Simu kali zenye mvuto za kichina usizozijua

TheChoji

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2009
Posts
6,710
Reaction score
20,717
Watu wengi tumekua tukidharau au kubeza simu zinazotoka China. Mtu unapokuwa na simu ya Mchina basi watu watakutania na kukuona umenunua simu mbovu na ya bei rahisi. Lakini katika siku za hivi karibuni zimeibuka simu kali na zenye mvuto wa kipekee kutoka China. Zifuatazo ni baadhi ya simu kali na zakuvutia za Kichina..

1. Oppo Find 5:
Ni kati ya simu kali kabisa kutoka China. Ina memory ya 2GB RAM 16Gb Internal, Camera 13mp, kioo inch 5 (441 ppi) na processor ya 1.5 GHz.
descarga.jpg

2. Huawei Ascend P6

Hii nayo ni kati ya simu matata kutoka kampuni ya Huawei. Hadi hivi karibuni, ilikuwa inashikilia rekodi ya kuwa simu nyembamba kuliko zote duniani ikiwa na wembamba wa milimita 6.2 tu! Ina kioo cha inchi 4.7 (312ppi), memory 2Gb RAM, 16/32 Gb Internal, Camera 8mp, na processor ya 1.5GHz.

huawei-ascend-p6.jpg

3. Lenovo K900

Hiki ni kitu kingine kikali kutoka kampuni ya Lenovo. Simu hii imetengenezwa kwa material ya aluminium ina processor ya Intel Atom 2Ghz, ina kioo cha inchi 5.5 (401 ppi), memory 2Gb RAM 16/32 Gb Internal, Camera 13mp, na ni kati ya simu nyembamba sana ikiwa na wembamba wa milimita 6.9 tu!

K900.png

4. Meizu Mx3

Ni moja kati ya simu za maana kutoka China. Simu hii ina kioo cha inchi 5.1 (412ppi), memory ya hadi 128Gb Internal, 2Gb RAM, 8mp Camera, na 1.6Ghz Processor.

Meizu-MX3-press-photos-and-camera-samples.jpg

5. ZTE Nubia Z5S

Hii ni simu kali kutoka kampuni kongwe ya ZTE. Simu hii ina kioo cha inchi 5 (441ppi), Internal memory 32Gb, RAM 2Gb, huku ikisukumwa na processor ya 2.3GHz. Pia ina Camera ya 13mp.

ZTE-Nubia-Z5S.jpg

6. Gionee Elife s5.5

Hii ndio simu inayoaminika kuwa nyembamba kuliko zote kuwahi kutokea duniani hadi sasa. Simu hii ina wembamba wa milimita 5.5 tu, huku ikiwa na kioo cha inchi 5 (441ppi), Internal memory 16gb, RAM 2Gb, Camera 13mp, na processor ya 1.7GHz.

black_phone.jpg

7. Doogee Turbo DG2014

Hii ni simu nyinginne ya kipekee kutoka China. Simu hii ya laini mbili ina processor ya 1.3GHz, RAM 1Gb na 8Gb Internal memory. Pia ina kioo cha inchi 5 na Camera ya 13mp. Simu hii pia ni nyembamba sana (6.3 milimita) na ina mfuniko wenye matundu matundu ambao.. nahisi kama nimeuona mahali hivi.. :smiling:

5.jpg

Na kadhalika.

Kama kuna nyingine ongezea na wewe
 
Bongo zipo nijipatie kamoko? Nipe na bei kabisa, hujaweka battery life, ungeweka hio nayo ingekua bombi nyumbi
 
Tanzania tunazipata duka gani?

Nimejaribu kutembea maduka mengi ya Tz hasa Dar, Arusha na Moshi simu hizo hakuna. Hii nadhani inatokana na watu wengi kutokuzifahamu na hivyo wenye maduka kutokuziagiza. Ndio maana ukitembea maduka mengi Tz utakuta brand zilezile kila unakokwenda. Nadhani tubadilike
 
zinapatikana china tuu
mbona bongo hamna
 
Nimejaribu kutembea maduka mengi ya Tz hasa Dar, Arusha na Moshi simu hizo hakuna. Hii nadhani inatokana na watu wengi kutokuzifahamu na hivyo wenye maduka kutokuziagiza. Ndio maana ukitembea maduka mengi Tz utakuta brand zilezile kila unakokwenda. Nadhani tubadilike

Hii kitu inaboa sana. Unajikuta unataka kutumia kitu tofauti lakini ukiingia madukani ni brand hizo hizo tuu! Otherwise uagize ughaibuni. Wafanyabiashara wa bongo kweli wanashindwa kutuvutia kabisa tusiopenda kutumia brand zinazokua kero mtaani.
 
Ishu sio kutozifahamu, izo simu sio za chini ya laki 4, ni ghali kulinganisha na vi clone vya samsung, kwa sababu vina brand name kabisa ambayo inatambulikana
 
Watu wengi tumekua tukidharau au kubeza simu zinazotoka China. Mtu unapokuwa na simu ya Mchina basi watu watakutania na kukuona umenunua simu mbovu na ya bei rahisi. Lakini katika siku za hivi karibuni zimeibuka simu kali na zenye mvuto wa kipekee kutoka China. Zifuatazo ni baadhi ya simu kali na zakuvutia za Kichina..

1. Oppo Find 5:
Ni kati ya simu kali kabisa kutoka China. Ina memory ya 2GB RAM 16Gb Internal, Camera 13mp, kioo inch 5 (441 ppi) na processor ya 1.5 GHz.
descarga.jpg

2. Huawei Ascend P6

Hii nayo ni kati ya simu matata kutoka kampuni ya Huawei. Hadi hivi karibuni, ilikuwa inashikilia rekodi ya kuwa simu nyembamba kuliko zote duniani ikiwa na wembamba wa milimita 6.2 tu! Ina kioo cha inchi 4.7 (312ppi), memory 2Gb RAM, 16/32 Gb Internal, Camera 8mp, na processor ya 1.5GHz.

huawei-ascend-p6.jpg

3. Lenovo K900

Hiki ni kitu kingine kikali kutoka kampuni ya Lenovo. Simu hii imetengenezwa kwa material ya aluminium ina processor ya Intel Atom 2Ghz, ina kioo cha inchi 5.5 (401 ppi), memory 2Gb RAM 16/32 Gb Internal, Camera 13mp, na ni kati ya simu nyembamba sana ikiwa na wembamba wa milimita 6.9 tu!

K900.png

4. Meizu Mx3

Ni moja kati ya simu za maana kutoka China. Simu hii ina kioo cha inchi 5.1 (412ppi), memory ya hadi 128Gb Internal, 2Gb RAM, 8mp Camera, na 1.6Ghz Processor.

Meizu-MX3-press-photos-and-camera-samples.jpg

5. ZTE Nubia Z5S

Hii ni simu kali kutoka kampuni kongwe ya ZTE. Simu hii ina kioo cha inchi 5 (441ppi), Internal memory 32Gb, RAM 2Gb, huku ikisukumwa na processor ya 2.3GHz. Pia ina Camera ya 13mp.

ZTE-Nubia-Z5S.jpg

6. Gionee Elife s5.5

Hii ndio simu inayoaminika kuwa nyembamba kuliko zote kuwahi kutokea duniani hadi sasa. Simu hii ina wembamba wa milimita 5.5 tu, huku ikiwa na kioo cha inchi 5 (441ppi), Internal memory 16gb, RAM 2Gb, Camera 13mp, na processor ya 1.7GHz.

black_phone.jpg

7. Doogee Turbo DG2014

Hii ni simu nyinginne ya kipekee kutoka China. Simu hii ya laini mbili ina processor ya 1.3GHz, RAM 1Gb na 8Gb Internal memory. Pia ina kioo cha inchi 5 na Camera ya 13mp. Simu hii pia ni nyembamba sana (6.3 milimita) na ina mfuniko wenye matundu matundu ambao.. nahisi kama nimeuona mahali hivi.. :smiling:

5.jpg

Na kadhalika.

Kama kuna nyingine ongezea na wewe

kweli mkuu umejitahidi kwa uchambuzi ila nasikitika kwa vile bongo hazipatikani.mkuu hata huawei hazipo tanzania?
 
Ishu sio kutozifahamu, izo simu sio za chini ya laki 4, ni ghali kulinganisha na vi clone vya samsung, kwa sababu vina brand name kabisa ambayo inatambulikana

Ya, ni kweli baadhi ya zimu nilizotaja hapo ni bei ghali kuliko hata baadhi ya Samsung na Iphone.
Mfano:
Oppo Find na Gionee Elife s5.5 ni kati ya US$ 600 - 900 (Tsh 1m - 1.5m)
Lenovo K900, Meizu Mx3, ZTE nubia na Huawei P6 ni kati ya US$ 350 - 600 (Tsh laki 6 - 9)
 
Hii kitu inaboa sana. Unajikuta unataka kutumia kitu tofauti lakini ukiingia madukani ni brand hizo hizo tuu! Otherwise uagize ughaibuni. Wafanyabiashara wa bongo kweli wanashindwa kutuvutia kabisa tusiopenda kutumia brand zinazokua kero mtaani.

Ila nadhani pia wateja wengi ni waoga kujaribu vitu vipya espeshale kwasababu watu tayari wana mtizamo hasi kwa vitu vya kichina. Mtu anataka mpaka aone mtu fulani anaitumia ndio na yeye anunue.. Matokeo yake ndio unakuta waatu wote mtaani mna simu aina moja! Ikiita moja kila mtu anajisachi!!
 
Ishu sio kutozifahamu, izo simu sio za chini ya laki 4, ni ghali kulinganisha na vi clone vya samsung, kwa sababu vina brand name kabisa ambayo inatambulikana

Kuna Simu ya laki4?? Lazima huyo ni feki baada ya kila mwaka kwa fundi. Simu nzuri na imara kuanzia sanasana laki 7
 
Ila nadhani pia wateja wengi ni waoga kujaribu vitu vipya espeshale kwasababu watu tayari wana mtizamo hasi kwa vitu vya kichina. Mtu anataka mpaka aone mtu fulani anaitumia ndio na yeye anunue.. Matokeo yake ndio unakuta waatu wote mtaani mna simu aina moja! Ikiita moja kila mtu anajisachi!!

Yanatakiwa matangazo kwa wingi kwenye tv. Wafanyabishara wagumu sana kutoa pesa kwa kutangaza biashara zao.
 
Ila nadhani pia wateja wengi ni waoga kujaribu vitu vipya espeshale kwasababu watu tayari wana mtizamo hasi kwa vitu vya kichina. Mtu anataka mpaka aone mtu fulani anaitumia ndio na yeye anunue.. Matokeo yake ndio unakuta waatu wote mtaani mna simu aina moja! Ikiita moja kila mtu anajisachi!!

android yenyewe ina diversification kubwa still watu bado wanaiongeza. mimi siwezi kumrecomend mtu akanunue simu yenye chip ya ajabu ajabu sababu itamtesa mbele ya safari.

hapo juu labda oppo na hao meizu wanadeserve kupewa shavu na kidogo zte hao waliobakia ni pointless.
 
Huawei P6 na Y300 zipo bongo, P6 imesimama kwenye 900,000/- na Y300 inasoma TZS. 250,000/- hizo nyingine sijaziona.
 
Oppo ndiyo simu ya kwanza kuwa na Official Cyanogenmod ROM kama stock ROM. Sidhani kama ukiwa na Oppo utachekwa maana ni simu popular sana U.S. kwa sasa. Na ina ubora wa hali ya juu.
 
Tatizo wafanyabiashara wa bongo wako conservative sana sio wabunifu wa kutafuta vitu vipya visivyojulikana. Wanafikiri wanunuzi wanataka tu bidhaa zile zile zilizo maarufu.
 
Back
Top Bottom