Simulizi: "Angamizo"

Simulizi: "Angamizo"

SIMULIZI: “ANGAMIZO” (16)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
---------------------------------------------------------

“We Boya unaulizwa umetumwa!” Mwingine akapaza sauti. Wote walikuwa wanamaumbo kama yangu. Inaonekana ni watoto tu wa mtaani waliokosa kila aina ya malezi kutoka kwa walezi wao.

Naam nikaona kabisa nisipokuwa ngangari basi naweza poteza malinda sehemu ile. Wanaweza kunionea, na kwa jinsi nilivyo mayai wanaweza hata kunibaka. Kwa maana sikuwa na salio lolote mfukoni ambalo litawavutia. Nikagangamara kama na mimi ni mtoto mwenzao wa mtaani. Nikawapa soga za kiteja teja kukurupuka mikoni mwao. Nilijua nimeshaingia choo cha kike… nikaanza kujitahidi kuigiza.

ENDELEA SEHEMU YA KUMI NA SITA…

“Oyi!, wadau, mbona njema tu..” nilijikakamua na lafudhi ya kwenye video.

“Mbona unaibuka ibuka tu bila taarifa, Au Majani yameanza changanya kwa Head!” Mwinmgine alidakia na kuwaona kabisa wameanza kuniamini.

“Ile ile ile ilee! Hahahahaha. Mi mwana tu wakali. Sema nini. Yangu imezima. Nataka bust tu mimi!” Nilisema kwa kujiamini sasa!.

“Unataka bust!. Unataka bust wakati hujavua hata nguo. Saula chapu hapo!. Hakuna cha bure mtaa hu” Mwingine aliyeshika simu ambayo inamulika tochi alidakia maongozi na alianza kinisogelea. Bado nilikuwa natafuta mbinu za kutoka sehemu hile. Nikaja kukumbuka nina kitu ambacho kitaniacha huru sehemu hile.

“Oi Mkali eh!, nina kitu cha moto hapa. Kipyaa. Bei kama bure. Ukipita tano tano mara mbili mbili inakuja kumi bila kukosa hapo”. Nilijitega kwamba nina kitu kitakacho wafaa.

“Huyu mwana mpelelezi nini maze” Mwingine ambaye alilowa zege la madawa ya kulevya alinikata kauli. Kauli ambayo ilimfunua kila mtu pale.

“kitu cha moto!” Walibaki kurudia lile neno.

Sikuchukua dakika mbili mtama wa ajabu ukafuata . kwa sababu ya kiza sikujua hata ni nani aliyenizunguka kwa muda hule. Nikajikuta nipo katikati. Nilikuwa tu nahofu usije dada yangu Maria akawa ameona tukio lile na kujisogeza maeneo yale. Ingekuwa hatari zaidi.

Niliamliwa kipiga magoti na kuinua mikono juu. Tayari panga na vifaa vingine kama visu vilianza kumulika kwa kumelemeta na giza lile. Bado yule aliyeshika tochi aliendelea kunimulika usoni, mtaa wote ukakaa kimya kinitazama.

“Aka kanatupotezea time wazee!, tukafanyaje?” Mmoja akatoa wazo la ghafla kwa kuuliza.

“Hebu mpitie huyo” sauti kutoka nyuma ya mwaga wasimu hile ikasikika. Ilikuwa ni sauti ya makwaruzo.

Nilibaki kukimbizana tu na mapigo ya moyo wangu, huku mapigo ya moyo yakinitangulia futi nne mbele. Nilikuwa nahema tu. Nikawa natafakari huko kupitiwa kuna maana gani!. Nikabaki tu kutumbua mimacho kama pima.

Mmoja ya wale mwenye panga lenye asili ya ubutu akanisogelea na kuanza kinisachi mifukoni. Alinisachi bila kutumia utaratibu maalumu. Hakukuta kitu. Akaniambia nisimame na nivue suruali huku wakitafakari ni wapi chombo cha moto kimewekwa. Kumbe nao walitaka wahakikishe.

Mapigo ya moyo yakasimama ghafla hasa bastora ilipoanguka mara baada kufungua tu zipu ya suruali. Niliona wote wanarudi nyuma nyuma kwa woga. Hawakuamini kama kijana kama mimi naweza miliki kitu kama kile. Nikapata ujasiri wa kufunga zipu yangu na kuokota bastora hiyo. Nikajua tayari wamepata hofu ikawa sehemu yangu ya kuwaonea.

“Wadau mbona mzuka tu!, mi kavu tu sema nini!!. Napitisha hii. Buku teni tu naacha mzigo theni nachomoka tu kwa amaniii kiroho safi ama nini”. Nilijichetua kuongea huku nikikagua bastora hiyo iliyokuwa ikiniwazisha mbali sana.

Ni chombo kilichotoa uhai wa mama na wengine ambao sijawai kuwashuhudia. Bado mmoja yule aliendelea kunimulika na kwa sasa wakakusanyika pande moja wote wa tano. Hakuna aliyetoa neno.

“Oya wakali najee!, Changamka basi miyayusho wazee!” Nilikuwa na ujasiri wa aina yake mara baada ya kuona kuwa hata hao nilikuwa nao ni lika yangu na bado walikuwa wageni katika kufanya matukio yatokanayo na siraha ya moto.

Baada ya kauli hiyo waka kaa sawa na kuanza kushuka bei. Maana walijua kabisa kinachofuata pale ni kuwaangusha kama mahindi mmoja baada ya mwingine. Walijichanga na ikafika hadi elfu nane. Wakanipatia. Na mimi nikatoa risasi zote kwenye bastora hiyo na kuwapatia. Sikutaka tena zibaki risasi mule hili iwadhuru wengine wasio na hatia. Zilibaki risasi tatu tu ambazo zote nilizitoa na kuwapa kopo hilo.

Nilijua kabisa litawasaidia kutishia nyau mjini kujiingizia pesa kwa utapeli. Tena watapata nyingi zaidi ya elfu nane wakikaza mwendo. Nikawa salama kutoka sehemu hile maana nilishajionyesha kuwa mimi sio mtu wa mchezo mchezo. Nikazimega hatua kutoka sehemu hile kuelekea alipo jificha dada yangu. Waliendelea kunimulika na tochi hadi natoweka eneo hilo.

Punde nilisikia kelele za mbio nao wakitoweka eneo hilo kuepusha msala. Sikuwa na muda nao tena, nikashukuru Mungu bado dada yangu alikuwa sehemu salama niliyomuacha.

“Umechelewa Kaka!” Maria alionyesha wasiwasi kidogo nilipojitokeza kwake, sikuwa na neno. Ilikuwa ni shughuli ya kiume. Nikatabasamu tabasamu zito ambalo halikuonekana na giza lile. Mwanaume nilitoka kutafuta pesa. Basi tukatoka pale na kutafuta sehemu ambayo tunaweza kulala. Muda ulikuwa umeshaenda.

Kama kawaida tulijisogeza sehemu ambayo kulikuwa hakuna binadamu wa kutubughudhi mlalo wetu. Labda wadudu watokanao na maji machafu na jaa linalotoa harufu lilipo maeneo jilani na pale ambapo tulikubadiliana tulale na mdogo wangu. Kabla ya kulala tukapitia mzigo wetu wa ukoko na kufanya matumbo yetu yaundwe tena kama mpira wa miguu wa makaratasi.

Ukimya wa mda mfupi baada ya kumaliza kula ulianza kuongea na dada yangu na kumkumbusha matukio ya siku nzima. Hakutaka kuonja radha ile ya kilio peke yake, akanishilikisha kwa kuongeza sauti. Alikuwa analia Maria. Alilia sana na kufanya na mimi niangushe chozi. Hatukuwa na la kufanya zaidi ya kuzidisha sala kwa mwenyezi Mungu na kupunguza lawama ambazo litabaki kuwa mzigo tu kwa Muumba wetu. Kwani alipangalo Mungu hakuna wa kupangua.

Nilimpagata mdogo wangu aliyekuwa analia huku anatetemeka. Nilizidi kumwonesha nipo karibu naye kwa kumshawishi kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Aniamini mimi kaka yake kwani Mama alishanikabidhi kabla hajapatwa na mauti. Nilimpa moyo wangu wa ziada huku nikiendelea kuwafukuza mbu wale waenezao magonjwa sugu mwilini mwetu.

Tuliweza kuvumilia hata ile harufu kali ya maji machafu yaliyoganda kama sanamu la Baba wa taifa makumbusho.. Kilio cha Maria kikapungua sauti na mwisho kukata kabisa. Ghafla kimya kikatanda tena. Giza likawa giza tena. Usiku ukawa usiku wa manene. Niligundua hali hiyo mara nilijikuta nipo ndotoni………

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (17)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
---------------------------------------------------------

Nilimpagata mdogo wangu aliyekuwa analia huku anatetemeka. Nilizidi kumwonesha nipo karibu naye kwa kumshawishi kuwa kila kitu kitakuwa sawa. Aniamini mimi kaka yake kwani Mama alishanikabidhi kabla hajapatwa na mauti. Nilimpa moyo wangu wa ziada huku nikiendelea kuwafukuza mbu wale waenezao magonjwa sugu mwilini mwetu.

Tuliweza kuvumilia hata ile harufu kali ya maji machafu yaliyoganda kama sanamu la Baba wa taifa makumbusho.. Kilio cha Maria kikapungua sauti na mwisho kukata kabisa. Ghafla kimya kikatanda tena. Giza likawa giza tena. Usiku ukawa usiku wa manene. Niligundua hali hiyo mara tu nilijikuta nipo ndotoni………

ENDELEA SEHEMU YA KUMI NA SABA…

Ndugu mwandishi, ndoto niliyoiota siku hiyo ilikuwa ni ndoto njema sana. Kwa macho yangu nilijiona nimekuwa. Nimekuwa mtu mzima sasa. Nimekomelea suti kali amabayo sizani kama kuna fundi wa kibantu anayo matilio ya namna ile. Hilo la maisha mazuri halikunifurahisha sana zaidi ya ili ninalo taka kusimulia saizi. Ndoto ile ya raha nilitamani iendelee bila kukata. Huwezi amini ndugu mwandishi. Labda ibaki ndoto na simulizi tu kama navyokusimulia.

Niliota kitu ambacho kipo moyoni. Niliota kitu mabacho kilibaki moyoni. Nikiwa na suti yangu nadhifu ya rangi ya udongo. Tai yangu yenye vipepeo kama mfakazi wa kampuni ya usafirishaji wa vipepeo duniani. Niliota nimempiga risasi ya kichwa baba mdogo. Nilimpiga risasi tatu kichwani na kumwangusha chini. Na nikapata amani ambayo niliitafuta kwa miaka mingi sana..

Ndugu mwandishi ndoto hii natamani itimie hata leo. Na natumaini itatimia. Japo imani ya mwanzo imeanza kupungua mara baada ya kuona ugumu wa mbeleni. Lakini. Lakini.. lakini ndugu mwandishi!. We acha tu. Bora ilibaki kuwa ndoto tu maana hata baada ya kuisha ndoto ile, niliendelea na maisha yangu yaleyale tu, ahsubui yake bado maisha ya taabu yakaendelea.”

Abdul akuacha kuvuta pumzi ndefu na kushushia maji kidogo kabla ya kuendelea. Aliendelea Abdul wala hakujali macho yetu yaliyosikitishwa na simulizi yake.….
---------------

Ndugu Mwandishi, licha ya kulala kwa tabu toka kuzaliwa kwetu, hatimaye asubuhi mpya ilituamsha. Hatukuwa na budi kukurupuka mida hile ya ubaridi. Bado mwanga wa asubuhi haukuwa mbali na eneo tulipo. Uso mzima ulivimba mno kwa makakatau ya mate na alama za maboksi tuliyolalia. Mdogo wangu alivimba mno kutokana na mbu wengi wa eneo hilo. Waligeuza miili yetu kuwa bucha la bure. Walitupigia kelele na kuchukua damu zetu bila ruhusa: hiyo ilikuwa kazi yao ya usiku.

Baada ya kuhakikisha tupo salama kila mmoja. Safari nyingine ya bila kujua wapi tunaenda ikafuata. Tulikuwa kama mazombi tu tukisongamana huku na kule. Tumeshikana mikono na mdogo wangu tukivuka mitaro ya maji machafu kuelekea barabara kuu.

Ndugu mwandishi!, huwezi amini miaka yangu yote kumi na minne sikupata kujua vizuri sehemu ambayo naishi. Hatukuwa na tamaduni ya kuujua mtaa. Sehemu ambazo nilikua nazijua mimi ni nje ya miji labda. Niambie sehemu kama Selou, Ngorongoro hivi naweza juwa. Ila mtaa wangu sijui kona wala chochoro. Hivyo tulikua tunaenda tu. Tena tunaenda pasipo juwa nini hatma ya maisha yetu.
***
Miguu ilishaanza pokea vizuri michomo ya lami ambayo imetandazwa barabara hiyo. Tulikua tukifuata tu lami. Mdogo wangu akijigongagonga karibu na bega langu la kulia. Mkono wangu wa kulia ukizunguka shingo yake na kutua katika kikonyo cha mkono na bega lake la kulia. Taratibu tunalisongesha sebene la bila mdundo katika lami iliyonyooka. Barabara yote ilikuwa kimya kutuonea aibu na kutushangaa wageni sisi ambao hatukuwa hata na kelele wala barua za taarifa kwamba tunapita.

Ni mawazo tu ambayo yalikuwa rafiki wa wote, kila mtu alikuwa mbali sana kimawazo. Mimi kila nikikumbuka maisha ya mbele bado ya nyuma yananirudisha. Picha ya Baba Mdogo iligoma kabisa kutoka kichwani kwangu. Roho ya kisasi ikanijia kwa kasi. Nikajikuta nasimama.

“Kaka...” Niliitwa na mdogo wangu lakini sikusikia. Bado nilisimama.

“Kaka, Kakaa..” Aliniita tena na nikashituka. Nikamwangalia bila kuitika wito wake na kuendelea kutembea.

“Tunaenda hadi wapi?” Lilikuwa ni swali ambalo liliniingia vyema kabisa katika ngoma zangu za masikio, lakini sikuwa na jibu la mapema la kujibu. Nikakausha. Kukaa kwangu kimya hakukuwa chochote kile kwa mdogo wangu Maria. Hakuuliza tena. Akasimama na kugoma kwenda mbele kuendelea na safari.

Nikaona amejawa na hasira kama kifuu ambacho kinatumika kuwashia moto. Nikamsogelea na kumfikia karibu. Nikapiga goti moja na kumfuta chozi ambalo lilianza kumpokonyoka.

“Mdogo wangu Maria. Maria Mama!, Si unajua tumetoka kwa shari?...” Nilimgusia kidogo maneno ya hekima na kumjenga kiakili. Nikaendelea.

“Naaam… Nina imani kabisa Baba Mdogo hawezi kutuacha wazima. Hawezi kabisa Maria!. Naamini anatutafuta atumalize, kwa maana anahitaji awe huru katika kumiliki mali za Baba. Ona Maria, Mama yupo wapi?, eh!. Baba naye?... yote ni mipango ya Baba Mdogo Frank. Kinachotakiwa ni kusonga tu mbele kwa sasa. Lazima atutafute sisi Maria hawezi miliki mali za Baba kwa kutumia tamaduni zao. Hajui!!, hajui wapi hata Hati sahihi za Nyumba na kila kitu zilipo. Mimi pekee najua zipo sehemu gani. Kwahiyo kamwe hawezi acha tuwe hai wote wawili.” Nilimshawishi Maria kwa kuendelea kumfuta machozi taratibu. Maneno yangu yalikuwa zaidi ya tiba.

“Sasa sikia Mama, japo hatujui ni wapi tunaelekea kwa sasa, lakini ninaimani kuwa ni mbali zaidi ya tunapotoka. Lengo ni kutafuta msaada wa kuweka kila kitu sawa. Sawa Mama!” Nilimaliza kwa kumuongeza na tabasamu lililopeleka shangwe la neno ndio kwa Maria. Maria aliitikia ndio, na hamu ya kuendelea na safari ikaongezeka.

Nikainuka kwa kumshika tena mkono na kuendelea na safari. Bado mwendo ulikuwa wa taratibu kulishawishi jua liwe kali lichome visigino vyetu. Bado ilikuwa ni asubuhi ambayo watu wa lika la kisasa walikuwa wakiamka. Sisi bado tulinyoka na lami tu.

Toka pale tuliposimama na kuianza tena safari ilituchukua dakika kama ishirini hivi na nukta. Tukiwa hatuna hili wala lile tulipitwa na upepo wa ghafla. Ulitokana na gari ambalo lipo kasi. Lilikuwa na spidi kama yale magari ambayo yanabeba watu ambao wakichelewa kuwaishwa hospitali basi wanaishia kufia njiani. Gari hilo lilitupita kwa kasi ya kimbunga na kusimama kwa mbele likiwa limetuzibia njia hatua tatu mbele.

Pasipochukua tahadhari ya mshangao, tayari watu wawili waliovalia nguo nyeusi na usoni kuvalia vinyago vya rangi nyeusi, wakashuka kwa kasi kuja tulipo. Tayari kengele ya hatari akalia kichwani kwangu kabla haijapokea yowe kutoka kwa dada yangu. Maria alikuwa wa kwanza kutimua mbio kurudi uelekeo tuliotoka, na mimi nikawa nyuma yake kwa hatua kama moja hivi.

Kama ilivyo kwa wahenga wa kipindi hicho ambao walipita maisha ya kweli pasi na kuigiza. Walitulia na kuja na usemi ufuatao: Mbio za sakafuni huishia ukingoni. Kukimbia kwetu hakukufua dafu kwa njemba zile. Tayari tulifika ukingoni mwa mbio zetu. Walitunyanyua sote kwa pamoja msobe msobe hadi kwenye gari waliokuja nayo. Kuingia tu ndani tayari gari likaweweseka kusonga mbele kwa kasi.

Nilipumua kwa shida sana hasa walipotuziba midomo tisipige kelele. Tukaanza kuzibwa na mifuko ya rangi nyeusi usoni kuwezesha tusione kinachoendea. Tulikuwa tunaangaika tu kwa kukosa pumzi.

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (18)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
---------------------------------------------------------

Kama ilivyo kwa wahenga wa kipindi hicho ambao walipita maisha ya kweli pasi na kuigiza. Walitulia na kuja na usemi ufuatao: Mbio za sakafuni huishia ukingoni. Kukimbia kwetu hakukufua dafu kwa njemba zile. Tayari tulifika ukingoni mwa mbio zetu. Walitunyanyua sote kwa pamoja msobe msobe hadi kwenye gari waliokuja nayo. Kuingia tu ndani tayari gari likaweweseka kusonga mbele kwa kasi.

Nilipumua kwa shida sana hasa walipotuziba midomo tisipige kelele. Tukaanza kuzibwa na mifuko ya rangi nyeusi usoni kuwezesha tusione kinachoendea. Tulikuwa tunaangaika tu kwa kukosa pumzi.

ENDELEA SEHEMU YA KUMI NA NANE…

Ni sauti tu za gia na micharuzo ya magurudumu ya gari tuliisikia kwa mbali. Hakuna hata mmoja ya wale waliotukamata kutoa neno. Mwendo ulikuwa wa kasi sana. Kwa mtu ambaye alikuwa njiani lazima angeweza kujua kuwa tulikuwa katika mashindano ya dunia na sasa tulikua katika nungwe ya fainali Mashindano ya kusaka dereva bora wa magari yaendayo kasi duniani.

Nilihisi kabisa kasi ile imepita hata gari ya kubebea wagonjwa. Labda tuunganishe spidi ya gari ya wagonjwa na spidi ya gari la askari wanapovamia kituo cha mwalifu. Labda!, labda tunaweza pata jumla ya spidi la gari lililotubeba.

Tulibaki tu kuangaika bila kujua nini kinafanyika nje ya sura zetu, wapi tunaenda na tunaenda kufanywa nini. Kuhusu wakina nani walitushika, sikuwa na shaka kabisa, jibu ni Baba Mdogo tu. Najua hawezi tuacha hai. Ni machozi tu yalijaa katika mifuko ile ya rangi nyeusi tuliyopachikwa usoni. Safari ya kasi ikaendelea..

Bado gari lilikuwa kasi sana, kelele nilizokuwa napiga mwanzo zikaanza kupungua kwa kukosa pumzi kutokana na kuzibwa kwa sehemu zangu za upumuaji na mifuko yao ya rambo. Walipoona inatosha kutunyanyasa wakatutoa mifuko hiyo na kutuacha huru. Ndugu mwandishi unajuwa kuhema wewe?, tulihema sisi jamani, kukosa pumzi sio tukio la ujasiri hata kidogo.

Kabla kutufanya chochote, wakaibua mjadala kidogo. Wakaanza kurumbana kwa maneno, walikuwa wanabishana kuhusu agizo walilopewa na bosi wao. Waliagizwa watunyonge kabisa. Watupoteze wote wawili.

Kutokana na agizo hilo wakaibuka wapinzani kwa kudai kuwa hawawezi kutuua, ila watampa bosi taarifa kuwa tumekufa. Wengine hawakutaka kibarua chao kiote nyasi. Walisimamia msimamo wao wa kutuangamiza. Dereva yeye hakuna na neno bado alikuwa spidi sana bila kuchangia mada. Aliwaacha wale wenzake wagombane tu.

Ugomvi wao ulihitimishwa na wababe wachache ambao walitoa hitimisho kuwa hatuwezi kufa. Walitoa hitimisho kuwa watutenganishe na kututelekeza. Nafsi zao zinawasuta kutoa zawadi ya kifo kwa watu ambao hawana hata chembe ya sababu ya kufa. Waliwakata kilimi wenzao na kufanya maamuzi waliyoyakusudia.

Baada ya kuona umbali tuliokuwepo unatosha kabisa kushusha miili yetu, wakafanya mambo mawili kwa wakati mmoja, lengo lao ni kufuta kabisa ushahidi ambao utajitokeza mbeleni. Ushaidi ambao utaipa sura mpya dunia juu ya manyanyaso yanayoendelea kwa watu wao.

Wakatutenganisha mimi na Dada yangu. Naomba unielewe hapo ndugu Mwandishi.. wale jamaa walitutenganisha mimi na Dada yangu. Mtengano ambao hadi leo hii bado unabaki alama tu katika bongo yangu kuwa nilikuwa na Dada aliyeitwa Maria.

Walichokifanya ni kuchukua kopo lenye mwonekano kama dawa ya kuulia wadudu, lilikuwa linafafana asilimia zote na dawa aina ya Rungu ambayo inaua wadudu wote wanaoruka, kutambaa, kikimbia na kutembea pia. Ilikuwa inamwonekano wa sprei.

Hawakuchelewa, tayari wakanyunyiza katika macho yangu. Hawakuwa na huruma hata kidogo, walinyunyiza yote ndugu Mwandishi. Dawa ilikuwa ni kali sana, ina harufu kali sana, hata radha yake ilikuwa ni ya uchungu, hii ni baada ya kufanikiwa kuionja pindi ilipomwagikia hadi mdomoni. Walimimina yote machoni mwangu.

Dah! Ndugu Mwandishi, baada ya hapo ni miwasho na machozi ndiyo yalikuwa yakibubujika kwa maumivu makali ya dawa ile. Walikuwa na lengo la kunipofoa macho!, na wakafanikiwa. Ndio wamefanikiwa ndugu yangu!!!. Wamefanikiwa kwa asilimia zote mia moja. Denis wa leo ni kipofu, Denis wa leo ni mfu, ameshakufa. Aaagh!!, Lakini Abdul bado anaishi.

Basi hawakuishia hapo ndugu Mwandishi waliendelea na kazi yao bila kusita, hawakujali kelele za mimi na dada yangu ambazo zilikuwa zinakimbizana na upepo tu na kupotea sehemu ambayo haijulikani. Kwa haraka baada ya kunipulizia dawa hiyo wakafungua mlango wa gari na kunirusha nje kama kiroba cha mahindi, gari likiwa bado kasi sana. Walinirusha mimi ndugu Mwandishi.

Hili ni jeraha la tatu baada ya vifo vya Baba, Mama na hatimae kupewa upofu, linafuata hili. Walinirusha nje gari lao na wakaondoka na dada yangu Maria. Wakaenda naye nisipopajua, tukapotezana. Ukawa mwanzo na mwendelezo wa kutojua nini hatma ya dada yangu. Nikabaki Denis dhaifu ambaye amepoteza kila kitu. Amepoteza kila thamani ya ulimwengu huu, hawezi ona au fanya chochote kile.

Kwa hatua kama hii. Tunapata kufuru ya kukashifu na kukejeri jitihada za Mungu kuhusu kuweka shida zinazowatesa watu wasio na tumaini. Kwa hatua hii Mungu aliniacha kwa kweli. Aliziba masikio yake; tena kwa pamba na kuendelea na uumbaji wake, Mungu alinitupa mimi Denis…

ITAENDELEA..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (19)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
--------------------------------------------------

Walinirusha nje gari lako na wakaondoka na dada yangu Maria. Wakaenda naye nisipopajua, tukapotezana. Ukawa mwanzo na mwendelezo wa kutojua nini hatma ya dada yangu. Nikabaki Denis dhaifu ambaye amepoteza kila kitu. Amepoteza kila thamani ya ulimwengu huu, hawezi ona au fanya chochote kile.

Kwa hatua kama hii ndugu mwandishi unapata kufuru ya kukashfu na kukejeri jitihada za Mungu kuhusu kuweka shida zinazowatesa watu wasio na tumaini. Kwa hatua hii Mungu aliniacha kwa kweli. Aliziba masikio yake tena kwa pamba na kuendelea na uumbaji wake, Mungu alinitupa mimi Denis…

ENDELEA SEHEMU YA KUMI NA TISA…
********
Hapo ukawa mwisho wa kipengele ambacho kilitupa majibu macheche kati ya mengi tuliyojiuliza. Ulikuwa ni mda wa majonzi. Mda wa hudhuni, na mda wa kushuhudia uwepo wa Mungu aliye hai.
Licha ya Abdul kukengeuka kwa kumkashifu Mungu, lakini bado anabaki kama kielelezo cha kumsifu Mungu kwani angekuwa hayupo upande wake basi hata miaka ishilini na nukta aliyokuwa nayo asingefikisha.

Bado tulikuwa katika tafakari ya mda mchache ya kutafuta mudi ya msimuliaji wetu, aendeleze mkasa wake wa maumivu. Kwa hakika hata mimi Mwandishi nilimchukia sana Baba yake mdogo na Abdul. Nilishavaa tayari uhusika wa Denis. Niliendelea kujipa ahadi kali za kisasi moyoni. Baada ya kimya kifupi Abdul akaendelea na mkasa wake. Mkasa ambao hata mimi sitausahau katika maisha yangu.

**********
“Basi ndugu mwandishi, waliponirusha nilianguka kwa kuviringika moja kwa moja kwenye mtaro wa maji machafu, maumivu yakaongezeka mara dufu baada ya michubuko niliyoipata wakati niliposeleleka kwenye lami kugusana na maji machafu.

Yalikuwa ni masikitiko ya maumivu ndugu mwandishi. Nilikua mgeni tena duniani. Sikuwa naona kitu chochote kile mbele yangu zaidi ya giza, ni dhairi shairi kuwa nilikuwa kipofu. Kipofu nisiye na msaada wa aina yoyote ile. Kipofu nisiye na wazazi. Kipofu nisiye na nguvu.

Kwa uchungu nikaanza kupiga kelele za kumshusha Mungu wangu aliyeko mbali aje na aone mateso na tabu nazopitia kijana wake. Bado nilikuwa katika maji yale machafu pasipopata hata nguvu ya kunyanyuka. Nanyunyukaje?, na nikinyanyuka naenda wapi?, na kufanya nini?. Niliendelea kuyapikicha macho yangu labda yanaweza yakaona lakini hora! Nikabaki kulia tu na Mungu wangu. Mungu wa Denis!, Mungu wa Abdul mimi!!.

Ndugu Mwandishi basi toka nipatwe na dhahama hiyo ya kupofolewa macho. Nimekuwa mtu wa kutangatanga na njia tu. Sikuwai kuona tena lolote lile lilitokea mbele yangu. Milango mingine ya fahamu ikapokea hali hii kwa huzuni na kufanya kazi ya ziada kuficha udhaifu huu. Mwandishi, kweli nilikuwa sioni lakini Mungu alinipa kipaji cha kutambua baadhi ya vitu.

Nilikuwa najiongoza mwenyewe bila msaada. Maisha yakanifundisha mimi Denis na hapo nikabadili jina rasmi kutoka Denis Ephrehem hadi kuwa Abdul na ubini usiojulikana. Jina hilo nimelitumia hadi leo hii ndugu yangu” Abdul akaacha kusimulia. Akaacha kimya kitawale tena mle ndani lakini safari hii hakukuwa na kimya kile tulichokizoea.

Mapigo ya moyo ya Maria yalikuwa yanasikika kwa sauti kubwa utadhani ni maporomoko Mawe yaliyotumiwa kujengea zile pembe tatu kule misri. Alikua na hofu moyoni mwake. Moyo wake ulikataa kukaa kimya. Abdul hakusita, wala kushituka na hali ile, akaendelea.

Maisha yakawa na maana nyingine kwangu, nilikua kinda lililo kosa mabawa. Yote tisa kumi ni kupotezana na dada yangu Maria, kwa kweli hili nipigo lililo ndani ya moyo wangu. Nikakosa kuliona tabasamu lake ambalo kwa asilimia zote lilifanana na tabasamu la Mama yangu mzazi, yaani ni Copyright. Labda angekuwepo yeye angeweza kuniongoza na upofu wangu.

Nakumbuka kuna siku nilipatwa na ajali ya kugongwa na gari, sikupata maumivu mazito kutokana na ganzi ambayo nilishaipata kipindi cha nyuma. Niliumia upande wa nyuma wa kichwa changu pamoja na kuteguka mguu wangu wa kushoto.

Jambo ambalo lilikuwa nzuri na la tumaini kuliko yote ni kuwa mhusika aliyenisababishia ajali hiyo alikuwa na moyo wa pekee sana. Akanikumbatia kwa kunipeleka hosoitalini, kubwa zaidi ni kusimamia gharama zote hadi nilipona. Katu sikuwahi kumwambia maisha yangu halisi. Nikabaki na ufeki wa jina langu la Abdul. Alihamasika kunisaidia mara naada ya kuona sina kimbilio.

Nilikaa nae kwa miaka kama mitano hivi, nilimwomba anisaidie kumtafuta dada nyangu ambaye nilimdanganya kuwa nimepotezana naye mazingira ya kutatanisha, nilimwambia tu kuwa ‘sisi tulijikuta tumezaliwa bila kuwaona wazazi wetu’.

Sio kama niliongopa kwa kukusudia, hapana. Ilikuwa ni kinga juu ya kuficha kupatikana kwangu na baba mdogo. Sikutaka kumwamini mtu katika maisha yangu, msaada ambao alinipa wakati nipo kipofu ulikuwa ni mkubwa sana, sio wa kumuongezea na hisia mbaya za maisha yangu na familia yangu. Kwahiyo nilimgusia kuhusu dada yangu tu na alihaidi kuna watu wengi anawafahamu mtaani atawaomba wamsaidie kumtafuta.

Mwandishi, nakumbuka mwanzo nilishakuambia kuwa chenye mwanzo hakikosi mwisho!, ndio. Narudia tena kukuambia!, kwa mazuri ya ndugu yule aliyenithamini kama mtoto wake wa mwisho sasa yalifikia mwisho. Alifaliki!, alifaliki baba yule mwenye roho nyepesi na yenye huruma ya kusaidia watu bila kukumbuka malipo.
Chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wake wa presha. Licha ya kusongwa na magonjwa mbalimbali mengi; si kisukali tu, Tb na Magonjwa mengine nayo yalikuwa sababu za kidaktari lakini taarifa iliyosambaa ni kuwa amefariki kwa presha.

Lakini nyepesi nyepesi ambazo nilishadokezwa na binti wa kazi wa pale nyumbani zilikuwa zinadadisi kuwa mzee analogwa na mke wake sababu kubwa ikiwa ni mali. Inasemekana lakini, binti huyo wa kazi alikuwa anaamuliwa na Mama mwenye nyumba kufanya vitu vya ajabu kwa mume wake ambaye yeye alikuwa Baba yake wa kazi tu.

Fununu zote nilizipata kutoka kwa binti huyo ambaye alikuwa mfanyakazi katika nyumba hiyo, tulizoeana sana. Alikuwa mweusi wa sura, mbaya wa tabasamu. Alipendeza sana akikupa kaumbeya.

Basi ndugu Mwandishi kifo cha Baba mwenye nyumba, kilikuwa pigo kwa mimi na mfanyakazi yule kwa jinsi tulivyofanikiwa kufanananaye tabia. Hatukuchukua raundi tukaanza kuteseka na kunyanyaswa haswa.
Mama yule wa Nyumba alikuwa ni mkubwa kiumbo, hakuwa hata na robo ya aibu. Matusi ya nguoni yakawa chakula chetu mimi na mfanyakazi yule. Yeyote kati yetu akifanya kosa basi tunaunganishwa, hakujali hata ulemavu wangu wa macho niliokuwa nao. Manyanyaso yalipozidi kuwa makubwa yakamkimbiza dada wa kazi. Akatokomea pasipojulikana.

Nikabaki pata mateso nikiwa mwenyewe, sina msaada, nashinda na njaa kutwa nzima, mimi na ndani, ndani na mimi. Nalazimishwa kufanya kazi ambazo hata siwezi kufanya kwa hali yangu ilivyo. Akawa anaingiza wanaume kila kuchwao.

Sikuweza kuwaona wanaume hao lakini sauti zao zilijulisha miaka yao. Alikuwa anatafuta wa kumridhisha kimapenzi. Vituko vilivyozidi ndani mule na mimi sikuona budi kukimbia. Nukatoroka mazima na sikuwai kurudisha tena maisha yangu sehemu ile. Yule mama alikuwa katili sina mfano.

Katu sitaki kuongelea ubaya juu ya Mama huyo niliyemkimbia, alikuwa Mama haswa wa kumfunza mtu. Alikuwa zaidi ya Mwalimu kwa kweli. Maisha yake ndio yalinifundisha mimi kutomwamini mtu, kuto kuangalia nyuma, kuto kuwa na huruma. alinivesha sura ya kikatili. Alikuwa zaidi ya Mwalimu kwa kweli. Katu!! Sitakuja kumsahahu Mama huyo. Siwezi kusahau yeye ndiye alinifundisha kuendeleza maisha ya mtaani kwa kupitiliza siku nzima bila kula. Siku nzima bila kuongea na mtu. Siku nzima bila kutoa chozi. Nilikua sugu kwa kweli…

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (20)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
--------------------------------------------------

Sikuweza kuwaona wanaume hao lakini sauti zao zilijulisha miaka yao. Alikuwa anatafuta wa kumridhisha kimapenzi. Vituko vilivyozidi ndani mule na mimi sikuona budi kukimbia. Nukatoroka mazima na sikuwai kurudisha tena maisha yangu sehemu ile. Yule mama alikuwa katili sina mfano.

Katu sitaki kuongelea ubaya juu ya Mama huyo niliyemkimbia, alikuwa Mama haswa wa kumfunza mtu. Alikuwa zaidi ya Mwalimu kwa kweli. Maisha yake ndio yalinifundisha mimi kutomwamini mtu, kuto kuangalia nyuma, kuto kuwa na huruma. alinivesha sura ya kikatili. Alikuwa zaidi ya Mwalimu kwa kweli. Katu!! Sitakuja kumsahahu Mama huyo. Siwezi kusahau yeye ndiye alinifundisha kuendeleza maisha ya mtaani kwa kupitiliza siku nzima bila kula. Siku nzima bila kuongea na mtu. Siku nzima bila kutoa chozi. Nilikua sugu kwa kweli…

ENDELEA SEHEMU YA ISHILINI…

Yote mnayoyaona kwangu kwa muda huu yalikuwa ni mapenzi na mafundisho mema ya Mama yule. Alinifundisha kuwa mwanaume. Mwanaume wa shoka. Kutokana na mafundisho yake amenifanya niwe na hisia za ajabu juu ya kila kitu nachokigusa mara moja tu. Nimekuwa mwepesi sana kuweka vitu vingi kichwani na kuvitumia vyema. Hakika nimekomaa.

Nakushukuru ewe Mama Mwalimu wa hisia zangu. Hakika umenijenga. Niliishi miaka na miaka zaidi bila msaada wa mtu yeyote, mpaka najielewa katika nyakati hizi. Sikupata kusumbuliwa na mtu yeyote yule, hata Baba mdogo hakujua wapi nipo. Nadhani alisahau kama nipo hai!. Alijua nimekufa tayari!...

Oh!! ndugu mwandishi, sijui nani tena alimwonesha kwamba Denis mimi bado naishi. Alianza kuniangamiza tena miaka mitatu iliyopita. Alinisaka katika kila kichaka, nilikuwa mjanja kugundua njia zake. Nikawa nakimbia na kutangatanga tu. Miaka hiyo tayari nilikuwa na mke wangu, mke niliyempata bila kujua thamani ya neno ndoa. Kipenzi changu na mtu wangu wa kwanza duniani kumwamini toka niitwe Abdul!., japo katu haikujua kweli hii. Rose!!”…
*******

Abdul aliishia hapo kwa kutuarakisha mno. Bado kuna kitu hakugusia kabisa, hakutaka kueleza ni lini na wapi walikutana na Rose!. Hatukutaka kumuumiza tukamwacha kwanza atunge sheria kwa kuinamisha kichwa chake.

Tulisubiri sana bila yeye kuongea chochote. Kimya chetu kilinyamazishwa na Rose ambaye alisogeza mikono yake mawili mkononi mwa Abdul, na kusogea kwa kupiga magoti toka sehemu aliyokaa. Ilikuwa ni zaidi ya kunyenyekea. Ilikuwa ni heshima ya wazi wazi.

“Pole mume wangu!, Dada yako yupo wapi?” swali hilo lilifanya Denis ainue kichwa chake kwa ghafla na kurusu mapigo ya moyo wake kwenda kasi. Tulishuhudia mipumuo tu isiyo na uhakika kwamba ndio moyo unatoka wote au nusunusu.

“Ni… nilijibu!.. ni-lijibu ilo swali mda mrefu.!” Abdul akameza mate kwa shida na kuendelea.

“Sina hakika kama amekufa!, sina hakika kama anaishi. Yaani… sina uhakika. Ila dada yangu jasiri sana. Hawezi kufa. Yah!! Hajafa yupo hai dada yangu.” Aliongea kidogo na kuacha alikuwa kama amechanganyikiwa. Hakujua anachokiongea.

“Utajuaje kama huyu ni dada yako ukikutana naye?!” Rose hakujali hali ya Abdul akaendelea kumtwanga maswali mazito mazito.

“Ahhhhgh!, namjua!!, sura yake naijua, sauti na umbo ni muda sana, nimesahau!!. Sina Macho Rose! Hakika nikipata macho yangu nitamtafuta dada yangu!. Na! na….. ndio nimekumbuka kitu! Ndio kipo!, kipo jamani. Dada yangu anakitu cha kipekee sana…” Abdul alikuwa kama mtu mwenye mawenge hivi, kila kitu aliongea na kila kitu alichokiongea hakumalizia. Akatuacha kwenye mataa. Tukashindwa kumuelewa

Ukimya wake ukamkumbusha kuwa anatakiwa kuongea. Anatakiwa kumalizia maneno aliyobakisha. Akatupa siri. Siri ambayo ilileta tena kizungumkuti.

“Mnajua nini??! Dada yangu ni mzuri wa sura. Anasura ya kipekee sana. Alikuwa anaumbo la kipekee sana toka mdogo. Ila kitu cha pekee zaidi ni kuwa dada yangu alikuwa na Kovu!. Kovu kubwa tu na kutosha kuchafua Paja lake la kushoto. Ilo ni kovu la kuzaliwa. Katu haliwezi kufutika!.. Yes! Dada yangu Maria anakovu!!..”.

“Whaaaat!!!!” ilikuwa ni sauti ya Rose ambaye ilimsindikiza mwenyewe hadi sakafuni. Baada ya hapo kimya kikatanda. Tukanyanyuka kwa kuweka mikono kichwani kwa mshangao, na pasipo jua nini kimetokea.

Rose alipatwa na mstuko wa ghafla. Alianguka chini na kuzima kwa muda. Abdul alipapasa tu bila kujua nini Rose kimempata. Tulianza hatua nyingine ya kumpepea Rose!. Kila mtu alijawa na shauku ya nini kilichompata Rose. Nyumba yote ilijawa mkosi wa vilio vya hudhuni.

Tulimpepea kwa siku nzima. Tukasahau kula. Tukafanya kazi ya kushinda sebureni hadi sa sita usiku. Tulipokezana tu kumpepea na kumwagia maji. Abdul alikataa kumpeleka hospital kwa maana itakuwa chambo ya wao kujulikana walipo. Tukatumia njia asilia kufanikisha kumzindua kutoka usingizini. Alizimia kwa masaa mengi sana. Alikuja kutupa matumaini sa tisa usiku.

Sa tisa usiku ndipo Rose alizinduka. Lakini hakuongea chochote. Alilia tu. Alilia usiku mzima, hatukujua sababu ya kilichomliza. Hadi kunakucha hakuna kilichoeleweka. Hali ilikua mbaya kwa upande wake.

Kwa vile siku hiyo ilikuwa ni jumatatu siku ya kazi, niliomba ruhusa kazini kwa kuongopa kuwa siku hiyo nilikua na majukumu mengi nyumbani. Kwa kuwa nilikuwa mtumishi mzuri, hawakusita kunipa mda wa kuweka mambo yangu sawa. Basi nikapata mda wa kuendelea kukaa na wageni wangu.
Saa kumi na mbili asubuhi ndipo Rose aliamua kuweka bayana jambo lililomgusa.

“Denis!, wewe ni kaka yangu!” aliongea maneno machache tu lakini yakawa bomu kwa kila mtu. Mimi mwili ulinisisimka kupita maelezo. Abdul na Rose ni Kaka na Dada??, Inakuaje dada na kaka wakaishi kama wapenzi?. Likawa jambo jingine geni masikioni mwetu.

Kauli hiyo iliibua mdajara mkubwa kati ya Abdul na Rose mioyoni mwao. Bado Rose aliendelea kuthibitisha kuwa yeye ndiye Maria ambaye Denis anamzungumzia. Kichwa changu kikagonga na kuanza kuuma haswa. Hakika nilichanganya mambo kwa kweli.

“Nisamehe Kaka yangu Denis!, ilo kovu unalolizungumzia mimi ninalo hadi leo na katu haliwezi kufutika, nilizaliwa nalo. Icho ndicho nilikuwa nakijua. Kaka nilipoteza kumbukumbu mimi. Hakuna ambacho nilikumbuka kwa wakati huo. Utambulisho wako wa kuwa ulimpoteza mtu mwenye kovu umefanya kumbukumbu zangu zirudi. Nakumbuka sasa. Nakumbuka kila kitu Denis!. AAaahgh! Ewe Mungu jamani kwanini hii inatokea, uwiiiii khaaaaa!, jamani.” Rose alikua anaongea hakiwa hana nguvu hata kidogo. Denis nae alikuwa anaangaika tu pasiposema chochote angali modomo yake ilijaa tamaa ya matamshi…

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (21)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
--------------------------------------------------

Kauli hiyo iliibua mdajara mkubwa kati ya Abdul na Rose mioyoni mwao. Bado Rose aliendelea kuthibitisha kuwa yeye ndiye Maria ambaye Denis anamzungumzia. Kichwa changu kikagonga na kuanza kuuma haswa. Hakika nilichanganya mambo kwa kweli.

“Nisamehe Kaka yangu Denis!, ilo kovu unalolizungumzia mimi ninalo hadi leo na katu haliwezi kufutika, nilizaliwa nalo. Icho ndicho nilikuwa nakijua. Kaka nilipoteza kumbukumbu mimi. Hakuna ambacho nilikumbuka kwa wakati huo. Utambulisho wako wa kuwa ulimpoteza mtu mwenye kovu umefanya kumbukumbu zangu zirudi. Nakumbuka sasa. Nakumbuka kila kitu Denis!. AAaahgh! Ewe Mungu jamani kwanini hii inatokea, uwiiiii khaaaaa!, jamani.” Rose alikua anaongea hakiwa hana nguvu hata kidogo. Denis nae alikuwa anaangaika tu pasiposema chochote angali modomo yake ilijaa tamaa ya matamshi…

ENDELEA SEHEMU YA ISHILINI NA MOJA…

“Kaka! Ni hostoria ndefu sana nimepitia dada yako!, baadhi ya historia hiyo ni hii ambayo imenifanya nibadili jina. Naiomba radhi mizimu ya Mama na Baba popote ilipo kwa kujikana na jina langu la Maria na kujiita jinaa hili Rose ambalo nalo nililipata tu kutoka kwa mtu!.... Jamani kaka. Ivi ni wewe kweli? Eh Denis!!, kwanini ulishindwa kunilinda jamani!!!!..” Rose alilalamika kwa vituo.

Muda huu alianza kupata nguvu na kumlaumu kaka yake kwa kushindwa kumshika mkono wakati huo. Alikuwa anamtikisa Denis bila huruma. Alikuwa na nguvu sasa Rose!. Tukaacha pasipojua nini tufanye, tunafanya nini kwenye ugomvi wa familia?. Tukabaki watazamaji tu mimi na mke wangu tukisindikizwa na michomo ya jua lililoanza kuchomoza madirishani.

“Kaka!, Kaka kumbe hupo eh!, nilishakuzika kichwani mwangu!. Nilishakupoteza kabisa. Kila hatua ya kukutafuta basi iligonga mwamba, nikaamua kufanya mazishi yasiyo na wazikaji kichwani mwangu. Nilikuzika kaka!.” Rose aliongea kwa uchungu sana, hakujali matemate yaliyomtoka kwa pupa mdomoni mwake na kuelekea usoni kwa mwenzake. Bado aliendelea kumtikisa tu Abdul ambaye hakuwa na neno zaidi ya kuduwaa tu. Alikuwa kama Shekhe aliyepata tenda ya kuuza pombe kali nchini Vatcan.

Kaka!.. ka ka.. khakaa unajua nini?!!.” Rose alichanganyikiwa mno kiasi kwamba alikua anafanya matendo yale waliyokuwa wanafanya mitume kumi na wawili kwa wakati mmoja. Alimwita kaka yake kwa upole, akaacha kumvuta vuta, akatulia chini ya sakafu na kuegema katika kona ya sofa alilokaa Abdul. Taratibu akafumba macho na kurusu insha ndefu itawale akili na mdomo wake….

********
“Ni kweli kabisa Kaka yangu!. Nakumbuka!, nakumbuka kweli nilibakwa siku ile ambayo tulishudia Mama yetu anapigwa risasi. Hiyo ndio siku ya kwanza ambayo waliaribu usichana wangu. Jambo la kumshukuru Mungu aliyenibaka mimi ni yuleyule mmoja ambaye alinishikilia. Sikupaswa kukuambia na kukukatisha tamaa. Nilifunga mdomo wangu. Nilivumilia kaka yangu…

Da! Kaka nakumbuka maisha yangu mimi Maria wa zamani baada ya kutengana na wewe. Sitokuja kusahau siku ile ambayo niliyaaga rasmi mapenzi yako. Ulipotupwa nje ya gari angali bado gari lilikuwa kasi. Tayari mapigo yangu ya moyo yalisimama na kushuhudia unakata pumzi. Moyo ulisema kabisa na mimi nimekupoteza Japo nilipingana sana na moyo wangu kwa kutaka kushuhudia japo mwili wako kaka yangu. Ahsante Mungu bado upo mzima.
***

“Kaka kwenye gari lilelile ambalo lilitushikilia na kukutupa wewe, kulitokea na ugomvi mkubwa sana. Ni kweli walikurusha nje ya gari lakini wengi hawakupenda tukio hilo. Walitaka watuue kabisa.

Kama ilivyo katika misemo tuliyoikuta kuwa ‘mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama’. Kuna mmoja mwenye nguvu mule ndani ndiye aliyeshinda, ni yuleyule aliyekutupa wewe nje kaka yangu. Alifanikiwa kuwanyamazisha wote. Kipindi hicho tayari walishanivua ile rambo na nilikuwa nashuhudia kila kitu.

Dereva na mtu yule waliwabadilikia wengine na kuwanyamazisha. Walitumia vyombo vya moto tu kaka yangu. Usisahau kama gari bado lilikuwa kasi. Kila kitu kilikuwa kinaendelea ndani ya gari. Tukabaki watu wa tano ndani ya gari, watatu wazima na wawili wafu. Sikuwa na lolote lile juu yao. Nilibaki kukulilia tu. Sikushughulika na magomvi yao. Nakuapia sikuwai kukusaliti katika kukulia. Nilikulilia sana kipindi hicho

Hatimaye tulifika vichochoroni kabisa ambapo hakuna njia ya kupita magari. Kila kona yalitawala manyasi lakini tuliweza kupita. Tulipita na mbele kulikuwa na nyumba. Walinifunga kamba tu ili nisiwasumbue. Nilikuwa nimeanza kuwazoea watekaji.

Tukaingia ndani ya nyumba hiyo. Haikuwa nzuri sana lakini ilionesha kuna mtu wa makamo anakaa, lakini kwa muda huo hapakuwa na mwenyeji wetu mahali pale. Nyumba ilikuwa kimya na sisi ndio tuliyoifungua. Tukaingia ndani. Watu wale walisogezana pembeni na kuambizana kitu na kisha yule dereva alinisogelea, yule mwingine alienda nje. Inaelekea alienda kutoa miili ya wale wenzao waliowaua kwenye gari.

“Unabahati sana mtoto mzuri!, wewe unatakiwa uishi sawa!.” Alininong’oneza lakini sikutia neno langu kwake. Nilikuwa kimya. Akaendelea.

“Huna budi kutekeleza lile ninalokuambia. Tumeamua bora uishi wewe. Tunataka kukusaidia na tutakutoa nje ya mji huu. Hiyo ni amri mama, hakuna nafasi ya kuchukua maoni kwamba umekubali au umekataa.” Aliendelea kuongea pekeyake bila kupokea majibu. Alikuwa yupo makini sana. Hakuwa na utani kwa lile aliongea. Alimaanisha.

“Hatuna mda wa kupoteza, sahau kila kitu kuhusu huku. Narudia tena sahau kila kitu kuhusu huku!...” aliendelea kujibizana na giza. Nilikuwa kimya bado.

Punde yule mwingine alikuja na kusimama mlangoni. Wakakonyezana tena kama kuna kitu wanakumbushana. Yule deleva akanyanyuka karibu yangu na kupapasa chombo chake cha moto na kukuta kipo salama. Aliangalia kama kina risasi za kutosha kumlinda, na kukiweka takoni.

Naaam nikaamuliwa kunyanyuka. Walinitoa katika nyumba hile na kunirudisha kwenye gari. Sikujua katika nyumba hile tulienda kuchukua nini. Halikuwa jukumu langu kuhoji. Nilikuwa mateka. Nilifuata walichoniambia tu.

Basi safari nyingine ngeni machoni mwangu ikaanza. Gari lilinyenyekea hadi barabara kuu. Tukaanza kuilima barabara kwa hatua moja hadi nyingine. Watu wale walikuwa sio waongeaji kabisa. Walielewana kwa matendo tu kuficha ushahidi.

Tulitembea hadi nilipohisi tumefika mipakani, watu ambao sura zao zilikuwa ngumu na nyeusi zilitapakaa japo walikuwa wachache. Hawakufanana kabisa na watanzania. Tuliama nchi tayari!. Nikawa najiuliza nchi gani hii ambayo ipo karibu hivi kiasi cha kuisogelea kwa gari? Niliwaza ndege tu. Nilijua kuhama nchi moja kwenda nyingine basi hakuna usafiri mwingine zaidi ya ndege. Yalikuwa ni mawazo ya kitoto kweli.

Mahali hapo wakanifungua kamba na tukashuka kwenye gari lile tulilopanda mwanzo. Walinifungua nikawa huru lakini chini ya ulinzi mkali. Tuliingia katika gari lingine ambalo nalo lilikuwa linatusubiri sisi. Ndani yagari hilo kulikuwa na mtu ambaye alitusalimu na kutukaribisha,

“Welcome Mozambique!” aliongea kwa lugha ambayo sio ngeni akilini mwangu. Niliidadavua mapema sana.

Tayari akili yangu ikacheza kwa uharaka zaidi. Nikapitisha macho huku na huku kuona ubovu wa nchi hiyo ya Msumbiji ambayo naisikia tu kwenye mihadhara ya watu na mwishoni kabisa mwa ramani ya Tanzania.

Toka hapo historia ya maisha yangu mimi Maria ikabadilika. Nilijikuta tu jina linabadilika na kuwa Rose. Jina ambalo nilipewa na mwenyeji wangu. Rasmi nikawa Rose nchini Msumbiji, Rose katili, Rose mtamu Msumbiji nzima…”

ITAENDELEA..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI: “ANGAMIZO” (22)
MTUNZI: XAVERY LUOGA (Starxav)
Email: xavemmanuel12@gmail.com
Namba: 0672493994
--------------------------------------------------

“Welcome Mozambique!” aliongea kwa lugha ambayo sio ngeni akilini mwangu. Niliidadavua mapema sana. Tayari akili yangu ikacheza kwa uharaka zaidi. Nikapitisha macho huku na huku kuona ubovu wa nchi hiyo ya Msumbiji ambayo naisikia tu kwenye mihadhara ya watu na mwishoni kabisa mwa ramani ya Tanzania. Toka hapo historia ya maisha yangu mimi Maria ikabadilika. Nilijikuta tu jina linabadilika na kuwa Rose. Rasmi nikawa Rose nchini Msumbiji, Rose katili, Rose mtamu Msumbiji nzima…”

ENDELEA SEHEMU YA ISHILINI NA MBILI…
----------
“Kaka yangu mpendwa. Msumbiji niliishi kwa raha sana, nilipata kila raha ambayo watu wanaita raha. Nilifanya kila kitu ambacho unahisi nilifanya. Nilikuwa huru. Nilikuwa sugu!, nilisahau kila kitu kwa muda mfupi. Na hakika kumbukumbu zangu zilipotea nikiwa huko. Nilimsahau Mama, Baba, na kila kitu kuhusu wewe.

Tulipofika salama katika moja ya nyumba kubwa ya kifahari. Ilikuwa ni nyumba ya yule nyemela dereva aliyetupokea mpakani. Tukapokelewa hapo kwa bashasha na tambwe za kila aina. Rose mimi nikakaribisha maisha mengine mageni.

Lugha ambayo kwa kiasi kikubwa ilikuwa inaongelewa ndani humo ni kireno na kiingeleza kwa uchache. Kiswahili kiliongelewa kwa uchache sana, tena sanasana ni nyakati za kuongea na mimi tu basi. Walijua siwezi kabisa kireno hivyo walitumia kufichia siri zao. Na walifanikiwa, kwani hakuna nilichokinyambua.

Nilikaa kwenye nyumba hiyo kwa siku tatu. Licha ya kugoma kuongea kabisa hawakuacha kuniongelesha. Nadhani walianza kuniteka kifikra sasa.

Kaka!, nilizoea sasa, nilizoea hali hile, nikahisi mimi moja kati ya samiliya yao. Nakili ilikuwa kosa lakini nafanyaje kaka yangu. Hakuna nilichokumbuka. Hakika!, hakuna hata moja. Nilikuwa sikumbuki kabisa nini kilitokea nyuma yangu. Inaonekana kwamba matatizo niliyopitia yalinichanganya kisaikolojia na kujikuta nimesahahu kila kitu.

Basi tuliishi vizuri tu tena bila matatizo ya hapa na pale, japo maisha ya huko yalikuwa maisha ambayo sikuyachagua lakini niliishi. Nakumbuka kuna siku yule dereva aliyenibeba Tanzania aliniambia kitu.

“Umekuwa mzoefu sana sasa!. Hiki ndicho kitu ambacho nilikisubiri kwa muda mrefu. Tunakwenda kufanya biashara sasa!!. Usiniangushe!.” Aliongea hivyo bila kusema ni biashara gani hiyo ambayo mtoto kama mimi naweza kuifaya. Hawakusubiri hata nimalize mwezi tayari walinipa tenda ya kuhudumu Baa. Haikuwa na kikwazo katika kuikataa wakati tayari nilikuwa mwenyeji wa vilevi na sigara hizi ndogondogo. Walinifundisha mengi kabla ya kunipa tenda hiyo.

Nikabadili saa yangu ya mkononi kwa kuyafanya masaa ya mchana kutumia usiku. Hakuna kazi inakera kama kazi hii ya kuhudumu baa, utazoea kazi lakini sio kila mteja atakayekuja. Mwanzaoni niligombana sana na wateja lakini kikazoea na kuwafanya wateja haswa. Nikawa nawauzia pombe na vingine wanavyotaka. Kwa mara ya kwanza nikaanza kutoa ile roho ya uchoyo na kugawa usiri wangu kwa baadhi ya wateja.

Nilikuwa mtoto lakini mambo hayo yakanikuza. Umbo likaongezeka na kuvutia wengi. Nikafanya biashara mbili kwa nyakati moja. Kama pesa hipo unaweza agiza vyote kwa mara moja. Wateja walichangamkia fursa kwa kweli.

Bosi wangu nae alitaka faida zaidi, hakaona baa haitoshi. Akaniongezea mtaji kwa kuniamisha hapo na kunipeleka sehemu ambayo inafaa zaidi katika maisha yangu. Alinipeleka katika dangulo la malaya na machangudoa maarufu nchini humo, yeye ndiye alikuwa mmiliki wa sehemu hiyo. Dangulo lipo katikati ya mji mkuu wa Msumbiji. Huko biashara ikawa nzuri mno.

Nikaanza kutumia pombe japo kwa uchache, madawa ya kulevya mara moja kwa wiki. Nilikuwa na laana kubwa ya Mama yangu mzazi!. Hakika kusahau kwangu kila kitu kulinipa laana. Nikawa mtu wa kulala na wanaume kila siku, saa nazo zikasogea mno, zikasukuma umri wangu na kuufanya kutimia namba nzuri ambayo serikali ya Msumbiji hutoa reseni, vibari na vitambulisho endapo ukiufikisha.

Nilikuwa na miaka kumi na nane sasa. Hakuna starehe nisiyoigusa. Nikawa mjanja hata kwa bosi wangu. Nikamchanganya na penzi langu zito la ajabu ambalo nadhani lilikuwa geni kwake. Nikaanza kumtawala na yeye. Kwa vile nilikuwa fundi, tena fundi haswa haikunipa shida kumteka.

Kaka kipindi hicho nilikuwa hakuna upande ambao sijawahi kugeuka. Ukinileta katika chumba kigeni uwezi amini, nitazijua kona zote ambazo unajificha. Na lazima niwe mshindi!, na hiii ndiyo ilinipa mechi nyingi za kirafiki kwa wengi kutokubali mchezo na kukata rufaa katika mahakama ya Ngono duniani. Nilikusanya pointi tatu muhimu na kutwaa taji la Ngono nchini Msumbiji. Nilikuwa zaidi ya Mesironaldo.

Nilipo mchanganya sana na mapenzi yangu alinipa kibari cha kutoka nje ya nchi. Hakika miaka ilisogea sana. Hakuna nilichokuwa nakumbuka Tanzania. Nilikunywa pombe na kubugia dawa za kulevya kwa kupunguza mawazo lakini nashangaa baada ya kupungua, mawazo hayo yakaondoka kabisa. Kaka sio bure waliniloga mimi, yaani sikumbuki hata jina la Mama yangu mzazi? lo!!.

Kaka mwache mwanamke apewe sifa zake za uke!, akiutumia vizuri uke wake, anakuwa mshindi katika kila pambano na mwanaume. Nilimshinda mwajiri wangu kwa kumteka kimapenzi na kuniruhusu kwenda Tanzania kusimamia miradi yake. Ila alinipa onyo. onyo lenye maneno machache tu.

Onyo la katu! Katu nisikaribiane na mtu anayeitwa Frank!, hakunipa maelezo ya ziada hata kidogo aliishia hapo. Nikajua ni marumbano yao ya kibiashara. Nikapiga moyo konde na kujiandaa na safari. Kaka kipindi hicho mimi ni mzuri sana. Sana!. Nilikuwa mzuri mno wa kumvutia kila mwanaume. Ila kibaya nilipoteza kumbukumbu. Sikukumbuka chochote kile. Likawa doa la uzuri wangu. Hata Baba Mdogo wangu sikumkumbuka.

Hata nilienda kufanya niliyoagizwa na bosi wangu uko Tanzania??, hahahahaha!!, ngoja nicheke Kaka!, ulikuwa ni upumbavu tu. Sio kwamba sikufika Tanzania!, nilifika sana lakini hakuna cha mradi wala maradi niliyosimamia.

Nakumbuka safari ile ya kuja Tanzania ilikuwa kama sio jumapili basi ni jumatatu ya mwanzoni mwa mwezi wa mvua zinazonyesha bila mpangilio. Kama ilivyo kawaida ya tope, halikosi utelezi. Dereva nae hana reseni yaani we acha tu. Alitupindua Kaka!.

Yaani ilikuwa hivi, tulitoka salama kabisa Msumbiji na basi la abiria. Sitaki kuwa shaidi wa spidi ya dereva, nadhani alikuwa sahihi!. Sasa shida nini?. Dereva alishindwa kuhimili mikikikiki ya matope njiani, barabara ilikuwa mbovu sana. Si ndio hizi hizi ambazo zimetengwa rasmi wazitengeneze karibia na uchaguzi?.

Kaka tulianguka vibaya sana. Tuliviringika nje ya barabara zaidi ya mara sita, baada ya gari nililopanda kuacha njia. Sikumbuki majeruhi wangapi na tuliwapoteza wangapi lakini kikubwa mimi bado naishi.

Mungu bado alikuwa na makusudi ya mimi kukutana na Kaka yangu Denis!. Hakika Mungu mkuu!.” Rose alipomaliza sumulizi hiyo alitabasamu tu na kuinua uso wake hadi kwa Kaka yake aliyoko karibu, akaliacha tabasamu hilo lisawili katika mashavu yake kisha kuendelea.

“Kaka kweli mimi sikufa, hata sikufa mimi katika ajari hiyo, si unajua dada yako jasiri eh!, nilichubuka kidogo tu. Hapa na hapa!” Rose aliendelea kusimulia huku akiwa mwingi wa matendo.

Alikuwa anaonesha sehemu zake za mikono ambazo zilipata majeraha. Lakini alionesha tu, kwani hazikuwepo kwa wakati huo. Zilishatoweka. Rose alikuwa mkakamavu wa matendo. Japo inasikitisha lakini inapendeza sana jamani.

“Naaaam!, japo sikufa na kuumia sana. Lakini nilizimia. Nilijikuta tu nipo sehemu ambayo kuna weupe weupe ule wa hospitali!. Nilipoteza tena kumbukumbu kwa mara ya pili. Jambo lingine la kumshukuru Mungu ni kuwa hakuna nilichokumbuka zaidi ya jina langu tu Rose!. Nilipozinduka hapakuwa na mtu yoyote sehemu hile.

Nikanyanyuka na kukaa kitandani kwa dakika kama moja kushangaa sehemu niliyopo. Chumba kilikuwa vizuri lakini hakuna nilichokumbuka. Nilijichekea tu mwenyewe. Kwa hali niliyokuwa nayo nilipaswa kabisa kupitilizwa hospitali kuu ya taifa ya vichaa Dodoma inaitwa milembe sijui. Nilikuwa sijielewi.

ITAENDELEA…

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom