Sehemu ya 105
Nikajikuta namwonea huruma tena mama, nafsi yangu ikajilaumu kwa kumsimanga mzazi wangu.
Sikutakiwa kufanya hivyo. Hapakuwa na tija ya kuendeleza lawama kwa mama hasa ukizingatia mimi mwenyewe nilibariki mchakato wa kutafutiwa mke kutoka kijijini kwetu.
Kama ni makosa tuliyafanya sote. Kimsingi mimi na wazazi wangu, kwa pamoja tulipuyanga katika fikra za kutafutiana mke wa kuoa.
Kwa dunia ya leo jambo la kuoa ama kuolewa hubakia kwa mtu binafsi, vinginevyo ni kuingizana lawamani. “Basi mama usijilaumu, hayo yamekwishapita.”
“Hili kosa litaendelea kunitafuna siku zote maishani, kwa kweli tulikosea sana kukuchagulia mwanamke mjinga wa kiwango hicho.”mama alilalama.
“Kuna jambo nataka nikuombe mama,”nilimwambia, nikamwondoa kwenye mada zile za mke wangu. “Jambo gani?”
“Nahitaji uje Dar es salam, ubakie na mji wangu maana kwa hali ya uchumi inayonikabili itabidi tatu arudi kwao.” “Hilo liko ndani ya uwezo wangu, unajingine?” “Ni hilo tu, hakuna jingine.” Tulizungumza mambo mengi kisha tukaagana.
Nilichofanya baada ya kuagana na mama ni kurejea nyumbani kwa ajili ya kuoga na kubadili nguo kabla ya kurudi tena hospitali kumuguuza mtoto.
Nilipofika nyumbani, nilimkuta dada wa kazi, Tatu, akiendelea na majukumu yake ya kawaida ya nyumbani. Nilimwita na kuongea naye: “Kwanza Tatu nakushukuru kwa wema wote ambao unaotenda hapa nyumbani...”nilisema nikaendelea.
“Pili nasikitika kukwambia, itabidi tuvunje mkataba wa kazi kuanzia muda huu.” “Kwa nini baba, nitakwenda wapi mimi?” Tatu alihamaki.
“Usijali Tatum, nitakulipa stahiki zako zote.” “Kuna jambo nimekosea?” “Hakuna, Ila nina matatizo mengi sana Tatu, ukiendelea kufanya kazi hapa, itafikia hatua nitashindwa kukulipa mshahara wako.”
“Kivipi baba?” Nilimuhadithia kwa kifupi. Tatu akaridhika kwa shingo upande. Nikamlipa stahiki zake zote, kisha akakusanya kila kilicho chake na kuondoka. Wakati Tatu anaondoka, kwa kweli nuilijisikia vibaya, Tatu