Naona imeenda na majiImekuwaje tena!!!!!
NyingineSEHEMU YA 06.
Sasa Masalu akachanganyikiwa, ilikuwa ni afadhali achanganywe na mke wake ambaye alimzoea na kulala naye chumba kimoja kila siku lakini si mwanamke kama Aisha. Alimpenda sana na alimuhitaji katika maisha yake.
Alipagawa, alitulia pale ofisini kwake lakini hakuona kama alitulia kama ipasavyo. Alifanya ujinga sana, hakutakiwa kumzingua mwanamke kama Aisha ambaye alikubaliana naye kwa kila kitu, yaani kwa ujinga wake tu mwisho wa siku likawa kama hilo la kutokea.
Alijifikiria sana kichwani mwake, akaona kazi hazifanyiki kama inavyotakiwa hivyo aliona ni jambo jema kama angerudi nyumbani kwake kupumzika. Akaaga na kuondoka.
Kila mtu alimshangaa, ilikuwa ni lazima kuwa hivyo kwa kuwa hakuonekana kueleweka hata kidogo. Alibadilika haraka sana tangu alipotoka huko Mbezi, kwa wakubwa wakahisi huko alikutana na jambo ambalo lilimfanya kuwa kwenye hali kama hiyo.
Hawakujua ni mwanamke ndiye aliyemfanya kuwa hivyo, hawakujua ni mapenzi ndiyo yaliyokuwa yakimpeleka kwa kasi kiasi hicho. Njiani alipokuwa akitembea kwa miguu kichwa chake hakikuacha kumfikiria Aisha, huyo mwanamke alikuwa namba moja moyoni mwake na hata kama angeulizwa kati ya Grace na Aisha alikuwa akimpenda nani, basi mwanamke huyo alikuwa namba moja.
Alitembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea nyumbani. Alipofika maeneo yale ya shule sasa akaanza kumkumbuka zaidi Aisha. Alikutana naye hapo mara ya kwanza, alimfahamia hapo, alimruhusu kumshika mapaja yake laini na kumuongezea hamu ya kufanya naye mapenzi.
Leo alikuwa akirudi nyumbani huku akiwa amemuudhi mwanamke huyo, alimkasirisha kupita kawaida. Hapo shule hakutaka kuvuka, akatulia, kulikuwa na kelele za wanafunzi waliokuwa darasani wakisoma lakini hakutaka kujali sana, ulikuwa ni wakati wa kumfikiria mpenzi wake na ilikuwa ni lazima kufanya hivyo.
“Hivi mbona nilizingua?” alijiuliza.
“Ila nilifanya ujinga sana,” akajijibu.
Alitulia hapo kwa dakika kama kumi hivi, muda huo alikuwa akijaribu kumpigia simu Aisha na kwa bahati mbaya kwake haikuwa ikipatikana. Hilo likamchanganya sana, alimpigia zaidi ya mara thelathini na saba kote huko aliambulia ziro.
Akaamua kusimama na kuondoka mahali hapo kuelekea nyumbani kwake. Safari yake nzima ilitawaliwa na mawazo makubwa ya Aisha, alijilaumu kwa ujinga alioufanya ambao sasa ulionekana kumuharibia kumkosa mwanamke huyo, na mbaya zaidi akaonekana kuwa Mswahili.
Hakuchukua muda mrefu akafika nyumbani kwake. Ilikuwa ni mapema tu, akamsikia mkewe akiongea na mtu ndani ya nyumba hiyo, hakuwa peke yake, bila shaka alipata mgeni ambaye alikuwa akizungumza naye. Akavua viatu na kuingia ndani.
Alipofika sebuleni tu, macho yake yakagongana na mkewe aliyeonyesha tabasamu lakini alipomwangalia mgeni aliyekuwa humo, akashtuka sana baada ya kumuona Aisha.
Ndiyo!
Alikuwa Aisha!
Aisha yuleyule wa shuleni!
Yuleyule aliyemzingua miadi ya kuonana naye.
Sasa mapigo yake ya moyo yakaanza kwenda kasi, hakuamini alichokuwa akikiangalia mbele yake. Alikuwa na hofu, mwili wake ukaanza kutetemeka kwa hofu na kijasho chembamba kikaanza kumtoka. Maswali kibao yakaanza kumiminika kichwani mwake.
Huyo Aisha alikuwa anafanya nini hapo?
Alijuanaje na mkewe?
Walikuwa marafiki kwa kipindi gani?
Sasa akatamani aulize maswali hayo yote.
Angeulizaje?
Aisha mwenyewe hakuwa na habari, ndiyo kwanza alikuwa akitoa tabasamu pana, na kubwa zaidi mwanamke huyo wala hakuonyesha kushtuka, ndiyo kwanza akasimama na kumsalimia.
“Habari yako shemeji!” alimsalimia Aisha. Sasa Masalu akawa na kitete.
“Salama! Karibu!”
Sasa mkewe akaanza kuwatambulisha. Hilo likafanyika, walikuwa wakijuana lakini kwa sababu mkewe alikuwa hapo sasa ikawabidi wazuge kama hawakuwa wakifahamiana hata kidogo na wakati siku hiyo tu walitaka kulala pamoja.
“Huyu rafiki yangu anaitwa Aisha!” alisema mkewe huku akimwangalia mumewe.
“Oh! Nimefurahi sana kumfahamu! Karibu sana,” alisema Masalu huku naye akijitahidi kutoa tabasamu, ila lile tabasamu ambalo halikutoka kabisa moyoni mwake.
“Basi mi nipo ndani!” alisema Masalu na kuelekea chumbani.
Humo, kwanza akajilaza kitandani, alichoka. Akili yake haikuwa sawa hata kidogo, alijiuliza huyo Aisha alikuwa akifanya nini chumbani hapo, halafu mbona mkewe hakuwahi kumwambia kama alikuwa na rafiki anayeitwa Aisha? Halafu akakumbuka kitu, siku ile mwanamke huyo alipokuwa ndani, mkewe aliporudi aliondoka kwa kupitia mlango wa nyuma, kwa nini hakubaki ndani?
Akaamua kupotezea japokuwa hakupata majibu ya maswali hayo. Huku akiwa humo chumbani mara simu yake ikaanza kuita, akaichukua na kuangalia, jina lilikuwa la Aisha, akashtuka, ila ikambidi apokee.
“We Aisha unataka nini kunipigia simu na wakati unajua mke wangu uo naye hapo?” aliuliza Masalu huku akionekana kushtuka.
“Nipo na mkeo? Unajitoa akili kwa sababu umenikosea sanaeeeee?” aliuliza mwanamke huyo.
“Aisha bhana!”
“Kwanza kwa nini umenifanyia hivi leo?”
“Najua nimekukosea. Ila tutaongea ukiondoka hapa nyumbani!”
“Nyumbani wapi? Hivi unajua nipo wapi?”
“Wewe si upo hapa nyumbani, nimekuacha sebuleni!”
“Masalu bwana! Yaani unanishangaza sana. Sasa mimi nije kwako kufanya nini? Mkeo mimi namfahamu kwani?’ aliuliza mwanamke huyo kwenye simu.
“Hebu subiri!”
“Sawa. Utanipigia nikusomee kesi zangu,” alisema mwanamke huyo na kukata simu.
Sasa hapo Masalu akashusha pumzi kwa nguvu, tena ile nzito kabisa. Maneno aliyozungumza huyo Aisha yalimchanganya mno, alimwambia hakuwa yeye, sasa yule sebuleni alikuwa nani? Alipoingia alimuona, halafu akamsalimia, tena alikuwa na uhakika alikuwa yeye, na jina lake aliitwa Aisha, sasa kama hakuwa Aisha, alikuwa nani?
Kwanza walifanana.
Sauti zao.
Sura.
Yaani kila kitu mpaka tabasamu.
Halafu eti anaambiwa siyo yeye! Akaona kama masihara.
Akatoka chumbani na kuelekea sebuleni, akateka kwenda kumuona kwa mara ya pili lakini alikuwa na uhakika aliyemuona alikuwa yuleyule Aisha. Alipofika sebuleni na kumwangalia. Hapo sasa akachanganyikiwa.
Hakuwa Aisha bwana!
Alimshangaa mgeni mpaka mgeni mwenyewe akajishtukia, maana haikuwa kwa kushangawa kule.
“Mimi nishakuwa mzee! Natoka kidogo! Hivi uliniambia mgeni anaitwa nani vile?” aliuliza Masalu huku akimwangalia mkewe, sasa akalazimisha tabasamu pana usoni mwake.
“Mwajuma!”
“Oh! Aya shemeji Mwajuma mimi natoka,” alisema Masalu na hakutaka kubaki mahali hapo, huyo akaondoka zake.
Mwajuma na Aisha! Mbona yalikuwa majina tofauti kabisa. Yaani aambiwe Mwajuma halafu yeye ahisi Aisha, hakika kwake ni kama kitu hicho hakikumuingia akilini mwake kabisa.
Sasa hapo kajifikiria ni wapi alitakiwa kwenda, kazini kwake ama wapi? Huku akiwa njiani kuelekea asipopajua akaona meseji ikiingia, kuifungua tu, mtumaji alikuwa Aisha.
‘Nipo huku karibu na uwanja wa mpira wa miguu, njoo huku’
Aliisoma meseji hiyo vizuri kabisa. Sasa akagundua Aisha alikuwa maeneo hayohayo ya karibu.
Je, nini kitaendelea?
Karibuni kutazama kazi nzuri kutoka FILAMU PICTURES
SEHEMU YA 09.
Hawakuchukua muda mrefu kufika nyumbani kwa akina Aisha. Mama’ake Aisha alipomuona Masalu tu akajua alikuwa ndiye mwanaume aliyekutwa makaburini, juu ya kaburi la marehemu binti yake. Alipomwangalia tu, kwa jinsi alivyokuwa, alikuwa tofauti na wenzake.
Akawakaribisha na kuingia ndani. Umati wa watu uliokuwa ukiwafuatilia ulibaki nje. Kila mtu alitaka kufahamu kilichokuwa kimetokea, ilikuwaje huyo mwanaume akae pale makaburini na kula majani? Halafu hakuwa peke yake, kulikuwa na wanaume ambao waliwahi kukutwa palepale makaburini kama yeye.
Masalu akakaa kwenye kochi, macho yake yalikuwa yakiangalia huku na kule. Nyumba aliyokuwa ndani yake muda huo ilikuwa ileile ambayo aliambiwa na Aisha ndipo alipokuwa akiishi.
Alishangaa sana.
Aliangalia kila kitu ndani ya nyumba hiyo, hakika ilikuwa ni ileile. Moyo wake ukawa na shauku ya kutaka kufahamu ni kitu gani kilitokea kwani kwa kila kitu kilimchanganya moyoni mwake, hata suala la kwenda kazini kwake hakutaka mpaka pale ambapo angejua ukweli wa kilichokuwa kimetokea.
Mama Aisha akaingia chumbani kwake na kuwaacha wageni wake sebuleni, baada ya dakika kama mbili hivi, akarudi huku akiwa na albamu iliyokuwa na picha kadhaa na kuanza kumuonyesha Masalu.
“Aisha!” alijikuta akijisemea baada ya kuiona picha ya msichana mmoja mrembo ambaye alisimama mbele ya maua. Alimfahamu mtu huyo, alikuwa Aisha wake.
“Huyo ndiye Aisha,” alisema mama yake.
“Nilimuona!”
“Uliyemuona si Aisha huyu! Hukumuona mtu, ulimuona jini,” alisema mwanamke huyo.
“Inawezekana vipi?”
“Kwani ilikuwaje?”
Hapo sasa Masalu akapata nafasi ya kuanza kusimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea tangu siku ya kwanza alipoonana na msichana huyo na kuzungumza naye, kumpenda na hatimaye siku moja kwenda nyumbani kwake.
Kila alichokuwa akikisimulia, halafu aliposema hakujua kama alikuwa jini, kila mmoja alishangaa! Lilikuwa jambo lisilowezekana mauzauza hayo yote yamtokee halafu hata asiwe na wasiwasi, yaani asigundue kama kulikuwa na kitu.
“Nini kilimtokea Aisha?” aliuliza Masalu baada ya kuona kila mtu mule ndani akimshangaa kwa kutokugundua kama msichana huyo alikuwa jini.
“Aisha alifariki dunia mwaka 1999 mwezi wa saba kwa kugongwa na gari hapo Manzese,” alisema mama yake na kuendelea:
“Baada ya hapo mjomba wake akasema twende tukamzike kijijini kama mila zetu zinavyosema, ila baba yake akakataa kufanya hivyo, hivyo tukamzika kwenye makaburi ya hapahapa Mburahati!” alisimulia mwanamke huyo.
Kila mmoja alikuwa kimya akimsikiliza, walihitaji kujua nini hasa kilichotokea mpaka Aisha kuwatokea watu na kuwapeleka makaburini.
“Ikawaje baada ya hapo?” aliuliza mwanaume mmoja, Masalu alikuwa kimya tu, yaani bado akili yake haikuwa sawa.
“Sasa ndiyo nahisi hili jini likaanza kuwatokea watu. Kuna wanaume kadhaa waliokuwa wakitokewa na mwisho wa siku kupelekwa makaburini na kuanza kula michanga. Kwa kweli ninashangaa sana, nadhani ni kwa sababu ya kukataliwa mwili wake kuzikwa Tanga, hivyo kuna mauzauza huwa yanatokea,” alisema mwanamke huyo.
Alisimulia mambo mengi. Kila mtu aliyekuwa akisikiliza mahali hapo alishangaa. Kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa na jini la Aisha ni kutisha watu tu, hakuwa akiwaua ama kuwapelekea matatizo yoyote yale, kazi yake ilikuwa ni kuwasumbua tu, kuwapelekesha na kuwapa mauzauza.
“Hebu subiri kwanza! Kwa maana hiyo huyu si mtu wa kwanza?” aliuliza jamaa mmoja.
“Ndiyo! Nililisema hilo kabla!”
“Ninachotaka kufahamu ni kitu kimoja mama! Kama huyu si wa kwanza, inamaana pia hatokuwa wa mwisho. Na mtu akiwa ametokewa hivi, nini kifanyike ili asitokewe?” aliuliza jamaa huyo.
“Subiri!”
Mwanamke huyo akainuka na kuelekea chumbani. Wageni wake wakabaki sebuleni, muda wote huo Masalu alikuwa kimya, ni kama alikuwa akifikiria yale yaliyokuwa yametokea, yalimtisha na kumuogopesha sana. Alikuwa na mkewe, akaingiwa na tamaa na kutaka kuwa na mwanamke mwingine, mwisho wa siku matokeo yake yakawa mabaya kama ilivyokuwa.
Mwanamke huyo hakuchukua dakika nyingi akarudi akiwa na unga fulani hivi na maji, akampa Masalu na kumwambia anywe, akafanya hivyo na kumsomea dua ndogo na baada ya hapo akamwambia kila kitu kingekuwa shwari kabisa, Aisha asingemtokea tena.
“Mama! Ninaogopa!” alisema Masali huku akimwangalia mama yake Aisha.
“Usiogope!”
“Mimi wa kula majani makaburini kweli?”
“Pole sana! Hutokea hayo! Usimtamani kila mwanamke mzuri unayekutana naye mtaani,” alisema mama Aisha na baaa ya hapo wageni hao wakaondoka mahali hapo.
Masalu akasindikizwa mpaka nyumbani kwake. Grace alipomuona mumewe akija na watu huku akionekana kama kutokuwa sawa akawa na hofu, akahisi kulikuwa na jambo baya lilimtokea, akawapokea na kumwangalia vizuri Masalu.
Ni kweli hakuwa sawa.
Akawauliza kilichotokea, akajibiwa kwamba ni matatizo tu ya kawaida, walimkuta akiwa amelala njiani, inaonekana alikuwa akiumwa. Hivyo akapelekwa chumbani na kutulia kitandani.
Hakuzungumza kitu chochote kile na kwa sababu watu wale walimwambia mkewe alikuwa mgonjwa, naye akaigiza hivyohivyo kiugonjwaugonjwa na kulala huku moyoni mwake akijiapiza kwamba mpaka atakapokufa hatochukua tena mwanamke njiani kama alivyofanya kwa Aisha.
Kutokana na hofu nzito aliyokuwanayo moyoni, hakutaka kurudia kupitia njia ile ya makaburini, akaamua kubadilisha na kupita barabarani.
Masalu akabadilika kabisa. Kila siku alikuwa akimfikiria Aisha, alimuogopa mwanamke huyo, japokuwa alikuwa akimpenda kipindi cha nyuma lakini hakutaka kuonana naye tena kwenye maisha yake.
Akabadilika!
Akaachana na mambo ya wanawake.
Akatulia na mkewe mpaka leo hii.
MWISHO.