DJI wameinzdua OSMO Pocket 4 Pro yenye Camera Mbili!

DJI wameinzdua OSMO Pocket 4 Pro yenye Camera Mbili!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
33,680
Reaction score
97,466
Baada ya kuzindua DJI OSMO Pocket 4 mwezi April, DJI pia walidokeza kidogo Pocket 4 Pro, ambayo ilionekana inakuja na lens mbili. Finnaly wamefanya officially launch.
IMG_9095.jpeg

Hii pocket gimbal camera imekuja na 1-inch sensor, f/2.0 aperture and 20mm focal length. Sensor ya pili ni telephoto camera ina 1/1.28-inch sensor, f/1.8 aperture, na 60mm focal length.
IMG_9096.jpeg

Telephoto camera ina optical zoom hadi ya 3x na digital zoom ya 12x.
IMG_9097.jpeg

Pia ina support 10-but video recording na D-Log2 color, bila kusahau 3-axis mechanical gimbal yenye intelligent subject tracking.
IMG_9098.jpeg

Kwenye video inarecord hadi resolution ya 4K 60fps, na slow-mo inarecord hadi 4K 240fps!
IMG_9099.jpeg

Kuhusu picha, inapiga 37MP na ina panorama mode.

Kwa mbele ina screen ya inch 2, inayoweza kuzunguka, microphones tatu, na ina internal memory ya 103GB ambayo unaweza kuongezea kwa microSD card hadi ya 1TB.

Ina battery la 1,545mAh linasupport fast charge ya 0-80% kwa dakika 18 na 0-100% kwa dakika 32.
IMG_9102.jpeg

Kwa sasa imeanza kuwekewa order China, standard kit ni $560 na Vlog kit ni $645 tu.
IMG_9105.jpeg

Ikumbukwe kampuni nyingine ya camera kutoka China Insta360 nao wametoa pocket gimbal yao ya kwanza wiki iliopita, inayoitwa Luna Ultra ambayo inafanana na Osmo Pocket 4Pro kwa asilimia zote.
IMG_9104.jpeg

Hii imepelekea DJI kuwafungulia mashtaka Insta360 ya patent infligment, kwa kucopy design yao.

DJI ndio waliointroduce hizi Pocket Gimbal camera, na wana series ndefu tokea Pocket 1 mwaka 2018, Pocket 2 mwaka 2020, Pocket 3 mwaka 2023 na sasa Pocket 4 na 4 Pro mwaka 2026.

Pia soma: DJI wamezindua OSMO Pocket 4 camera!
 
Mm umeniacha hicho kifaa kina kaz gani
Hii ni camera, kwa wanaofanya content au waandishi wa habari wachukua matukio hii wanaitumia. Rahisi kubeba, chaji zaidi ya masaa 2, video nzuri zaidi ya simu
 
Back
Top Bottom