boga la kiangazi
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 504
- 683
dah mzuka mzukani
asante shunie
asante shunie
Thanks Shunie*Sehemu ya 06.*
Prosper alipolisikia jina la Mfugambwa alielewa ni nani aliyekuwa amekaa naye mahabusu! Halikuwa jina geni kabisa kwake masikioni kwake, alishalisikia jina hilo mara nyingi tu tangu akiwa mtoto mdogo, Mfugambwa alikuwa jambazi aliyejulikana sana mikoa ya Tabora,Mwanza, Shinyanga na Kigoma ni yeye aliyeteka mabasi na treni za abiria na kuwanyanganya mali zao!
Alidaiwa kuwa na madawa yaliyomsaidia kushinda kesi aliyoyapata kutoka nchini Zaire, alishakamatwa mara nyingi kwa makosa hayo lakini alishinda kesi zote kiajabu ajabu na kuwa huru.
Sekunde chache baadaye Prosper alisikia jina lake likitajwa na kutembea hadi mlangoni ambako alifungwa pingu mikononi na mlango wa mahabusu ukafungwa.
“Tangulieni nje nyie wauaji”
“Kwani kuua ni kitu cha ajabu bwana, usitunyanyase!” Savimbi alimjibu askari bila woga kwa jibu hilo alipokea kipigo cha kitako cha bunduki na kupasuka usoni,damu zikamtoka lakini bado hakuacha kutoa matusi.
Walipandishwa ndani ya gari la polisi na ulinzi mkali wa msafara wa magari kama matano hivi uliongoza safari kwenda mahakamani.
Mahakamani waliteremshwa na kuanza kusukumwa kuelekezwa katika mahabusu iliyokuwepo nje ya mahakama, Prosper alipotupa macho pembeni alimwona mama yake akilia, machozi huku akiwa ameshikiliwa na dada zake.
Alionekana akijaribu kujitoa mikononi mwao ili asogee mbele lakini alishindwa, mdomo wake ulifunikwa na viganja vya binti zake ili maneno aliyokuwa akiyatoa yasisikike, lakini bado Prospe alisikia kilichosemwa na mama yake!
“Niachieni! Niende kwa mwanangu nikawaeleze polisi ukweli ili wamwachie”
Prosper aliposikia maneno hayo alimkonyeza mama yake lakini bado aliendelea kupiga kelele, jambo lililofanya dada zake waamue kumwondoa mahakamani haraka iwezekanavyo.
Prosper na Savimbi walisomewa mashtaka yao tofauti na kurudishwa mahabusu, hawakutakiwa kujibu kitu chochote sababu kesi zao zilikuwa za mauaji.
****************
Walipotoka mahakamani hawakurudishwa tena polisi bali walipelekwa moja kwa moja gereza la Isanga ambako waliwekwa mahabusu, huo ndio ukawa mwanzo wa Prosper kuishi gerezani na kila mwezi alipelekwa mahakamani ambako kesi yake ilitajwa tu!
Kila siku iliyokwenda kwa Mungu Prosper alikuwa na mawazo mengi juu ya maisha yake, lakini mawazo yaliyomsumbua zaidi ni juu ya msichana Belinda, alikaa na Belinda kwa muda mfupi shuleni na kumzoea na ni wazi alimpenda, kila alipoikumbuka siku waliyoachana shuleni baada ya Belinda kumpa nauli za kumpeleka likizo, roho ilimuuma sana Prosper!
Alikuwa na mapenzi makubwa sana kwa msichana huyo na aliamini hata yeye alimpenda na alimkubali pamoja na umasiki aliokuwa nao!
Alishindwa kuelewa Belinda angepata vipi taarifa juu ya matatizo yaliyomkuta, kumbukumbu juu ya Belinda zilimtia simanzi zaidi.
********************
Belinda Dar es Salaam, Julai:
Siku chache kabla ya shule kufunguliwa kwa pesa aliyopewa na baba yake Belinda alimnunulia Prosper zawadi mbalimbali zikiwemo nguo, viatu na hata vitabu vizuri kwa ajili ya masomo yao.
“Prosper atafurahi sana kupokea zawadi hizi na ndio ataamini kuwa kweli ninampenda!” Aliwaza Belinda wakati akipakia mabegi yake katika gari tayari kwa kuondoka kwenda shule.
Belinda alikuwa na hamu kubwa ya kukutana na Prosper na aliona gari halifiki Moshi, alipofika shuleni hakumkuta na alikaa kwa mwezi mzima shule bila kumwona alianza kupata wasiwasi mkubwa moyoni mwake, alihisi pengine alikuwa amekosa pesa ya ada!
Aliamua kumwandikia barua haraka na kumwomba aje shule na kama tatizo lilikuwa ada basi yeye angemlipia.
Kwa miezi miwili mfululizo haikujibiwa akaamua kuandika tena barua nyingine, lakini nayo pia haikupata majibu, Belinda akazidi kuchanganyikiwa hakuelewa ni kitu gani kilimpata Prosper!
Maisha ya shuleni yalikuwa magumu sana bila Prosper ! Kila siku alilia akiomba Prosper aje tena shule waendelee na maisha yao lakini haikuwa hivyo kwani hadi mwisho wa muhula Prosper alikuwa bado hajaripoti shuleni.
****************
Miaka mitatu baadaye:
Belinda alisoma kwa mateso bila kumwona Prosper tena, roho yake ilimuuma kila siku na mpaka anamaliza kidato cha sita alikuwa ni mtu wa kumlilia Prosper tu! Wanafunzi wenzake walimcheka, alipomaliza kidato cha sita alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya sheria, mawazo yake yalikuwab bado kwa Prosper!
Likizo yake ya kwanza aliamua kusafiri bila kuwataarifu wazazi wake kwenda Tabora, Belinda alidandia treni lililompeleka hadi Tabora mjini ambako alipanda tena basi la Sabena lililokwenda hadi Mbeya, basi hilo lilimshusha kijijini kwao na Prosper Tutuo kilometa kama thelathini kutoka Tabora mjini.
Aliingia Tutuo saa saba mchana na kuulizia nyumbani kwa akina Prosper akaonyeshwa, kila mtu kijijini alimshangaa kwa mavazi aliyovaa!
Alishangazwa na hali aliyoikuta nyumbani kwao na Prosper ilikuwa ni nyumba ndogo mno iliyokandikwa kwa udongo na ilianguka upande mmoja.
Alipobisha hodi alipokelewa na mama mmoja aliyevaa nguo zilizochanika na alionekana kuwa mgonjwa alikohoa kila baada ya kuongea sentensi moja! Mama huyo alifanana sana na Prosper.
“Karibu binti!” Alisema mama huyo na kumpokea Belinda begi lake na mmoja wa wasichana alilipeleka ndani, akavuta kigoda kilichokuwa karibu na kumpa Belinda akikalie, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Belinda aliyezaliwa katika familia ya kitajiri kuwa katika familia ya aina ile na alielewa ni kwanini Prosper aliishi maisha duni shuleni.
Baada ya salamu Belinda hakusita kueleza sababu ya safari yake! Wasichana wawili waliovaa magauni yaliyochakaa walikaa pembeni ya mwanamke huyo wakisikiliza.
“Mama mimi naitwa Belinda!”
“Wewe ndiye Belinda? Uliyeandika barua hapa miaka miwili na nusu iliyopita?” Uliyekuwa ukisoma na prosper Moshi?” Angelina mama yake Prosper alilipokea jina la Belinda kwa mshangao.
“Ndiyo mama na madhumuni ya safari yangu ni kujua aliko Prosper kwa sasa, sababu ni miaka miwili na nusu sijamwona! Roho inaniuma sana kumpoteza kwani ninampenda!”
Badala ya kujibu ombi la Belinda mama yake Prosper aliangua kilio na hata wasichana waliokaa karibu yake nao walianza kulia machozi.
Belinda alishindwa kujizuia na kujikuta nae akilia ingawa hakujua sababu ya wao kulia ilikuwa ni ipi!
“Niambieni basi ili nifahamu Prosper yupo wapi hasa?”
“Yupo gerezani!”
“Alifanya nini Prosper?”
“Alimuua baba yake!” Mama yake Prosper alishindwa kuueleza ukweli!
Belinda alianguka chini na kuanza kugalagala akilia kwa uchungu walijaribu kumbembeleza lakini hakusikia, alipotulia swali lake lilikuwa moja tu!
“Ni kwanini alimuua baba yake masikini Prosper?”
“Unaniona mimi nilivyo mwanangu?”
“Ndiyo!”
“Sikuzaliwa hivi unavyoniona yote hii ni kazi ya baba yake prosper, alinitesa sana kwa kunipiga kila siku na kunitoa viungo vyangu kwa kisu, Prosper alimuua baba yake kwa bahati mbaya akijaribu kunisidia mimi!” Alisema mama huku pia akilia machozi.
“Nahitaji kumwona Prosper mama hata huko gerezani mnipeleke!” Alisema Belinda.
“Prosper yupo gereza la Isanga lakini siku ya kumwona ni Jumapili pekee!”
Je, nini kitaendelea?
Thank madame shunie. Hebu tupiamo vipande viwili viwili kwa siku basi Kama uwezekano upo.*Sehemu ya 06.*

Be blessed...Cc the_legend Norshad bobefu zoefu Pablo PAKAYA Ibney blackstarline Bryece Tater, Bigjahman marybaby, ram, kisukari, Madame S, carbamazepine, Astelia, culture gal , Prisoner of hope, kuku mweus, moneytalk, Tumosa, Mine eyes, swahiba92, ludist, Toyota escudo, Clkey, macson3, Thad, boga la kiangazi, macson3, LEGE, Smart911, Richard @irakunda, skfull, Krizy Beat, hearly nipo2 MWINDAJI HARAMU kakhulu Katavi Norami mbududa iron2012 popie Bughy Harry Kinondoni Sweetheart SUPER EMILY
Shunie, huyu mtunzi wa hii story, hakika yupo vizuri sana. Honest nimependa jinsi anavyosuka matukio(visa) katika uandishi wake.....*Sehemu ya 06.*