Simu iliyobadilisha maisha yangu

Simu iliyobadilisha maisha yangu

Ndio maana nasema kipimo cha mwanaume si kuvaa suruali. Binafsi nikikushauri umuache mumeo utakuwa umempa nafasi huyo kahaba ya kujaza nafasi uliyoacha, pia nikijaribu ushauri wa kuondoka basi utakuwa umevunja viapo vya ndoa ambavyo moja ya hivyo vinahimiza uvumilivu.
Basi jambo la kukushauri mweleze muumba wako matatizo yako yeye atakujibu, pengine hiyo ikawa ni dalili ya kutokuwepo mahali sahihi kutokana na maamuzi yako uliyoyaamua kipindi cha nyuma kabla ya ndoa.
 
Duh natamani ningekuoa Mimi aiseee, umetumia akili ya hali ya juu mno. Safi sana yaani ukitaka kuujuaa ukweli unatakiwa uwe mpole, fanya uchunguzi tena uchunguzi ambao sio biased, kimya kimya, utajua mengi sana lakini ukipaniki tu, imekula kwako. Nimekupenda bure aiseee na naamini ndoa yako ni nzuri sana. Mshauri Theodora atulie aende mdogo mdogo ataujua ukweli tu, hebu imagine unapniki weee halafu mwisho wa mchezo ni kwamba walikua wanakutania tu, utafanyeje? Nimependa hio, eti mtembee au mruke.....hahaahhahahah God bless you mwanamke mwenye busara
sala zAko ndo mkombozi wako
jiulize huyo mtu mzima ovyooo
kajiamini nini mpaka kakufata kukupa live?
je km ni muong?picha zipo hata za kuunganishA!
usikurupuke anza uspy taratibu
ukweli utaujua
mi mwenzio (natoa ushuhuda )niliona mme wangu hana uhuru na simu yake ikipgwa silence tena saa 6 usiku sikuuliza nikasubir kalala nikachuku a simu nkakuta 7misd call,3dialled calls,4 ricvd calls za mtu mmoja
nikachukua namba asubuh kaondoka nkapiga mdada kapokea nkauliza unamjua fulani akasema simju nkamwambia sasa umjue usimjue huyo mtu ana mke na ana watoto na mi ndo mkewe siondoki leo walA kesho
dada akaanza kujishauashaua pale nsamehe mi kaniAmbia hana mke il sijatembea nae
nkamwambia mi sjui mtembee mruke ujumbe umeupata tena mwambie mkeo kanipigia
akaomba msamaha
AM SORY STORY NDEFU ila nataka nkwambie km ni kweli huyo mmama anatoka nae
hao ndo wanaume na ktk dunia hii UKITAKA MKAMILIFU MUUMBE MWENYEWE
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
U never know labda bi mkubwa ndio Daimond...pole sana yani, mapenzi yapo complicated mno.
 
Really BAK?

Yaani unataka amsamehe halafu aendelee kuishi na huyo mume mzinzi?

Wewe ukigundua mkeo anamegwa na mtu mwingine utamsamehe tu na kuendelea na maisha yeu?

Kama ni hivyo kweli watu mna moyo!

Na mimi nilitaka nimuulize hivyo hivyo, ingekuwa ni yeye ndo amegundua mkewe kafanya hayo angesamehe? kwa kweli tunatofautiana mioyo
 
Nawasabahi wanaMMU.


Swali - Why would a man take the risk of losing a diamond to pick stones?

Pole sana dada. It works both way. Hata baadhi ya akina dada walioolewa hufanya hivyo hivyo. Wanaacha diamond nyumbani na kwenda ku-pick a piece of wood.
 
Ndio maana nasema kipimo cha mwanaume si kuvaa suruali. Binafsi nikikushauri umuache mumeo utakuwa umempa nafasi huyo kahaba ya kujaza nafasi uliyoacha, pia nikijaribu ushauri wa kuondoka basi utakuwa umevunja viapo vya ndoa ambavyo moja ya hivyo vinahimiza uvumilivu.
Basi jambo la kukushauri mweleze muumba wako matatizo yako yeye atakujibu, pengine hiyo ikawa ni dalili ya kutokuwepo mahali sahihi kutokana na maamuzi yako uliyoyaamua kipindi cha nyuma kabla ya ndoa.

The Intelligent we toa tu ushauri usiogope matokeo. Sasa unamsukumia kwa muumba kana kwamba muumba anaongea na mtu uso kwa uso? Muumba si alitufanya kama yeye isipokuwa uwezo wa kuishi milele? (yaani uwezo wa kujua jema na baya). Muumba pia anaweza kukutumia wewe kumpa majibu huyu dada. Na mjumbe hauwawi. Kusema akimuacha mumewe kahaba atachukua nafasi yake si sababu nzuri ya kubaki kwenye ndoa. Abaki kwenye ndoa kwa sababu inamfanya ajiskie vizuri. Pia kahaba (binafsi sithubutu kumuita kahaba) hana shida na ndoa kwa mujibu wa maelezo ya huyu dada. Ukimshauri kuondoka unaogopa atavunja viapo vya ndoa vinavyohimiza uvumilivu. Sijui ni ndoa gani zina viapo hivi, ila najua kiapo kikuu cha ndoa zote ni kuwa mwaminifu (na kwa ndoa za kingereza mpaka kifo kitakapowatenganisha). Mume kavunja hiki kiapo kikuu cha uaminifu , unasemaje hapo? Kiapo kingine ni kuwa pamoja katika shida na raha. Katika shida ndo kunatakiwa uvumilivu. Sasa kwani hawa kuna mmoja mwenye shida? (kama ugonjwa, kufilisika, kufungwa......). Mume kuning'inia kwenye kiuno cha "mama yake" si shida, ni raha zake. Mwishoni umeongea jambo limenigusa: huenda ndo muumba anamwambia hayuko mahali sahihi achape mwendo maana mwenyewe kasema amefupisha habari kasema ingekuwa ni mtu mwingine angekuwa mirembe. Manake hiki si kisa pekee. Kweli tumeumbiwa majaribu, na nia ya majaribu ni kutujenga. Tatizo linakuja kwenye jinsi tunavyotafsiri ushindi kwenye majaribu. Kusalitiwa mara moja, mbili, tatu, nne..... wewe upo tu huli, hunywi, hulali, hucheki, vidonda vya tumbo vyako, hasira zako, presha yako, depression yako...upo tu unashindana na majaribu hautajengeka bali kubomoka. Matokeo ya kushinda majaribu ni kuwa ku-gain character - kuwa mtu bora/imara zaidi. Sasa ukaja kuugua au kufa ili "kahaba" asichukue nafasi yako si muumba atakushangaa sana? Si kila mwanandoa anayesamehewa ukahaba wake anaacha. Mwingine akisamehewa anafikiri mwenzie kamkubali kama alivyo, anaendelea tu. Kwa hiyo mdada aangalie pia mumewe ni mtu wa aina gani.
 
Pole dada........
Mbona unakubali kushindwa kirahisi sana!!!!!!!!!!!!" hata muwe kumi we ndo namba moja be strong kuwa tayari kupokea mabadiliko muda wowote katika maisha na ujue namuna ya kuhandle otherwise u'll always be a loser
 
Mkuu NANDERA nimekuelewa lakini ushauri wangu kwa huyu dada siwezi kumwambia amuache mumewe labda kama kungekuwa na ulingano wa madai kati yake na mumewe hapa jukwaani ningepima madai yao na kutoa ushauri. Unajuaje kama huyu dada hamnyimi/kumtoshereza mumewe kwenye tendo la ndoa? vingine basi kuna kitu ambacho huyo kahaba anampa mumewe ambacho hawezi kukipata kwake, je hapo unasemaje?
Unajuaje kama huyo mumewe alipumbazwa kishirikina na huyo kahaba ili amlie pesa, je mwanaume atajinasuaje? haya yapo.
 
Last edited by a moderator:
Huwezi vunja ndoa kwa kisikiliza maneno ya mtaani. Utavunja ngapi. Umeongea na mumeo. Kakuambia nini. Je usingeambiwa na huyo ajuza juu ya huo uhusiano usingekuwa unajua. Je lipi bora., kuachwa huyo ajuza na wewe kujua au kutokujua na wao waendelee ukiwa ndani ya ndoa. Punguza hasira. Ongea na mwenzio msamehane maisha yasonge. Huyo kigagula alipoachwa kaamua kumuharibia huyo mwanamume ili kinuke nae kwa mkewe. (Kakataa bara basi hata pwani asipate) Usivunje ndoa kwa mikono yako. Huu ndo muda mzuri wa kufukia mabonde utakapo ambiwa nini tatizo na mwenzio. Hizo ndo challenge za ndoa. Jitahidi kuzishinda.
 
Pole mwaya!!
Usifanye maamuzi ukiwa na hasira jipe muda utulie kwanza.
Inasikitisha ila ukweli ni kwamba ku cheat kwa wanaume imekuwa kama kawaida tu so ukiamua kumuacha mumeo kwa sababu hiyo ujue chance ya kupata mwingine asiye cheat ni almost zero!
 
Pole mwaya!!
Usifanye maamuzi ukiwa na hasira jipe muda utulie kwanza.
Inasikitisha ila ukweli ni kwamba ku cheat kwa wanaume imekuwa kama kawaida tu so ukiamua kumuacha mumeo kwa sababu hiyo ujue chance ya kupata mwingine asiye cheat ni almost zero!

Si kweli. Wasio cheat wapo tena wengi tu. Hii ni kama ushirikina. Mtu mshirikina akitaka kukuvutia kwenye ushirikina hukuambia watu wote wamefanikiwa vile walivyo sababu ya ushirikina - ukiuliza ushahidi hakuna! Kusema eti wanaume wote wana cheat ni uongo kwani ukiulizwa ushahidi uko wapi - hakuna.
 
Si kweli. Wasio cheat wapo tena wengi tu. Hii ni kama ushirikina. Mtu mshirikina akitaka kukuvutia kwenye ushirikina hukuambia watu wote wamefanikiwa vile walivyo sababu ya ushirikina - ukiuliza ushahidi hakuna! Kusema eti wanaume wote wana cheat ni uongo kwani ukiulizwa ushahidi uko wapi - hakuna.[/QUOTE]

Tukubaliane kutokukubaliana,amini wapo wasio cheat mie naamini hamna na unaoona bado basi wape muda kidogo tu kabla hawajawa walimu!
Hapo kwenye red,mie ushahidi ninao ila sijaulizwa tu!!!!
 
Si kweli. Wasio cheat wapo tena wengi tu. Hii ni kama ushirikina. Mtu mshirikina akitaka kukuvutia kwenye ushirikina hukuambia watu wote wamefanikiwa vile walivyo sababu ya ushirikina - ukiuliza ushahidi hakuna! Kusema eti wanaume wote wana cheat ni uongo kwani ukiulizwa ushahidi uko wapi - hakuna.[/QUOTE]

Tukubaliane kutokukubaliana,amini wapo wasio cheat mie naamini hamna na unaoona bado basi wape muda kidogo tu kabla hawajawa walimu!
Hapo kwenye red,mie ushahidi ninao ila sijaulizwa tu!!!!

Haya naomba nikuulize utoe ushahidi wa wanaume wote ku-cheat. Please utoe ushahidi huo, manake umesema unao!
 
Pole yako dada, najua unapitia wakati mgumu sana katika ndoa yako kwa sasa, ebu chukulia kama ni moja ya changamoto ulizoambiwa utakutana nazo katika ndani ya ndoa

Jipe muda wa kutafakari tena, mpe nafasi mwenzako akuambie ukweli wake, Nina imani umekaa naye kwa muda utakuwa unamfahamu vizuri then baadaa ya hapo pima uzito.

Kuachana naye siyo suluhisho la matatizo maana naamini kuna mengi mmefanya pamoja, na kama ukifikia maamuzi hayo kilahisi itakuwa ni ushindi mkubwa sana kwa huyo kizee

Please don't give up on him easily kama akikiri kosa msamehe na msonge mbele.
 
Ungekuwa mstaarabu na mjanja ww ungekaa na huyo mama umuulize yy anamfanyia nn mmeo mpaka wanaendelea ili naww umfanyie astoke ndan,kuwa almas huwi mbinifu n sawa na kuwa mawe ya kuchezea bao uswaz huko

Kama mi siyo mstaarabu, drama ya tukio ingekuwa kwenye magazeti ya udaku. Mm nilitumia emotional intelligence. Kwanza jimama ndani ya miezi mitatu tayari sleeping with somebody's hubby is cheap na kama ndiyo ujanja - samahani unaweza kuniita na majina mengine, that will not make me feel any better or worse.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Theodora umenifurahisha sana kwa hekima na busara zako za hali ya juu. Hilo la kukaa na hilo jimama likikuelezea kuhusu mumeo kwa nia ya kutaka kuvunja ndoa yako bila hata ya kumrukia na kuanza kumtandika linahitaji EI ya hali ya juu. Naamini kabisa kutokana na kujaliwa EI utainusuru ndoa yako. Pole sana katika hiki kipindi kigumu unachopitia katika ndoa yako. Kaeni chini mliongee hili kwa marefu na mapana.

Kama mi siyo mstaarabu, drama ya tukio ingekuwa kwenye magazeti ya udaku. Mm nilitumia emotional intelligence. Kwanza jimama ndani ya miezi mitatu tayari sleeping with somebody's hubby is cheap na kama ndiyo ujanja - samahani unaweza kuniita na majina mengine, that will not make me feel any better or worse.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom