Simulizi: "Angamizo"

Simulizi: "Angamizo"

SIMULIZI: “ANGAMIZO” (23)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
--------------------------------------------------

“Naaaam!, japo sikufa na kuumia sana. Lakini nilizimia. Nilijikuta tu nipo sehemu ambayo kuna weupe weupe ule wa hospitali!. Nilipoteza tena kumbukumbu kwa mara ya pili. Jambo lingine la kumshukuru Mungu ni kuwa hakuna nilichokumbuka zaidi ya jina langu tu Rose!. Nilipozinduka hapakuwa na mtu yoyote sehemu hile.

Chumba kilikuwa vizuri lakini hakuna nilichokumbuka. Nilijichekea tu mwenyewe. Kwa hali niliyokuwa nayo nilipaswa kabisa kupitilizwa hospitali kuu ya taifa ya vichaa Dodoma inaitwa milembe sijui. Nilikuwa sijielewi.

ENDELEA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU…
Nilikaa hapo kitandani hadi alipofika mtu kwa cheo cha nesi. Alinijulia hali na kuniuliza maswali kadhaa ambayo majibu yake yalikuwa yanafanana.

“Sikumbuki chochote nesi!” ilo ndio jibu la kila swali nililoulizwa. Nilikuwa mkali haswa.

Uwezi amina Kaka, nilikumbuka jina langu tu Rose! Basi. Na kila nikijaribu kuwaza na kufikilia mimi ni nani kichwa kinaniuma tu!. Sijui nililogwa tena kwa mara ya tatu?.! Lakini nisiseme hivyo ni mipango ya Mungu.

Basi nilipotoka hospitali sikuwa na sehemu wala mwelekeo wa kwenda. Nilipitia vipindi vigumu vigumu kiasi kwamba kila kazi ya mbele ilikuwa yangu!. Nilikuwa msaidizi wa Mama ntile: Nikafukuzwa!, nilikuwa mfanya kazi wa ndani: Nikafukuzwa, nilikuwa muuza mboga mtaani: Nikaachishwa, nikarudi kuwa Msadizi wa Mama ntilie sehemu nyingine.

Huko ndipo nilipokutana na wewe Abdul, Abdul ambaye ni mpenzi wangu niliempenda sana. Abdul niliyekubali kumtunza na kumlea kwa miaka yote. Abdul ambaye niliangaika naye kutafuta mtoto na nikakosa. Abdul ambaye alikuwa mwamba wa kugundua vichochoro na njia za kutafuta pesa. Kumbe Abdul ni we-we, we!, Denis!

Kaka toka hapo hadi nakutana na wewe!, sikuwai kumbuka historia ya maisha yangu!, lakini naamini Damu!, Damu Kaka!. Damu ni nzito kuliko maji!.khaa!, umewezaje kunirudisha tena Utotoni kaka!. Nakumbuka sasa, nakumbuka hata mapigo ya moyo ya kipindi hiko tunasakwa na Baba Mchafu Frank!. Kumbe ndio huyu mbwa ambaye anatufuatilia kututokomeza kila siku! Bustard!..

Kaka ni mimi mdogo wako kabisa Maria!, ona!, ona kovu hili! Ona Kaka.!” Maria alinyanyuka pale alipo bila woga na kuanza kupandisha gauni lake refu kuonyesha kovu aliloongelea. Hakumaliza kulionesha lote akafunika na kufumba macho, akavuta hewa ndefu iliyopitia puani.. Kilio cha maneno machache kikafuata!.

“Oh!! Kaka kumbe huoni e?!. nijibu Kaka! Huoni?!” alifunika nguo yake na kulia bila mpangilio. Nilipoangaza kwa Abdul!, nae alikuwa ameshachanganya kabisa kulia.

Alihakikisha analia polepole ili kila aliyeko mahali pale asijue kama analia. Anafichaje sasa? Ficha moyo sio machozi!. Tulishaligundua hilo. Abdul ambaye ndiye Denis alikuwa anabwabwaja tu midomo kabla ya kusikika anachoongea. Mwishoni akatoa sauti.

“Ma….. Mari…… Maria! Maria eh!, Itika mdogo wangu!. Napaswa adhabu ya kushindwa kukutunza mdogo wangu. Nimekuaribia maisha yako!. Laana ya mwenyezi mungu hakika ipo mbele yangu. Katu siwezi tena kuwa mchafu!, Kama nilivyokuwa mwanzo. Nisamehe wewe Maria jamani.. nimela-la na we-we ki-ta-nda kimoja bila kutambua wewe ni mdogo wangu. Tena sio mara moja. Tumelala zaidi ya neno kulala. Eh!! Mungu ni nini hiki!. Hii si aibu jamani? Oh jamani!. Lakini… lakini mimi nimelala na Rose sio Maria!. Aaaaagh!!” Denisi alikuwa anahangaika tu. Walishikana mikono kwa kila mtu kumjulisha mwenzake hali ya moyo wake. Mimi na mke wangu ni miduwazo tu kila mda!. Mara tunalia mara tunashangaaa, mara tuna… da. Jamani Denis na Maria!, tumewakutanishaje??. Vichwa vyetu vilijaa alama za mshangao tu.

“Kaka!, tungejuaje sasa?, Naona macho ya kila mtu yakiwa karibu. Hakuna budi kuandika yote haya katika kitabu kimoja. Mwandishi usijali utatumia karatasi ngapi!, kikubwa we andika tu. Usifiche chochote. Nimeikimbia dhambi ya kujulisha uma kuwa nimethubutu kutoa maisha yangu kafara kwa nia ya kutetea watu wengine. Sijali ni malipo gani Mungu atanipa lakini hakuna namna hata kama akiamua kuchukua pumzi yake. Hakika tumekosea sana Kaka. Nashindwa nikutazame vipi!. Ivi wewe ni Mume wangu Abdul au Kaka yangu Denis?. Nimekubali kufa, hata kufa kwa kunyongwa lakini lazima nilipe kisasi kwa baradhuri Fred na ukoo wake!. Baada ya hapo kifo chema kitakuwa juu yangu. Ni ta po te a, nitapotea kaka!.” Alikuwa ni Rose mikononi mwa Abdul. Mtu na mke wake wa zamani. Mtu na dada yake wa sasa! Wanayoyaongea wanajua wenyewe..

********
Naaaaam!, hatukuwa tena na muda wa kupotea tokea hapo. Kilichobaki ni kutetea matumbo yetu yasiteketee kwa njaa. Niliwapanga wote Denis na Dada yake Maria kuwa wawe watulivu, suala lao lipo katika mchakato wangu.

Nikawaambia kuwa simulizi yao itakuwako katika kila haina ya chombo cha habari Tanzania, Afrika na Duniani kwa ujumla. Nikawaahidi kuwa wahusika wote waliosababisha maangamizo hayo watatiwa nguvuni, na si vyema kufuata sheria za bongo zao maharufu kama Sheria mkononi. Kwani Sheria ina pande zote mbili.

Sikusita kupata ujasiri wa kuwaahidi kuwa mali zote zitarudi mikononi mwao, kwa kuwa tayari Denis alishadokeza sehemu ambayo hati za mali za Baba yake zilikuwepo. Alisema.

“Kila kitu kipo kwa mwanashiria, alikuwa ni mwanasheria wa kijitegemea wa Baba. Kama baba alijua hivi, alimkabidhi kila kitu Mwanasheria huyo kwa kuhisi kabisa ipo siku mali zake zitaingia mikononi mwa wanajangili. Kama alitabiri hivi Mzee Yohana. Lakini sijui kama huyo Mwanasheria bado yupo hai au la!. Na kama yupo hai basi yupo nje ya nchi au amejificha sehemu za maficho. Bila shaka naye amepitia wakati mgumu kama sisi!.

Ndio mwandishi anaitwa Mwanasheria Credo Mwanuta!.!, Ndio, Ndio siwezi sahau jina lake kwa kuwa alikuwa rafiki yangu sana. Alikuwa ni mtani wangu kila tunapokutana. Ndio… Ndio…. ni Credo Mwanauta!.” Denis alitaja jina ambalo sio ngeni sana kwangu. Alikuwa ni Mwanasheria wa kujitegemea kwa kipindi hicho, aliwika sana miaka ya tisini kwa kuitambua vizuri sheria. Baada ya hapo. Akapotea!. Jina lake likasahaulika.

Nilianza harakati za kumtafuta kwa kutumia mitandao ya kijamii. Sikumtapa, kwani akaunti zake zote zilionesha zimefungwa mda mrefu sana. Siku hiyo niliitumia kumaliza kila kitu kinachohusu historia hii. Kumaliza hii simulizi ya vijana wawili ambao bila shaka dunia inapaswa kujifunza mengi kutoka kwao.

Kwa vile nilikuwa na ruhusa kazini na taaluma yangu iliruhusu kuingia kila sehemu, nilifanikiwa kukutana na muweka kumbukumbu na historia za wanasheria wilayani Ndugu Kharimu bin Mussa. Huko nikakutana na taarifa nusunusu tu kuwa mwanasheria huyo aliamia mkoa wa jirani wa Mtwara, kwa kujishughulisha na shughuli za kilimo cha korosho. Sio Mtwara hii unayoijua wewe!, ni Mtwara ndani ndani huko.

Nikachukua anuani zake na siku hiyo hiyo kupanda gari. Nilikuwa mimi mwenyewe binafsi na ushawishi wa kumfanya mzee huyo akubali wito wangu. Denis na dada yake niliwaacha na mke wangu nyumbani.

Ruhusa kutoka kazini haikuwa kikwazo kwangu. Ni kuomba tu na kupewa barua ya kuruhusiwa, si mambo ya kikazi bhana!. Na mimi ndio Baba lao!. Hivyo nikaenda Mtwara na kumtafuta huyo mzee ambaye alikuwa anawasimamia tu vijana wake kufanya kazi kwa jitihada, alikuwa ni mzee ambaye bila shaka alioga na kunywa chumvi nyingi sana. Nilifanikiwa kukutana naye na tukakaa kitako na kumpa dukuduku langu la kumuhitaji.

Hilo ndio tukio ambalo alikuwa analisubiri na kuliota kila siku!. Lini Denis atakuja kuchukua mizigo yake!!!. Sikupata shida kabisa katika kumwaminisha tayari alikuwa na hekima za uwelewa.

“Kijana, sheria imepinda sasa!, haijawa wima kama ilivyo mwanzo. Sasaa! Yaani ni bunda, chai, kahawa, na majani tu!. Pesa mbele, vifungu nyuma. Hakuna sheria kabisa sikuhizi!.” Alinidokeza Mzee Mwanauta ambaye alikuwa mwanasheria nguli kwa kipindi hiko.

Alikuwa akinipa fununu za kukengeuka kwa sheria kutoka zama za utu hadi zama za pesa!. Kila kitu ni mshiko tu!. Alinipasha yote wakati tupo kwenye gari kuja Songea. Hakuacha kunipasha pia kuhusu hamu yake ya kumuona mtoto wake Denis ambaye alisema pia alikabidhiwa na baba yake Denis Mzee Yohana kwani alimsimamia katika mafundisho ya dini yote, kuanzia kupokea Ubatizo wake.

Tulifika Songea na kumpeleka hadi sehemu ya tukio. Sehemu ambayo dhana ya nyumba ilitoweka kabisa na kubaki kuwa sehemu ya kupokea vilio na kukutanisha watu wasiojulikana.

Uzee wa Credo Mwanauta haukuwa kikwazo katika kutambua Denis ni yupi kati yetu. Aisee!, Mzee alilia. Alilia haswa!, alilia sio tu kutomuona Denis kwa kipindi kirefu hapana!. Bali ni afya tu ya Denis iliyopotelea sehemu isiyojulikana.

Ukubwa dawa!, hatukumnyamazisha, alitulia mwenyewe!. Alitumia busara sana. Hakuacha kumtazama Denis na kusikitika. Cha kushangaza akaongea neno ambalo lilifanya mapigo yangu ya moyo yabadili mwelekeo wake, yalipoteana kabisa yani. Eti nini!..

ITAENDELEA..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (24)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
--------------------------------------------------

Uzee wa Credo Mwanauta haukuwa kikwazo katika kutambua Denis ni yupi kati yetu. Aisee!, Mzee alilia. Alilia haswa!, alilia sio tu kutomuona Denis kwa kipindi kirefu hapana!. Bali ni afya tu ya Denis iliyopotelea sehemu isiyojulikana.

Ukubwa dawa!, hatukumnyamazisha, alitulia mwenyewe!. Alitumia busara sana. Hakuacha kumtazama Denis na kusikitika. Cha kushangaza akaongea neno ambalo lilifanya mapigo yangu ya moyo yabadili mwelekeo wake, yalipoteana kabisa yani. Eti nini!...

ENDELEA SEHEMU YA ISHILINI NA NNE…
“Nawe Maria!, unamwachaje kaka yako anapatwa na hali hii!?... Ni kweli baba yenu mwembamba sana lakini si kwa umbo kama hili. Denis umekufaa! Umekufa Denis Lo!.” Yaani, Mzee huyo alimtambua Maria bila hata kuonyeshwa. Hali ambayo ikatupa asilimia mia kabisa kuwa Damu ni nzito kuliko maji jamani. Mtu chake!. Aliwatambua bila tatizo lolote lile. Akatuacha hoi.

“Sasa wanangu, tunawezaje kulipa yote haya tuliyofanyiwa? Maana mtu anayetuumiza yupo karibu yetu!. Laiti angejua kama na mimi bado nipo hai. Basi msingepata bahati ya kuniona. Nilikimbia mapema mno na kustahafu.” Aliyasema hayo mara baada ya kupata tarifa na kisa cha wao kuwepo hapo. Tukaungana na kuwa timu ya watu watano.

Nikabeba majukumu ya kuwahudimia na kuwa mstari wa mbele kufungua kesi!. Sikujali sheria imepinda sijui, imefanyaje!. Niliamini katika ushawishi wangu wa maandishi unaweza kufanya Tanzania nzima kuwa upande wetu. Nilijiamini na kuwaambia kuwa hakuna muda wa kupoteza. Lazima kesi ifike mahakamani.

Kwa kuwa nilikuwa na mwanasheria mstaafu alinielekeza kila hatua za mwanzo na mwisho katika kuifikisha kesi hiyo mbali. Ilikuwa rahisi kwangu kujenga historia mpya ya Denis, Maria, Mke wangu, Mwanasheria na Mimi mwenyewe kuwa katika kumbukumbu za vichwa vingi vya wanadunia na hatimaye kutosahaulika kabisa duniani. Nilikua naamini kuwa ‘Wino unaishi!’.

Harakati za mafunguzi ya jarada la kesi namba 721 zikatimia. Kuhofia kupoteza mda, nilipeleka jarada hilo katika mahakama kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam. Kipindi hicho niliamua kusimama kazi kwa muda kuleta urahisi wa kufanikisha jambo hili kwa haraka zaidi.

Pesa zangu zote za miezi mitatu ya mwisho na pesa nyingine kutoka kwa Mwanasheria ndizo zilitumika katika kufanya safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Luhuwiko-Ruvuma kwenda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere! Dar es Salaam. Tulifika salama na kupata kila aina ya mahitaji.

Tulikuwa wote watano Denis na Dada yake Maria. Mimi na Mke wangu mtarajiwa bila kusahau Mwanasheria nguri mstaafu Credo Mwanauta. Tulihakikisha kila mtu anakuwa salama. Tulifikia hotelini nzuri tu ya kutosha kuhifadhi usalama wetu.
Sababu za kukata rufaa ya kuhamishia kesi hiyo ngazi ya Taifa ni kuwa, kwanza ukubwa wa kesi. Pili, usalama wetu. Tatu kukwepa vitendo ambavyo vingekwamisha mpango huo kama vile rushwa na fitina. Na nne ni kufuata sheria zote za aina ya kesi yetu. Kesi ilikuwa kubwa mno kiasi kwamba kila mwanachama wetu alikuwa na uchungu na Mshtakiwa.

Tuliitwa katika hatua za mwanzo kabisa kuwasilisha shutuma zetu juu ya mstakiwa. Denis alimaliza kila kitu. Punde tu washitakiwa Ndugu Fred Ephrehem na wenzake waliswekwa rumande, kutokana na muswada wa mwenasheria wetu wa kuwakata wakamatwe kwanza ili wasije kukimbia. Jambo la kumshukuru Mungu serikali ilikuwa upande wetu.

Serikali ikasimamisha kesi kesi kwa muda, walimpeleka kwanza Denis katika kufanyiwa uchunguzi kuhusu afya yake. Majibu yalionesha amepatwa na maradhi ya moyo. Lakini kitu cha kumshukuru Mungu ni hii ripoti ya kuwa macho ya Denis yanaweza kuona, kwani alipofolewa tu kwa kuwekwa kemikali mbaya na sio kuyaua kabisa.

Lakini mshauri kutoka kitengo cha macho alishauri kumpeleka Denis nje ya nchi kufanya matibabu, alisema Macho yake yamejawa na uchafu mwingi sana na wa kipindi kirefu. Hivyo alitupa barua ya kuomba michango kwa baadhi ya ofisi za serikali. Kwa jina la Baba Mungu wa Majeshi, kiasi kikubwa tu kilikusanywa.

Haikuwa kazi rahisi kuelekea China. Lakini sikupata bahati hiyo Mimi. Alienda Denis, Dada yake na kiongozi mmoja ambaye alikuwa kama msimamizi wetu. Walisafiri na kuelekea China kwa matibabu. Tuliobaki tukavuta subira na kushikilia imani zetu vizuri ili zisipotee katika kushuhudia Denis anaona.

Siku ya tano tu Denis alirudi Tanzania akiwa Denis kweli kweli!, kweli China sio mchezo!, alikuwa anaona hadi wale wadudu wadogo wanaoonekana vyema kwa kutumia lenzi au maikroskopu.

Denis alikuwa mzima kabisa. Hakuwa kipofu tena. Pumzi na uhai wa mwanzo ukarudi tena. Denis aliyekufa sasa akafufuka. Kazi wakapata wale mashororo waliomfanya mtoto wa watu bidhaa ya embe kwa kuibonyeza na kuuliza bei tu pasi na kununua!. Mbona waliisoma!.

Naaaaam! Tulipangiwa tarehe rasmi tarehe ya kusikilizwa kesi yetu juu ya Mstakiwa mwenye makosa zaidi ya Elfu moja. Kuua, kubaka, kumiliki siraha, kudhurumu mali, ukatili, unyanyasaji na mengine kedekede.
Denis na Dada yake walishikana mikono kumtokomeza Baba yao mdogo Frank!. Shaidi namba moja akiwa Mwanasheria kama mzazi wa kijitolea kwa wanandugu hao. Mimi na mke wangu tukafunga ukurasa wa mashidi wa tatu ambao waliona na kusadifu kwa maneno na matendo walipitia wanandugu hao. Watu waliipenda Mahakama jamani!!!!.
********

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (25)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
--------------------------------------------------

SEHEMU YA MWISHO
Mapema ya jumatatu asubuhi ya tarehe 21 mwezi wa Disemba, tayari palikucha. Ubaridi ukawa tulizo la mahakama nzima. Kumbi nzima ya Mahakama ilipendezeshwa na idadi kubwa ya watu wenye sura za uchungu na wenye sura za shauku kwa wote kusikiliza kesi hii ya Masikitiko ya hisia.
Labda nikuonjeshe tu kwa ufupi baadhi ya radha zilizopendezesha kumbi hiyo.

Tukianza na watazamaji au wasikilizaji wa kesi hiyo walikuwa na mwonekano tofauti tofauti huku wengi wakiwa na shauku ya kujua hukumu; walipendezeshwa na sura za huzuni kila wakimwona Mshitaki ambaye alipata shida kwa miaka zaidi ya therethini. Wote walikuwa na hasira na kesi hiyo. Kama kawaida nilikaa upande wa mashaidi dawati la mbele kabisa kama shaidi wa kesi hiyo. Katika dawati la washikati walipendeza sana Mtu na Dada yake ambao katu hakuonesha sura ya kucheka toka wakanyage mahakamani hapo.
Mstakiwa alikuwa amesimama kizimbani kujibu mashitaka zaidi ya elfu yanayomwandama. Wenzake waliopatikana walisimama nyuma yake.

Majaji wawili na mahakimu, wote walipendezeshwa na sare zao tukufu za mhakama kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Polisi nao hawakuwa mbali kuhakikisha watu wanaingia, wanatulia na kuondoka salama, walikuwa kulinda rahia na mali zao. Ukumbi mzima ulikuwa kimya sana.

Licha ya ukumbi mzima kujaa watu bila punje ya nafasi, waliokosa viti hawakutaka kukosa taarifa hizo. Walikuwa wamejazana nje ya mahakama na wengine majumbani mwao kusikiliza na kutazama kupitia vifaa vyao vya umeme. Mbali na watu hao wa dasilama pia wa mikoani nao walikuwa na masikio na macho!, kwanini wasione na kusikia jamani!!. Nchi ikawa kimya kwa muda. Ilitulia sana bila kupumua, Haikuhema siku hiyo. Vijana waligoma kabisa kufanya kazi hadi wasikie hukumu ya mwisho ya Majaji kuhusu kesi hiyo.

Naaam! Ukumbi mzima ulizizima mara baada ya Denis kumalizia mashitaka yake. Alitoa historia kwa ufupi sana kuweka bayana maovu ya Baba yake mdogo Frank; alitoa kwa urefu na kwa ufupi maisha aliyopitia hadi kufika hapo, alichagua vipengele vinavyoumiza tu!, alitoa mauvu yote hadharani, maovu ambayo yalikaziwa na Dada yake Maria. Maria hakuogopa kuacha kitu, aliongea bila kuacha, lakini ikafika hatua akamaliza. Waliolia walilia, waliosikitika walisikitika. Wamama walishikilia nguo zao mikononi kwa kukosa nguvu. Wenye moyo mweusi tayari walianza kunyanyuka kwenye nafasi zao kuelekea upande ambao mshitakiwa amesimama. Polisi walikuwa karibu kuhakikisha sheria inafuta mkondo.

Naaaam! baada ya ushahidi wa Mwanasheria Credo Mwanauta ambaye alithibisha kutokea kwa matukio hayo pamoja na mtuhumiwa kutekeleza maangamizo kadhaa dhidi yake hadi kupelekea Mwanasheria huyo kuhama makazi yake baada ya kustahafu.

Alikabidhi hati za Marehemu Mzee Yohana ndani ya mahakama. Hati zilizosainiwa majina harisi ya wamiliki za mali, ambaye ndio Mhusika mkuu wa kesi hii naye siye mwingine bali ni Denis Ephrehem kama Mrithi namba moja na Dada yake akifuata kama mrithi namba mbili;

Nikafuata mimi kama shaidi namba mbili. Na mimi sikuacha dukuduku langu, nilieleza mazingira ambayo nilikutana na Denis hadi kufikia mahari hapo. Sikuacha kitu. Mke wangu akawa wa mwisho. Naye alikazia maarifa yaleyale tuliyoyaanzisha sisi. Ikabaki kazi ya Majaji tu kufasiri vifungu vyao wakiongozwa na Katiba tukufu ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.

“Mshitakiwa, unalolote la kijitetea!” Jaji mkuu wa Jahmuhuri wa Muungano wa Tanzania Profesa Oscar Charles Kilongo aliinua makwapa yake ya kushoto kuelekea kwa mtuhumiwa.

“Ah!, Ndio!!. Ndio Mheshiwa Jaji. Nipo na neno la kusema kabla ya hukumu.” Aliishia hapo na kisha kuangalia umati uliopo mahari hapo. Alijua kabisa hana chake mahali pale. Alivuta pumzi na kurudisha macho kwa Jaji Mkuu. Katu hakuwaangalia watoto wake waliomshitaki yeye, alikuwa Denis na Dada yake Maria.

“Ka.. Katika mahakama yako hii tukufu, nakiri.. nakiri kufanya makosa hayo!..” Aliishia hapo na kuwa kimya kuruhusu minong’ono na maneno ambayo watu walianza kuporomosha. Ilikuwa ni tafaruku ya muda mfupi sana. Jaji akatoa tamko la kutulia na Mshitakiwa Frank akaendelea.

“Ndio!, ni mimi ndiye niliyesababisha mambo yote hayo. Nakumbuka mimi ndiye niliyepanga ajali ya Kaka yangu Mkubwa Mzee Yohana mkoani Morogoro kwa kuongea na dereva wake asababishe ajali na kisha yeye kutoweka, niliahaidi kumpa ujira na mlo mzuri na akafanya kweli. Hivyo tukampoteza mkubwa wa familia

Mheshimiwa mkuu, ni mimi niliyesababisha kubakwa na kuuwawa kwa Shemeji yangu, mke wa kaka ambaye ndiye Mama wa watoto hawa wa hapa!. Nakiri hilo mheshimiwa. Lakini pia nakili kosa la kusababisha vifo vya Denis na Mdogo wake Maria ambao nilitamani sana wafe!, wafe mapema maana nilijua wakiwa wazima yatakuja kutokea haya ambayo wengi leo wanashuhudia. Niliagiza watu wawatokomeze watoto hawa lakini walinigeuka na kuwaacha hai, wakaja kunipa taarifa kuwa wamewatokomeza tayari, kwa maana sitawaona tena katika mboni zangu. Lakini Hapana. Sura hizi nizionazo leo hii mbele yangu ndio zilezile. Hakuna kilichobadilika. Huyu ni Denis na yule na Mdogo wake Maria!, sikuwahi kuwaona watoto hawa tokea walivyo wadogo, ndio nakuja kuwaona tena leo hii. Cheki walivyo, hawajapotea kabisa na sura ya Mama yao.

Nikaja sikia eti bado Denis anaishi na ni kipofu, nilipatwa na hasira sana, hivyo nikaendelea tena harakati za kuwaangamiza.” Fank aliongea kwa hisia na wakati huu aliwatazama watoto wake wa ukoo. Hakuwa na aibu hata kidogo japo uzee ndio kwanza ulianza kumkaribisha.

“Mkuu, nakili kumiliki siraha na makundi ya kiharifu kama mashitaka yanavyodai. Siwezi kupinga hata moja. Yote! Yote yangu Mheshimiwa. Hata mali zo-ote zote nilizonazo si halali yangu kuwa nazo, ni mali za hawa watoto. Ndio maana kulijua hilo nikaamua kuwaangamiza” alipomaliza maneno hayo Frank alionekana dhairi kuwa chozi linamtoka. Alikuwa mnafiki. Alilia bila sababu lakini hakuna aliyemwona mwema kwa wakati huo.

“Mkuu, napenda kutoa rahi kwa watu wote duniani. Mali sio kitu kabisa!. Tamaa sio kitu kabisa!, Ukatili sio kitu kabisa kwani vyote ukivifanya kwa ubaya basi vinakurudia kwa ubaya. Nilipenda mali ambazo hazikuwa jasho langu. Zimenipelekesha sana, zilinipelekesha mno... Hadi kutulia na mali hizo ni msaada tu kutoka kwa mganga mmoja huko Ludewa. Tamaduni za koo yangu pia zimenipoteza. Zimenidanganya mimi ndiye mrithi wa Mali za kaka yangu.

Hivyo nasubiri hukumu yangu!, nimeipokea kwa mikono mawili…. Na, labda tu niwaombe msamaha watanzania wote. Nisamehe, Denis, Nisamehe Maria: Nisamehe Mahakama na taifa kwa ujumla.” Frank alimaliza na kuweka uso wake chini kuashilia hana neno tena.

Minong’ono ikaanza tena kwa kila mtu kupendekeza adhabu ambayo angepaswa kumpa mstakiwa. Wengine waliwaza kumpiga risasi mia tatu na kuhakikisha amekufa, wengine waliwaza kuwa wangemtupa kwenye Mamba wakubwa wamle na kuishia huko. Wengine walisadiki kutabiri kuwa mahakama itamwachia huru ili wananchi wampige hadi kufa. Lakini haikuwa hivyo.

Jaji alimwangalia mtuhumiwa kwa sekunde kadhaa. Akatikisa kichwa na kuyarudia tena makaratasi yake. Aliyasoma mara mbilimbili kwa ukimya bila sauti. Akainua kichwa juu na kuweka kalamu yake mdomoni. Akaitoa na kurudia tea kusoma maelezo yake. Alipoyamaliza akayanyanyua makaratasi yake na kuzigonga-gonga mezani.. Jaji Mkuu akawasiliana na Jaji msaidizi kwa sekunde kadhaa, na kurudia kipaza sauti. Waliokuwa wakinong’ona wakanyamaza.

“Bila kupoteza mda. Ushaidi wa pande zote mbili yaani upande wa mshitaki na mshitakiwa umewasilishwa vyema. Na mshikiwa amekubali makosa yake kwa asilia mia moja. Leo tarehe 21/12/2019 mahakama hii tukufu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inamuhukumu Ndugu Fred Ephrehem kunyongwa hadi kufa. Adhabu hiyo itatelekezwa kesho asubuhi ya tarehe 22/12/2019. Mwisho wa kesi!, jarada limefungwa!.”. Jaji akagonga meza yake kwa nyundo hiyo kuashilia mambo yamekwisha. Kila mja wa eneo hilo alikuwa na furaha ya aina yake. Denis na Dada yake wakakumbatiana, vilevile mimi, mke wangu na mwanasheria tulipokezana tu kutabasamu, hakika haki imefuatwa. Alistahili.

Basi habari hile ikawa sherehe kwa taifa. Kila mtu akamjua Denis kila mtu akamjua Maria. Kila mtu alimjua Frank. Kila mtu aliijua sheria. Taifa likajawa na furaha. Miti iliyokunyamana ikaimarika kwa kuchomoza majani mapya ya upando, na ikawa na ahadi ya kuishi milele….
----------------

Historia ya Frank haikuishia kunyongwa kamailivyoamuliwa na mahakama. Frank alijifyatulia mwenyewe risasi ya kichwa nje tu ya mahakama. Alipata nafasi hiyo mara baada ya kusongwa songwa na maaskari wengi kumpeleka sehemu ya kuhifadhiwa kusubiri kunyongwa hadi kufa. Japo alikuwa na pingu mikononi lakini aliweza kujanjaruka. Kweli jambazi ni jamabazi tu!. historia yake ikaishia hapo.
****

Denis alikabidhiwa kila kitu cha Baba yake. Zilikuwa ni nyumba sita, na makampuni ya biashara kumi na nane, magari na vikorokoro vingine vyote vikawa mikononi mwa Denis na Dada yake Maria.

Simanzi iliyoje ni mwisho wa maisha wa mdogo wa Denis, Maria. Maria alipoteza maisha mwezi mmoja tu baada ya hukumu ya Baba yake mdogo. Taarifa za kuthibisha kifo chake na sababu za kifo zilikuwako katika ujumbe wake wa maandishi aliouandika kabla ajafariki.

“Kaka na wengine mnaosoma ujumbe wangu!, nimejiuwa kutokana na aibu ambayo inaendelea kunisuta moyoni mwangu. Nilibakwa na kufanya na mapenzi na wanaume tofauti. Nilipoteza utu wangu. Ilo sio tatizo, tatizo ni kulala kitanda kimoja na kaka yangu wa Damu. Nisamehe Denis, nisamehe Dunia. Nashindwa ficha aibu yangu. Nawatakia maisha mema.”
Huo ulikuwa ni ujumbe wa Maria aliouandika kabla mauti hayajamchukua. Lilikuwa ni pigo zito sana kwetu hasa kwa upande Denis lakini hakuwa na la kufanya. Likabaki kovu tu. Kovu lisilofutika. Maria alikuwa kovu.

Baada ya muda Denis aliamua kunitunuku kampuni moja ambayo ilikuwa inahusiana na masuara ya uandishi na uchapishaji wa magazeti. Ilikuwa jijini Dar es Salaam na toka hapo nikwa mwenyeji Dar es Salaam. Mimi mke wangu na Denis tukawa ndugu sasa. Hata Mwanasheria wetu nguri mstaafu akawa huru kuishi popote alipopataka. Bado alikuwa karibu yetu.
************

Kitu kilichonipa tuzo ya mwanafasihi wa kimataifa ni hii kazi ya ANGAMIZO. Kazi ambayo niliamua kuichapisha katika magazeti kama mwendelezo wa simulizi ya maisha ya Denis. Nilitengeneza kitabu ambacho kiliweza kusomwa na watu wa kila lika na kusambaa nchi nzima.
Nilipata nafasi ya kupeleka Kitabu cha ANGAMIZO mataifa ya karibu na mbali na Tanzania. Denis aliyasafisha maisha yangu na kukamilisha ndoto zangu. Nilikuwa mwandishi BORA wa kimataifa wa Fasihi.
--------
Naweka nukta yangu kwa kuwashukuru sana ndugu wasikiliazi na wasomaji wa mkasa huu. Yaliyomema ni ya kujifunza na yasiyo mema ni ya kuchomwa. Tulianza mwanzo pamoja na sasa kuhitimisha pamoja.

“Hakika ANGAMIZO ni ANGAMIZO tu; WALIANGAMIZANA”

*******MWISHO******

Simulizi inasikitisha sana... inahuzunisha na kutia simanzi...

Chapter closed...

Cc: mahondaw
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom