Simu Zetu za Miaka Ile Tulipoanzia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simu Zetu za Miaka Ile Tulipoanzia

Discussion in 'Jamii Photos' started by Yo Yo, Oct 8, 2011.

 1. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]Motorola MicroTAC hii ilionekana Poa Baadae ikaja Model Mpya yake Ikaitwa Star Tac Ukiifunika inatoa mlio wa Tac Poa Sana
  [​IMG]Nokia 101 Ilikuwa lazima ucharge kila siku ukitoka job

  [​IMG]NEC P100 hizi zilikuja zikakosa soko so Zikauzwa kwa Sale Offer bei elfu 17 zikiwa na line na salio la elfu mbili Wabongo waliingizwa mkenge year 2000 nakumbuka fresh UK Zilikuwa na sifa ya kukaa na charge muda mrefu zilipozinduliwa year 1993

  [​IMG]bt Diamond II hizi zilipendwa kwa kuwa na charge yake hapo hapo ila ilisumbua ukiwa na safari sababu charge haikai sana ziliboa zilitumia line na pack yake bila kuipachua unaidumbukiza chini ya keypard
  [​IMG]Motorola FlipPhone 2 hii nayo kama Diamond waliigana hahaha

  [​IMG]Ngoma Star Tac 3000 Iliuzwa bei Mbaya sana nadhani ndio ilikuwa simu ghari zaidi Duniani ilipozinduliwa Marekani january 1996 ikauzwa $1,500 ione hivyo hivyo mh! kwetu ilipofika iliishia bei ya laki tatu baadae ikawa ishapitwa na wakati mpya zake zilitoka

  [​IMG]Nokia Ringo 1997 Ilitesa Mbaya hapa ilipofika kwani ilionekana ni ndogo sauti safi bila mikwaluzo Iliuzwa bei ya Mawazo! Nadhani ilkaa bei juu hadi Anologue zilipopotea sokoni bei yake ilisimama laki na 30 madukani waliozea nazo

  [​IMG]Motorola 8900X-2 Mobitel Now You Talk

  [​IMG] Mambo hayo Unapiga Simu namba 091 Unauliza Saa Sauti Nzito Inakutajia Muda '''Usikiapo Sauti ya Tindo Hivi Sasa ni Saa Tatu usiku na dakika mbili sekunde saba nukta tisa. simu inakatika mtu unafanya kama mchezo kila mara unapiga oi
  [​IMG] Orange Ipo Poa kulikuwa na Rock zake Watoto wasichezee au bill isije kuwa kubwa ukipiga long distance call mwisho wa mwezi baba hana mshahara funguo anaenda nayo kazini oi

  [​IMG]Hii Sijaitumia lol
   
 2. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG] Hii Ilisifika kwa Jina la Twanga Pepeta Siemens C-25

  [​IMG]Siemens S-10 Rangi zake zilikuwa poa na infared msg unaprint kwenye printer zenye infared pia

  [​IMG]Hii ilipoingia walikuwa nayo wazito tu au viongozi wa mashirika na serikali Tritel ndio waliziuza kwa Sana bei zaidi ya milion hakuna mrofa aliyezigusa hadi zilipopitwa na wakati zikaja tumiwa na wapigisha simu huku zikipata jina jipya Sabuni ya Mshindi muhaaha.. kuhusu charge yake hazijambo hakuna simu iliyofikia kwa kukaa na charge kama Siemens S-10

  [​IMG]Ericsoon T 10 Ilipendwa nayo dah ila network vimeo
  [​IMG]Ericsson T 20 Nazo Pia mulemule Network
  [​IMG]Ericsson GA 628 Hizi Zilitesa Balaa wengi waliweza kuzinunua[​IMG]
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,220
  Trophy Points: 280
  mamobiteli hayo
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  Hizi siyo simu za zamani, hadi leo zinatumika. Sema tu tofauti leo wengi tunatumia cell phone. Lakini aina hii ya simu ni zile za mkongo wa landline. Tembelea maofisini utakuta simu za kikazi ambazo ni landline zipo za aina hiyo. Hali kadhalika majumbani zipo nyingi tu. Na kama ni wireless basi distance yake ni ndogo yaani kuzunguka nyumba tu.

  Na si Tanzania tu, duniani kote utazikuta simu aina hiyo. Na kama utaweka landline home phone tegemea kuwa na simu aina hiyo. Hizi si portable phone kama zilivyo cell phones. Wengine kwa vile wamezoea kuwa na cell phone tu wanafikiri aina hii ni ya zamani haipo tena, kumbe hawajakumbuka aina ya simu na matumizi yake hali kadhalika aina ya simu ya mazingira ya matumizi yake.

  [​IMG]

  Hizi ndizo simu za zamani ambazo kwa sasa zipo kwenye majumba ya makumbusho ya mambo ya kale. Ila tunaozidharau ni sisi watanzania kwa sababu ya kasumba. Wazungu kuna baadhi ya maeneo ya public wameweka simu aina hiyo kwa matumizi ya kulipia kwa miito ya mbali kama kitega uchumi na pia ni pambo maridhawa na kuwaonyesha vijana wa kizazi cha leo teknologia ya mawasiliano ya simu yalikoanzia.
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  [​IMG]Siemens s-25 Ilikuwa poa[h=3]1992 – Motorola International 3200[/h] [​IMG]
  * * *​
  [h=3]1992 – Nokia 1011[/h] [​IMG]
  * * *​
  [h=3]1994 – Ericsson GH 218[/h] [​IMG]
  [​IMG][h=3]1995 – Sony CMD Z1[/h] [​IMG]
  * * *​
  [h=3]1996 – Motorola StarTAC 75[/h] [​IMG]

  [h=3]1998 – Samsung SGH-500[/h]


  * * *​
  [h=3]1998 – Nokia 9000[/h] [​IMG]
  * * *​
  [h=3]1998 – Nokia 9110i[/h] [​IMG]
  * * *​
  [h=3]1999 – Panasonic GD-70[/h] [​IMG]


  [h=3][/h] [h=3]1994 – Ericsson GH 218[/h] [​IMG]
  1996 – Motorola StarTAC 75
  [​IMG]
  * * *​
  [h=3]1997 – Nokia 8810[/h] [​IMG]Hii ilikuwa si Mchezo Simu Kali hadi Taa zake mwanga mweupe ila ikichoka noma utakuta imewekwa super glue kila kona oi
   
 6. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Nakubali Mkuu Ila mtu unaweza sema ni za zamani sababu hata ukizipata tatizo battery utapata shida na ukipata haitakaa na charge
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Oct 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Dah! Hizi simu waliokuwa nazo walikuwa wakiziwekea kufuri ndogo sehemu ya ku dial, ila tuliokuwa wajanja, tuliweza kupiga hizo simu bila ya kuzungusha zungusha, just kwa mtindo wa Morse code, yaani tukitumia hiyo sehemu ya kukatia simu... click click mara tisa ina maanisha ni zero.
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  duu hii imenikumbusha mbali sana..
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,791
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Tritel sh 750 000 kwa mwezi!!!Posta unaomba simu asubuhi unakuja kupata jioni tena uwe unajuana na operator wa posta
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Duh, umenikumbusha maana ilifikia hata maofisini kuweka kufuli, ukitaka kupiga simu lazima umwone boss, vinginevyo jenga urafiki na ps.
   
 11. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tumetoka mbali, enzi hizo ulikuwa ukiweka dollar 5 (Tshs. 5,000/=) unapiga dakika 3 tu kwisha!
   
 12. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #12
  Oct 9, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Duh! nakumbuka enzi hizo nasoma Jangwani Sec kuna kaka-teacher wetu anaishi jirani na kwetu basi kazi yangu kumpokelea simu za girl friends zake wengine wakiwa ni wanafunzi wenzangu. Basi wakawa wanadhani teacher ni kaka yangu. Dingi akitoka namwita teacher anakuja kupiga simu. Mh! tumetoka mbali.
   
 13. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Dah!!!alafu zilikuwa ghali niaje!!kutoka laki mbili enzi hizo,eti leo zinauzwa 5000 na change zinarudi!!!
   
 14. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Duh! umenikumbusha cm yakuzungusha kila namba ukitaka kupiga leo hii tuna mbofya
   
 15. a

  actus Senior Member

  #15
  Oct 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh umenikumbusha wakati huo hata unaempigia inabid awe na salio kwenye simu yake ndo mtaweza kuwasiliana na wakati huo na yeye mkiwa mnaongea anakatwa salio..duh jamani haya makampuni yametengeneza hela mbaka basi.
   
 16. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #16
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,522
  Likes Received: 12,782
  Trophy Points: 280
  asee nimekumbuka na miimi nilikuwa na yale ya
  mobitel na tritel yana kaeria nilikuwa nazungumza
  kwa nguvu ili watu wajue na mie ninasimu
  lol lilikuwa linanilemea.
  kweli tumetoka mbali sana
  na bado eti hapa tuko nyuma
   
 17. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #17
  Oct 11, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,580
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  Ilikuwa simu ikisumbua utasikia mtu akisema 'mobitel yangu inasumbua!'
   
 18. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #18
  Oct 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,522
  Likes Received: 12,782
  Trophy Points: 280
  bwana wee ilikuwa kaazi kweli


   
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Oct 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Enzi za mshindi na motorola.
   
Loading...