Simuelewi wifi yangu

Simuelewi wifi yangu

Huyo ni mtu mstaarabu sana sababu hapo ni kwako sasa akikurupuka mpaka jikoni wakati hajakaribishwa ungesema anakuingilia!!!!!!!
Either ways wewe siku ya tatu tu ushaanza mpaka ku post huku, je angekuja mgonjwa kukaa hapo mwezi mzima!!!????
Kwanza wewe mtu wa kazini so hushindi hapo kazi anafanya dada labda sasa wewe nini taabu yako!!!!???
Leo wkend kesho sikukuu muamshe mwambie mwende sokoni mkanunue vya kununua na mkija fikia naye jikoni mpe nyanya muombe akusaidie wakati wewe unafanya mengine then anzisha story kuwa uko happy kwa ujio wake sababu sikukuu mtapika vyakula mbalimbali kwa kushirikiana, mtamaliza mapema na ku enjoy.................

Sikuhukumu ila ni kama hupendi ndugu wa mume au una ghubu flani kama sio mvivu..........ungekuwa mke wangu ningekuchana live!!!!!

mzee ushauri umesimama kinoma yani,ushawahi kuishi na mawifi nini?
 
Wifi yangu amekuja juzi. Ni dada wa mume wangu. Alipofika sikuwepo nilikua kazini. Nilipofika toka kazini nikamkuta amelala. Nikamsubiri alipoamka akaja tukatambulishana tukaendelea na maongezi.

Jana siku ya pili kaamka kaoga kawasha tv, akitoka anaenda kulala. Anaamka anakula anarudi kulala. Leo siku ya tatu ameamka mapema tu ameoga karudi tena kulala. Mwenzenu Simuelewi huyu mwanamke mwenzangu hata mlango wa jikoni haujui. Nimekua kama nina waume wawili. Kuolewa kuna shida wenzangu.
Ulivyoweka hizo ka-ka-ku huu utakuwa umbea tu....
 
Aisee Leo ndo nimegundua wanaume mnawajua wanawake kwa undani yani mnaandika yanayotokea in reality
Wengine hatujaoa lkn tunamshukuru mungu tuna experience ya hayo maisha na ufahamu wa kuangalia maisha ya ndoa na usiano kwa macho mengi..wewe chunguza kwa umakini hakuna jiko linalopikwa na wanawake wawili(mke na wifi)..mfano dada apike ile sawa sawa aweke chakula mezani na kaka mtu akisifu chakula kitamu na mke yupo kwa nature ya wanawake utaona kinacho fuata, au dada mtu asafishe nyumba na mke yupo alafu kaka mtu asifu usafi utaona kinachofuata..and vice versa..wengine kuepuka shari wanakaa pembeni tu...so mtu mwenye busara anatake control zaidi maana anaachiwa nyumba yake..aiendeshe
 
Naona tatizo kubwa lipo kwako wewe uliyeandika huu uzi wa kumshutumu wifi yako. Kuna mambo kadhaa ambayo ungepaswa kuyafanyia utafiti kabla hujaja kumfinisha huyo unayemwita wifi yako na sisi wana jf.

Je una muda gani tangu uolewe na huyo mumeo? Je unafahamiana na ndugu wa mume wako? Kwa maelezo yako inaelekea huyu unayemwita wifi mlikuwa hamfahamiani hadi alipokuja kuwatembelea siku tatu zilizopita.

Je unalijua lengo/sababu ya huyo wifi yako kuja kwa kaka yake? Amekuja kumtembelea tu au ana tatizo/matatizo? Huko kulala kwake unakokuzungumzia kama ni kero kwako unajua kumesababishwa na nini? Je unajua kama anaumwa au kuna tatizo la kisaikolojia linamsumbua? Kutokana na maelezo yako mwenyewe, ni wazi kuwa huna mawasiliano mazuri na huyo wifi yako hata baada ya kufika kwako. Inawezekana kabisa ule ukaribisho uliompa ndiyo umemfanya awe analala akiwaza aondoke. Kwa bahati mbaya sana wanawake wengi kutokana tu na kutumia akili za kuambiwa bila kuchanganya na za kwao, pindi wanapoolewa tu wanaanza kujijengea ukuta/defence kwa kuanza kuwachukia mawifi na mama wakwe zao bila sababu ya msingi kwa vile tu waliambiwa na wenzao kuwa mama wakwe na mawifi ni wabaya. Huu mara nyingi huwa ndiyo mwanzo wa uadui na ugomvi katika familia familia. Sikatai kuwa kuna mama wakwe na mawifi ambao ni chanzo cha shida katika ndoa za watoto/kaka zao ila ni kuwa ikiwa wewe mke ndiyo chanzo cha kuwachukia basi ujue hutaishi kwa raha katika ndoa yako. Kumbuka huyo unayemchukia ndo aliyemzaa mumeo, hao mawifi ni ndugu wa damu moja na mumeo, mumeo hataweza kukuvumilia kuona wewe ukiwachukia wazazi/ndugu zake bila sababu. Ikitokea kuwa mama mkwe aau mafifi ndiyo wamekuchukia wewe basi vumilia na uwe na amani, ukweli ni kwamba wanaume wengi wapo tayari kuwalinda wake zao pale wanaponyanyaswa na mama mkwe au dada zao lakini hawapo tayari kumvumilia wake zao kuwachukia ndugu za mwanaume.
 
Weeeeeeee wifi kama hana manenoo unamuachaa kwan kuna tatizo gani kumpikiaa kila siku kumbuka wifi ni kama mume wako
Mi kwa hilo sina shida maana hajaja kunifanyia kaziii kaja kusalimiaaa
ila kama amekuja kishariii ni kumpelekeshaa mpaka atakomaa akiondoka tu kaka yakee vitimbi hivyo hatasahauuuu
Yani Dinazarde umenifanya nicheke sana jinsi ulivyomaliza yaani nimepata picha ndo uko kwenye eksheni sasa duuh mama wa kambo kasingiziwa
 
Wachangiaji wengi wamemaliza kila kitu. Kiukweli siku tatu ni chache mno. Nafkiri pia umetake advantage kwa kua ni ndugu wa mbali. Sidhani kama anafanya makusudi, alafu hebu kuwa friendly nae hata ukirudi mwite jikoni mkae mcheke mwambie asikae pekeake ajiskie huru na kuwa amefika nyumbani. Nenda nae sokoni mrudi Mike ikiwezekana pia tokeni nae out, uone kama hatabadilika.I don't want to judge u ila I can smell some fishy on u.Kitchen party sijui huwa zinaplay part gani sielewi. Wanawake hebu tusiaibishane, vitu vingine vidogo mno jamani.
 
Wakati mwingne sisi ndio chanzo cha maneno na mawifi zetu kwan akifanya hivyo anakunyima nin wewe bi dada jaman 2jifunze kuishi na watu wewe mchukulie poa usianzishe maneno.

mara nyngne unakuta huyo wifi hata hana shida na mtu mnaishi vizur tu lakn hapo utamchokonoa had muanze ugomvi loo!! wanawake kwa gubu mmmh ni kero jaman
 
Mi huyo wifi ningempenda, anakusumbua nini? Chakula si kilikuwa kinapikwa kabla hajaja? Sasa issue iko wapi wewe ongeza vikombe viwili vya mchele maisha yaendelee kama kawa... alale, asilale hajaja kwako kupika
 
Ulipotambulishwa ungeuliza kaja kufanya nini,ni vyema kujua kama kaja kupika,kupumzika,kulima,n.k
 
Naona tatizo kubwa lipo kwako wewe uliyeandika huu uzi wa kumshutumu wifi yako. Kuna mambo kadhaa ambayo ungepaswa kuyafanyia utafiti kabla hujaja kumfinisha huyo unayemwita wifi yako na sisi wana jf.

Je una muda gani tangu uolewe na huyo mumeo? Je unafahamiana na ndugu wa mume wako? Kwa maelezo yako inaelekea huyu unayemwita wifi mlikuwa hamfahamiani hadi alipokuja kuwatembelea siku tatu zilizopita.

Je unalijua lengo/sababu ya huyo wifi yako kuja kwa kaka yake? Amekuja kumtembelea tu au ana tatizo/matatizo? Huko kulala kwake unakokuzungumzia kama ni kero kwako unajua kumesababishwa na nini? Je unajua kama anaumwa au kuna tatizo la kisaikolojia linamsumbua? Kutokana na maelezo yako mwenyewe, ni wazi kuwa huna mawasiliano mazuri na huyo wifi yako hata baada ya kufika kwako. Inawezekana kabisa ule ukaribisho uliompa ndiyo umemfanya awe analala akiwaza aondoke. Kwa bahati mbaya sana wanawake wengi kutokana tu na kutumia akili za kuambiwa bila kuchanganya na za kwao, pindi wanapoolewa tu wanaanza kujijengea ukuta/defence kwa kuanza kuwachukia mawifi na mama wakwe zao bila sababu ya msingi kwa vile tu waliambiwa na wenzao kuwa mama wakwe na mawifi ni wabaya. Huu mara nyingi huwa ndiyo mwanzo wa uadui na ugomvi katika familia familia. Sikatai kuwa kuna mama wakwe na mawifi ambao ni chanzo cha shida katika ndoa za watoto/kaka zao ila ni kuwa ikiwa wewe mke ndiyo chanzo cha kuwachukia basi ujue hutaishi kwa raha katika ndoa yako. Kumbuka huyo unayemchukia ndo aliyemzaa mumeo, hao mawifi ni ndugu wa damu moja na mumeo, mumeo hataweza kukuvumilia kuona wewe ukiwachukia wazazi/ndugu zake bila sababu. Ikitokea kuwa mama mkwe aau mafifi ndiyo wamekuchukia wewe basi vumilia na uwe na amani, ukweli ni kwamba wanaume wengi wapo tayari kuwalinda wake zao pale wanaponyanyaswa na mama mkwe au dada zao lakini hawapo tayari kumvumilia wake zao kuwachukia ndugu za mwanaume.

pamoja saaaaana. Ni kweli kabisa, nikijitolea mfano mimi mwenyewe nipo tayari kumlinda mke wangu kwa gharama yoyote ile kama nitaona anapata manyanyaso na lawama zisizo na msingi kutoka kwa mama mkwe au wifi zake. Pia nipo tayari ya kwa lolote hata kumuacha mke ikibidi kama nitaona analeta dharau za wazi kwa mama yangu pamoja na ndugu niliozaliwa nao bila sababu yoyote.
 
we mwanamke hufai kabisa,tena wewe mwenyewe ndo hujielewi!!! yaani kitu hicho kidogo tu unakuja kushtaki huku? angekuwa dada yako wewe au ndugu yeyote wa upande wako ungekuja kumshataki humu? acha hizo wewe, ukipenda boga penda na maua yake. wanawake wengine (sio wote) mmeolewa kwa bahati mbaya tu hamkustahili kabisa......We unadhani mama yako angekuwa hivyo we ungekuwa na uhusiano na ndugu wa upande wa baba yako? mnawaonea sn mawifi, wakati mwingine nyie wenyewe wake zetu(sio wote) ndo wenye gubu na wapenda uchokozi, tena mkome kabisa!
 
Mi kwa kweli jikoni kwangu ndiko ufalme Wang ulipo.naamini hivyo hats nikienda kwa mtu.
Unless uniambie njoo tupike.
Kila nyumba na kila mwanamke ana namna yake ya upishi.
Sitegemei mdada analilia mtu kuingia jikoni kwake.

loh. tupo wengi, nitakusafishia nyumba yako nzima ila jikoni kwenye swala la mapishi labda niitwe. kwanza sipend wageni waje kwangu waanze kufanya kazi za nyumban, kwani bila huyo mgen kazi hazifanyki!!
 
pamoja saaaaana. Ni kweli kabisa, nikijitolea mfano mimi mwenyewe nipo tayari kumlinda mke wangu kwa gharama yoyote ile kama nitaona anapata manyanyaso na lawama zisizo na msingi kutoka kwa mama mkwe au wifi zake. Pia nipo tayari ya kwa lolote hata kumuacha mke ikibidi kama nitaona analeta dharau za wazi kwa mama yangu pamoja na ndugu niliozaliwa nao bila sababu yoyote.

Is gud and busara being optimistic bro but no kweli wanaume wrote tunajielewa HV?
 
Wifi yangu amekuja juzi. Ni dada wa mume wangu. Alipofika sikuwepo nilikua kazini. Nilipofika toka kazini nikamkuta amelala. Nikamsubiri alipoamka akaja tukatambulishana tukaendelea na maongezi.

Jana siku ya pili kaamka kaoga kawasha tv, akitoka anaenda kulala. Anaamka anakula anarudi kulala. Leo siku ya tatu ameamka mapema tu ameoga karudi tena kulala. Mwenzenu Simuelewi huyu mwanamke mwenzangu hata mlango wa jikoni haujui. Nimekua kama nina waume wawili. Kuolewa kuna shida wenzangu.

Labda amemimbwa au anaumwa
 
Back
Top Bottom