SEHEMU YA 99
Nilipoingia ndani ya baa ile wala haikupita muda mrefu, nikampta George.
Baada ya salamu na stori za hapa na pale nikamweleza shida yangu. “Kwa hiyo gari lenyewe liko wapi?” akaniuliza. “Lipo nyuma hapo nimekuja nalo.” “Twende tukalione.” Tukaongozana hadi nje.
Lahaula!! pale nilipokuwa nimepaki, gari halikuwepo! “Liko wapi gari!” nilimaka. George akabaki akinishangaa. NILIHISI akili inanizunguka kwa kasi sana, kwa muda mfupi, nikatambua gari langu lilikuwa limeibwa.
Bila kutaraji nilijikuta naketi chini kitako, nikanyoosha miguu kisha nikaangua kilio kama mtoto mdogo. Ndani ya nusu dakika watu walifurika kama siafu, wakanizunguka.
Goerge akawa na kazi moja tu. Kuwaelezea kisanga kilichonikuta. “Amekutwa na nini?” watu waliuliza. “Ameibiwa gari lake.” “Wapi?” “Hapahapa.” “Aina gani?”
“Ni Land Rover Discovery 3 la rangi nyeusi” “Hilo gari niliona wakati limepaki hapa, lakini muda mfupi badaye nikaona linatoka, sikuona aliyekuwa anaendesha, na pia sikujua kama ndio linaibwa.”
Mtu mmoja alisema. “Itabidi tukatoe taarifa polisi.”George alinishauri. Nilisimama wima, nilikuwa nimetapakaa vumbi, na kwa kweli nilikuwa nimeghafirika vibaya sana.
Tukaelekea kituo cha polisi cha mabatini na kufungua RB. Kama mjuavyo taratibu za kipolisi wa nchi yetu, baada ya kufungua jarida la kesi, nikaambiwa nirudi siku inayofuatia ili nikutane na mpepelezi ambaye atakabidhiwa shauri langu.
Tukio lile lilichukuliwa kawaida tu askari polisi, hakuna aliyeonesha kustushwa, ilikuwa ni kama kuibiwa kuku tu mtaani. Nilirejea nyumbani nikiwa nimezodoka, mwili na nafsi.
Nilikuwa napitia mkandamizo mkubqwa sana maishani. Niliwasili nyumbani kwangu na kuingia ndani, nyumba niliiona ilikuwa kubwa mno, halafu ilikuwa impooza. Tofauti na siku nyingine, siku hiyo niliona upweke umezidi zaidi.
Zadi ya mtoto wangu Mwanda na dada wa kazi, hapakuwa na mtu mwingine aliyekuwa akiishi nyumbani kwangu. Kiu ya faraja ikanizidi, kwa masaa mchache nilikuwa nimepitia majaribu makubwa. Maisha yangu yalikuwa yamevurugika kwa kasi sana.