Simshangai Pasco wa JF tu; hapana, nawashangaa waandishi wote wa habari popote pale mlipo nchini!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,065
22,758
th

Huyo hapo juu ni aliyekuwa mwandishi wa habari na mwakilishi wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi. Mwangosi, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu na kusambaratisha mwili wake wakati polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 2, 2012



296587_4672851945587_1395901855_n.jpg

Pamoja na msemaji wa Polisi mwanzoni kukanusha askari kuhusishwa kwenye tukio la hilo la kuhuzunisha, ushahidi wa picha ulikuja kutolewa ukimuonesha polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) akimlipua Mwangosi ambaye muda huo tayari anakula kichapo kutoka kwa polisi wenzake. Polisi huyo, Pasificus Cleophace Simon (23) mwenye namba G2573 alifanya mauaji hayo mbele ya wakubwa wake akiwemo aliyekuwwa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya RPC Michael Kamuhanda.



IMG-20120904-WA034.jpg

Mke wa Marehemu, akiwa na uchungu kufuatia kifo cha mumewe akitoa heshima zake za Mwisho siku ya mazishi. Alikuwa na imani kubwa kwamba waandishi wa habari hawangemtelekeza na kwamba kuna siku ukweli ungewekwa wazi na wahusika wote nao waonje machungu kama yaliyompata yeye na wanawe kwani silaha za kujibu mapigo kwa mwenzao wanayo.


582728_4673002029339_659749645_n.jpg

Hapo juu anaonekana Marehemu Daudi Mwangosi akihojiana na RPC Michael Kamuhanda muda mfupi kabla hajafikwa na umauti. Baadaye Michael Kamuhanda alikuja kupandishwa cheo kutoka SACP (Senior Assistant of Police) kwenda DCP (Deputy Comissioner of Police).

Sasa swali langu kwa Pasco na waandishi wote wa habari popote mliopo Tanzania, je mpo? Kama mpo vipi ile silaha yenu ya kalamu inayodaiwa kuwa kali kuliko bomu, kwa Mwangosi mmesalimu amri?
 
Last edited by a moderator:
Kuna waandishi wengine wanashangaza kweli kweli k.m. yupo huyu wa Mwananchi anaitwa Neville Meena; anaenda Marekani kutafuta kunakodaiwa kazikwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Ballali, badala ya kutafuta ukweli kuhusu ugonjwa wake ulivyotokea. Ballali aliitwa Dodoma akiwa mzima kabisaa, katoka Dodoma akiwa na wasiwasi na maisha yake na ghafla huyooo anaumwa. Kaondoka kwenda Marekani kwa matibabu huku serikali ikidai haina taarifa na kudai haijui Ballali yuko wapi au kalazwa hospitali gani huko Marekani au anagharamiwa na nani...waandishi hao ambao sasa wanadai sasa kufuatilia liliko kaburi lake walikuwa wapi? Toka 2008!

Haya Daudi Mwangosi, mwanataaluma mwenzao kalipuliwa mchana kweupee na polisi chini ya usimamizi wa OCD, OCO, na RPC mwaka 2012. Msemaji wa Polisi, Advera Senso anakanusha na kudai kalipuliwa na Chadema, picha inatolewa ikionesha ukweli wa kilichotokea, akina Neville Meena kama vile hawapo, haliwahusu! Advera Senso pamoja na uongo wake wote ameendelea na wadhifa wake kama vile ni tukio tu la kawadia. Wakuu wa Polisi wote wanaohusishwa na mauaji ya wananchi wasokuwa na hatia adhabu yao ni kupandishwa vyeo! Je ni waandishi gani wanafuatilia mambo haya? Leo Mwangosi, je kesho? Meena? au yeye ana kinga maalum! Je Kibanda?
 
Najaribu kuona Pasco anahusikaje nashindwa kabisa....au tumemgeuza punching bag humu?
 
Last edited by a moderator:
Mbona waandishi wa habari wengine hawakuuliwa siku hiyo? jiulize, kilichomfanya akamvae kamanda wa FFU na wameshatangaza watu kutawanyika na kuondoka hapo ni nini?

Msitake kujaza watu ujinga, si kuna chama cha waandishi wa habari, si kuna mawakili wa kutetea haki za binaadam? si kuna mawakili wa kutetea haki za waandishi wa habari? kwanini wasifunguwe mashtaka kuishtaki Serikali? wameona hakuna kesi, huyo alikuwa na makosa alipomkimbilia kamanda wa FFU na kumvaa.

Nyinyi ndio msiojuwa mlitendalo, hata manapoona kuna makosa yamefanyika hamtaki kukubali. Huo ni ujinga dhahiri shahiri.

Mngekuwa na akili japo kiduchu ya kufikiri mngeelewa kuwa "upiganaji" si siasa ni vita. Na ukiamuwa kwenda kuwa "mpiganaji" matokeo yake ndio hayo, lakini hutokuta mwana siasa, ambae anajuwa kuwa siasa maana yake ni kuondoa tofauti zenu kwa amani na kwa nguvu ya hoja na kukubaliana kutokukubaliana na kuridhiana, hutokuta yanamkuta kama hayo.
FaizaFoxy, nitavunja mwiko wangu wa kutojibizana na wapuuzi kama wewe mara hii moja tu halafu sitahangaika na wewe tena. Kwa ufahamisho, hii ndiyo ilikuwa ripoti iliyotolewa na polisi kupitia kwa msemaji wake, Advera Senso, kuhusu kulipuliwa kwa Mwangosi.
th

Advera Senso said:
Mwandishi alikuwa akikimbia kutoka upande wananchi na kuelekea walipokuwa Polisi. Marehemu inasemekana alipigwa na kitu ambacho mpaka sasa hakijafahamika bado mpaka uchunguzi ufanyike.Kuna kitu kilirushwa kikitokea upande wa Wananchi na kumfikia ambacho kilimjeruhi pia Askari akiwamo Mkuu wa kituo cha Polisi. Jeshi la polisi limewakamata 32 waliokuwa wakienda Mbeya kwenda kufanya vurugu, wakitokea Iringa kuhusiana na kifo cha Daudi Mwangosi.
FaizaFoxy, hii ilikuwa ni ripoti iliyotolewa na Jeshi la Polisi; ni wapi unatoa ripoti ya marehemu kumvaa RPC? Wakati Mwangosi analipuliwa RPC alikuwa ndani ya gari akishuhudia na kutoa maelekezo. Endelea tu kujianika kwa kutetea ujinga...that's exactly what is expected of you.
 
FaizaFoxy, nitavunja mwiko wangu wa kutojibizana na wapuuzi kama wewe mara hii moja tu halafu sitahangaika na wewe tena. Kwa ufahamisho, hii ndiyo ilikuwa ripoti iliyotolewa na polisi kupitia kwa msemaji wake, Advera Senso, kuhusu kulipuliwa kwa Mwangosi.
th


FaizaFoxy, hii ilikuwa ni ripoti iliyotolewa na Jeshi la Polisi; ni wapi unatoa ripoti ya marehemu kumvaa RPC? Wakati Mwangosi analipuliwa RPC alikuwa ndani ya gari akishuhudia na kutoa maelekezo. Endelea tu kujianika kwa kutetea ujinga...that's exactly what is expected of you.

Kama nimemwelewa vizuri Faiza,anasema:Marehemu Mwangosi alienda kumvaa kamanda wa kikosi cha FFU na siyo RPC kwa uelewa wangu hawa ni watu wawili tofauti au siyo Faiza?
 
@...faizafoxy ...always wewe unaleta upinzani yaani unaleta ligi hata kwenye kifo cha mwanhosi, R.I.P mwangosi hao wote waluyokufanyia unyama huo malipo dunia watayapata....watateseka na wataishi ktk hali ngumu sana washenzi wakubwa
 
Sasa swali langu kwa Pasco na waandishi wote wa habari popote mliopo Tanzania, je mpo? Kama mpo vipi ile silaha yenu ya kalamu inayodaiwa kuwa kali kuliko bomu, kwa Mwangosi mmesalimu amri?

Mkuu Mag3, kwanza asante kutukumbushia hili la Mwangosi japo kwa kiasi fulani umetonesha vidonda vya machungu yaliyopita, lakini pia sometimes ni muhimu kukumbushana ili follow up ya kinachoendelea iendelee kufuatiliwa kwa kupashana habari!.

  1. Kiukweli tukio la Mwangosi lilitugusa karibu waandishi wengi, and we did what we could do by then, lakini nakiri wazi, we didn't do enough ukiondoa zile emotions na machungu ya kifo, maandamano na rambi rambi, baada ya kuzikwa I'm not if we did much!, sijapata follow up ya mjane wake anaishije maajaliwa ya familia yake na maendeleo ya kesi, hivyo huku ni kutuamsha kama tumelala sio tuu tutimize wajibu wetu kwa jamii, pia tumtendee Daudi Mwangosi haki ili roho yake ipumzike kwa amani.
  2. Kwa upande wangu binafsi, kupitia kalamu yangu humu jf, kilichomkuta Daudi Mwangosi ni matokeo tuu, sio chanzo!. Wengi wanajikuta very emotional ku deal na matokeo lakini ni wachache wanajishughulisha na kushughulikia chanzo!. Mimi ni miongoni mwa wachache hao ambao nimedeal na chanzo hivyo naomba unifuatilia katika michango yangu hii.
  3. Historia yangu na haraka niliwahi kuiweka hapa [h=3]Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar[/h]
    Ni mimi ndie nilyepiga zile picha za vurugu za 1996 kule Zanzibar, na nilishikwa kuswekwa ndani kituo cha Mwembe Madema nikiwa na Ali Saleh na Khalfani Saidi akiwa mpiga picha wa gazeti la Majira. Nikanyang'wa kamera ya DV, polisi wakaniambia niwaonyeshe picha nilizopiga, nikawaambia sijapiga picha!. Wakaichukua kamera kuipeleka TVZ, Mungu bariki, TVZ walikuwa bado wako VHS, DV hawajui, wakairudisha na kuthibitisha hakuna picha!. Nikafukuzwa Zanzibar under escort. Kufika bara, jioni mimi mwenyewe nikatangaza vurugu za Zanzibar na picha juu!. Ulimwengu ukaona!. Picha hizo zilipelekea Kituo cha DTV na Gazeti la Majira kupigwa marufuku Zanzibar!.

    Pia ni mimi niliyetangaza zile vurugu za Mwembechai nikiwa in a line of fire!.
    Hivyo kutangaza police brutality sikuanza jana!.
  4. Kabla ya kilichokuta Daudi Mwangosi, niliwahi kuupandisha huu uzi humu,[h=3]Police Brutality in Tanzania: The World has a Right to Know...[/h] nani aliwahi kuusoma na jee nilikuwa ninazungumzia nini?! sehemu ya uzi huo nilisema hivi
    Nimeangalia ITV news hiyo kamata kamata ya jana ya waunini wa kanisa la Ephata, vijana wako wameonyesha udhaifu mkubwa!.
    Baada ya kuwalipua wale waumini kwa mabomu ya machozi na kuwa contain, walitumia risasi za moto za nini kukabiliana na watu wasio na silaha yoyote?.

    Kitu cha kusikitisha zaidi ni watuhumiwa hao kuendelea kushushiwa kipigo hata baada ya kuwa mikononi mwa palisi!.

    Baada ya vijana wako kuwakamata watuhumiwa kuna sababu gani ya kuendelea kuwashushia kipigo mpaka wakiwa ndani ya defender ya polisi?.

    Naomba niwakumbushe tuu baadhi ya visa vya police brutality and no one amechukuliwa hatua zozote!.

    Kuna kisa cha watuhumiwa fulani 4 kilichotokea Arusha ambapo watuhuniwa hao walikamatwa toka nyumbani mwao mmoja baada ya mwingine wakiwa wazima huku wakitembea wenyewe siku ya Ijumaa.

    Jumamosi ndugu zao wakafika kituo cha polisi kuwaletea ndugu zao chakula, walielezwa watuhumiwa hao wamepelekwa mahali kwa mahojiano.

    Kesho yake Jumapili waliporudi polisi walielezwa ndugu zao wamepelekwa hospitali ya Mt. Meru.

    Walipofika hospitali waliinyeshwa miili ya watu wanne waliouwawa kinyama na majeraha ya vipigo!. Polisi walipoifikisha miili hiyo hospitalini hapo, waliandikisha kuwa wameiokota eneo la Unga Limited baada ya kupigwa na watu wenye hasira!.
    The story ended up there and then!. Hakuna chochote kilicho fuatia hata tuu japo kuulizwa kama ile kesi ya Zombe!.

    Kwa nini mtuhumiwa aliyekuwa mzima afie mikononi mwa polisi bila uwajibikaji wowote wa jeshi la polisi?!.

    Kamanda Mwema, haya yanatokea kwa sababu mnajua Watanzania hawajui haki zao, polisi wako hawajui haki za binaadamu na kama arrest kama za jana zenye police brutality zimefanywa mbele ya camera, and no body cares, huko behind bars ni nini haswa kinafanyika?. Si ndio itakuwa worse?!.

    Yote haya yanawezekana kwa sababu Watanzania hatujui haki zetu, chochote kinachofanywa na polisi wanajua ndio haki yao tena watu hawajui kabisa kuwa raia wa kawaida anaweza kulishitaki jeshi la polisi!.

    No one is above the law, please stop this police brutality inayofanywa wazi wazi and behind clossed doors!.

    Thanks.

    Pasco.
  5. Kilichomtokea Mwangosi, nilipandisha uzi huu,
  6. [h=3]IGP Mwema, Please, Please, Please, Stop This Police Brutality,[/h]sehemu ya uzi huu nilisema hivi
    3. Najua Mkuu Kamanda Mwema, inawezekana wewe hupati muda kupita humu JF kwa vile mtandao huu 'hauna jema la kuisifia serikali yako', na vile vile 'uko bize sana' na shughuli za ulinzi wa raia na mali zao (japo wengine kwa kuwaua kwa makusudi mazima), lakini naamini vijana wako wanapita humu na watakuletea hizi salamu zetu, tunakuomba sana sana sana, stop this police brutality, utakuja kumponza bure shemeji!.

    4. Tanzania tuna uchache sana wa wanasheria, na waliopo wengi hufanya kazi kwa wenye nazo, hivyo tangu huu mlolongo wa mauaji ya polisi, hakuna mwanasheria, shirika, wanaharakati, au chama chochote cha siasa kimelifikisha jeshi la polisi mahakamani, simply because wanaokufa wote ni watu hohehahe, familia zao hazina uwezo wa hata tuu wa kujua haki zao za kudai fidia rasmi serikalini, bali uwezo wa kuajiri mwanasheria kuwatetea mbele ya haki kwa kulishitaki jeshi la polisi!.

    5. System ilipoamua kumshuhulikia Imram Kombe kwa kutumia polisi wazembe, angalau familia ile ilikuwa na uwezo wa kuajiri wakili jeshi la polisi likashitakiwa na serikali ikalipa fidia ya kifuta machozi cha mamilioni, japo mlizuga kuwa askari wale walihukumiwa vifungo japo hawakuvitumia lakini familia ile angalau chochote kitu ilipata, milioni 300 kwa miaka hiyo, japo hailingani na uhai wa binadamu, lakini angalau ilikuwa sii haba!, hawa wengine wote, hawakuwa na wa kuwapigania lakini kwa Mwangosi, its a wrong button!.
  7. Baada ya Polisi kumfungulia mashitaka polisi mmoja tuu, yule aliyepush the trigger, nikauliza why only him while he was following order, nikapandisha uzi huu [h=3]Waziri Nchimbi na IGP Mwema, Mnasubiri Nini Kujiuzulu? hapa nilisema hivi.
    Wale wenye kumbukumbu ya Kesi ya Mauaji Mwanza, kilichomtokea Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi sote tumekiona, sasa nauliza hivi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Nchimbi na IGP, Saidi Mwema, mnasubiri nini kujiuzulu ili kusetiri aibu ya serikali?!.
    [/h]
    Kwa mnaokumbuka hiyo kesi, naomba niwakumbushe kwa mujibu wa kumbukumbu yangu, nilikuwa darasa la 4 hivyo baadhi ya facts zinaweza zisiwe right!.

    Kwa kawaida askari wale mlio washuhudia wamemzingira Mwangosi, wao walikuwa wanatimiza wajibu wao kwa mujibu wa amri amri halali ya mkubwa wao!. Baada ya kutokea kilucho tokea, huyo mkubwa wao aliyetoa amri, anasubiriwa nini ili hali by now alitakiwa awekwe chini ya ulinzi then and there!, na wakuu wao Nchimbi na Mwema walipaswa by now wawe wameshawasilisha barua zao za kujiuzulu!.

    Askari polisi hawezi kushitakiwa kwa kutekeleza amri halali ya mkuu wake, anayetakiwa kushitakiwa kwanza ni aliyetoa amri!.

    Kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, iliyotokea mwaka 1976 na kesi kuendeshwa mwaka 1979 baada ya kutokea vifo vya watuhumiwa wawili wa mauaji ya vikongwe, Bw. Masanja Mazengenuka na Isaack Mwana Mkoboko, Waziri wa mambo ya Ndani wakati huo Ali Hasan Mwinyi alijiuzulu, mkuu wa Polisi, Pundugu alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mzena alistaafishwa kwa manufaa ya umma. Walioshitakiwa ni RPC wa Mwanza, Cassian Mkwawa, RS wa Mwanza, Andrew M na DSO, Jemes Ihuya!.

    Wakati huo, Peter Kisumo ndiye alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, naye pia aliwajibika!.

    Wakuu hao watatu wa polisi walikuwa wakiishi nyumba tatu zilizofuatana zikiwa Isamilo ya chini ikianza ya Ihuya, ikafuatia ya Andew M na ya mwisho ni ya Mkwawa!. Just imagine hali ilikuwaje mtaani wakati vigogo watatu wanene wa mutaa wote wanashitakiwa kwa kosa la mauaji!.

    Kama ni kweli polisi mfyatuaji risasi atapandishwa kizimbani, then RPC wake nae ndie amtangulie, huku waziri Nchimbi na IGP Mwema, wao bado wanasubiri nini kuwajibika?.

    Hata hivyo, damu ya mtu, haiwezi kupotea bure!, sio damu tuu ya Mwangosi, bali damu za wote zilizo mwagika bila hatia, kwa mujibu wa sheria kubwa kabisa iitwayo The Law of Karma, damu zote hizo lazima zitafidiwa kwa damu au kwa adhabu kubwa zaidi ya damu!. Tatizo la fidia, inaweza kuwa kubwa kuliko tukio lenyewe au hata kuwakumba na wasio husika ili kuisafisha roho ya marehemu!.

    Hivyo hata wahusika wasipowajibishwa, then at the end of the day, ni muwajibishaji wa mwisho ndio atakaye lipia the final price!.

    [h=3]Pasco!.
    [/h]
  8. Waandishi wenzangu wa habari walipojidai watasusia kuandika habari za polisi kufuatia hasira ya kifo cha Daudi Mwangosi, Wa kwanza kutofautiana nao ni Maggid Mjengwa, na mimi pia niliungana na Maggid nilitofaitiana nao [h=3]Waandishi Kugomea Habari Za Kipolisi; Naomba Nichangie ..nilisema hivi,
    Wakuu mimi namsupport
    maggid, ila pia nazama deep zaidi kidogo kuliko maggid,
    [/h]
    1. Kisuso cha waandishi, sio kisuso cha kweli, ni kisuso cha hasira na uchungu wa kufiwa, siku zikipita, uchungu utapungua, hasira zitapungua na kwa RPC waandishi wataripoti!.

    2. Wengi wa waandishi ni watumwa tuu, hawafanyi kazi kwa utashi wao bali hufanya kwa utashi wa editor na edotors ambao sio wamiliki wa vyombo vyao, nao pia ni watumwa tuu wa wamiliki, au waajiri wao, hivyo nao hawafanyi kazi kwa utashi wao bali utashi wa wamiliki "he who pays the piper may call the tune"!.

    ila mimi kama Pasco wa JF, ni mwandishi wa kujitegemea, sijaajiriwa na yoyote, wala situmwi na yoyote, na siitegemei media yoyote kutumia habari zangu kwa sababu mwamuzi ni mimi ndio ninaamua habari gani niandike na media ipi nipeleke, hivyo nikiamua kugoma, naweza kugoma kiukweli!, na ninavyomfahamu Maggid, nae ni kama mimi, ni mwanahabari wa kujitegemea, hivyo waandishi wenye uwezo wa kususia habari zozote sio za kipolisi tuu, ni wale tuu wanaojitegemea na sio hawa wanaotegemea vyombo vya habari!.
  9. Katika utetezi wangu kwa haki za wanyonge, sikuishia kwa polisi tuu, kwenye kutafuta haki, the most powerful person in this country kuliko hata the the president of URT ni mtu anayeitwa DPP, yeye pia sikuacha kumzungumzia!. Katika uzi huu, [h=3]DPP wetu kizuizi katika mapambano dhidi ya ufisadi - Page 2, nimesema hivi
    Sio tuu mimi na wewe hatuwezi kumbana DPP, bali hakuna yoyote mwenye uwezo wa kumbana, hata rais hawezi!.
    [/h]Mzee MMKJJ, yote uliyosema kuhusu DPP ni kweli, lakini pia kwa mujibu ya sheria iliyounda ofisi ya DPP, havunji sheria yoyote kwa kutofanya uchunguzi wowote kwa vile hayo ndio mamlaka yake ambayo kisheria, anayatumia at his discretion as he pleases at his pleasure na sheria inamlinda.
    Kwa maoni yangu, tatizo sio DPP, tatizo ni mamlaka ya ajabu yaliyochini ya DPP.
    Niliwahi kuchangia mahali nikaainisha sheria yetu iliyounda ofisi ya DPP, amepewa mamlaka makubwa yac ajabu, nguvu haswa za DPP ni pamoja na 'power to declare nolle proseque' yaani hakuna kesi ya kujibu. DPP huyu anauwezo wa kuingilia kesi yoyote ya jinai, ikiwa mahakama yoyote na ikiwa katika hatua yoyote kabla ya hukumu, kuisimamisha, kingilia, ama kuifuta bila kulazimika kutoa sababu zozote wala maelezo yoyote.
    Sheria ya DPP inamtaka kutimiza wajibu wake bila shinikizo lolote kutoka popote na hata akiletewa kesi yoyote ni discretion yake aprosecute ama asiprosecute na hakuna chombo chochote ndani ya JMT chenye mamlaka ya kumuuliza lolote DPP, hata rais hana mamlaka hayo!.
  10. Hayo na mengine mengi ndio the most I could do as a journalist humu jf, ila pia nimefikia final stages za mwisho wa powers za mwandishi ni kuishia kuandika tuu, kupiga kelele wasikie au wasisikie hapo ndio mwisho!, nime realize, there is still a chance ya mimi kutoka kwenye kuandika na kupiga tuu kelele, na kuingia kwenye kutenda, to take actions, to act kwa vitendo, muda huo ukifika, it might be too late kwa Daudi Mwangosi lakini better late than never!.
Pasco
 
