ikambidi Masalu asimame.

“Bila samahani!”
“Nampigia simu mdogo wangu, kumbe vocha imeniishia, unaweza kunisaidia?” aliuliza huyo mwanamke.
Kwenye maswali yote aliyowahi kuyasikia akiulizwa kwenye maisha yake, Masalu akakiri swali la siku hiyo lilikuwa la kipumbavu kuliko maswali hayo yote. Eti unaweza kunisaidia? Sasa nani angekataa kumsaidia msichana mrembo kama huyo? Hata kabla ya kujibu swali hilo, harakaharaka akatoa simu na kumpa.
“Mpigie humu!”
“Nisije kukumalizia dakika zako!”
“Wewe usijali! Humo kuna dakika nyingi mpaka zinamwagika,” alimjibu huku akitabasamu.

Msichana huyo akampigia mtu aliyetaka kumpigia, alimwambia alikuwa ndugu yake, simu ikaanza kuita na baada ya sekunde kadhaa akawa anaongea na mtu huyo.

Masalu alisimama huku akimwangalia tu, kichwa chake kilikuwa kikifanya mahesabu mazito. Kwanza akakubali kwamba alipagawishwa na huyo mwanamke, alimpenda na kitu alichotaka kutoka kwake ni kuishi naye, sasa ingewezekanaje na wakati alikuwa na mke?

“Basi wahi nakusubiri huku uwanjani! Ukichelewa naondoka!” alisema msichana huyo.

Alipomaliza, akamrudishia simu Masalu. Sasa si ushatoa msaada, ondoka zako. Weee! Kwa Masalu haikuwezekana kabisa. Unatoaje msaada halafu unaondoka bila kuupambania ule msaada wako? Hapo akahitaji malipo ya msaada huo, na malipo yenyewe yalitakiwa kuwa namba ya simu.

“Amesemaje?”
“Nani?”
“Huyo ndugu yako!”
“Anakuja!”
“Ila huogopi kuwa hapa peke yako?”
“Naogopa sana! Kunatisha! Unajua hata nilipokuona unakuja huku, bado nusu nizimie! Naomba usiondoke, unipe kampani hadi atakapokuja,” alisema msichana huyo.

Aya sasa! Hebu jiulize, hata kama ungekuwa wewe ungekataa kumpa kampani mwanamke mzuri kama huyo? Yaani baada ya Masalu kuambiwa hivyo, akatamani ampigie mkewe simu na kumwambia nitarudi nyumbani asubuhi.

Kuonana naye ilikuwa ni kama bahati. Kwanza inawezekana baada ya kumuona siku hiyo, asingeweza kumuona tena. Ni kweli kama mwanaume hakutakiwa kuwa na haraka lakini kwa mwanamke wa namna hiyo, alitakiwa kukamilisha mambo yote mapema kabisa.

Alitakiwa kumuomba namba, ila napo kwanza alitakiwa kuwa na uhakika kama angepewa ama la! Kulikuwa na mademu waliojiona watoto wa mjini kumbe walikuwa washamba tu. Mtu amesaidiwa, kutoa namba ya simu anaona kama muombaji atapata mamilioni.

Sasa akajiuliza, je, huyo ndugu yake akija, hatotaka kuondoka na kumshukuru tu na kutokomea zake? Hilo nalo inawezekana kabisa lingetokea, sasa yeye kama mwanaume rijali, aliyejinasibu mwanamke hakuwa na uwezo wa kumpinga alitakiwa kumuonyesha hilo.

“Twende tukakae pale, hapa isije miguu ikaingia tumboni,” alisema Masalu.
“Sawa haina shida.”

Wakaenda na kukaa kwenye ngazi ndogo za kupandia kwenye floo ya madarasa. Sasa hapo Masalu akaanza kupiga mahesabu yake makubwa kichwani. Walikaa, kwa jinsi alivyovaa mwanamke yule, hakika alionekana kuwa mtoto wa mjini, halafu wala siyo mchoyo.

Na kama si mchoyo?
Alitakiwa kuombwa!
“Kwanza unaitwa nani?”
“Aisha!”
“Oh! Umependeza sana aisee!” alimwambia.
“Nashukuru!”
“Unanukia vizuri! Una ngozi nzuri halafu inaonekana lainiiiii...” alimwambia, hiyo kauli ilisindikizwa na mkono wake uliokwenda mpaka kwenye paja la msichana huyo, halafu Aisha alivyokuwa na makusudi, akamsogezea upaja ili ashike vizuri.

“Huku ndiyo kuokota dodo chini ya muarobaini,” alijisemea.

Sasa akaleta utawala kuanza kulitawala paja lile.

“Una haraka jamaniiiii! Yaani ndiyo kwanza tumeonana leo,” alisema msichana huyo.
“Hamna haraka jamani! Nimeipenda tu ngozi yako!

“Aya bwana! Ndugu yangu nahisi yule pale,” alisema msichana huyo, akasimama harakaharaka na kuiweka vizuri sketi yake fupi kwa kuishusha chini manake mshika mapaja aliipandisha juu kidogo, kwa mbali kulikuwa na mtu mwingine amesimama. Akaanza kumfuata.

Masalu akajilalamikisha moyoni mwake, kwa nini ndugu yake huyo alifika mahali hapo kwenye hatua kama ile. Akabaki akiwaangalia, watu hao wakaanza kuondoka.

“Eeh! Hata namba sijachukua!” alisema kwa kushtuka, akaanza kupiga hatua, hakujua nini kilichotokea, yaani kuangalia pembeni tu na kuyarudisha macho, watu hao hakuwaona.
“Wamepitia wapi?” alijiuliza.
“Itakuwa kona hii!”
”Hapana! Ama walipitia ile kule?” alijiuliza maswali mengi, akakosa jibu.

Njia zote hakuwaona watu hao, akanyong’onyea na uondoka zake kurudi nyumbani kwake. Njia nzima alikuwa akimuwaza msichana huyo mrembo, alitembea mpaka alipoimaliza shule na kuingia kwenye barabara, akaivuka na kuingia kwenye kichochoro na kuelekea kwake.

“Usiku tena!” alisema mkewe, alikuwa sebuleni akimsubiri.
“Si saa nne mama kama siku nyingine!” alimwambia.
“Saa nne? Saa yako inafanya kazi kweli?”
Hapo ikambidi Masalu aangalie saa yake, alipigwa na mshtuko baada ya kuona ilikuwa saa saba usiku. Eeeh! Ilikuwaje?

Aliondoka Kagera saa nne, kutoka hapo mpaka shuleni ni mwendo wa dakika tano tu, akakutana na yule mwanamke, akaongea naye kama kwa dakika ishirini tu na kuondoka, sasa ilikuwaje muda huo iwe saa saba? Hiyo saa saba ilifikaje?

“Imekuwaje saa saba?” aliuliza kwa mshtuko.
“Ndiyo nikuulize wewe! Kwani ulikuwa wapi?”
Wanawake bwana! Sasa alitegemea kabisa Masalu amwambi nilikuwa na demu uwanjani! Ataanzaje? Lilikuwa suala gumu.

“Kazi tu! Halafu nilipitia mpirani! Si unajua leo kulikuwa na mechi za UEFA,” alimwambia, japokuwa hakukuwa na mechi yoyote ile, alijua mwanamke hakuwa mtu wa kufuatilia mipira.
“Ngoja nikakuwekee maji uoge,” alimwambia.

Akaondoka na kuelekea huko kumuwekea maji. Masalu akaelekea chumbani, bado moyo wake uliendelea kujilaumu juu ya mwanamke yule kutokuipata namba yake. Huku akiwa na taulo, ghafla meseji ikaingia, hakujua ilitoka wapi, akaichukua simu na kuifungua.

‘Usiku mwema msamaria mwema. Aisha wa shuleni hapa!’

Masalu akapigwa na mshangao, hakuamini alichokiona kwenye simu yake. Alikuwa yule msichana wa shuleni, alimtumia meseji, namba yake aliitoa wapi? Hakumpa, na hakuwa na namba ya huyo mwanamke, cha ajabu akatumiwa meseji, na mbaya zaidi haikuja namba tupu, bali iliseviwa jina la Aisha, kwa maana hiyo aliisevu namba hiyo.

“Mmh!” akaguna.
Halafu ghafla tu harufu nzuri ya yale manukato aliyoyanusa uwanjani yakaanza kuingia ndani ya chumba hicho. Masalu akachanganyikiwa.

Je, nini kitaendelea?

bk.jpg
 
View attachment 2263596
MUENDELEZO
 
SEHEMU YA 02

Huku akiwa kwenye hali hiyo, mara mkewe akaingia chumbani humo na kumwangalia Masalu usoni, alionekana kuwa na kitu fulani ambacho hakujua kilikuwa ni kitu gani. Alionekana kama mtu fulani aliyekuwa akiweweseka.
Akataka kuuliza lakini akaamua kubaki kimya kwani kwa kila kitu kilichotokea siku hiyo kilionekana kuwa tofauti kabisa na siku nyingine. Tatizo kubwa lilikuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani.
Kwa nyakati za usiku watu hukutana na mambo ya ajabu njiani, kwenye daladala na hata sehemu nyingine, aliamini inawezekana wakati mumewe akiwa njiani kurudi nyumbani hapo, labda alikutana na kitu kibaya njiani, hivyo hakutaka kujali sana.
“Maji tayari!” alisema huku akimwangalia. Masalu akashtuka.
“Unasikia hii harufu?” alimuuliza mkewe huku akimwangalia.
“Harufu gani?”
“Hii ya manukato!”
Mkewe akasogea na yeye kujaribu kunusa.
“Hakuna harufu yoyote ile.”
“Pua zako zina nini? Zimeziba ama?” aliuliza Masalu, japokuwa swali lake lilikuwa kama na utani fulani lakini ukweli ni kwamba hakuwa kwenye utani hata kidogo.
Alipoona mkewe hahisi chochote kile, akaamua kutoka na kuelekea bafuni. Kichwani alikuwa akimfikiria huyo Aisha, sasa haukuwa uzuri bali ile harufu aliyoinusa chumbani. Je, mwanamke huyo alikwenda humo ndani ama alipita nje kwa dirishani? Kama kweli alifanya hivyo, je, alijua kama alioa?
Akachukua kopo kutoka kwenye ndoo na kuanza kujimwagia maji. Huku akiendelea kuoga, mara umeme ukakatika. Hilo lilimkasirisha, kwenye mashirika aliyokuwa akiyachukia, la kwanza lilikuwa Tanesco.
Dar es Salaam kulikuwa na joto kali lakini wao wala hawakujali, sasa usiku kama huo, muda ambao walijiandaa kulala, walikata umeme, ilimaanisha wangelala na giza, tena kukiwa na joto kali.
Sasa akaendelea kuoga kwa hisia kwa maana ya kujua mahali ndoo ilipokuwa na kupeleka mkono kwa kupapasa. Wakati akioga, mara akasikia mlango wa bafuni ukifunguliwa, kwanza alishtuka lakini baada ya kumgusa mtu aliyeingia, akaachia tabasamu, alihisi alikuwa mkewe.
“Na wewe umekuja tuoge baada ya kuona umeme umekatika,” alisema Masalu huku akicheka, mkewe wala hakujibu kitu zaidi ya kumkumbatia, kwa mguso huo tu, wakajikuta wakianza kufanya mapenzi humo.
Walichukua dakika chache tu, alipomaliza, mkewe akatoka, akachukua taulo na kujifuta, hapohapo umeme ukarudi, akatoka na kuelekea chumbani kwake. Akaangalia huku na kule, mkewe hakuwemo, alikuwa sebuleni.
“Wanawake bhana!” alisema Masalu huku akiachia tabasamu, akavaa pensi yake na kumfuata sebuleni, alitaka kumwambia baada ya kuoga, walitakiwa kulala.
“We’ mwanamke mzuri, watu wakishatoka kuoga, kinachofuata ni kulala,” alisema huku akipiga hatua kuelekea sebuleni, alipofika akamkuta mkewe anamuwekea chakula.
Akamwangalia!
Akashtuka!
Alikuwa vilevile kwa maana ya mavazi, hakuonekana kuoga wala kutoka kwenda sehemu, yaani alivyokuwa kama alivyoingia.
“Hutakiwi kulala bila kula! Njoo ule kwanza na mimi nikaoge,” alisema huku akimwangalia, tabasamu pana lilikuwa usoni mwake.
“Kwani hujaoga?” aliuliza huku akishtuka.
“Ndiyo! Nilikuwa bize na kazi, nikasema ukirudi, nitaoga, ila si unajua kazi nyingi, nikakuacha ukaoge peke yako,” alisema mkewe huku akimwangalia.
Sasa hayo maneno yakamshtua zaidi. Kwamba hakuwa ameoga, sasa yule aliyeingia bafuni na kuoga naye alikuwa nani kama hakuwa yeye? Hapo akavurugwa kabisa, akatamani kumwambia kwamba alipokuwa bafuni alikuja mwanamke na kuoga naye, wakafanya mapenzi lakini hakutaka kumwambia, ni kwa sababu angemfanya kuwa na hofu.
Sasa akakumbuka kuuliza kitu.
Umeme.
“Hivi umeme ulikwisha?”
“Hapana!”
“Ulikatika?”
“Hapana! Kwa nini unauliza?”
“Nilitaka kujua kama ulikwisha niweke mwingine,” alimjibu.
“Niliweka mchana! Upo full!’
Kama mkewe angejua kilichokuwa kimetokea, angesema tu kweli ulikatika kwa dakika chache na kuwaka, ila kwa kile alichokisema, kilimfanya kukosa amani kabisa.
Sasa akaogopa!
Hofu ya mizimu ikaanza kumuingia moyoni mwake. Akahisi kabisa ile nyumba ilianza kuwa na maruweruwe, haikuwa kawaida hayo kutokea kipindi hicho, yaani kwa usiku mmoja, kulikuwa na mambo lukuki yaliyomchanganya.
Hakuwa na la kufanya zaidi ya kukaa mezani na kuanza kula. Chakula hakikuwa kitamu kama siku nyingine, hakikuwa na ladha hata kidogo. Ila akajilazimisha kula mpaka akamaliza.
“Ngoja nikaoge kwanza,” alisema mkewe na kuondoka kuelekea bafuni kuoga.
Sasa akabaki peke yake sebuleni, alichokifanya ni kuchukua simu na kuangalia namba ya Aisha, alikumbuka alimtumia meseji, alitaka kumpigia na kuwasiliana naye, alianza kuhisi chanzo cha matatizo alikuwa huyo msichana. Ikaanza kuita.
“Halo Aisha!” aliita baada ya kupokewa.
“Halo Masalu! Hujalala tu?” aliuliza msichana huyo.
“Nitalalaje na wakati unaniwekea mauzauza?” aliuliza.
“Unasemaje?”
“Nitalalaje na wakati unanitisha usiku wote huu?”
“Eeh! Mbona sikuelewi!”
“Kwanza ulisema nilikupa namba yangu ya simu, nilikupa wakati gani?” aliuliza Masalu akaamua kuvaa mabomu na kujilipua.
“Eeh! Wanaume nyie!”
“Nijibu kwanza!”
“Sasa mimi nitakujibu nini hapo? Ulichukua simu yangu, ukajibipu, halafu ukaondoka. Ulipokuwa njiani ukanitumia meseji, ukasifia muonekano wangu, ukasema nisikutumie meseji tayari ulikuwa unaingia nyumbani, nikasema sawa,” alisema msichana huyo.
“Mimi ndiyo nilisema hivyo?”
“Ndiyo! Ukasema mkeo, Grace anaweza kuleta matatizo akigundua nachati na wewe,” alimwambia.
Sasa hapo Masalu akachanganyikiwa zaidi. Kwanza vile vyote alivyoambiwa havikuwa kweli hata kidogo. Hakuchukua simu ya msichana huyo na kujibipu kwa kuwa alimwambia haina vocha na ndiyo maana alimuazima simu yake. Sasa ilikuwaje achukue simu ya msichana huyo na kujibipu?
Ukiachana na hayo yote, kutajiwa jina la mkewe napo kuliongeza ukichaa kichwani mwake. Huyo Aisha ilikuwa ni mara ya kwanza kuonana naye, hakuwa amemtajia mkewe, alikuwa na uhakika huo lakini cha ajabu kabisa, leo hii alimtajia jina la mkewe.
Akahisi kama ilikuwa kweli vile.
Kama haikuwa kweli! Aisha alimjuaje Grace?
“Hapana! Si kweli!” alimwambia.
“Hebu angalia utaniamini nikisemacho,” alisema msichana huyo na kukata simu.
Haraka sana Masalu akafungua sehemu ya simu zilizoingia, ni kweli akakutana na namba ya mwanamke huyo, muda uleule aliokuwa amembipu ili kuichukua namba yake.
Hilo halikumuingia kichwani hata kidogo. Hakufanya kitu kama hicho. Akafikiria sana, sasa kilichotokea, akaanza kukumbuka namna alivyochukua simu ya msichana huyo na kujibipu. Alikumbuka vilivyo kabisa alifanya kitu kama hicho.
“Eeeh!” alijishangaa.
Akaenda sehemu ya meseji, kama alivyosema Aisha ilikuwa vilevile. Ni kweli walichati kidogo na kumwambia alikuwa akikaribia nyumbani, wangewasiliana kesho.
Hapo kwa mara nyingine kichwa chake kikaanza kumkumbusha namna alivyokuwa amechati na Aisha kwa simu yake wakati akirudi nyumbani kwake. Hapo akapagawa, hakujua kama yeye ndiye hakujielewa kiasi cha kuchanganya mafaili ama kulikuwa na kitu.
Akiwa anashangaa! Mara meseji ikaingia kwenye simu yake, haraka sana akaichukua na kuiangalia, ilitoka kwa Aisha ambayo ilisomeka;
‘Pumzika kwanza! Naona umechanganyikiwa sana’.
Alichokiandika Aisha kilikuwa kweli kabisa. Alichanganyikiwa kweli, hakuwa anadanganya hata kidogo kwani kwa kile alichokuwa akihisi muda huo na ukweli wa mambo ulivyokuwa, vilikuwa vitu viwili ambavyo havikumuingia kichwani hata mara moja.
“Nitakuwa nimeanza kuzeeka! Leo Aisha kaniweza!”
Usiku hakulala vizuri, bado kichwa chake kilikuwa na mambo mengi ya kufikiria kuhusu usiku huo na kile kilichotokea, sasa huyo Aisha alionekana kuwa tofauti na wanawake wengine ambao aliwahi kuonana nao.
Alipata usingizi majira ya saa kumi na moja, kwa kuwa jana ilikuwa ni Jumamosi na Jumapili hakuwa akienda kazini kwake, aliamka majira ya saa tano na kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kuchukua simu yake na kuangalia kioo.
Alitumiwa meseji kutoka kwa Aisha, haraka sana akaichukua na kuanza kuisoma.
‘Hebu amka! Mwanaume mzima unalalaje mpaka saa tano!’
Ikambidi afikiche macho yake kwanza aiangalie meseji hiyo alitumiwa muda gani. Meseji iliingia majira ya saa moja asubuhi, sasa alijuaje kama angelala mpaka saa tano? Akaamua kumpigia.
“Aisha!” alimuita mara baada ya simu kupokewa.
“Niambie Masalu! Mume wa mtu, mshika mapaja maarufu Tandale,” alisema Aisha halafu akacheka kumaanisha kile alichokiongea kilikuwa ni utani tu.
“Niko poa tu mzururaji wa usiku anayemsubiri mshika mapaja aje amshike,” naye Masalu akatania na kucheka kidogo.
“Nimekumiss!”
“Nimekumiss pia! Inabidi leo tuonane!”
“Muda gani?”
“Hata baadaye!”
“Au nije nikuone?”
“Wapi? Nyumbani?”
“Ndiyo!”
“Unapajua sasa? Halafu si unajua nina mke!”
“Najua una mke! Ila Grace hatoweza kuniona!”
“Una maana gani? Utayeyuka?”
“Hapana! Namaanisha yeye si amekwenda kwa mama yake Ubungo, nitaondoka kabla ya hajarudi!”
“Grace amekwenda Ubungo?”
“Sasa unashangaa nini? Kwani hakukuaga?”
“Hapana! Ndiyo naamka! Aiseee! Nimekumbuka! Nilimsikia asubuhi kama akiniambia Ubungo, ila nilikuwa na usingizi sikusikia vizuri Ubungo nini!” alimwambia.
“Ndiyo hivyo! Mimi nakuja, siwezi kuvumilia,” alimwambia huku akiwa hana aibu hata kidogo.
Mpaka Masalu akashangaa!

JE, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 03

Sasa Masalu akaanza kuhaha kwa ajili ya mwanamke huyo, alitamani kumpigia simu na kumzuia lakini hilo halikuwezekana, Aisha aliamua moja tu, kwamba ni lazima afanye kila liwezekanalo anafika nyumbani hapo.
Huku akiwa anajiuliza ni kipi alitakiwa kufanya, ghafla akasikia mlango ukigongwa, hakutaka kujiuliza alikuwa nani, alijua tu ni Aisha tu. Sasa kama alikuwa ndiye mwenyewe, alifikaje hapo?
Unajua kwa nini? Alikumbuka alizungumza naye dakika kama moja iliyopita na kumwambia angefika nyumbani hapo, hilo halikuwa tatizo, tatizo kubwa lilikuwa ni muda alioutumia kufika hapo. Yaani ndani ya dakika moja tu tayari alifika!
Alipowasiliana naye alikuwa njiani?
Au alikuwa nje ya nyumba?
Akaufuata mlango na kuufungua, macho yake yakatua kwa msichana mrembo sana, aliyekuwa na uzuri uliovutia kupita kawaida, alimwangalia, kwa jinsi alivyokuwa akitabasamu, alilikumbuka tabasamu hilo tangu usiku uliopita, alimvutia na hakika hakujuta kuonana naye.
Sasa leo hii alimfuata nyumbani kwake, akiwa peke yake kabisa. Shetani wa ngono akamvaa na kumwambia sasa kazi ilikuwa kwake, kama jana alikutana naye usiku, leo alimfuata nyumbani kabisa, tena mchana.
Leo hakutakiwa kuitwa mshika mapaja, alitakiwa kubadilishwa jina na kuitwa Mwanaume mwenye uwezo wake kwenye kitanda cha sita kwa sita. Alisimama huku akimwangalia Aisha tu ambaye alibaki akimtolea tabasamu pana.
“Unaniangalia sana mpaka nasikia aibu,” alisema msichana huyo, lile tabasamu lake hakika likaongezeka maradufu, likampagawisha Masalu wa watu.
“Ninastaajabu sana uzuri wako! Ni kweli uliumbwa kwenye dunia hii hii tunayochimbia vyoo ama?” Masalu akasema na kuuliza swali, naye akatoa tabasamu pana, hakuwa mwenye sura nzuri lakini aliamini kwa tabasamu lile lingemfanya msichana huyo kujisikia huru.
“Niruhusu niingie ndani basi, mpaka mkeo anikute hapa mlangoni!” alisema Aisha.
“Karibu sana!”
Akamkaribisha na msichana huyo kuingia ndani. Hakuacha kuangalia huku na kule, ni kama alikuwa akichunguza nyumba hiyo, alimwangalia Masalu, mwanaume huyo hakuwa na uhuru hata kidogo.
Alionekana kuwa na hofu nzito moyoni mwake. Aisha kuwa ndani ya nyumba hiyo hakukumfanya kuwa huru, alijua tu inawezekana kungekuwa na jambo baya lingetokea. Vipi mkewe angerudi nyumbani bila taarifa halafu akamkuta msichana huyo humo ndani?
Yaani wakati yeye hayupo, mumewe mpendwa akaingiza mwanamke ndani na kukaa naye, tena nyumba ileile ambayo kila siku walikuwa wakipambana kutafuta watoto, hakika ilikuwa ni dharau kubwa sana.
“Jana ulinipagawisha sana,” alisema Masalu huku akimwangalia Aisha.
“Na ndiyo maana nimekufuata nikupagawishe vizuri!” alimwambia.
“Ila nyumbani hapa naona kuna hatari sana!”
“Unaogopa nini?”
“Mke wangu akitokea!”
“Hawezi kutokea!”
Huyu Aisha hakuonekana kabisa kumuogopa mke wake, yaani alikuwa akiongea kana kwamba yeye ndiye alikuwa mke mwenyewe. Hata macho yake hayakuonekana kabisa kuwa na hofu na wakati Masalu alikuwa anaogopa kupita kawaida, tena hakuwa na amani hata kidogo humo ndani.
Aisha aliligundua hilo, alikuwa akiongea mfululizo huku akimtaka atoe presha, alifika hapo kwa kuwa alijua mkewe hayupo na hata iweje asingeweza kumkuta. Unajua nini? Hapa kuna kitu ambacho kwa kipindi hicho hakukielewa, inawezekana hata wewe unayesoma hapa hukukielewa, acha nikueleweshe sasa.
Aisha alikuwa jini, sasa kwa kipindi hicho Masalu hakuwa analijua hilo. Alipomwambia mke wake hawezi kumkuta hata iweje yaani alimaanisha hata kama angetokea muda huo na kuingia ndani, asingeweza kumkuta, sasa yeye sikuifikria hiyo kauli.
Akamshika mkono!
Sasa hapo ndipo akaona hali ya tofauti mwilini mwake. Kwanza alikuwa natetemeka sana, kwa mbali kijasho chembamba kilikuwa kinamtoka mwilini. Hakujua kwa sababu gani alikuwa naogopa na kutetemeka hivyo kwani kama ni masuala ya wanawake, alizoea sana, tena alikuwa mtaalamu mwenyewe ila kwa Aisha, alikuwa mdogo tu.
"Mbona unatetemeka hivyo jamani?" aliuliza huku akimwangalia.
"Hamna! Nipo poa!"
"Kweli?"
"Ndiyo!"
Akamwambia sasa alikuwa tayari kwa kila kitu, Masalu kama mwanaume alitakiwa kumuelewa tu. Akamchukua na kuanza kumpeleka chumbani. Sikia, mule ndani kulikuwa na vyumba vinne lakini hakujua Aisha alijuaje kama kile alichokuwa akikifuata ndicho kilikuwa chumba chake.
Alionekana kama mzoefu wa nyumba hiyo. Wakaingia ndani, akamsukuma na kuangukia kitandani.
'Puuu'
Halafu akaanza kuvua nguo zake, akabaki kama alivyotoka tumboni mwa mama yake, ama kama Hawa alivyoumbwa ubavuni mwa Adamu. Sasa Maalu akaanza kumwangalia kwa macho ya matamanio.
Aisha alikuwa akimwangalia kwa yale macho yaliyoonyesha alikuwa tayari kwa kila kitu, yaani kama ni tunda, liliiva na kumsubiri mtunguaji aje alitungue na kulila. Huku akimsubiri pale kitandani na akiendelea kuvua nguo zake, sasa Masalu akaanza kusikia mtu akipiga hodi.
"Hodi humu ndani!" aliisikia sauti ya mwanamke.
Akashtuka!
Akatoka ndani harakaharaka huku akiwa na hasira. Wanaume mnajua ni kwa kiasi gani muda kama huu, tena kwenye kitendo kama kile mwanaume huwa na hasira kiasi gani, sasa ndivyo ilivyokuwa kwa Masalu muda huo. Alipoufikia mlango, akaufungua, macho yake yakakutana na mwanamke aliyekuwa akiuza sabuni za kusafishia choo.
"Karibu!" alimwambia, yeye mwenyewe alijua kabisa hakuwa sawa, yaani alitaka aongee harakaharaka aondoke zake.
Hata kabla hajaitikia hiyo karibu. Mama yangu weeee! Akamuona mke wake akitokea mahali hapo, alipomuona mama yule wa sabuni, akatoa tabasamu pana. Hivi unajua ni kwa kiasi gani alishtuka hapo? Unajua ni kwa kiasi gani alishikwa na hofu kali? Kutetemeka kukaanza upya, tena sasa hivi kulikuwa ni kwa hofu kali kupita kawaida.
"Mkeo amerudi!" alisikia sauti ikiniambia kichwani mwake.
Sasa akatamani kile alichokuwa akikiona kiwe ndoto ama mawazo fulani tu. Huyu mwanamke alirudi, lakini mbona kuondoka kwake kwenda Ubungo alitakiwa kuchukua hata masaa mawili lakini ndiyo kwanza alichukua dakika kadhaa?
Sasa akaanza kumfikiria huyo Aisha aliyekuwa chumbani. Angemtoaje? Nyumba ilikuwa na milango miwili, wa kwanza ulikuwa huo na wa pili ni wa nyuma, ila ilipita kama miaka miwili hakuwahi kuutumia, yaani hata ukimuuliza ufunguo wake upo wapi? Wala hafahamu.
"Imekuwaje tena?" alimuuliza, sasa akahisi miguu ikikosa nguvu ya kuendelea kusimama.
"Nilipiga simu, kumbe hawapo! Nikaona bora nirudi!" alimwambia mumewe na kumwangalia mama muuza sabuni.
"Karibu mama!"
"Ahsante!"
"Ile sabuni sijamaliza! Rudi tena wiki ijayo," alimwambia na baada ya hivyo, yule mwanamke akaondoka zake na yeye kuingia ndani.
Haraka sana Masalu akawahi, hakutaka aelekee chumbani kwani kulikuwa na mwanamke mwingine. Kama angemuona, hakika ingekuwa mwanzo wa vita ya tatu ya dunia, na kusingekuwa na mtu wa kuamua vita hivyo.
Halafu akajiuliza tena.
Inawezekana vipi amzuie huyu mwanamke kuingia ndani na wakati palikuwa kwake? Yaani inakuwaje hapo mkeo kaja halafu unamwambia hakuna kuingia chumbani? Lingekuwa suala gumu sana. Sasa kama mwanaume alitakiwa kufanya yake.
Ila pia akajiuliza.
Ingekuwaje kama huyo Aisha angetoka chumbani na kuja pale sebuleni? Angeweza kupambana na mke wake? Huyu mwanamke alivyokuwa kisirani sasa, aliona kabisa anaaibika mtu mzima.
Akamuona mke wangu akisimama na kuanza kwenda chumbani, alitamani amzuie ila akashindwa kufanya hivyo. Akabaki sebuleni huku akiwa hana hata amani, akajikalia sebuleni, sasa akawa anasikilizia ni kipi kingetokea huko chumbani.
Akasikilizia kelele weeeee......
Kimyaaaaa!
Ikabidi sasa asimame na kuelekea chumbani.
Akaingia chumbani

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 04.

Mule chumbani, Masalu akamkuta mkewe akibadilisha nguo zake na alipoangalia huku na kule, Aisha hakuwepo. Hilo likamchanganya kichwa chake, ilikuwa ni vigumu sana kumkosa mwanamke huyo ndani.
Alipotoka na kwenda kuufungua mlango kwa ajili ya mama muuza sabuni, alikumbuka kabisa alimuacha humo ndani, na alikuwa na uhakika hakutoka, sasa kama humo ndani hakuwemo, alikwenda wapi?
Alikuwa na wakati mgumu wa kulijua hilo mpaka wakati mwingine akatamani kumuuliza mkewe kwamba alipoingia ndani ya chumba kile alimkuta Aisha ama hakumkuta? Akaona hilo halitoshi, sasa akaamua kuanza kumtafuta humo ndani.
Kama hakuwemo ndani, ilimaanisha alitoka, na kama alifanya hivyo basi mlango pekee ambao inawezekana aliutumia ulikuwa ni wa nyuma. Sasa hapo napo kukamuacha akiwa na maswali kadhaa, mlango huo wa nyuma ilipita miaka miwili hawakuwa wameutumia, kama huyo mwanamke aliutumia, aliutumiaje? Aliupata ufunguo? Hakika majibu yalikuwa ni hapana.
Akatoka chumbani na kuelekea huko jikoni ambapo kulikuwa na mlango wa nyuma, akakuta ukiwa wazi, sasa akapata majibu kwamba Aisha alipitia hapo, ila swali pekee lililomjia kichwani mwake, aliupata wapi ufunguo wa mlango huo?
Huku akiwa anajiuliza, na macho yake yakiwa kwenye ufunguo uliokuwa kwenye kitasa cha mlango huo, mkewe akatokea, alionekana kushangazwa na mlango huo kuwa wazi kwani kwa kipindi kirefu waliutafuta ufunguo wake, hawakuupata.
“Eeeh! Umeupata wapi ufunguo?” aliuliza Grace huku akionekana kushangazwa mno.
“Ulikuwa chumbani, nyuma ya kabati. Yaani mwenyewe mpaka nikashangaa uliikaje kule,” alisema Masalu huku akijitahidi kujifanya kuwa bize kuushikashika mlango huo ili aonekane tu hakudanganya kile alichokisema.
“Na hapa bado hatujapata mtoto, siku tukiwa na mtoto, kuna vitu vitapotea sana,” alimwambia mumewe.
“Tuombe asiwe mtundu sana.”
Waliongea kidogo na mwanamke huyo kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Masalu hakutaka kubaki nyumbani, akaufunga mlango na kutoka, akamuaga mkewe alikuwa akienda kuonana na rafiki yake.
Akaondoka huku kichwa chake kikimfikiria Aisha, aliendelea kujiuliza kwa kile kilichotokea, ilikuwaje mpaka mwanamke huyo aondoke kwa kupitia mlango wa nyuma? Yaani ufunguo aliupata wapi? Akiwa njiani mara simu yake ikaanza kuita, akaichukua na kuangalia jina la mpigaji, alikuwa Aisha, akaipokea.
“Upo wapi?” aliuliza Masalu hata kabla ya salamu.
“Nyumbani kwangu!”
“Wapi?”
“Hapa Mburahati!”
“Naruhusiwa kuja?”
“Haina shida, karibu!”
“Nielekeze!”
Akaanza kuelekezwa.
Sasa akaanza safari ya kuelekea huko Mburahati, ilikuwa ni lazima kuonana na Aisha kwani kulikuwa na mengi ya kumuuliza. Kwa kuwa kulikuwa na umbali fulani, akaamua kuchukua pikipiki. Hiyo ilimsaidia kwani alichukua dakika chache akafika huko.
Alipita kwenye vichochoro kadhaa huku akiendelea kuelekezwa na Aisha mpaka alipofika mbele ya nyumba moja kubwa na nzuri, aliiangalia, kwa harakaharaka aligundua tu familia iliyokuwa ikikaa humo ilikuwa ile iliyokuwa na uwezo mkubwa kifedha.
Akalisogelea geti na kugonga, mlango ukafunguliwa na Aisha aliyekuwa na tabasamu pana. Akamsalimia na kumkaribisha ndani, wakaingia na kutulia sebuleni.
Hapo akazidi kuamini kama msichana huyo alitoka kwenye familia bora. Aliangalia mazingira ya hapo sebuleni, yeye mwenyewe alikiri hakuwahi kuingia kwenye nyumba iliyokuwa na muonekano mzuri kwa ndani, hasa kwa nyumba zilizojengwa katika mitaa ya Kiswahili kama hiyo.
“Karibu mgeni,” alimkaribisha Aisha.
“Nashukuru sana!”
“Utakunywa nini?”
“Hapana! Usijali mama!”
“Jamaniiiii! Hata maji!”
“Wala usijali!”
Macho yake hayakuacha kuangalia huku na kule, alipaangalia vizuri tu na baada ya msichana huyo kutulia, sasa akaanza kumuuliza maswali yake. Kwanza alitaka kujua kama pale palikuwa kwao ama la.
Alichomjibu ni kwamba palikuwa nyumbani kwake, yaani mwanamke huyo alikuwa akiishi hapo. Masalu akashangaa sana, hakutegemea kukuta Aisha akiwa na maisha hayo aliyokuwanayo. Alitegemea kukuta akiishi kwenye chumba kimoja tu, lakini la ajabu akakutana na kitu tofauti.
Sasa hapo akaanza kujiambia jingine kwamba inawezekana huyo Aisha alipangishiwa hapo na bwana wake, yaani kulikuwa na mwanaume aliyeingiza mkono mfukoni na kumpangishia nyumba hiyo kubwa, akamuuliza kama kulikuwa na shemeji.
Akaambiwa hayupo.
“Unafanya kazi gani?” aliuliza Masalu, sasa akashindwa kuvumilia, akataka kulinganisha kazi ya Aisha na nyumba hiyo aliyokuwa akiishi.
“Hayo tutaongea siku nyingine. Usiwe na haraka sana,” alimjibu huku akiachia tabasamu.
Hata kile kilichomfanya kumpeleka huko kikasahaulika kwa muda. Mambo aliyokutana nayo huko hayakuwa ya kawaida hata kidogo. Sasa akaanza kumuheshimu kutokana na namna alivyokuwa.
“Najua umekuja ili uniulize kuhusu mlango,” alisema Aisha huku akiachia tabasamu pana
Ndiyo!
Sasa hapo Masalu akakumbuka kuhusu suala hilo, alihitaji sana kuonana na msichana huyo ili amuulize kuhusu suala la mlango. Aliupataje ufunguo na kuufungua mlango huo na wakati yeye na mkewe waliutafuta kwa kipindi kirefu?
“Kwanza ilikuwaje mpaka ukaupata ufunguo?” alimuuliza huku naye akitabasamu.
“Ulikuwa chini ya kitanda. Yaani nilipouona tu, nikajisemea huu utakuwa ufunguo wa mlango wa nyuma, nikauchukua na kukimbilia huko,” alimjibu.
Ni kweli alikuwa akidanganya, tena kiwaziwazi lakini kwa sababu tayari Masalu alipenda, alikiona kila kitu kuwa ukweli kabisa, yaani alikubaliana naye kwa asilimia mia moja kwamba kweli ufunguo ulikuwa chini ya kitanda na wakati kila siku mkewe alikuwa akifagia na hakubahatika kuuona.
“Halafu mimi kuna baadhi ya mambo yananichanganya sana, hasa kuhusu wewe!” alimwambia.
“Mambo gani tena?”
“Yaani acha tu!”
“Kwamba unahisi mimi si mtu wa kawaida?”
“Wala siyo hivyo!”
“Kwamba mimi mchawi?”
“Yamefika huko tena!”
Aisha akatabasamu na kumsogelea Masalu pale kwenye kochi na kukaa karibu naye, akajisogeza mpaka akaubusu mdomo wake. Lile busu ni kama lilibadilisha kila kitu vile, akasahau mambo mengi, machache yaliyokumbukwa ni kwa namna alivyokuwa akimpenda msichana huyo.
Moyo wake ulikufa na kuoza, alikiri kwamba aliwahi kupenda mara nyingi tu lakini kwa huyo Aisha, mambo yalikuwa tofauti kabisa. Alimpenda kuliko alivyowahi kupenda huko nyuma.
Baada ya kubusiwa, sasa wakaanza kubadilishana mate. Hilo likakivuruga kabisa kichwa cha Masalu na kuona alikuwa akienda kuzidiwa. Akaanza kuipeleka mikono yake maungoni mwa Aisha na kutaka kulivua dela alilokuwa amelivaa.
“JamaniiiiiiiiiiiI!” alisema Aisha huku akijaribu kuitoa mikono hiyo.
“Tulia kwanza!”
“Yaani unataka unifanyizie humuhumu ndani kwangu?” aliuliza Aisha huku akichekacheka kimahaba.
“Kwani kuna ubaya?”
“Ndiyo! Kwa nini tusifanye kesho!”
“Kesho muda gani? Kwa nini linalowezekana leo lisifanyike leo mchumba?” aliuliza, yaani muda huo alikuwa amekwishavurugwa kabisa.
“Naomba tufanye kesho! Nitakupa kila kitu! Yaani kila kitu,” alimwambia.
Japokuwa alikuwa aking’ang’aniwa kupewa muda huo lakini alijishangaa kukubaliana na Aisha hivyo kumuacha, wakaendelea na maongezi yao na kuondoka mahali hapo.
Safari hiyo ilikuwa ni ya kwenda nyumbani kwake. Moyo wake ulikuwa na furaha tele, hakuamini kama alifanikiwa kubadilishana mate na mwanamke huyo. Nafsi yake iliridhika na hivyo kujipanga kwa ajili ya siku inayofuatia, yaani itakapofika basi afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anamvua nguo zote Aisha na kumuacha kama alivyotoka tumboni mwa mama yake.
“Kesho ndiyo kesho! Yaani atauona moto wangu!” alijisemea, muda huo alikuwa akiita bodaboda ili arudi nyumbani kwake.

JE, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 05.

Masalu akarudi nyumbani kwake akiwa na furaha tele. Njia nzima alikuwa akimfikiria Aisha. Alikuwa mwanamke wa tofauti kabisa na wote ambao aliwahi kuwashika maungoni mwao. Ngozi yake ilikuwa laini na alinukia mno.
Mwili wake ulikuwa na tamaa kubwa na kuahidi kwamba siku inayofuata ingekuwa balaa, yaani angetumia uwezo wake wote kumdatisha mwanamke huyo, yaani mpaka pale ambapo angeachana naye, angetamani kuwa naye kitandani mwake.
Akafika nyumbani. Siku hiyo alionekana kuwa na furaha mpaka mkewe alimshangaa. Ilikuwa ni vigumu kumuona mume wake akiwa na furaha kubwa kama siku hiyo. Akamuuliza chanzo cha furaha yake lakini ndiyo kwanza akamwambia habari za mpira kwamba timu yake ya Ulaya ilichukua kombe.
Mwanamke huyo akakubaliana naye, wala hakuwahi kuwa na hofu na mumewe. Alimpenda na kumwamini kuliko mtu yeyote yule kwa sababu hakuwahi kumkamata akiwa na mwanamke mwingine ama simu yake kuwa na tatizo lolote lile.
Siku hiyo Grace alimuhitaji usiku, alimpapasa mgongo na kila sehemu ya maumbile yake lakini Masalu akakaza, hakutaka kufanya naye mapenzi, alihitaji kuwekeza nguvu kwa ajili ya Aisha.
“Bebi! Leo nimechoka sana,” alimwambia huku akimwangalia kwa macho ya uchovu.
“Kidogo tu! Nina hamu na wewe!”
“Naomba tufanye kesho! Asubuhi na mapema!”
“Jamaniiiiiii!”
“Nakuomba mama!”
Japokuwa Grace alilalamika sana kumuhitaji mumewe lakini haikuwezekana hata kidogo, akalala zake na asubuhi ilipofika, akajifanya kuwa na haraka, huyo akaondoka zake kuelekea kazini.
Sasa akamkumbuka Aisha! Mwili wake ukasisimka mno, akaamua kuchukua simu yake na kumpigia. Kwanza ikaita mpaka ikakata. Akaona ameingizwa kwenye mataa, hakutaka kukubali, akampigia tena, simu ikaanza kuita kwa mara nyingine.
Aisha akapokea.
Sauti yake ilikuwa ileile.
Ya kumtoa nyoka pangoni.
Masalu akaweweseka zaidi.
“Mami umeamkaje?” alimsalimia.
“Salama tu! Ndiyo najiandaa hapa, nilitaka nikupigie simu!” alimwambia, maneno hayo yakamfanya Masalu kuweweseka zaidi, mpaka maeneo yake ya zipu ya suruali yakatuna.
“Aiseee! Kumbe ni kama bahati kukupigia. Kwa hiyo utataka tuonane wapi?” alimuuliza.
“Wewe unataka wapi?”
“Twende Magomeni Kanisani. Kuna kalodge fulani katamu sana!”
“Nielekeze!”
Akamuelekeza, tena kwa makini sana kama hatokuja kumuelekeza mtu tena kwenye maisha yake.
“Ila sasa....” alisema msichana huyo.
“Kuna nini?”
“Sikai sana. Ni kuanzia saa nne mpaka saa tano. Hakikisha saa nne kamili unakuwa hapo bebi! Usiniweke! Saa tano na nusu nitatakiwa kuwa Mabibo,” alimwambia.
“Hilo halina shida.”
“Sawa.”
Kulikuwa na mambo mengi sana ya kuchelewa lakini si ya miadi na mwanamke. Mwanamke ambaye ulikuwa umemtafuta kwa kipindi kirefu, tena alikupa mwili wake uupapase, akakupagawisha halafu ghafla tu eti uchelewe.
Kwa mwanaume, ilikuwa ni rahisi kuchelewa kazini, apewe adhabu ya kukatwa mshahara ama vyovyote vile ila si kuchelewa miadi ya mwanamke aliyekuwa amemtafuta sana halafu hajawahi kumvua nguo zake.
“Hivi nitachelewaje kwenye miadi na mwanamke?” alijiuliza na kucheka sana.
Ilikuwa ni majira ya saa tatu asubuhi. Akaona kwanza apige kazi na itakapofika saa tatu na dakika arobaini achukue bodaboda na kuelekea huko. Alifanya kazi zake kwa dakika ambazo alizijua yeye kuwa chache sana ila cha ajabu sasa akaenda dukani na kujikuta anaangalia saa yake na kugundua ni saa tano kasoro kumi.
Akashtuka.
Ilikuwaje tena?
Hilo inawezekana halikumshtua sana! Kilichomshtua zaidi ni kuangalia mazingira ya maeneo aliyokuwepo, hayakuwa ya kazini kwake, yaani yeye si alijua alikwenda kwenye duka la jirani hapo gereji kwake, ila alipoangalia duka ambao alisimama mbele yake, halikuwa duka lile la kazini kwake.
“Eeeh!” akamwangalia muuzaji.
“Umesema unataka vocha na nini?” alimuuliza muuzaji.
Akashtuka!
Akamwangalia muuzaji huyo. Hakumfahamu. Maeneo ya hapo pia hakuyafahamu, alikumbuka kabisa kwamba alikuwa kazini kwake Mburahati lakini ghafla tu akajikuta akiwa mahali ambapo hakupafahamu kwa haraka.
“Bro!” aliita muuzaji.
“Umesema nimeagiza vocha?”
“Ndiyo! Si umenipa elfu tano hapa. Ndiyo nauliza vocha gani!”
“Hebu subiri. Hapa wapi?”
“Mbezi Kwa Msuguri!”
“Mbezi Kwa Msuguri? Nafanya nini?” alimuuliza muuzaji.
Ni kweli alichanganyikiwa kupita kawaida. Hakuamini kama alikuwa Mbezi Kwa Msuguri. Alikuwa akifanya nini huko? Hakuwa na miadi ya kwenda huko, kwa siku kama hiyo ya Jumatatu ya kazi ilikuwa ni lazima kwenda ofisini kwake, ila ghafla tu alikuwa Kwa Msuguri.
Alikuwa akifanya nini huko?
Mara simu ya mkewe ikaingia. Akaipokea.
“Mama amenipigia simu amesema mzigo ameupata!” alisema mkewe.
Akashtuka zaidi.
Ni kweli huko Mbezi Kwa Msuguri ni nyumbani kwa wakwe zake. Sasa yeye alikwenda kufanya nini? Alipeleka mzigo, mzigo gani sasa?
“Mzigo gani tena?”
“Jamaniiiii! Si kile kitenge ulichomnunulia!” mkewe akamjibu.
“Ooh! Sawa! Haina shida,” alisema na kukata simu.
Eti alimnunulia kitenge mkwewe! Lini hiyo? Mbona hakuwa akikumbuka lolote lile. Ikambidi ampigie simu mfanyakazi mwenzake wa gereji na kumuuliza zaidi, alitaka kupata uhakika wa kile alichokutana nacho. Simu ikaanza kuita.
“Oya unatoka muda gani huko Mbezi?” aliuliza rafiki yake hata kabla ya kuongea lolote lile.
“Mbezi?”
“Ndiyo! Fanya fasta uje kazini basi!” alisema rafiki yake huyo.
Kama uliwahi kuchanganyikiwa! Nikwambie tu kwamba Masalu alichanganyikiwa zaidi yako. Sasa akayapeleka macho yake kwenye saa, ilikuwa ni saa tano kasoro dakika tano. Akapagawa.
Hakutaka kuchelewa, haraka sana akaita bodaboda na kuondoka mahali hapo. Alimwambia dereva aendeshe kwa kasi sana kwani alikuwa akiwahi mahali, dereva akafanya kama alivyoambiwa. Mpaka wanaingia Mburahati, tayari ilikuwa ni saa tano na dakika kumi na sita.
Akachoka hoi! Akaanza kumfikiria Aisha sasa. Mara simu ya msichana huyo ikaanza kuingia. Akaogopa, ikambidi tu aipokee.
“Leo umenikera sana! Yaani umenikera mno! Nimevaa cheni ya dhahabu kiunoni, nimekuvalia bikini, nimejipulizia marashi ya Pemba halafu umeniuza kifala sana! Aya bwana! Naona mkeo amenizidi ujanja, baki naye,” alisema Aisha hata kabla ya salamu.
Halafu akakata simu.
“Haloooo! Halooo! Aishaaaa! Halooo!” aliita huku kijasho chembamba kikimtoka.
Sasa Masalu akaanza kuhaha! Akampigia simu Aisha, ikawa inaita tu lakini haikuwa ikipokewa. Hilo likamchanganya kupita kawaida. Alipiga na kupiga lakini majibu yalikuwa ni yaleyale, simu haikupokewa.
Sasa akajiona fala! Ila pamoja na kujiona hivyo, aliendelea kujiuliza ni kipi kilikuwa kikiendelea? Ama alikuwa akiota? Hapana bwana! Akajing’ata mdomo, hakushtuka usingizini, akajipiga vibao napo ilikuwa vilevile.
“Oya! Mbona unajipiga vibao?” aliuliza rafiki yake, alimwangalia Masalu aliona kabisa alichanganyikiwa.
“Yaani acha tu!”
“Kuna nini?”
“Hivi nilikwenda Mbezi saa ngapi?”
“Asubuhi! Ulinipigia simu na kuniambia unakwenda Mbezi utachelewa kurudi!”
“Mimi nilikupigia simu?”
“Ndiyo!”
“Muda gani?”
Akaonyeshwa missed calls zake mbili. Ni kweli alimpigia simu saa tatu asubuhi.
“Mimi nilikupigia simu?”
“Ndiyo! Namba si ni hii hapa.”
Ikambidi kwanza aende pembeni na kutulia, aliendelea kujifikiria kilichotokea, bado hakuwa na majibu sahihi ya kulielezea suala hilo. Kwa kitendo cha mkewe kumpigia simu na kumwambia kuhusu suala la kitenge, kitendo cha kupigiwa simu na rafiki yake, tena alipopokea tu akamuuliza kuhusu suala la Mbezi, alikuwa na uhakika alikwenda huko yeye mwenyewe.
Ila muda gani?
Mbona hakukumbuka kabisa kuhusu suala la kwenda huko? Sasa akahisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, ila kwenye hilo hakutaka kumuhisi Aisha, alihisi tu labda alikuwa akienda kuwa chizi. Ikabidi ampigie tena Aisha simu, muda huu hakuwa akipatikana.
Yaani kwa hasira alizokuwanazo, akaamua kumzimia simu.

Asante
 
Similar Discussions

10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom