Simulizi:Death Of Innocent

*Sehemu ya 15*


“Prosper!”
“Naam Belinda!”
“Sitakusamahe maishani mwangu na hata kama nitakusamahe basi sitasahau siku zote!” Alisema Belinda na kuanza kutembea kwa haraka kutoka chumbani kwenda nje ya gereza.

“Belinda! Belinda! Belinda usiondoke!” Prosper aliita wakati Belinda akitoka chumbani lakini hakugeuka kuangalia nyuma alizidi kutembea kwa haraka huku akilia.
*****************

Alitoka hadi nje ambako alitembea hadi kituo cha mabasi madogo na muda mfupi baadaye daladala moja lilikuja na kusimama pembeni yake, alimbeba vizuri mtoto wake na kuingia ndani na kuchukua kiti cha nyuma kabisa, alikuwa bado na hofu ya kusababisha harufu lakini alipokumbuka kuwa alishafanyiwa operesheni na kuwa mkavu hofu hiyo ilitoweka mara moja.

Belinda aliendelea kububujiwa na machozi hadi wakati anafika mjini, watu wote ndani ya gari walimshangaa na walipomuuliza ni kwanini alilia machozi kiasi kile hakueleza chochote.

Alipomwangalia mtoto wake mzuri Alicia, aliyekuwa ameketi mikononi mwake roho yake ilimuuma zaidi, alikuwa mtoto mzuri mno kufa kwa Ukimwi!

Ilimuuma sana Belinda kujua kuwa hata mtoto wake hakuwa na maisha marefu mbele yake, lakini Alicia hakuwa na taarifa na kilichokuwa kikiendelea aliendelea kutabasamu huku akimpigapiga mama yake usoni.

Alipofika mjini Tabora aliteremka ndani ya basi, alihisi kukata tamaa ya kila kitu! Hakuona sababu ya kurudi tena Tutuo, kijijini kwao Prosper alichofikiria wakati huo ni kurudi tena Dar es Salaam kwa baba yake na kujaribu kumwomba msamaha! Lakini alipokumbuka jinsi baba yake alivyomfukuza kama mbwa roho iliingiwa wasiwasi na kujikuta akisita kuchukua hatua hiyo.

“Kwa kweli baba asingekuwa na matatizo ningerudi Dar , acha tu nirudi Tutuo!”
Baada ya kuwaza sana hatimaye mawazo yake yalimfikisha katika hatua hiyo lakini alipokumbuka kuwa nyumba aliyofikia ingekuwa tayari imekwishabomolewa na mwarabu aliyeinunua ili ajenge mashine, Belinda alikosa mahali pa kuelekea kwa sababu hakuona mahali pengine popote pa kufikia kijijini Tutuo.

“ Lakini acha tu niende, Wanyamwezi ni watu wakarimu sana, nitaomba kukaa kwa mtu yeyote au nitarudi tena kuomba kazi nyumbani kwa Mwarabu Mzee Mohamed nafikiri safari hii atakubali kwa sababu sina mimba na sinuki kama ilivyokuwa zamani!”

Belinda aliamua kurudi kijijini na alichofanya ni kwenda stendi ya basi ambako alipanda basi la kumpeleka kijijini Tutuo, njia nzima aliendelea kulia alijua maisha yake yalikuwa yamefika mwisho! Alihisi hakuwa na maisha tena mbele yake, binafsi hakujionea huruma sana aliyemtia simanzi zaidi alikuwa ni mtoto wake Alicia.

“Masikini Alicia anakufa kwa kosa lisilo lake akini kwanini hasa mtu amuue mtoto asiye na hatia? Prosper alishindwa kuvumilia shida? Nasema sitaki kumwona tena maishani mwangu!” Alisema kwa uchungu Belinda, hakujua alikuwa akiongea kwa sauti kiasi kwamba watu wote ndani ya basi waligeuka kumwangalia.
*******************

Gerezani:
Baada ya kuachwa chumbani Prosper alinyanyuka kwa unyonge na kutembea hadi chumba cha mahabusu na kwa muda mrefu aliendelea kulia na hakuona tena sababu ya kuendelea kuishi, alitamani kufa kukwepa aibu ya kuwaua mke na mtoto wake kwa Ukimwi lakini alishindwa kuelewa ni kwa njia ngani angeweza kujitoa uhai akiwa ndani ya gereza.

Alilia usiku mzima hadi asubuhi, alijuta kwa yote aliyoyafanya na alitamani sana kuonana tena na Belinda ili apate kuongea naye na kumwomba msamaha! Alijua hilo lisingewezekana hata kidogo kwani alikuwa na uhakika Belinda asingerudi tena.

“Laiti ningejua nisingejiingiza katika mchezo huo mbaya, shida za gerezani zingeniua mbona watu wengine wanaishi?”

Aliwaza Prosper huku akilia.
Prosper alikuwa na watu wengi sana wa kuwalaumu kuhusiana na suala hilo lakini watu waliopaswa kuzibeba lawama zote hizo walikuwa ni mama na dada zake kwa kitendo chao cha kumuua baba yake, bila wao kufanya hivyo Prosper aliamini asingeingia gerezani katika maisha yake!

“Ni wao ndio walilaumiwa niliingia gerezani kumwokoa mama na dada zangu, mama mwenyewe amekwishakufa na hata hao dada zangu hakuna hata mmoja anayefika hapa gerezani kunitembelea na bado nyumba na kiwanja alichoacha baba wameuza na kupotea, huu ni ukatili wa hali ya juu sana!” Aliendela kuwaza Prosper.

Baada ya siku hiyo Prosper hakuwaona tena Belinda na mtoto wake Alicia, kesi yake iliendelea katika mahakama kuu kanda ya Tabora na miezi mitatu baada ya Belinda kuondoka kesi hiyo ilifikia hukumu yake, alionekana kuwa na hatia mbele ya sheria baada ya yeye mwenyewe kukiri mauaji hayo ya baba yake mzazi mbele ya jaji Mohamed Simbila na kuhukumiwa kifo kwa kuchomwa sindano ya sumu
Mahakama nzima ilipigwa na butwaa baada ya hukumu hiyo, Prosper hakuonyesha huzuni wala kulia badala yake alitabasamu kwa furaha baada ya hukumu hiyo kutolewa.

“Una namna yoyote ya kujitetea?”
“Sitaki kujitetea Mhesimiwa Jaji, hukumu yako ni sahihi na hii ndiyo niliyoisubiri ili iniepushe na kifo cha mateso kilichopo mbele yangu!Nakushukuru sana mheshimiwa jaji na ninakupongeza sana kwa hukumu hiyo nzuri!” Alisema Prosper huku akicheka.

Bila kuchelewa maaskari walimpiga pingu mkononi na kumwondoa mahakamani, jaji aliyemkuhumu alibaki na maswali mengi sana kichwani mwake, alishafanya kazi ya kuhukumu watu kwa miaka karibu ishirini na alishahukumu watu wengi kifo lakini hakuwahi hata siku moja kumhukumu mtu kifo akicheka! Wengi walilia na kuomba kupunguziwa kifungo!

Siku iliyofuata Prosper ilitolewa amri Prosper ahamishiwe gereza la Keko jijini Dar es Salaam ambako angepambana na kifo chake! Alipakiwa ndani ya treni la abiria kutoka Mwanza kwa safari ya kwenda Dar es Salaam.

Prosper alilia lakini hakulia sababu ya hukumu ya kifo aliyopewa ila alilia kwa sababu alikuwa anapelekwa kufa bila kuonana na mke na mtoto wake kwa mara ya mwisho, alikuwa anakwenda kufa bila Belinda kufahamu ukweli juu yake! Pia alilia sababu yeye alikuwa anakwenda kufa na kuwaacha mkewe na mwanae wakiteseka kwa ugonjwa wa Ukimwi aliowaambukiza yeye.
*****************

Alicia, kijijini Tutuo:
Tayari alishazoea maisha ya nyumbani kwa mzee Mohamed, alifanya kazi kwa nguvu zake zote ili aweze kumridhisha mama mwenye nyumba, alipewa chumba kidogo ambacho alilala na mtoto wake kwa kutandika jamvi chini kila siku!

Ilikuwa ni kawaida yake siku zote kudamka mapema na kufanya kazi zote za ndani na ilipotimu sawa nne aliacha kazi hizo na kuanza kupasua kuni, baada ya kupasua kuni alianza kupika chakula cha mchana na baadaye alianza shughuli za ufuaji wa nguo za kila mtu nyumbani.

Zilikuwa ni kazi ngumu lakini Belinda alizifanya ili aweze kuishi na mtoto wake, katika miezi yote aliyokaa nyumbani kwa mwarabu Mzee Mohamed hakuwahi kumkumbuka Prosper lakini asubuhi ya siku hiyo akipasua kuni kumbukumbu za Prosper zilimsumbua kichwani, alitamani sana kumwona na aliona uamuzi aliouchukua haukuwa wa busara kwa sababu usingeweza kuubadilisha kitu chochote katika maisha yake kama ni virusi alishavipata na ni lazima yeye na mtoto wake wangekufa.

*Je, nini kitaendelea?*
 
Asante mama @Shunie
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana Shunie
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Japo tunachukulia kama hadithi tu lakini huwezi amini kuna watu wanayapitia haya kiuhalisia..Mungu atunusuru!
 
Thanks shunie lkn kama kuna kamkanganyingo fulani hivi, episode ya 12 iliishia Belinda alikuwa kafika kwao na mara babake akatokea.....nilitegemea tuanzie hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*Sehemu ya 16*


“Ninaamini hivi sasa Prosper anahitaji msaada wangu kuliko wakati mwingine wowote katika maisha yake!” Aliwaza Belinda huku akiendelea kupasua kuni.

Alimfikiria Prosper kwa muda mrefu hatimaye aliamua kuliweka shoka pembeni na kuketi chini, mawazo juu ya Prosper yaliendelea kumiminika mwake.
“Hapana nakwenda gerezani!”

Alisema Belinda na kulitupa shoka pembeni, akambeba mtoto wake mgongoni na kwa kutumia khanga yake iliyochanika alimfunga vizuri na kuondoka kuelekea ndani ambako alimkuta mke wa mzee Mohamed na kumwomba ruhusa lakini hakuruhusiwa kuondoka.

“Belinda wewe hapana ondoka iko kazi nyingi leo!”
“Hapana mama ni lazima nikamwone Prosper nikishindwa leo ni mpaka wiki ijayo!”

“Hapana!” Mke wa mzee Mohamed alikataa katakata.
“Mama nimekwishasema naondoka,nitafanya kazi nikirudi!” Belinda alisema na kunyanyuka.
“Wewe ondoka kwa nguvu eh! Pana rudi hapa!”
“Sawa mama!”
*****************

Alifika gerezani saa nne asubuhi, kitu cha kwanza alichofanya ni kuomba kuitiwa Prosper.

“Dada yangu ulikuwa wapi siku zote hizi?”
“Nilikuwa safarini!” Belinda alidanganya!”
“Karibu sana!”
“Ahsante! Prosper yupo!”

“Prosper?” Askari magereza aliuliza.
“Ndiyo mbona unauliza kwa mshangao!”
“Amesafirishwa jana kwenda gereza la Keko Dar es Salaam, alihukumiwa kifo!
Belinda alichanganyikiwa na kwa kutumia basi alirudi hadi mjini ambako alipanda basi jingine lililompeleka hadi Tutuo.

Hakukaribishwa tena nyumbani kwa mzee Mohamed na kwa sababu hakuwa tena na haja ya kufanya kazi aliomba mishahara yake na kuondoka tena hadi stesheni ya treni mjini Tabora ambako alipanda treni jioni ya siku hiyohiyo kurejea Dar es Salaam lengo lake likiwa ni kuishi kabla Prosper hajanyongwa!
*******************

Treni iliingia Dar es Salaam saa saba mchana, Belinda aliona bado muda ulimruhusu kwenda gerezani Keko kuonana na Prosper, hakutaka kabisa afe kabla hajaongea nae na kumjulisha kuwa tayari alishamsamehe yote yaliyotokea.

Kutoka stesheni ya reli ya Dar es salaam hadi gereza la Keko ilikuwa kama nusu kilometa hivi, kwa umbali huo mdogo Belinda hakuhitaji gari alitumia njia ya mkato hadi kufika gerezani.

“Dada mwenye mtoto nikusaidie nini?” Askari magereza aliyekuwa akilinda nje ya gereza alimuuliza
“Nimekuja hapa kumwona mume wangu!”
“Leo siyo siku ya kuwaona wafungwa njoo Jumamosi ama Jumapili umesikia!”

“Sawa lakini……..!” Alisema Belinda huku akimsogelea askari.
“Lakini nini? Dada hiyo ni sheria ya gereza!”
“Nilikuwa naomba kukuuliza kitu sababu sijui!”

“Kitu gani?”
Belinda alimsimulia askari huyo kila kitu juu ya Prosper na kwamba alitaka kuhakikisha kama kweli alikuwepo gerezani au la!

“Katokea gereza gani?”
“Isanga Tabora!”
“Nisubiri hapa niulizie!” Alisema askari huyo na kuingia hadi ndani ya gereza na alipotoka alikuwa na jibu la Belinda.

“Nasikitika hayupo!”
“Hayupo? Hayupo vipi wakati mimi Tabora wamenieleza amehamishiwa gereza hili!”

“Amepelekwa gereza la Segerea sababu hapa hakuna nafasi ya wafungwa kama yeye!”

“Ah! Sawa nashukuru sana kaka yangu!” Belinda alishukuru lakini hakuwa tayari kusubiri hadi jumamosi ndio aonane na Prosper alihisi kufikia siku hiyo tayari angekuwa amekwishayongwa!
“Na nitakwenda huko segerea wakinizuia nitatumia hata hii pesa kidogo niliyonayo mpaka nimwone!” Aliwaza Belinda.

Kutoka gerezani Keko hadi kituo cha mabasi cha Shule ya Uhuru ambako mabasi ya Tabata na Segerea yaliegeshwa ilimchukua dakika 30 na kutoka shule ya Uhuru sababu ya ubovu wa barabara ya Tabata ilimchukua saa nzima hivyo alifika gerezani segerea saa tisa na nusu ya jioni na kwenda moja kwa moja hadi mapokezi ambako alimkuta askari magereza wa kike.

“Shikamoo dada!” Belinda aliamkia.
“Marahaba, nikusaidie nini mdogo wangu?”

‘Dada unavyoniona hivi ninatoka Tabora, huyu ni mwanangu nimekuja hapa kumfuata mume wangu anaitwa Prosper, yeye kahamishwa kutoka gereza la Isanga huko Tabora ni mfungwa aliyehukumiwa kifo, nataka kumwona kabla ya kifo chake.
“Kwani vipi mbona unanieleza vitu vingi kwa wakati mmoja?” Askari magereza aliuliza.

“Nisaidie dada, nisaidie mimi mwanamke mwenzio!” Aliendelea kusema Belinda na baadaye kumsimulia askari huyo kila kitu kilichotokea katika maisha yake na Prosper, askari alishindwa kujizuia na kujikuta akichukua kitambaa chake na kujifuta machozi usoni mwake.

“Ni sawa nimehuzunishwa sana lakini sina jinsi ya kukusaidia kwa sababu si rahisi kukuingiza gerezani siku ya leo mdogo wangu,nenda uje Jumapili!”
“Dada tafadhali nisaidie!”

“Haiwezekani labda nimwite tu umwone kwa mbali lakini siwezi kukuruhusu uingie ndani ya gereza, kwani unaitwa nani?”
“Naitwa Belinda!”
“Belinda nani?”
“Belinda Thomson Komba!”
“Thomson Komba yule mfanyabiashara?”
“Ndiyo!”
“Sawa wewe mbona una hali hiyo?”
“Maisha tu dada yangu!” Belinda alijibu huku akilia.

Alisimama wima mbele ya 
askari magereza wa kike, 
mtoto wake Alicia akiwa mgongoni, mtoto huyo hakuelewa kitu chochote kilichoendelea aliendelea kulala mgongoni kwa mamaye.

Baada ya kujieleza kwa muda mrefu akimbembeleza askari magereza amwitie Prosper ili aonane naye kabla ya kifo chake hatimaye askari alilainika na kuanza kutembea kuondoka eneo hilo na kuingia ndani ya gereza.

Hakurudi mpaka dakika kama kumi na tano hivi baadaye, askari huyo aliporejea mbele yake akiwepo Prosper! Tayari alishavalishwa nguo za wafungwa na alionekana kukonda sana.

Prosper alionekana kutoyaamini macho yake alipomwona Belinda! Alitaka kukimbia kwenda upande wa pili kumkumbatia lakini alizuiliwa na nondo nzito zilizotenganisha ndani na nje ya gereza! Ziliwekwa maalum kuwazuia wafungwa kutoroka.

“Afande nifungulie basi nisalimiane na mke wangu kwa karibu zaidi!”
“Haiwezekani hata kidogo Prosper kwanza si ruhusa leo wafungwa kuonwa nimewafanyia upendeleo vinginevyo ningeweza kukataa kwanza haraka kabla mkuu wa gereza hajaja mnasikia?” Askari magereza aliongea kwa msisitizo.

Hakuna aliyemjibu kitu afande bali Prosper alisogea karibu na uzio wa nondo, Belinda nae alifanya vivyo hivyo mpaka wakakaribiana kabisa na kupenyeza midomo yao katikati ya nondo na kuanza kupigana mabusu mdomoni mbele ya askari bila kuogopa wala kuona aibu.

Ghafla kabla hawajasema lolote hata kusalimiana wote walianza kudondosha machozi na baadaye kulia kwa sauti, walionekana kuwa na uchungu mkubwa mioyoni mwao! Waliangaliana na kukumbuka mambo mengi yaliyotokea katika maisha yao tangu walipokutana mara ya kwanza shuleni, yalikuwa ni mateso makubwa mno waliyoyapitia na bado walikuwa wakiendelea kuteseka.

Waliendelea kulia kwa kwikwi kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kumwambia mwenzake chochote hadi Prosper alipoanza kuvutwa na askari magereza kurudishwa gerezani!

Machozi yalimbubujika Belinda kwa wingi, alimwonea huruma sana Prosper na kabla hajaingizwa ndani aligeuka nyuma na kuwaanglia Belinda na mtoto wake, roho ilimuuma sana na alitamani mambo yangekuwa tofauti na ilivyokuwa, ndani ya nafsi yake Prosper alijilaumu kwa uamuzi wake wa kuyakiri mauaji ambayo hakuyatenda jambo ambalo hata Belinda hakulifahamu.

Mtu aliyekiri mauaji hayo ili amuokoe kutoka gerezani,yaani mama yake tayari alikuwa ni marehemu na dada zake nao walishamtelekeza gerezani baada ya kutoka gerezani na yeye kuingia!

“Nakupenda Belinda, ahsante sana kwa kuja tena, nisamehe kwa kila kosa nililoliyafanya najua sina maisha marefu duniani, kwa sababu watu wenye virusi hufa upesi sana gerezani isitoshe nimeshahukumiwa kifo tayari, namuonea huruma sana mwanangu kwa sababu hataishi kuja kuniona mimi baba yake!

Tafadhali Belinda mtunze vizuri mtoto wetu Alicia lakini usije kumwambia niliua!” Alisema Prosper huku askari magereza akisubiri amalizie.

*Je, nini kitaendelea?*
 
[emoji24][emoji24][emoji24]Loh,,hii simulizi sio ya kusoma sk km ya leo tena muda huu.[emoji22]
Asante Shangazi Shunie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inasikitisha mnooh....

Asante dada Shunie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…