Mbona waandishi wa habari wengine hawakuuliwa siku hiyo? jiulize, kilichomfanya akamvae kamanda wa FFU na wameshatangaza watu kutawanyika na kuondoka hapo ni nini?

Msitake kujaza watu ujinga, si kuna chama cha waandishi wa habari, si kuna mawakili wa kutetea haki za binaadam? si kuna mawakili wa kutetea haki za waandishi wa habari? kwanini wasifunguwe mashtaka kuishtaki Serikali? wameona hakuna kesi, huyo alikuwa na makosa alipomkimbilia kamanda wa FFU na kumvaa.

Nyinyi ndio msiojuwa mlitendalo, hata manapoona kuna makosa yamefanyika hamtaki kukubali. Huo ni ujinga dhahiri shahiri.

Mngekuwa na akili japo kiduchu ya kufikiri mngeelewa kuwa "upiganaji" si siasa ni vita. Na ukiamuwa kwenda kuwa "mpiganaji" matokeo yake ndio hayo, lakini hutokuta mwana siasa, ambae anajuwa kuwa siasa maana yake ni kuondoa tofauti zenu kwa amani na kwa nguvu ya hoja na kukubaliana kutokukubaliana na kuridhiana, hutokuta yanamkuta kama hayo.

Wewe unadhani halujisalimisha? Alijisalimisha kwa kias kikubwa kwa kunyoosha mikono na bado hakusiklizwa na tatizo la huyo ni kwamba alikuwa anaandika ukweli kuhusu maovu yalokuwa yanafanywa na hao wakubwa na kwa taarifa yako alishapewa taarifa kuwa asiende huko lkn kwa sababu yeye alikuwa anatenda haki hakuona ubaya wake alienda kwenye tukio kumbe kamanda na vijana wale walikuwa na chuki binafsi ya kumuua ila wale waandishi kajanja hawakupewa adhabu hiyo.

Kwa hiyo dada yangu kumuona hapo Mwangosi sio kwamba alikuwa amemvamia kamanda Hapana ila alishajisalimisha bado hakusikilizwa akaona kuwa akienda kwa kamanda atapona kumbe yeye ndo alikuwa anaamlisha "piga tu" waandishi wao wa serikali hawakuwa na kosa kwao na hao ndo tunaowaongelea hapa na kuwakumbusha kwa nini hawamkumbuki mwenzao na hata hilo unalosema la kushitaki?

Hawashitaki kwa sababu wale viongozi wao wote wako mifukoni mwa mafisi-hadi,kwa hiyo unapaswa kuelewa dada yangu sio kukalia mambo ya siasa za Chadema na Ccm hat kwenye mambo silias kama haya. Amka dada yangu!
 
Issue ya Mwangosi tulifeli wote kama taifa hatukufanya lolote zaidi ya kulalamika tu kama mtoto aliyenyimwa pipi. Tujilaumu wenyewe. Kamanda aliyesimamia mauaji haya na cheo kapandishwa, wote tunasubiri Dr Slaa atangaze maandamano.

TUKUBALI SISI WATANZANIA KAMA JAMBO HALIJAKUTOKEA BINAFSI HATUJALI ZAIDI YA KUSIKITIKA TU: hail:

RIP Mwangosi
 
Pasco umeutendea haki uzi huu, hakika mengi umeyaeleza. Jambo nalipata hapa ni kwamba kuna uhaba wa kujua sheria, kufuatilia haki zetu na hata umaskini wa kipato kugharamikia kesi! zaidi ni pamoja na uwezo wa nani anaenda kudai haki, kwa maana ya kufungua kesi mahakamani.

Swali : Hivi chama cha waandishi haikiwezi ku file case ya mauaji ya Daudi mwangozi?
SP
 
Waandishi wa habari Tanzania wengi ni mateka wa wanasiasa, Binafsi sijawai kuona nguvu ya vyombo vyetu vya habari kufatilia na kuripoti matukio.

Vinaendeshwa kwa kufuata upepo na sio kuchimbua matukio.

Angalia kuelekea Uchaguzi mkuu unajua kabisa chombo fulani kipo mahususi kwa kumpigia debe mgombea wa kambi fulani matokea yake Mwananchi analishwa matango pori hadi siku ya Uchaguzi inafika anakua hujui sifa za mgombea anaetaka kumchagua.
 
Pasco umeutendea haki uzi huu, hakika mengi umeyaeleza. Jambo nalipata hapa ni kwamba kuna uhaba wa kujua sheria, kufuatilia haki zetu na hata umaskini wa kipato kugharamikia kesi! zaidi ni pamoja na uwezo wa nani anaenda kudai haki, kwa maana ya kufungua kesi mahakamani.
Swali : Hivi chama cha waandishi haikiwezi ku file case ya mauaji ya Daudi mwangozi?
SP

Suala ndo hilo kwamba ni kweli hawa viongozi wa chama cha waandishi wa habari hawawezi kuitisha kesi mahakamani na watu wakaenda kutoa ushahidi? Tatizo hapa ni ukanjanja woooote hasa viongozi wao wanafanya kazi za serikali na hii ni kama tunayoona kwenye mihimili ya serikali yaan huwezi kutenganisha Bunge Mahakama na serikali kuu vyoote vinafanya kazi moja ya kuitetea serikali badala ya kusimamia taaluma zao na kuenenda na sheria,taratibu na kanuni. Na hata kwa waandishi wa habari ni hivyo hivyo hawana uwezo wa kujisimamia hivyo tusitegemee jipya hapo.

R.I.P.Mwangosi.
 
Najaribu kuona Pasco anahusikaje nashindwa kabisa....au tumemgeuza punching bag humu?

Naona kuna kampeni ya mskusudi kumrushia mawe Pasco wa JF, nina wasiwasi na baadhi ya waandishi makanjanja labda wamepunjwa mgawo wa bahasha?
 
Last edited by a moderator:
Naona kuna kampeni ya mskusudi kumrushia mawe Pasco wa JF, nina wasiwasi na baadhi ya waandishi makanjanja labda wamepunjwa mgawo wa bahasha?
Pasco anaponzwa na umaarufu wake humu ingawa sasa hivi hayuko active sana na issue za uandishi nje ya deals zake matangazo, humu binafsi nawajua waandishi wengi lakini watu wengi wanamfahamu Pasco kutokana na kuwa very active humu hasa quality ya michango yake kama mwanahabari wa muda mrefu.
 
Last edited by a moderator:
Waandishi wetu wengi wanahitaji kuonewa huruma. kwanza wengi ufahamu wao wa mambo mbalimbali ni limited sana. pili tatizo la ajira nchini linawalazimisha kuwa watumwa wa waajiri. hapo weledi wa taaluma hautumiki kabisa. katika mchanganyiko wa yote ndo maana wote wana bei kwa wanasiasa na mafisadi.

Wanaona heri ajijenge binafsi, na unapojumlisha na tishio la usalama ndo basi tena. leo hii kuna mwandishi gani mwenye ujasiri kama aliokuwa nao marehemu stan katabalo wa gazeti la mfanyakazi miaka ya mwanzo ya tisini?
 
Back
Top Bottom