Simulizi:Dereva Taxi (Dar mpaka Chuga)

Simulizi:Dereva Taxi (Dar mpaka Chuga)

TITLE: DAR MPAKA CHUGA.
SEHEMU YA TANO.

SIKU KADHAA BAADAE-HOSPITALI
Mkwere yupo wodini amelala kitandani mkononi akiwa na pingu iliyounganishwa pale kitandani, “mimi wale sipo nao wala siwajui..huo ndio ukweli wangu” anasema Mkwere, pembeni yupo Afande Okwi na Afande P, “mimi ni dereva wa taxi tu” anaongeza Mkwere, “unaahidi utatoa ushirikiano tunaohitaji?” anasema Afande Okwi, “nitatoa ushirikiano kadri niwezavyo” anasema Mkwere, “kama ulijua mapema kuwa wale ni Watu hatari sasa ni kwa nini ulibishana nao na kuhatarisha maisha yako?” anauliza Afande P, “kwa sababu nilijua hata ningewafikisha wanakoenda wasingeniacha hai” anasema Mkwere, “kwa nini ulidhani hivyo?” anauliza Afande Okwi, “Nimeendesha taxi kwa muda..nisingeweza kuwaamini kama wangeniacha hai hata kama ningewafikisha waendako” anasema Mkwere, wanabaki kimya kwa muda, Afande Okwi anashusha pumzi, “sasa kwa kuwa hali yako imetengemaa..kesho alfajiri tunaenda Dar na ninaamini utatupa ushirikiano wako kadri inavyowezekana” anasema Afande Okwi, “wala msitie shaka afande” anasema Mkwere,wanabaki kimya kwa sekunde chache, “ila..naomba kama inawezekana mnipe simu niongee tu na familia yangu” anasema Mkwere, Afande Okwi na Afande P wanaangaliana, “natumai namba za mkeo unazo kichwani” anasema Afande Okwi huku anatoa simu na kumpa Mkwere.

JIJINI DAR-SIKU MOJA BAADAE-NYUMBANI KWA YKIKEKE-MCHANA.
Mkwere, akiwa na amevaa plastiki nzito shingoni inayotumiwa na waliovunjika shingo na bandeji kubwa mkononi, yupo na Afande Okwi, Afande P na Suzi, wapo barazani, “unajua shughuli za baba yako?” Afande P anamuuliza Suzi, “ni mfanya biashara” anajibu Suzi, “biashara gani?” anauliza Afande Okwi, “Hoteli na nyumba za kulala Wageni Dar na Arusha”anasema Suzi, wanabaki kimya kwa muda, “sasa ni hivi” anasema Afande Okwi, “kuanzia sasa hivi upo chini ya ulinzi” anasema Afande okwi huku Suzi akionekana kupata mshtuko, “na sasa hivi tunaongozana mpaka Arusha na utatuonyesha alipo baba yako” anaongeza Afande P, Suzi anabaki na butwaa, “ukitaka kazi iwe rahisi itakuwa rahisi” anasema Afande Okwi, Suzi anashusha pumzi huku akionekana kuishiwa nguvu, anaketi chini, “kwani ana kosa gani?” anauliza Suzi, “hana kosa lolote..tunahitaji tu kuonana naye” anasema Afande P huku akimuinua Suzi pale chini na kumpeleka lilipo gari aina ya Land Cruizer, "naomba nikavae vizuri" anasema Suzi, "nguo tutakupa" anasema Afande P huku akimuingiza Suzi garini, "TV nimeiacha on" anasema Suzi baada ya kuketi, "ya hapa nyumbani hayakuhusu tena kwa sasa..tumewaletea Wasaidizi" anasema Okwi huku akimuonyesha Suzi Wanaume Wanne waliojihami vema waliosimama kuzunguka eneo la nyumba, Afande Molu anawasha gari na kuiondoa.

JIJINI ARUSHA-NYUMBANI KWA YKIKEKE.
Gari aina ya Nissan Patrol yenye nembo ya APS ubavuni (Arusha Parcel Services), kampuni ya kusambaza vifurushi ipo getini, nje ya jumba moja kubwa la kifahari, geti linafunguka na gari inaingia, Afande Okwi akiwa amevalia suti maridadi anateremka akiwa na kifurushi mkononi na kufika mlangoni, anabonyeza kengele, mlango unafunguliwa, anatoka Ykikeke akiwa amevalia tracksuit maridadi nyeupe, anapokea kifurushi na kitabu na kalamu na kusaini, mara kwenye gari anatoka Afande Bodu, “upo chini ya ulinzi” Ykikeke anashtushwa na sauti kali ya Afande Okwi, huku akimuona Afande Bodu akiwa na bastola, Ykikeke anainua tshirt na kutaka kutoa bastola yake, “na usijisumbue Mzee” anasema Afande Okwi huku akimuonyesha juu ya nyumba iliyopo jirani, Ykikeke anaangalia na kuwaona Jamaa kadhaa waliojihami sawasawa wakiwa juu ya paa, anageuka na kuwaona wengine juu ya ukuta unaozunguka nyumba yake, wote wakiwa na silaha zao tayari tayari, “shit” anatamka Ykikeke kwa sauti ya kukata tamaa, "ukirudi ndani tunaiteremsha nyumba nzima" anasema Afande Bodu, huku na Afande P naye anakuja walipo naye akiwa amejihami vilivyo, “mikono juu” anasema Afande Bodu huku akiipeleka bastola usoni kwa Ykikeke, Ykikeke ananyoosha mikono juu, huku Afande Bodu akimpa Okwi na P ishara za kuingia ndani ya nyumba, Afande P na Afande Okwi wanaingia ndani huku wakizikoki bastola zao mkononi tayari tayari, Afande Bodu anamsachi Ykikeke na kuitoa bastola iliyo kiunoni, kisha anatoa pingu na kumfunga mikono.

Sekunde kadhaa baadae anatoka Afande Okwi na P wakiwa na yale mabegi mawili yenye pesa, huku wakitanguliwa na Adamuu ambae ana bandeji kubwa mguuni huku akichechemea kwa kutumia magongo, “kaa hapo chini” Afande Bodu anamuamuru Adamuu, Adamuu anaketi kwa shida akionekana mwenye maumivi makali, Adamuu anajaribu kutoa bastola, mara anapatwa na risasi mbili kifuani zilizotokea kwenye paa la nyumba ya jirani, Adamuu analala pale sakafuni na kutulia tuli, “mmeniacha mkiwa nyie Wakenge” anasema Ykikeke huku akimuangalia Adamuu alivyotulia pale chini, “funga mdomo” anang’aka Afande Okwi huku akibamiza mbata nzito utosini kwa Ykikeke na kusababisha mlio kama wa puto lililopasuka.

JIJINI DAR-NDANI YA OFISI YA BENKI MOJA KUBWA.
Mkwere, Mr Top na Helen wapo ofisini, “umewezesha kusambaratishwa kwa mtandao mkubwa sana wa uhalifu” anasema Mr Top, “walitusumbua sana hawa Washenzi” anaongeza Mr Top, “kwa hiyo leo tunakukabidhi hii cheki” anasema Mr Top huku Bi Helen akitoa cheki na kumpatia Mkwere, “milioni ishirini” anasema Bi Helen, “nashukuru sana” anasema Mkwere huku akiipokea cheki ile na tabasamu kubwa usoni.

MWISHO.
 
Duh,.....sio Watu wa michongo sio?
Angevunga tuu.angejikuta ana.ela.yake safi tuu.anaogopa sna kifo wakati atakufa tuu.
Anaogopa kumuacha mke wake mmoja tu wakati kule mbinguni angepata 72 tena mabikra
 
Angevunga tuu.angejikuta ana.ela.yake safi tuu.anaogopa sna kifo wakati atakufa tuu.
Anaogopa kumuacha mke wake mmoja tu wakati kule mbinguni angepata 72 tena mabikra
Duh, hiyo kali aise.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom