Simulizi : Beyond Love (Zaidi Ya Mapenzi)

SEHEMU YA 20 YA 50

Anavuta midomo yake...

Ananiambia mimi ni mwanamke mbaya...

Mimi mbaya?...

Nakimbilia chini ya daraja, nalia...

Pamela

“No! Haiwezekani Tom kwanini unanitesa kiasi hiki Tom? Mimi ni mwanamke mbaya kiasi hicho? Nimelala hospitali kwa miaka mitano kwa sababu ya kukuokoa uhai wa baba yako lakini haukujali yote hayo unaniletea mwanamke anitusi. Tom! Kwanini mimi?” Pale pale Mariam alianza kulia baada ya kukumbuka picha nzima ya tukio lote lilivyokuwa.

“Pole sana binti haya ndiyo maisha!”

“Lakini inaniuma sana!”

“Najua lakini usijali, Mungu atakupa mwanaume mwingine!”

“Dada, si kama Tom wangu niliyempenda na kujitoa kwake!”

“Jitahidi tu!”

“Siwezi, siwezi nimekaa miaka yote hiyo nikimsubiri yeye, sikujua alipoelekea sasa amerudi namhitaji!”

“Mariam!”

“Bee!”

“Wewe hivi sasa ni mgonjwa unahitaji kutulia na kufikiria afya yako kwanza!”

“Najua, lakini inaniuma sana!”

“Pole sana!”

“Ahsante!” Muda huo huo Pamela akaingia akiwa na maua mkononi mwake.

“Mariam umezinduka?” Pamela aliuliza kwa mshangao.

“Ndiyo namshukuru Mungu!”

“Pole, unaendeleaje sasa?”

“Nasikia vizuri!”

“Utapona usijali!”

Walizungumza mambo mengi na Mariam kuhusu tukio zima lilivyokuwa na jinsi wanafunzi wanavyomchukulia. Pamela alitumia muda mwingi sana kumshauri na kumfanya ajisikie kawaida. Ilikuwa kazi ngumu lakini aliimudu ipasavyo.

Wiki moja baadaye ikiwa ni baada ya Mariam kupata Ushauri Nasaha kwa madaktari hali yake ilirejea vizuri na alikuwa tayari kuishi bila Tom. Akarejea chuoni na kuendelea na masomo kama kawaida.

***

Mapenzi ya Tom na Juliana yalipamba moto huku mipango ya ndoa ikiwa katika hatua za mwisho kabisa. Tayari ndoa yao ilishaandikishwa Kanisani na ilitarajiwa kufungwa wiki moja baadaye. Tom akapata safari ya ghafla kikazi ya kwenda Arusha. Alishindwa ni jinsi gani angemweleza Juliana akamwelewa juu ya safari hiyo lakini ilikuwa ni lazima amweleze.

Alichokifanya ni kuwahi nyumbani kisha akaoga pamoja na mpenzi wake baadaye wakaungana pamoja mezani kwa chakula cha usiku. Tom aliona hiyo ndiyo ilikuwa nafasi pekee ya kumweleza mchumba wake juu ya safari iliyokuwa mbele yake. Hata hivyo alisita.

“Darling inaonekana kuna kitu kinakutatiza leo!”

“Ahaaa, hapana usijali mpenzi nipo sawa tu!”

“Nakujua vizuri sana mpenzi wangu si kawaida yako kuwa hivyo!”

“Ni kweli mpenzi lakini nafikiria ni namna gani utakavypokea ujumbe ninaotaka kukueleza!”

“Ni ujumbe gani, hata kama ni mbaya nieleze tu!”

“Nimepata safari ya ghafla ya kwenda Arusha kesho mchana!”

“Kuna nini tena?”

“Akina Jamali wameniita, kuna tatizo kidogo kule kwenye ofisi yangu ya kule sina budi kwenda ili nikalitatue, hata hivyo kesho kutwa tu nitakuwa hapa!”

“Mh! Darling nitabaki na nani? Kumbuka zimebaki siku chache tu kabla ya ndoa yetu!”

“Sasa?”

“Siyo vizuri kusafiri!”

“Hizo ni imani tu, ondoa shaka mpenzi wangu wewe umeshakuwa wangu tayari!”

“Sawa, lakini usizidishe kesho kutwa!”

“Usijali”

Siku iliyofuata Tom alijiandaa kwa safari ya kwenda Arusha na baadaye akiwa safarini kuelekea Uwanja wa Ndege akapigiwa simu na kufahamishwa kwamba tatizo lilishatatuliwa, kwa maana hiyo hakuhitajika tena kwenda huko. Tom alifurahi lakini aliamua kumshtukiza mkewe.

Akaondoka na kwenda kwa marafiki zake Msasani, alikaa huko mpaka saa tano za usiku ndipo aliporejea nyumbani. Baada ya mlinzi kumfungulia aliegesha gari mahali pazuri kisha akafungua mlango mkubwa na kwenda moja kwa moja chumbani kwake. Macho yake hayakutaka kumeza yalichokiona mbele yake.

Juliana alikuwa na mwanaume kitandani, tena rafiki mkubwa wa Tom aliyeitwa Joseph. Tom aliyatoa macho bila kuamini alichokiona, akafikiria siku ya ndoa yake, akafikiria jinsi alivyoalika wageni wengi, akawaza juu ya gharama alizozitumia kuandaa sherehe hiyo, akachanganyikiwa.

“Juliana...Joseph, mnanifanyia hivi?” Tom alisema maneno hayo akitetemeka. Ghafla akaanguka chini kama mzigo, puuu!

Picha ya Mariam ikamjia kichwani mwake. Akapoteza fahamu.





Kilikuwa chumba kizuri kuliko kawaida, dari lilikuwa limepigwa rangi nyeupe, chini kukiwa na zulia la manyoya laini lenye rangi nyeupe, ukuta ulikuwa umepigwa rangi nyeupe, mashuka nayo yalikuwa meupe kabisa huku feni iliyokuwa juu ikisambaza hewa nzuri chumbani mle ikiwa nyeupe!

Kila kitu kilikuwa cheupe! Macho yake yalikuwa yakizunguka kila kona ndani ya chumba hicho bila kujua alikuwa mahali gani, baadaye akataka kuamka, lakini akashindwa! Alishindwa kwasababu alihisi maumivu katika mkono wake wa kuume, ni hapo alipogundua kwamba mkono wake ulikuwa umetobolewa na dawa iliyokuwa ikitokea kwenye drip ilikuwa ikiingia katika mishipa yake ya damu!

Huyu ni Tom au Papaa Bill kama alivyojulikana na wengi, hapo akili yake ikafanya kazi ipasavyo. Akagundua kwamba alikuwa hospitalini! Anaumwa nini? Ni swali ambalo alijiuliza bila kupata jibu sahihi. Baadaye alipogeuza uso wake akamuona Muuguzi akiwa amesimama mbele yake. Akatabasamu.

“Pole sana kaka!”

“Ahsante sana!”

“Unajisikiaje sasa?”

“Vizuri, kuna nini?”

“Unaumwa!”

“Na nini?”

“Huwezi kukumbuka, ulipoteza fahamu!”

“Hapa ni hospitali gani?”

“Ocean Road!”

“Umesema Ocean Road?”

“Ndiyo!”

“Nani alinileta?”

“Juliana!”

“Nani?”

“Juliana!”

“Umesema Juliana?”

“Ndiyo!”

Hapo picha nzima ikamjia, akakumbuka tukio zima la fumanizi kati ya Juliana na Joseph, moyo wake ulisononeka sana. Machozi yakaanza kutiririka machoni mwake kama maji yatiririkavyo katika kijito kilichopo mlimani. Moyo wake ulipata majeraha makubwa sana, hakuwa tayari kupata maumivu makali kiasi kile, akamchukia sana Juliana.

“Kwani vipi kaka?”

“Dada dunia hii...dunia dada!”

“Imefanya nini? Kwanza ni nini kilitokea?”

“Dada nimeamini unaweza kuwa na fedha nyingi sana lakini ukakosa mapenzi ya dhati kutoka kwa mtu mwenye penzi la dhati!”

“Unamaanisha nini kaka yangu?”

“Dada ninavyokuambia wiki ijayo nilitakiwa kufunga ndoa na mpenzi wangu wa moyo Juliana, lakini alichonifanyia siwezi kusahau katika maisha yangu yote!”

“Amefanya nini?”

“Si ulisema Juliana ndiye aliyenileta hapa?”

“Ndiyo!”

“Basi huyo mwanamke ndiye ambaye nilikuwa natarajia kufunga naye ndoa wiki ijayo, lakini nimemfumania na mwanaume mwingine, mbaya zaidi ni rafiki yangu wa karibu ambaye ninamsaidia vitu vingi ikiwemo pesa!”

“Pole sana Mungu atakusaidia!”

“Nashukuru sana dada yangu! Hivi, nilizimia kwa muda mrefu sana?”

“Siyo sana, uliletwa jana usiku na sasa ni saa saba na nusu mchana!”

“Yaani nimepoteza fahamu kwa masaa yote hayo?”

“Ndiyo, lakini usijali hali yako sasa inaendelea vizuri na utapata nafuu, usijali!”

“Nashukuru sana!”

Yule Muuguzi akaondoka na kumuacha Tom akiwa amelala peke yake kitandani, akili yake ikiwachambua wanawake wawili; Juliana na Mariam! Moyo wake ulikuwa unamuuma sana kwa makosa aliyomfanyia mpenzi wake wa zamani Mariam, hakuona kama alistahili kufanyiwa yale. Alishanza kuamini kwamba laana ya Mariam ndiyo iliyokuwa ikiusambaratisha uhusiano wake na Juliana.

Ilikuwa lazima atumie akili nyingi sana, ndivyo alivyofanya. Hakutakiwa kuwa na papara katika hali ngumu aliyokuwa nayo, alipaswa kuwa makini, mwenye mawazo endelevu katika matatizo aliyokuwa nayo. Busara zake zilikuwa zinahitajika sana kwa wakati.
 
Simulizi Zinazorushwa na BURE SERIES Msimu wa kwanza

1. Simulizi: Kurudi Kwa Moza

Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Kurudi Kwa Moza

2. Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad
Bonyeza hapa chini kusoma
Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

3.Simulizi: Nini maana ya mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi: Nini maana ya mapenzi

4. Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi
Bonyeza hapa chini kusoma
Simulizi : Nguvu Ya Mapenzi

5. Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

6. RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Sauti Yake Masikioni Mwangu

7. NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)
Bonyeza hapa chini kusoma
NDOA ILIVYOTETERESHA IMANI YANGU (Kisa Cha Kweli)

8. RIWAYA: Mume Gaidi
Bonyeza hapa chini kusoma
RIWAYA: Mume Gaidi

9. STORY: Sitaki Tena

Bonyeza hapa chini kusoma
STORY: Sitaki Tena

10. Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)

Bonyeza hapa chini kusoma
Nilivunja Ndoa Zangu 3 Kulipiza Kisasi (Kisa Cha Kweli)
 
SEHEMU YA 21 YA 50

“Ndiyo...lazima niwe makini sana hapa, nikicheza hapa naweza kupoteza muelekeo wa maisha yangu! Napaswa kuwa mjanja huku nikiiacha akili yangu ichanganue mambo kwa nafasi, vinginevyo nitakuwa nakaribisha machozi tena katika maisha yangu, jambo ambalo napingana nalo kwa nguvu zote!” Aliwaza Tom.

“Lakini hapa sina ujanja tena, nimeamini hakuna mapenzi ya kweli, ni bora nikarudiana na Mariam wangu, ambaye ana mapenzi ya dhati na mimi, kwanza alinipenda kabla sijawa na kitu, kwanini nisiamini kama ananipenda?

“Nisidanganyike na hawa wasichana wa mjini, watanipotezea mwelekeo wa maisha yangu, nitakuja kulia halafu niishie kuchekwa na wabaya wangu. Mariam...Mariam wangu, tafadhali sikia kilio changu, ni kweli nimekukosea, lakini lazima ukumbuke hii dunia ina vishawishi vingi sana.

“Nilipoteza mawasiliano na wewe mpenzi wangu, sikujua kama ulipata matatizo makubwa kiasi ulichonieleza. Akili yangu ilinituma kwamba umeamua kunisusa na kumuacha baba yangu afe wakati wewe ukiwa katika matatizo makubwa.

“Nisamehe tafadhali, nisamehe mpenzi wangu na ninakuomba unikaribishe katika himaya ya mapenzi yako tena. Nisamehe mpenzi wangu, kukosea ni ukamilifu wa binadamu...tafadhali....nipo chini ya miguu yako....” akiwa anawaza hayo, ghafla mlango wa wodi aliyokuwa amelazwa ukafunguliwa.

Macho yake yakakutana na ya Juliana akimwangalia kwa huzuni huku machozi yakianza kumlengalenga! Mikononi mwake alikuwa amebeba maua mazuri yenye rangi nyeupe. Akasogea hadi kitandani alipokuwa amelala Tom, akapiga magoti chini huku mikono yake iliyobeba maua akiwa ameielekeza kwa Tom. Muda wote huo Tom alikuwa kimya akimtizama, hakunyanyua mdomo wake wala kufanya jambo lolote zaidi ya kumwangalia.

“Najua nimekukosea sana mpenzi wangu, kumbuka kwamba mimi ni binadamu, naomba unisamehe!” Juliana akasema akilia kwa uchungu.

“Nikusamehe?” Tom akauliza kwa sauti ya upole sana.

“Ndiyo naomba unisamehe mpenzi wangu, kwanza kumbuka kwamba Joseph alinilazimisha, nilipoona anazidi kuning’ang’ania nikamwacha!”

“Kwahiyo kila mtu akija kukulazimisha wakati mimi sipo utakuwa tayari kufanya naye uchafu kama mliofanya na Joseph siyo?”

“Sina maana hiyo mpenzi wangu!”

“Kumbe una maana gani?”

“Nilipitiwa mpenzi wangu, naomba unisamehe tafadhali!”

“Naomba kukuuliza swali moja la msingi sana!”

“Nakusikia!”

“Unafahamu kwamba wiki ijayo tutatakiwa kupanda madhabahuni kufunga ndoa?”

“Najua!”

“Sasa kuna ndoa gani ambayo kabla hata haijafungwa imeshaanza kuwa na usaliti?”

“Mpenzi wangu kumbuka tutaingia aibu sana kama tusipofunga, tumealika watu wengi sana na isitoshe wanatuheshimu sana, sasa tutaficha wapi nyuso zetu mpenzi wangu?”

“Jiulize wewe utauficha wapi uso wako siyo mimi!”

“Najua sweetie ndiyo maana nakuomba msamaha! Kumbuka wazazi wangu wananipenda na kuniamini sana, wakisikia nimefanya mambo haya itakuwa aibu kubwa sana kwangu na kwa familia nzima kwa ujumla, naomba unisamehe tafadhali!”

“Sawa, nimeshakusamehe!” Tom akasema huku akilia, maumivu aliyokuwa nayo moyoni mwake yalikuwa makali sana.

“Kweli Tom? Umenisamehe kweli mpenzi wangu?”

“Niamini mpenzi, ni kweli nimekusamehe!”

“Nashukuru sana kusikia hivyo!”

“Hata mimi pia, lakini lazima uwe makini na jambo moja!”

“Nakusikia mpenzi wangu!”

“Siku nikukufumania kwa mara nyingine, ujue itakuwa ndiyo mwisho wa penzi letu!”

“Nimekuelewa!”

“Siyo uelewe pekee, uweke akilini mwako na uhakikishe hurudii kosa hilo tena!”

“Nakuahidi mpenzi wangu!” Juliana akaondoka hospitalini pale akiwa na furaha sana.

Taratibu za sherehe zikaendelea kama kawaida, Juliana alikuwa na hamu sana ya kufunga ndoa na Tom, alikuwa kijana mwenye mafanikio makubwa sana. Ndoa yao ilipangwa kufungwa kifahari sana, kwanza ingefungiwa katikati ya bahari wakiwa kwenye meli na sherehe nzima ya ndoa yao ingemalizikia huko. Furaha yake ikarejea kwa mara ya pili.

“Nashukuru sana Mungu amenisaidia, Tom wangu amenisamehe, nilikuwa na mashaka sana juu ya mpenzi wangu, sikuwa na uhakika wa kurudi tena katika himaya yake, hasa ndoa ambayo ilitaka kuingia dosari.

“Lakini na mimi nimezidi tamaa, Joseph ana nini kiasi cha kunichanganya akili yangu kiasi kile? Hata hivyo, sina sababu ya kuwaza mambo yaliyopita, acha niyaache yaliyopita yaende zake na mimi nibaki na maisha yangu nikisubiria ndoa yangu iliyopo mbele yangu!” Juliana akawaza huku akitabsamu.

*****

Siku iliyofuata Tom aliruhusiwa kurudi nyumbani baada ya afya yake kutengemaa, Juliana ndiye aliyeenda kumchukua hospitalini na kumrudisha nyumbani, njiani wakizungumza mambo mengi yaliyohusu ndoa yao.

Kila mmoja alionekana kuwa na hamu sana na ndoa yao, wakawa wanakwenda Kanisani kwa ajili ya Mafundisho ya Ndoa kama kawaida, wageni wengi walikuwa wamealikwa kwa ajili ya kwenda kushuhudia ndoa hiyo ya aina yake iliyopangwa kufanyika kwenye meli.

Kila kitu kilikwenda sawa ingawa Tom alikuwa na maumivu makali sana katika moyo wake, alikuwa akiwaza sana juu ya mabaya aliyofanyiwa na Juliana. Siku aliyomkuta Joseph ambaye alikuwa rafiki yake kipenzi kifuani mwa Juliana, ilijirudia akilini mwake kila wakati huku akihisi maumivu makali sana ya mapenzi.

Walishirikiana kwa kila kitu, lakini Tom alikataa kufanya mapenzi na Juliana kwa kisingizio kwamba anasubiri hadi siku ya ndoa.

“Lakini mbona tumekuwa tukifanya siku zote hizo?”

“Siyo sababu!”

“Ni sababu!”

“Siyo sababu mpenzi wangu, unajua hata kama tumemkosea Mungu kwa siku zote hizo, halafu tumekuja kugundua baadaye kwamba tulikuwa tunamkosea ni vizuri tukabadilika!”

“Hapana...!”

“Nataka niwe na wewe mpenzi wangu, kumbuka siku ya ndoa huwa na mshawasha wake, isitoshe tutakwenda fungate, huoni kwamba itakuwa siku nzuri kwa sisi kufanya mapenzi tena, halafu isitoshe wakati huo tutaita tendo la ndoa nadhani itakuwa nzuri sana!”

“Sawa lakini moyo wangu bado una maswali mengi sana!”

“Maswali ya nini?”

“Nahisi kama kuna kitu kinaendelea moyoni mwako!”

“Acha wasiwasi wako mpenzi wangu, nini hicho kinaendelea moyoni mwangu?”

“Basi tuachane na hayo!”

“Sawa basi, tulale!”

“Mwaaa!” Wakapeana mabusu motomoto na kulala.

*******

Zikiwa zimebaki siku tatu tu kabla ya ndoa ya Tom na Juliana, huku vyombo mbalimbali vya habari vikitangaza na kuandika juu ya ndoa hiyo ya aina yake nchini Tanzania, Tom alikuwa mwenye mawazo mengi sana. Ni kweli alikuwa akimpenda sana mpenzi wake Juliana, lakini kitendo cha usaliti kiliendelea kusafiri akilini mwake siku zote tangu siku ya tukio lile na baadaye kulazwa.

Alihisi moyo wake ulikuwa unakosa kitu muhimu sana, alimhitaji sana Mariam wake hata kama asingemuoa. Alichokifanya ni kuandaa kadi kwa ajili ya Mariam kisha akampigia simu na kumtaka aonane naye.

“Umesema unaitwa nani?”

“Thomas!”

“Tom?”

“Ndiyo!”

“Unataka kuonana na mimi?”

“Ndiyo!”

“Kuna nini?”

“Ni vizuri tuonane, siwezi kuzungumza kwenye simu!”

“Namba yangu ni nani amekupa?”

“Hilo siyo la muhimu kujua kama ambalo linanifanya nikuite!”

“Tukutane wapi sasa?”

“Nitakuja Mlimani City!”

“Wapi sasa?”

“Samaki Samaki!”

“Sawa, saa ngapi?”

“Saa mbili kamili usiku nitakuwa hapo!”

“Huwezi kufanya mapema zaidi?”

“Muda huo ni mzuri zaidi kutokana na aina ya maongezi niliyonayo!”

“Ok!”

“Kazi njema!”
 
SEHEMU YA 22 YA 50

Moyo wa Mariam ulilipuka sana, hakujua Tom alikuwa na kitu gani cha kumwambia hasa ukizingatia alikuwa akisikia kila kukicha juu ya maandalizi ya ndoa yake. Hata hivyo, aliisubiri jioni hiyo kwa hamu kubwa sana, alihisi kama mshale wa sekunde hautembei ipasavyo. Ikawa saa la kwanza, la pili hatimaye saa moja na nusu ilipofika alikuwa kwenye teksi akielekea Mlimani City kukutana na Tom.

Alifika Mlimani City saa 1:48 za usiku, akiamini alikuwa amewahi sana lakini cha ajabu alimkuta Tom akiwa anamsubiri kwa hamu kubwa sana. Mariam akamsogelea sehemu aliyokuwa amekaa akitetemeka kwa woga, hakuamini kama aliyekuwa amekaa mbele yake alikuwa Tom.

“Habari yako mrembo?” Tom akamsalimia.

“Nzuri! Mbona tumekaa sehemu ya wazi kiasi hiki? Kumbuka wewe ni mtu maarufu na isitoshe ndoa yako ipo mbioni kufungwa, huogopi wapiga picha wa udaku?”

“Wapo wanaosimamia hilo, siyo rahisi kupigwa picha, vijana wangu wapo kazini!”

“Sawa basi, sema ulikuwa unasemaje?” Mariam akauliza akiwa mtulivu sana.

Tom hakuongea chochote zaidi ya kutoa kadi na kumkabidhi. Mariam akaifungua na kuisoma, ilikuwa ni kadi ya mwaliko wa harusi yake ambayo ilikuwa inafanyika siku tatu zilizofuata.

“Umeamua kuja kunitukana? Hujatosheka na mateso uliyonipa?”

“Tulia mrembo huwezi kujua nina maana gani, lakini naomba usiache kuja, nina bonge la surprise kwa ajili yako!”

“Surprise?”

“Ndiyo, niamini tafadhali, naomba usipuuze!”

“Lakini wewe siku hiyo ndiyo unaoa na unafahamu kabisa ni kiasi gani nakupenda, unataka niumie moyo wangu kwa mara nyingine?”

“Sina maana hiyo Mariam, nakuomba uje halafu nakuhakikishia furaha. Amini siku hiyo itakuwa ya furaha kuliko zote zilizowahi kutokea katika maisha yako!” Tom alitumia kila aina ya maneno matamu kumshawishi, mwishowe akakubali.

Akatoa bahasha ya khaki ambayo ndani ilikuwa na milioni moja, akamkabidhi kama nauli. Mariam akakubali kufika kwenye harusi ya Tom.

******

Watu walikuwa wamefurika ndani ya meli, wakisubiria kwa hamu kubwa sana ndoa ya Julina na Tom ambayo ilikuwa ya aina yake. Ibada iliendelea kama kawaida, baadaye Mchungaji akawaita Tom na Juliana mbele kwa ajili ya kuwafungisha ndoa. Watu walipiga vigelegele na makofi wakiwashangilia.

“Je, Bi. Juliana David Mongara, umekubali kuolewa na Bw. Thomas Chacha, awe mumeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Mchungaji Samwel Kiswele aliuliza.

“Ndiyo Mungu anisaidie!” Juliana akajibu akimtizama Tom machoni mwake, moyo wake bado ulikuwa na wasiwasi mwingi.

Baada ya hapo Mchungaji Kiswele akamgeukia Tom na kumuuliza; “Je, Bw. Thomas Chacha, umekubali kumuoa Bi. Juliana David Mongara, awe mkeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Hilo lilikuwa swali gumu sana kwa Tom, akamwangalia Juliana usoni kisha akarudisha macho yake kwa waalikwa, yakagongana na ya Mariam.

Machozi yakaanza kumtoka.

“HAPANA MCHUNGAJI SIPO TAYARI!” Watu wote wakapingwa na butwaa. Juliana akiwa haamini alichokisikia, Tom akatoka mbio na kwenda kumshika Mariam mkono, ambaye mpaka wakati huo alikuwa haelewi kinachoendelea, akamwongoza hadi mbele. Akatoa pete iliyokuwa mfukoni mwake, kisha akachukua kidole cha Mariam na kumvalisha.

“Kuanzia sasa, wewe ndiye mchumba wangu na ninakuahidi sitakutesa katika siku zote za maisha yako! Tumuombe Mungu siku ya ndoa yetu ifike. Sherehe hii ni kwa ajili ya kumvalisha mchumba wangu Mariam pete ya uchumba, aliyonifanyia Juliana yanatosha!” maneno hayo yalipenya moja kwa moja masikioni mwa Juliana, hakuamini alichosikia,

Ghafla akahisi kizunguzungu, akaanza kuporomoka taratibu, mwisho akaanguka chini kama mzigo.







Ikiwa imebaki wiki moja tu kabla ya ndoa ya Juliana na Tom, Juliana anamsaliti Tom kwa kutembea na rafiki yake wa karibu sana aitwaye Joseph! Tom anashuhudia kwa macho yake jinsi mpenzi wake aliyempenda Juliana akifanya uchafu katika kitanda chao.

Haikuwa rahisi kuvumilika, Tom akaanguka chini kama mzigo! Baadaye akazinduka akiwa katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam. Muda mfupi baadaye anatoekea Juliana ambaye analia na kuomba msamaha.

Tom anakubali kumsamehe na wanakubalina kufungua ukurasa mpya! Taratibu za ndoa zinaendelea kama kawaida, ingawa akilini mwa Tom kulikuwa na kitu kingine zaidi, alipanga kumuumiza Juliana siku ya ndoa yao.

Alichokifanya ni kukutana na mpenzi wake wa zamani Mariam ambapo alimuomba sana asiache kuhudhuria hasuri yake ambayo ilipangwa kufanyikiwa ndani ya meli katikati ya Bahari ya Hindi. Mariam anakataa lakini baada ya kumshawishi kwa muda mrefu akakubali.

Siku ya ndoa, Juliana alipoulizwa na Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom alikubali, lakini Tom alipoulizwa kama alikuwa tayari kumuoa Juliana alikataa. Muda mfupi baadaye akamwita Mariam mbele na kumvalisha pete ya uchumba mbele za wageni waalikwa.

Watu walishangaa sana, Juliana akashikwa na uchungu mwingi sana, akashindwa kuzuia hisia zake, akaanguka chini na kupoteza fahamu. Je, nini kitatokea? SONGA NAYO....



Ukumbi mzima ulikuwa kelele tupu, utulivu uliokuwepo awali ulitoweka ghafla. Kulikuwa na makundi mawili katika kelele zile, wapo waliokuwa wakimsapoti Tom na wengine waliokuwa wakipingana naye. Waliokubaliana na Tom ni wale waliokuwa wakifahamu vizuri historia yake na Mariam.

Mama yake Tom hakuamini kilichotokea, akaenda mbele haraka akimfuata mwanaye. Wakati huo huo wengine walikuwa wakimchukua Juliana na kumpeleka kwenye chumba cha Huduma ya Kwanza kwa ajili ya kumhudumia.

Dakika moja baadaye mama Tom alikuwa ameshafika mbele baada ya kujipenyeza katikati ya watu waliokuwa wakizozana kutokana na tukio lililokuwa limetokea siku hiyo. Tom hakuwa na habari kabisa na mama yake, aliendelea kumkumbatia Marima huku machozi yakimtoka.

Mariam hakuamini kabisa kilichokuwa kikitokea, alihisi kama alikuwa katika njozi kali na pengine baada ya muda mfupi angezinduka. Hata hivyo baada ya kutingisha kichwa chake kwa nguvu aligundua kwamba hakuwa anaota kama alivyokuwa akifikiria.

“Tom mwananu, umefanya nini?” Mama Tom akamuuliza mwanaye.

“Unaaminisha nini mama?”

“Kwanini unatuharibia sherehe?”

“Sijaharibu sherehe mama, sherehe iliyopo hapa ni ya kumvalisha pete ya uchumba Mariam, hiyo ndoa yangu na Juliana haipo na wala sitaki kuisikia!”

“Kwanini hukusema mapema kuliko kuja kumuaibisha mwenzio na familia yake?”

“Ilikuwa lazima nifanye mama!”

“Kwanini unasema hivyo?”

“Naomba MC anipe kipaza sauti nitoe sababu za msingi za mimi kukataa kumuoa Juliana dakika za mwisho, najua mnanihukumu bure na hiyo ni kwasababu hamjui kilichotokea. Nipeni nafasi niseme ukweli!” Tom akasema akimtizama mama yake kwa makini sana.

Mama Tom akatoka na kumfuata MC ambapo alimuomba kipaza sauti na kumpelekea Tom ambaye bila kuchelewa alianza kuzungumza.

“Najua wengi mnanilaumu kwa kitendo changu cha kukataa kumuoa Juliana, lakini naamini nikiwapa sababu za msingi mtanionea huruma. Hata wewe mama yangu ambaye umekuja hapa mbele na kunisema kwamba nimekuabisha, utagundua kuwa Juliana ndiye aliyekuabisha.
 
SEHEMU YA 23 YA 50

“Naamini hata wazazi wa Juliana na ndugu zake wote watajua wazi kwamba mtoto wao ndiye aliyeleta aibu hii katika hii sherehe. Juliana hafai kabisa, ni mwanamke mwenye sura ya kike lakini siyo mke.

“Nilimpenda sana Juliana, moyo wangu nikamkabidhi yeye nikiamini kwamba angekuwa furaha ya maisha yangu, lakini imekuja kuwa tofauti. Juliana ameniumiza sana, amenitesa na nina uhakika alidhamiria kuniua,” Tom alikuwa akizungumza kwa hisia sana huku ukumbi mzima ukiwa makini kumsikiliza atakachokiongea.

Mpaka wakati huo, bado Tom alikuwa hajataja sababu ya msingi ya kuachana na Juliana, hivyo watu walikuwa na shauku kubwa sana ya kutaka kujua atakachokiongea.

“Wengi wenu mnafahamu kwamba wiki moja iliyopita nilikuwa nimelazwa, lakini hamjui sababu ya mimi kulazwa, ila leo nataka kuwaelezeni ukweli kwamba Juliana ndiyo cha mimi kulazwa. Nilianguka na kupoteza fahamu baada ya kumfumania Juliana akifanya mapenzi na rafiki yangu wa karibu sana Joseph!” Tom aliposema hivyo ukumbi mzima ulipigwa na butwaa.

“Aaaaaah!” Wati wote walisikika wakiguna.

“Ni maumivu kiasi gani aliyonipa Juliana? Ni nani ambaye angeweza kuvumilia maumivu hayo? Baada ya mambo hayo kutokea, niliamua kutulia, nikawaza kwa makini sana hatua ya kuchukua. Nilijua hakuna atakayenielewa kama ningehairisha ndoa.

“Kitu cha msingi ambacho kilikuwa kichwani mwangu ni kuacha taratibu zote ziendelee lakini akilini nikijua kwamba itakuwa ni sherehe ya kumvalisha Mariam pete ya uchumba na siyo ya ndoa yangu na Juliana. Nilikumbuka mengi aliyonifanyia Mariam, nikasikia uchungu sana.

“Mariam alinisaidia sana wakati nikiwa na shida, aliiba gari lao na kumpeleka baba yangu hospitalini akiwa hoi usiku wa manane. Kwa bahati mbaya wakati anarudi nyumbani, alipata ajali mbaya na kulala kitandani akiwa hajitambui kwa zaidi ya miaka minne!

“Yote hayo alifanya kwa ajili yangu, sikuwa na zawadi nyingine ya kumpa zaidi ya penzi la kweli kwake. Hiyo ndiyo zawadi ya pekee ambayo naona inamfaa kwa wema wote alionitendea. Mariam alikuwa katika hatari ya kufa, kupoteza fahamu kwa zaidi ya miaka minne ni nusu ya kufa, inawapasa wote mfahamu kwamba Mariam alikuwa katika hatari hiyo kwa ajili ya penzi lake kwangu!

“Kwanini nimuumize tena? kwanini nimtese tena? Pamoja na utajiri nilionao sasa, usaliti wa Juliana ulinifanya nikumbuke maisha yangu ya dhiki na taabu. Ni kitu gani alichokikosa kwangu hadi aanze kutembea na Joseph? Huyo Joseph ana nini ambacho mimi sina? Kwa hakika Juliana alinipa kidonda kikubwa sana katika moyo wangu lakini sasa nimeshapata tiba.

“Mariam ni tiba tosha katika maisha yangu. Naomba sherehe iendelee lakini ikumbukwe kwamba ni sherehe ya kumvalisha mchumba wangu Mariam pete, ni matumaini yangu kwamba siku chache zijazo, mtashuhudia ndoa yetu nzuri sana, itakayopendeza!” Tom alisema watu wakiwa kimya kabisa kumsikiliza.

Maneno aliyoongea yalikuwa makali san, watu wote walimwonea huruma, lakini wapo waliompongeza kwa ujasiri wake.

“Ana moyo sana huyu mtoto!” Mama mmoja aliyealikwa alimwambia mwenzake.

“Ni kweli, kama ni mtu mwingine asingeweza kuvumilia!”

“Lakini kuna kitu nahisi!”

“Kitu gani?”

“Unajua kwa jinsi Mariam alivyomsaidia, ilikuwa lazima arudiane naye siku moja!”

“Kwanini unasema hivyo?”

“Mapenzi yana nguvu sana ndugu yangu, kama mtu aliweza kuhatarisha uhai wake kwa sababu ya mapenzi, unadhani uhusiano wa aina hiyo unaweza kufa hivyo?”

“Kweli kabisa, mwacheni Mungu aitwe Mungu!”

“Yeye ni kila kitu, akisema iwe na inakuwa hivyo, akisema hapana, inakuwa hapana. Hakika yeye ni mwema!” Kila mtu alikuwa akiongea lake latika ukumbi huo uliokuwa kwenye Meli.

Sherehe ikaendelea kama kawaida, ingawa utaratibu haukuwepo na hakuwa na utaratibu wa kutoa zawadi. Walishauriwa warudi nazo kwanza hadi siku ya ndoa ya Mariam na Tom. Watu walikunywa, kula na kusaza.

“Tom!” Mariam alimwita walipokuwa wamejibanza kwenye eneo lenye giza totoro.

“Nakusikiliza mpenzi!”

“Umenishangaza sana!”

“Kwanini?”

“Sikutegemea!”

“Hata mimi pia, lakini leo nimeamini kwamba Mungu yupo na akipanga lake hakuna yeyote chini ya jua anayeweza kupangua. Nakuhakikishia Mariam, Mungu alipanga mimi niishi na wewe!”

“Ni kweli mpenzi wangu, tumetoka mbali!”

“Kweli kabisa, nakuhakikishia utafurahia maisha siku zote za uhai wako ukiwa na mimi. nataka kulipa fadhila zote kwako, nataka kukuonyesha kulala kwako kitandani kwa zaidi ya miaka minne ukiwa huna kumbukumbu ya chochote kinachoendele haikuwa bure!”

“Nitashukuru sana mpenzi wangu!”

“Mariam mpenzi!” Tom akaita kwa sauti iliyojaa mahaba.

“Naomba unifanyie kitu kimoja....”

“Sema tu, mpenzi!”

“Naomba unibusu!”

“Hilo tu, sema lingine!”

“Siyo zaidi ya busu lako!”

“Haya bwana! Mmwaaaaaaaaa...” Mariama akamuangushia Tom busu maridhawa kabisa.

“Ahsante sana mpenzi!”

Baada ya sherehe kuisha, meli ilirudi hadi Bandarini na kutia nanga, watu wakashuka na kutawanyika. Tom akampeleka Mariam Hotelini kwake. Mapenzi yao yakarudi upya, yalikuwa motomoto.

******

Mwezi mmoja baadaye taratibu zote zilikuwa zimeshakamilika. Tom alitambulishwa rasmi nyumbani kwa akina Mariam kama mchumba wa Mariam, wazazi wa Mariam hawakuwa na kipingimizi. Waliruhusu watoto wao waendelee na mapenzi yao kutoakana na ukweli kwamba walianza kupendana muda mrefu kabla wakati wanasoma.

Mipango ya ndoa ikafanyika haraka sana, ilipangwa kufanyika ndoa ya kifahari kuliko kawaida. Kama ilivyokuwa wakati akitaka kufunga ndoa na Juliana ndivyo alivyofanya pia safari hii, aliamua kufunga ndoa yake katikati ya Bahari ya Hindi, wakiwa kwenye meli.

Ndivyo ilivyokuwa, siku ya harusi ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa ilifika, waalikwa walikuwa ni wengi sana. Mariam na Tom walikuwa haamini kabisa kilichotokea, walikuwa na nyuso za furaha sana kufunga ndoa yao.

Mchungaji akawaita mbele wakiwa na wapambe wao, ambapo mara moja shughuli ya kuwafungisha ndoa ikaanza.

“Je, Bw. Thomas Chacha, umekubali kumuoa Bi. Mariam Isaya, awe mkeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Hilo lilikuwa swali rahisi sana kwa Tom, akamwangalia Mariam usoni kisha akarudisha macho yake kwa waalikwa, baada ya hapo akajibu.

“Ndiyo, Mungu anisaidie!” Ukumbi mzima ukapiga vigelegele na makofi kwa furaha.

Baada ya Tom kujibu, Mchungaji aliyekuwa akifungisha ndoa akamgeukia Mariam na kumuuliza; “Je, Bi. Mariam Isaya, umekubali kuolewa na Bw. Thomas Chacha, awe mumeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Mchungaji akamuuliza lakini Mariam hakujibu.

Mchungaji akaamua kuuliza kwa mara ya pili, bado Mariam alikuwa kimya. Ghafla Mariam akaanza kutoa miguno ya taratibu, baadaye akashindwa kujizuia na kuanza kuangua kilio. Tom akashtuka sana, hata waalikwa nao walipigwa na butwaa.

“Mariam kuna nini?”

“Hakuna!”

“Mbona hujibu maswali ya Mchungaji!”

“Hapana...”

“Hapana nini?” Tom akazidi kumuuliza akiwa haelewi kinachoendelea. Mariam alizidi kulia.





Tom haamini macho yake alipomkuta mpenzi wake ambaye walikuwa na mipango ya kufunga ndoa, Juliana akimsaliti, tena na rafiki yake wa karibu aliyeitwa Joseph.

Lilikuwa tukio lililomsononesha sana, hali iliyomsababishia simanzi, kabla ya kuanguka chini na kupoteza fahamu. Baadaye anazinduka akiwa katika Hospitali ya Ocean Road, ambapo Juliana anakuwa wa kwanza kuonana naye na kumuomba msamaha.
 
SEHEMU YA 24 YA 50

Tom anakubali kumsamehe na wanakubaliana kufungua ukurasa mpya! Taratibu za ndoa zinaendelea kama kawaida, ingawa akilini mwa Tom kulikuwa na kitu kingine zaidi, alipanga kumuumiza Juliana siku ya ndoa yao.



Akafanya mpango wa kukutana na mpenzi wake wa zamani Mariam ambapo alimuomba sana asiache kuhudhuria harusi yake ambayo ilipangwa kufanyikiwa ndani ya meli katikati ya Bahari ya Hindi. Mariam anakataa lakini baada ya kumshawishi kwa muda mrefu akakubali.



Siku ya ndoa, Juliana alipoulizwa na Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom alikubali, lakini Tom alipoulizwa kama alikuwa tayari kumuoa Juliana alikataa. Muda mfupi baadaye akamwita Mariam mbele na kumvalisha pete ya uchumba mbele za wageni waalikwa.



Siku chache mbele, Mariam na Tom wakaamua kufunga ndoa! Kama ilivyokuwa awali, ndoa yao ilifungwa katikati ya bahari, kwenye meli. Kitu cha kushangaza, Mariam alipoulizwa na Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom, alinyamaza.



Baadaye akaanza kulia kabisa. Tom alipomuuliza kama kulikuwa na tatizo lolote, Mariam hakujibu. Je, nini kitatokea? SONGA NAYO....



Kitendo cha Mariam kukataa kujibu swali la Mchungaji kama alikuwa tayari kuolewa na Tom au lah, kilimchanganya sana Tom, alishaanza kuhisi mchezo mchafu ulikuwa ukichezwa nyuma ya pazia. Ukimya wa Mariam ukazidi kumchanganya.



Hata hivyo alikosa raha zaidi baada ya kushangaa Mariam akianza kulia, hapo akili yake ikaenda mbali zaidi, alianza kufikiria kwamba, inawezekana Mariam alilazimishwa kumuumiza siku ya ndoa yao ili ampe maumivu lakini yeye hakuwa tayari.



Zote hizo zilikuwa hisia zilizoutawala ubongo wake, lakini mwenye majibu sahihi alikuwa ni Mariam pekee, alitakiwa kutumia kila njia anayoifahamu ili aweze kujua kilichokuwa kikiendelea. Akamgeukia Mariam wake ili amuulize kwa ajili ya kupata uhakika zaidi, tayari akili yake ilishabadilika, alipoteza matumaini ya kuwa na Mariam tena.



“Kuna nini Mariam?”



“Nishakujibu Tom.”



“Kwamba?”



“Sina tatizo.”



“Mbona unashindwa kumjibu Mchungaji, hujui kwamba ni wewe ndiye unayesubiriwa ili ndoa iweze kufungwa?”



“Najua...”



“Sasa?”



“Nashindwa kuamini kabisa.” Marim akasema akionekana kuwa na hofu sana na maneno aliyokuwa akiyaongea.



“Huamini nini tena? Kwani kuna nini?”



“Nashindwa kuzuia hisia zangu Tom, nimeshindwa kabisa.”



“Hisia za nini tena?”



“Machozi Tom, unajua wewe ndiye mwanaume pekee ambaye nilikukabidhi moyo wangu, siamini kabisa kwamba nimeweza kuwa na wewe tena katika ndoa!” Mariam akasema machozi yakizidi kumtoka.



“Amini mpenzi wangu...mwambie basi Mchungaji aendelee kwanza, haya mambo mengine tutazungumza wenyewe baadaye,” Tom alisema akiwa haamini kama Mariam hatamkataa, akili yake ilimtuma moja kwa moja kwamba lazima Marim angemkataa ili amuumize kama ambavyo yeye alivyomuumiza siku alipokutana naye Chuo Kikuu alipokwenda kutoa semina ya Ujasiriamali.



“Mchungaji unaweza kuendelea....” Mariam akamwambia Mchungaji.



“Nini kilitokea?” Mchungaji akauliza.



“Hakuna...” Mariam akajibu.



“Hpana...kuna kitu mnanificha. Kama kuna tatizo liwekeni wazi.”



“Hakuna Mchungaji, niamini mimi, hakuna kitu kingine zaidi ya furaha. Siamini kabisa kwamba leo naolewa na Thomas.”



“Hilo tu.”



“Kwani dogo Mchungaji? Kuolewa na mwanaume ambaye unampenda kwa moyo wako wote, nafikiri ni jambo la baraka sana!”



“Ni kweli kabisa, sasa naweza kuendelea Mariam?’



“Bila shaka.” Maram akajibu akionyesha tabasamu pana kabisa lililochanua vyema usoni mwake.



Muda wote huo Kanisa lilikuwa kimya kabisa, wakisubiri kitakachoendelea. Baadaye Mchungaji akamgeukia Mariam, ambaye sasa machozi yake yalishafutika na alikuwa akitabasamu muda wote kwa furaha. Mchungaji akamuuliza; “Je, Bi. Mariam Isaya, umekubali kuolewa na Bw. Thomas Chacha, awe mumeo, kwenye shida na raha, taabu na matatizo? Umpende, kumtunza na kumheshimu siku zote za maisha yako, hadi kifo kiwatenganishe?” Mchungaji akauliza, safari hii akiwa mtulivu sana.



“Ndiyo, Mungu anisaidie!” Mariam alipojibu jibu hilo, ukumbi mzima ulilipuka kwa vigelegele, makofi na vifijo.



Tom hakuamini kama ni kweli Marim alikuwa ameamua kuolewa naye. Aliendelea kuwa na mashaka hadi pale waliposaini pamoja katika vyeti vya ndoa. Baada ya hapo sherehe iliendelea hadi usiku kabisa ambapo meli ilirudi hadi Bandarini, ikatia nanga, wageni wakaanza kushuka na kwenda kuingia moja kwa moja kwenye magari kwa safari ya kurudi majumbani mwao.



Ilikuwa sherehe iliyopendeza sana, huo ukawa mwanzo wa maisha mapya ya ndoa, kati ya Tom na Mariam.



********



Maisha yao ya ndoa yalikuwa ya furaha sana, lakini tatizo lilikuwa moja tu, Tom alikuwa mtu wa starehe sana. Kila siku alikuwa haishi kwenda kwenye majumba ya starehe na kurudi usiku wa manane. Kisingizio chake siku zote kikawa ni kazi nyingi alizonazo.



Ingawa Mariam alikuwa na elimu nzuri, lakini Tom alimzuia kufanya kazi kwa kisingizio kwamba atamdharau. Siku zote Mariam alikuwa akijitahidi sana kumuelewesha Tom juu ya hilo lakini hakumuelewa.



“Na kwanini unalazimisha sana kufanya kazi?”



“Napenda mume wangu.”



Kuna unachokosa kutoka kwangu?”



“Sina maana hiyo.”



“Sasa kwanini unang’ang’ania kufanya kazi? Mimi nina uwezo na ninakutimizia kila kitu, nini kinachokufanya utafute kazi?”



“Ni vizuri kila mmoja akatoka, unajua ninapokaa hapa ndani nalemaa.”



“Unalemazwa na nini?”



“Lakini kwanini nimesoma sasa kama nilikuwa sina haja na kazi? Elimu yangu inanisaidia nini kama sitaitumikia jamii?”



“Hiyo jamii na mimi, ni nani mwenye umuhimu zaidi kwako?”



“Ni wewe mume wangu.”



“Basi sihitaji ufanye kazi.”



“Nimekuelewa ila kuna kitu kingine nataka tuzungumze.”



“Juu ya nini tena?”



“Tom mume wangu, umekuwa ukichelewa sana kurudi nyumbai, wakatiu mwingine unanikuta nimeshalala kabisa, uwe unajitahidi basi kuwahi kidogo!”



“Mariam una nini leo? Kwanza niwahi kuja kufanya nini? Mimi napika?”



“Hupiki, lakini unatakiwa kuja kula na mimi, ndiyo mapenzi hayo mume hayo mume wangu.”



“Nimekuelewa!” Tom akajibu kwa kifupi kisha akaondoka.



Maisha yao hayakuwa na furaha kama ilivyokuwa mwanzo, Tom alikuwa hana muda maalum wa kurudi nyumbani. Mbaya zaidi alirudi akiwa amelewa sana na hakutaka kula chakula cha mkewe. Jambo hilo lilimkosesha sana raha Mariam lakini hakuwa na jinsi, aliamua kuvumilia akiamini siku moja angebadilika.



*******



Ilikuwa siku ya Jumamosi usiku, ndani ya Ukumbi wa 56 Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Watu walikuwa wamejaa sana kushuhudia uzinduzi wa albamu mpya ya Bendi ya Kigingi Music Band ambapo pia mbali na uzinduzi wa albamu yao mpya, pia walikuwa wakiwatambulisha wanamuziki wapya walionunuwa na Tom ambaye ambaye alikuwa akiitwa Papaa Bill.



Pesa haikuwa tatizo, Papaa Bill (Tom) aliwanunua wanamuziki hao kutoka nchini Congo ambapo walikuwa wakifanya kazi katika bendi kongwe za muziki nchini humo, lakini kwa fedha alizokuwa nazo Papaa Bill, aliweza kuwaleta Tanzania na kuwalipa fedha nyingi sana.



Baadhi ya watu walikuwa wakimsikia tu Papaa Bill kwenye vyombo vya habari hasa magazeti na redio, lakini walikuwa hawajawahi kumuona. Kati ya hao alikuwa ni Mayasa. Msichana ambaye alikuwa na hamu kubwa sana ya kumuona Tom.



Mayasa alikuwa na nia zaidi ya kumfahamu, yeye alipanga kumuweka mkononi mwake. Pamoja na kusikia kwamba alikuwa na mke, lakini kwake halikuwa tatizo, alishaandaa mbinu za kutosha kwa ajili ya kumsana Tom. Huyu ni Mayasa wa Mbagala jijini Dar es Salaam.
 
SEHEMU YA 25 YA 50



Usiku huo alikuwa amevalia gauni jepesi sana linaloonesha kila kitu ndani! Kwa mwanaume yeyote ambaye hana matatizo, ilikuwa lazima ashtuke sana pindi atakapokutanisha uso wake na Mayasa. Kiasili alikuwa maji ya kunde, lakini mkorogo ulifanya kazi yake ambapo alionekana mweupe sana isipokuwa kwenye viungio vya ugoko wa miguuni na mikono, ambapo kutokana na ngozi kuwa ngumu sana, haikuweza kuchunika kwa mkorogo!



“Leo lazima nimuone huyo Papaa Bill!” Rafiki yake na Mayasa alisema.



“Bora wewe unayetaka kumuona, miye naondoka naye kabisa...” Mayasa alisema akionyesha kuwa na nyodo za wazi kabisa.



“Haya tuone. Unafikiri Papaa Bill ni sawa na hao wanaume wako wa Mbagala, huyu ni matawi ya juu.”



“Sasa nitajua kama Mbagala ipo Dar es Salaam au Lindi?” Mayasa alisema akionyesha kujiamini sana.



Dakika chache baadaye, wakati wakiendelea na mazungumzo yao, Mc wa siku hiyo, alisimamisha muziki kwanza kisha akamuomba Papaa Bill atoke mbele ya jukwaa ili awatambulishe wanamuziki wapya. Papaa Bill akatoka.



“Ninayo heshima kubwa sana, kumkaribisha Papaa Bill a.k.a Tom ili aje awatambulishe wanamuziki wetu wapya. Kwa taarifa tu ni kwamba, pamoja na kwamba yeye ndiye anayewalipa wanamuziki hao mishahara pamoja na kuwanunua, pia ndiye aliyeenda kuwachukua mwenyewe Congo!” Mc aliposema maneno hayo, ukumbi mzima ukashangilia.



Tom ‘Papaa Bill’ akapanda jukwaani kwa mbwebwe sana, jioni hiyo alikuwa amevalia suruali yake ya jeans ya rangi ya blue na fulana ya kubana ya rangi nyeupe. Mikononi na shingoni alichafuka cheni za madini ya fedha!



“Sina mengi ya kuongea, naomba niwatambulishe wanamuziki wetu wageni ambayo mimi mweny....” Tom alishindwa kumalizia sentesi yake, baada ya kugonganisha macho yake na Mayasa.



“Haki ya nani tena, sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kiasi hiki! Mh...wa wapi huyu?” Tom aliwaza akiwa amezidiwa vilivyo na hisia kali za mapenzi.



Kwa hali aliyokuwa nayo, alikuwa tayari kumsaliti Mariam wake.



“Naitwa Tom....bila shaka mimi ni Tom a.k.a Papaa Bill...namuhitaji huyu mwanamke, ni lazima nilale naye, lazima...” Tom akawaza huku akimtizama kwa matamanio.



Wakati huo Mayasa ndiyo akazidisha vituko, akapandisha gauni lake juu zaidi na kuacha sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa wazi. Tom akasikiza mwili wake ukipiga shoti!





Tom au Papaa Bill kama alivyojulikana na wengi amekuwa tajiri mkubwa sana nchini Tanzania, pamoja na utajiri wake amejikuta akiwa mtu wa starehe kupita kiasi. Hakuona tabu kutumia fedha nyingi katika sterehe. Alidhamini Bendi nyingi za muziki jijini Dar es Salaam kwa kutumia fedha ili kulinda heshima yake!

Siku moja katika uzinduzi wa Albamu mpya ya Kigingi Music Band, ndani ya Ukumbi wa 56 Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Tom alikutana na kitu ambacho

kiliuvuruga ubongo wake kwa muda! Macho yake yalikutana na msichana mrembo sana !

Huyu ni Mayasa, binti wa Mbagala jijini Dar es Salaam, anayejua kila aina ya utundu. Tom akaapa kuondoka naye, hakujua kama Mayasa naye alikuwa akimtega.

Je, nini kitatokea? Tom ataondoka na Mayasa? SONGA NAYO.....

Tom alibaki kimya kwa nukta kadhaa akizidi kumkodolea macho Mayasa ambaye kwa wakati huo vituko ilikuwa sawa na kiitikio kwenye nyimbo za Muziki wa Kizazi Kipya! Alihisi mapigo ya moyo wake kubadilika, alishasahau kwamba alikuwa jukwaani na alitakiwa kuwatambulisha wanamuziki wapya kutoka nchini Congo . Mayasa alishajua udhaifu wa Tom, alichokifanya ni kugeuka nyuma kisha akaanza kutembea kwa mwendo wa madoido akiacha sehemu kubwa ya miguu yake mizuri ikionekana kwa nyuma.

“Duh! Jamani hivi huyu mwanamke yupo katika dunia hii hii ya siku zote au ameshuka? Huyu lazima nitumie fedha zangu,” Papaa Bill akawaza kisha kwa taabu akajitahidi kuanza kuzungumza kwenye kipaza sauti.

“Samahanini sana kwa ukimya wa muda mfupi uliojitokeza, unajua nilikuwa nawaza ni kiasi gani tutakuwa na mashabiki wengi katika hii bendi yetu, wanamuziki niliokuja nao kutoka Congo ni wakali sana na bila shaka watafurahia mazingira ya Tanzania .

“Mimi sitakuwa na mengi sana ya kuzungumza, acha nimpishe Kiongozi wa Bendi, Abuu Sekidevi awakaribishe ili wapenzi wa bendi yetu wawaone,” Tom au Papaa Bill akasema kisha akakabidhi kipaza sauti kwa Mc wa siku hiyo.

Watu wakashangalia sana . Abuu ambaye alikuwa ndiye Kiongozi wa Bendi, akapewa kipaza sauti na kuwakaribisha wanamuziki wapya kutoka Congo .

Walishangiliwa sana .

“Kuna binti alikuwa amesimama pale,

mzuri-mzuri hivi, mweupe sana ni wa wapi?” Tom akamuuliza Jomba ambaye alikuwa mpambe wake.

“Yupi?”

“Alikuwa amesimama pale na wenzake!”

“Amevaa nguo za rangi gani?”

“Gauni jepesi!”

“Aaah! Nilimuona, vipi kwani?”

“Kanidatisha!”

“Kakudatisha?!”

“Ndiyo mkubwa, sasa ustaarabu unakuwaje?”

“Kwa mara ya kwanza nakuona ukianza kuzungumzia wanawake wa nje ya mkeo!”

“Ni kweli lakini leo nimezidiwa, lazima nikubali, sina ujanja!”

“Sasa vipi unamtaka?”

“Tena haraka sana !”

“Nipe dakika kumi tu!”

“Kweli?!”

“Nkuhakikishia!”

“Poa kaka, nakuaminia!”

“Ni kazi ndogo sana kwangu, msubiri sasa hivi anakuja kukaa na wewe meza moja, hayo mambo mengine nakuachia wewe!”

“Mambo gani tena?”

“Kumuimbisha!!”

“Sitazungumza kitu, fedha itanisaidia!”

“Nakuamini kaka!”

Jomba akaondoka akiwa anatembea kwa mbwebwe sana , alikuwa na uhakika wa kurudi na Mayasa, siyo kwa sababu anajiamini, bali alikuwa anamfahamu vizuri sana Mayasa. Siku zote msichana huyo alijua fedha na siyo mapenzi ya kweli.

Hakutembea sana , akakutana na Mayasa akiwa na kampani yake, akasimama mbele yao . Akatabasamu. Mayasa hakupata shida sana kujua kuwa Jomba alikuwa mpambe wa Papaa Bill. Alichokifanya na yeye ni kutabasamu.

“Mambo vipi warembo?” Jomba akasalimia.

“Poaaaaa....” Wote wakaitikia.

“Naona mpo!”

“ Kama unavyotuona!”

“Samahani mrembo, naweza kuzungumza na wewe kidogo?” Jomba akamwambia Mayasa.

“Kuna nini tena?”

“Nisikilize kwanza, mbona unakuwa na wasiwasi kiasi hicho?”

“Siyo wasiwasi, ni vyema nikajua hata dondoo kwanza!”

“Ni ujumbe wako!”

“Poa!” Mayasa akakubali. Wakaenda pembeni kuzungumza.

“Unamfahamu Papaa Bill?”

“Namsikia, kwani vipi?”

“Amesema nikuite!”

“Anataka nini?”

“Mtoto wa kike vipi? Mbona unakuwa na mashaka, twende umsikilize anasemaje?” Jomba akamwambia Mayasa ambaye hakubisha zaidi. Wakaongozana hadi kwenye meza aliyokuwa amekaa Papaa Bill.

Tom alipomuona alichanganyikiwa, kwanza hakuamini kabisa kwamba Jomba alifanikiwa kumleta Mayasa. Msichana huyo akakaa kwenye kiti akitabasamu kwa manjonjo ya kimahaba.



Tom haamini kama msichana aliyekaa pembeni yake ndani ya gari lake alikuwa Mayasa. Hata yeye alijishangaa, kwani hakuwahi kupenda kama alivyompenda Mayasa. Msichana huyo alimwingia akilini mwake kwa kasi ambayo hata yeye mwenyewe alishindwa kupata majibu kila alipojiuliza.“Yaani sijawahi kupenda katika maisha yangu kama ninavyompenda Mayasa, huyu mwanamke ameniingia hadi mimi nashangaa, sijui kuna nini bwana? Lakini hata hvyo ni mzuri sana, naamini uzuri wake ndiyo unanizuzua.” Tom akawaza wakati akiwa anashuka katika bonde lililopo eneo la Mkwajuni, Barabara ya Kawawa, akiifuata barabara inayoelekea Magomeni.“Papaa...” Mayasa akaita.“Vipi baby?”“Naona kama una mawazo, kuna nini?”“Hapana, hakuna tatizo, nipo sawa kabisa!”“Nahisi kuna kitu unajaribu kunificha!”“Hapana...”“Sawa kama hakuna kitu lakini nahisi kama kuna kitu kinakuchanganya akilini mwako, au unamuwaza mkeo?”“Nimuwaze mke wangu wakati nipo na wewe?”“Kwani
 
SEHEMU YA 26 YA 50

haiwezekani?”“Nitakuwa mwanaume wa ajabu sana.”“Kwanini unasema hivyo Papaa Bill?”“Kama nilikuwa naona ananifaa, ananitosha, ananiridhisha, ananivutia kwanini nihangaike kukusumbua? Lakini kwasababu kuna mapungufu katika maeneokadhaa ndiyo maana nimeona wewe unaweza kusaidia kuziba hayo mapengo!”“Kwahiyo mimi nipo na wewe kwa sababu ya kuziba mapengo tu?!”“Hapana...amini kwamba nimekupenda lakini wakati huo huo, tambua kwamba nina mke. Wewe utakuwa na nafasi yako kwangu na yeye atakuwa na nafasi yake, pia ni vizuri kila mmoja akaheshimu nafasi ya mwenzake....hasa wewe...” Tom alimwambia Mayasa akionyesha hana masihara kabisa na kilichokuwa kikitoka kinywani mwake.Pamoja na usaliti ambao alikuwa anataka kumfanyia mkewe Mariam, lakini moyo wake ulikuwa na maumivu makali sana. Hakutaka Mariam wake adharauliwe kwa sababu ya mwanamke wa nje, tena aliyekutana naye Club.Tom akaendesha gari kwa kasi alipofika Morocco,


kwenye makutano ya Barabara ya Uzuri na Kawawa ambayo alikuwa anaitumia, alikata kulia na kuifuata Barabara ya Uzuri hadi Sinza Kijiweni ambapo alikata kushoto kufuata Barabaraya Shekilango.Kasi ya gari ilikuwa ni ile ile, alibadilisha gia kila baada ya muda, hakuona haja ya kupunguza mwendo kwenye matuta ya barabarani, alikuwa akipita kwa mwendo ule ule. Alipofika kwenye mataa ya Shekilango, akakata kulia akifuata Barabara ya Morogoro ambapo aliendesha gari hadi kwenye mataa ya makutano ya Barabara za Morogoro, SamNujoma na Mandela, hapo alikata kushoto akiifuata Barabara ya Mandela.Hakufika mbali sana, kabla ya kufika RiverSide, akaingiza gari ndani ya geti jekundu,katika hoteli moja nzuri sana. Moja kwa moja wakaenda hadi Mapokezi wakipitia mlango maalum, akalipia chumba na kiupandishwa ghorofa ya nne kwenye chumba chake.“Karibuni sana.” Mhudumu akasema.“Tunashukuru lakini zingatia maadili ya kazi yako.” Tom akamwambia.“Kwanini unasema hivyo bosi?”

“Nafikiri unanifahamu vizuri!”“ Ndiyo....”“Ni nani?”“Papaa Bill!”“Sasa sitaki mtu yeyote ajue kuwa nimelala hapa, nenda na hilo kichwani mwako!”“Naheshimu na kuzingatia sana maadili ya kazi yangu!”“Usiku mwema!”“Nawe pia.”Tom aitumia muda mwingi sana kumwangalia Mayasa ambaye alikuwa na sura na umbo la kuvutia sana. Msichana hoyo, akipita sehemu yoyote ambapo kunamwanaume asiye na matatizo yoyote katika via vyake vya uzazi basi lazima asisimke.“Hebu simama.” Tom akamwambia Mayasa.Mayasa akasimama.“Zunguka nyuma!”

Tom akamwambia huku akitabasamu na kutingisha kichwa. Mayasa akafanya hivyo.“Sasa simama upande upande!”“Kwani vipi?”“Nataka kukuona vizuri!”“Kwani hukuniona?”“Ndiyo maana nimesema vizuri.”“Sawa bwana!” Mayasa akageuka, safari hii alikuwa akigeuka kwa mapozi, huku akipandisha gauni lake na kuacha miguu yake wazi, ambayo ilianza kupandisha presha yake ya mapenzi.“Hakika wewe ni mwanamke mrembo sana, sema chochote unachotaka nikupe ilikuonyesha mapenzi yangu kwako!” Tom akamwambia Mayasa akitabasamu.Mayasa akamfuata mahali Tom alipokuwa amekaa, akakaa na kupandisha mguu wakemmoja juu ya miguu ya Tom. Tom akahisi shoti ya umeme ikipita mwilini mwake. Mayasa alikuwa mwanamke aliyemchanganya sana ubongo wake.Akasogeza kinywa chake karibu kabisa nasikio la kuume la Tom, kisha akaanza kuzungumza kama anamnong’oneza; “Ni kweli unanipenda Papaa?”“Kwanini huniamini?”“Siyo kama sikuamini Papaa!”“Sasa kumbe nini?”“Kama nilivyokuambia kule Club, wewe ni mwanaume tajiri na maarufu, kila mtu anakufahamu, nitawezaje kuwa na wewe kama sitanyang’anywa?”“Mimi ndiyo mwamuzi, na ni mimi ndiye niliyekupenda. Ndiyo maana nimekuwambia chagu chochote utakacho nikupe ili kuonyesha penzi langu la kweli kwako!”“Sawa, naona itakuwa vizuri sana kama ukinihamisha nyumbani!”“

Una maana gani?”“Naishi na wazazi wangu na umri wote huuni aibu sana, kwanza nina wadogo zangu wawili wa kike na wote wanaishi na mabwana zao, nimebaki mimi tu, nyumbanikwahiyo naona itakuwa vyema kama utanipangishia chumba!”“Chumba au nyumba?”“Utakavyoona mwenyewe Bill”“Acha nikutafutie nyumba nzima, kuhusu samani za ndani niachie mimi, kila kitu utakikuta ndani ya nyumba!”“Nitafurahi sana Papaa Bill!”“Anza kufurahi kuanzia sasa!”“Sawa mpenzi wangu.” Mayasa akasema akicheka kwa sauti kubwa sana.“Nilitaka kusahau, unataka maeneo gani?”“Utakayoona yanafaa!”“Chagua mwenyewe!”“Kinondoni au Mwananyamala.”“Basi nipe muda mfupi sana, haitazidi mwezi mmoja!”“Sawa baby!” Baada ya hapo, lugha ya Kiswahili haikutumika tena.Hata hivyo lugha iliyozungumzwa badala ya Kiswahili haikuwa Kiingereza, Kifaransa wala lugha nyingine yoyote ambayo hutumika kama njia ya mawasiliano duniani. Walikuwa wakizungumza lugha ya mapenzi!*******Pamoja na kwamba Tom alikuwa anapenda sana starehe, haikuwahi kutokeahata siku moja, akaacha kurudi nyumbani. Siku hiyo hadi kufikia saa tisa na dakika zake za usiku, Mariam alikuwa hajamtia machoni mwake mumewe.Siku zote alikuwa mtu wa starehe sana lakini alipompigia simu alipopokea na kumweleza mahali alipo na wakati mwingine hadi muda aliokuwa akitarajia kurudi nyumbani. Siku hiyo ilikuwa tofauti sana, simu ya Tom ilikuwa haipatikani ka bisa!

“Masikini mume wangu, sijui atakuwa amekumbwa na balaa gani tena, siyo kawaida yake kuwa hajarudi nyumbani hadimuda huu, mbaya zaidi hata simu yake haipatikani,” Mariam akawaza akiwa amejilaza kwenye sofa kubwa sebuleni akiwa hoi kwa uchovu akimsubiria mume wake bila mafanikio.Mapenzi yao sasa yalibadilika, hayakuwa sawa na ilivyokuwa awali, mara nyingi Mariam aliishia kulala mwenyewe nyumbaniakiwa hana la kufanya. Hata alipotaka kutafuta kazi, Tom alikataa akidai kuwa uwezo wa fedha alionao, haumruhusu yeyekufanya kazi, kwani ana uwezo wa kumuachia fedha za matumizi kila siku bilamatatizo.Hakupata usingizi hadi asubuhi akiwa yuposebuleni akimsubiria mumewe, hadi kufikia saa mbili za asubuhi, Tom alikuwa hajafika nyumbani, mawazo yakazidi kumjaa akilini mwake.“Lazima nifanye jambo la ziada hapa, natakiwa kwenda kutoa taarifa Polisi kwanza!” Mariam anawaza kisha akaamua kwenda kubadilisha nguo haraka na kutokanje.Akiwa ndiyo kwanza, amewasha gari, anasikia honi ikipigwa mlangoni. Mlinzi anafungua mlango, gari la Tom linaingia na kuegeshwa pembeni. Mariam haamini macho yake.

Alitegemea kumuona Tom akiwa na huzuni kutokana na matatizo aliyohisi kuwa nayo, lakini alishuka akiwa na tabasamu pana.Mariam akashuka garini, akiwa ameyatulizamacho yake kwa Tom ambaye hakuonekana kuwa na chembe ya wasiwasi. Akaingia ndani na kumuacha Mariam akiwa amesimama nje, ni jambo ambalo lilichukua muda mrefu sana kuaminika akilini mwa Mariam.Mariam akamfuata Tom ndani, macho yakeyakianza kupatwa na unyevunyevu na kubadilika rangi na kuwa mekundu. Akamkuta Tom akiwa amejilaza kwenye sofa kubwa.“Vipi Tom mume wangu?”“Salama, za tangu jana?”“Mimi ndiyo natakiwa kukuuliza wewe!”“Ooooh! Hivyooeh....mimi mzima, sina matatizo!”“Lakini ulilala wapi?!”“Kitandani!”“Hayo ndiyo majibu gani Tom?”“Nimekwambia nimelala kitandani!”“Eti?”“Hujasikia au hujapenda? Halafu we’ mwanamke...naona sasa unataka kunipanda kichwani, tafadhali naomba uniache, usipende kufuatilia sana mambo yangu!” Tom akasema kwa sauti kubwa iliyoonyesha kujaa hasira.Mariam hakuwa na kitu kingine cha kuzungumza zaidi ya kwenda kujifungia chumbani, alichokifanya huko ilikuwa ni kulia akiamini alikuwa anapunguza hasira zake.Tom ameshaanza kubadilika, sasa ameanza tabia ya kulala nje na anarudi nyumbani bila woga kwa mkewe.



..Machozi ya Mariam yalikuwa na thamani kubwa, thamani hiyo ilitokana na kipimo cha mapenzi kilichokuwa ndani yake! Alimpenda sana Tom wake, lakini badilikola tabia yake lilimkosesha raha moyoni mwake.Mariam hakuwa na amani, alishindwa kuelewa ni shetani gani aliyemwingia mumewe na kumbadilisha kiasi kile. Hadi wakati huo hakuwa na uhakika kama aliyemjibu majibu machafu kiasi kile alikuwa Tom wake aliyemfahamu siku zote.“Sasa amezidi! Amefikia hatua ya kulala nje, Tom kwanini
 
SEHEMU YA 27 YA 50

unanitesa lakini?” Mariamalisema maneno hayo huku akilia kwa uchungu, chumbani alipokuwa amekimbilia.Hasira zilipomzidi Mariam, alijikuta akizidisha kilio, jambo lililomuudhi sana Tom ambaye haraka alitoka na kwenda chumbani kumfuata kwa lengo la kumpa kipigo.“Pumbaaaafu....hapa siyo Klinik, umeelewa? Naomba unyamaze haraka sana!”“Sinyamazi.”“Unasema?”“Sinyamazi Tom, niache nilie hasira zanguziishe. Unanitesa sana Tom lakini sasa umeona ili kunidhibitishia kwamba ni kwelihunipendi, umeamua kulala nje kabisa, sasanina thamani gani kwako mimi?!”“Hivi wewe mwanamke, nimekuoa au umenioa?”“Tumeoana!” Mariam akajibu kwa kujiamini huku akifuta machozi machoni mwake.Hakujua ni kiasi gani lilikuwa jibu baya kwa Tom. Alimwangalia kwa jicho la hasira kisha akamsogelea polepole huku akitetemeka kwa hasira zilizoonekana dhahiri.“Hivi, hii jeuri unaipata wapi wewe mwanamke? Nakuuliza wewe...hii jeuri unaipata wapi?”“Tom mpenzi wangu, kukuliza ulilala wapi imekuwa jeuri?”“Hata kama, mimi ni mwanaume na nina mambo mengi, na kama nilikuwa nahangaika na biashara zangu, utajuaje?”

“Ni lini uliwahi kulala nje Tom, kama kuchelewa ulikuwa unanipa taarifa, iweje kwenye kulala nje ushindwe kuniambia?”“Kwahiyo kila ninachokifanya lazima nikuambie siyo?”“Mimi kama mkeo, natakiwa kufahamu hayo yote, kumbuka uliahidi nini siku ya ndoa, kumbuka Tom mume wangu!”“Hata kama, lakini nimekuambia kuwa ninakazi nyingi na ndizo nilizokuwa nahangaika nazo, nilitegemea ungenipokeana kunipa pole, lakini mwenzangu ndiyo kwanza unaanza ugomvi!”“Lakini simu zilikuwa hazipatikani!”“Ziliisha chaji!”“Hapakuwa na njia nyingine ya kunijulisha Tom!”“Lakini mbona umeshikilia sana hilo jambo? Kitu kidogo unataka kiwe kikubwa?”“Natetea uhai wangu Tom, hivi unafikiri kama ukizoa maradhi huko na kuyaleta hapa nyumbani itakuwaje kama siyo kuniua?”“Unasemaje wewe mwanamke? Yaani mimini ukimwi? Sasa naona upole wangu unaniponza, unataka kunipanda kichwani sasa!” Tom akasema hayo huku akivua mkanda wake wa suruali.Kilichofuata baada ya hapo ilikuwa ni kipigo cha nguvu, ambapo pamoja na Marim kuomba msamaha Tom aliendelea kumpiga!“Nisamehe mume wangu utaniua, naomba msamaha, tafadhali Tom...nakufaaaaa...” Mariam alipiga kelele lakini Tom aliendelea kumpiga mpaka hamu yake ilipoisha akaamua kuachana naye.******BAADA YA MIEZI SITAMapenzi ya Tom na Mayasa yalizidi kushamiri huku mateso, manyanyaso na matusi kwa Mariam yakiwa ni vitu vya kawaida kila kukicha! Tom alibadilika sana, akawa hasikii wala haambiwi kwa Mayasa.Kama ni mapenzi basi yalitakiwa kutafutiwa jina lingine maana katika penzila wawili hao yalikuwa makali zaidi ya neno lenyewe!

Walikuwa kama kumbikumbi,kila mahali walikuwa pamoja.Tom alishindwa kuelewa kwanini alijikuta akizidisha mapenzi kwa yule mwanamke kwa kasi ambayo hata yeye mwenyewe hakujua ilipotokea. Alimuona Mariam kamakinyaa mbele yake, hakuwa na muda wa kukaa na Mariam hata kujadili kuhusu mambo mbalimbali ya familia yao.Muda mwingi alikuwa na Mayasa, Tom hakujua siri ya kumpenda zaidi Mayasa, kulikuwa na kitu kilichosababisha mapenzi kati yao kuongezeka! Mayasa alikwenda kwa Mtalaamu wa Kienyeji ambaye alimuwekea mambo yote sawa! Tom alikuwa mkononi mwa Mayasa na hakuwa na uwezo wa kufurukuta kwa namna yoyote ile! Alikuwa kama bendera ambayosiku zote huwa inafuata upepo.Siku moja Tom akiwa na Mayasa mjini, Tom alijikuta akifanya jambo la hatari sana. Baada ya kupungukiwa na fedha, waliamua kwenda kwenye mashine ya kutolea fedha ya CRDB Tawi la Azikiwe na kumtuma Mayasa aende akachukue pesa.“Sasa nitawezaje wakati sifahamu namba zako za siri?”“Hilo tu, nitakupa!”“Lakini ni vizuri ukaenda mwenyewe, mambo ya pesa hasa akaunti ni siri ya mhusika mpenzi wangu! Hebu shuka kwenye gari uende ukachukue pesa, acha uvivu wako!” Mayasa alimwambia Tom lakini alikuwa anamtania kwani alikuwa anajua kwamba dawa ndizo zilizokuwa zikifanya kazi.“Wewe ni mpenzi wangu siyo?” Tom akauliza.“Hata hili gari linajua hivyo.”“Umejibu vizuri sana, sasa sina haki ya kukutuma?”“Unayo!”“Namba za siri za hiyo kadi ni 1343, nenda katoe laki tano haraka!”“Sawa baba, isiwe ugomvi!” Mayasa akasema kisha akatoka kwa mwendo wa maringo kuelekea kwenye mashine.Tom alibaki hoi akikodolea macho makalio ya Mayasa, yaliyokuwa yanavutia sana. Watu waliomwona akipita, walishindwa kuzuia hisia zao na kujikuta wakimtimzama kwa macho ya matamanio.Ilibaki kidogo Mayasa azimie baada ya kuona fedha zilizokuwa kwenye akaunti yaTom, pamoja na kwamba alikuwa anafahamu Tom alikuwa na fedha nyingi sana, lakini hakuwahi kufikiria kwamba akanuti yake ingekuwa na fedha nyingi kile.

Akaunti ya Tom ilikuwa na zaidi ya bilionithelathini, hata hivyo alikuwa na akaunti nyingine katika Benki za NBC na Barclays ukiachilia mbali akaunti nyingine zilizokuwa nje ya nchi. Mayasa akachukua kiasi kile cha fedha na kurudi kwenye gari.“Umefanikiwa?”“Ndiyo!”“Twende!” Tom akawasha gari na kuondoka na Mayasa, safari yao iliishia katika moja ya Hoteli za sasa iliyokuwa ufukweni mwa Bahari ya Hindi.Wakiwa huko Mayasa alikumbushia ahadi ya kupangishiwa nyumba, aliyoahidiwa na Tom.“Haraka ya nini? Subiri kwanza!”“Lakini dear nitaendelea kukaa Mbagala hadi lini? Sina hadhi ya kukaa kule tena!”“Ni kweli lakini nimekuambia subiri mpenziwangu, nakuandalia kitu cha maana na muda mfupi baadaye utafurahia!”“Tutaona!” Walikula raha huko usiku mzima.******Wiki mbili baadaye Tom alimpigia simu Mayasa na kutaka wakutane kwa ajili ya kumpatia zawadi nzuri sana aliyoiandaa kwa ajili yake.“Kwani we’ uko wapi?” Mayasa akamwuliza.“Uwanja wa nyumbani 56 Club!”“Mimi nipo Mwananyama, acha nichukue taxi mara moja nakuja hapo sasa hivi!”“Nakusubiri mpenzi wangu!” Muda mfupi baadaye Mayasa akafika.Bila kupoteza muda Tom akamwambia Mayasa aingie kwenye gari. Akaingia. Wakaangaliana kwa pamoja na kuachia matabasamu mapana sana usoni mwao.“Leo ni siku ya furaha katika penzi letu, nataka kukuonyesha kwamba nakupenda, nakuthamini, nakuheshimu na nataka kuwa na wewe katika siku zote za maisha yangu!”“Mbona unanitisha mpenzi, kuna nini?”“Usijali, fumba macho yako, halafu nitakufunga kitambaa cheusi kisha nitakufungua baada ya kufika mahali zawadi ilipo, sawa?”“Hakuna shida mpenzi wangu!”

Tom akatoa kitambaa na kumfunga Mayasa usoni, kisha akaondoa gari.Safari yao iliishia Kinondoni B, karibu kabisa na Shule ya Sekondari Biafra ambapo kulikuwa na nyumba nzuri ya kifahari iliyokuwa na kila kitu ndani! Nje ya nyumba hiyo, kulikuwa kumeegeshwa gari mpya aina ya Toyota Rav 4 la rangi la Buluu, ukoka ukiwa umechukua nafasi kubwa pamoja na bustani nzuri iliyokuwa pembeni ya bwawa la kuogelea.Tom alipoegesha gari lake, akafungua mlango na kumtaka Mayasa atoke. Baada ya hapo akamfungua kitambaa usoni mwake na kumpa funguo mbili, moja wa gari na mwingine wa nyumba.“Huu ni funguo wa nyumba yako, na huu ni wa gari lako, lile pale. Kuanzia leo, hii ni nyumba yako, ina kila kitu ndani, furahia maisha mpenzi wangu!” Tom akasema akitabasamu.Mayasa hakuweza kuelewa kama yaliyokuwa yakitokea yalikuwa ni ndoto autukio la kweli. Akamwangalia Tom huku akitetemeka kwa furaha, midomo yake ikaanza kutingishika!“Ni nyumba ya kupanga au...” Tom hakumuacha Mayasa amalizie sentesi hiyo, akamkatisha.“Nimeinunua na hati yake hii hapa, nimekuwa nikifanya ukarabati na kuifanya ya kisasa kwa miezi sita sasa, hii ni nyumba yako....mali yako!” Tom akamwambia Mayasa akitabasamu.Tayari macho ya Mayasa yalishajaa machozi, akamsogelea Tom na kumkumbatia kwa nguvu, mabusu motomotomashavuni mwa Tom yalitawala.“Nimeamini unanipenda Tom!”“Tena sana, kuliko hata
 
SEHEMU YA 28 YA 50

Mariam!”“Kweli?”“Nakuhakikishia!”“Leo ni siku ya furaha ya penzi letu, ili niamini vizuri kama kweli unanipenda, twende tukalale nyumbani kwako, hapo utanifanya nione unanithamini na kunipenda na humpendi mkeo!” Mayasa akasema akiwa ameyatuliza macho yake usoni mwa Tom.Maneno yale yalizunguka kwenye ubongo wa Tom zaidi ya mara kumi bila kupata jibu la kumpa Mayasa.“Tom, nahitaji jibu lako mpenzi wangu!”Tom akafungua kichwa chake, macho yake yakitizama chini huku akionekana kuwa na mawazo mengi sana yaliyomkumba ghafla. Kila alipotaka kuzungumza alionekana kusita.







Kama ni mtihani, huu ulikuwa mkubwa kuliko yote kwa Tom! Pamoja na kumpenda sana Mayasa, lakini kitendo cha kumwambia akalale naye nyumbani kwake kilikuwa cha udhalilishaji mkubwa kwa mkewe wa ndoa Mariam.

Ni kweli Tom alikuwa katika mtihani mzito sana na hakuweza kufungua mdomo wake kusema chochote, hadi dakika mbili baadaye, Mayasa alimtingisha kwa nguvu na Tom kurejewa na kumbukumbu zake vizuri. Ni kama hakuwepo mahali pale.

“Mbona umenyamaza?”

“Unasema?”

“Mbona upo kimya, nahitaji jibu lako!”

“Najua Mayasa, lakini fahamu kwamba umenipa mtihani mkubwa sana!”

“Mtihani mkubwa kivipi?”

“Mayasa!” Tom akaita.

“Nakusikia mpenzi wangu!”

“Huoni kuwa huo ni mtihani mkubwa sana kwangu?”

“Labda nikuulize swali kabla ya kujibu lako!”

“Endelea...”

“Unanipenda?”

“Mayasa mpenzi wangu, hata wewe unaweza kunisaidia kujibu!”

“Pengine ninalo jibu, lakini yawezekana jibu nililonalo mimi ni tofauti na fikra zako!”

“Hapana...unavyowaza ndivyo nilivyo!”

“Kwahiyo sasa nikuambie ninavyowaza jibu yako?”

“Ndiyo!”

“Utaniamini?”

“Kwanini nishindwe?”

“Tom hunipendi, hunipen...” Mayasa akasema akilia.

Tom hakutaka kuyaona machozi ya Mayasa, haraka akaanza kumfuta machozi yake na kumbembeleza anyamaze.

“Niache nilie Tom, ni haki yangu!”

“Haki ya kuli? Kivipi?”

“Napenda nisipopendwa!”

“Usiseme hivyo mpenzi wangu, mimi nakupenda sana!”

“Kama unanipenda kwanini unanifanyia hivi?”

“Kumbe yote haya niliyoyafanya huoni thamani yake?”

“Sina maana hiyo, nataka udhihirishe penzi lako kwangu mbele ya mkeo, nataka mkeo afahamu kwamba yupo unayempenda zaidi, ambaye ni mimi. Kwanini unanitesa kiasi hicho Tom?” Mayasa alikuwa akizungumza kwa hisia sana huku machozi yakimtoka machoni mwake.

Tom hakujua kilichokuwa akilini mwa Mayasa, alifanya yote hayo kwa sababu alikuwa akihitaji Mariam afukuzwe ili aweze kuzitawala vizuri mali za Tom, hiyo ndiyo iliyokuwa ndoto yake siku zote. Kuchota mali za Tom ingewezekana kama Mariam angeondoka ndani ya nyumba ya Tom na hatua ya kwanza kwake ilikuwa ni kwenda nyumbani kwa Tom na kulala pale.

Aliamini kwa kufanya kungemchukiza Mariam na kuamua kundoka zake kwenda kwao. Wazo lake lilikuwa zuri sana ingawa hakujua ni kiasi gani lilikuwa sumu kwa mwenzake.

Ukimya wa mrefu ukapita, wote wakiwa hawazungumzi chochote hadi Tom alipoamua kuanzisha mazungumzo.

“Nina swali moja kwako!”

“Uliza!”

“Unanipenda?”

“Saaana!”

“Sasa sikiliza, mimi ni mwanamke na wewe ni mwanaume, sawa?”

“Ndivyo ilivyo!”

“Wewe una nafasi yako kama mke na mimi nina nafasi yangu kama mume ni kweli?”

“Hujakosea kitu!”

“Lakini pia unakubali kwamba, mwanaume ndiye kichwa cha nyumba?”

“Hata kwenye maandiko ipo!”

“Sasa mimi kama mumeo, kichwa cha nyumba, msemaji wa mwisho, naomba unielewe kwamba, kwa leo haitawezekana kwenda kulala nyumbani, lakini naweza kulala na wewe hapa kwa ajili ya kuizundua nyumba, umenielewa?” Tom akasema kwa kujiamini sana ingawa alitarajia kukutana na jibu la kukataliwa.

Kinyume na matarajio yake, Mayasa alimsogelea Tom na kukumbatia kwa nguvu, kisha akausogeza mdomo wake karibu kabisa na wa Tom, akautoa ulimi wake haraka na kuutumbukiza kinywani mwa Tom. Wakaanza kufurahia mapenzi.

“Nimekuelewa mpenzi wangu, hakuna shida!”

“Nami nimefurahi sana kwa uelewa wako mpenzi wangu, naona sasa umekuwa na unatambua nafasi ya mwanaume katika mapenzi.” Tom akasema akishangulia ushindi moyoni mwake.

“Ahsante mpenzi wangu!” Maneno hayo yalitoka kinywani mwa Mayasa lakini moyoni ilikuwa ni tofauti kabisa; “Huna ujanja wewe, nakulea-lea kwanza, lakini kuna siku utaingia mkenge tu.”

Tom akamshika mkono Mayasa, wakaingia ndani. Macho ya Mayasa hayakuwa tayari kuamini kilichokuwa mbele yake, ilikuwa sebule nzuri ya kisasa yenye kila kitu cha maana!

Kwanza kulikuwa na seti ya masofa mazuri, chumba maalumu cha chakula (dinning room), jokofu kubwa, redio kubwa, luninga na deki yake na kila aina ya anasa.

Hayo yangekuwa makazi mapya ya Mayasa baada ya kuishi muda mrefu katika maisha duni huko Mbagala. Hakuamini macho yake, kama kweli Tom alikuwa amedhamiria kumjengea nyumba nzuri nzuri kiasi kile. Macho yake yalizunguka kila kona ya sebele ile ya kisasa yakitizama vitu vizuri vilivyokuwepo.

“Ahsante sana mpenzi wangu, siamini macho yangu!” Mayasa akasema akimwaga machozi kama mvua.

“Amini, amini mpenzi wangu, wewe ndiye niliyekuchagua kutoka moyoni mwangu!”

“Nakuamini mpenzi!”

“Sasa twende nikakuonyeshe bed room!” Tom akamwambia na kumshika mkono kisha wote kwa pamoja wakaongozana hadi chumbani.

Huko Mayasa ndiyo alishindwa kuelewa namna gani atakavyotoa shukrani zake. Kilikuwa chumba kikubwa, kizuri na chenye kila kitu! Kwanza kulikuwa na kabati kubwa la nguo, kitanda kikubwa cha futi sita kwa sita ambacho kilitengenezwa kwa kutumia ngozi, meza ya vipodozi pamoja na vikorobwezo kibao!

Choo na bafu vyote vilikuwa ndani, kukiwa na bomba la maji ya mvua ambayo hutoka ya moto, baridi na ya mchanganyiko! Kilikuwa chumba cha kisasa sana. Mayasa akamwangalia Tom, kisha akajikuta hisia zake za mapenzi zikimpanda sana, akamsogelea na kumtupia kitandani. Kilichoendelea huko ilikuwa ni shughuli nzito iliyomalizika baada ya saa moja.

Wote wakiwa na furaha wakatoka na kwenda nje kuogelea katika bwawa la kuogelea. Hakika yalikuwa maisha ya kifahari sana, kila kitu kilikuwa kipya kwa Mayasa. Siku hiyo hawakutoka kabisa, kila kitu kilikuwa ndani. Vyakula vyote vilikuwa kwenye majokofu.

Walipomaliza Tom alijipumzisha nje, wakati Mayasa akiendelea kupika chakula ndani. Mayasa alijiona mshindi katika maisha mchezo ule hatari wa kuisambaratisha ndoa ya watu.

“Haya ndiyo maisha, lakini mambo bado, nitahakikisha ananyooka, mimi ndiyo Mayasa mtoto wa mjini, niliyezaliwa, kukulia na kusomea katika jiji la wanjanja, jiji la Dar es Salaam,” Mayasa alijisemea moyoni mwake wakati akipika chakula cha usiku.

Baadaye walikula na kulala usingizi wa mapenzi mazito.

******
 
SEHEMU YA 29 YA 50

Macho ya Mariam yaliganda katika saa ya ukutani iliyokuwa ikionyesha kuwa ilikuwa imeshatimia saa 7:55 usiku! Zilibaki dakika tano tu, kabla ya kufika saa 8:00, muda ambao kwa hakika, wanandoa wengi huwa katika harakati za kutafuta watoto!

Mariam alikuwa sebuleni akiwa anamsubiria mume wake bila mafanikio. Machozi yake sasa yalikuwa ya kawaida. Vituko na mateso kutoka kwa mumewe vilizidi, hakuona kama alikuwa na thamani kwa mumewe tena. Siku zote alikuwa wa kumangwa na kutukanwa kuwa yeye mgumba, neno lililomuuma sana.

“Kwahiyo kwasababu sijashika mimba ndiyo anichukie kiasi hiki? Tom hanitendei haki, ananinyanyasa!” Mariam alisema kwa sauti kubwa na kuamua kwenda chumbani kulala, hapakuwa na matumaini ya Tom kurejea.

Asubuhi ya saa 4:30, gari la Tom lilikuwa likipiga honi nje, mlinzi akafungua na Tom akaingiza gari na kuegesha mahala pazuri. Akashuka na kuingia ndani. Alipokutana na Mariam sebuleni, hakuonyesha kama kuna kosa alilokosea, akamsalia katika hali ya kawaida kabisa.

“Umeamkaje Mariam?!” Tom akamsalimia huku akielekea chumbani.

“Salama!” Mariam alipojibu, Tom akaongeza mwendo kwenda chumbani.

Mariam hakuweza kuvumilia zaidi, akamfuata nyuma nyuma hadi chumbani. Hakuwa na ukali kwa mume wake, akamwacha akavua nguo na kwenda bafuni, aliporudi ndipo alipomwomba kuzungumza naye.

“Lakini mume wangu, kwanini umebadilika tabia kiasi hiki? Kila siku unalala nje, kwanini lakini?” Mariam akamwuliza Tom.

“Mazungumzo yenyewe ndiyo haya?”

“Ndiyo, kwani unaona ni madogo mume wangu?”

“Makubwa, tena makubwa sana!”

“Sasa una mpango gani?”

“Wa kuendelea kulala nje kila siku!”

“Naomba usifanye hivyo Tom wangu, unajua ninakupenda sana!”

“Hata mimi nakupenda sana, lakini kipo kinachokifanya nilale nje, sasa kama unataka nianze kulala nyumbani, basi niruhusu niwe nakuja na kinachokifanya nilale huko nje!”

“Hilo ni jambo dogo sana kwa mtu anayempenda mpenzi wake kama mimi. Hakuna tabu, nimekuruhusu!”

“Kweli?”

“Niamini mpenzi wangu!” Wakakumbatiana kwa furaha.

Siku nzima Tom alishinda nyumbani akiwa na mkewe, tena akijitahidi kumpa haki ya ndoa kwa kikamilifu, lakini jioni akamuaga Mariam kuwa anatoka kidogo.

“Unakwenda wapi tena?”

“Kuchukua hicho kinachonifanya nisilale nyumbani karibu kila siku!”

“Sawa!” Mariam alijibu akitabasamu.

******

Mariam alichukulia maneno ya Tom kama utani, hakujua kama mwenzake alikuwa akimaanisha alichokuwa akikizungumza. Tom alipoondoka, moja kwa moja alikwenda nyumbani kwa Mayasa ambaye alimkuta akitizama luninga sebuleni.

“Njoo chumbani nina habari njema mpenzi wangu!”

“Habari njema? Kuhusu nini tena?”

“Jiandae tuondoke!”

“Tunakwenda wapi?”

“Nimesema jiandae twende!” Ndani ya dakika kumi tu, Mayasa alikuwa ameshamaliza kuvaa na walikuwa njiani wakielekea nyumani kwa Tom, ingawa Mayasa alikuwa hajui.

“Tunakwenda wapi lakini?”

“Leo tunaenda kulala kwangu, nataka Mariam ajue nina akili na nilifunga naye ndoa kwa bahati mbaya, wewe ndiye unayefaa kuwa mke wangu wa ndoa na siyo yeye!”

“Sijakusikia vizuri, umesema tunaenda wapi?”

“Nyumbani kwangu!”

“Nakupenda sana Tom, kweli sasa umeamua kudhihirisha penzi lako kwangu, naomba ukanyage mafuta sawasawa tumuwahi huyo mwehu wako!” Mayasa alimwambia Tom kwa sauti iliyojaa mahaba mazito, kweli Tom akafuata maagizo aliyopewa na Mayasa, akakanyaga mafuta kisawa-sawa.

Alikuwa anamuwahi Mariam, hakika alidhamiria kumuumiza.





Mayasa alikuwa akishangilia ushindi moyoni mwake, alijiona mwenye akili kuliko kawaida. Alimshukuru sana mganga wake kimoyomoyo, akiamini ndumba zilikuwa zinafanya kazi ipasavyo.

“Huu ni mwanzo mzuri sasa, naamini kila kitu kitakwenda sawa, utajiri wa Papaa Bill utakuwa wetu na siyo wake.

“Halafu inaonekana hicho kimwanamke chake hakijui mapenzi, sasa ngoja nimuonyeshe mji, mimi ndiyo mtoto wa mjini bwana!” Aliwaza Mayasa akimtizama machoni Tom.

“Tom...” Mayasa akaita.

“Nakusikiliza mpenzi wangu!”

“Nimeamini kwamba unanipenda sana, wewe ni mwanaume wangu wa maisha na sasa najihakikishia kuwa na wewe siku zote za maisha yangu.”

“Ni kweli kabisa, usiwe na wasiwasi Mayasa wangu, yaani mpaka najuta kumfahamu Mariam, sijui kwanini nilikutana na yule mjinga-mjinga, yaani nina mkosi wa ajabu sana, simpendi yule mwanamke hata chembe!”

“Pole sana, lakini mimi nipo kwa ajili ya kukupa furaha katika maisha yako, usiwe na wasiwasi mpenzi wangu, kila utachokitaka kwangu utakipata, sawa sweetie wangu?!” Sauti ya mahaba ilimtoka Mayasa, tena kwa kutokea puani.

Tom alikiri kwamba mwanamke yule alifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kuufanya moyo wake mateka. Hakuwa na la kufanya zaidi ya kukubali kuwa katika himaya ya mapenzi ya Mayasa.

“Naweza kukuliza!” Mayasa akamwuliza Tom.

“Maswali mangapi?”

“Moja tu!”

“Uliza.”

“Nataka kujua tutalala wapi?”

“Una swali la nyongeza?”

“Hapana.”

“Umesema unataka kujua mahali tutakapolala?”

“Ndiyo!”

“Hilo tu?”

“Kwani dogo?”

“Ok! Vizuri sana, acha nikujibu kwa vitendo!”

Alichokifanya Tom ni kuchukua simu yake kisha kubonyeza namba za Mariam, ikaita na baada ya muda ikapokelewa. Tom akaweka sauti ya juu ‘loud speaker’ kisha akaanza kuzungumza naye.

“Vipi Tom mume wangu?”

“Salama mama, habari za hapo nyumbani?”

“Nzuri, sijui wewe?”

“Mie ni mzima wa afya njema!”

“...ah Tom wangu, kama kuna siku umenifurahisha ni leo, yaani umenipa raha sana!”

“Kweli eh?!”

“Saaana, halafu naomba uwahi, usiku wa leo utakuwa kwa ajili yetu, nitakuonyesha mambo zaidi ya mchana!”

“Sawa mpenzi, hakuna shida, umepika nini?”

“Chakula chako ukipendacho!”

“Nini?”

“Bunia!”

“Kama siyo ndizi samaki, basi itakuwa ugali samaki!”

“Ni ugali samaki mpenzi wangu, mboga za majani na mtindi, najua leo utajilamba sana!”

“...hasa kama samaki wenyewe watakuwa sato!”

“Ni lini nimekupikia samaki wengine tofauti na sato?”

“Utakuwa mlo mzuri sana kwangu!”

“Basi uwahi Tom, angalau tuoge pamoja!”

“Hakuna tabu, lakini nitakuwa na mgeni, sasa ni vizuri kama utaandaa kile chumba cha wageni vizuri!”

“Hilo tu mume wangu, labda useme lingine!”

“Na chakula chake pia!”

“Hakuna shida!”

“Basi baadaye mpenzi wangu!”

“Sawa...mwaaaaaaa....”

“Mwaaaaaa...” baada ya mazungumzo hayo kwenye simu, Mariam alimuangushia busu mwanana Tom ambaye naye alijibu kisha akakata simu.

Baada ya hapo akamgeukia Mayasa akamwangalia kwa jicho lililojaa mahaba, huku akitabasamu kwa furaha. Alikuwa akishangilia ushindi!

“Nadhani umesikia kila kitu!”

“Sina la kuongeza mpenzi wangu, sasa moyo wangu mweupeeeee!”

“Leo ni siku yake, atajuta kukutana na mimi, mwanamke ananing’ang’ania utafikiri aliambiwa mwanaume nipo peke yangu? Nimeshafanya kila aina ya vituko lakini hasikii, sijui ni mwanamke wa aina gani yule?”

“Kwanza mwanamke gani mgumba? Subiri nikuzalie watoto haraka-haraka, upate warithi wa mali zako!” Mayasa akadakia.
 
SEHEMU YA 30 YA 50

Ilikuwa kauli ambayo ilimsisimua sana Tom, kuambiwa kwamba angezaliwa mtoto, tena haraka-haraka kulimpa faraja sana moyoni mwake, akawa na matumaini ya kuwa baba baadaye.

“Umenifurahisha sana Mayasa, hakuna kitu ninachokitamani kama kuwa baba, unanifanya nijisikie vizuri sana, ahsante sana mpenzi wangu, ahsante!”

“Tena nipe muda mfupi tu, kutoka sasa!”

“Tutaona!”

“Sasa?”

“Nini tena?”

“Tunakwenda moja kwa moja nyumbani au tunapitia mahali kwanza?”

“Wewe unaonaje?”

“Nilikuwa naona ingekuwa vizuri zaidi kama tutapitia mahali tuzungumze zaidi kwanza, kabla ya kwenda nyumbani. Nafikiri muda mzuri ni kuanzia saa tano au sita za usiku!”

“Tufanye saa saba!”

“Sawa, twende wapi?”

“Corner Bar!”

“Sawa!” Safari yao ikabadilika, wakaenda moja kwa moja Corner Bar, iliyopo Sinza, Afrika Sana, jijini Dar es Salaam.

******

Furaha iliyokuwa moyoni mwa Mariam, haikuwa rahisi kuelezeka, alimuona kama Tom wake alikuwa mpya kabisa, sasa alikuwa na imani kwamba Mungu wake alikuwa ameshamsikia na yake yalikuwa majibu.

Hakuwa na chembe ya hisia tofauti na hizo, hakujua kama muda huo, Tom alikuwa na mwanamke Bar, tena alikuwa akipanga kwenda kulala naye nyumbani kwao. Hilo halikuweza kuchukua nafasi kabisa katika moyo wake.

Alichokifanya ni kuhakikisha anamridhisha mumewe ipasavyo siku hiyo, kitu cha kwanza kabisa kufanya ilikuwa ni kupika chakula kizuri sana ambacho mumewe alikuwa akikipenda sana, ugali sato! Kitu kingine alichokifanya ni kuhakikisha chumba chao kinakuwa kisafi kuliko zote, baada ya hapo akafanya usafi katika chumba cha wageni.

Alipomaliza maandalizi yote hayo, akakaa sebuleni akimsubiria kwa hamu kubwa sana mumewe ambaye mpaka wakati huo, saa 2:00 za usiku, wakati taarifa ya habari ya Kituo cha Televisheni cha ITV ikianza, alikuwa hajafika!

Saa moja ikaondoka, ya pili, tatu na hatimaye ilifika saa 6:00 za usiku, Tom akiwa bado hajafika, hapo ndipo alipoanza kupatwa na wasiwasi ambapo aliamua kumpigia simu. Hata hivyo simu yake haikupatikana!

Hakuingia chumbani, akabaki pale pale sebuleni akimsubiria mumewe kwa shauku kubwa! Saa saba kasarobo za usiku, honi ilisikika getini, Mariam hakuwa na mashaka kwamba aliyekuwa mlangoni alikuwa mumewe. Mlinzi akafungua geti, Tom akaingia ndani na kuegesha mahala pazuri.

Akafungua mlango na kushuka garini, kisha akazunguka upande wa pili na kumfungulia Mayasa, akashuka.

“Karibu nyumbani mpenzi!”

“Ahsante sana.”

“Twende.”

“Tangulia.” Wakaongozana moja kwa moja, hadi ndani.

Mariam akawapokea kwa furaha sana, hakujua kilichokuwa nyuma ya pazia. Tofauti na matarajio yake, Tom alipita moja kwa moja na Mayasa hadi katika chumba anacholala yeye na Mariam kila siku.

Mariam akashindwa kuelewa kilichokuwa kikiendelea, kuna wakati alikuwa akifikiria labda mumewe aliamua kumfanyia mzaha. Alidumu sebuleni kwa dakika mbili tu, sebule haikukalika tena, akaondoka na kuwafuata chumbani. Dakika mbili zilikuwa nyingi sana kwa Tom na Mayasa.

Aliwakuta wakiwa kama walivyozaliwa, huku wakicheza michezo ya kimahaba bila wasiwasi!

“Tom!!!”

“Mariam!?”

“Nini unafanya na huyu mwanamke huku chumbani kwetu?”

“Sitaki kuamini kama macho yako yamepoteza uwezo wa kuona kiasi hiki!” Tom akasema kwa sauti tulivu sana, ambayo ilionekana dhahiri kabisa alidhamiria.

“Toooom...”

“Yes Mariam!”

“Umeona haifai kufanya uchafu wako huko nje, na sasa umeniletea hapa nyumbani kabisa!” Sauti ya Mariam sasa, ilianza kukata-kata, huku machozi yakifanana kabisa na maji machoni mwake.

“Lakini ukiona hivi ujue hutakiwi, kwanini unang’ang’ania? Mwanamke gani wewe, hata shepu huna, hebu ona wenzako tulivyojazia...hivi wakati wazuri tunaumbwa, we’ ulikuwa wapi mwenzetu? Hebu toka utuachie nafasi tujinafasi!” Mayasa akasema, akimtizama Mariam kwa dharau sana.

Wakati huo Mayasa alikuwa akijitingisha-tingisha akiwa kama alivyozaliwa. Mapigo ya moyo wa Mariam yaliongezeka kasi kuliko kawaida, akahisi kizunguzungu na kuanguka chini kama gunia la mchele.

“Haaaaah, Mariam?!” Tom akapiga kelele.

“Wa nini, mwache afe!” Mayasa akasema.

“Lazima tumsaidie!”

“Sasa amua kuwa na mkeo au mimi!” Mayasa akasema akianza kuvaa nguo zake tayari kwa kuondoka.

“Usifaye hivyo Mayasa, lakini tunatakiwa kumsaidia!”

“Inaonekana bado unampenda huyo mkeo, sasa baki naye!” Sasa Mayasa alikuwa anatoka nje ya chumba kile.

Tom hakutaka kuruhusu jambo lile litokee, akamfuata na kumrudisha chumbani, pamoja na kwamba moyo wake ulikuwa ukimuuma sana, lakini kwa kumridhisha Mayasa, Tom akaamua kumburuza Mariam hadi sebuleni kisha akarudi chumbani kulala na Mayasa. Hadi wakati huo, Mariam alikuwa hajazinduka.





Kitendo cha Tom kukubali kumuacha Mariam akiteseka sebuleni na kwenda chumbani kulala na Mayasa, kilimfurahisha sana Mayasa, alijiona mwanamke mshindi ambaye ana nguvu ya ushawishi. Hali ilikuwa tofauti sana na Tom, yeye moyoni mwake alikuwa mwenye uchugu mwingi sana, ingawa ni kweli alikiri kwamba Mayasa alikuwa moyoni mwake zaidi kuliko Mariam.

“Umenifurahisha sana mpenzi wangu, sasa naamini kweli unanipenda kwa mapenzi ya dhati, wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu, siwezi kukuacha hata siku moja!” Mayasa akasema akimkumbatia Tom aliyekuwa anaonekana dhahiri hana furara aliyokuwa nayo awali.

Jambo hilo liligundulika haraka sana na Mayasa, alijua wazi kwamba Tom hakuwa na furaha aliyokuwa nayo awali, jambo ambalo kwa kiasi kikubwa hakulipenda, siku zote alitaka kuibuka mshindi, kupotea kwa furaha ya Tom, kwa kiasi kikubwa kulimaanisha ushindi wake ulikuwa katika hati hati za kutoweka.

Ni jambo ambalo Mayasa alipingana nalo siku zote, kwake kulikuwa hakuna kitu kinachoitwa kushindwa, ushindi ndiyo kitu pekee ambacho kilikuwa na maana kubwa katika maisha yake, akili yake iliwaza ushindi pekee, bila kujali njia ambayo ushindi huo ungepatikana!

Alimwangalia Tom kwa jicho la hasira, kisha mkono wake akaupeleka moja kwa moja hadi kwenye sidiria yake alipokuwa amefunga hirizi yake na kuiminya kwa nguvu!

“Una nini Tom?” Mayasa akauliza kwa ukali sana.

Tom hakujibu!

“Hivi, nazungumza mwenyewe?”

“...hapana...” Tom akajibu kama alikuwa ametokea katika usingizi mzito.

“Bali?”

“Mbona upo hivyo?”

“Vipi Mayasa?”

“Umeniitaje?!”

“Mayasa!”

“Yaani umefikia hatua unaniita Mayasa?”

“...samahani mpenzi wangu, nilipitiwa kiudogo, unasemaje mpenzi wangu?”

“Inaonekana bado unampenda huyo mkeo, kama ndivyo ni bora uniambie niondoke zangu, sikulazimishi kuwa na mimi!”

“Hapana, kwani kuna nini?”

“Mbona sioni uchangamfu wako? Hukuwa hivyo Tom, naona una mawazo ya mkeo!”

“...hapana...nani? mariam? Mimi...ah no! Labda siyo Thomas, siwezi kabisa kuwa na mwanamke mbovu kama yule, tena sijui nilikutana naye usiku au vipi? Tena usikumbushe kuhusu hilo lijanamke, hebu tuzime taa tulale...” Tom akajikuta akiropoka bila kujua maneno yale yalitokea wapi.

Kwa Mayasa ulikuwa ushindi ambao alikuwa akiutegemea siku zote. Kama ni barabara, basi hiyo ilikuwa imenyooka! Hapakuwa na kitu kingine zaidi kupanda kitandani na kulala usingizi wa kiutu uzima!

***

Kila alipojaribu kuvuta kumbukumbu juu ya watu waliokuwa mbele yake, hakuweza kuwajua kabisa. Hilo halikuwa na maana sana kwake kwa wakati huo, lakini kwanini waliamua kumtesa na kumnyanyasa ndiyo jambo ambalo lilimnyima kabisa raha.
 
SEHEMU YA 31 YA 50

Huyu ni Tom, akiwa katikakati ya wanaume sita waliokuwa wamejazia vyema vifuani mwao, wakimwangalia kwa hasira huku wakimhakikishia kifo!

“Lazima ufe, we bweha!” Mmoja wa wanaume wale walioonekana kuwa na hasira sana akauliza.

“Nimefanya nini lakini?”

“Utajua mwenyewe, jiulize ni nani ambaye una ugomvi naye!”

“Ugomvi?”

“Ndiyo, ugomvi...ni nani ambaye huna maelewano naye?”

“Mbona naishi na watu vizuri sana!”

“Hata hivyo, hiyo siyo kazi yetu, tunachojua sisi ni kukuua tu na hiyo ndiyo kazi yetu ambayo tumelipwa kuifanya, hayo mambo mengine hatuna haja nayo!”

“Msiniue tafadhali!”

“Tutakuua tu lazima, hakuna kitu cha kubadilisha ukweli huu, lazima ufe.” Mtu mwingine ambaye alionekana kama ndiye mkuu wa wengine alisema kwa hasira.

Tom alishindwa kuelewa mahali pale palikuwa ni wapi na alifikaje? Alijaribu kuwaza kama kuna mtu alikosana naye, lakini hakumuona. Ghafla akashangaa amepoteza fahamu, alipozinduka baadaye, alikuwa katika katikati ya pori nene, mbele yake kukiwa na shimo kubwa, akiwa amezungukwa na wale vijana wenye silaha mikononi mwao.

Tom alikuwa amefungwa kamba mikono yote na miguu na hakuw ana uwezo wa kufanya jambo lolote. Tom alitetemeka sana.

“Naombeni mnisamehe tafadhali!”

“Hatuwezi kukusamehe, lakini tutafanya jambo moja kwa ajili yako!” Kiongozi wa lile kundi akasema.

“Ni nini?’

“Tutakuonyesha picha ya mtu ambaye ametuagiza tukuue!”

“Sawa, naombeni nimuone!” Tom akasema akiwa na hamu kubwa sana ya kujua ni nani ambaye aliamua kufanya njama za kumuua.

“...ambaye anataka ufe ni huyu hapa...halafu acha kufuatilia maisha ya watu...kufa salama...” Yule mtu akamwambia akimwonyesha ile picha.

Macho ya Tom hayakuwa tayari kuamini mtu wake wa karibu, mpenzi wake wa kweli ambaye aliamua kuachana na mkewe kwa sababu yake ndiye aliyekuwa akitaka auawe. Ilikuwa picha ya Mayasa. Tom akachanganyikiwa.

“Mayasa, nooooooooo.....” Tom akapiga kelele.

Katika hali ya kushangaza sana, wale wakaanguka mmoja mmoja baada ya kupigwa risisi kama mvua miilini mwao. Tom hakuweza kugundua ni nani aliyewapiga risasi. Ghafla akashangaa kumuona mtu mbele yake akiwa amevaa kininja, akijifunika hadi usoni.

Mtu huyo akaanza kuvua zile nguo za Kininja, kisha akavua ile kofia iliytofunika hadi uso wake, hapo ndipo Tom alipogundua alikuwa ni Mariam. Tom akashtuka sana.

“Mariam?!”

“Ndiyo ni mimi ninayekupenda, ambaye penzi langu halina mashaka kwako, nakupenda Tom ndiyo maana nimekuja kukuokoa...” Mariam akasema akitokwa na machozi kama mvua.

“Siamini macho yangu...Mariam....”

“Ni mimi!”

“Marimuuuuuuuuu....” Tom akapiga kelele kwa sauti ya juu sana. Muda huo huo akazinduka usingizini, alikuwa amelala kitandani na Mayasa, hapo ndipo alipogundua kwamba alikuwa ndotoni.

Ilikuwa ndoto ya ajabu sana, hakuweza kujua maana ya ile ndoto. Alipogeuza macho yake kumwangalia Mayasa, alimkuta akiwa anakoroma usingizini, akawasha taa na kunyanyuka polepole kitandani, kisha akaizima taa na kutoka hadi sebuleni kwenda kumfuata Mariam.

Moyo wake ulimuuma sana kumkuta Mariam hadi wakati ule hajazinduka, alichokifanya ilikuwa ni kumbeba hadi chumba cha wageni na kumlaza kitandani, akamfunika shuka na kumwekea chandarua. Moyo wake ulikuwa kama umepigwa ganzi, alishindwa kulewa ilikuwaje hadi akamchukia Mariam kiasi kile.

“Nashindwa kuelewa kwanini inakuwa hivi, ni kweli mimi siyo wa kwanza kuwa na mwanamke wa nje, lakini mbona mimi namfanyia mke wangu vituko kiasi hiki? Kuna nini lakini?” Tom akajikuta akijiuliza maswali mfululizo kichwani mwake bila kupata majibu yakinifu.

Akiwa anamwangalia Mariam aliyekuwa amelala pale kitandani kwa huruma, akashangaa mtu akimgusa mgongoni.

“Hivi we’ mwanaume una nini? Hutosheki? Umeona uje na huku?”

“Ah! Mayasa?!”

“Ndiyo mimi, unashangazwa na nini?”

“Samahani mpenzi wangu?”

“Imekuwaje tena?”

“Ah, hakuna kitu.”

“Unafanya nini hapa?”

“Nimeamua kumleta Mariam huku.”

“Kwanini?”

“Mbu zilikuwa zinamng’ata sebuleni.”

“Una uhakika hakuna zaidi ya hivyo?”

“Ndiyo, hakuna kitu.”

“Kwanini hukuniaga?”

“Sikuona sababu ya kukusumbua.”

“Haya twende chumbani.” Mayasa akamuamrisha Tom ambaye hakubisha.

Mayasa alikuwa mbabe kupitiliza, alikuwa na kitu kilichomfanya awe na jeuri aliyokuwa nayo, nguvu za giza alizokuwa akizitumia zilikuwa zinafanya kazi vyema bila ya Tom kugundua chochote. Walipofika chumbani, kazi ilikuwa moja tu, kupeana mapenzi motomoto hadi asubuhi.

Hawakulala tena, Tom hakuwa na kumbukumbu za Mariam tena, kichwani mwake kulikuwa na mtu mmoja tu, Mayasa. Alimuona mwanamke mzuri kuliko kawaida.

“Nakupenda sana Mayasa!” Tom akamwambia.

“Una uhakika?’

“Ndiyo, nakupenda sana, huoni mambo niliyokufanyia?”

“Mambo gani?”

“Nimekujengea nyumba nzuri, nimekupa gari na kila kitu utakacho nakupa, hiyo haitoshi kukufanya uamini kwamba nakupenda?”

“Haitoshi!!!”

“Unataka nifanye nini tena, sema chochote nitafanya!”

“Kweli?”

“Ndiyo, nakupenda sana na sitaki kukufanya uumie kwa ajili yangu!”

“Nataka umfukuze Mariam hapa nyumbani, tuishi kwa furaha!”

“Na kule kwako?”

“Nitaweka mpangaji, nataka kuishi na wewe hapa!”

Tom hakuwa na jibu.

*******

Jicho lake la kuume ndilo lilikuwa na kwanza kufumbuka, kisha likafuata la upande wa kushoto. Taratibu kumbukumbu zikaanza kumrejea Mariam. Kilikuwa chumba ambacho siyo alichokuwa akilala siku zote. Akapiga jicho kila upande na kujaribu kuvuta kumbukumbu zaidi, akatambua kwamba ni kweli siyo chumba anacholala siku zote.

Akakumbuka vyema kwamba kilikuwa chumba cha wageni, tena alichokiandaa jioni yake kwa ajili ya mgeni ambaye Tom alimwambia angekuja naye. Kufikia hapo, akakumbuka kila kitu. Alikuwa amelala katika chumba cha wageni. Hakuweza kukumbuka aliingia vipi na muda gani. Akaamka kichovu na kupiga hatua za taratibu kuelekea chumbani kwake.

Alipofika mlangoni, akasikia kelele za mahaba zikitokea chumbani. Walikuwa ni Tom na Mayasa wakipeana maraha chumbani. Mariam akachanganyikiwa, lilikuwa tukio la udhalilishaji sana. Mariam akachungulia kupitia tundu la ufunguo lililokuwa mlangoni, alichokiona humo ndani hakifai kuandikika hapa! Akaanza kulia.

“Tom mume wangu, ni nini unafanya na huyo mwanamke wako? Kwanini unakuwa hivi lakini? Yaani umeshindwa kufanya uchafu wako huko nje, unakuja kunifanyia hapa nyumbani, tena chumbani kwetu, katika kitanda ninacholala na wewe...Tom...Tom...Tom...kwanini unafanya hivi lakini?!” Mariam akapiga kelele akilia kwa uchungu.

Muda mfupi baadaye mlango ulifunguliwa, Mayasa akatoka akiwa amevaa upande wa kanga, tena kanga yake mwenyewe, uso wake ulikuwa umejaa makunyanzi, akamsogelea na kumzaba kibao kikali sana shavuni mwake.

“Koma kuharibu starehe za watu, ungekuwa na maana angenileta hapa? Huna jipya, mwanamke hujui mapenzi zaidi ya kufua na kupika, unafikiri kwa mtindo huo ataacha kutafuta mtoto wa mjini anayeweza kumpa raha kama mimi? Na utalijua jiji na mitaa yake...” Mayasa akasema akibenua midomo yake.

Uso wa Mariam ulilowana kwa machozi, alishindwa kuelewa kwanini mateso yale yalikuwa kwake tu na siyo kwa mwingine.

“Halafu Mariam uwe na adabu, naomba usijaribu kumsumbua mpenzi wangu, nenda kalale chumbako kwako kule!” Tom naye akatoka na kumwambia Mariam.

Mariam alihisi alikuwa ndotoni, lakini ukweli ni kwamba haikuwa ndoto, kila kilichokuwa kikitokea katika maisha yake kilikuwa yakini kwa maana ya yakini haswa.





Masikio ya Mariam yalikuwa hayataki kuamini yalichosikia wakati macho yake yakikataa katakata kukubaliana na kilichoonekana kupitia tundu la funguo, mambo yaliyofanyika chumbani yalikuwa mazito sana. Alishindwa kuelewa ni kosa gani kubwa alilomfanyia Mungu kiasi cha kumpa adhabu kubwa kiasi kile.

Ilikuwa lazima afikirie kitu cha kufanya, mawazo pekee yasingeweza kutosha kukabiliana na tatizo lililokuwa mbele yake. Alijua kitu kimoja moyoni mwake, kwamba alikuwa anampenda sana Tom, na mambo yote yaliyokuwa yakitokea ni juhudi za shetani kutaka kumharibia mume wake.

“Mungu ni wewe peke yako ndiye mwenye uwezo wa kunisaidia tatizo hili, naomba msaada wako baba, sina uwezo peke yangu, nisaidie mwanao...” Mariam aliomba moyoni mwake machozi machoni mwake yakitiririka.

Mara akapata wazo jipya, aliona ni bora aendelee kumuomba Tom abadili mawazo yeke. Aachane na huyo mwanamke kwani yeye ndiye mkewe wa ndoa aliyekuwa kwa ajili yake.

“Tom mume wangu, kwanini unanitesa kiasi hiki? Ni kosa gani nililokufanyia lakini mume wangu mpenzi? Kumbuka ahadi yako siku ya ndoa Tom, kumbuka!” Mariam alisema akitokwa na machozi.

“Huna kosa Mariam...” Tom akajibu akiwa chumbani.

“Sasa kwanini unanitenda hivi?”
 
SEHEMU YA 32 YA 50

“Huna mvuto mtoto wa kike, ndiyo maana ameona awe na mimi mwenye mvuto.” Mayasa akajibu.

“Sijakuuliza wewe!”

“Kumbe umemuuliza nani?”

“Mume wangu!”

“Unachekesha sana wewe, hivi Tom ni mumeo kweli wewe?”

“Kwani mume wa nani?”

“Yupo na nani chumbani? Hivi angekuwa anakuthamini angekulaza chumba cha wageni? Ameona huna jipya ndiyo maana amekususa, mwanamke usiye na haya, unayesubiri kutupiwa mabegi nje?! Kwani huoni kuwa hutakiwi humu ndani? Si uondoke...” Mayasa alisema maneno hayo macho makavu akiwa hana woga hata kidogo, alimchukia Mariam kuliko kitu chochote.

Mariam alikuwa ni kama anaharibu mambo yake, wazo la kwamba yeye ndiye aliyemwingilia mwenzake nyumbani kwake halikupata nafasi kabisa akilini mwake. Aliona kama Mariam ndiye aliyekuwa akimwingilia yeye.

Mariam alilia kwa uchungu mwingi sana, aliamini machozi yake pengene yangemuuma Tom na kubadilisha uamuzi wake, lakini ilikuwa tofauti kabisa, Tom alikuwa kimya chumbani akila raha na Mayasa, hakuonyesha kujali hata kidogo thamani ya chozi la Mariam.

Maisha yaliendelea kwa mtindo wa Mariam kulala chumba cha wageni na Tom kulala na Mayasa huku Mariam akishurutishwa kufanya kazi zote za nyumbani. Ni kama alikuwa mfanyakazi wa ndani! Kazi kubwa ya Mariam ilikuwa ni kusali, akimuomba Mungu wake amsaidie. Maisha yalikuwa ya shida sana.

Afya ya Mariam ikaanza kuzorota, kila siku kwake ilikuwa ni kilio. Tom hakuonyesha kujali, Mayasa alikuwa ndiye kila kitu nyumbani kwake, alipanga na kutoa amri ya kila jambo ndani ya nyumba. Usiku mmoja Mariam hakulala kabisa, alitumia kuwaza maisha yake, kwa muda wa miezi mitatu aliyovumilia, hakuna hata siku moja ambayo Tom alionyesha dalili za kubadilika tabia wala msimamo wake.

Tom alizidi kuwa mkali kwake na hakutaka kushirikiana naye kwa chochote, Mariam hakuona kama kuna sababu ya kuendelea kuteseka kwa mwanaume ambaye alikuwa hana mapenzi na yeye tena. Akapanga nguo zake usiku huo kwa safari ya kuondoka asubuhi yake. Alishachoshwa na vituko vya Tom.

*****

Saa kumi na mbili asubuhi, Mariam alikuwa ameshajiandaa kuondoka. Akiwa na begi lake la nguo, alikwenda hadi mlangoni mwa chumba cha Tom na Mayasa na kugonga. Alitumia muda wingi sana kugonga bila kufunguliwa.

“Nani?” Tom akauliza kwa ukali.

“Ni mimi!” Mariam akajibu kwa sauti ya unyonge sana.

“Sawa wewe, lakini nani?”

“Mariam!”

“Unataka nini asubuhi yote hii? Kwanini unatuharibia starehe zetu?”

“Samahani, sina nia mbaya!”

“Shida yako ni nini?”

“Nimekuja kukuaga Tom, naenda kwetu, nakuacha uendelee kuishi na mwanamke wako ambaye umeona anafaa kuliko mimi!”

“Siyo kwamba nimeona anafaa kuliko wewe, bali ndiyo uweli wenyewe ulivyo. Sasa unaondoka sasa hivi au baadaye?”

“Nimekuja kukuaga sasa hivi naondoka!”

“Hakuna neno wasalimie wote, waambie Tom au Papaa Bill sasa anakula bata na mtoto mzuri Mayasa!”

Mariam hakujibu tena, akaanza kulia akivuta mabegi yake kwenda nyumbani kwao. Kwa Mariam ilikuwa siku mbaya sana ambayo kwa hakika isingeweza kufutika katika maisha yake, lakini kwa Mayasa na Tom, ilikuwa siku nzuri sana kwao, kwani walikuwa wanaachiwa uhuru wa kufanya kila kitu wanachotaka kwa nafasi!

*****

“Vipi tena mwanangu? Mbona hivyo?!”

“Mama acha tu!”

“Nini?”

“Matatizo!”

“Matatizo gani? Mbona sikuelewi?”

Mariam hakuweza kujibu kitu tena zaidi ya kulia. Mama yake akamfuata huku naye machozi yakimtoka, lakini kabla hajamfikia, Maram alianguka chini na kupoteza fahamu.

“Mungu wangu, mwanangu ana nini jamani? Nini kimempata tena jamani?” Mama yake na Mariam alipiga kelele, muda huo huo baba yake Mariam akatoka ndani.

“Vipi kuna nini?”

“Mariam amekuja analia...kaanguka chini kabla hata sijajua kinachomsumbua!”

“Amesema ana tatizo gani?”

“Hajasema chochote, tumpeleke hospitalini kwanza, hayo mambo mengine tutajua baadaye!”

“Sawa!”

Hawakuwa na muda wa kupoteza, wakamwingiza Mariam kwenye gari na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Nusu saa baadaye tayari walishafika hospitalini na Mariam apelekwa katika chumba cha mapumziko kwanza kwa ajili ya kupewa huduma ya awali.

“Nini kimempata?” Daktari aliwauliza wazazi wa Mariam.

“Ameanguka ghafla!”

“Kabla ya hapo alikuwa anaumwa?”

“Kwakweli hatuna uhakika maana alitokea kwa mume wake asubuhi hii akiwa katika hali hii, inawezekana amegombana naye!”

“Mmejaribu kumtafuta kwenye simu?”

“Ndiyo, hapatikani.”

“Ok! Subirini kidogo nje, acha sisi tufanye kazi yetu!” Daktari yule akasema akiwatizama wenzake ambao walitingisha vichwa kumuunga mkono alichokizungumza.

Wazazi wa Mariam wakatoka nje na kuwaacha madaktari wakijaribu kuokoa maisha ya Mariam.

“Sijui atakuwa amepatwa na nini mwanetu jamani!” Mama Mariam akamwambia mume wake.

“Inawezekana kuna kitu wamekorofishana na mume wake, maana naona hata afya yake siyo nzuri kabisa.”

“Mungu amsaidie apate nafuu kwanza, tutazungumza naye baadaye!”

Waliendelea kuzungumza juu ya afya ya mtoto wao hadi saa moja baadaye, mmoja wa madaktari waliyekuwa wakimhudumia Mariam alipotoka nje.

“Anaendeleaje sasa?” Mama Mariam alikuwa wa kwanza kumuuliza daktari.

“Msijali, inabidi mkubaliane na matokeo, maana hatuwezi kubadili kitu kilichopo!” Daktari akasema kwa utulivu sana.

“Dokta sema tu, nini kimetokea?”

“Punguzeni wasiwasi kwanza, tulieni...”



mwenyewe...

Mwili wa mama yake na Mariam ghafla ulikuwa kama umemwagiwa maji ya baridi, alishahisi lazima mwanaye atakuwa amekubwa na matatizo makubwa sana, kitu pekee ambacho kilizunguka ubongoni mwake ilikuwa ni kiifo! Kwa vyovyote vile uso wa daktari yule ulisomeka kwamba taarifa zilizokuwa zikiwajia baadaye zilikuwa za msiba.

Machozi kama maji yalianza kutiririka ghafla machoni mwa mwanamke huyo ambaye uso wake ulishajaa makunyanzi. Machozi yake yalisbabisha hata baba yake na Mariam naye apatwe na wasiwasi mkubwa sana. Hisia za mwanaye alikuwa marehemu ziliutawala moyo wake kwa kasi ambayo hata yeye hakujua ilipotokea!

“Dokta kuna nini, mbona unatutisha?” Baba yake na Mariam akauliza akiwa na wasiwasi mwingi sana moyoni mwake.

“Sema tu, kama mwanangu amekufa, hakuna jambo jipya hapo na wala huna haja ya kujaribu kutuficha!”

“Hapana wazee wangu, hebu tulieni kwanza, hakuna jambo baya lililotokea, na kwa hakika tunahitaji sana msaada wenu katika tatizo hili!”

“Tatizo gani?”

“La binti yenu!”

“Sawa, kwani amekufa?”

“Hapana...Mariam ni mzima na kwa bahati nzuri ameshazinduka sasa, lakini kuna jambo limejitokeza ambalo ndilo lililosababisha nije kuwaona kwanza!”

“Ni nini dokta?” Mama Mariam alikuwa wa kwanza kuuliza kwa sauti iliyojaa wasiwasi mwingi sana.

Angalau sasa tabasamu la baba yake na Mariam sasa lilianza kuonekana, uso wenye makunyanzi ulianza kupotea taratibu na nuru kuanza kushamiri katika nyuso za wazee hawa ambao kwa hakika walikuwa na mapenzi mazito sana kwa mtoto wao.

“Enhee dokta, tatizo ni nini?”

“Binti yenu baada ya kuzinduka tu, ametaja jina la Tom, tena akipiga kelele akidai kwamba anamnyanyasa sana. Sasa sijui kama mnamfahamu huyo Tom!”

“Ndiyo tunamfahamu!”

“Ni nani?”

“Mumewe!”

“Ameachana naye?”

“Hapana, wanaishi pamoja ila leo asubuhi hii ndiyo amekuja nyumbani lakini kabla ya kuzungumza chochote tukashangaa amepoteza fahamu kwa inavyoonekana watakuwa wamekwaruzana kidogo!”

“Ok! Sasa hatua gani mmekwishachukua kama wazazi?”

“Kubwa ambalo kwetu sisi lilikuwa la maana zaidi ilikuwa ni kuhangaikia afya ya binti yetu kwanza, ingawa pia tumejaribu kumpigia mwenziye simu lakini hapatikani!” Baba yake na Mariam alisema.

“Ok! Poleni sana!”

“Tunashukuru, nini kinaendelea kwa muda huu?”

“Mariam itabidi abaki hapa hospitalini kwa siku tatu zaidi, tunahitaji kuwa naye karibu sana kwa kipindi hiki, anahitaji ushauri wa Kisaikolojia na baadaye tutawapa taratibu za kuzungumza naye kwa ukaribu zaidi ili kuweka haya mambo sawa!”

“Tunashukuru sana dokta, tunaweza kumuona?”

“Hakuna shida, lakini tunashauri msimuulize maswali magumu sana kwa kipindi hiki ambacho anaonekana kuwa na mawazo sana akilini mwake, msalimieni na mumpe pole tu, tafadhali msimuulize mambo magumu sana. Akili yake kwasasa inahitaji kupata wasaa wa kupumzika!”

“Hakuna tabu dokta!”

Dakika mbili baadaye wazazi wa Mariam walikuwa wameshaingia katika chumba kile ambapo walimkuta Mariam akiwa amelala juu ya kitanda, macho yake yakiwa yamejaa machozi.

“Mama....baba....” Mariam aliita akionekana kuwa na majonzi sana.

“Mwanangu, pole sana mama...utapona mama usijali!” Mama yake Mariam alisema akimwangalia mwanaye aliyekuwa ametulia kitandani.

Hakuwa na uwezo hata wa kukaa mwenyewe. Mariam alitia huruma sana, muda huo mama yake alipata nafasi ya kuweza kugundua kwamba Mariam alikwa amedhoofu sana, afya aliyokuwa nayo, haikuwa yake ya siku zote. Mariam alikuwa amepungua sana.

“Ahsante mama, lakinia alichonifanyia Tom kinauma sana mama yangu...nimevumilia lakini nimeshindwa!”
 
SEHEMU YA 33 YA 50

“Amekufanyia nini?” Baba yake Mariam akadakia.

“Tom ameamua kuwa na mwanamke mwingine sasa!”

“Umejuaje?”

“Anaishi naye pale nyumbani, mwanzoni alikuwa anafanya siri, lakini sasa ameweka kila kitu wazi, kaamua kuja naye nyumbani na ni muda mrefu sasa mimi nalala chumba cha wageni, Tom amebadilika, ananichukia sana sasa hivi!”

“Usijali mwanangu, kila kitu kinapangwa na Mungu, binadamu hatuwezi kupanga mambo mama, na hata kama tukipanga Mungu mwenyewe ndiye mwenye uwezo wa kubadilisha, kitu cha msingi kwako kwa sasa ni kutuliza akili yako na kumwachia Mungu kila kitu! Yeye ndiye atakayejua kitu cha kufanya, atakupigania na kukufanya huru tena, mkabidhi yeye kila kitu na maisha yako yatakuwa mapya mwanangu. Mungu ni kila kitu mama, asikudanganye mtu mwanangu!” Mama yake Mariam alihakikisha anamuweka sawa mwanaye ili aweze kukabiliana na tatizo alilokuwa nalo.

“Lakini mama, hamuwezi kuzungumza naye, nampenda sana Tom wangu mama, nampenda Tom, nitawezaje kuishi bila yeye?”

“Sawa, acha tujaribu kwanza, lakini nakusihi tuliza akili yako mama, afya yako imezorota sana mwanangu, kumbuka sisi wazazi wako tupo na tunakupenda sana, hatutaweza kukubali tukuache uteseke, sawa mama?” Mama Mariam alizungumza kwa sauti ya upole iliyojaa mapenzi mazito.

“Sawa mama, lakini lazima mjaribu kuzungumza na Tom kwanza!”

“Sawa, usijali!”

Baada ya hayo, wazazi wa Mariam wakatoka nje ya chumba kile na kuwaacha Madaktari wakiendelea kumtibu Mariam.

******

“Karibuni sana, sijui mnamuhitaji nani?” Ilikuwa sauti ya Mayasa ambayo ilitokea puani huku ikiwa na sifa zote za ushangingi.

“Mwenye nyumba!” Mama yake na Mariam akasema kwa sauti tulivu sana.

“Hivi nyie ni kina nani?”

“Siyo kazi yako binti, nahitaji kuonana na mwenye nyumba!” Mama Mariam akasisitiza.

“Unajua nawashangaa sana, haiwezekani nyie mkawa wageni wa hapa halafu mnashindwa kujua kuwa mimi ndiyo mama mwenye nyumba!” Mayasa akasema kwa nyodo za wazi kabisa.

Ilikuwa kauli kali ambayo ilimnyomnyong’onyesha sana mama Mariam na mumewe.

“Sikiliza binti, tunahitaji kuonana na Tom!” Baba Mariam akasema kwa sauti ya ukali.

“Oh! Tom, sasa mtaingia ndani au nimuite hapa nje?”

“Mwite huku nje, tutazungumza naye hapa hapa!”

“Nimwambie ni akina nani?”

“Wageni wake wa kibiashara!”

“Ok!” Mayasa akaondoka na muda mfupi baadaye, Tom akaja akiwa ameongozana na Mayasa.

“Mnataka nini kwangu?” Tom akauliza kwa ukali sana.

“Unasemaje?” Baba yake Mariam akauliza kwa sauti iliyojaa mshangao mkubwa.

“Kwani masikio yako umeweka pamba? Kwanza ondokeni kwangu, sina muda wa kupoteza kuzungumza na nyie, mnanipotezea muda wangu wa kustarehe na mpenzi wangu!”

“We’ Tom umechanganyikiwa? Hujui kuwa sisi ni wakwe zako? Tumekuletea taarifa muhimu, mwenzako amelazwa Muhimbili!”

“Mwenzangu ndiyo nani?”

“Mariam!”

“Mariam siyo mwenzagu, siwezi kuishi na mwanamke kama yeye, mwenzangu ni Mayasa! Huyu mnayemuona hapa ndiye mke wangu ambaye ninampenda kuliko kitu chochote katika maisha yangu, sihitaji kusikia habari nyingine tofauti na Mayasa wangu. Nawaomba mtoke kwangu!” Tom alisema maneno hayo huku akibamiza geti na kufunga kwa komeo.

Mama Mariam na mumewe wakabaki wanaangaliana, machozi machoni mwao ndiyo faraja pekee ambayo ingewasaidia kwa wakati huo. Wakaangaliana kwa uchungu, wakasogeleana kisha wakakumbatiana na kuanza kulia. Walishindwa kuelewa ni mkosi wa aina gani uliompata binti yao.

“Binti yetu wa pekee Mariam, kwanini anapatwa na balaa kubwa kiasi hiki, kwanini lakini?!” Baba yake na Mariam alisema huku machozi yakilowanisha shingo ya mkewe aliyekuwa amelala kifuani mwake.

“Lakini naamini siyo Tom, yupo aliye nyuma ya akili zake, ni shetani pekee ndiye anayemsumbua!”

“Mungu adhihirishe utukufu wake!”

“Amen!” Wakatoka kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono, wakalifuata gari lao, wakaingia na kuondoka taratibu. Msaada pekee uliobakia ulikuwa ni Mungu pekee.





Haikuwa rahisi kugundua kwamba kwa muda wote wa robo saa Dk. Joseph Kisanga aliuokuwa akiutumia kuzungumza na Mariam, alikuwa akizungumza mwenyewe! Dk. Kisanga alikuwa akizungumza kwa sauti ya taratibu, ukimya wa hali ya juu ukiwa umetawala na akihakikisha kwamba Mariama anarejea katika hali yake ya kawaida, lakini kumbe akili ya Mariam haikuwa pale!

Mapenzi yake kwa Tom ndiyo yaliyokuwa akilini mwake na siyo ushauri wa Dk. Kisanga ambao kwake ulikuwa sawa na porojo zisizo na maana yoyote. Kilikuwa chumba kimya, chenye mwanga hafifu, lakini kilichokuwa na hewa ya kutosha iliyozalishwa kwa mashine maalumu ya kisasa.

Mariam akiwa ameketi kwa mtindo wa kutazamana na Dk. Kisanga ambaye ni Mtaalamu wa Magonjwa ya Afya ya Akili na Mshauri wa Mambo ya Saikolojia na Maisha katika ofisi yake hii ambayo siku zote huwa ni tulivu sana akiwashauri watu wengi hasa waliokata tamaa. Ni Dk. Kisanga ndiye aliyemsaidia mzee Mallya, mfanyabiashara wa maarufu jijini Dar es Salaam, aliyetaka kujiua baada ya bohari lake la kuhifadhia mizigo muhimu kuungua na kumsababishia hasara ya mamilioni ya pesa!

Dk. Kisanga pia ndiye aliyemshauri msanii maarufu Bisongi ambaye aliathiriwa na dawa za kulevya lakini baada ya kuzungumza naye akimpa ushauri, akakubali kuacha na kubadilika kabisa! Naam. Dk. Kisanga ni mshauri maarufu ambaye amejizolea umaarufu mkubwa sana katika kutoa ushauri na kubadilisha maisha ya watu!

Hali ilikuwa tofauti sana kwa upande wa Mariam. Ilimchukua muda mrefu sana Dk. Kisanga kugundua kwamba muda wote huo alikuwa akizungumza peke yake.

“Mariam bila shaka tupo pamoja!” Dk. Kisanga akasema akimtizama Mariam usoni.

Mariam alikuwa kimya.

“Mariam...Mariam...we, Mariam...!” Dk. Kisanga akamwita kwa mara nyingine.

“Abee Dokta!”

“Mbona kama haupo hapa?”

“Tupo pamoja!”

“Unakumbuka nilizungumza nini mara ya mwisho?”

“Ndiyo!”

“Nilisemaje?”

“Ah! Dokta...nakuelewa vizuri sana!”

“Hapana lazima unisikilize vizuri Mariam, maisha yako yana thamani kubwa sana, hutakiwi kuyapa mapenzi kipaumbele zaidi kuliko maisha yako. Ni kweli mapenzi yana umuhimu mkubwa sana katika maisha yako lakini maisha yako yana thamani zaidi kuliko hayo mapenzi ambayo kwasasa yamekuwa tatizo kubwa kwako....” Dk. Kisanga aliendelea kumshauri Mariam kwa muda mrefu sana, akijitahidi kuzungumza naye kwa upole huku akihakikisha hali ya afya yake inarudi kuwa nzuri.

Mariam alionekana kumsikiliza Dk. Kisanga kwa makini sana, lakini kilichokuwa kikifanyika kilikuwa ni sawa na mchezo wa kuigiza, kwani alionekana kumsikiliza kwa umakini mkubwa lakini ndani ya moyo wake kulikuwa na kitu tofauti kabisa, moyoni mwa Mariam kulikuwa na maandishi makubwa yaliyosomeka; TOM! Ni yeye tu ndiye aliyekuwa wimbo moyoni mwake.

“Nimekuelewa Dk. Kisanga, nashukuru sana kwa kubadilisha maisha yangu, naamini sasa nimekuwa mpya na nitahakikisha natulia na kuishi maisha yangu bila matatizo wala kumuwaza Tom!” Mariam alisema kwa utulivu sana.

“Nimefurahi sana kusikia hivyo, amini kila kitu hupangwa na Mungu, hivyo ni wajibu kuhakikisha yeye anakuwa nguzo yako namba moja katika maisha yako. Nimefurahi sana Mariam, naona sasa unaweza kurudi nyumbani, hakikisha unafika hapa hospitalini kuonana na mimi kila mwezi hadi hali yako itakapokaa sawa.”

“Hakuna tabu Dokta, nashukuru sana!”

“Ahsante!”

Siku hiyo hiyo Mariam aliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa ameonekana kuwa na nafuu kubwa. Wazazi wake walifika hospitalini na kumchukua kwenda naye nyumbani. Walikuwa na matumaini makubwa sana ya mwanao kuwa mpya, walimwamini sana Dk. Kisanga kutokana na uwezo wake mkubwa wa kushauri.

“Vipi mama, unajisikiaje sasa?!” Mama yake na Mariam alimwuliza akiwa anatizama usoni.

“Nina nafuu sasa mama!”

“Kweli?”

“Ndiyo mama.”

“Kwahiyo unataka kutuambia kwamba, sasa hivi hali yako imetengemaa.” Baba yake akadakia.

Mariam hakuwa na jibu!

Alitulia kimya bila kuzungumza chochote, ni jambo lililowashtua sana, hawakutarajia kama mwanawo angekaa kimya kwa muda mrefu kiasi kile, hasa kutokana na ukweli kwamba alikuwa akionyesha ushirikiano wa kutosha kuanzia mwanzoni.

“Vipi mbona umenyamaza?”

“Kuna tatizo baba!”

“Tatizo? Tatizo gani tena, si umesema unaendelea vizuri mwanangu?”

“Baba bado mawazo juu ya Tom yananisumbua na kuna jambo ambalo ni bora kama ningelifanya ili kuepukana na haya matatizo.”

“Ni nini?”

“Nahitaji kuwa mbali na Dar es Salaam, mbali na Tom, mbali na Mayasa, mbali na Vyombo vya Habari. Sihitaji kusikia wala kujua chochote kinachohusiana na Tom, nimechoshwa na mambo yake, nataka kutulia sasa.” Mariam akasema huku akilia kwa uchungu.

“Mwanangu huwezi kuwakimbia watu na hata kama unaweza, utawakimbia hadi lini?” Mama yake akadakia.

“Naweza mama, inawezekana kabisa kuwakimbia, sina jinsi zaidi ya kuondoka hapa Dar es Salaam!”

“Uende wapi sasa, uende wapi mwanangu?” Baba yake akadakia.

“Nitakwenda kwa bibi!”

“Yupi?”

“Wa Morogoro, acha niende nikapumzike Matombo!”

“Lini?”

“Kesho!”

“Mbona haraka sana?”

“Kesho ni siku nzuri sana kwangu, acha nianze kujiandaa!”

******

Mapenzi ya Tom na Mayasa yalizidi kupamba moto, Tom akawa hashikiki wala hakamatiki, kila kitu ilikuwa ni Mayasa. Tayari alishamkabidhi kila kitu katika maisha yake. Siri zote za kibiashara alikuwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom