Simulizi:Dereva Taxi (Dar mpaka Chuga)

Simulizi:Dereva Taxi (Dar mpaka Chuga)

JOTO LA MOTO

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2018
Posts
766
Reaction score
562
SCRIPT ZA IMA.​

MTUNZI:MSANII JOTO LA MOTO.
SEHEMU YA KWANZA.

NYUMBANI KWA MKWERE CHUMBANI-ASUBUHI.
Mkwere, kijana, 30, yupo kitandani amelala, pembeni kwenye kochi wapo Erin,mtoto, binti wa miaka 7,na Roda,mdada wa miaka 27, wameketi kwenye sofa wakipata kifungua kinywa, Erin akiwa amevaa sare za shule, Roda anainua kikombe na kumnywesha Erin kumalizia chai kidogo iliyopo kwenye kikombe, “haya inuka twende” Roda anasema huku anainuka na kumuinua Erin, Erin anachukua begi lake na wanatoka.

Zinapita dakika kadhaa, mlango unagongwa, Mkwere bado yupo kitandani amelala, mlango unagongwa mara kadhaa, anashtuka na kuinua kichwa, mlango unagongwa tena, anainuka na kushuka kitandani, anachukua T shirt iliyotundikwa kwenye msumari ukutani na kuivaa kisha anaenda mlangoni na kuufungua mlango, mlangoni yupo Mama Tufe, mama wa makamo, wa miaka 67 hivi, Mkwere anashtuka, “mama shikamoo” anasalimu, “pesa yangu” anasema Mama Tufe kwa sauti ya chini lakini inayoashiria shari, Mkwere anashusha pumzi, “sasa ni hivi..naomba mtoe vitu vyenu nje kuna Mpangaji namleta sasa hivi” anasema Mama Tufe kisha anaondoka, Mkwere anabaki ameduwaa kwa muda, kisha anafunga mlango na kwenda kuketi kwenye kochi, zinapita sekunde kadhaa, mlango unafunguka anaingia Roda, Mkwere ameketi kochini kinyonge huku amejishika tama, “kulikoni baba Erin?” Mkwere anainua kichwa, “kwa nini hukuniamsha?” anauliza Mkwere, “lini nimekuamsha na ukaamka kwa wakati huo huo Baba Erin?” anauliza Roda, Mkwere anabaki kimya, anashusha pumzi,“Mama Mwenyenyumba amekuja amenikuta” anasema Mkwere, “dawa ya deni ni kulipa Baba Erin..sio kukimbia” anasema Roda, Mkwere anabaki kimya, “kwa hiyo amesemaje?” anauliza Roda,“amesema tutoe vitu nje” anasema Mkwere huku Roda akiketi pale kochini, “Mungu wangu” anasema Roda na kushuhsha pumzi “kwa hiyo sasa tunafanyaje?” anauliza Roda, “itabidi tufungashe” anasema Mkwere kwa sauti ya kukata tamaa, Roda anashusha pumzi na kutulia kwa muda, “Baba Erin..tukifukuzwa tena na hapa..namchukua Erin tunarudi zetu shamba” anasema Roda, “umeanza” anasema Mkwere kwa mshtuko huku akigeuka kumuangalia Roda, “habari ndio hiyo Baba Erin” anasema Roda, wanabaki kimya kwa muda, “ulijigamba umepata kazi mambo mazuri..kumbe”, anasema Roda na kutulia, “kila siku ni kulalama tu” Roda anaendelea kusema, “kama hilo gari bovu unang’ang’ania hiyo kazi ya nini?” anasema Roda, wanabaki kimya kwa muda, Mkwere anashusha pumzi, “mimi ni Mwanaume..sitakosa ufumbuzi” anasema Mkwere huku anainuka, “na hilo la kurudi Shamba utarudi wewe mwenyewe mwanangu haondoki hapa” anasema Mkwere huku anachukua mswaki na taulo na kutoka, “tutaona” anasema Roda baada ya Mkwere kutoka nje.

NYUMBANI KWA BONGE-ASUBUHI.
Mkwere akiwa juu ya bodaboda wanafika mbele ya geti, anashuka kutoka kwenye boda boda na kwenda kugonga geti, geti linafunguliwa na Mzee Matata,mzee wa miaka 70, “Shikamoo Mzee” Mkwere anamsabahi Mzee Matata huku anaingia getini,“marahaba kijana wangu..vipi leo mbona unaonekana mnyonge?” anauliza Mzee Matata huku akitoa Daftari na kumpatia Mkwere, “achana na madaftari yako kwanza..bosi yupo?” anasema Mkwere bila kupokea lile daftari, “ameshatoka..kwani vipi?” anauliza Mzee Matata, “Mke wake?” anauliza tena Mkwere, “yupo ndani..kuna nini mbona sikuelewi” anauliza Mzee Matata, “kazi yao siitaki tena” anasema Mkwere huku anaketi kwenye kiti kilichopo pale getini, “namsubiri Mkewe hapa nimwambie” Mzee Matata anabaki anamuangalia Mkwere kwa mshangao, “ningeamua kuishia huko huko lakini maisha kuna leo na kesho..acha niwaage tu vizuri” “kwa hiyo nikupe maagizo aliyoacha Mzee ama niache tu?”, “maagizo gani?” anauliza Mkwere, “alisema leo utumie hiyo Premior mpya ya Mama” Mkwere anashtuka na kumuangalia Mzee Matata, kisha anageuka kuiangalia ile Toyota Premior mpya ya silva yenye usajili wa DDM kwenye plate number, “ndio alivyosema?” anauliza Mkwere kwa mshangao, “na kasema ukiikwaruza hata kwa kucha unarudia kwenye ule mkweche wako” anaongeza Mzee Matata huku akimpatia Mkwere ufunguo wa gari, Mkwere anapokea ule ufunguo huku akionekana bado ana butwaa, “uwe makini..si unamjua huyu Mama mtiti wake?” anasema Mzee Matata huku wanaelekea ilipo gari, “na ukipata trip ya madongo kuinama achana nayo”, “usinifundishe kazi wewe mzee..maana unaongea sana kama redio ya kijiji” anasema Mkwere huku anafungua mlango na kuingia kwenye gari, anapiga moto, “hujasaini” anasema Mzee Matata huku akimpa Mkwere daftari, Mkwere anapokea daftari, anasaini na kumrudishia Mzee Matata lile daftari kisha anafunga mlango na kutoa simu na kuibofya, “Mama Erin” Mkwere kwa bashasha na tabasamu kubwa anaongea na simu, “nenda kwa Mama mwenye nyumba mwambie pesa yake ipo tayari” anasema Mkwere, “imekuwaje kwani?” anauliza Roda kwenye simu, “leo nimeanza kazi rasmi” anasema Mkwere, “umepata kazi mpya?” anauliza Roda, “kazi ni ile ile gari ndio mpya” anasema Mkwere, “bado sijakuelewa Baba Erin”, anasema Roda, “napita hapo muda si mrefu utanielewa tu” anasema Mkwere, “mmh” anaguna Roda, “baadae ngoja nikapige kazi” anasema Mkwere na kuitoa simu sikioni, anashusha kioo “fungua geti wewe Mzee” Mkwere anapayuka, “usinifundishe kazi wewe Mtoto” Matata anasema huku akienda getini na kufungua geti na gari inatoka.

HOTELI MNAZI MMOJA-NDANI-ASUBUHI
Idd Riss, kijana wa miaka 27 hivi, mtanashati aliyevalia maridadi, anafika mapokezi huku akiwa amebeba jaketi mkononi na mkoba mdogo wa ngozi, anaangalia saa yake ya mkononi, “Watu wa Arusha utawajua tu” anashtushwa na maneno ya Adela, dada mrembo wa pale mapokezi “narudi nyumbani ooo” Idd Riss anaimba huku akisogea na kuweka mkoba na jaketi juu ya meza ya mapokezi, “lete bili yangu” anasema Idd Riss, “ndio safari?” anauliza Adela, “sio kitu ya kuuliza” anajibu Idd Riss huku akipokea bili kutoka kwa Adela, anaingiza mkono mfukoni na kutoa waleti, anatoa bunda la noti na kumpatia Adela, Adela anapokea na kuanza kuhesabu “keep chenji” Idd Riss anasema huku akiinua mkoba na jaketi lake na kuondoka, Adela anabaki akiwa na tabasamu kubwa usoni, “safari njema” anasema Adela kwa sauti ya juu iliyojaa bashasha huku Idd Riss akitoka mlangoni.

HOTELI BLUE SEA KARIAKOO-NDANI-ASUBUHI
Adamuu, jamaa,27 aliyevalia maridadi nguo zenye gharama, yupo mapokezi akiwa na jaketi mkononi, anatoa pesa na kumpatia bwana aliyepo pale mapokezi, kisha anachukua mkoba ulio juu ya meza ya mapokezi, anaelekea mlangoni na kutoka.
 

Attachments

  • 3.jpg
    3.jpg
    165.4 KB · Views: 83
3.jpg


HOTEL BLUE SEA-NJE-UPANGA-ASUBUHI.
Adamuu anatoka na kwenda kwenye gari moja ya kifahari aina ya BMW nyeupe iliyopaki pembeni, kwenye gari yupo Ommy, kijana mtanashati, 26,“vipi Bro” anasalimia Ommy baada ya Adamuu kuufungua mlango na kuingia, “poa” anajibu Adamuu,“wapi?” anauliza Ommy huku mdomoni anatafuna jojo, “tunampitia Idd Riss Mnazi mmoja” anasema Adamuu huku akiwa bize akibofyabofya simu yake, Ommy anawasha Gari na kuondoa.

NYUMBANI KWA MZEE YKIKEKE-UPANGA
Gari linafika nje ya geti, mbele ya jumba moja kubwa la kifahari, geti linafunguka na gari linaingia, wanateremka Idd Riss na Adamuu, wote wakiwa na mikoba na majaketi mikononi, “Dar mnakuja lini tena Wakuu?” anauliza Ommy akiwa ametoa kichwa dirishani, Adamuu bila kujibu anafanya ishara ya simu sikioni akimaanisha ‘tutakupigia’, Ommy anaitikia kwa kichwa huku akiondoa gari, Idd Riss na Adamuu wanaelekea ulipo mlango mkuu wa jumba lile na kuingia.

Sebuleni ameketi Ykikeke ,Bwana wa makamo, miaka 50 hivi, Mtanashati akiwa amevalia maridadi, shati zuri la kitenge na suruali nyeusi ya kitambaa, ameketi kwenye sofa akisoma gazeti, Idd Riss anampa Adamuu ishara ya kuwa kimya akiweka kidole kwenye mdomo, polepole wanavuta viti na kuketi kwenye meza ya chakula iliyo pembeni.

wanabaki wameketi kimya, anakuja Suzi, Binti mrembo,20, akiwa na trei iliyosheheni maakuli, mapochopocho ya aina mbali mbali “shikamooni” anasalimia Suzi “marahaba” wanaitikia Idd Riss na Adamuu kwa pamoja. “karibuni” anasema Suzi huku akiweka mzigo ule mezani, Adamuu na Idd Riss wanachukua vikombe na kuanza kujihudumia yale maakuli. Zinapita dakika kadhaa ukimya ukiwa umetawala, zikisikika tu sauti za kutafuna na kunywa chai na mlio wa kurasa za gazeti analofungua Ykikeke,“tuna nusu saa tu” wanashtushwa na sauti ya Ykikeke inayokatisha ukimya ule “na nina imani kila kitu kitaenda kama tulivyopanga”, anaongeza Ykikeke huku akiangalia saa yake mkononi, wanabaki kimya kwa sekunde chache, “Idd Riss” anaita Ykikeke, Idd Riss anashtuka huku akimuangalia Ykikeke, “dakika tano zinakutosha kutafuta usafiri” anasema Ykikeke huku macho yake bado yakiwa kwenye lile gazeti “sawa bosi” Idd Riss anasema huku anainuka na kuelekea mlangoni na kutoka.

MTAANI UPANGA.
Idd Riss anatoka getini na kuanza kutembea pembezoni mwa barabara, anaenda kwa mita kadhaa na kusimama ukingoni mwa barabara, anatoa simu yake na kuanza kuitumia huku akiangalia kwa makini kila gari linalokuja, inakuja gari moja ndogo aina ya Carina, inapunguza mwendo “Taxi kaka” anasena Dereva wa ile gari anapofika usawa wa Idd Riss, Idd Riss bila kujibu anaisogelea gari ile huku akiikagua kwa makini, “nafika mikocheni ila nina buku mbili tu bro” Idd Riss anamwambia Dereva “Duh..hayo ni matusi ndugu yangu” anatamka Dereva kwa mshangao, “Mikocheni ni elfu ishirini kaka” anasema Dereva “Ah basi bwana acha nisubiri Bajaji” anasema Idd Riss, Gari linaondoka.

Zinapita dakika kama tano, inakuja gari nyingine, Toyota premior ya silva, Inapunguza mwendo “Taxi mzee” Mkwere anasema huku katoa kichwa dirishani, Idd Riss anabaki kimya kwa muda akiiangalia ile gari, kisha anaisogelea “nafika Mlimani City” Idd Riss anamwambia Mkwere huku anafungua mlango na kuingia, “Habari ya asubuhi ndugu” Idd Riss anamsalimia Mkwere “salama tu ndugu yangu”, “Ila nitaomba msaada wako kidogo..nachukua kompyuta yangu pale ndani” anasema Idd Riss huku akionyesha lilipo geti, “hamna shaka ndugu” anajibu Mkwere kisha anaelekeza gari lilipo geti, anapiga honi, geti linafunguliwa na gari inaingia na kupaki nje ya mlango wa kuingilia ndani, Idd Riss anateremka na kuelekea ndani ya jumba lile.

Sekunde chache baadae Idd Riss anarudi akiwa amebeba boksi la ukubwa wa wastani huku akimpa Mkwere ishara ya kufungua buti, buti inafunguka na Mkwere anateremka kwenda kumsaidia Idd Riss kuingiza lile boksi, mara Mkwere anashtuka kumuona Adamuu na Ykikeke wanatoka, Adamuu akiwa amebeba dumu la mafuta la lita ishirini, na Ykikeke akiwa amebeba mfuko wa sandarusi mkononi “upo na wenzako?” anauliza Mkwere kwa mshangao, “ndio” anajibu Idd Riss, “na tunaenda Arusha” anasema Ykikeke huku akifika pale walipo Idd Riss na Mkwere.
 
TITLE: DEREVA TAXI(DAR MPAKA CHUGA)
SEHEMU YA PILI.


Mkwere anashtuka na kubaki anaduwaa huku akimuangalia Idd Riss, “ni shilingi ngapi?” anauliza Ykikeke huku akiuweka ule mfuko kwenye buti, Mkwere kwa kuibia anaangalia ule mfuko na kugundua kumechomoza mdomo wa SMG, Ykikeke anafunga lile buti,Mkwere anapatwa na uoga na uso unaanza kutoka jasho jembamba, “Wazee mtanisamehe mimi siwezi kwenda Arusha” anasema Mkwere kwa sauti iliyojaa unyenyekevu na uoga, “naomba niwatafutie gari nyingine” anaendelea Mkwere, Idd Riss, Adamuu na Ykikeke wanaangaliana, Idd Riss anatoa bastola, huku Adamuu akiingia garini na kufungua kifuniko cha mafuta na kwenda kwenye tenki na kuanza kujaza mafuta yaliyopo kwenye lile dumu kwa kutumia mpira, “utachagua moja ndugu” Idd Riss anamwambia Mkwere huku akikoki bastola, “ufanye hii kazi tukupe ujira wako..au ukose kila kitu” anasema Idd Riss, Mkwere anabaki ameduwaa kwa hofu, “unataka shilingi ngapi?” anauliza tena YKikeke, Mkwere bado amebaki ameduwaa, “milioni moja itakutosha?”, “au mbili..au tatu” anaongeza Ykikeke, Mkwere anashusha pumzi “tufanye hivi Wazee” anasema Mkwere, “nawaachia hii gari nyie muende mnapoenda” anasema Mkwere, “hivi unaelewa kiswahili we Tumbili wa kike” anadakia Ykikeke kwa ukali na kumkwida Mkwere, “hakuna mwenye shida na huu mkweche wako” anasema Ykikeke kwa sauti iliyojaa vitisho, “sisi tunachotaka utupeleke Arusha tu basi” anasema Yikeke, Mkwere anabaki ameduwaa, “lete simu yako” anasema Ykikeke, Mkwere anaingiza mkono mfukoni na kutoa simu na kumpatia Ykikeke, Idd Riss anamsachi Mkwere mifukoni, anatoa wallet, anaifungua na kutoa leseni ya udereva na kumpatia Ykikeke, kisha anamrudishia Mkwere ile waleti,“ingia kwenye gari” Ykikeke anamuamuru Mkwere, Mkwere anaingia garini.

Ykikeke anaelekea ndani ya nyumba, baada ya muda kidogo anatoka akiwa amebeba mabegi mawili ya ukubwa wa wastani na kupokewa na Adamuu, “muonyeshe huyo Ndezi aelewe tunachoongea” anasema Ykikeke, Adamuu anachukua begi moja na kwenda kwenye gari na kulifungua, Mkwere anaangalia begi lililosheheni mabunda ya pesa mpya za nchini pamoja na dola za kimarekani, “ukikamilisha kazi utachota zinazokutosha ukale maisha” anasema Ykikeke, “yapo mabegi mawili” anasema Adamuu huku akifunga zipu ya begi na kwenda kuyaweka mabegi yale kwenye buti, Suzi anakuja na boksi ambalo ndani yupo Jogoo mkubwa mweusi, anampatia Adamuu lile boksi, kisha Adamuu, Idd Riss na Ykikeke wanaingia kwenye gari.

Wote wanabaki kimya kwa sekunde kadhaa huku Ykikeke akiwa ameketi siti ya mbele akiangalia ile leseni ya Mkwere, “Mkwere” anaita Ykikeke na kumfanya Mkwere ashtuke, Idd Riss anampatia Ykikeke ile simu ya Mkwere, Ykikeke anaipokea na kuiangalia kwa muda kisha anamuonyesha Mkwere picha inayoonekana kwenye ile simu “hii ni familia yako bila shaka?” Ykikeke anamwambia Mkwere huku kwenye simu inaonekana picha ya Mkwere,Roda na Erin, Mkwere anabaki kimya “ni hivi ndugu..tunaenda Arusha” Ykikeke anamwambia Mkwere kwa sauti ya upole huku akimpatia ufunguo wa gari, “na ukiharibu hii kazi hutokutana na hii familia yako tena” anaongeza Ykikeke, Idd Riss na Adamuu wanatoa bastola na kuzikoki kwa pamoja, “nadhani unaona tulivyokamilika” anasema Ykikeke, wanabaki kimya kwa muda,“tungeendesha sisi lakini trafiki hawatozipenda leseni zetu” anasema YkiKeke, Mkwere anashusha pumzi na kubaki kimya kwa sekunde mbili hivi, “ok Wazee..ninawapeleka Arusha..ila na mimi nina ombi moja” anasema Mkwere kwa sauti iliyojaa hofu, “mniachie tu uhai wangu” anasema Mkwere huku akimuangalia Ykikeke, Ykikeke anampa Mkwere mkono, Mkwere anasita kidogo kisha ananyoosha mkono kumpa Ykikeke, “deal” anasema Ykikeke huku wakishikana mikono, kisha Mkwere anawasha gari, geti linafunguka na gari linatoka.
 
TITLE DEREVA TAXI (DAR MPAKA CHUGA)
SEHEMU YA TATU.


BARABARANI-CHALINZE PWANI
Gari, Toyota Premior linaenda na kufika mita kadhaa kabla ya njia panda ya Chalinze, “ingia hapo kulia” Ykikeke anamuamuru Mkwere kukatisha njia na kuchukua njia ya vumbi, wanaenda kwa mwendo kama wa kilomita tano hivi, “kwenye nyumba ile” anasema Ykikeke huku akionyesha nyumba moja kuukuu ya udongo iliyojitenga, wanafika na kusimama mbele ya nyumba ile, “shuka” Ykikeke anamuamuru Mkwere, wote wanateremka huku Adamuu akishuka na lile boksi lenye Jogoo, wote wanaelekea mlangoni huku Idd Riss akimuamuru Mkwere nae kuingia baada ya kuonekana anasita sita, wanaingia kwenye kona ameketi Mzee Mbirikolo, babu wa miaka 75 hivi, akiwa amevalia kaniki nyeusi na shuka nyekundu na usinga mkubwa mkononi, Wanavua viatu na kuketi kwenye mkeka ulio mbele ya Mzee Mbirikolo, Adamuu anafungua box, anamtoa Jogoo na kumuweka mbele ya Mzee Mbirikolo, wanabaki kimya wametulia huku Mzee Mbirikolo kwa muda wote huo amefunga macho na kutoa ishara na mingurumo kama Mtu anayeugulia maumivu, huku akipunga usinga huku na kule ,anamaliza na kufungua macho “mmmh” Mzee Mbirikolo anatoa sauti kama ishara ya kuwa yupo tayari kuwasikiliza “Mzee wanao ndio tunarudi” anasema Ykikeke, “mmefanikiwa bila shaka?” anauliza Mzee Mbirikolo, “tumefanikiwa” Ykikeke anajibu huku Mzee Mbirikolo akitoa unga wa kijivu kwenye kibuyu na kuwapulizia usoni mmoja baada ya mwingine, “nawatakia safari njema” anasema Mzee Mbirikolo, Ykikeke anatupia noti kadhaa za elfu kumi kwenye ungo uliopo pembeni ya Mzee Mbirikolo, kisha wanainuka na kutoka.

BARABARANI MLANDIZI PWANI.
Maeneo ya Mlandizi gari inaenda kwa muda, wanakuta kizuizi, Afande anawapiga mkono “usijaribu kufanya ujinga wowote” Ykikeke anamwambia Mkwere, “kumbuka sisi hatuogopi Polisi wala nani” anaongeza Ykikeke huku Mkwere akizungusha usukani kuingia kando ya barabara na kusimamisha gari, wanabaki kimya garini, Afande anafika dirishani, “habari zenu” anasalimia Afande, “salama afande” wanaitikia wote kwa pamoja, “naomba leseni yako” Afande anamwambia Mkwere, Mkwere anatoa leseni na kumpatia Afande, Afande anaiangalia kwa muda kisha anairudisha kwa Mkwere “safari njema” anasema Afande huku akiondoka na kuelekea lilipo gari lingine mbele yao, Mkwere anafungua mlango, Ykikeke anashtuka na kumkwida Mkwere kabla hajatoka, huku Adamuu naye akiinuka kwa haraka na kuufunga mlango kisha anamuweka roba ya nguvu,“tutakulipua mbele ya hawa Polisi..usicheze na sisi bata wewe” anatamka Adamuu huku akihema juu juu kwa jazba, “unataka kuonana tena na binti yako hutaki?” anauliza Ykikeke, zinapita sekunde kadhaa, “nataka” anatamka Mkwere kwa taabu, Adamuu anamuachia, Mkwere huku anahema juujuu kama Mtu aliyezama majini na kuibuka, “ondoa gari” anaamuru Ykikeke, Mkwere anaweka gia na kuondoa gari huku akigugumia maumivu shingoni, safari inaendelea.

BARABARANI SAME KILIMANJARO-MCHANA.
Gari lipo kwenye mwendo, Ykikeke anaangalia saa mkononi, “muda wa kula” anasema Ykikeke, “thanx God” anasema Adamuu huku akishusha pumzi nzito, “naunga mkono hoja” anasema Idd Riss, “paki hapo pembeni” Ykikeke anamuamuru Mkwere, Gari inaingia pembeni na kusimama kando ya pori lenye miti na vichaka vya kutosha, “fungua buti” Ykikeke anamwambia Mkwere huku wakiteremka garini, “kumbuka wote tuna silaha” anaongeza Ykikeke, Idd Riss anaenda kwenye buti na kutoa mfuko huku Adamuu na Ykikeke wakienda pembeni na kujisaidia, Idd Riss anatoa Hot pot nne zenye chakula na kuziweka juu ya boneti, huku akimpatia kila mmoja kijiko “mimi sitokula” anasema Mkwere kabla ya kupokea kijiko kutoka kwa Idd Riss, “nahitaji tu kujisaidia” anasema Mkwere, wanarudi Ykikeke na Adamuu, “jamaa anataka kujisaidia” Idd Riss anawaambia Ykikeke na Adamuu, “Adamuu msindikize” Ykikeke anamwambia Adamuu, “twende” Adamuu anamwambia Mkwere, wanaelekea pembeni kilipo kichaka “thubutu kufanya ujinga wowote nikumalizie huku huku porini” Adamuu anamwambia Mkwere huku akimuonyesha bastola iliyopo kiunoni kwake, wanaenda mita kadhaa “hapo panatosha” Adamuu anamwambia Mkwere “ni haja kubwa” anasema Mkwere, Adamuu anabaki kimya kwa muda akimuangalia Mkwere “tunataniana” Adamuu amauuliza Mkwere “Nikutanie ili iweje kaka” Mkwere anasema, wanabaki kimya kwa muda, “ok..sogea pale” anasema Adamuu, “na ole wako” anasema Adamuu kwa sauti iliyojaa msisitizo, Mkwere anasogea kichakani na kuanza kufungua mkanda huku Adamuu akimkazia macho, Mkwere anainua macho na kushtuka kumuona Adamuu akimkodolea macho “sidhani kama utaniangalia ninavyojisaidia?” Mkwere anamuuliza Adamuu, Adamuu anageuka pembeni huku akitoa pakiti ya sigara, Mkwere anachuchumaa na kubaki ametulia, Adamu anatoa kiberiti na kuiwasha sigara iliyo mdomoni mwake, Mkwere anabaki ametulia kwa sekunde kadhaa, kisha pole pole anaanza kutambaa kuelekea ulipo mfereji.
 
SEHEMU YA NNE.

Adamuu amesimama akivuta sigara, Mkwere anatambaa hadi pale mferejini, anamuona Binti mdogo wa miaka 14 hivi, ameinama akiteka maji ya mferejini, Mkwere anainuka na pole pole na kujongea alipo yule binti huku akiwa ameinama, Adamuu anaendelea kupiga pafu kadhaa kisha anashtuka na kugeuka, anasogea pale kichakani hamuoni Mkwere, “shit” anasema Adamuu kwa mshtuko, Mkwere anafika kwa yule binti, Binti anashtuka na kuinuka, “hujambo?” Mkwere anamsalimia Binti, “sijambo shikamoo” Binti anaitikia na kusalimia huku akionekana na hali ya uoga, “nenda kamwaambie Baba au Mama yako apige simu polisi” anasema Mkwere huku anahema juu juu, “ile gari ya silva pale juu barabarani ni ya Majambazi” anaongeza Mkwere huku akigeuka geuka kuangalia nyuma, “hata mimi hapa wameniteka..wamekuja hapa mtaani kwenu kufanya ujambazi” anaongeza Mkwere, Binti anachukua ndoo yake na kuondoka kwa haraka, Adamuu anaenda mita kadhaa, anamuona Mkwere, anamkimbilia, anamfikia na kumkwida huku akimtandika ngumi na mateke, “unataka kufanya nini fala wewe” anasema Adamuu huku akiendelea kumpiga ngumi mfululizo na mateke, “twende” anasema Adamuu huku akimkokota Mkwere.

Binti anafika alipo Jole, bwana, 40, akiwa anatengeneza baiskeli,“mjomba..kuna mtu kaja pale mferejini kasema tupige simu polisi kuna gari ya Majambazi” anasema Binti huku anahema kwa uoga Mjomba anashtuka “Majambazi wamerudi tena?” anasema Jole kwa mshtuko, “wapo pale barabarani” anasema Binti, Jole na Binti wanaondoka na kuelekea kilimani, wanawaona Ykikeke, Adamuu, Idd Riss na Mkwere wakiwa pembeni ya gari, huku Adamuu amemkwida Mkwere, “tena labda haya ndio yale yaliyemuaa Kaka yangu”, Jole anasema huku anatoa simu mfukoni na kuibofya, anaiweka sikioni,“hallow.. hapo Polisi..kuna tukio hapa Same kijiweni” anasema Jole, “Yale Majambazi yamerudi tena” anaongeza Jole, “mkifika tu hapa kijiweni kwenye mnara mtaona gari ndogo ya silva imesimama” anaongeza Jole na kuitoa simu sikioni,“wanakuja” Jole anamwambia Binti huku wakibaki pale wakiwaangalia kina Mkwere.

YKikeke anasogea na kumkwida Mkwere, “kwa hiyo umeamua liwalo na liwe sio?” Ykikeke anamwambia Mkwere kwa ukali, anamuachia, “ingia kwenye gari” Ykikeke anamuamuru Mkwere huku akimfungulia mlango wa nyuma wa abiria, Mkwere anaingia na kuketi, Yikeke anaufunga mlango na kusogea walipo Adamuu na Idd Riss, “hebu mlaze” Ykikeke anamwambia Adamuu, Adamuu anaenda kwenye buti na kutoa kichupa chenye maji maji ya njano, anafungua na kumimina kwenye kitambaa, kisha anaenda kwenye gari, anafungua mlango na kukandamiza kitambaa usoni kwa Mkwere, Mkwere analegea na kujilaza kwenye kiti, Adamuu anafunga mlango na kurudi walipo Ykikeke na Idd Riss,“itabidi tumalizane kabisa na huyu ndezi..naona atatusumbua tu” anasema Ykikeke, “hata mimi nilidhani hivyo bosi” anasema Idd Riss, “Adamuu” anaita Ykikeke, “sasa hivi?” anauliza Adamuu “ndio ninachosema” anasema Ykikeke, “tungerahisisha lakini risasi itakuwa mazoea?” anasema Ykikeke “lakini bosi kwa nini tusisogee mbele kidogo kuna bwawa hapo mbele..tumuache” anasema Idd Riss,“ammalize sasa hivi tukifika huko ni kumuacha tu” anasema Ykikeke, “utaendesha” Ykikeke anamwambia Idd Riss huku akielekea garini na kuingia, Adamuu anavua saa na miwani na kuingia garini, Idd Riss anawasha gari huku Adamuu akimpiga Mkwere roba ya nguvu, Mkwere ambaye tayari anaonekana hana uwezo wa kujitetea.

Mara mbele yao inapaki defender, “shit” anatamka Ykikeke, “wanataka nini tena hawa wakuda” anasema Idd Riss kwa mshtuko, Afande Sabu anatoka garini na kuja lilipo gari la kina Ykikeke, anafika dirishani “habari zenu?” anatamka Afande, “nzuri afande” anajibu Ykikeke, “tupo kwenye ukaguzi wa kawaida” anasema Afande Sabu, “tunaomba mteremke mara moja alafu mtaendelea na safari yenu” anaongeza Afande Sabu, kimya kinatawala kwa muda, “ondoa gari” anaamuru Ykikeke, Idd Riss kwa haraka anaweka gia na kukanyaga mafuta huku akikata kona na kuelekea njia ya vumbi, Afande Sabu anarudi mbio na kuingia kwenye defenda, Difenda inaondoka mbio kuwafuata.

Wanakwenda kwa mwendo wa kilomita kadhaa, Afande Sabu anafyatua risasi kadhaa juu, mbio zinaendelea kwa muda, Afande Sabu anaanza kufyatua risasi kuelekea kwenye gari na kusababisha matundu kadhaa sehemu ya nyuma ya gari, gari ndogo inakwenda kwa kasi na kuiacha Difenda kwa mita kadhaa, inafika kwenye kona na kuingia huku vumbi kubwa likiwa limebaki kwa nyuma, Difenda inakuja kwa kasi na kupitiliza, Difenda inaenda kwa umbali fulani kisha wanasimama, “wametupoteza” anasema Afande Dule aliyepo kwenye usukani, anageuza Difenda kwa haraka huku akiangalia huku na kule, wanarudi walipotoka huku wakiangalia pande zote kwa makini, wanafika na kuioana gari ndogo ikiwa imeegeshwa pembeni jirani na nyumba moja kuu kuu, Difenda inasimama huku Afande Dule akiwa na redio call, “tunaomba msaada ova” anasema Afande Dule huku Afande Sabu anateremka akiwa amejihami na silaha na vesti ya kuzuia risasi, anashtushwa na mlio wa bunduki na risasi inayotua kwenye mlango wa difenda, “wana SMG” anatamka Afande Sabu, “wana silaha ova” anasema Afande Dule kwenye radio call huku naye anateremka na silaha yake, huku Afande Sabu akiinama na kukoki SMG yake, naye anaanza kuvurumisha risasi kuelekea zinapotoka risasi kwenye ile nyumba, majibizano yanaendelea kwa muda, kisha kunabaki kimya.

Afande Sabu ananyata na kufika lilipo gari dogo,na kumkuta Mkwere akiwa amelala hoi siti ya nyuma, mara mlio wa risasi unasikika na kumpata Afande Sabu mkononi, Afande Dule anakuja alipo Afande Sabu, anafyatua risasi kadhaa kuelekea kwenye nyumba ambayo wapo Ykikeke, Adamuu na Idd Riss ambao nao wote wana silaha, risasi moja inampata Idd Riss, anakwenda chini huku akionekana kushikilia tumbo lake sehemu ya chini kidogo ya kitovu, “shit” anasema Ykikeke huku akimuangalia Idd Riss pale chini, Ykikeke anampa Adamuu ishara, wanainuka na kutoka mbio huku wote wakiwa wamebeba begi mkono mmoja na silaha mkono mwingine.

Afande Dule huku akikazana kuongeza mzigo kwenye silaha yake na pembeni yake amelala Aande Sabu akigugumia maumivu, Afande Dule anawaona Adamuu na Ykikeke wakikimbia, anafyatua risasi kadhaa kuelekea walipo, moja inampata Adamuu mguuni na anaenda chini, Ykikeke anageuka na kuvurumisha risasi kadhaa kwa kutumia SMG yake, kisha anarudi kwa Adamuu na kumkokota mpaka nyuma ya ukuta wa nyumba iliyo jirani, milio ya risasi inatulia, Afande Dule bado yupo na redio call mdomoni, “hali ni mbaya afande Sabu yupo chini ova” anasema afande Dule, kisha anachana mkono wa shati na kufunga kwenye jeraha la Afande Sabu pale mkononi.

Upande wa pili Ykikeke naye anamsaidia Adamuu kufunga lile jeraha mguuni, unasikika mlio wa pikipiki, Ykikeke anainuka na kusogea barabarani, anaisimamisha bodaboda inasimama, Ykikeke anampiga kijana ngumi moja nzito inayotua katikati ya paji la uso, kijana anaenda chini huku Adamuu akijikongoja, Ykikeke anasogeza Pikipiki na kumsaidia Adamuu kupanda, anachukua mabegi yao na silaha, kisha anapanda na kuiondoa Pikipiki kwa kasi.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom