Xav Emmanuel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2018
- 215
- 316
- Thread starter
- #21
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (06)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: Xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
Social Net: @star_xav
Baba alikuwa mtu mkubwa amabaye, hata akiomba sehemu awe kiongozi basi wapinzani wote wanarudi nyuma kwa kuogopa ushindani; pesa zilitupa kiburi mno. Nadhani huu ndio mshahara wa dhambi zetu, umenitesa sana Baba!, umemtesa Mama, Umemtesa Maria, Umenitesa mimi na kizazi chako kijacho!, ziko wapi pesa zako Baba!!”. Abdul aliishia hapo na kuanza tena kulia, kilio chake hakikuwa cha sauti, nyumba yote ilikuwa kimya sana.
Mke wangu alikuwa ameduwaa kwa utamu na uchachu wa machungu wa maneno alikuwa anautoa Abdul, Abdul alikuwa fundi wa lugha kweli kweli, kwa hatua hii hakuna asiyeamini kuwa mtaa ulimfunza. Baada ya kufuta chozi mwanaume akaendelea…
ENDELEA SEHEMU YA SITA…
“Mwandishi, si unajuwa kuwa Akipangacho Mungu, binadamu katu hawezi pangua?. Usiangaike kujibu, ni kweli kabisa Mwandishi, Mungu alipanga na ikatokea.
Ilikuwa siku ya jumapili ya mwaka 2000 Jioni ya saa kumi na mbili kasoro, Nilikuwa nyuma ya kochi alilokaa Mama akiwa anaangalia televisheni ya Taifa, ulikuwa muda wa taarifa ya habari. Mimi nilikuwa naendelea kujisomea na kujiandaa na mambo yangu ya kishule kwani ndio ulikuwa mwaka wangu wa mwisho kumaliza elimu yangu ya msingi.
Lakini ghafla nilisikia kishindo cha ghafla nyuma yangu kama kitu kizito kimeanguka. Haraka nikakimbilia eneo ambalo kishindo kimesikika. Nilimwona Mama yangu mzazi akiwa chini, nilipigwa na bumbuwazi la maana kwa kushitushwa na hali hiyo. Nilianza kumwita kwa kumwamsha nikitumia sauti kubwa huku mikono yangu ikikazana kumtikisa nimwamshe. Katika kuangaza angaza nilikumbana na mwisho wa taarifa ya habari kutoka runingani. Nikatulia tuli kuimalizia..
“...Afisa wa polisi mkoa wa Morogoro amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo mnamo majira ya saa kumi na mbili jioni. Afisa ametoa angalizo kwa madereva ya magari binafsi kufuata taratibu na sheria za barabarani kuepusha ajali kama hizo. Roho ya marehemu Mzee Yohana Ephrehem ilazwe mahali pema peponi… Amina” Mwisho wa habari hiyo iliandamana na baadhi ya picha za gari lililochakaa kwa kujimega upande mmoja wa mbele, wahudumu wa kwanza wakifunika maiti na kupakia katika mifuko maalum ya kuhifadhia, kisha kuweka katika gari tayari kwa kuutoa mahali pale..
Picha ambazo zilionekana runingani ni picha ya ajali ya gari. Gari la Baba! Nilishituka na mikono yote kujikuta ipo juu ya kichwa changu kwa sekunde tu.. nikaja kujuwa kuwa Mama amepoteza fahamu kutokana na mshituko wa taarifa hiyo.
Nikapiga ukunga wa maana uliomwamsha hadi mdogo wangu usingizini, tuliungana kujitahidi kumwamsha Mama lakini mdogo wangu hakujua sababu na chanzo cha mama kupoteza fahamu. Sikuweza kumwambia. Mikono na sauti vilikazana kumwamsha Mama; ila akili ilikuwa mkoa wa morogoro kwenye maiti ya Baba. Tulishaachwa na kiongozi wa familia tayari.
Hakuna jilani yeyote aliyesikia kilio chetu. Hata kama wangesikia ni dhairi kuwa hakuna hata mmoja ambaye angethubutu kukanyaga kwetu. Hatukuwa na ushirikiano mzuri na majirani wenzetu, kwani tulijua pesa ndio kila kitu.
Tulilalama mimi na mdogo wangu hadi mashangazi wa karibu walipofika mkuku baada ya kupata habari kupitia televisheni zao makwao. Walitutoa pale na kutupeleka chumbani na wao wakaendelea na taratibu za kumpa Mama huduma ya kwanza. Kutokana na kushindwa vumilia hali nilikuwanayo nilianza kugombana na mtu ambaye tulikabidhiwa chumbani humo ili awe mwangalifu kwetu, nilikuwa mbishi kwa kutaka kumwona Mama yangu yu katika hali salama.
Ubishi wangu ulipelekea kumshinda nguvu mwanamama yule wa rika, nilimtoka mikononi mwake na kupitiliza moja kwa moja katika mlango wa kutokea chumbani humo. Sikufika mbali hata, nilipiga mweleka wa nguvu katika marumaru ambazo kila siku tulimsifia fundi kuwa katumia kipaji chake kwa kuzinakshi vyema.
Siku hiyo zilinisaliti, nilianguka kama jiwe na kupoteza fahamu hapohapo…” Ndugu Mwandishi. Nakupa onyo! Katu usilingie mali! Mali si kitu kwa kweli, ona sasa. Hadi marumaru nilizozizoea kuchezea na kukimbia nazo kila siku niendapo shule zimenisaliti kwa kunizimisha kabisa. Nilizimia mimi mwandishi…
ITAENDELEA…
Sent using Jamii Forums mobile app

Banadamu